Muujiza Katika Chembe Ya Atomu

SHUSHA KITABU

Download (DOC)
Maoni

SURA ZA KITABU

< <
2 / total: 4
Muujiza katika chembe ya Atomu - Harun Yahya
Muujiza katika chembe ya Atomu
   

 


Ngazi ya pili kuelekea kwenye

Maada (Matter): Molecules

Kitu gani kinachosababisha maumbile mbalimbali kwenye mazingira kuonekana tafauti? Kitu gani kinatafautisha rangi zake, maumbile yao, manukato yao na maonjo yao? Kwanini umbile moja huwa mororo na jingine gumu, vile vile maji maji ya aina moja kuwa meepesi na mengine kuwa mazito? Kutokana na yale tuliyojifunza mpaka sasa hivi, unaweza kusema kuwa “tafauti kati ya atomu zinazoifanya vitu hivi ndivyo vinavyosababisha”.

Pamoja na hili bado jibu hili haitoshelezi kwa sababu kama chanzo ni tafauti za atomu basi kungekuwa na mabilioni ya atomu zenye tabia tafauti ijapokuwa ni za aina moja. Kiukweli hivi sivyo ilivyo, kwani vitu vingi vinaonekana tafauti, zikiwa na tabia tafauti ijapokuwa zina atomu za aina moja. Sababu hasa ya hili ni kuwa zina viungo vya kikemikali zilizotafauti zinazounganisha atomu kufanya Molecules.

Katika kuelekea kwenye maada (matter) Molekuli (Molecules) ni hatua ya pili baada ya atomu. Molecule ni kiwango kidogo kuliko yote inayoifanya tabia ya kikemikali ya maada. Maumbile haya madogo ya molekyuli hufanywa na atomu mbili au zaidi na baadhi ya maelfu ya makundi ya atomu. Atomu huunganishwa pamoja ndani ya molekyuli kwa muungano wa kikemikali ambazo hutokeza kwa nguvu za umeme-smaku (electromagnetic) za uvutano, kwa maana ya kwamba kiungo hiki (bonds) kinatokea kwa misingi ya chaji zilizopo kwenye atomu. Kwa usemi mwingine ni kuwa chaji za atomu hutokana na chaji zilizopo kwenye electrons kwa njia yake ya nje kuliko zote.

Mipangilio mbalimbali ya molekyuli husababisha aina tafauti za maada (matter) tunazoziona zinatuzunguka. Hapa ndipo mahali tunapoona muungano wa kikemikali (chemical bonds) unavyosababisha uwanja wa vitu (maada) mbalimbali.

Muungano wa kikemikali (Chemical bonds)

Kama tulivyoeleza awali, viungo vya kikemikali (Chemical bonds) hufanyika na kuhusisha mizunguko ya electrons katika njia ya nje ya electrons katika atomu. Kila atomu hupendelea kujaza njia zake kwa electron za viwango vinavyohitajika ikiwa idadi ya juu inayokubalika ni 8 kwa ile ya nje. Ili kukamilisha azma hii, atomu ama hupokea electons kutoka kwa atomu zingine ili kujaza nafasi iliyobakia katika njia yake ya nje kuwa 8 au kama zina electron chache katika njia hii ya nje basi huzitoa na kuzipa atomu zinginezo. Hali hii ya kupokea au kutoa ni msingi mkubwa sana wa muungano wa kikemikali (Chemical bonds) zinazofanyika baina ya atomu.

Msukumo na nguvu hii inayoifanya nia ya atomus kuongeza idadi ya electrons katika njia yake ya nje kufikia ile idadi yake ya juu, hufanya atomu kuwa na muungano wa aina tatu baina yake na atomu nyinginezo. Muungano (bonds) wa aina hii ni ionic bonds, Covalent bonds na metallic bonds.

Ionic Bonds (Muungano wa Ayonik)

Atomus zinazoungana kwa aina hii hujaza idadi ya electrons katika njia yake ya nje kufikia nane. Atomu zenye electrons kufikia nne katika njia yake ya nje hutoa electrons kwa atomu ambayo huungana nayo. Atomu zenye electron zaidi ya nne katika njia yake ya nje hupokea electrons kutoka kwa atomu ambayo hutokana na muungano huu huwa na umbile la Cabic. Mfano wa aina hii ya molecule ni ule wa chumvi maarufu kama NaCl. Kwa nini atomu zinakuwa na mwenendo huu? Je, nini kitatokea iwapo isingekuwa hivi?

Mpaka leo hii, muungano au kiungo kinachofanya na atomu huelezwa katika namna ya ujumla sana. Bado si rahisi kuelezea kwa nini atomu inafuata utaratibu huu. Labda tujiulize kama ni atomu pekee iliyojiamulia kwamba tuseme namba au idadi ya electron katika njia yake ya nje iwe nane? Kwa hakika jibu ni sio. Hii ni uamuzi dhahiri unaotokana na ufumbuzi nje ya atomu yenyewe kwa sababu atomu haina akili, uwezo na umahiri wa kiubongo.

Idadi hii ni ufunguo katika michanganyo ya atomu kufanya molekuli ambayo husababisha ngazi ya pili katika kuifanya maada (matter) na mwisho wake, ulimwengu. Kama atomu isingekuwa na tabia hii kwa misingi ambayo inakubalika, basi molekuli, na hatimaye maada (matter) isingekuwepo. Pamoja na yote, kuanzia mwanzo kabisa wa uumbaji wake, atomu zimetusababisha kuwepo kwa molekuli na maada katika mpango mahsusi kabisa ambao tunapashwa kushukuru kwa tabia hii.

Covalent Bonds (Muungano wa Kovalenti)

Wanasayansi ambao wamejifunza muungano wa bondi (bonds) kati ya atomu wamekuwa wakishangazwa sana. Wakati baadhi ya atomu zimetoa electrons kwa ajili ya bondi (muungano), baadhi ya atomu zimekuwa zikishirikiana kupitia electrons katika njia yake ya nje.

Utafiti wa kina umedhihirisha kuwa molekuli nyingi ambazo zimekuwa na umuhimu wa pekee kwa maisha zimesababishwa kuwepo kwao na hii bondi ya kovalenti (covalent bonds).

