Usije Ukajuta

SHUSHA KITABU

Download (DOC)
Maoni

SURA ZA KITABU

< <
6 / total: 6
|
USIJE UKAJUTA - Harun Yahya (Adnan Oktar)
USIJE UKAJUTA
   

 


Majuto ya Makafiri kwenye Moto

Wakati makafiri wanapata adhabu kali, watakuwa na majuto ya kutoamini kwa Mwenyezi Mungu walipokuwa duniani. Kwa bahati mbaya majuto haya hayatakuwa na faida yoyote. Walipokuwa duniani walipewa fursa nyingi ambazo hawakutumia. Wakati watafahamu haya, watalaumu kila mtu na kila kitu kilichowazuia kuamini kwa Mwenyezi Mungu na siku ya Kiyama na kuwafanya wapende mambo ya dunia sana.

Kulingana na Qurani makafiri watakuwa na hasira kubwa kama vile Mwenyezi Mungu anasema kwenye aya zifuatazo:

Siku ambayo nyuso zao zitapinduliwapinduliwa (zitakapounguzwa ) Motoni, waseme: “Laiti tungemtii Mwenyezi Mungu na tungemtii Mtume.” Na watasema: “Mola wetu! Hakika tumewafuata mabwana wetu na wakubwa wetu, basi wao wametupoteza njia. Mola wetu! Wape hawa adhabu maradufu na uwalaani laana kubwa.” (Surat al-Ahzab: 66-68)

Hata atakapotujia atasema (kumwambia shetani): “Laiti ungalikuwa umbali wa mashariki na magharibi baina yangu na wewe.” Na rafiki mbaya ulioje wewe! (Na Mwenyezi Mungu atawaambia): “Haitakufaeni leo- mlivyodhulumu (nafsi zenu)- kwamba nyinyi mnashirikiana katika adhabu. (Surat az-Zukhruf: 38-39)

Kama vile aya hizi zinaashiria, makafiri wanafikiri wataokolewa kwa kulaumu wale waliowapotosha kutoka kwa njia ya haki. Lakini ukweli ni kwamba Mwenyezi Mungu alimpa kila mtu ubainifu wa kujua njia ya haki. Na pia Mwenyezi Mungu amempa binadamu hiari ya kuamua. Kwa hivyo, mwanadamu amepewa chaguo mbili na elimu ya kujua la kweli na lisilo la ukweli na hivyo basi ni juu yake kuchagua analolitaka. La muhimu ni kwamba Mwenyezi Mungu anajua imani ya mtu au ukafiri wake kwenye moyo wake. Kwa hivyo wale wanaofanya wengine kuingia Motoni na wale wanowafuata wataadhibiwa kwa uadilifu. Siku hiyo hakuna atakaye beba mzigo wa mtu mwingine.

Wakati ule watu hawa walikuwa wakishawishi na kutenda maovu na haikuwajia kwamba siku moja watahukumiwa siku ya Kiyama na hawakuzingatia kabisa. Walihimizana kumkadhibisha Mwenyezi Mungu wakisema, “Nitachukua jukumu la kila unalolifanya” naye Shetani kwa upande mwingine aliwashawishi na kuwaahidi na kuwapotosha. Lakini Mwenyezi Mungu kakita ayah hii , “... na atatujia peke yake.” (Surah Maryam: 80), anatufahamisha kwamba ahadi hizo hazitakuwa na maana.

Siku hiyo makafiri watajiona wakiwa peke yao. Watafahamu jambo la muhimu: mbali na Mwenyezi Mungu binadamu hana rafiki wala mlinzi. Wakiwa Motoni wale watu waliowachukulia ndio wakufunzi wao au marafiki wakiwa duniani watawaacha peke yao. Vile vile shetani, ambaye alimuasi Mwenyezi Mungu , atawakataa na kuwaambia:

