< <
2 / total: 9
Pepo: Makazi ya kudumu ya WachaMungu - Harun Yahya
Pepo:
Makazi ya kudumu ya WachaMungu
   

 


Sura ya Kwanza
Pepo ni Nini na Kupi Kufanikiwa kwa Kweli

Qur'an, ufunuo kutoka Mwenyezi Mungu Muumba wa kila kitu, inaieleza Pepo kwa lugha ya picha  yenye  umbile lenye mandhari, mazingira na hali ya kijiografia inayotofautiana na maumbile ya Ulimwengu huu. Pepo ni moja ya maumbile yanayounda mandhari ya Akhera. Akhera kama ulivyo Ulimwengu, ni ombwe linalokusanya maumbile anayoyajua Mwenyewe Mwenyezi Mungu, moja wapo likiwa Pepo yake tukufu.  Peponi si mbinguni wala Pepo si mbingu, bali ni umbile ambamo ndimo yalimo makazi matukufu yaliyoandaliwa rasmi kwa ajili ya majini na watu walioishi kwa kuchunga mipaka ya Mwenyezi Mungu hapa Ulimwenguni.

Ilivyokuwa Dunia ni makazi ya muda ya Watu, majini, wanyama, wadudu na viumbwa vyenginevyo, iliyowekewa kila kilichohitajika katika kuwezesha maisha yao yakiwemo maji, hewa munasibu, vyakula na kila kilichohitajika, Pepo kwa upande wake imeandaliwa kuwa makazi ya waja wema tu ikiwa imewekwa vyakula, matunda, vinywaji visivyoondoa akili, burudani zisizo za kipuuzi, nguo na hewa ya aina yake, majengo, mito, mabwawa, mabustani yaliyopangwa vizuri, vijia, njia na barabara zilizojengwa tayari kwa ajili ya matumizi ya wakazi wake watarajiwa. Tofauti na ilivyokutwa dunia zama za awali za maisha ya watu, ikiwa haina majengo bali misitu, wanyama, wadudu, mito, mabwawa, bahari na majangwa; mpango wa ujenzi wa Pepo umefanywa na Mwenyewe Mwenyezi Mungu, kwa hiyo atakaefuzu na kupata zawadi hiyo atakuwa amefaulu kwa kiwango kisichoweza kumithilishwa.

Hata hivyo, mawazo yaliyomea na kustawi duniani kote hivi sasa ni kwamba, maisha ya mtu yatakuwa yamekamilika baada ya yeye kupata utajiri au kuwa na mume au mke mwenye heshima na hadhi za kidunia katika jamii kwa sababu ya cheo au nafasi yake nzuri. Qur'an haiyakubali mawazo haya kwani yenyewe inasema kuwa maisha haya ya dunia kamwe hayatafikia mahala pa kukamilika na kutokuwa na changamoto au matatizo kwani maisha yenyewe yamekusudiwa kuwa mtihani.

Mzizi wa neno "dunia" una maana pana sana. Ni kiyambishi cha kisifa "daniy" chenye maana ya duni, isiyo na raha, yaani chini na isiyo na maana kabisa. Kwa hiyo Dunia maana yake ni mahali penye sifa hizo. Ndiyo maana Qur'an, mara zote inayaponda maisha ya dunia kuwa si chochote na hayana maana yoyote. Inavitaja vitu kama utajiri, mali, mume, mke au wake, watoto, hadhi na mafanikiyo ambayo ndiyo yanayodhaniwa kuwa yanayafanya maisha yawe mazuri kuwa si chochote na ni ya kupita tu na ya hadaa.

Katika aya moja ya Qur'an Mwenyezi Mungu anasema:

Juweni ya kwamba maisha ya dunia ni mchezo na upuuzi na pambo na kufurahishana baina yenu(kwa nasaba), na kufurahishana kwa mali na watoto.(Na hali ya kuwa vyote hivi hamdumu navyo. Mfano wake) ni kama mvua ambayo huwafurahisha(wakulima) mazao yake kisha yanakauka, ukayaona yamepiga umanjano kisha yanakuwa mabuwa(hayana chochote). Na Akhera kuna adhabu kali(kwa wabaya) na piya msamaha wa Mwenyezi Mungu na radhi yake(kwa wema). Na hayakuwa maisha ya dunia ila ni starehe idanganyayo(mara huondoka).(57:20).

