< <
7 / total: 9
Pepo: Makazi ya kudumu ya WachaMungu - Harun Yahya
Pepo:
Makazi ya kudumu ya WachaMungu
   

 


Sura ya Sita
Muumini huishi mahali gani Peponi?

Ili kupata Pepo, watu wanapewa mitihani katika maisha ya Dunia.Waumini hufanya juhudi na bidii kubwa kutafuta radhi za Mola wao. Wanaelekea na kujitupa kwake kwa ikhlasi. Wakimtukuza na kumshukuru wakati wote, wakimuomba Yeye tu na wanatubia kwake. Kwa ajili hiyo Allah huwapa neema za Peponi. Peponi, Allah (S.W) Huwaruzuku waumini kila aina ya matunda na nyama wanayoipenda, nyama zisizosababisha ongezeko la lehemu wala kukifu. Na tangu hapo umbile watakalokuwa nalo halitaruhusu udhaifu kama huo.

‘'Na Tutawapa (kila namna ya)Matunda na (kila namna za) nyama,kama vile watakavyopenda''(52:22)

Na atawapa nyama yoyote ya ndege wanayoipenda.
 
‘'Na matunda(namna kwa namna) kama watakavyopenda. Na nyama za ndege kama watakavyotamani (wenyewe).''(56:20-21).

Isitoshe chakula chao hakitakwisha:

 ‘'Hakika hiyo ndiyo riziki yetu isiyomalizika''(38:54).

Waumini wataingia katika Pepo ambamo wataruzukiwa pasipo hesabu.

''Afanyaye ubaya hatalipwa ila sawa na uovu wake,na afanyaye wema akiwa mwanaume au mwanamke naye ni Muislamu,basi hao wataingia peponi waruzukiwe humo bila hesabu''(40:40).

Wataweza kula  kwa kiasi wanachotaka, na watakula vyakula vya aina kwa aina vilivyomo humo. Vyakula hivyo havitapunguwa na hakuna atakayeshindwa kula kwasababu ya shibe au ugonjwa. Matunda ndiyo chakula kilichotajwa sana katika Qur'an. Peponi, Waumini watapata aina kwa aina za matunda wanayotamani.Qur'an inaeleza hivi:

''Na vivuli vyake vitakuwa karibu yao ,na mashada ya matunda yake yataning'inia mpaka chini.(76:14).

 Hivyo tunafahamishwa kuwa matunda ya Peponi yanastawi mitini katika mazingira asilia na kwamba waumini wataweza kuyachuma na kuyala. Surati  waqia 28-29 watakuwa  katika  vivuli  vya   mikunazi  isiyo na miba. Na migomba  iliyopangiliwa vizuri  mazao  yake. Maana  yake   ni kuwa  matunda  hayo   yanaweza  kupatikana  kirahisi  kwani  neema  za  peponi hazina  hesabu. Matunda  ni  mengi  mno  matawi ya miti  yapo chini chini , hivyo  ni rahisi kuyafikia. Matunda haya yatawekwa kwenye vibebeo vya  dhahabu na fedha  na sahani za kupendeza zilizosaniwa na kunakshiwa kwa ajili ya waumini ambao kila mmoja atakuwa kwenye jumba lake la fahari watakuwa wameketi kwenye viti vya fahari wakizungumza.

Makokwa, makovu ya uozo,  makambakamba ambayo husumbua watu pale walapo  matunda ya dunia hii vyote havitaonekana  ili kuleta raha ya pepo. Matunda yote hayo yanatolewa bure kwa waumini huku yakipendeza machoni mwao na yakiwa hayana upungufu wowote ule. Aidha matunda haya  yameongezewa rangi na uzuri kwa ajili ya pepo. Haiba ya miti ya matunda hayo yenye rangi mbalimbali yaleta mvuto zaidi wa mandhari.

