Usije Ukajuta

SHUSHA KITABU

Download (DOC)
Maoni

SURA ZA KITABU

< <
2 / total: 6
USIJE UKAJUTA - Harun Yahya (Adnan Oktar)
USIJE UKAJUTA
   

 


Majuto Anayohisi Binadamu duniani

Na rejeeni kwa Mola wenu na mnyenyekee kwake kabla ya kukujieni adhabu, kisha hamtanusuriwa. Na fuateni yaliyo bora katika yale yaliyoteremshwa kwenu kutoka  kwa Mola wenu kabla kukujieni adhabu kwa ghafla, na hali hamtambui. (Surat az-Zumar: 54-55)

Binadamu akiwa  katika hatari ya  mauti, nafsi yake inaanza kufanya hesabu ya matendo yake. Kama mtu hakuishi katika maadili ya kidini ya Mwenyezi Mungu na wala hakufanya matendo mazuri duniani, basi atakumbwa na huzuni na majuto makubwa. Mambo mengi ambayo alidharau kwa maisha yake yote yatajitokeza mbele ya macho yake kwa uwazi. Labda kwa mara ya kwanza atahisi vipi mauti yako karibu sana. Atakiri kwamba aliishi maisha ambayo hastahiki kupata pepo. Binadamu huyo atajua kwamba alikosa shukrani kwa Mwenyezi Mungu. Hofu kubwa itamzunguka na atajua kwamba ni Mwenyezi Mungu peke yake ndiye atamuokoa kwa hali ambayo yuko. Kisha atamuahidi Mwenyezi Mungu kuwa atakuwa na shukrani na kufuata njia ya haki na kukumbuka hali ambayo yuko. Anamuomba Allah kwa dhati amuokoe kwa hatari ambayo yumo. Anaomba nafasi ya kuokolewa na kuomba fursa ya kuishi tena.

Lakini  baada ya kuokolewa na mauti, binadamu wengine hawaweki ahadi ambayo walimuahidi Mwenyezi Mungu. Pindi Mwenyezi Mungu Anamuokoa mtu huyo, anarudi kwa njia zake za awali. Hisia za majuto na kusalimu zinabadilishwa na ukosefu wa shukrani. Anasahau yale alifikiria wakati alikumbwa na mauti na anamsahau Mwenyezi Mungu kana kwamba hakujuta na kumuomba. Anarudia matendo yake na kuipenda dunia zaidi. Qurani tukufu inaashiria hisia za watu kama hawa:

Yeye ndiye anayekuendesheni katika bara na bahari. Hata mtakapokuwa katika majahazi Na yanakwenda nao Kwa upepo mzuri Na wanafurahi nao; mara upepo mkali unayajia Na mawimbi yanawajia kutoka kila upande, na wanaanza kufikiri ya kwamba wametingwa. (hapo ndipo) wanapomuomba mwenyezi Mungu kwa kumtakasia utii, wakisema: “Ukituokoa katika haya bila shaka tutakuwa miongoni mwa wanaoshukuru.”

Lakini anapowaokoa, mara wanafanya maasi (tena) katika ardhi bila haki. “Enyi watu! Jeuri zenu zitakudhuruni wenyewe. Na starehe (chache tu) za maisha ya dunia, kasha marejeo yenu yatakuwa kwetu. Hapo tutakuambieni (yote) mliyokuwa mkifanya.” (Surah Yunus: 22-23)

Na inapokufikieni taabu katika bahari, hupotea wale mnaowaita isipokuwa Yeye tu. Lakini anapokufikisheni salama nchi kavu, mnakengeuka. Ama mwanadamu ni mwingi wa kukanusha. Je! Mmesalimika kuwa hatakudidimizeni upande wa nchi kavu au kuwaletea tufani la kokoto, kisha msipate wa kutegemea? (Surat al-Isra: 67-68)

Kama vile imesisitizwa kwenye aya hii, vipi mtu atakuwa na uhakika kwamba hatakumbwa na shida kama hiyo au zaidi ya hiyo kwa mara nyingine. Na pia vipi mtu atakuwa na uhakika kuwa ataokolewa tena. Bila shaka hakuna aliye na uhakika kuwa mambo haya hayawezi kutendeka. Kwani mwishowe kila mtu atakufa wakati wake ukifika. Na majuto hayatakuwa na manufaa yoyote.

