Muujiza Katika Chembe Ya Atomu

SHUSHA KITABU

Download (DOC)
Maoni

SURA ZA KITABU

< <
3 / total: 4
Muujiza katika chembe ya Atomu - Harun Yahya
Muujiza katika chembe ya Atomu
   

 


Atomu zijazo hai

Mpaka wakati huu, tumezungumza kuhusu atomu na jinsi maada (matter) inavyoumbwa pasipo na chochote. Tulisema kuwa atomu ni matofali yanayojengea kila kitu ama chenye uhai au kisichokuwa na uhai. Ni muhimu kufahamu kuwa atomus hujenga vitu vyote vilivyo na visivyo uhai. Kwa sababu atomu ni chembechembe isiyo hazina uhai, inashangaza jinsi zinavyoweza kuwa matofali ya kujengea miili yenye uhai. Hili ndilo jambo ambalo ni vigumu kuelezeka.

Kama ilivyo vigumu kufikiria jinsi vipande vya mawe kuwepo pamoja na kusababisha uhai wa viumbe, vile vile ni vigumu kuelewa jinsi ambavyo atomu zisizo na uhai zinavyoweza kusababisha uhai. Fikiria lundo la jabali na kipepeo ambapo moja haina uhai na nyingine ina uhai. Bado, tunapofikiri vyanzo vyake, tunaona zote zinatokana na chembechembe hizi ndogo za atomus.

Mfano ufuatao unaweza kuwa na maelezo zaidi kuhusu kutokuwezekana kwa maada isiyo hai kujigeuza baadaye kuwa na uhai.

Je, Aluminium itaweza kuruka? Jibu ni hapana. Tukichanganya aluminium na plastiki na petroli je itaweza kuruka? Jibu ni hapana. Pale tu tunapoviweka vitu hivi pamoja na kujenga ndege ya Aeroplane ndipo inapoweza kuruka.

Kwa hiyo ndege yenye mbawa, injini na rubani wa kuiendesha huweza kuruka. Haziwezi kuruka pekee bila ya mwendeshaji. Kwa hakika zote, ndege huwa ni michoro na uhakiki madhubuti ikifuatiwa na ujenzi wa uhakika wa ndege ndio baadaye huweza kuruka.

Vitu vyenye uhai navyo si tafauti sana. Cell yenye uhai hufanyika kwa mpangilio maalum wa atomu katika matengenezo madhubuti sana. Uwezo wa chembe chembe hizi za uhai (Cell) kama kukua, kuzaliana na vinginevyo ni matokeo ya mpango mahsusi zaidi kuliko tu kuwa ni tabia ya molekuli. Mpango huu tunaouona hapa ni wa Allah (s.w.) kaumba maisha kutoka kwenye vitu visivyo na maisha:

Mwenyezi Mungu ndiye mpasuaji (mwoteshaji) wa mbegu na kokwa (zikawa miti). Hutoa nzima katika maiti, naye (pia) ndiye mtoaji maiti katika mzima. Huyo ndiye Mwenyezi Mungu. Basi mnageuzwa wapi? (Surat Al-An’am: 95).

Ni Mwenyezi Mungu (s.w.) Mwenye nguvu na mwenye busara anayeweza kuvipa maisha vitu visivyo na uhai, hivyo kuumba viumbe hai. Mtandao wa maisha huwa katika muundo wa ajabu sana ambao huwa taabu kuelezea hasa pamoja na kuwepo kwa teknolojia ya hali ya juu kabisa ulimwenguni leo hii. Hata hivyo, kuna ukweli wa namna fulani unaotuwezesha sisi kufahamu maendeleo haya kwa msaada wa sayansi na teknolojia ya kisasa katika karne hii ya 21.

Maisha ya viumbe ni kitu ambacho kuwepo kwake ni kwa namna ya ajabu sana isiyo ya kawaida. Wakati maelezo ya Evolution yalipotolewa katika karne ya 19, utafiti uliofanywa kisayansi kupitia vikuza vitu (Microscope) vya hali ya chini sana vilionyesha kuwa Cell ni kama tu mkusanyiko wa maada (matter) .

