Usije Ukajuta

SHUSHA KITABU

Download (DOC)
Maoni

SURA ZA KITABU

< <
3 / total: 6
USIJE UKAJUTA - Harun Yahya (Adnan Oktar)
USIJE UKAJUTA
   

 


Mwanzo wa kujuta kwa makafiri ni Kifo

Kila nafsi itaonja mauti, na tunakufanyieni mitihani kwa shari na ya kheri; na kwetu (nyote) mtarejeshwa. (Surat al-Anbiya': 35)

Wale ambao hawaamiini akhera wanachukulia mauti kama ndio mwisho wa kila kitu. Hii ni fikra potofu kwani kifo sio mwisho bali ni mwanzo. Kwa waumini ni mwanzo wa maisha mazuri, pepo ya kudumu ambayo haina maovu wala upungufu.Na kwa makafiri ni safari ya kuelekea motoni pahali palipo na adhabu kali.

Wale ambao wanafahamu ukweli huu hupata raha wakati mauti yanapowafikia na kisha maisha ya raha akhera. Lakini kwa upande mwingine, makafiri  watajuta wakifikiwa na mauti na watakumbuka yale waliyoonywa. Watapata adhabu na hawatakuwa na hiari ya kukimbia kwa kadiri Mwenyezi Mungu atapenda.

Hata kama binadamu hapendi kutafakari kuhusu mauti, ni kitu cha lazima. Hii ni kwa sababu Mwenyezi Mungu ameumba kifo kama mwisho wa maisha ya duniani. Hadi leo, hakuna mtu yeyote ambaye ameweza kuepuka kifo. Hakuna cha kuokoa mtu yeyote na kifo, iwe mali, kazi au marafiki wandani. Kwa hakika kila mtu lazima akumbane na mauti. Mwenyezi Mungu aeleza hili katika aya nyingi za Qurani:

Popote mlipo mauti yatakufikieni, hata mkingiwa katika ngome madhubuti . (Surat an-Nisa: 78)

Sema: Hakika mauti mnayoyakimbia, bila ya shaka yatawakuta. Kisha mtarudishwa kwa Mwenye kuyajua ya ghaibu na yanayoonekana. Hapo atawaambia mliyokuwa mkiyatenda. (Surat al-Jumu'a: 8)

Wala Mwenyezi Mungu hataiakhirisha nafsi yoyote inapofika wakati yake; na Mwenyezi Mungu ana habari ya mnayotenda . (Surat al-Munafiqun: 11)

Je! Kutotafakari kuhusu mauti na maisha baada ya kifo kutamuepusha mtu na ukweli? Kwa hakika jawabu ya swali hili ni “La”. Kwa vile binadamu ni mwingi wa kuhangaika kuhusu kifo, la maana kufanya ni kutafakari kila wakati kuhusu kifo na kujiandaa kwa maisha ya akhera, kama vile Mtume Muhammad (s.a.a.s) alituelezea “Tafakari kuhusu kifo kwa wingi. Mwenyezi Mungu hufungua moyo wa yule anayetafakari kuhusu kifo na hufanya kifo chake chepesi” (Imeripotiwa na Abu Huraira)

Wale ambao wanapuuza kutafakari kuhusu maisha ya akhera kwa kupotezwa na mambo ya dunia watashangazwa na mauti. Wale ambao wanasema “ kwa vile bado tuko kwa ujana na lazima tuutumie vizuri na baadaye ndipo tutafikiria kuhusu kifo” watajua kwamba hawatawahi kupata fursa kama hiyo. Hiyo ni kwa sababu mauti yamekadiriwa na Mwenyezi Mungu. Yawezekana mtu afariki kabla hajazeeka. Kwa hivyo kufanya mipango ya baadaye bila ya kutekeleza maamrisho yake kutapelekea mtu kwa majuto makubwa.

