Usije Ukajuta

SHUSHA KITABU

Download (DOC)
Maoni

SURA ZA KITABU

< <
4 / total: 6
USIJE UKAJUTA - Harun Yahya (Adnan Oktar)
USIJE UKAJUTA
   

 


Majuto Siku ya Kiyama

Na litapigwa baragumu watazimia waliomo mbinguni na waliomo ardhini ila Yule amtakaye Mwenyezi Mungu. Tena litapigwa mara nyingine, ndipo watasimama wakiangalia. Na ardhi (siku hiyo) itang’aa kwa nuru ya Mola wake, na daftari (ya vitendo) itawekwa; na wataletwa Manabii na mashahidi, na kutahukumiwa baina yao kwa haki wala hawatadhulumiwa. Na kila nafsi italipwa kwa yale iliyoyafanya, naye (Mwenyezi Mungu) anajua sana wanayotenda.  (Surat az-Zumar: 68-70)

Wote ambao waliishi duniani watafufuliwa siku ya kiyama. Wakati wa kufufuliwa ni wakati mgumu kwa makafiri. Mwenyezi Mungu katika Qurani Anataja hofu na mazungumzo ya kushangaa baina ya makafiri wakati wa kufufuliwa

Wanasema, “Ole wetu! Nani aliyetufufua malaloni petu?” “Haya ndiyo yale anayoahidi (Mwenyezi Mungu) Mwingi wa rehema na waliyoyasema kwa haki Mitume.” (Surah Ya Sin: 52)

Na itafika ile ahadi ya haki. Hapo ndipo yatakodoka macho ya wale waliokufuru (wakisema): “Ole wetu! Bila shaka tulikuwa katika mughafala na (Jambo) hili, bali tulikuwa madhalimu (wa nafsi zetu) (Surat al-Anbiya': 97)

Matumizi ya maneno “Ole wetu” yanaashiria hofu kubwa na kutetemeka kwa makafiri. Wakati wa kufufuliwa, watajua kwamba wale waliowaonya kuhusu akhera walikuwa wakweli. Kwa masikitiko makubwa, wanafahamu sasa kwamba onyo hizo zitaonekana moja baada ya nyengine. Wakati huu wote hawatakuwa na njia ya kutoroka wataingizwa kwa adhabu ambayo hawakudhania mbeleni kama ni ukweli

Baada ya kufufuliwa, makafiri watasimamishwa mbele ya Mwenyezi Mungu. Kisha watahitajika kutoa hesabu  ya yale waliyofanya duniani na kisha uamuzi utafanywa vilivyo. Kwa sababu hii, wataletwa mbele ya Mwenyezi Mungu pamoja na wenye kiburi wale ambao walipitisha mipaka alizoweka Mwenyezi Mungu.

Siku itakapopigwa parapanda nanyi mtafika makundi makundi (Surat an-Naba: 18)

Kaitika hiyo siku ya kiyama, makafiri watafahamu kwamba hakuna jambo la muhimu isipokuwa kupata radhi za Mwenyezi Mungu na kuepukana na hasira Zake. Hili pia limetajwa kwenye hadithi ya Mtume Mtukufu (s.a.a.s) ambapo alitoa mfano wa kafiri anapoulizwa siku ya kiyama:

Kafiri ataletwa Siku ya Kufufuliwa na ataulizwa. “ Je! Lau ungekuwa na dhahabu kiasi cha dunia nzima, je ungetoa kuokoa nafsi yako? Atajibu: “Naam” Kisha ataambiwa, “ Uliulizwa ufanye jambo lepesi kuliko hilo (maana kuukubali Uislamu, lakini ulikataa)

Majuto yao yanaongezeka kwa kuwa hawakuzingatia ishara za uwezo wa Mwenyezi Mungu na kuwepo kwake zilikuwa dhahiri. Siku hiyo wataona kwa uwazi kwamba walipoteza fursa hii. Majuto yao yataonekana namna wanazungumza.

Na siku (hiyo) dhalimu atajiuma mikono yale na huku akisema : “Laiti ningalishika njia (ya haki nikawa) pamoja na Mtume!” Ee ole wangu! Laiti nisingalimfanya fulani rafiki. Amenipoteza nikaacha mawaidha baada ya kunijia;” na kweli shetani anamtupa binadamu. (Surat al-Furqan: 27-29)

Siku ya kiyama, makafiri watajishughulisha na shida zao mpaka watasahau mwito wa watoto wao, wake zao, mama zao na baba zao. Tunafahamishwa kwenye Qurani kwamba:

Basi itakapokuja sauti kali iumizayo mashikio. Siku ambayo mtu atamkimbia nduguye, na mamaye na babaye, na mkewe na wanawe. Kila mtu miongoni mwao siku hiyo atakuwa na hali itakayomtosha mwenye, (hana haja ya mwenziwe) (Surah Abasa: 33-37)

Fikra ya nasaba au familia inakosa maana. Toka hapo kitu ambacho anatafuta ni kuokolewa na adhabu ya Mwenyezi Mungu. Kwa kuwa hili ndilo muhimu siku hiyo, makafiri watakuwa radhi kutoa fidia watoto wao wenyewe, wake zao, ndugu zao n.k