Aya nyingine inayoelezea jinsi watu wanavyopofushwa na maisha bandia ya dunia ni hii;

"Lakini nyinyi mnapenda zaidi maisha ya dunia. Hali ya kua maisha ya Akhera ndiyo bora(zaidi kabisa) na yenye kudumu(87:16-17).

Kama isemavyo aya hiyo, watu hawa huyachukulia maisha haya ya dunia kuwa ni bora kuliko yale ya Akhera na kwamba ndio mwisho wa kila kitu na hakuna maisha mengine. Mtazamo huo dhaifu huwafanya wakane imani juu ya Allah na Kitabu chake.

Allah anawaelezea watu hawa kama:

"Wale wasioogopa kukutana na sisi na wakawa radhi na maisha ya dunia na wakatuwa kwayo, na wale walioghafilika na aya zetu(10:7).

Na Qur'an inabainisha kuwa watu hao watakutana na mateso ya kudumu Jahannamu. Hata hivyo upungufu hauna maana kuwa dunia haina vitu vizuri la hasha! Allah ameujazia ulimwengu vitu vizuri vya kutukumbusha Pepo. Mazuri ya Peponi na mabaya ya motoni yakiwa yametahafifishwa yamechanganywa pamoja hapa duniani kwani hapa duniani ni pahala pa mtihani. Kwa hiyo wale walioamini hupata hisia za starehe zote mbili na hivyo basi badala ya kukumbatia maisha haya mafupi ya muda, wao huyaelekea yale maisha halisi ya milele.

Qur'an inailezea Akhera kuwa ndiyo makazi halisi na ya milele ya kila mtu. Lakini pamoja na ukweli huo watu wengi hudhani wanaweza kujitengezea maisha kamili hapa hapa duniani. Wanautazama upungufu kama wa maradhi, uchovu, maumivu, hofu, wasi wasi na mashaka kuwa ni mambo ya kawaida ya kimaumbile. Lakini kumbe Allah ameumba upungufu huu kwa makusudio yaliyofichikana, ili watu wayatafakari barabara makusudio hayo na wapate mafundisho sahihi. Ni jambo ambalo lingewezekana kabisa kwetu kuishi bila ya kuuguwa, kusikiya uchovu unaotulazimu kupumzika na kulala. Watu wangeliweza kuwa na stamina na nguvu za kuishi bila kuchoka kama Mwenyezi Mungu angalitaka tuwe hivyo. Angeweza kutuumba bila ya upungufu au matatizo hayo lakini hasha, yeye ametuumba na upungufu na matatizo hayo ili tujielewe kuwa, sisi ni viumbe dhaifu tusiojitegemea wenyewe.

Kila mtu hulazimika kukabiliana na udhaifu na unyonge wake katika maisha yake. Ila wakati kiwiliwili chake ambacho mwenyewe anakiona bora sana daima humkumbusha udhaifu wake. Aamkapo kila asubuhi na kuianza siku, uso wake huwa umevimbiana na huwa ovyo ovyo. Kinywa chake huwa harufu mbaya na yey huwa anajisikia ovyo kwa sababu ya uchafu katika ngozi, nywele na mwili mzima.

Iwapo haogi sawa sawa basi hawezi kuondokana na hali hii ya kujisikia ovyo ovyo. Tena basi, kuoga huko lazima kurudiwe mara kadhaa kwa siku kwani kila baada ya kupita muda fulani uchafu hurudi tena mwilini. Na akipitisha siku chache tu bila kuoga, lazima ya kuoga huongezeka na hudhihirika kwani hufikia mahala pa kuwafanya wenzie waliokaribu naye wakose raha kabisa. Mwili wa binaadamu siyo mgumu kama jiwe au metali bali wenyewe umejengwa na vitu vinavyoharibika haraka zaidi, vitu hivyo ni pamoja na nyama.