Na hii ndio hali inayowakumba wale ambao hawaambatanishi maisha yao na dini. Mwenyezi Mungu Anaeleza hali hii kama ifuatavyo:

Na dhara inapomgusa mtu hutuomba (anapolala) ubavu, au hali ya kukaa au kusimama. Lakini tunapomuondolea dhara yake hupita (akafanya yake atakayo) kama kwamba hakutuomba tumuondeshee dhara iliyompata. Namna hivi wamepambiwa wapitao mipaka yale waliyokuwa wakiyatenda. (Surah Yunus: 12)

Yakiwapata watu madhara humuomba Mola wao kwa kumnyenyekea, kisha Anapowaonjesha rehema Yake, hapo baadhi yao mara humshirikisha Mola wao. (Surat ar-Rum: 33)

Watu waliotajwa katika aya hizi ni wale wanamrudia Mwenyezi Mungu wakiwa na matatizo. Na pindi shida zao zikiondolewa wanasahau ahadi walizoweka kwa Mwenyezi Mungu na kukosa shukrani. Hii yaonyesha kwamba majuto waliyokuwa nao ni kwa sababu ya kutokuwa na uwezo wa kujiokoa.

Lakini kwa upande mwingine majuto ya waumini ni tofauti na vile tumetaja hapo juu kwani majuto yao ni ya manufaa. Majuto ya kweli hayasauliki haraka. Majuto hayo huwa ni ya mabadiliko makubwa pamoja na kurekebisha tabia ya mtu. Yeyote ambaye ana majuto ya kweli kwa moyo wake ataishi maisha yake yote kulingana na maamrisho ya Mwenyezi Mungu akitarajia rahma na msamaha wa Mwenyezi Mungu. Anapopata neema harudi kwa makosa aliyokuwemo kwa anaona huo ni ukosefu wa shukrani na itakuwa ni hasara kwake.

Mwenyezi Mungu Anaeleza hali ya kisaikolojia ya watu wanaokabiliwa na mauti wakiwa kwenye meli ili iwe onyo kwa watu wote. Hii ni kwa sababu hali hii hupatikana kwa kila binadamu. Kwa hivyo ili kunufaika na funzo lililotajwa kwenye aya zilizotajwa, ni lazima kuepukana na mambo mabaya ya kiroho na kujihesabu nafsi yake na kisha kujiuliza swali hili:

“Nafsi yangu ingekuwa kwa hali gani kwama ningekumbwa na mambo hayo.? Je nini ningelifanya ili nionyeshe kujuta? Ni mabadiliko gani ningefanya kwa tabia yangu kama nikiokolewa? Ni maasi gani ningeepukana nayo na nini ningeazimia kufanya.”

Ni vizuri kutafakari kuhusu haya mambo hata kama humo hatarini kwani yaweza kuja wakati wowote na pia yawezekana kwamba hutawahi kupata hatari kwa maisha yako. Lakini ukweli ni kwamba kifo kifikapo, mtu atajikuta ghafla amezungukwa na malaika wa kifo. Na wakati huo atafahamu ukweli wa kifo na kama hakuishi kulingana na maamrisho ya Mwenyezi Mungu kwa hakika, atakuwa ni mwenye kujuta.

Ili kuepukana na majuto ya hapa duniani na akhera, kitu cha pekee cha kufanya ni kumrudia Mwenyezi Mungu, kufuata maamrisho ya Mwenyezi Mungu kama vile imenukuliwa katika Qurani. Mauti yapo karibu sana, kwa hivyo binadamu asichelewehe kufanya mambo ambayo anafaa kuyafanya. Lazima aazimie kufanya matendo mema kwa subra na bidii. Ni lazima mtu awe na ikhlasi na kuwa karibu na Mwenyezi Mungu kama vile anavyohisi wakati akiwa kwenye shida.

Ni muhimu kukumbuka kwamba lengo la kuumbwa binadamu ni kumuabdu Mwenyezi Mungu na kuwa mja mwema atafutaye radhi ya Mwenyezi Mungu. Mambo mengine duniani kama vile mali, familia, kazi n.k ni namna ya kumfikisha mja karibu na Mwenyezi Mungu. Na wote wanaotafuta vitu hivi na kusahau kwamba wamepewa neema na Allah ili wamshukuru, watakuwa wenye kuhasirika. Manufaa ya muda yanayopatikana duniani hayatakuwa na maana siku ya akhera. Katika Qurani Mwenyezi Mungu anasema kwamba hawa ni watu watakaokuwa na huzuni kubwa.