Na shetani atasema itakapokatwa hukumu “Mwenyezi Mungu alikuahidini ahadi ya kweli (na leo ameitimiza), nami nilikuahidini; lakini sikukutimizieni. Wala sikuwa na mamlaka juu yenu (ya kukulazimishieni kunifuata), isipokuwa nilikuiteni tu, nanyi mkaniitika. Siwezi kukusaidieni wala nyinyi hamuezi kunisaidia. Hakika mimi nilikataa kunishirikisha kwenu kutoka zamani.” Kwa yakini madhalimu watakuwa na adhabu iumizayo. (Surah Ibrahim: 22)

Hivyo ndivyo itaonekana ukosefu wa uaminifu kwa wale waliowachukua kama marafiki ni hii itakuwa yaongeza majuto kwa makafiri. Je! Hawaoni kwamba hakuna wa kumkimbilia isipokuwa Mwenyezi Mungu. Lakini watakapojua kuwa kufahamu hili halitawapunguzia shida zao watakereka zaidi. Siku hiyo watagombana wao kwa wao wakikiri madhambi yao. Mwenyezi Mungu anaeleza haya kwenye aya hii:

Watasema: (kuwaambia wale waliokuwa wakiwaabudu) – na hali ya kuwa wagombana humo. “Wallahi, kwa yakini tulikuwa katika upotofu ulio dhahiri. Tulipokuwa tukikufanyeni sawa na (Mwenyezi Mungu) Mola wa walimwengu wote. Na hawakutupoteza ila wale waovu; basi hatuna waombezi, wala rafiki halisi. Laiti kama tungalikuwa na marejeo (ya kurejezwa ulimwenguni) tungekuwa miongoni mwa waumini.” (Surat ash-Shu'ara: 96-102)

Kama vile imeelezwa hapo juu kwenye aya, makafiri, kwa majuto makubwa, watatamani kurejeshwa duniani ili wafanye matendo mema ambayo yatawaletea manufaa akhera. Lakini, ni matamanio yasiyokubalika. Watafahamu kwamba kila kitu walichokimbilia duniani hakina maana ikiwa ni utajiri, urembo, kazi n.k Mwenyezi Mungu anaeleza kwenye Qurani majuto ya makafiri Akisema:

Walakini atakayepewa daftari lake katika mkono wake wa kushoto basi yeye atasema: “Oo! Laiti nisingalipewa daftari langu; wala nisingalijua ni nini hisabu yangu, laiti (mauti) yangemaliza (kila kitu changu), mali yangu haikunifaa, usultani (ukubwa) wangu umenipotea (kusemwe) : “Mkamateni na mtieni makongwa, kasha mtupeni Motoni, tena katika mnyororo wenye urefu wa dhiraa sabini muingizeni. Hakika yeye alikuwa hamuamini Mwenyezi Mungu Mtukufu. Wala hahimizi kulisha maskini. Basi leo hapa hana rafiki mpenzi. (Surat al-Haqqa: 25-35)

... Basi Siku hiyo italetwa Jahanamu. Siku hiyo mwanadamu atakumbuka, lakini kukumbuka huko kutamfaa nini? Atasema: “Laiti ningalitanguliza (wema) kwa ajili ya uhai wangu (huu wa leo)”

Vile vile makafiri watakapoona watu wa Peponi wana furaha kubwa, majonzi na masikitiko yao yataongezeka. Wataona tofauti kubwa ya maisha ya watu wa Peponi na yao. Mwenyezi Mungu Anatuonyesha tofauti ya watu wa Peponi na watu wa Motoni.