Wale ambao huishi maisha yao kinyume na maamrisho ya Mwenyezi Mungu na kutubia wakati wanapoona mauti yako karibu, watakuwa na majuto kama haya. Lakini kutubia kunakotokana na hofu ya mauti bila ya niya safi ya kujitakasa yaweza kukataliwa na Mwenyezi Mungu. Watu kama hawa waliopenda dunia kupita kiasi hutaka kuokolewa mauti yanapokaribia na hii haitowafaidi na lolote. Mwenyezi Mungu anajua niya yao mbaya kwani Yeye Mwenyezi Mungu yuko karibu na binadamu zaidi kuliko mshipa wa damu Anajua yaliyomo ndani ya binadamu pamoja na fikra zake za ndani na siri zake za ndani. Mwenyezi Mungu Anatufahamisha katika Qurani kwamba Hatakubali tauba inayotokana na hofu ya mauti kwa dakika ya mwisho.

Na si toba ya wale ambao hufanya maovu mpaka mmoja wao akafikiwa na mauti akasema: sasa mimi nimetubia, wala ambao hufa wakiwa makafiri. Hao tumewaandalia adhabu iumizayo(Surat an-Nisa: 18)

Na imetajwa katika aya nyingi kwamba watu kama hawa ambao nia yao si safi wakipewa fursa nyingine wao hurudia nyendo zao za ukafiri.

Na ungeliona watakaposimamishwa motoni waseme: Laiti tungerudishwa (duniani) wala hatutakadhibisha ishara za Mola wetu na tutakuwa katika wanaoamini. Bali yamewadhihirikia waliyokuwa wakiyaficha zamani. Na kama wangalirudishwa, bila shaka wangeyarudia yale waliyokatazwa na hakika wao ni waongo. (Surat al-An'am: 27-28)

Kwa hivyo ni makosa kuwa na itikadi kwamba ‘nitatubia ikifika wakati mwafaka’ kwani fikra kama hii haitamuokoa mtu kutokana na adhabu ya moto. Basi ikiwa mtu hataki kupata adhabu kali ya milele baada ya ya kifo, ni lazima aishi maisha yenye lengo, akijua kwamba bila shaka atakutana na Mwenyezi Mungu na atatoa hesabu ya vitendo vyake.

Majuto ya makafiri wakati wa mauti

Watu wengi maishani mwao wamekuwa wakikumbushwa kuhusu pepo na jahanam na kwamba lazima wajitayarishe kwa maisha ya akhera. Lakini makafiri wanafunga masikio yao kwa maonyo haya. Wakati wanafikiwa na mauti, watakiri kwamba walijipelekea wenyewe kwenye uangamizi. Hakuna aliyewalazimisha, wao wenyewe kwa chaguo lao, wamefikia mwisho mbaya. Wakati wa mauti makafiri wanaanza kuumia kwa huzuni. Hofu kubwa inayowakumba mwanzo wa mauti yao ni ishara ya adhabu ambayo Mwenyezi Mungu anaielezea katika Qurani akisema:

Na utakapoambatanishwa muundi kwa muundi. Siku hiyo ndiyo kupelekwa kwa Mola wako! Basi hakusadiki, wala hakuswali. Bali alikanusha, na akageuka. Kisha akenda kwa watu wake kwa matao. Ole wako, tena ole wako! Kisha ole wako, tena ole wako! (Surat al-Qiyama: 29-35)

Ni lazima tujue kwamba ni makafiri ndio wanapata adhabu ya hofu hii. Waumini wanaishi maisha yao kutenda mema ili kumridhisha Mwenyezi Mungu na kupata mapenzi Yake. Kwa sababu hii kila mara wao wana matumaini.  Kinyume na makafiri ambao hupata majuto makubwa wanapojiwa na mauti. Lakini kwa bahati mbaya majuto haya hayaondoshi adhabu kwani ni majuto ya kuchelewa. Katika Qurani imetaja kwamba wakati makafiri wanafikiwa na mauti roho zao hutolewa kwa uchungu na uzito.