Sema: Je! Tukujulisheni wenye hasara katika vitendo (vyao)? Hao ambao bidii yao (hapa duniani) imepotea bure katika maisha ya dunia, nao wanafikiri kwamba wanafanya amali njema! Hao ni wale waliozikataa (waliozikanusha) Ishara za Mola wao na (wakakataa) kukutana naye. Kwa hivyo vitendo vyao vimeharibika, wala hatutawasimamishia mizani Siku ya Kiyama (Surat al-Kahf: 103-105)

Mradi mtu anafikika kiwango cha kuridhiwa na Mwenyezi Mungu hapa duniani kupitia tabia njema na vitendo vyema, Mwenyezi Mungu atamlinda duniani na akhera. Lakini akipoteza fursa hii duniani, atajuta sana wakati malaika wa kifo wanapomjia. Fursa hii itakuwa vigumu kulipizwa na itakuwa ni majuta ya kudumu –isipokuwa mapenzi ya  Mwenyezi Mungu. Katika Quran Allah Anaeleza majuto siku watu watahisi wakiwa mbele yake hivi:

Atasema: “Laiti ningalitanguliza (wema) kwa ajili ya uhai wangu (huu wa leo)”. (Surat al-Fajr: 24)

... na akawa anasema, “Laiti nisingalimshirikisha Mola wangu na yoyote!” (Surat al-Kahf: 42)

... “Laiti ningalishika njia (ya haki nikawa) pamoja na Mtume!”(Surat al-Furqan: 27)

Yeyote ambaye hangependa kunena maneno haya ni lazima achukue nafasi wakati huu ajisalimishe kwa Mwenyezi Mungu na aishi kulingana na sheria Alizoziweka Muumba wetu.

Ni lazima kujihadhari na majuto anayohisi mtu hapa duniani

Maisha ya duniani ni fursa nzuri aliyopewa mwanadamu ili apate maisha mema na ya kudumu ya akhera.

Wale ambao hawatumii hii fursa na wanaishi maisha yasiyoambatana na dini ya Kiislamu watajuta kuishi kwao duniani watakapoona adhabu ya akhera. Hii ni kwa sababu walionywa mara nyingi na kufahamishwa aina mbili ya makazi - Janna (Pepo) na Jahannam (moto). Na pia walifahamishwa kuwa nyenendo zao ndizo zitaamua makazi gani watachuma. Kama vile anatufahamisha Mtume Mtukufu (s.a.a.s) : “ dunia ni shamba la akhera.” (Ihya’ al-ulum ) .

Mwenyezi Mungu Mkarimu Anawapa binadamu mafunzo ya majuto duniani kwa kusisimua fikra na hisia zao ili wasije kufikia kiwango hiki kibaya. Na pia Mwenyezi Mungu Anawapa watu muda maalum ili wajitakase kutokana na makosa yao na tabia mbaya. Kila binadamu katika maisha yake, anapewa fursa ya kutubu na kuishi maisha yaliyobaki kwa njia ya Mwenyezi Mungu.

Ukizingatia haya utaona kwamba hisia ya majuto ni fursa kubwa ambayo Mwenyezi Mungu amempa binadamu. Hii ni kwa sababu yeyote anayejuta kwa moyo wake wote na kumrudia Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu humpa uongofu wa kudumu kwa ikhalsi yake. Kinyume cha hayo, yeyote anepuuza onyo na fursa hii, basi adhabu yake itakuwa kubwa na hataokolewa kutokana na huzuni isipokuwa kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu.

Katika Qurani, Mwenyezi Mungu Anatuonyesha mifano ya watu waliojuta makosa yao. Hizi hisia za majuto ziliwapelekea kikundi cha watu kumrudia Allah na Akawaokoa

Bila Shaka Mwenyezi Mungu Amekwisha pokea toba ya Mtume na Muhajiri na Ansari waliomfuata yeye (Mtume ) katika ile saa ya dhiki; wakati ambao nyoyo za kundi moja miongoni mwao zilikuwa karibu kugeuka (kufuata ukafiri); basi akawaelekea (Mwenyezi Mungu) kwa rehema. Kwa yakini yeye  (Mwenyezi Mungu) kwao ni Mpole (na) Mwenye rehema.