Tutazame mfano rahisi ambao tunaweza kuielezea bondi ya kovalenti kwa namna rahisi. Kama tulivyoeleza awali katika mada ya electrons, atomu huchukua idadi kubwa kuwa electron mbili katika njia yake ya ndani kabisa. Atomu ya Haidrojeni (haidrojeni) ina electron moja pekee na ina tabia ya kuongeza idadi ya electron ili kufikia mbili ili iwe atomu yenye ukamilifu (stable). Kwa hiyo, atomu ya Haidrojeni hufanya bondi ya kovalenti (covalent bond) na atomu ya pili ya Haidrojeni. Hii ni kusema atomu mbili ya Haidrojeni zinashirikiana na electron iliyopo kwa akila mmoja wao ili kukamilisha idadi ya electron mbili. Hivyo H2 moleculi (ya Haidrojeni) hutokea.

Metallic Bonds (Muungano wa kimetaliki)

Pale ambapo idadi kubwa ya atomu zinapokuja pamoja kwa kushirikiana na electron iliyobaina yao, hii huitwa “bondi ya kimetaliki”. Metaliki kwa mfano, chuma, shaba, zinki, aluminiam na kadhalika ambayo huwa ni malighafi ya vyombo mbalimbali vya vifaa na mitambo iliyotuzunguka katika maisha yetu ya kila siku. Imepata umaarufu mkubwa kwa sababu ya bondi ya metaliki, inayofanyika na atomu zinazohusika.

Wanasayansi bado hawajaweza kuweka bayana sababu zinazofanya electrons katika njia zake kuwa na tabia hii. Viumbe vyote, vinapaswa kuishukuru tabia hii ambayo husababisha kuwepo kwao.

Hatua inayofuata: Kompaundi (The next step: Compounds)

Je, unafahamu ni kompaundi ngapi ambazo ni za aina tafauti zinazotengenezwa na bondi hizi? Kila siku kwenye maabara, kompaundi mpya hutengenezwa. Kwa sasa hivi inawezekana kuzungumzia kiasi cha kompaundi kama milioni mbili hivi. Kompaundi ya aina nyepesi na rahisi zaidi inaweza kuwa ndogo kama ile ya molekuli ya haidrojeni, wakati kuna kompaundi ambayo hutengenezwa na mamilioni ya atomu [27].

Je, ni idadi gani ya kompaundi inayoweza kutemgenezwa na elementi kwa kiwango cha juu? Jibu la swali hili ni la kushangaza kabisa kwa sababu, kwa upande mmoja kuna elementi ambayo haichanganyiki na nyingine yoyote (gesi ya inati) na kwa upande wa pili kuna atomu za Carboni ambayo huweza kufanya kompaundi zifikazo 1,700,000. Kama tulivyoeleza awali idadi ya jumla ya kompaundi inakaribia milioni mbili. Elementi 108 kati ya 109 hufanya kompaundi 300,000. Hata hivyo Carbon hufanya kompaundi 1,700,000 yote kwa peke yake kwa namna ya kushangaza kabisa.

Matofali yajengayo maisha

Atomu ya Carbon

Carbon ni elementi muhimu sana kwa viumbe vinavyoishi, kwa sababu kila chenye uhai hujengeka kutokana na kompaundi ya Carbon. Idadi kubwa ya kurasa zahitajika ili kuelezea aina za Carbon ambazo ni muhimu kwa maisha yetu. Bado sayansi ya kemia haijamaliza kugundua maelezo kamilifu kuhusu Carbon. Hapa tutaorodhesha baadhi tu ya sura na tabia za Carbon.

Maumbile na mpangilio wa Carbon unafanana na ile seli ya membrini, pembe za wanyama, matawi ya miti, mboni ya jicho, utandu wa buibui ambayo ni baadhi tu ya mifano ya kompaundi ya Carbon. Carbon inapounganika na hewa ya Haidrogeni, Oksijeni na Nitrogeni kwa viwango vingi tafauti na maumbile tafauti hutokea aina mbalimbali ya vitu yenye maumbile na tabia mbalimbali. Hivyo, ni sababu gani, Carbon huweza kuwa na uwezo wa kufanya kuwepo kwa kompaundi milioni 1.7

Aina moja muhimu ya tabia ya Carbon ni uwezo wake wa urahisi wa kufanya minyororo na mahusiano ya kuzipanga atomu za Carbon moja baada ya nyingine. Mnyororo mfupi wa Carbon hufanywa na atomu mbili za Carbon. Pamoja na kutokuwepo idadi kamili ya Carbon ambayo hufanya mnyororo mrefu kuliko yote ya Carbon, bado tunaweza kuzungumzia mfano wa mnyororo wenye viungo sabini. Tukiangalia mfano wa atomu ambayo huweza kufanya mnyororo mrefu baada ya Carbon atomu kuwa ni atomu ya silicon kufanya viungo sita, nafasi ya pekee ya Carbon inaweza ikaeleweka zaidi.

Sababu ya Carbon kuwa na uwezo wa kufanya minyororo na viungo vingi ni kuwa minyororo yake sio lazima uwe kama mstari. Minyororo huweza kuwa kama matawi na huweza kuwa ya maumbile tafauti.

Kwa wakati huu, aina ya minyororo ni muhimu sana. Katika aina mbili ya kompaundi ya Carbon, kwa mfumo kama atomu za Carbon zinapokuwa za idadi sawa na bado zikawa katika aina tafauti ya viungo vya minyororo basi aina mbili tafauti za bidhaa hupatikana. Maumbile haya tuliyoyataja hapa juu ya Carbon atomu husababisha molekuli ambazo ni adimu na muhimu kwa maisha. Tunaweza kuzungumzia mfano wa mnyororo wenye viungo sabini. Tukiangalia mfano wa atomu ambayo huweza kufanya minyororo mrefu baada ya Carbon atomu kuwa ni atomu ya Silicon kufanya viungo sita, nafasi ya pekee ya Carbon inaweza ikaeleweka zaidi.

Sababu ya Carbon kuwa na uwezo wa kufanya minyororo na viungo vingi ni kuwa minyororo wake sio lazima uwe kama mstari. Minyororo huweza kuwa kama matawi na huweza kuwa ya maumbile tafauti.

Kwa wakati huu, aina ya minyororo, ni muhimu sana. Katika aina mbili ya Kompaundi ya Carbon kwa mfano kama atomu za Carbon zinapokuwa za idadi sawa na bado zikawa katika aina tafauti ya viungo vya minyororo basi aina mbili tafauti za bidhaa hupatikana. Maumbile haya tuliyoyataja hapa juu ya Carbon atomu husababisha molekuli ambazo ni adimu na muhimu kwa maisha.