… Na kama ungewaona madhalimu watakapokuwa katika mahangaiko ya mauti, na Malaika wamewanyoshea mikono yao (na kuwaambia) “zitoeni nafsi zenu! Leo mtalipwa adhabu ifedheheshayo kwa sababu ya yale mliyokuwa mkiyasema juu ya Mwenyezi Mungu pasipo haki, na kwa vile mlivyokuwa mkizifanyia kiburi Aya Zake,” (Surat al-An'am: 93)

Basi itakuwaje (hali yao), Malaika watakapoifisha? watawapiga nyuso zao na migongo yao. (Surah Muhammad: 27)

Hakika ni vigumu sana kuelewa yale yanayowapata makafiri wakati wa kifo. Lakini Mwenyezi Mungu Anatuonyesha picha ili mwanadamu atafakari na kuepuka kufikiwa na jambo kama hili wakati wa mwisho. Malaika wa mauti, kama vile aya zinatueleza watatoa roho za makafiri ilihali wakiwapiga kwa nyuso zao na migongo yao. Wakati huo, watapata machungu ya kimwili ikiandamana na majuto makubwa kwani watafahamu kwamba hawatapata fursa ya kurudi duniani.

Wakati wa mauti, mwanadamu ataona wazi yale ambayo atakumbwa nayo. Huu ndio mwanzo wa maisha ya milele. Kifo ni njia ya kuvuka tu kwani ni kutolewa roho kwenye kiwiliwili.

Kulingana na adhabu wanayoipata, makafiri wanafahamu kwamba adhabu hiyo ni ya kudumu. Wale wote walioishi maisha yao bila ya kufuata maamrisho ya Mwenyezi Mungu wanaanza kumuomba Mwenyezi Mungu msamaha na amani. Wanamuomba warudishwe duniani ili wafanye matendo mema ambayo hawangeweza kufanya. Lakini matakwa yao hayatakubaliwa “kwani walipewa maisha ya kutosha ili wapate mawaidha.”  kama vile Mwenyezi Mungu Anataja kwenye aya. Walipewa bishara ya pepo na onyo kuhusu jahannam lakini waliyapa mgongo maneno ya ukweli. Mwenyezi Mungu anasema kwamba watakataa ukweli lau wakipewa fursa nyingine.

Hata yanapomfikia mmoja wao mauti husema: “Mola wangu! Nirudishe (ulimwenguni). Ili nifanye mema sasa katika yale niliyoyaacha. (Hujibiwa na Malaika akaambiwa) “Hapana!” Hakika hili ni neno tu analolisema yeye......(Surat al-Muminun: 99-100)

Makafiri kwa makusudi walikataa kumsujudia Mwenyezi Mungu, na kukataa kufuata maamrisho Yake na pia kutokuwa na tabia nzuri. Mwenyezi Mungu Anasema katika Qurani kwamba wakati mauti yanawafikia hawawezi kamwe kumsujudia.

Hiyo siku kutakayokuwa na mateso makali, na wataitwa kusujudu lakini hawataweza. Macho yao yatainama chini; unyonge utawafunika.  Na hakika walikuwa wakiitwa kusujudu walipokuwa salama (na walikataa) (Surat al-Qalam: 42-43)

Nukta nyingine ya kuongezea ni kwamba makafiri wanapojuta wakati wa mauti wanafahamu kwamba ahadi za Mwenyezi Mungu ni za kweli. Kwa upande mwingine waumini ambao hawakuaminiwa na makafiri na pia kufanyiwa masikhara wakiwa duniani, hawapati huzuni wanayoipata makafiri siku kama hiyo. Waumini wanalipwa malipo mema kwa sababu umri wao wote waliishi wakitaka radhi za Mwenyezi Mungu. Kinyume na makafiri, roho za waumini zinatolewa kwa upole bila uchungu. (Surat an-Naziat: 2). Kama vile Mwenyezi Mungu Anataja kwenye aya, Malaika wanawasalimia waumini na kuwapa bishara ya pepo.

