Usije Ukajuta

SHUSHA KITABU

Download (DOC)
Maoni

SURA ZA KITABU

< <
5 / total: 6
USIJE UKAJUTA - Harun Yahya (Adnan Oktar)
USIJE UKAJUTA
   

 


Majuto kwenye Jahannam

(Moto huo) utakapowaona tangu katika mahali pa mbali, watasikia hasira (yake) na mngurumo (wake) (Surat al-Furqan: 12)

Majuto watakuyokuwa nayo makafiri watakapouona Moto

Hesabu ikishakamilika siku ya Kiyama, watu watakusanywa na kupelekwa Motoni kwenye vikundi. Miongoni mwao watakuwa ni wale walikadhibisha dini na kukataa kuwepo Mwenyezi Mungu na wale walikataa ishara za Mwenyezi Mungu kwa ujeuri. Kutakuwa na wale walifurahia mali na ufahari. Kwa masikitiko vile vitu walivipa umuhimu duniani havitawafaa na kuwaondolea adhabu ya milele. Mwenyezi Mungu anatufahamisha kwenye Qurani kwamba makafiri wote wataingizwa Motoni kwa fedheha. Wenye kuchunga Moto, watawafanya makafiri wakiri makosa yao kwa mara ya mwisho na kuwaingiza ndani. Mwenyezi Mungu kwenye Qurani  anaeleza namna makafiri watapelekwa Motoni:

Na waliokufuru watapelekwa katika Jahanamu makundi kwa makundi; mpaka watakapoifikia itafunguliwa milango yake; na walinzi wake watawaambia: “Je! Hawakukujieni Mitume miongoni mwenu wakikusomeeni Aya za Mola wenu na kukuonyeni mkutano wa siku yenu hii?” watasema: ndiyo, Lakini limetimia neno la adhabu juu ya makafiri. Itasemwa: “Ingieni milango ya Jahanamu mkakae humo.” Basi ni ubaya ulioje wa makazi ya wanaotakabari! (Surat az-Zumar: 71-72)

“Haya ni kwa sababu mlikuwa mkifurahi katika ardhi pasipo haki, na kwa sababu mlikuwa mkijivuna. Ingieni katika milango ya Jahanamu mkakae humo milele; basi ni mabaya yalioje makazi ya wanaotakabari!” (Surah Ghafir: 75-76)

Hakuna mtu yeyote kwenye kikundi atasimama kusema hakuonywa kutokana na hii siku. Hii ni kwa sababu Mwenyezi Mungu ambaye ni muadilifu, aliwatuma mitume kwa kila mtu kumkumbusha kuhusu kuwepo kwa Mwenyezi Mungu, siku ya Kiyama, Pepo na Jahanam. Kwa hivyo, makafiri watakiri kwamba wanastahiki adhabu ya Jahanam.

Walikuwa na kiburi mbali na kuwa walionywa na pia walikataa kumuabudu Mwenyezi Mungu, Yule aliyewaumba, Mwenyezi Mungu Anamjulisha mwanadamu kenye Quran kwamba watu aina hii watadhalilishwa kwenye Jahanam.

Na Mola wenu anasema: “niombeni nitakujibuni. Kwa hakika wale wajuvunao kufanya ibada yangu, bila shaka wataingia Jahanamu, wakifedheheka.  (Surah Ghafir: 60)

Mtume wa Mwenyezi Mungu (saas) pia amesisitiza nukta hii akisema :

Je! Niwajulisheni watu wa Motoni? Itakuwa na kila katili, kila mwenye vurugu, mwenye kiburi na kila mwenye kujivuna (Bukhari)

Walijiona kama wenye nguvu duniani na wakamuasi Mola wetu. Walidhani usultani utawaokoa. Walipokumbushwa kuhusu sifa ya Mwenyezi Mungu ya al-Qahhaar ( Mwenye Nguvu), kuwepo Moto na Pepo, na kuelezwa kufuata njia ya Mwenyezi Mungu walijibu:

 “Mbona Mwenyezi Mungu hatuadhibu kwa haya tunayoyasema?” Basi (moto wa) Jahanamu utawatosha kuwatia adhabu; watauingia; napo ni mahali pabaya sana pa kurudia.  (Surat al-Mujadala: 8)

Kwa sababu ya kuasi kwao, wataingizwa kwenye milango ya Moto na hawataweza kutoka humo isipokuwa Mwenyezi Mungu Akipenda kuwaondoa. Wakati wanapoona moto, watahisi majuto makubwa kwa makosa yao. Mwenyezi Mungu Anaeleza kwenye Qurani kwamba huu ndio wakati watafahamu kwa uwazi kwamba hakuna njia ya kutoka nje ya Moto.