Baahi ya molekuli kompaundi ya Carbon zinasababishwa na idadi chache tu za atomu, nyingine maelfu na hata mamilioni. Vivyo hivyo, hakuna elementi nyingine ilivyo makini kama Carbon hasa katika kufanya molekuli yenye umadhubuti na ustahimilivu. Tukimnukuu mwandishi David Burnie katika kitabu chake

Molekuli tatu zinazofanana matokeo: Aina tatu tafauti za bidhaa

Pamoja na tafauti za atomu chache baina ya molekuli husababisha matokeo tafauti kabisa. Kwa mfano ukitazama kwa makini sana kwenye molekuli zifuatazo hapa chini: Zote zinaonekana kufanana isipokuwa kwa tafauti ndogo ya viwango vya Carbon na Haidrojeni. Matokeo yake ni bidhaa au kemikali mbili tafauti kabisa.

C18 H24 O2 na C19 H28 O2

Je unaweza kutabiri hizi ni molekuli gani? Ile ya kwanza huitwa Oestrogen na nyingine huitwa testosterone. Hii ni kusema ya mwanzo ni homoni inayosababisha tabia za kike na ya pili ni homoni inayosababisha tabia ya kiume. Cha kushangaza zaidi, hata tafauti za atomu chache huweza kusababisha tafauti za tabia za kijinsia. Hebu saa tazama fomula hii ifuatayo:

C6 H12 O12

Je, molekuli hii haijafanana sana na Oestrogen na testosterone molekuli za homini? Je, sasa hii ni molekuli ipi? Je, ni homoni nyingine tena?

Jibu la swali hili moja kwa moja: Hii ni molekuli ya sukari. Kutokana na mifano hii mitatu ya molekuli ambayo hufanywa na elementi ya aina moja ni kuwa namna gani elementi za aina moja zinavyoweza kutengeneza vitu tafauti. Kwa upande mwingine unaona homoni za aina tafauti na vile vile bidhaa kama sukari, chakula cha msingi.

Carbon ni aina ya pekee katika elementi. Bila ya kuwepo kwa Carbon na tabia zake za pekee, maisha ya duniani hapa isingewezekana.

Kuhusiana na umuhimu wa Carbon kwa maisha ya viumbe, mkemia mmoja wa Kiingereza Nevil Sidgwick anaandika katika kitabu chake “Elementi ya Kemikali na Kompaundi yake”:

Carbon ni ya pekee katika elementi kwa idadi na aina kwa aina ya kompaundi inazozifanya. Zaidi ya robo ya milioni imewezekana kutenganishwa na kuelezewa, lakini nguvu itokanayo na elementi haijawa wazi kwa sababu ni chanzo cha kila aina ya maisha ya viumbe. [30]

Daraja za kompaundi zinazofanywa na Carbon na Haidrojeni huitwa “hydrocarbons”. Hii ni familia ya kompaundi ambayo hujumuisha gesi ya asili, bidhaa za maji ya mafuta (petroleum), mafuta taa, na oili za kulainishia. Hydrocarbon ya aina ya ethylene na propylene hufanya kuwepo kwa viwanda vya kemikali itokanayo na mafuta. Hydrocarbon kama benzene, tomene na turpentine ni maarufu kwa wale wanaoshughulika na kazi za rangi. Vile vile naphalene zinazotoa kinga kwa nguo zetu kutoliwa na mende ni aina nyingine ya hydrocarbon. Hydrocarbon zinapoungana na Klorini au Florini hufanya kitu kiitwacho anaesthetics, kemikali inayotumika kwenye vifaa vya kuzimia moto (fire extinguishers) na Freons inayotumika katika vyombo vya kupoozea - barafu (friji).

Kama alivyosema mkemia Sidgwick hapo awali, akili ya binadamu ni dhaifu kuweza kuelewa kwa ujumla wake, uzito na umuhimu wa ujumla wa atomu ambao ina proton sita na neutron sita na electron sita tu. Haiwezekani kwa angalau tabia moja tu ya atomu, ambayo ni muhimu kwa maisha kuwepo kwa kubahatisha. Atomu ya Carbon kama ilivyo vitu vingine, imeumbwa na Muumba kwa uwezo mkubwa usio kifani na kwa ajili ya viumbe viishivyo ambavyo vimeumbwa kwa atomu hizi na Allah (s.w.) mpaka kiwango cha chini kuliko yote ya atomu.

Na ni vya Mwenyezi Mungu tu vyote vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini. Na Mwenyezi Mungu ndiye aliyevizunguka vitu vyote (kwa kuvijua nje yake na ndani yake0. [Surat An-Nisa:126]

Kitu gani kingetokea kama kila atomu iliyokuwa karibu zingeathirika mara moja?

Tulikwishasema kuwa ulimwengu wote umetokana na athari ya maingiliano ya atomu ya elementi tafauti 109. Hapa kuna nukta ambayo inahitaji kutajwa ambayo ni sababu muhimu ili athari ya maingiliano hayo yaweze kutokea.

Kwa mfano, maji hayafanyiki tu kwa kuwepo na Oksijeni na Haidrojeni. Hivyo hivyo Chuma hakipati kutu pale tu kinapokutana na hewa. Kama ingefanyika hivyo madini ya chuma ambayo ni ngumu na hung’aa yangebadilika na kuwa “Ferrows Oxide” ambayo ni pauda laini, katika dakika chache. Kwa namna hii hakuna kitu cha namna ya chuma kingebakia hapa duniani na mpangilio wa ulimwengu ungeathirika sana. Kama atomu ambazo zingetakiwa kuwa karibu kwa umbali fulani zingeungana mara moja bila ya kutekeleza masharti fulani, atomu za vitu viwili tafauti zingeingiliana na kutoa athari wakati huo huo.

Kwa namna hii ingekuwa vigumu hata mtu kukaa kwenye kiti, kwa sababu atomus zinazokifanya kiti zingeiliana na kuathiri atomus zinazofanya mwili wkao na kingetokea kle ambacho ni baian ya kitu na mwanadamu. Ni wazi kuwa kwa duniya ya namna hii maisha yangekuwa hayawezekani. Je, hali hii inaepukika kwa namna gani?

Kwa kutoa mfano, Haidrojeni na Oksijeni molekuli zinaingiliana na kutoa athari pole pole sana katika joto la kawaida kwenye vyumba. Hii ni kusema maji hufanyika pole pole sana katika joto hili. Bado, pale joto linapoongezeka katika mazingira, nguvu iliyoko kwenye molekuli inaongezeka na maingiliano na athari zake zinazongezeka na hivyo maji hutokea kwa kasi zaidi. Kiwango cha chini cha nguvu inayohitajika kwa ajili ya molekuli kuathiriana na nyingine huitwa “Nguvu ya activation”. Kwa mfano, ili molekuli ya Haidrojeni na Oksijenii ziathiriane kutengeneza maji, nguvu zao lazima ziwe kubwa kuliko nguvu ya (activation) kuathiri.