Mwenyezi Mungu Anatuelezea kwenye Qurani hali ya watu wa Motoni akisema:

Macho yao yatainama chini, unyonge utawafunika. (Surat al-Qalam: 43)

Na nyuso siku hiyo zitakunjana. (Surat al-Qiyama: 24)

Kwa upande Mwingine Mwenyezi Mungu Anawasifu watu wa Peponi Akisema:

Siku hiyo nyuso nyingine zitanawiri, zitacheka, zitachangamka (Surah Abasa: 38-39)

Chakula cha makafiri kitakuwa ni maji moto, usaha, miiba chungu, na mti wa zaqqum. Lakini kwa upande mwingine, waumini watatuzwa mito ya maziwa na asali, vinywaji vitamu kwenye vikombe, aina yote ya matunda na chochote watakacho. Katika aya hii, Mwenyezi Mungu Anasifu chakula cha watu wa Peponi Akisema:

Mfano wa Pepo waliyoahidiwa watawa (wacha Mungu itakuwa hivi): imo mito ya maji yasiyovunda, na mito ya maziwa isiyoharibika ladha yake, na mito ya ulevi wenye ladha kwa wanywao, na mito ya asali iliyosafishwa; tena humo watapata matunda ya kila namna, na msamaha kutoka kwa Mola wao. Basi hao watakuwa sawa na wale watakaokaa Motoni? Na kunyweshwa maji yachemkayo yatakayokata matumbo yao. (Surah Muhammad: 15)

Kwa hakika huwezi kulinganisha neema wanazopewa waumini na chakula cha makafiri ambacho hakiondoi njaa bali ndio chanzo cha adhabu ya milele. Watakuwa kwenye moto kwa karne; ngozi zao zitabadilishwa baada ya kuchomwa; wataomba kupunguziwa na kupewa starehe. Watamani neema wanazopata watu wa Peponi ambao wamestarehe kwenye kivuli na watajiombea. Mola wetu Anasimulia haya kwa Qurani tukufu Akisema:

Na watu wa Motoni watawaita watu wa Peponi, (kuwaambia): “tumimieni maji au katika vile Alivyokupeni Mwenyezi Mungu.” Waseme (watu wa Peponi): “Hakika Mwenyezi Mungu Ameviharamisha vyote viwili hivyo kwa makafiri.” (Surat al-Araf: 50)

Mwito wa makafiri hautaitikiwa. Mwenyezi Mungu Anasisitiza hili kwenye aya hii:

....Hakika tumewaandalia madhalimu moto ambao kuta zake zitawazunguka. Na wakiomba msaada (kwa kiu kikubwa kilichowashika) watasaidiwa kwa (kupewa) maji kama ya shaba iliyoyayushwa itayoziunguza nyuso (zao). Kinywaji kibaya kilioje hicho! Na mahala pabaya palioje! (Surat al-Kahf: 29)

Vile vile, Mwenyezi Mungu Atawatuza watu wa Peponi nguo za kijani za hariri nyororo, jamdani la fakhari, bangili za dhahabu na fedha. Lakini kwa upande mwingine, makafiri watakuwa na nguo za lami na moto walizotengezewa. Waumini wataishi kwenye makao mazuri na vyumba vya kifahari, wakiegemea jamdani la fakhari lakini makafiri makao yao yatakuwa ni Jahanam itakayofunikwa na safu.

Mwenyezi Mungu Anatufahamisha kwenye Qurani kwamba waumini watapata kila watakacho na watu wa Peponi watakirimiwa kwa maisha ya raha na amani Peponi.

Watapata watakayotaka kwa Mola wao. (Surat ash-Shura: 22)

Basi Mwenyezi Mungu Atawalinda na shari ya siku hiyo na kuwakutanisha na neema na furaha. (Surat al-Insan: 11)

Kama makafiri wangewajibika na kufuata maamrisho ya Mwenyezi Mungu kwa moyo msafi, hawangepata adhabu ya Jahannam siku hiyo. Kwa hivyo masikitiko ya makafiri yanaongezeka wanapoona watu wa Peponi. Mwenyezi Mungu anaeleza adhabu wanayoipata na majuto wanayosikia kama “mateso” na kila mara makafiri watajaribu kukimbia mateso wataongezewa adhabu nyingine:

Kila mara watakapotaka kutoka humo (adhabuni) kwa sababu ya uchungu, (maumivu) watarudishwa mumo humo na (kuambiwa): “Ionjeni adhabu ya kuungua.”