Na (pia akawaelekea kwa rehema) wale watatu walioachwa nyuma (kukubaliwa toba yao kwa yale makosa yao makubwa waliyoyafanya); hata ardhi ikawa finyu juu yao, pamoja na wasaa wake; na nafsi zao zikadhikika juu yao, na wakayakinisha ya kwamba hapana pa kumkimbilia Mwenye Mungu ila (kuelekea) Kwake, kisha (Mwenyezi Mungu) akawaelekea ili wapate kutubu. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye apokeaye toba na Mwenye rehema. . (Surat at-Tawba: 117-118)

Kama vile tunafahamu kutokana na aya hizi, watu watatu walioachwa nyuma, walipata majuto makubwa kwenye nyoyo zao. Na kwa hivyo walitambua kuwa njia pekee ya kujiokoa ni kuomba msamaha na kumrudia Mwenyezi Mungu. Ni majuto haya ya ukweli ambayo huwahamasisha na kuwabadilisha watu na pia kuwafanya warekebishe makosa yao. Watu aina hii wataishi maisha ya kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu rehema Zake. Mwenyezi Mungu Anatufahamisha katika Qurani kwamba kwa hakika anakubali msamaha kutoka kwa waja wake na kuwasamehe:

Ila Yule atakayetubia na kuamini na kufanya vitendo vizuri; basi hao ndio Mwenyezi Mungu atawabadilishia maovu yao kuwa mema; na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe (na) Mwingi wa kurehemu.

Na aliyetubia na kufanya wema, basi kwa hakika yeye anatubu kwa Mwenyezi Mungu toba ya kweli. (Surat al-Furqan: 70-71)

Na wale waliotenda maovu, kisha wakatubiya baada yake na wakaamini, hakika Mola wako baada ya hayo ni mwenye kusamehe mwenye kurehemu (Surat al-Araf: 153)

Na hakika Mimi ni Mwenye kusamehe sana kwa anayetubia na kuamini na kutenda mema, tena akashika uwongofu. (Surah Ta Ha: 82)

Vile vile imesimuliwa katika Qurani kwamba watu ambao walitumiliwa na mitume walijuta matendo yao maovu. Kama vile watu wa Nabi Musa (as) ambao hawakuweza kumsubiri arejee kutoka mlima Sinai na wakamsahau Mwenyezi Mungu na wakarudia kuabudu sanamu. Mwenyezi Mungu anaonyesha toba kubwa walioifanya watu hawa kwa madhambi yao:

Na baada yake watu wa Musa walimfanya katika mapambo yao kiwiliwili cha ndama kilichokuwa na sauti. Je, hawakuona kwamba huyo hasemi nao wala hawaongozi njia? Walimfanya (mungu) na wakawa wenye kudhulumu.

Na walipojuta na wakaona kwamba wamekwishapotea walisema: Kama Mola wetu hataturehemu na kutusamehe bila shaka tutakuwa miongoni mwa waliopata hasara (Surat al-A’raf: 148-149                                                                                           

Mwenyezi Mungu anasisitiza tena kwenye Qurani kuhusu hadithi ya wenye shamba. Mwenyezi Mungu aliwapa shamba kama neema. Lakini walikuwa wajeuri na wakaona shamba kama ni lao, na wakasahau kumshukuru Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo adhabu waliyoipata iliwafanya wajute vitendo vyao na kumrudia Mwenyezi Mungu. Aya zinazoeleza kuhusu wenye shamba ni kama ifuatavyo:

Hakika tutawatia kwenye mtihani (Makureshi) kama tulivyowatia mtihanini wenye shamba, walipoapa kwamba watayavuna (mazao yake) itakapokuwa asubuhi (ili wasionekane na maskini wakaombwa). Wala hawakusema: Inshallah. Basi ulilifikia (shamba hilo) msiba mkubwa utokao kwa Mola wako; na hali wao walikuwa wamelala. Ikawa kama iliyong’olewa. Asubuhi wakaitana ya kwamba: “Nendeni mapema kondeni mwenu ikiwa mnataka kuvuna. Basi walikwenda na huku wakinong’onezana ya kuwa: Leo maskini asiingie humo mwenu” na wakenda asubuhi, hali wanadhani kuwa wanao uwezo wa kuzuia. Basi walipoona wakasema: “Bila shaka tumepotea. Bali tumenyimwa. Mbora wao akasema: “Je! Sikukuambieni, (msitie nia mbaya ya kuwazuilia haki yao maskini? Sasa) rejeeni kwa Mola wenu, mtubie kwake.” Wakasema: “Utukufu ni wa Mola wetu! Hakika tulikuwa madhalimu. Basi wakakabiliana kulaumiana. Wakasema: “Hasara yetu! Hakika tulikuwa tumeruka mipaka (ya Mwenyezi Mungu) huenda Mola wetu Atatubadilishia (shamba) lililobora kuliko hili; hakika sisi tunajipendekeza kwa Mola wetu” (Surat al-Qalam: 17-32)