Wale ambao Malaika huwafisha katika hali njema, wakasema: “Amani iwe juu yenu; ingieni Peponi kwa sababu ya yale (mema) mliyokuwa mkiyatenda. (Surat an-Nahl: 32)

Na hii ni adhabu ya kisaikolojia kwa makafiri. Walipewa fursa sawa ambayo walipewa waumini duniani. Lakini wao waliuza akhera ya pepo kwa maisha mafupi ya dunia. Licha ya kukumbushwa kwamba dunia ni pahali pa mtihani kwa mwanadamu na kwamba maskani ya kweli ni akhera, wao walijifanya kutojua. Kwa hivyo hawakufanya matendo ya kustahikia pepo. Makafiri wanapoona mazuri wanaopata waumini, majuto yao huongezeka.

Mwenyezi Mungu asema katika aya moja:

Je! Wanafikiri wale waliofanya maovu kuwa tutawafanya kama wale walioamini na kutenda mema kwamba maisha yao na mauti yao yawe sawa? Ni mabaya wanayoyahukumu. (Surat al-Jathiyya: 21)

Kwa hivyo kila mtu atalipwa vilivyo, wema na bishara na waovu kwa adhabu kali.

Hofu itawajaa makafiri zaidi wakijua kuwa wametayarishiwa Jahannam baada ya kuonja uchungu wa mauti. Hakika huo uchungu unawaashiria adhabu inayofuatia.

Majuto haya ya makafiri ambayo yanaanza na mauti yatadumu kama vile atataka Mwenyezi Mungu, watabaki kwenye adhabu ya kudumu na hawataokolewa na kujuta.

Lakini  kila binadamu anaweza kuepuka adhabu ya majuto makubwa. Kungoja wakati wa mauti si njia peke yake ya kuweza kujua uhakika wa mauti na maisha ya baadaye. Kwa waumini, ahadi ya Mwenyezi Mungu inatosha. Baada ya kifo, uadilifu wa Mwenyezi Mungu ndio utabaki; makafiri wataadhibiwa kwa moto nao waumini watalipwa kwa pepo.

Kwa hivyo jambo la hekima analopaswa kufanya mtu kabla hajafikiwa na mauti ni kuomba kinga kutoka kwa Mwenyezi Mungu na kumuomba msamaha wake. Na pia lazima mtu azingatie Qurani ambayo ndio njia pekee ya kuongoza wanadamu kwa njia iliyonyooka na pia kuelewa na kufuata sunnah ya Mtume Mtukufu (s.a.a.s). Badala ya kuhepa kutafakari kuhusu mauti, mtu atapata faida ikiwa atafikiria kuhusu mauti na kutenda mema.

Yule ambaye anamuelekea Mwenyezi Mungu atapata radhi katika dunia na akhera na ataingia pepo, akiwa ameridhia

Ewe nafsi yenye kutua! Rudi kwa Mola wako, hali ya kuwa utaridhika (kwa utakayopata) na (Mwenyezi Mungu) aridhike nawe. Basi ingia katika (kundi la) waja Wangu (wazuri) Uingie katika Pepo Yangu. (Surat al-Fajr: 27-30)

Njia ya kuokolewa na majuto na kupata maisha mazuri ya akhera ni kutafakari kuhusu mauti na akhera na kufuata njia ya Mwenyezi Mungu, Muumba wa binadamu.

 

 

   

    
3 / total 6
You can read Harun Yahya's book Usije Ukajuta online, share it on social networks such as Facebook and Twitter, download it to your computer, use it in your homework and theses, and publish, copy or reproduce it on your own web sites or blogs without paying any copyright fee, so long as you acknowledge this site as the reference.
About this site | Tengeneza kurasa yako ya nyumbani | Add to favorites | RSS Feed
Mambo yote yanaweza kuynakiliwa, kuchapwa na kusambazwa kwa kurejea katika kurasa hii
(c) All publication rights of the personal photos of Mr. Adnan Oktar that are present in our website and in all other Harun Yahya works belong to Global Publication Ltd. Co. They cannot be used or published without prior consent even if used partially.
© 1994 Harun Yahya.www.harunyahya.com
page_top