 Rangi ya kijani ndiyo itakayokoza zaidi na ndani yake itakuwa na rangi ya manjano, rangi ya machungwa na rangi nyekundu. Mchanganyiko huo utaleta  haiba maridadi ya kuliburudisha jicho la mwanadamu. Hii ikiwa ni ishara  ya usanii  mkubwa kwa Allah (S.W) ambao utakuwa sababu ya waumini kumtukuza na kumuhimidi Allah (S.W).

Navyo vinywaji teletele vitakuwa na ladha bora kabisa.  Surati As-saaffati, aya ya 43.

 Katika bustani za neema. Wako juu  ya vitanda[Viti vya enzi vya fahari], wamekabiliana[wanazungumza]. Wanazungushiwa gilasi zenye vinywaji safi. Vyeupe vyenye ladha kwa hao wavinywao; kwa vinywaji hivyo hautokua udhia wala kutokwa na akili. Huko peponi watanyweshwa vinywaji (vizuri) vilivyofungwa ( kwa vizibo madhubuti).Mwishowe (vinywaji hivyo vinaleta harufu ya) miski .Na katika(kupata) haya washindani wenye kushindana.Na mchanganyiko wake ni maji ya Tasnymu .(Hiyo ni) chemchem watakayoinywa( watu) waliokaribishwa na (Mwenyezi Mungu.)(83:25-28).

Kama zisemavyo aya hizi,kile wakinywacho pia hutoa harufu nzuri na ukweli.. Allah (S.W) anasema kuwa vinywaji hivi vitamiminwa katika gilasi. Havitamletea mnywaji maumivu kichwani au kumfanya apoteze  akili .Wanaotoa huduma ya vinywaji hivi ni vijana walioteuliwa na Mwenyezi Mungu.

'Mwenyezi Mungu amewaahidi wanaoamini wanaume na waumini wanawake mabustani yenye mito mbele yake wakae humo daima na makazi mazuri katika mabustani hayo yenye kudumu.Na radhi za MwenyeziMungu ndizo kubwa zaidi.Huko ndiko kufuzu kukubwa (9:72).

Kama tulivyosema mwanzo,makazi ambayo waumini huishi makazi yao ya dunia ni mahali ambapo Allah ametaka pajengwe majumba ambamo jina lake likumbukwe na litukuzwe. (Waonekane kwa kusali nyakati tano) nyakati ambazo Mwenyezi Mungu ameamrisha zitukuzwe na litajwe jina lake Misikitini humtukuza humo asubuhi na jioni(24:36). Makazi ya Peponi yako kama hivyo,ni sehemu zenye starehe nzuri zisizo na kifani ambamo Allah (S.W) hudhukuriwa, hutajwa na kushukuriwa. Kama vile majumba na maghorofa yajengwavyo  katika haiba nzuri, ya Peponi yamejengwa mfano wa hayo  kwa usanifu na teknolojia bora zaidi. Majumba yaliyotajwa katika Qur'an kwa ujumla yamejengwa kwa rosheni.

''Lakini waliomcha Mola watapata ghorofa zilizojengwa juu ya ghorofa;chini yake hupita mito Ndiyo ahadi ya Mwenyezi Mungu naye havunji ahadi yake''(39:20).

 Maghorofa hayo yaliyojengwa sehemu zenye miinuko,  yakiwa na mapambo sehemu zote mpaka chini yakionesha mandhari ya Miji (cities) ya kupendeza inayotoa fursa kwa wakazi wake kutazama vitu vingi na vizuri kwa wakati mmoja.  Qur'an inabainisha kutakuwa na maji yanayotiririka chini ya maghorofa hayo yaliyojengwa vilimani. Hivyo ili kuyaona mandhari hayo, maghorofa yanaweza kuwa na vyumba maalumu vya kukaa na madirisha yenye vioo katika pande zote nne. Maghorofa hayo yamesaniwa kuiburudisha nafsi ya mwanaadamu kwa raha kemkem. Waumini watakaa kwenye viti vyao vya fahari, wakifaidi matunda na vinywaji vizuri huku wakitazama chini  kwa starehe wakiangalia kivutio kimoja baada ya kingine.

