< <
6 / total: 9
Pepo: Makazi ya kudumu ya WachaMungu - Harun Yahya
Pepo:
Makazi ya kudumu ya WachaMungu
   

 


Sura ya Tano
Mandhari ya Pepo na Uzuri wake

"Mfano wa pepo waliyoahidiwa wamchao Mwenyezi Mungu (ni hivi); mbele yake inapita mito, matunda yake ni ya daima na (pia) kivuli chake.  Huu ndio mwisho wa wale wamchao Mwenyezi Mungu.  Na mwisho wa makafiri ni moto (13:35).

   Uzuri wa mandhari ya Pepo  yenye rangi ya kijani kibichi ni miongoni mwa neema za kupendeza za Peponi.  Aidha, maghorofa  yaliyojengwa mabustanini yakiwa na mito mbele yake ni mapambo ya Peponi.  Humo hamna jua kali wala baridi kali.

"Humo wataegemea viti vya enzi, hawataona jua kali wala baridi kali.  Na vivuli vyake vitakuwa karibu yao, na mashada ya matunda yake yataning'inia mpaka chini.  (76:13-14).

Pepo ina hali hiyo ya hewa ya kupendeza, kwamba humo hakuna mtu atakayekosa raha.  Pepo haina joto kali wala baridi kali.  Katika Pepo Mwenyezi Mungu Atawaingiza  waumini katika vivuli vizuri kabisa;

  "Na wale walioamini na kufanya vitendo vizuri, tutawaingiza katika mabustani yapitayo mito mbele  wakae humo milele.  Humo watakuwa na wake waliotakasika na tutawaingiza katika vivuli vizuri kabisa (4:57).

   Usemi huu "vivuli vya raha" mbali na kubainisha kuwa hali ya hewa itakuwa ya kustarehesha kama vile mtu atakavyotaka  pia unaonesha kuwa mazingira na hali ya Peponi vimesaniwa kwa namna ya kuipa nafsi ya mwanadamu raha na starehe kamili.  Kila kitu na kila hali katika pepo kitakuwa vile atakavyo muumini.  Mojawapo ya starehe za mandhari ya Peponi ni mtiririko wa maji;

"Na maji yanayomiminika (kwa vizuri) (56:31)"

Kama tuonavyo katika maisha haya, nafsi ya mwanadamu huburudika inapoona maji yatiririkayo katika mito, maziwa, chemchem na vijito vinavyotiririka mwituni.  Vyote hivi vinaburudisha nafsi ya mtu. Mabwawa ya kuchimbwa, mashamba, mabustani pamoja na vijikondo vya asili vyote vinatengenezwa kutokana na raha hiyo ya nafsi.  Vitu hivyo huistarehesha nafsi.  Sababu kuu ya vitu hivyo kuleta raha kwa binadamu ni kwamba nafsi ya mtu imeumbwa kwa ajili ya pepo.  Starehe hizi zinaelezwa hivi;  "Humo mna chem chem  mbili zinazotoka maji kwa nguvu." (55:66).

Kuyatazama maji na kusikia mvumo wa maji yanayotiririka nako kwaustarehesha  na kuuburudisha moyo wa mtu.  Kule kuyaona na kuyasikia maji yanavyobubujika kutoka juu kunaleta raha na ni mojawapo  ya neema  ambazo watu wamshukuria na kumtukuzia Mwenyezi Mungu.

Hasa hasa maji yanapotiririka kutoka milimani katikati ya miti au juu ya mawe kwa kweli yanapendeza kuyatazama na hata pale yanapomwagika na kujikusanya kutengeneza bwawa.  Daima maji yanayotiririka ni ishara ya starehe kubwa isiyochosha.  "Na hakika wanaomcha Mwenyezi Mungu watakuwa katika mabustani na chemchem (zinazopita mbele yao)" (15:45).

"Bila shaka wamchao Mungu watakuwa katika vivuli na mito."  (77:41)

  "Vivuli ni sehemu makhususi zilizoumbwa ili waumini waweze kukaa na kupata starehe yote hiyo (Allahu A'alam).  Na kuhusu maghorofa, vivuli hivi pia vina wekwa mahala pa juu ili watu wa peponi waone mandhari yao wakiwa  juu na watazame  vyote vilivyomo.  Vivuli hivyo vinaleta raha na starehe makhususi kwa waumini.  Watu wanapewa vyakula mbalimbali na matunda ya aina kwa aina na wanakabiliana kufanya maongezi kwa furaha. Tena mbele yao kuna mito ambayo inaiburudisha nafsi ya binadamu na kuwaongozea mvuto machoni mwao.  Katika mito hiyo yanatiririka maji matamu.