Na wabaya watauona Moto (wakti huo) na watajua ya kwamba wao lazima wataingia humo; wala hawatapata pa kuuepuka. (Surat al-Kahf: 53)

Makafiri wataona ukweli ukiwa wazi wakiwa Motoni, chochote walichojisahaulisha duniani kitakuwa wazi kwao. Watafahamu kuwa waliishi maisha yao kwa malengo ya upuzi na hatimaye watatambua kwamba maisha mafupi ya raha waliyopata duniani ni lazima sasa kuishi kwenye adhabu isiyo na mwisho. Muda walioishi duniani ulionekana mrefu kwao lakini hawakutafakari kuhusu maisha ya akhera. Hawakujiandaa kwa maisha ya akhera ambayo hayana udhaifu  wa mwili, njaa au uchovu lakini wao walichagua maisha ya duniani ambayo hayana raha. Wanapoingia kwenye milango za Moto wanafahamu  kwamba hakuna kuepuka. Na wanadhani kwamba wanaweza kutoa fidia ya kila walichokuwa nacho duniani ili kuokoa nafsi zao. Lakini juhudi zao za upuzi zinaelezwa ifuatavyo:

… Na wale wasiomuitikia, hata kama wangalikuwa na vyote vilivyomo ardhini na (vingine) kama hivyo pamoja navyo, bila shaka wangalivitoa kujikombolea. Hao watakuwa na hisabu mbaya, na makao yao ni Jahanamu. Na ni mahali pabaya palioje! (Surat ar-Rad: 18)

Lakini, juhudi hizi za mwisho zitaambulia patupu wakati wa kuingia Motoni. Mwenyezi Mungu Anatufahamisha kwamba majaribio hayo hayatakuwa na faida yoyote.

“Basi leo hakitapokelewa kwenu kikomboleo wala kwa wale waliokufuru. Makazi yenu ni Motoni; ndio rafiki yenu; nayo ni marejeo mabaya kabisa.” (Surat al-Hadid: 15)

 Kwa hakika kuna sababu inayofanya majaribio hayo yasiwe na manufaa. Mwenyezi Mungu Aliwaonya kuwa kuna Moto walipokuwa duniani. Kila kitu kiliwekwa wazi kwamba hakuna mtu atasaidia mwengine na hakuna atakayeweza kutoa fidia. Aya ambayo Mwenyezi Mungu aliteremsha kuelezeza hoja hii ni:

Na iogopeni Siku ambayo nafsi haitafaa nafsi nyingine cho chote, wala hayatakubaliwa kwake maombezi, wala hakitapokewa kikomboleo kwake; wala hatanusuriwa. (Surat al-Baqara: 48)

Licha ya onyo zote, walisisitiza kukadhibisha kwao na kwa hivyo walijiandalia mwisho huu mbaya. Siku hiyo watakiri kwamba matendo yao yaliyowafanya kuingia Motoni.

Majuto hayo yatakuwa ni ya adhabu ya milele bila kuokolewa isipokuwa kutaka kwa Mwenyezi Mungu. Na watajua nukta muhimu; kwamba lau wangejitolea maisha yao kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu badala ya kufuata malengo duni, wangeingizwa Peponi badala ya Motoni. Kwa sababu ya kutofuata njia sahihi wanapata hasara kubwa.

Mwenyezi Mungu Anataja kwenye aya ya ishirini ya Surat al-Balad “Moto uliofungiwa (kila upande) utakuwa juu yao.” wanapoingia kwenye milango za Moto, watafungiwa ndani. Na mbele ya milango hizo ni adhabu ya Motoni isiyokuwa na mwisho na wataadhibiwa hadi pale anapotaka Mwenyezi Mungu. Kwa makafiri hakuna njia ya kuihepa adhabu hiyo. Mwenyezi Mungu Anauita moto huo ‘Huthwama’

Na ni jambo gani litakalokujulisha ni nini Huthwama? Ni Moto wa Mwenyezi Mungu uliowashwa.ambao unapanda nyoyoni. Hakika huo (moto) watafungiwa. Kwa magogo marefu marefu . (Surat al-Humaza: 5-9)

Adhabu wanayokumbana nayo makafiri Motoni

Kabla hatujataja majuto watakayokumbana nayo makafiri akhera, itakuwa vyema kueleza adhabu ya Motoni. Bila kufahamu aina ya adhabu Motoni, mtu anaweza kughafilika kiwango cha majuto yaliyomo.