Katika karne ya 20, uchunguzi na utafiti uliofanyika kwa kutumia vifaa bora zaidi kama Electron Microscope ulionyesha Cell ambazo ni kama matofali ya kujengea maisha, ambayo ilikuwa na umbile la ajabu kabisa ambalo lingeweza kuwepo kwa mpango ambao si wa kawaida kwa mwanadamu.

Muhimu zaidi ni kuwa, utafiti ulionesha kuwa Cell hizo haziwezi kuwa zimetokeza tu kwa kubahatisha kutokana na visivyo hai. Chanzo cha maisha na maisha pekee. Ukweli huu umedhihiri kwa majaribio [38].

Hili ndilo tatizo ambalo nadharia ya Evolution imeshindwa kupata ufumbuzi. Tatizo hili limewafanya wanasayansi wa Evolution kushindwa kutoa ukweli wa kisayansi na badala yake kueleza hadithi ambazo hazisemi chochote zaidi ya michapo ya mtu anayetazama dirishani na kujaribu kuelezea anayoyaona. Zinaweka mbele yote yasiyo na busara na hazina ushahidi wa kisayansi kuwa maada zina akili, uwezo, na matakwa ya namna yake. Hata hivyo vile vile hadithi hizo nazo hawaziamini na mwisho wake wanakiri kuwa maswali makubwa hayawezi kujibika kisayansi:

Kuna wakati mmoja kabla ya maisha yetu, wakati dunia ilikuwa jangwa kiasi cha kuhuzunisha. Dunia yetu leo hii imeshamiri maisha. Je, hii ilitokeaje? Vipi bila maisha, molekuli za Organik ziliweza kutokea? Je, ilikuwaje kutokea kwa maisha ya mwanzo? Ilikuwaje kwa vitu hai kujitengeneza katika namna hii ya ajabu na kwa chanzo kipi? [39].

Kufahamu maajabu ya kuumbwa ni majibu ya chanzo cha maada, jinsi ilivyotokea katika dunia na ulimwengu wetu huu na kwa nini itokane na molekuli hai kwa namna ya ajabu. [40]

Kwa jinsi wanamapinduzi wa kisayansi wanavyokiri, malengo ya msingi ya nadharia ya Evolution ni Mwenyezi Mungu (s.w.) aliyemuumba wa vyote vilivyo hai na visivyohai. Ijapokuwa, ukweli wa uumbaji umewekwa wazi katika mtizamo wote wa ulimwengu na yote yaliyomo unaonesha dhahiri kuwa kila unapotafuta undani unakuta unatokana na mpango madhubuti sana. Umadhubuti ambao akili ya binadamu haiwezi kufanya maumbile haya na vile vile haiwezi kuwa umetokea tu kwa kubahatisha. Nadharia hii inajitahidi kutumia akili ya kibinadamu kujichanganya changanya. Mwenyezi Mungu (sw) anatueleza kwenye Qur’n:

Vipi mnamkanusha Mwenyezi Mungu na hali mlikuwa wafu, akakuhuisheni, kisha atakufisheni, kisha atakuhuisheni, kisha kwake mtarejeshwa (atakapokufufueni). (Al-Baqara:28).

Badala ya kuamini ukweli, wanasayansi wa Evolution hupendelea kuongea kuhusu uwezo wa maada na jinsi vitu visivyo na uhai vinavyoweza kujibadilisha kuwa vile vyenye uhai. Wakati wanafumba macho kwenye ukweli, wanasayansi hawa wanajiweka mahali ambapo huweza wakapata aibu. Ni wazi kuwa shutuma za kuwa atomu zina namna fulani ya uwezo na hutumia uwezo huo kujibadilisha kuwa kwenye vitu hai haina uhusiano na namna yetu ya kutafakari mambo.