Raha za milele za peponi

Kwanza watu wasidhani kwamba Peponi ni kama jumba kubwa, humo watu wamejazana kwa pamoja wakiangalia hiki na kile kwa pamoja wakiwa wamekaa au kusimama. Mandhari ya Peponi ni yale yafananayo na miji mikubwa yenye shughuli nyingi zisizo na mfano, safi, iliyopangwa vizuri kiujenzi, tangu safu za nyumba na majumba, vichochoro, vijia, njia na barabara. Peponi kuna nyumba, majumba na maghorofa yaliyojengwa  na kurembwa kwa nakshi nzuri na rangi mchanganyiko yakiwa na viti vya burudani na vya fakhari.  Waumini watakaa huku wakiwa wameelekeana;

 "Watakuwa juu ya viti vya fakhari vilivyotonewa (vilivyotiwa mapambo).  Wataviegemea waelekeane (wanazungumza)"  (56:15-16).

"Watakuwa wameegemea juu ya viti vya fakhari vilivyopangwa safu safu, na Tutawaoza wanawake wanaopendeza wenye macho ya mazuri (Makubwa)"  (52:20).

   Wale waumini ambao Mwenyezi Mungu amewapa neema za peponi watamshukuru Mwenyezi Mungu.  Qur'an inasema; wataingia katika mabustani ya enzi ambamo watavishwa vikuku vya dhahabu na lulu na ambamo nguo zao zitakuwa za hariri.  Watasema Al-hamdulillahi,  "Mabustani ya milele watayaingia, humo watapambwa vikuku vya Dhahabu, na Lulu, na nguo zao humo zitakuwa za hariri.  Na watasema (katika kushukuru kwao) sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu aliyetuondolea huzuni, kwa yakini Mola wetu ni Mwingi wa msamaha na Mwenye kushukuru. (35:33-34).  Wakiwa wamekalia makochi laini waumini,  watatazama huku na kule;  "Wakae juu ya viti vya fakhari wakitazama (starehe zao) (83:23).  Watakuwa wakiangalia vivutio na starehe za Pepo na neema kubwa kubwa.  Hii itakuwa dhifa yenye uhondo mkubwa kweli kweli kwa waumini.

Waumini watazifaidi starehe na raha hizi kwa pamoja pasipo kujali tofauti ya wakati na zama walizoishi duniani.  Hii ni neema inayopatikana peponi tu.  Mathalani kutembeleana na kukaa kwenye viti vinavyoelekeana na kuongea na watu mliopendana, uliosikia umaarufu wao kiibada katika zama zao,  huku mkimdhukuru Allah pamoja nao ni starehe ambayo haiwezi kupatikana duniani.  Starehe hii ipo Peponi tu.

Peponi, kila kitu wanachotamani waumini kitaletwa kwao na watumishi (matarishi, wahudumu) maalumu walioteuliwa kwa kazi hiyo.  Qur'an inatufahamisha;

Iwe wanawapitia watumishi wao wanaopendeza kama kwamba ni Lulu zilizomo ndani ya chaza (ndio kwanza zimepasuliwa) (52:24).

 Waumini ambao Allah (S.W) amewaruzuku Pepo ni watu waliochaguliwa na ni watu wenye heshima.  Kule kutajwa kwao kuwa wako katika nafasi yenye cheo kunabainisha heshima ambayo Allah amewapa;

 "Hao ndio watakaopata riziki maalum.  Matunda ya kila namna na wataheshimiwa." (37:41-42).
 
Wale waliotajwa punde, ambao wanawahudumia waumini kila watakavyo na kuwapatia huduma muda wote, wametajwa katika Qur'an kama watu wasio badilika kiumri:

 "Na watawazunguukiya (kuwatumikia wavulana wasiochakaa, ukiwaona utawafikiri ni lulu zilizotawanywa.  (76:19),

 Waja hawa ambao kazi yao pekee ni kuwahudumia waumini vile watakavyo na kwa vile neema zenyewe zinatolewa bure basi uhudumu huo wa daima ni sehemu ya starehe.  Vyombo vitakavyotumiwa katika kazi hii ya uhudumu pia vina thamani kubwa  na ni bora kabisa;  watakuwa wanapitishiwa sahani za dhahabu na vikombe (vya dhahabu); na vitakuwamo ambavyo nafsi zinavipenda na macho yanavifurahia, na nyinyi mtakaa humo milele (43:71).