Starehe nyingine ni malisho yaliyomo kwenye mabustani, kwa mfano; Sura ya 42, Aya ya 22 inasema; "Na wale walioamini na kutenda mema watakuwa katika mabustani ya Peponi; watapata watakayoyataka kwa Mola wao hiyo ndiyo fadhila kubwa. Vyote vilivyomo humo ni kwa ajili ya waumini tu.  Moja kati ya mambo yaliyomo humo ni mandhari yenye mseto wa vivutiyo.  Humo mna mimeya inayostawi bila kukauka, mimeya yenye harufu nzuri na mna aina ya wanyama tunaowajuwa na tusiowajuwa. Mabustani haya yanapambwa na matunda ya aina mbalimbali na miti mbalimbali na nyanda zenye majani ya kijani kibichi;

 "Yenye rangi nzuri ya kijani kilichowiva (barabara)." (55:64)

Yana mimeya na maua na mahali pengine pana mabwawa na mabubujiko;  "Watakuwa katika vivuli vya mikunazi isiyo na miba.  Na migomba iliyopangiliwa vizuri na kupangiliwa mazao yake." (56:28-29).

 Kwa kuzingatia vitu vyote hivi tunaweza kujenga picha ya jumla ya Pepo. Baadhi ya sifa zake zinatukumbusha vitu vilivyopo hapa duniani na neema nyingine ni za aina yake, zina starehe za aina yake ambazo hakuna mtu yeyote ambaye amewahi kuziona au hata kuzisikia na kwamba hata akili zetu haziwezi kuzifikiria au kuzielezea.

  Lazima tufahamu kuwa vitu hivi vizuri  na raha za aina kwa aina zinawasubiri waumini.  Hivi vimeandaliwa kwa elimu ya Allah isiyo na ukomo na iliyo nje ya akili zetu.  Kama inavyosema Aya 22 ya Suratil-As-Shura, watapata kila wanachokitamani kwa Mola wao.  Hii ni neema kubwa.  Kila kitu Peponi,  pamoja na starehe zake, kimeumbwa kwa kuzingatia utashi na raha ya muumini.  Kwa maneno mengine Allah (S.W) huziachia hisia za muumini kazi ya kuyajenga mazingira ya Peponi ikiwa ni rehema yake.

Raha isiyo na mwisho

(Waambiwe); kuleni na kunyweni kwa furaha kwa sababu ya yale mliyokuwa mkiyatenda.  (77:43).

Qur'an imetangaza kuwa watu wa Peponi watastareheshwa kwa kila watakachokitamani vikiwemo vyakula vitamu na vinywaji mbalimbali.  Huko watu hawahitaji shibe kwani vyakula na vinywaji hivyo vimeumbwa kwa ajili ya kustarehesha tu.  Chakula hiki kinafanana na chakula cha dunia hii.  Watu wa Peponi wataulezea mfanano huo kwa maneno haya;

 "Na wabashirie walioamini na kufanya vitendo vizuri kwamba watapata mabustani yapitayo mito mbele yake; kila mara watakapopewa matunda humo kuwa ni chakula watasema; haya ndio yale tuliyopewa zamani (ulimwenguni).  Kwani wataletewa (matunda hayo) hali ya kuwa yamefanana); na humo watapata wake waliotakasika na watakaa milele humo. (2:25).

Vyakula vingi katika dunia vinalika kutokana na hamu ya kula ya watu na vinaleta raha kwa haiba na ladha yake.  Allah (S.W), Ameshaviumba vyakula vinavyofanana huko peponi ili kuleta raha kwa waumini.  Isipokuwa, tafauti na vyakula vya Duniani, hapatakuwa na khofu ya kunenepeana, kulimbikiza lehemu mwilini, kuvimbiwa wale, kwani Allah (S.W) atawaambia;

"Kuleni na kunyweni kwa furaha kwa sababu ya yale mliyokuwa mkiyatenda (77:43).

Kuweza kula na kunywa pasi na kiasi ni neema kubwa inayoleta raha kweli kweli.

 
   
    
6 / total 9
You can read Harun Yahya's book Pepo: Maskani Ya Waumini online, share it on social networks such as Facebook and Twitter, download it to your computer, use it in your homework and theses, and publish, copy or reproduce it on your own web sites or blogs without paying any copyright fee, so long as you acknowledge this site as the reference.
About this site | Tengeneza kurasa yako ya nyumbani | Add to favorites | RSS Feed
Mambo yote yanaweza kuynakiliwa, kuchapwa na kusambazwa kwa kurejea katika kurasa hii
(c) All publication rights of the personal photos of Mr. Adnan Oktar that are present in our website and in all other Harun Yahya works belong to Global Publication Ltd. Co. They cannot be used or published without prior consent even if used partially.
© 1994 Harun Yahya.www.harunyahya.com
page_top