Baada ya kusoma mfano tutaounukuu, nawe utaamua upendavyo kuhusu hekaya hizi zisizo na ukweli za Evolution. Hapa ndipo mahala wana Evolution hudai kuwa mabadiliko ya visivyo na uhai kuwa vyenye uhai, na muhimu zaidi kuwa watu wenye uwezo wa juu wa akili na ufahamu.

Baada ya mlipuko mkubwa unaoitwa Big Bang atomu zilizo na nguvu kubwa zenye uwiano madhubuti, kwa namna fulani zimejileta kwa kuwepo kwake. Wakati baadhi ya atomu zenye kujitosheleza kwa idadi kufanya ulimwengu mzima, zimeifanya nyota na sayari mbalimbali, na vile vile dunia yetu hii.

Baadhi ya atomu zilizofanya dunia, mwanzo zilifanya ardhi na baadaye, haraka kufanya viumbe hai! Atomu hizi zilijibadilisha kuwa Cells kwa umbile la hali ya ajabu kabisa na kutoa Cells nyingi zilizogawanyika mara mbili na baadaye kuanza kuzungumza na kusikia.

Hivyo hivyo, atomus hizi zikajigeuza kuwa Maprofesa katika vyuo vikuu, vikijitizama kwenye vikuza umbile (electron microscope) na kujinadi kuwa zimejitokeza kwa bahati mbaya. Baadhi ya atomu zikajifanya wahandisi wa ujenzi na kuanza kujenga madaraja na maghorofa makubwa. Wengine wakajenga vyombo vya angani na atomu zingine kujigeuza kuwa wataalamu wa fizikia, kemia na bailojia.

Atomu kama zile za Carbon, Magnesium, Phosphorns, Potassium na Iron zikaungana badala ya kuunda bonge kubwa la kitu cheusi ikaunda ubongo madhubuti na wa ajabu, ambao siri yake mpaka sasa haijajulikana kwa ukamilifu.

Ubongo ukawa unaona vitu kwa daimensheni-3 katika namna ya usahihi kabisa ambayo teknolojia tuliyonayo sasa hivi haijaifikia. Baadhi ya atomu zikafanya vichekesho na zikatuchekesha. Na baadhi yake kutengeneza muziki ambao watu hufurahia kusikiliza.

Inawezekana kurefusha aina hii ya simulizi, lakini ni vizuri tuishie hapa na tutengeneze majaribio (experiment) kuonesha kuwa simulizi hizi sio za kweli na haikubaliki. Tuwaachie wana Evolution wachukue atomu nyingi wazipendazo kwenye pipa, kwa elementi zote wapendazo zinazosababisha maisha. Tuwaachie wachanganye na waongeze chochote kilicho hapa ulimwenguni katika atomu hizi na halafu wasubiri. Wasubiri kwa miaka 100, 100 na ikiwa lazima miaka 100 milioni kuona kama kuna mtoto yeyote atakayezaliwa. Au tuseme kama kuna Profesa atakayetokea hapo.

Ni wazi kuwa haitatokea, kwa muda wowote watakaosubiri. Si hivyo tu bali hakutatokea, maisha kama ndege, samaki, vipepeo, nyani, tembo, mauwaridi, michungwa, nyuki, mbu wala kitu chochote chenye maisha.

Atomu zisizo na fahamu zatoa DNA!

Swali la kujiuliza ni kama Atomu zisizo na fahamu iwapo zinaweza kujilipukia tu na kufanya molekuli za DNA ambazo ni msingi wa maisha na protini.

DNA(Deoxyribonucleic Acid) ni jina la kitaalamu kwa tindikali hii, ambayo katika nucleasi ya celli, inakusanya njia kuu zote za mwili wa binaadamu.

Siri ya njia hizi za fahamu ni mtandao mgumu na wa ajabu sana kiasi ambacho wanasayansi wengi imekuwa vigumu kuutafsiri angalau kwa uchache mpaka kwenye miaka ya 1940 hivi. DNA ambayo huwa na taarifa zote muhimu zinazohusu maisha, vile vile huwa na uwezo unaotokana na mkusanyiko wa atomu zinazohifadhi na jinsi zinavyozaliana kwa kujirudufisha bado ni maswali yasiyo na majibu.