Kama tulivyotaja hapo awali, majuto ya makafiri yanaanza pindi wanapouona Moto na majuto ya milele. Mazungumzo baina yao wakiingia Motoni yatakuwa hivi:

Na waliomkufuru Mola wao iko adhabu ya Jahanam (inawangojea) na ni marejeo mabaya yalioje! Watakapotupwa humo watasikia rindimo (mngurumo) lake, nalo lafoka. Unakaribia kupasuka kwa hasira . kila mara litakapotupwa humo kundi (la wabaya ) walinzi wake watawauliza: “Je! Hakuwafikieni Muonyaji? Watasema : “Kwa nini? Alitujia Muonyaji, lakini tulimkadhibisha na tulisema “Mwenyezi Mungu hakuteremsha chochote, nyinyi hamumo ila katika upotofu mkubwa. Na watasema : “ kama tungalikuwa tunasikia au tungalikuwa na akili hatungekuwa katika watu wa Motoni. Wakakiri dhambi zao; basi kuangamia kumewastahikia watu wa Motoni (Surat al-Mulk: 6-11)

Kama vile imetajwa kwenye aya, watakaporushwa kwenye Moto, watasikia mngurumo. Mwenyezi Mungu Anaeleza mngurumo huo kwenye aya ya saba ya Surat al-Mulk kama mngurumo unaofoka

Mngurumo huo utawaingiza hofu kwa makafiri. Katika aya nyingine Mwenyezi Mungu anaeleza kuwa Moto wa jahanam kuwa moto  unaokaribia kupasuka kwa hasira (Surat al-Mulk: 8).

Watakuwa kwenye hali ya taharuki kwani watafahamu kwamba adhabu watakayoipata itakuwa ya kutisha na ya uchungu, imeelezwa kwamba Jahanam ni pahali pabaya pa kuishi.

.....napo ni mahala pabaya pa kurejea (Surah Al 'Imran: 162)

Napo ni pahali pabaya kabisa pa mtu kurudia (Surat an-Nisa: 115)

Na makazi yao yatakuwa Motoni, na ni mabaya yalioje maskani ya madhalimu. (Surah Al 'Imran: 151)

Jahannamu, wataingia; na ni mahali pabaya kabisa pa kukaa (Surah Ibrahim: 29)

Mtume (S.a.a.s) pia ameelezea Jahannam kwenye hadithi zake tukufu kwamba:

Miongoni mwa watu wa Jahannam ni wale wataingizwa motoni hadi kwenye vifundoni vyao , wengine hadi kwenye magoti, wengine hadi viuno na wengine hadi kwenye koo zao . (Muslim)

Wakazi wa Motoni watatupwa mahala hapa pabaya kwa umati. Katika aya inasema “Basi watatupwa humo wao na waaasi (wengine) (Surat ash-Shu'ara: 94)

Hawatapata heshima yoyote Motoni wala rahma. Watakuwa kuni za Moto na wataishi kwenye maumivu na huzuni milele. Mwenyezi mungu anazungumzia haya kwenye aya hizi: 

Hakika nyinyi na wale mnaoabudu, kinyume cha Mwenyezi Mungu, ni kuni za Jahannamu; mtaifikia. (Surat al-Anbiya': 98)

… Na hao (watakuwa) kuni za Moto (Surah Al 'Imran: 10)

Mwenyezi Mungu anatufahamisha kwenye Qurani sampuli za adhabu Motoni. Wengi wa watu wataishi humo milele kumaanisha wataadhibiwa namna atataka Mwenyezi Mungu. Tunaweza kueleza aina za adhabu kama :