  Katika dunia hii waumini hupata vitu vingi, baadhi yao wakipata neema karibu kama zile za maisha ya peponi.  Tunaweza kuona malighafi bora inayotumika kutengenezea nguo za peponi.  Allah anawaagiza watu kuvaa nguo nzuri katika dunia hii  kama inavyoelezwa hapa;

(Anasema Mwenyezi Mungu kuwaambia wanadamu wote tangu hao wa zamani huko).  Enyi wanadamu! Hakika tumekuteremshieni nguo zifichazo tupu zenu na nguo za pambo; na nguo za utawa ndizo bora zaidi.  Hayo ni katika ishara (neema) za Mwenyezi Mungu ili wapate kukumbuka.  (7:26).

  Katika Surati A'raf, aya 31, Allah (S.W) anawahimiza waumini kuvaa nguo safi na nzuri;

  Enyi wanadamu! Chukuweni mapambo yenu wakati wa kila swala; na kuleni vizuri na kunyweni vizuri.  Lakini msipite kiasi.  Hakika yeye (Mwenyezi Mungu) hawapendi wapitao kiasi (wapindukiao mipaka).

Kwa hiyo nguo zinazovaliwa peponi zitakuwa bora na maridadi zaidi kuliko zile za duniani.  Qur'an hasa hasa inataja aina mbili za malighafi zinazopatikana Peponi, hariri laini na hariri nzito;

Watavaa hariri laini na hariri nzito; wakikabiliana (wanazungumza). (44:53).

   Hapa duniani malighafi hizi ni adimu sana, ghali sana na ndizo zenye ubora mkubwa.  Uzuri na umaridadi wa vazi hilo utawazidishia mvuto wale wanaolivaa.    Ni kweli kuwa malighafi na nguo zinazopatikana humo siyo tu za aina hizo mbili.  Kwani Allah (S.W) aliyetoa neema hizi atawavisha watu wa Peponi mavazi mengine mengi maridadi yatokanayo na malighafi nyinginezo nyingi na nzuri nzuri.  Anaweza kuumba mitindo ya mavazi na malighafi zisizojulikana katika dunia hii.  Qur'an inatuambia kuwa nguo maridadi inayopambwa kwa vito vya thamani huzidisha mvuto.  Vikuku vya dhahabu, Fedha na Lulu ndio hasa vimetajwa kama aya hizi;

  "Hakika Mwenyezi Mungu atawaingiza wale walioamini na kufanya vitendo vizuri katika mabustani yapitayo mito mbele yake.  Humo watavishwa mapambo ya mikononi ya dhahabu na lulu, na mavazi yao humo yatakuwa hariri." (22:23).

   "Juu yao wana nguo za hariri, za kijani kibichi na za hariri nzito.  Na watavikwa vikuku vya fedha, na Mola wao atawanywesha vinywaji safi kabisa." (76:21).

 
   
    
7 / total 9
You can read Harun Yahya's book Pepo: Maskani Ya Waumini online, share it on social networks such as Facebook and Twitter, download it to your computer, use it in your homework and theses, and publish, copy or reproduce it on your own web sites or blogs without paying any copyright fee, so long as you acknowledge this site as the reference.
About this site | Tengeneza kurasa yako ya nyumbani | Add to favorites | RSS Feed
Mambo yote yanaweza kuynakiliwa, kuchapwa na kusambazwa kwa kurejea katika kurasa hii
(c) All publication rights of the personal photos of Mr. Adnan Oktar that are present in our website and in all other Harun Yahya works belong to Global Publication Ltd. Co. They cannot be used or published without prior consent even if used partially.
© 1994 Harun Yahya.www.harunyahya.com
page_top