Usije Ukajuta

SHUSHA KITABU

Download (DOC)
Maoni

SURA ZA KITABU

< <
1 / total: 6
USIJE UKAJUTA - Harun Yahya (Adnan Oktar)
USIJE UKAJUTA
   

 


Utangulizi

Wakati  fulani binadamu akiwa duniani  huwa na huzuni wa kimwili na wa kiroho. Hisia zingine ni kubwa zaidi na haziwezi kulinganishwa na uchungu wa kimwili. Hizi hisia ambazo zinailetea roho ya binadamu machungu na dhiki zinaitwa majuto.

Kuna aina mbili za majuto. Majuto ya watu wenye imani kwa upande mmoja na wasio kuwa na imani kwa upande mwingine. Hisia hizi mbili zinatofautiana sana

Waumini ni wale walio na  imani thabiti kwamba lolote linalotokea ni kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, na lolote linalowapata ni kwa kutaka kwake Mola. Ndio maana utaona waumini wana imani kwa Mwenyezi Mungu, imani ambayo haitingishiki wakati wowote uwe wa raha, au wa shida au   wakifanya makosa. Mtume Muhammad (s.a.a.s) katika hadithi yake tukufu amesifu tabia ya muumini akisema:

Mfano wa muumini ni kama mmea shambani ambao unatikiswa na upepo lakini utarudi kwa nafasi yake ambayo ni thabiti katika mizizi yake. (Muslim)

Muumini anapotenda kosa, yeye humrudia na kumuomba Mwenyezi Mungu msamaha. Kwa hivyo haumii kwa muda mrefu akisikitika. Majuto anayokuwa nayo muumini yanamsukuma aombe msamaha na kujitakasa na yanamfanya asilirudie kosa lile. Hili huwasaidia kurekebisha makosa yao na ili wasikose matumaini katika maisha. Na pia majuto haya hayapunguzi bidii yao katika mambo ya ibada.

Kwa upande mwingine, majuto ya kafiri ni ya kudumu na kuumiza kwani hawana imani na Mwenyezi Mungu pindi wanapokumbwa na shida au wakitenda kosa. Kwa maisha yao yote wao hunena “Laiti singelifanya hili…” “ Laiti singesema hivi…” na kadhalika.

Lakini watakuwa na majuto makubwa siku ya kiyama. Wale ambao hawakuishi maisha ya kidini watajuta sana. Walionywa na kualikwa kwa njia iliyonyooka. Walikuwa na wakati muafaka wa kutafakari na kufuata njia ya ukweli. Lakini hawakusikiza.

Hakika Tunakuhadharisheni adhabu iliyo karibu (kufika), siku ambayo mtu atayaona yaliyotangulizwa na mikono yake miwili, na kafiri atasema: “Laiti ningalikuwa udongo (nisipate adhabu hii inayoningoja sasa)” (Surat an-Naba': 40)

Na ungeliona watakaposimamishwa motoni waseme: Laiti tungerudishwa (duniani) wala hatutakadhibisha ishara za Mola wetu na tutakuwa miongoni katika wanaoamini. (Surat al-An'am: 27)

 “ Na watasema: “Kama tungalisikia au tungalikuwa na akili hatungekuwa katika watu wa motoni (leo) (Surat al-Mulk: 10)

Lengo la kitabu hiki ni kuwaonya watu kwa siku ambayo watajuta wakisema” Laiti tungefahamu...,” “Laiti hatungekadhibisha aya za Mola wetu...,” “Laiti tungeliwafuata wale waliotuletea ujumbe...,” “Laiti tungelifanya hili au lile” n.k lengo pia ni kuwaita watu waishi maisha kwa ajili ya Mwenyezi Mungu kama wangali hai ili warekebishe makosa yao.

Ni lazima kufahamu vyema kwamba majuto siku hiyo hayatamkinga mtu yeyote na hasira ya Mwenyezi Mungu. Njia pekee ya kuepukana na majuto hayo ni kujisalimisha kwa Mwenyezi Mungu kama wakati bado upo na kufuata maamrisho ya Mwenyezi Mungu.

Kitabu hiki ni cha kulingania kwa njia ya Allah na kukumbusha adhabu isiyoepukika katika maisha ya akhera siku ambayo hakuna pa kujificha wala kuokolewa. Mwenyezi Mungu anatukumbusha kenye Qurani tukufu akisema:

Mwitikieni Mola wenu kabla ya kufika siku isiyoepukika itokayo kwa Mwenyezi Mungu, siku hiyo hamtakuwa na pa kukimbilia wala hamtakuwa na (njia) ya kukataa. (Surat ash-Shura: 47)

 

 

   

    
1 / total 6
You can read Harun Yahya's book Usije Ukajuta online, share it on social networks such as Facebook and Twitter, download it to your computer, use it in your homework and theses, and publish, copy or reproduce it on your own web sites or blogs without paying any copyright fee, so long as you acknowledge this site as the reference.
About this site | Tengeneza kurasa yako ya nyumbani | Add to favorites | RSS Feed
Mambo yote yanaweza kuynakiliwa, kuchapwa na kusambazwa kwa kurejea katika kurasa hii
(c) All publication rights of the personal photos of Mr. Adnan Oktar that are present in our website and in all other Harun Yahya works belong to Global Publication Ltd. Co. They cannot be used or published without prior consent even if used partially.
© 1994 Harun Yahya.www.harunyahya.com
page_top