Mwili huu unafunikwa na ngozi nyembamba inayoweza kuchanika wakati wowote inapopata ajali ndogo tu. Kwa jumla nyama ya kiwiwili ni rahisi sana kuathirika. Yaweza kujeruhiwa, kuchubuka na kukunjamana kwa kipigo kidogo kabisa. Na kadri umri unavyokwisha mtu huanza kupoteza unyororo, unga'vu na husinyaa, kukauka na kukunjamana. Baada ya kufa, huanza kuoza. Majuma machache tu baada ya kuzikwa mwili huanza kuchakachika, kuliwa na mabubu na hatimaye huchanganyikana na udongo na kutoweka kabisa.

Upungufu wa kimaumbile alionao Mwanaadamu umeumbwa kwa makusudi maalumu. Udhaifu huwo unatukumbusha kwamba tupo duniani kwa makusudio maalumu. Chanzo cha umbile la Mwanaadamu ni udongo na baadaye nyama. Badala ya nyama wangaliweza kuumbwa kwa vitu vingine bora zaidi au wangeweza kuumbwa katika hali ya kutosikia maumivu, kutopata magonjwa na kutokudhurika. Lakini hasha, yote hayo yameumbwa kwa minajili ya kuwakumbusha Wanaadamu jinsi walivyo dhaifu na jinsi wanavyohitaji msaada wa Allah licha ya hiyari, utambuzi na uhuru waliotunukiwa katika kuendesha maisha yao. Sifa kuu ya Mwanaadamu juu ya viumbwa vyengine ni kwamba, yeye si mtambuzi tu bali ni mtambuzi wa nafsi yake. Si hivyo tu bali upungufu walionao, unawaonesha kuwa makazi ya hapa duniani si ya kudumu na yeye si mtawala wa mwisho wa mambo yake. Tunapouangaliya upungufu huu twaweza kujiona udhaifu wetu na kuielewa starehe ya mpito ya madaraka na mazuri yote ya dunia hii. Wakati huo huo huwaelewa watu wanaoabudiwa badala ya Muumba, tunaojaribu kuwafurahisha au kuwatukuza. Kumbe na wao ni dhaifu, wana upungufu kama watu wengine. Lakini wengi hawaelewi hili na hawaoni udhaifu na upungufu wa dunia, ndiyo maana wanahangaika na starehe za maisha ya dunia hii. Kwa hakika haya ni matokeo ya ujinga na matokeo ya kushindwa kukitumia vyema kipawa cha akili tulichotunukiwa. Mwenendo huo unaelezwa hivi katika Qur'an:

"Basi jiepushe na wale waupao kisogo ukumbusho wetu huu(Qur'an). Na wala hawataki ila maisha(ya starehe) ya dunia. Hakika Mola wako ndiye amjuaye anayepotea njia yake, na ndiye Amjuaye anayeongoka(53:29-30).

Wale wasioujua ukweli huu ndio wanaoshikwa na matamanio ya maisha haya ya dunia. Hao ni watu wasioelewa kitu kama aya isemavyo. Sasa basi ni ufahamu gani tunaotakiwa kuwa nao katika jambo hili? Kwa kweli si kingine bali ni elimu ya Pepo ambayo Allah ametuahidi. Hatuwa muhimu kabisa ya kuiendea Pepo hiyo ni kuielewa vema Qur'an na kutafakari kwa makini yale inayoyasema. Katika Qur'an Mwenyezi Mungu anayaelezea makazi halisi ya waumini kwa maneno haya:

"Na hayakuwa maisha ya Dunia ila upuuzi na mchezo; na nyumba ya akhera ndio maisha hasa: Laiti wangalijua(29:64).

Hadithi inamkariri Mtume(s.a.w) akisema kuwa pepo ni makazi halisi ya Wanadamu, ni mahali ambapo hapatakuwa na udhaifu wa kibinaadamu. Mwenye kunadi atanadi, mtakuwa na ubukheri wa afya wa milele, katu hamtaugua, mtakuwa na uhai wa milele, katu hamtakufa, mtakuwa na ujana wa milele katu hamtazeeka, na raha ya milele, katu hamtakuwa katika hali ya kutotosheka(Muslim). Qur'an inawaahidi Waumini kufaidi kukubwa na malipo yasiyokoma, na starehe za milele za maisha ya Peponi.