Katika aya ya kumi na tatu ya Surat al-Furqan, Mwenyezi Mungu Anaeleza kwamba makafiri watatupwa “mahala pafinyu hali wamefungwa” kwa hakika kufungwa mahala finyu hata kwa dakika chache kunamfanya mtu kuhangaika. Kidogo unaweza kufananisha na  kufungiwa kwa chumba kunahofisha katika dunia. Lakini huwezi kufananisha adhabu ya duniani na ile ya akhera. Watakapofungiwa katika mahala finyu, watapata adhabu ya moto. Na vile watakuwa wamefungwa pamoja hawataweza kusongea na kuhepa kutoka kwenye moto haitowezekana. Kujaribu kutafakari kuhusu kisa hiki kunaleta uchungu

Katika aya nyengine Mwenyezi Mungu anawajulisha makafiri kwamba watabaki kwenye “kivuli cha moshi mweusi sana” (Surat al-Waqia: 43). Kwa kawaida neno kivuli  kinakuwa ni cha kutuliza. Lakini ni kinyume sana kwenye Moto ambako Mwenyezi Mungu Anatujulisha kwamba kivuli hicho si baridi wala cha starehe.

Aina nyingine ya adhabu katika Jahannam ni kukosekana mauti. Kifo ni njia moja ya kuokolewa. Kwa sababu hii Mwenyezi Mungu hatakubali watu wa Jahannam kufariki kama vile anasisitiza katika aya “na mauti yatamjia kutoka kila mahali, naye hatakufa” (Surah Ibrahim: 17).

Mtume Muhammad (s.a.a.s) pia amesimulia kuwa hakuna mauti akhera akisema:

Watu wa peponi watakapoelekea Peponi nao wa Motoni kuelekea Motoni, mauti yataitwa na kuwekwa baina ya Pepo na Moto. Kisha itatangazwa: “Enyi watu wa Peponi! Hakuna mauti tena! Enyi watu wa Motoni! Hakuna mauti tena! Hili litaongeza furaha kwa watu wa Peponi na kuongeza huzuni kwa watu wa Motoni (Muslim)

Katika dunia kuchomwa na moto mkali kunamletea mtu mauti baada ya muda mfupi. Hakuna anayeweza kustahmili moto. Na kama mtu huyo hatakufa na kupata majeruhi peke yake, itachukuwa muda mrefu vidonda kupona vizuri. Lakini katika Motoni, adhabu ya Motoni haina mfano wa moto tunaoujua duniani. Katika Motoni, ngozi zitabadilishwa tena ili kuonja adhabu kali tena. (Surat an-Nisa: 56). Kwa ufupi, watu wa Motoni watapata adhabu ya milele inayosababishwa na Moto hadi kupenda kwa Mwenyezi Mungu.

Mwenyezi Mungu anaelezea aina nyingine ya adhabu inayosababishwa na moto katika aya ya kumi na tatu ya Surat adh-Dhariyat anaposema watu wa Motoni wataadhibiwa na moto. Ni vigumu kuelewa uchungu huo. Ukizingatia kuwa uchungu mdogo anaoupata mwanadamu hapa duniani, anaweza kufahamu mauvimu hayo.

Mwanadamu pia atapata yafuatayo:

Tena katika mnyororo wenye urefu wa dhiraa sabini muingizeni (Surat al-Haqqa: 32)

Hakika sisi tumewaandalia makafiri minyororo na makongwa na Moto mkali (Surat al-Insan: 4)

Na kwa ajili yao (yatakuwapo) marungu ya chuma (Surat al-Hajj: 21)

Siku yatakapotiwa moto katika moto wa Jahanamu, na kwa hayo vikachomwa vipaji vya nyuso zao na mbavu na migongo yao.

Yatamiminwa juu ya vichwa vyao maji yachemkayo. (Surat al-Hajj: 19)

Nguo zao zitakuwa za lami, na Moto utazijaa nyuso zao. (Surah Ibrahim: 50)

Hawatapata kinywaji cha kustarehesha. Siku hiyo ni maji moto (Surat al-Sad: 57) damu na usaha (Surat al-Haqqa: 36) ndio vinywaji vyao.