Protini ni matofali yajengayo maisha ya viumbe na huwa na kazi muhimu katika shughuli muhimu za viumbe. Kwa mfano, haemoglobin ambayo ni sehemu muhimu kwenye damu husafirisha Oksijen mahali pote katika mwili, wakati “antibodies” hukinga maradhi katika miili yetu, na “enzymes” husaidia kuyeyusha vyakula tulavyo na kugeuza ili tupate nguvu. Fomula inayopatikana katika DNA yetu utengenezaji wa aina 50,000 tafauti za protini. Kama ilivyo wazi, protini ni muhimu sana kwa maisha ya viumbe hai na kutokuwepo kwake kutafanya maisha kutokuwezekana. Haiwezekani kisayansi kuwa DNA na protini kila mojawapo ikiwa ni molekuli kubwa, muhimu kuwa ni kitu tu cha kujitokezea kwa kubahatisha hivi hivi. Mwenyezi Mungu SW anatuambia katika Qur’an tukufu:

Kinamtukuza Mwenyezi Mungu kila kilichomo mbinguni na ardhini, na yeye ndiye mwenye nguvu, mwenye hikima. Ufalme wa mbingu na ardhi ni wake, Anahuisha na kufisha. Na yeye ni Mwenye uweza juu ya kila kitu(surat alhadid:1-2).

DNA ni mfululizo wa mpangilio madhubuti wa kile wanasayansi wanachokiita “nucleotides”. Protini ni mfululizo vile vile wa tindikali ya “Amino” iliyo katika mpangilio madhubuti sana. Kwanza kabisa, kimahesabu haiwezekani kuwa ama molekuli ya DNA au ya protini ambazo huja katika maelfu ya aina kuamua kuchgua aina maalum ambayo ni umuhimu kwa maisha kwa kubatisha. Katika mahesabu ya kubahatisha ya probability inaonesha kuwa uwezo kuwa molekuli ya protini kuweza kufikia usahihi wa kuweza kubahatisha kwa ajili ya maisha ni sifuri. Tunachoweza kusema ni kuwa yote haya yameumbwa na Mwenyezi Mungu (s.w) ambaye ni mkamilifu wa kila kitu.

Kwa nyongeza ya hili ya kutokuwezekana kwa kimahesabu, kuna matatizo ya kimsingi ya kikemikali kwamba molekuli hizi zimetokea kwa kubahatisha. Ikiwa uhusiano kati ya DNA na protini ni matokeo ya muda, kubahatisha, pilika pilika za asili, basi kungekuwa na tabia ile ya kikemikali kwa molekuli hizi za DNA na protini kuingiliana, kuchanganyikana, kuathiriana kwa sababu tindikali na kinyume chake huathiriana. Kwa mantiki hii, kama kubahatisha ingekuwa na nafasi hivyo basi, tindikali za sukari, aminephosphoric na kemikali zote za asili zingeathiriana na mtandao mzima wa DNA na protini, hivyo maisha yote tuonayo leo hii yasingekuwepo.

Je tabia hii ya asili ya vipande vya DNA na protini kuathiriana kikemikali, hupendekeza kuwa muda, kubahatisha na kanuni za kikemikali, mwisho wake utasababisha maisha kutokana na mchanganyiko huu wa molekuli? Jibu ni hapana na tuseme ni kinyume chake. Tatizo ni kuwa athari yote ya hizi kemikali za asili ni ile yenye madhara kama maisha hasa inavyohusika. Kuachia muda, ubahatishaji na tabia ya kikemikali ya DNA na protini, athari yake ni maangamizi ya maisha na maendeleo ya kuishi. Mwenyezi Mungu(s.w) anatueleza katika Qur’an kwamba:

Na vinamsujudia Mwenyezi Mungu vyote vinavyokwenda mbinguni na katika ardhi; katika wanayama na malaika pia nao hawatakabari. Wanamuogopa Mola wao aliye juu yao, na wanatenda wanayoamrishwa.(Surat an Nahal:49-50).

