< <
1 / total: 9
Pepo: Makazi ya kudumu ya WachaMungu - Harun Yahya
Pepo:
Makazi ya kudumu ya WachaMungu
   

 


Neno la Mfasiri

Kuandaliwa kwa Kitabu hiki ni jitihada ya kujaribu kutoa picha halisi na muelekeo  sahihi unaofunzwa na Uislamu kinadharia juu ya maisha ya Peponi. Pepo ni umbile tukufu ambalo ni zawadi watakayotunukiwa watu na majini watakaofuzu mtihani wa maisha  ya ulimwenguni kwa matendo yao mema kulingana na alivyoamrisha Muumba. Kitabu hiki kinatoa  picha  ya jumla na ya kweli juu ya umbile la Pepo na maisha ya Peponi ili kuwaongezea tamaa na hamu wale wote wanaofanya jitihada ya kumcha Mwenyezi Mungu. Hamu na tamaa ambazo kwa Tawfiiq ya Mwenyezi Mungu zitawapa hamasa ya kuzidisha na kudumisha matendo mema, yatakayowafanya wafanikiwe na wawe miongoni mwa wakazi wa umbile la Pepo lenye jiografia ya ajabu. Maudhui ya kitabu hiki yanamjenga msomaji aweze kukabiliana na changamoto za kuepuka makatazo na kufuata maamrisho ya Mwenyezi Mungu kwa matarajio ya kufaulu na kuingia Peponi.

Dhana na picha ya kimawazo inayochorwa na kitabu hiki, ni nyenzo za kumsaidia msomaji kupata taswira na kuuchambua ukweli juu ya maisha haya. Inatarajiwa nyenzo hizo ziwe msukumo wa kufanya utafiti wa kina ili kupata usahihi juu ya dhana, itikadi na maelezo mengi yatolewayo juu ya maisha yajayo yenye uhai wa milele. Usaidizi wa nyenzo hizo, utamuwezesha msomaji kubaini hakika juu ya maisha ya Peponi na kuweza kuyasawiri kifikra akiwa na hakika nayo.

Kwa kuwa ufahamu juu ya maisha ya Peponi umezungukwa na hakika za kiimani, basi ulinganishi uliofanyika kitabuni humu unawianishwa na maisha halisi ya ulimwengu huu. Katika baadhi ya sura au sehemu, yametolewa maelezo linganishi ili kumuwezesha msomaji kupima na kutafakari ili kupata uoni huru unaotokana na hakika za kimsingi zenye hoja madhubuti. Kitabu hiki kimelenga kusaidia kumpa msomaji uhalisia wa kile ambacho pengine amekuwa akikisikia, kujifunza na kukiamini muda wote bila ya kuwa na walau tawira yake.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu aikubali jitihada hii, atusamehe upungufu wetu na atie Tawfiiq wasomaji wake waweze kuyafahamu vyema maudhui ya kitabu hiki na ili kwayo, waweze kuishi kulingana na atakavyo YEYE, wapate kufaulu na kuzawadiwa Pepo tukufu katika maisha yajayo ya Akhera baada ya haya ya Ulimwengu.

 
   
    
1 / total 9
You can read Harun Yahya's book Pepo: Maskani Ya Waumini online, share it on social networks such as Facebook and Twitter, download it to your computer, use it in your homework and theses, and publish, copy or reproduce it on your own web sites or blogs without paying any copyright fee, so long as you acknowledge this site as the reference.
About this site | Tengeneza kurasa yako ya nyumbani | Add to favorites | RSS Feed
Mambo yote yanaweza kuynakiliwa, kuchapwa na kusambazwa kwa kurejea katika kurasa hii
(c) All publication rights of the personal photos of Mr. Adnan Oktar that are present in our website and in all other Harun Yahya works belong to Global Publication Ltd. Co. They cannot be used or published without prior consent even if used partially.
© 1994 Harun Yahya.www.harunyahya.com
page_top