Kwa vile waumini wameahidiwa Pepo basi hata hapa duniani wataneemeshwa kwa rehma na ukarimu mkubwa wa Allah(s.w). Qur'an inasema kuwa Waumini wanaotenda mema katika Dunia hii pia watapewa maisha mema hapa Duniani.

"Wafanyaji mema, wanaume au wanawake hali ya kuwa ni Waislamu tutawahuisha maisha mema na tutawapa ujira(Akhera) mkubwa kabisa kwa sababu ya yale mema waliyokuwa wakiyatenda(16:97).

Katika aya nyinginezo ahadi hiyo njema inasema wataifaidi waumini wote wa kweli, Mitume ndiyo wakiwa wa mwanzo miongoni mwa waumini. Kwa mfano Mtume Muhammad(s.a.w) ambaye katika Qur'an amepewa habari njema za vyeo vya juu peponi, alikuwa ni mtu ambaye Allah alimtajirisha hapa duniani.

"Na akakukuta fakiri akakutajirisha(93:8).

Mbali ya hivyo, Qur'an pia inatutajia utajiri wa mali walizopewa Manabii Daud, Suleiman(a.s), Ibrahim(a.s) na watu wema kama Dhul Qarnain. Kutowa neema na starehe dunia hii kama ujira na motisha na kama ishara ya Rehema na Mapenzi ya Allah kwa waumini wa kweli ni moja kati ya kanuni za kudumu za Mwenyezi Mungu. Kwa kuwa utajiri, raha na sterehe ndizo sifa kuu za Peponi, Mwenyezi Mungu kaumba mfano wa neema hizo hapa duniani, kama ukumbusho kwa wale aliowachagua kuingia Peponi. Na ili kuwaongezea hamu na uchu wa kupata Pepo. Swala wanazoswali na kila jema wanalolifanya, liwe kubwa au dogo ili kupata radhi zake. Mbali na yote hayo, wao pia hujua kuwa Malaika huziandika amali zao katika madaftari na kwamba watalipwa Akhera kwa yale waliyoyafanya. Hii ni hisia ya kujichunga ambayo inatokana na kule kuelewa kwao kuwa Allah amewasaidia kwa Majeshi ya Malaika mbele yao na nyuma yao ili wawalinde kwa amri ya Mwenyezi Mungu:

"Ana(kila mtu) kundi la Malaika mbele yake na nyuma yake. wanaomfuatilia kwa amri ya Mwenyezi Mungu.(13:11).

Kwa hali hiyo watazishinda nguvu zote za upinzani wanazokabiliana nazo katika njia ya Mwenyezi Mungu na daima wao huwa na shauku ya ile ahadi nono ya Pepo. Hivyo waumini wa kweli kama Allah alivyowaambia Malaika hawatokuwa na hofu wala unyonge kwani:

(Kumbukeni) Mola wenu alipowafunulia Malaika(akawaambia): Hakika mimi ni pamoja nanyi, basi watieni nguvu wale walioamini nitatia woga katika nyoyo za makafiri, basi wapigeni katika shingo(zao) na kateni kila ncha za vidole vyao.(8:12).

 
   
    
2 / total 9
You can read Harun Yahya's book Pepo: Maskani Ya Waumini online, share it on social networks such as Facebook and Twitter, download it to your computer, use it in your homework and theses, and publish, copy or reproduce it on your own web sites or blogs without paying any copyright fee, so long as you acknowledge this site as the reference.
About this site | Tengeneza kurasa yako ya nyumbani | Add to favorites | RSS Feed
Mambo yote yanaweza kuynakiliwa, kuchapwa na kusambazwa kwa kurejea katika kurasa hii
(c) All publication rights of the personal photos of Mr. Adnan Oktar that are present in our website and in all other Harun Yahya works belong to Global Publication Ltd. Co. They cannot be used or published without prior consent even if used partially.
© 1994 Harun Yahya.www.harunyahya.com
page_top