Hii ni kwa sababu hakuna kujitoa kwenye Jahannam. Ni mahala ambapo hisia za kujuta hazimfaidi yeyote. Vile vile kwenye Jahannam fikra ya majuto haijabainishwa. Wakati makafiri wanaaga dunia, malaika watawaambia hawatawahi kuonja uzuri hadi milele isipokuwa kutaka kwa Mwenyezi Mungu.

Siku watakayowaona Malaika haitakuwa furaha siku hiyo kwa wenye makosa na watasema: (Mungu) atuepushie mbali adhabu hii iliyotukabili.” (Surat al-Furqan: 22)

Makafiri wataona njia peke ya kusalimika kwao ni kuangamizwa kabisa. Wataomba kuangamizwa lakini haitawezekana. Hii ni kwa sababu walipewa umri mrefu wa kupata mawaidha lakini wao walikataa na kukengeuka ukweli. Mwenyezi Mungu atawajibu akisema:

“Msiyaite leo mauti mamoja bali yaiteni mengi.”  (Surat al-Furqan: 14)

 “Uingieni, mkistahamili au msistahamili, ni mamoja kwenu; mnalipwa mliyokuwa mkiyatenda.” (Surat at-Tur: 16)

Katika aya ya arubaini ya Surat al-Araf, Mwenyezi Mungu anaeleza kutowezekana kwa makafiri kutolewa Motoni na kuingizwa Peponi akisema “hawataingia Peponi mpaka aingie ngamia katika tundu la sindano.” Na kisha Mwenyezi Mungu anasema makafiri watasahaulika kwa sababu wakiwa duniani walienda kinyume na hakina kupuuza kukutana Siku ya Kiyama. Hawatapata mwitikio wala msaada kutoka kwa Mwenyezi Mungu:

Atasema “Ndivyo vivyo hivyo. Zilikujia Aya Zetu ukazisahau, (ukazipuza), na kadhalika leo utasahauliwa.” (Surah Taha: 126)

Na itasemwa: “Leo tunakusahauni (Motoni) kama nyinyi mlivyosahau siku yenu hii; na mahali penu ni Motoni, wala hamna wa kukunusuruni.” (Surat al-Jathiyya: 34)

Ambao walifanya dini yao kuwa upuzi na mchezo, na maisha ya dunia yakawadanganyia. Basi leo Sisi tunawasahu kama walivyosahau mkutano wa siku yao hii, na kwa sababu ya kule kuzikataa Aya zetu. (Surat al-Araf: 51)

Watamsihi na kumuomba Mwenyezi Mungu awaondoe kwenye moto na Mwenyezi Mungu atawajibu hivi:

“ Mola Wetu! Tutoe humu (Motoni, uturejeshe ulimwenguni, tukafanye amali nzuri); na tufanyapo tena bila shaka tutakuwa madhalimu ( wa nafsi zetu kweli kweli).”

Makafiri watapata adhabu kali na hawatapata msaada wowote kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu hatawaonyesha huruma yake, wala ulinzi wowote na pia hatawasamehea madhambi na makosa yao. Kama wangemrudia Mwenyezi Mungu wakati wangali duniani wangelimpata Mwenyezi Mungu Mwingi wa msamaha na Mwingi wa huruma kwao. Lakini pindi wanapoingia Motoni kujua hilo halitawasidia kamwe.

Baada ya kusema haya yote, ni lazima kila mtu azingatie haya : kwamba Mwenyezi Mungu ni mwingi wa rehema kwa waja wake na binadamu anahitajia Mwenyezi Mungu peke yake awe rafiki na mlinzi wake. Mtu akishafungiwa milango za Jahanam nyuma yake, hazitafunguliwa hadi Mwenyezi Mungu atataka na hatapata fursa kama aliyoyipata akiwa duniani. Katika Qurani, Mwenyezi Mungu anaeleza kuwa kuokoka ni kama ifuatavyo:

Isipokuwa wale waliotubu na wakajitengenezea na wakamshika Mwenyezi Mungu na wakaukhalisisha utii wao kwa Mwenyezi Mungu, basi hao wako pamoja na Waislamu waumini . Na Mwenyezi Mungu atawapa ujira mkuu waumini. Mwenyezi Mungu hakuadhibuni kama mtashukuru na mtaamini. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kupokea shukrani ndiye Mwenye kujua. (Surat an-Nisa: 146-147)

Je! Vipi kuepuka majuto Siku ya Kiyama?