Lakini hali zikibadilika au watu wakipewa fursa, wengi wao husahau onyo ambalo lengo ni kuwafanya wajute, watubie, na kuwafanya watende mambo mema. Wale ambao wanapuuza onyo  na kurudia nyendo zao kwa kweli wataadhibiwa ikiwa hawatatubia kwa wakati kama vile ilitendeka na watu wa Thamud, watu wa Nabi Salih (a.s). Watu hawa walikataa onyo ya Nabi Salih (a.s) mbali na kujua kwamba watajuta kuangamizwa kwao. Kwa hakika Mwenyezi Mungu havunji ahadi yake ya kutekeleza amri Yake. Mwenyezi Mungu Anatujulisha haya ili iwe funzo kwa watu wote:

Akasema: Huyu ngamia jike; awe na zamu yake ya kunywa na nyinyi muwe na zamu yenu ya kunywa katika siku maalum. Wala msimguse kwa ubaya isije ikawashika adhabu ya siku kubwa. Lakini wakamuua wakawa wenye kujuta. Basi ikawashika adhabu. Hakika bila shaka katika hayo ipo ishara, lakini wengi wao si wa kuamini. Na hakika Mola wako ndiye Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu. (Surat ash-Shu'ara: 155-159)

Ni lazima tukumbuke kwamba Mwenyezi Mungu ni Muadilifu na haachi kosa lolote bila kulipiza lakini kwa upande mwingine analipa watu kwa matendo mazuri waliofanya kwa ajili yake. Anawapa habari njema ya rehema na pepo kwa wale wanaomuelekea na kutubia kikweli. Ukizingatia haya ni lazima ujiulize, je waweza kulinganisha majuto ya hapa duniani na majuto ya akhera ambayo ni ya milele? Bila kusahau kwamba majuto ya akhera yatakuwa kwenye jahanam.

Kwa hakika hakuna mtu ambaye angependa kufikia kiwango cha kujuta siku hiyo ya kiyama. Kwa hivyo ni lazima kila mtu atumie fursa aliyonayo akiwa bado duniani. Yeyote anayetumia neema hii ya Mwenyezi Mungu si tu ataokolewa na moto bali pia atapata baraka za hapa duniani na akhera.

Kwa hivyo yeyote ambaye anafanya bidii ya kupata hizi baraka na kuepuka majuto ya watu wa motoni ni lazima ajitakase kwa kumridhisha Mwenyezi Mungu. Na ni lazima afuate ile njia ya  kumtoa kutoka kwa giza hadi kwenye nuru (mwangaza) Mwenyezi Mungu anatuelezea katika aya hizi:

Yeye ndiye anayewaswalia na malaika wake, ili awatoe katika giza na kuwatia katika nuru. Naye ni mwenye kuwarehemu waumini. Maamkuzi yao siku ya kukutana naye yatakuwa ni Salaam na amewaandalia malipo yenye heshima. (Surat al-Ahzab: 43-44)

 

 

   

    
2 / total 6
You can read Harun Yahya's book Usije Ukajuta online, share it on social networks such as Facebook and Twitter, download it to your computer, use it in your homework and theses, and publish, copy or reproduce it on your own web sites or blogs without paying any copyright fee, so long as you acknowledge this site as the reference.
About this site | Tengeneza kurasa yako ya nyumbani | Add to favorites | RSS Feed
Mambo yote yanaweza kuynakiliwa, kuchapwa na kusambazwa kwa kurejea katika kurasa hii
(c) All publication rights of the personal photos of Mr. Adnan Oktar that are present in our website and in all other Harun Yahya works belong to Global Publication Ltd. Co. They cannot be used or published without prior consent even if used partially.
© 1994 Harun Yahya.www.harunyahya.com
page_top