Hebu tazama, pale ambapo joto katika dunia lilikuwa kubwa kidogo, atomu zingeathiriana kwa haraka zaidi, ambazo zingeharibu uwiano wa kimaumbile. Kinyume chake ingekuwa joto duniani ni ndogo, atomu zingeathiriana kwa polepole zaidi. Hiyo vile vile ingeharibu uwiano wa kimaumbile.

Na hii kuelezea sababu ya umbali wa dunia kutoka kwenye jua ni ile ambayo ni yenye kutosha kuwezesha maisha duniani kuwepo. Ni wazi kuwa uwiano unaohitajka ni kuwezesha maisha kuendelea.

Kuwepo kwa mstari ambao dunia huzungukia katika nyuzi maalumu, uzito wa dunia, na eneo lake, na gesi iliyopo kwenye dunia na katika viwango maalum, umbali kati ya dunia na sayari, mwezi na vitu vingine umekuwa katika viwango maalumu kuwezesha maisha kuwepo. Hizi zote hazipo kwa kubahatisha ila kwa matakwa ya Muumba (s.w.), mmiliki wa nguvu zote, anayejua haki zote zinazofaa kwa maisha ya viumbe.

Kwa ujumla, lengo la sayansi katika matokeo yote haya ni kutaja kanuni za kifizikia ambazo zinaonekana. Kama tulivyoeleza hapo awali, yanapothibiti matukio hayo, maswali kama “nini?”, “vipi?” na “namna gani?” yanajitokeza. Kitu gani tunaweza tukafikia kwa maswali haya ni maelezo ya kanuni ambazo tayari zipo. Maswali muhimu ni “kwa nini?” na “nani aliyeumba kanuni hizi?”

Majibu ya maswali haya yanabaki bado ni utata kwa wanasayansi ambao kwa upofu wao bado wanajiegemeza katika nadharia ya “Materialist”. Wakati huu ambapo Materialist wamejikuta kufungiwa milango, picha ipo wazi kabisa kwa yule anayetazama matukio kwa kutumia akili yake na busara yake. Uwiano usio kifani ulimwenguni ambao hauelezeki kwa kubahatisha, bali huwa kama Mwenyezi Mungu alivyoeleza:

Allah anakitazama kila kitu... na ameumba kila kitu kwa mpangilio kwa mahesabu yenye uhakika, kwa nidhamu na uwiano.

Muungano baina ya Molekuli: Muungano dhaifu (Weak Bonds)

Muungano, unaounganisha atomu kwenye molekuli ni wenye nguvu sana kuliko ule uliodhaifu baina ya molekuli na molekuli nyingine. Muungano wa namna hii husaidia kufanya mamilioni na wakati mwingine mabilioni mbalimbali ya molekuli.

Je, ni namna gani molekuli huunganika kufanya maada (matter)? Kwa sababu molekuli huwa imara sana katika umbile lake, hivyo hazibadilikibadiliki. Je, sasa zinashikiliwa vipi pamoja? Katika kujaribu kujibu swali hili, wanakemia wakatoa nadharia nyingi sana. Utafiti umeonnesha kuwa molekuli zinauwezo wa kuungana kwa namna mbalimbali kutegemea na namna na hali za atomu zilizopo katika mchanganyiko huo.

Viungo hivi ni muhimu sana katika fani ya kemia ya Oganik, ambayo ni chem. chem ya vitu vilivyo hai, kwa ajili ya molekuli muhimu zinazosababisha maisha kwa viungo hivi. Tuchukue mfano wa protini. Umbile ngumu la protini ambayo ni sawa na matofali ya kujengea mwili wa binadamu, hutokana na viungo hivi.

Hii ina maana, kuwa viungo vya kemikali vilivyo dhaifu kati ya molekuli ni muhimu na lazima kama ilivyo ile ya viungo vyenye nguvu ya kemeikali kati ya atomu zinazosababisha maisha. Ni wazi, nguvu ya viungo hivi lazima ziwe za viwango maalum.

Tunaweza tukaendelea na mifano ya protini. Molekuli zinazoitwa "Amino acids" zinaungana kufanya protini ambazo ni molekuli kubwa zaidi. Atomu ni molekuli kubwa zaidi. Atomu ambazo zinafanya Amino acid kuungana kwa bondi za kovalenti (Covalent bonds).

Viungo dhaifu huunganisha amino acids hizi kwa namna ya kufanya mfumo wa daimensheni tatu. Protini huweza kufanya kazi katika viumbe vyenye uhai pale zinapokuwa katika daimensheni tatu za maumbile. Hivyo, kama viungo hivi visingekuwepo, basi protini na hivyo hivyo maisha yasingekuwepo.

Viungo vya hydrojeni ni mfano mzuri wa viungo dhaifu, ambavyo ni muhimu kwa utengenezaji wa bidhaa ambazo ni muhimu kwa maisha ya binadamu. Kwa mfano, molekuli zinazotengeneza maji, ambayo ni msingi wa maisha, zinatokana na muungano wa hydrojeni na oxyjeni.

Je! Huoni kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.) huteremsha maji kutoka mawinguni, ma mara ardhi inakuwa chanikiwiti? Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye Kujua yaliyofichikana na Mwenye kujua yaliyodhahiri. (Surat-al-Hajj:63).

Maajabu katika Molekuli: Maji

Maji ni bidhaa maalum iliyochaguliwa kwa ajili ya maisha ya viumbe na imeshika theluthi mbili ya nafasi ya dunia. Miili ya viumbe hai hapa duniani imefanywa na maji katika kiwango kati ya asilimia 50 hadi 95. Maisha yamekuwepo katika kuwapo kwa maji, kuanzia kwenye joto linalokaribia hata maji kuchemka kama bakteria hadi maji yaliyo katika mfano wa barafu inayoyeyuka.

Hata katika tone moja la mvua iliyobaki katika jani la mti basi panakuwepo maelfu ya viumbe hai walio wadogo sana ambao wanazaliana na hufa.

Je, dunia ingekuwaje kama maji yasingekuwepo? Ni wazi kila pahala pangekuwa jangwa. Kungekuwa na hali ya kukata tamaa na ya kutisha pasipo na bahari. Anga ingekuwa bila ya mawingu na rangi yake ingekuwa ya ajabu sana.