Mwenyezi Mungu hakuadhibuni kama mtashukuru na mkaamini. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kupokea shukrani ndiye Mwenye kujua. (Surat an-Nisa: 146-147)

Binadamu wameumbwa kwa udhaifu na kutokamilika. Katika umri wetu, tunasahau mambo mengi na kufanya makosa mengi. Lakini kupitia kuomba msamaha ambao Mwenyezi Mungu ametupa kama fadhla kubwa tunaweza kurekebisha makosa yetu. Kwa hakika huo ndio msingi wa maisha ya duniani: tunafundishwa, tunatahiniwa, na kutakaswa makosa yetu. Yawezekana kwamba tunajuta makosa yetu au namna tumeendesha maisha yetu. Lakini tunaweza kurekebisha kwa kuomba msamaha na kutarajia kusamehewa na Mwenyezi Mungu.

Katika Qurani, Mwenyezi Mungu anatoa bishara kwamba Atasamehe madhambi ikiwa mtu ataomba msamaha kwa dhati. Mwenyezi Mungu anajua fikra zetu na kila neno tunaloficha. Anajua ikiwa tuko wakweli au la. Mwenyezi Mungu anaonyesha ukaribu wake na waja wake akisema:

Mola wenu anajua sana yaliyo nyoyoni mwenu Kama mkiwa wema. Kwani Yeye ni Mwenye kuwaghufiria wenye kurejea (kwake) (Surat al-Isra: 25)

Lakini linalojitokeza ni kwamba, baada ya kifo, haitawezekana kurekebisha makosa na madhambi yaliyofanywa duniani isipokuwa atakavyotaka Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo tusipoteze muda wetu hada kidogo. Madakika yanasonga kwa kufumba na kufumbua macho na kila muda unaposogea, tunakaribia mauti. La kuzingatia ni kwamba hatuwezi kujua wakati wa kifo utakapowadia. Siku, saa na dakika haijulikani. Hatimaye sote tutafariki na lazima tutoe hesabu ya vitendo vyetu mbele ya Mwenyezi Mungu.

Kwa hivyo binadamu lazima azingatie kuwa anaweza kufariki wakati wowote. Ikiwa hataki kujuta akiwa akhera, ni lazima atafakari kuhusu maisha yake.

Mwenyezi Mungu ndiye Muumba wetu na kila linalotakikana kwa mtu mbele ya Mwenyezi Mungu ni kutekeleza wajibu wake kama mja wakati akiwa duniani. Muumin hutekeleza wajibu wake wa dini ipasavyo, anasimamisha swala tano kwa furaha, kufanya wudhu, kufunga kama vile ameamrishwa na Mwenyezi Mungu kwa maisha yake yote.

Ameripoti Ibn 'Umar (ra):

Mtume (s.a.a.s) amesema: “Dini ya Uislamu imejengwa kwa misingi tano: kushuhudia kwamba hakuna wa kuabudiwa isipokuwa Allah, kuwa Muhammad (s.a.a.s) ni mja na Mtume Wake, kuswali, kufunga na kuhiji.” (Bukhari and Muslim)

Ikiwa wakati wa mauti umefika sasa, je! Mtu ambaye hakutekeleza wajibu wake kama mja wa Mwenyezi Mungu ataweza kutoa hesabu ya yote aliyoyafanya akiwa duniani?

Ni nini umefanya hadi sasa ili upate radhi za Mwenyezi Mungu?

Je! Umetekeleza maamrisho ya Mwenyezi Mungu kwa ukamilifu?