Siku mbingu zitakapokuwa kama shaba iliyoyayuka. Na milima itakuwa kama sufi. Wala jamaa hatamuuliza jamaa (yake). Watafanya waonane. Mwenye kosa atatamani ajikomboe katika adhabu ya siku hiyo kwa kuwatoa watoto wake. Na mke wake na ndugu yake. Na jamaa zake waliomzunguka kwa kila upande. Na (kuvitoa) vyote vilivyomo katika ardhi, kisha aokoke. . (Surat al-Ma'arij: 8-14)

Kwa hakika juhudi hizi za makafiri zitaambulia pa tupu. Lengo kubwa la makafiri hapa duniani lilikuwa ni kukusanya mali, kuwa na kazi, na watoto. Waliishi maisha yao wakitafuta malengo haya. Lakini siku ya kiyama watafahamu kwamba fikra hizi zote hazina thamani yoyote. Siku ya kiyama ni siku makafiri watatamani kutokomea. Lakini kwa upande wa waumini, ni wakati waliousubiri kwa hamu na gamu.Mwenyezi Mungu anaelezea haya katika aya hizi:

Siku hiyo nyuso nyingine zitanawiri. Zitacheka, zitachangamka, na nyuso nyingine Siku hiyo zitakuwa na mavumbi juu yake, Giza Totoro litazifunika. Hao ndio makafiri watenda mabaya. (Surah Abasa: 38-42)

Kwenye Siku ya Hesabu, vitu vya thamani mtu atakuwa navyo ni matendo mema yaliyofanywa kwa ajili ya kupata radhi za Mwenyezi Mungu. Lakini makafiri hawakufanya juhudi yoyote ya kupata thamani hii ambayo ingewapa uokovu wa milele. Hawana tendo hata moja zuri wataweza kuonyesha Siku hiyo kwa Mwenyezi Mungu. Kwa sababu hawakuwa na imani yoyote kwa Mwenyezi Mungu, matendo yote waliyoyatenda hayatakuwa na maana.

Sema: Je! Tukujulisheni wenye hasara zaidi kwa vitendo (vyao)? Hao ambao bidii yao (hapa duniani) imepotea bure katika maisha ya dunia, nao wanafikiri kwamba wanafanya amali njema. Hao ni wale waliozikataa Ishara za Mola wao na kukutana naye. Kwa hivyo vitendo vyao vimeharibika wala hatutawasimamishia mizani siku ya kiyama. (Surat al-Kahf: 103-105)

Wale waliokanusha dini na kuwa na shaka kuwepo siku ya kiyama, hawakufanya matayarisho kwa siku hiyo. Kwa maisha yao yote walijishughulisha kutafuta mali na kufuata matamanio yao. Sasa wanakabiliana na majuto ambayo hawatawahi kujiondoa. Mwenyezi Mungu anataja katika Qurani Akisema:

Wasema: “Ole wetu! Hii ndiyo (ile) siku ya Malipo! (Waambiwe) “Hii ndiyo siku ya Hukumu mliyokuwa mkiikadhibisha.” (Surat as-Saffat: 20-21)

La ziada ni kwamba makafiri watapata matendo yao yote ya ulaghai, ya kukosa shukrani na yote mabaya yatadhihirishwa mbele ya Mwenyezi Mungu. Wao wenyewe watashuhudia madhambi waliyotenda. Mwenyezi Mungu Anaelezea katika Qurani kwamba:

Na watahudhurishwa mbele ya Mola wako safu safu, (na wataambiwa): “Bila shaka mumetujia kama tulivyokuumbeni mara ya kwanza. Bali mlidhani ya kuwa hatukukuwekeni miadi (hii). Na daftari yatawekwa (mbele yao) ndipo utawaona waovu wanaogopa kwa sababu ya yale yaliyomo (daftarini); na watasema: “Ole wetu! Namna gani daftari hili! Haliachi dogo wala kubwa ili inalihesabu” na watakuta yote yale waliyoyafanya yamehudhurishwa hapo; na Mola wako hamdhulumu yoyote. (Surat al-Kahf: 48-49)

 Siku hiyo watu watatoka (makaburini) vikundi – vikundi ili waonyeshwe vitendo vyao. Basi anayefanya wema (hata ) sawa na chembe atauona. Na anayefanya uovu (hata) sawa na chembe atauona. (Surat az-Zilzal: 6-8)

Kama vile anasimulia Mwenyezi Mungu katika Qurani, ni wakati wa makafiri kuona rekodi ya vitendo vyao.