Pamoja na yote haya, kile ambacho ni muhimu sana kwa maisha ya binadamu, maji yana ugumu sana katika kufanyika. Kwanza, tujalie molekuli ya hydrojeni na Oxyjeni ambazo hufanya maji zimewekwa kwenye bakuli la glasi. Halafu tuziache hapo kwenye bakuli kwa muda mrefu. Bado gesi hizi mbili hazitafanya maji hata kama zitabaki hapo kwa miaka mia moja. Na hata kama zitaifanya, haiwezi ikawa zaidi ya kiasi kidogo sana katika sehemu ya chini ya bakuli na hii huweza kufanyika katika hali ya pole pole sana, na labda baada ya miaka elfu au zaidi.

Sababu ya maji kufanyika pole pole sana katika hali hii ni joto. Katika joto la kawaida la chumbani Oxyjeni na Hydrojeni huingiliana pole pole sana.

Oxyjeni na Hydrojeni zinapokuwa huru, hupatikana kama H2 na O2 za Molekuli. Ili kuungana na kufanya molekuli ya maji, lazima pawepo na mgongano.

Baada ya mgongano huo, viungo vinayoifanya molekuli ya Hydrojeni na Oxyjeni hudhoofishwa, na kutoa vikwazo kwa muungano wa atomu za Oxyjeni na Hydrojeni. Joto huongeza nguvu na hivyo kasi ya molekuli hutokana na kuongezeka kasi ya migongano.

Hata hivyo, mpaka sasa hivi, hakuna joto la kiwango cha juu linaloweza kufikia kiwango cha kusababisha maji yote yaliyopo duniani hivi sasa. Joto lililohitajika kwa kufanyika maji yote haya lilitokea wakati wa kuumbwa kwa dunia na ulimwengu kwa ujumla ambao ulisababisha sehemu tatu ya nne ya dunia kufunikwa na maji. Kwa sasa hivi, maji yanageuka kuwa mvuke na kwenda angani ambapo hupoozwa na kurudi duniani kama mvua. Hii ni kusema hakuna nyongeza ya maji bali ni badiliko katika mzunguko.

Maajabu katika tabia ya maji

Maji yana aina ya tabia ya pekee kabisa ya kemikali. Kila molekuli ya maji inayofanyika kwa muungano wa atomu za Hydrojeni na Oxyjeni. Ni jambo la kufurahisha sana kuwa gesi za aina mbili, moja inaunguza na nyingine inaunguzwa huungana kufanya maji kwa namna ya ajabu kabisa.

Sasa kwa ufupi tutazame namna ambayo maji hutokea kikemikali. Chaji ya umeme ya maji ni sifuri, hivyo ni "neutral". Hata hivyo, kutokana na ukubwa wa atomu ya Oxyjeni na Hydrojeni kwa kiwango fulani molekuli ya Oxyjeni ya maji inakuwa na chaji hasi wakati ile ya Hydrojeni inakuwa na chaji chanya. Pale ambapo molekuli zaidi ya moja ya maji zinapokaribiana, chaji hasi na chanya huvutana na husababisha kiungo maalum kiitwacho The Haidrojeni bond. Kiungo hiki cha Haidrojeni ni dhaifu sana na hivyo hudumu kwa muda mfupi sana.

H + H + O = H2O

Haidrojeni + Haidrojeni + Oksijeni = Water Molekule.

Muda wa kiungo cha hydrojeni (Haidrojeni bond) ni kiasi cha moja ya mia moja bilioni ya sekunde. Lakini baada tu kuvunjika kwa (bondi) kiungo, nyingine hutokeza. Hivyo, molekuli ya maji hujishikiza kwa nguvu sana kwa nyinginezo wakati huo huo zinabakia katika hali yake ya umajimaji kwa sababu zimeunganishwa na kiungo dhaifu. Viungo vya hydrojeni vile vile huwezesha maji kuhimili mabadiliko ya joto. Hata ikitokezea kuwa joto la hewa limeongezeka ghafla, joto la maji huongezeka pole pole na hivyo hivyo, kama joto la hewa linateremka ghafla, joto la maji linashuka pole pole.

Mabadiliko makubwa ya joto yanahitajika ili kusababisha mabadiliko makubwa ya joto la maji. Kiwango kikubwa cha nguvu ya joto la maji yana faida kubwa kwa maisha. Ili kutoa mfano rahisi, kuna kiasi kikubwa cha maji kwenye miili yetu. Kama maji yangekuwa yanabadilika kwa kiwango kidogo cha mabadiliko kwenye hewa, basi tungekuwa mara tunatetemeka au kuganda kwa baridi.

Kwa maelezo hayo hayo, maji yanahitaji kiwango kikubwa cha nguvu ya joto ili kuwa mvuke. Kwa sababu maji yanatumia kiwango kikubwa cha nguvu joto ili kuwa mvuke, joto lake hushuka. Kutoa mfano tena katika mwili wa binadamu, joto la kawaida la mwili ni nyuzi 36oC na juu tunayoweza kuvumilia ni nyuzi 42 oC. Tafauti hii ya 6 oC ni ndogo sana ambayo ukifanya kazi katika jua kwa muda mfupi tu inaweza ikaongeza joto kwa kiwango hicho.

Bado miili yetu inatumai nguvu joto nyingi kwa kutokwa na jasho, na hivyo kusababisha maji yatokayo mwilini kutoweka kama mvuke ambayo kwa uande mwingine hufanya miili yetu kuwa baridi na joto kushuka. Kama miili yetu isingekuwa na mfumo huu, kufanya kazi katika mfupi tu kwenye jua ingekuwa hatari sana.

Viungo vya hydrojeni huwezesha maji na tabia nyingine ya pekee kabisa ambayo husababisha maji kuwa mazito zaidi yakiwa katika hali ya majimaji kuliko inavyokuwa katika hali ya ugumu kwa mfano barafu.

Kiukweli bidhaa mbalimbali duniani huwa nzito katika hali yake ya ugumu kuliko ikiwa katika hali yake ya majimaji. Tafauti na bidhaa zingine, maji hutanuka pale yanapokuwa barafu. Hii ni kwa sababu atomu ya hydrojeni, viungo vyake hudhibiti molekuli ya maji kuwa na viungo vya vyenyewe kwa vyenyewe kwa namna isyo na nguvu kubwa, na kwa ajili hii nafasi nyingi huachwa kati yao. Viungo vya hydrojeni vinaweza vikavunjwa wakati maji yanapokuwa katika hali yake ya umajimaji, ambayo husababisha atomu za Oxyjeni kuja karibu sana na kusababisha umbile ambalo ni ngumu zaidi.