Huenda mtu akawa na jibu la ndio kwa maswali haya. Lakini akitubu na kufanya jukumu la kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu, ataweza kutarajia msamaha wa Mwenyezi Mungu. Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.a.s) alikuwa akitafuta msamaha kwa Mwenyezi Mungu mara kwa mara:

Naapa kwa Mwenyezi Mungu, mimi huomba msamaha na kurejea Kwake zaidi ya mara sabini kila siku. (Bukhari)

Ni lazima kujikinga na Mwenyezi Mungu, ambaye ni al-Ghaffar (Mwenye kusamehe, Mwingi wa Kusamehe,) al-Halim (Mvumilivu) na al-Tawwab (Mwenye kukubali tauba) kwa hakika Mwenyezi Mungu Atawatuza wenye subira na wanaomrejea. Na kwa hakika Atawasamehe waja Wake ambao wana imani na kuwatuza kwa matendo mema waliyofanya kulingana na uwezo wao. Kwenye Qurani Mwenyezi Mungu anatoa bishara akisema:

Mlivyo navyo vitakwisha na vilivyoko kwa Mwenyezi Mungu (vya jaza yenu) ndivyo vitakavyobakia. Na kwa yakini sisi tutawapa waliosubiri ujira wao kwa yale mazuri waliyokuwa wakiyatenda. Wafanyaji mema, waume na wanawake,hali ya kuwa ni Waislamu, tutawahuisha maisha mema, na tutawapa ujira wao (akhera) mkubwa kabisa kwa sababu ya yale mema waliyokuwa wakiyatenda. (Surat an-Nahl: 96-97)

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.a.s) amewahimiza waumini kuwa na msimamo kwa kutenda matendo mema na akawapa bishara kuwa watalipwa na Mwenyezi Mungu wakifanya hivyo.

Mtume (s.a.a.s) amesema: “Endelea kutenda (mambo mema), kwani kila mtu ataliona rahisi kufanya (lile ambalo litampeleka pahala pake). Kisha akasoma aya “ Na Yule anayetoa (zaka, sadaka na vinginevyo) na kumcha Mwenyezi Mungu na kusadiki jambo jema (akalifuata), tutamsahilishia njia ya kwenda Peponi. Na anayefanya ubakhili, asiwe na haja na viumbe wenzake, na akakadhibisha mambo mema, tutamsahilishia njia ya kwenda Motoni.” (Bukhari)

Tusisahau kwamba mmoja wetu anaweza kupatikana na mauti na hata akiwa na majuto, hatakuwa na fursa ya kurekebisha makosa aliyoyafanya. Kwa hivyo tusipoteze fursa ya kuomba msamaha kwa Mwenyezi Mungu na kufungamana na maamrisho Yake na sunna ya Mtume (s.a.a.s). Hii ndio njia peke ya kuwa mja maybe Mwenyezi Mungu Anamneemeshea rahma na mapenzi. Na ndio njia pekee ya kufika kwenye Pepo, mahala pa kudumu anakotayarisha Mwenyezi Mungu kwa waumini Wake wa dhati.

Wakasema (Malaika): “Utakatifu ni wako! Hatuna ilimu isipokuwa ile uliyotufundisha ; bila shaka wewe ndiye Mjuzi na ndiye Mwenye hikima. ”(Surat al-Baqara: 32)

 

 

   

    
6 / total 6
|
You can read Harun Yahya's book Usije Ukajuta online, share it on social networks such as Facebook and Twitter, download it to your computer, use it in your homework and theses, and publish, copy or reproduce it on your own web sites or blogs without paying any copyright fee, so long as you acknowledge this site as the reference.
About this site | Tengeneza kurasa yako ya nyumbani | Add to favorites | RSS Feed
Mambo yote yanaweza kuynakiliwa, kuchapwa na kusambazwa kwa kurejea katika kurasa hii
(c) All publication rights of the personal photos of Mr. Adnan Oktar that are present in our website and in all other Harun Yahya works belong to Global Publication Ltd. Co. They cannot be used or published without prior consent even if used partially.
© 1994 Harun Yahya.www.harunyahya.com
page_top