Waumini watapata rekodi zao kwa upande wa kulia ilihali makafiri watapewa kwa upande kwa kushoto. Tangu wakati wa kutolewa roho, makafiri walipata adhabu kubwa na wakati wanapewa rekodi zao ni adhabu nyingine. Wanahepa kuangalia matendo maovu waliyotenda na wanatamani kupotea. Mwenyezi Mungu anaeleza katika aya hizi:

Walakini atakayepewa daftari lake katika mkono wake wa kushoto basi yeye atasema: “Oo! Laiti nisingalipewa daftari langu. Wala nisingalijua ni nini hisabu yangu. Laiti (mauti ) yangemaliza (kila kitu changu). Mali yangu haikunifaa usultani (ukubwa ) wangu umenipotea.” (Surat al-Haqqa: 25-29)

... Siku ambayo mtu atakapoona yaliyotangulizwa na mikono yake miwili, na kafiri atasema: “Laiti ningalikuwa udongo!" (Surat an-Naba: 40)

Lakini atakayepewa daftari lake kwa nyuma ya mgongo wake, basi yeye atayaita mauti na ataingia Motoni. Maana alikuwa na furaha pamoja na watu wake, (na) alidhani kuwa hatarejea (Kwa Mwenyezi Mungu) Kwa nini (asirejee) Mola wake alikuwa akimuona; (Surat al-Inshiqaq: 10-15)

Makafiri wanaposhuhudia haya, wanafahamu fursa waliyopoteza wakiwa duniani na watahisi majuto makubwa. Kuongezea kwa majuto haya, ni pale wanapoona waumini wakistarehe peponi. Na hii ni kwa sababu waliitwa na waumini kwenye njia ya haki lakini walifunga masikio yao kwa ujeuri.

Lakini sasa “Mizani za uadilifu” (Surat al-Anbiya’: 47) zimewekwa. Watu wataelekezwa Motoni au Peponi kulingana na vitendo vyao. Katika Siku ya Kiyama, makafiri wataona kule wanaelekea na hofu itawaingia:

Utawaona (siku ya Kiyama) madhalimu wanavyotetemeka kwa sababu ya yale waliyochuma, nayo yatawatokea tu (Surat ash-Shura: 22)

Uadilifu wa Mwenyezi Mungu utaenea na utakuwa wa kulipwa na pia kuadhibiwa.

Nasi tutaweka mizani za uadilfu siku ya Kiyama, na nafsi yoyote haitadhulumiwa hata kidogo. Na hata kama ikiwa uzito mdogo wa chembe ya khardali nalo tutaileta; Nasi tunatosha kuwa wenye kuhisabu (Surat al-Anbiya': 47)

Njia itakuwa nyepesi kwa waumini lakini ngumu sana na ya uchungu kwa makafiri. Wataulizwa kwa kila neema waliyopewa na Mwenyezi Mungu duniani. Watatoa hesabu ya wakati wao wote; ya kutofuata maamrisho ya Mwenyezi Mungu; ya kutokuwa na shukrani; ya fikra mbovu na matusi; onyo walizopuuza. Zile udhuru walizozitoa duniani hazitakubaliwa kamwe. Mwenyezi Mungu Anaeleza hali makafiri watakuwemu siku hiyo Akisema:

Ole wao siku hiyo hao wanaokadhibisha! Hii ni siku ambayo hawatasema (kitu) Wala hawatapewa ruhusa (kutoa udhuru) wakapata kutoa. Ole wao siku hiyo hao wanaokadhibisha! (waambiwe) : “Hii ni siku ya Hukumu, tumekukusanyeni nyinyi na waliotangulia. Ikiwa mnayo hila ifanyeni juu yangu.” Ole wao siku hiyo hao wanaokadhibisha! (Surat al-Mursalat: 34-40)

Wale makafiri ambao hawatakuwa na matendo mema mbele ya Mwenyezi Mungu “watajua walichotayarishiwa. Mwenyezi Mungu Anaeleza pahali hapa adhabu kama shimo lisilo na mwisho.

Basi Yule ambaye mizani yake itakuwa nzito, huyo atakuwa katika maisha yanayompendeza. Na yule ambaye mizani yake itakuwa nyepesi, huyo maskani yake yatakuwa katika (huo Moto)-Hawiya. Na ni jambo gani litakalokujulisha ni ni hiyo (Hawiya)? Ni Moto uwakao kwa ukali. (Surat al-Qari'a: 6-11)

Ni muhimu kufahamu majuto makubwa watakayohisi makafiri siku ya Kiyama. Yeyote atakayejuta  siku ya Kiyama atakuwa ni wa kuchelewa sana. Yeyote atakayefahamu haya na bila kupoteza wakati akaanza kutenda mambo mema, ataweza kutarajia “Mizani nzito (ya matendo mema) ni hiyo tu itakayoweza kumuokoa mtu kwa majuto makubwa.

 

 

   

    
4 / total 6
You can read Harun Yahya's book Usije Ukajuta online, share it on social networks such as Facebook and Twitter, download it to your computer, use it in your homework and theses, and publish, copy or reproduce it on your own web sites or blogs without paying any copyright fee, so long as you acknowledge this site as the reference.
About this site | Tengeneza kurasa yako ya nyumbani | Add to favorites | RSS Feed
Mambo yote yanaweza kuynakiliwa, kuchapwa na kusambazwa kwa kurejea katika kurasa hii
(c) All publication rights of the personal photos of Mr. Adnan Oktar that are present in our website and in all other Harun Yahya works belong to Global Publication Ltd. Co. They cannot be used or published without prior consent even if used partially.
© 1994 Harun Yahya.www.harunyahya.com
page_top