Hii vile vile husababisha barafu kuwa nyepesi zaidi kuliko maji. Kwa kawaida, unapoyeyusha chuma (metal) cha aina yoyote, na halafu ukatupia au kuchanganya na vipande vichache vya chuma (metal) kile kile, vipande hivi vitazama moja kwa moja chini. Kwenye maji, mambo ni tafauti kwani magunia ya barafu yenye maelfu ya tani huelea kwenye maji. Hivyo, kuna manufaa gani kwa tabia hii ya maji kwetu sisi?

Tujibu swali hili kwa kutazama mfano wa mto.Wakati hewa ni baridi sana, sio mto wote unaokuwa barafu bali inayokuwa barafu ni sehemu ya juu tu ya mto. Mfano huu ni madhubuti hasa kwa nchi za Ulaya ambayo hali ya hewa huwa wakati mwingine ni baridi sana. Maji huweza kufikia uzito wake wa mwisho ifikapo +4 oC. Na pindi inapofikia joto hili, huzama mara moja hadi chini. Barafu hutokeza juu ya maji mithali ya mtu aliyetandika kitu. Chini yake maji bado huweza kutiririka na kwa sababu joto la nyuzi +4oC huruhusu viumbe kuweza kuishi, hivyo maisha huweza kuendelea kwenye maji chini ya barafu.

Hali hii isiyo ya kawaida ambayo Muumba ameipa maji, inafanya maisha kuwezekana hapa duniani. Katika Qur'an tukufu Mwenyezi Mungu (s.w.) anaelezea umuhimu wa fadhila hii kubwa aliyompa binadamu kwa kusema:

Yeye ndiye anayekuteremshia maji kutoka mawinguni, kwa hayo mnapata kinywaji na kwa hayo (inaota) mimea ambayo humo mnalisha (wanyama); (Na kwa hayo) hukuotesheeni mimea (ya kila namna) na mizeituni na mitende na mizabibu na kila matunda. Na bila shaka katika hayo imo ishara kwa watu wenye kufikiri (kuwa yuko Mwenyezi Mungu (s.w.). [Surat-Nahl: 10-11].

Tabia za maji

Sote tunafahamu kuwa maji huchemka katika nyuzi joto 100oC na huganda katika nyuzi joto 0oC. Hakika, katika hali ya kawaida, maji yanapashwa kuchemka sio katika nyuzi joto 100oC. Kwanini?

Katika jedwali ya elementi (periodic table), tabia za elementi zilizo kwenye kundi moja zinatafautiana kutoka kwenye elementi nyepesi kuelekea kwenye elementi nzito. Hali hii hujithibitisha sana katika kompaundi za hydrojeni. Kompaundi za elementi zinazoshirikiana kundi moja na Oxyjeni katika jedwali ya elementi huitwa "Hyrides". Kusema kweli maji ni Hydride ya Oxyjeni. Hydride ya elementi nyinginezo kwenye kundi hili zina umbile la kimolekuli sawa kabisa na ile ya maji.

Viwango vya nyuzi joto vya kuchemka vya kompaundi hizi hutafautiana kwa namna ya ongezeko kutoka kwenye Sulphur kuelekea kwenye zilizo nzito. Hata hivyo, kuchemka kwa maji bila ya mategemeo huenda kinyume na hali hii. Maji (hydride ya Oxyjeni) huchemka katika 80oC chini zaidi ya inavyotakiwa.

Hali nyingine ya kushangaza inahusiana na joto la kuganda kwa maji kuwa barafu. Hapa pia kulingana na nafasi katika jedwali la elementi, maji yanapaswa kuganda katika nyuzi joto -100oC. Bado maji yanakiuka kanuni hii na kuganda katika 0oC, nyuzi joto 100oC juu ya joto lililokuwa linatarajiwa. Hii huleta swali akilini la kuwa kwanini sio hydride nyinginezo ila ile ya maji pekee inayokiuka misingi hii ya jedwali. Kanuni za kifizikia, vile vile za kikemia, na zote zile ambazo zimeorodheshwa kama sheria, zinajaribu kuelezea mambo yasiyo ya kawaida hapa ulimwenguni, na ufafanuzi wa kuwepo kwake. Utafiti wote katika karne ya 20 unaonesha kuliko wakati mwingine wowote kuwa uwiano uliopo hapa ulimwenguni ni kwa ajili ya kufanikisha maisha ya mwanadamu. Utafiti umedhihirisha kuwa kanuni zote za kifizikia, kemia, biolojia zilizopo ulimwenguni na angani, kwenye jua, kwenye atomu na molekyuli na kadhalika zimejitosheleza ili kufanikisha maisha ya binadamu. Maji kama yalivyo elementi zilizotajwa hapo awali, zinafaa kwa maisha kwa namna ambayo hailingani na majimaji ya aina nyingine yoyote. Maji yameshika nafasi kubwa katika dunia yetu kwa kiasi kamili kinachohitajika na mwanadamu. Ni wazi kuwa haya yote hayawezi kuwa yanatokea kwa kubahatisha, isipokuwa pamekuwepo na mpangilio maalum wa vitu vyote hapa ulimwenguni. Mwenyezi Mungu (s.w.) anasema:

Mwenyezi Mungu ndiye aliyeziumba mbingu na ardhi na akateremsha maji kutoka mawinguni. Na kwa hayo akaotesha matunda kuwa riziki kwa ajili yenu. Na akakutiishieni majahazi ili yapite katika bahari kwa amri yake, na akakutiishieni mito. Na akakutiishieni jua na mwezi, maisha yao (yanafanya yaliyaamrishwa, ya kuchomoza na kuchwa na mengineyo kwa ajili ya manufaa yenu). Na akakutiishieni usiku na mchana. Na akakupeni kila mlichomuomba (na msichomuomba). Na kama mkihesabu neema za Mwenyezi Mungu, hamtaweza kuzihisabu. Bila shaka mwanadamu ni dhalimu mkubwa asiyeshukrani (mwizi wa fadhila). (Surah Ibrahim: 32-34)

Tabia ya kushangaza ya kifizikia na kikemia ya maji inaonesha kuwa kmiminika hichi kimeumbwa makusudi kwa ajili ya maisha ya mwanadamu. Mwenyezi Mungu (s.w.) ametoa maisha kwa watu kwa kupitia maji na kutoka kwenye maji ameleta yote ulimwenguni yanayofaa maisha. Allah (s.w.) amewataka watu watafakari maelezo haya kama ilivyo kwenye Qur'an:

Na yeye ndiye aliyeteremsha maji kutoka mawinguni, na kwayo tunaotesha mimea ya kila kitu. Kisha tunapelekea kuchipua majani ya kijani katika (mimea) hiyo; tukatoa ndani yake punje zilizopangana. Na katika mitende (vinatoka) katika makole yake vishada vyenye kuinama (vinakaribia kufika chini kwa vilivyotia, hata vimekuwa vizito). Na anakuotesheni bustani za zabibu na zaituni na makomamanga, yanayofanana na yasiyofanana. Angalieni matunda yake yanapotoa na (angalieni) kuwiva kwake. Bila shaka katika hayo ziko hoja (kubwa) kwa watu wanaoamini. (Surat al-An-am: 99).