Na chakula cha watu wa Motoni ni matunda machungu ya mti wa zakkum. Mwenyezi Mungu vipi zaqqum itakuwa adhabu kwa makafiri:

Bila shaka mti wa Zakkum ni chakula cha waasi, (kwa joto lake ni) kama shaba iliyoyayushwa, huchemka matumboni, kama mchemko wa maji ya moto. (kuambiwe) “Mkamateni (huyo asi) na mburureni mpaka katikati ya Jahanamu. Kisha mwagieni juu ya kichwa chake adhabu ya maji ya moto. Onja! Ulikuwa (ukijidai kuwa) wewe ni mwenye nguvu, mhishimiwa! Hakika hii ndiyo ile (adhabu) mliyokuwa mkibishana” (Surat ad-Dukhan: 43-50)

Kutokana na maelezo ya Qurani, tunafahamu kwamba chakula cha Motoni kitakuwa cha kusonga. Watajaribu kunywa maji kwa pupa lakini hawataweza kumeza. Usaha ambao ni kitu kisichopendeza kabisa hapa duniani kwa rangi, ndio chakula cha watu wa Motoni. Hii itakuwa na machungu makubwa lakini kwa kukosa hiari hawatakuna na budi ila kula hivyo hivyo ingawa watakachokula hakitawafaa kwa njaa yao na watakuwa na uchungu wa njaa kwa milele.

Hawatakuwa na chakula isipokuwacha miba. Hakinenepeshi wala hakiondoi njaa. (Surat al-Ghashiyya: 6-7)

Mwenyezi Mungu anaelezea pahala pengine kwenye Qurani kuhusu adhabu ya Motoni akisema:

Wao humo watapiga kelele, (Surat al-Anbiya': 100)

Wakae humo dahari nyingi (karne baada ya karne). (Surat an-Naba: 23)

Humo watakaa milele. Hawatapunguziwa adhabu wala hawatapewa nafasi ya (ya kupumzika) ... (Surah Al 'Imran: 88)

Watataka watoke katika Moto, lakini hawatatoka humo. (Surat al-Maida: 37)

Kwa hakika adhabu hiyo itakuwa ni ya uchungu mkali na majuto kwa makafiri. Ili kutaka kuokolewa wataomba mara nyingi na watakuwa radhi roho zao kutolewa. Mwenyezi Mungu katika Qurani tukufu  Anatufahamisha mazungumzo ya watu wa Motoni akisema:

Na watapiga kelele (kumwambia Yule Malaika anayewaadhibu waseme): Ee Malik! Naatufihse Mola wako!” (Malik )_aseme: “Bila shaka mtakaa humu humu. Kwa yakini tulikuleteeni haki, lakini wengi katika nyinyi mlikuwa mnaichukia haki.” (Surat az-Zukhruf: 77-78)

Kuipa dini mgongo na kukosa kusikiza onyo itakuwa ndio sababu ya kuangamia kwa watu hawa kama vile amesimulia Mwenyezi Mungu katika Qurani. Mwenyezi Mungu naye hatasikiza vilio vyao na atawaweka kwenye adhabu hadi atakapotaka.

Hizi ni baadhi ya adhabu watakazopata wale walimkadhibisha Mwenyezi Mungu na kuwepo Jahanam na Pepo. Na makafiri watakuwa na aina nyingine ya adhabu ambayo ni hisia ya majuto ambayo hakuna atakaye weza kusahau. Na hisia hizi zitaongezeka pale watakapoona kwamba wanapelekwa Motoni, pahala pa kutisha sana. Kama vile imesemwa awali, kila makafiri wataonja adhabu, watakumbuka kwamba lau wangefuata njia ya haki, haya yote hayangewapata lakini hakuna njia ya kuepuka majuto haya.

 

 

   

    
5 / total 6
You can read Harun Yahya's book Usije Ukajuta online, share it on social networks such as Facebook and Twitter, download it to your computer, use it in your homework and theses, and publish, copy or reproduce it on your own web sites or blogs without paying any copyright fee, so long as you acknowledge this site as the reference.
About this site | Tengeneza kurasa yako ya nyumbani | Add to favorites | RSS Feed
Mambo yote yanaweza kuynakiliwa, kuchapwa na kusambazwa kwa kurejea katika kurasa hii
(c) All publication rights of the personal photos of Mr. Adnan Oktar that are present in our website and in all other Harun Yahya works belong to Global Publication Ltd. Co. They cannot be used or published without prior consent even if used partially.
© 1994 Harun Yahya.www.harunyahya.com
page_top