Kinga ya juu angani: Ozone

Hewa tunayovuta, tuseme ni sehemu ya chini ya anga, ipo katika mahali ambapo hewa ya Oxyjeni ndiyo inayotawala. Kwa hewa ya Oxyjeni tuna maana O2. Hii ni kusema molekuli ya Oxyjeni inaweza wakati mwingine ikawa na atomu tatu O3. Kwa hivyo ile iliyopo katika sehemu ya chini ya anga mara nyingi ni Oxyjeni yenye atomu mbili (O2). Sehemu ya juu yenye molekuli yenye atomu tatu (O3) haiitwi Oxyjeni tena bali huitwa "Ozone" kwa sababu hewa hizi mbili zinatafautiana sana kutoka moja hadi nyingine.

Ni muhimu tuelezee hoja moja hapa kwamba wakati Oxyjeni hutokea wakati atomu mbili za Oxyjeni zinajumuika pamoja, kwanini gesi tafauti ya Ozone itokee wakati atomu tatu za Oxyjeni zinapoungana? Mwisho wa yote, je, si atomu za Oxyjeni zinazoungana iwe ni mbili au tatu? Sasa vipi iweje gesi mbili tafauti zitokee? Kabla hatujajibu maswali haya, ingekuwa vizuri tuone vipi gesi hizi mbili zinavyotafautiana.

Hewa ya Oxyjeni (O2) inapatikana katika sehemu ya chini ya anga na hutoa maisha kama pumzi kwa kila kiumbe. Ozone (O3) ni gesi ya sumu ambayo ina harufu mbaya sana. Inapatikana katika tabaka la juu kabisa la anga. Kama ingekuwa tuvute hewa ya Ozone badala ya Oxyjeni hakuna yeyote angekuwa hai.

Ozone ipo katika anga ya juu, kwa sababu pale ina kazi muhimu kwa maisha. Hufanya tabaka nzito yenye kina cha mithili ya kilometa 20 juu ya anga kuzunguka dunia. Tabaka hili haliruhusu mionzi kama ya ultraviolet inayotolewa na jua, kuifikia dunia katika kiwango chake. Kwa sababu ultraviolet ina nguvu kubwa sana, kufika kwake duniani kungesababisha vitu vyote kuungua na kusababisha kutoweka kwa maisha. Kwa sababu hii, tabaka la Ozone ni kama ngao ya kinga angani.

Ili maisha yawepo hapa duniani, kila kinachoishi lazima kiweze kupumua na kuweza kujikinga na mionzi iumizayo kutoka kwenye jua na vinginevyo. Yule anayetengeneza mfumo huu wa kinga ni Muumba ambaye anatawala kila atomu na kila molekuli iliyopo. Bila kuwepo uwezo wa Allah (s.w.), hakuna yeyote angeweza kuzifanya atomus hizi zifanyazo gesi ya Oxyjeni na Ozone katika viwango hivi madhubuti.

Molekuli tunazoonja na tunazonusa

Sehemu za mwili zinahusika na vionjo pamoja na vinuso zinaleta hisia ambazo hufanya maisha ya mwanadamu hapa duniani kuwa ya burudani sana. Furaha inayopatikana kwayo, imekuwa ni jambo la kupendeza tokea siku nyingi na imegunduliwa hivi karibuni tu kuwa hii husababishwa na maingiliano ya molekuli. "Onjo" na "harufu" ni hisia ambazo zinasababishwa na molekuli tafauti katika viuongo vyetu vya fahamu. Kwa mfano, harufu ya chakula. vinywaji au matunda ya aina mbalimbali na hata mauwa tunazonusa zinakuwa na molekuli ambazo huwa mvuke. Sasa hii hutokea vipi?

Molekuli fukivu kama vile harufu nzuri ya (vanila) lavani au waridi (rose) huvifikia vinyweleo katika sehemu ya pua iitwayo "epithelium" na maingiliano baina yao huleta hisia ya mnuso mzuri sana. Hivyo hivyo kama harufu ya Miski. Maingiliano haya hufika na kupokelewa mpaka kwenye ubongo wa binadamu. Mpaka sasa hivi aina saba tafauti ya mapokezi (receptors) zimekwisha tambulika katika mifereji ya pua (nosal cavity) ambayo imeambatishwa an ngozi nyepesi ya kunusia (smelling membrane) kwenye eneo kama sentimenta za mraba kiasi cha 2 au 3. Zote kati ya sehemu hizi za mapokezi ya vinuso hunasibishwa na harufu ya msingi. Hivyo hivyo kuna sehemu nne tafauti za mapokezi ya kikemikali sehemu ya mbele ya ndimi zetu. Hizi zinakwenda sambamba na onjo za chumvichumvi, utamu (sukari), uchachu (sour) na uchungu (bitter). Ubongo wetu unapokea molekuli zinazofika kwenye mapokezi haya kama wimbi la umeme litokanalo na kemikali. Imegunduliwa jinsi onjo na vinuso vinavyopokelewa na jinsi inavyotokea na bado wanasayansi hawajakubaliana kwa nini baadhi ya bidhaa au vitu vina harufu kali na vingine vina harufu nyepesi au havina harufu kabisa. Halikadhalika kwa nini vitu vingine vinanukia na vingine vinanuka .

Tafakari kwa dakika moja. Tungekuwa tunaishi katika duniya isiyokuwa na manukato au mnuko. Kwa sababu hatujui kuhusu vionjo au vinuso isingetokea kwetu sisi kuwa na hisia zozote. Kwanini sasa atomu hizi ambazo kwa upande mmoja huja pamoja na namna isiyo ya kawaida na kufanya maada (matter) huunganika na kwa upande mwingine, kutoa muonjo na manukato? Ijapo kuwa tunazichukulia kiurahisi na bila ya kujali zinatusaidiaje, zinasababisha burudani ya pekee kwa dunia yetu hii katika namna ya usanii mkubwa. Ama, kwa upande wa maisha ya viumbe vingine, baadhi hula majani na wengine vyakula vya aina mbalimbali. Ni wazi kuwa hakuna kati ya hizi zinazonukia vizuri na kuwa na uonjo mzuri. Hata kama zingekuwa nazo basi hazina thamani yoyote kwao kwani hazina fahamu kama walivyo binadamu. Sisi vile vile, tungeweza kuwa tunakula aina moja tu ya chakula kama wao. Je, umewahi kufikiri jinsi ambavyo ingelikuwa kuna labda aina moja tu ya chakula na maji kila siku? Hivyo onjo na mnuso kama ilivyo kwa vyote tumekirimiwa na Allah (s.w.), mmiliki wa kila kitu na mwenye fadhila isiyo na kikomo. Amemtunuku binadamu kwa fadhili zake. Upungufu wa viungo hivi viwili peke yake ungefanya maisha ya binadamu kuwa ya kinyonge sana. Kwa shukrani ya fadhila zote hizi alizopewa binadamu, anachotakiwa kufanya ni yale yanayomridhia Allah (s.w.) kwa fidia ya tabia hii, Mwenyezi Mungu ameahidi maisha mazuri na makubwa, ambayo hayana upungufu na yamejazwa fadhila kubwa zaidi ya yale tuliyopewa hapa duniani ambazo ni chache kwa yale ya akhera. Kinyume na hapo maisha yanayokosa kumshukuru Allah (s.w.) kwa kutojali, itakuhumiwa vile vile:

"Na (kumbukeni) alipotangaza Mola wenu (kuwa) kama mkishukuru, nitakuzidishieni, na kama mkikufuru (jueni) kuwa adhabu yangu ni kali sana". [Surat Ibrahim: 7]

Tunaitambuaje maada (Matter)?

Kwa yale tuliyoyaeleza mpaka sasa, imedhihirisha kuwa tunachokiita maada (matter) sio tu kile kitu maalum tu chenye rangi, harufu na onjo fulani kama tulivyoamini kuwa hivyo. Tulichofikiria kuwa ni maada (matter) ni miili yetu, vyumba vyetu, majumba yetu, dunia yetu na ulimwengu mzima, kuwa si chochote ila ni nishati (energy) ya aina fulani. Sasa je kitu gani kinachosababisha vinavyotuzunguka viweze kushikika na kuonekana?

Sababu inayotufanya tuhisi vitu vinavyotuzunguka kama maada (matter) ni migongano ya elektron katika njia zake kwenye atomu ambazo huwa na proton na neutron. Vile vile atomu zimepokuwa na uwezo wa kuvutana au kusukumana.

Tuseme usingekuwa unagusa kitabu ambacho umekishika katika mikono yako ya kulia. Kusema kweli, atomu za mikono yako zinaisukuma atomu za kitabu na hisia za kugusa hutegemea ukubwa wa misukumo ya atomu hizi. Kama tulivyotaja wakati tulipozungumzia maumbile ya atomu, kuwa zinaweza zikaja karibu na nyinginezo kwa umbali usiozidi kipenyo cha atomu. Zaidi ya hapo, atomu pekee zinaweza kuwa karibu kiasi hiki ni zile zinazoingiliana baina yao. Kwa hiyo, wakati hata atomu za kitu kimoja haziwezi kugusana, haiwezekani katu sisi kugusa vitu tunavyovishika, kuvikandamiza au kuvibeba katika mikono yetu. Hakika kama tungeweza kuwa karibu sana na vitu vilivyo katika mikono yetu basi kungetokea maingiliano ya kikemikali (chemical reaction) baina yetu na vitu hivyo. Kwa maelezo haya isingewezekana kwa binadamu au kiumbe chochote kuendelea kuishi hata kwa dakika moja.

Viumbe vinavyoishi vingeingiliana na hatimaye kudhurika kutokana na vitu vyote wanavyoshika, wanavyokanyaga, wanavyokalia au wanavyoegemea na kubadilika kuwa vitu vingine tafauti baada ya maigiliano haya.

Picha ya mwisho inayojitokeza katika hali hii ni muhimu sana: Tunaishi katika dunia ambayo asilimia 99.95 imejazwa na atomu ambazo zimejaa nguvu (energy) [37]. Kwa hakika hatugusi chochote tunachosema "tunashika na tunabeba".

Hivyo, ni kwa kiasi gani tunavyotambua maada tuonavyo, tuvisikiavyo na tuvinusavyo? Je, vitu hivi vipo kweli kama tunavyoviona au kuvisikia? Kabisa sio hivyo. Tuligusia jambo hili tulipozungumzia kuhusu elektrons na molekuli. Kumbuka, ni kitu kisichowezekana kwetu sisi kuona maada (matter) tunayoamini kuwepo na tunavyoiona, kwa sababu kile ambacho tunaita kuona hujumuisha vitu kama vivuli (images) vinavyofanyika katika ubongo wetu kutokana na photons zitokeazo kwenye mwanga kama wa jua au kifaa kingine. Mwanga huu hugonga maada ambayo huchukua sehemu ya mwanga ifikayo na kuachia au kutupa zilizobakia ambazo hufika kwenye macho yetu. Hii ndio kusema maada (matter) tunayoona ni ile tu tunayoipata kutoka kwenye photon zinazoifikia macho yetu. Sasa, kiasi gani ya takwimu zinazotokana na maada inayotufikia sisi? Hatuna uthibitisho wa hali ya awali ya maada iliyo mbali na ile tu iliyotufikia.

 
   
    
2 / total 4
You can read Harun Yahya's book Muujiza Katika Chembe Ya Atomu online, share it on social networks such as Facebook and Twitter, download it to your computer, use it in your homework and theses, and publish, copy or reproduce it on your own web sites or blogs without paying any copyright fee, so long as you acknowledge this site as the reference.
About this site | Tengeneza kurasa yako ya nyumbani | Add to favorites | RSS Feed
Mambo yote yanaweza kuynakiliwa, kuchapwa na kusambazwa kwa kurejea katika kurasa hii
(c) All publication rights of the personal photos of Mr. Adnan Oktar that are present in our website and in all other Harun Yahya works belong to Global Publication Ltd. Co. They cannot be used or published without prior consent even if used partially.
© 1994 Harun Yahya.www.harunyahya.com
page_top