Kama tunavyoona, ni kuwa haitowezekana kwa DNA na protini ambayo kwa namna yoyote ile haiwezi kufanyika hovyo hovyo bila ya kuwa na mdhibiti ili kuifanya kuwa maisha. Bwana mmoja aitwaye Jean Gruiton, mwanafalsafa akielezea kutokuwezekana huku katika kitabu chake kiitwacho”Dieu et la Science”(Mwenyezi Mungu na sayansi), anasema kuwa maisha yasingewezekana kutokea kwa kubahatisha:

Kutokea na “kubahatisha” kupi ambako atomu zinasogeleana kufanya molekuli za amino acid? Vile vile, kwa vipi kubahatisha kutokee DNA”, anauliza maswali haya rahisi kama mwanasayansi wa kibailojia kama alivyofanya Francois Jacob:

“ Nani aliyepanga kuwepo molekuli ya DNA ya awali, kutoa taarifa ya kuzaliwa kwa Cell ya mwanzo iliyo hai”?

Kama kuna yeyote anayeridhika na dhana hii ya kubahatisha, maswali haya na mengine mengi bado hayana majibu; Hii ndio sababu wanabaiolojia wengi miaka hii ya karibuni wameanza kubadili mitazamo yao. Bado watafiti wakubwa hawaridhishwi na kanuni za Darwin, bila ya kufikiri zaidi upungufu wa nadharia hizi. Nadharia hizi zimeegemea wazo la uongozi kuliko mabadiliko ya maada.

Bwana Jean Guitton anasema sayansi imefikia mahali ambapo, kwa mwanga uliopatikana baada ya tafiti za uvumbuzi mbali mbali kwenye karne ya 20, kuwa Nadharia za Darwin za “evolution” hazinapakushika kwa vyovyote vile. Mwanasayansi, mwanabiolojia aitwaye Michael Behe anazungumzia jambo hili kwenye kitabu chake kiitwacho Darwin’s Black Box(Boksi jeusi la Darwin:

“Sayansi imepiga maendeleo makubwa katika kufahamu jinsi kemia ya maisha inavyofanya kazi, lakini ugumu na uthabiti uliopo katika maumbile ya molekuli zifanyazo maumbile ya kibaiolojia, zimefanya sayansi kupata taabu kuyatolea maelezo. Imeshindikana kutoa ufafanuzi wa chanzo hasa cha vitu maalum kama “biomolecular”, angalau tu kwa maendeleo yake.

Kama jinsi ulimwengu mzima ulivyoumbwa pasipo na chochote, hivyo hivyo viumbe viishivyo vimeumbwa pasipo na chochote. Kama tuseme hakukuwa na chochote inavyotokea ikiwepo bila ya kuwepo chochote kwa kubahatisha, vitu visivyo na uhai hawezekani kujiunganishi kwa kubahatisha kufanya vilivyohai. Ni Allah(s.w), Mmiliki wa uwezo usio na kifani, mwenye busara na ufahamu usio na kifani ndiye Mwenye Nguvu ya kufanya vyote hivi: Qur’an:

Hakika Mola wenu ni Mwenyezi Mungu aliyeziumba mbingu na ardhi kwa siku sita. Kisha akatawala juu ya arshi yake. Huufunika usiku kwa mchana, uufuatiao upesi upesi). Na (ameliumba) jua na mwezi na nyota> (Na vyote vimetiishwa kwa amri yake(Mwenyezi Mungu) viwe vya manufaa makubwa(nanyi). Fahamuni kuumba( Ni kwake tu Mwenyezi Mungu) na amri zote ni zake(Mwenyezi Mungu). Ametutaka kabisa Mwenyezi Mungu, Mola wa ulimwengu wote(Suratil Al Aaraf: 54).

Nguvu kubwa ya Atomic/Nuklea

Tunafahamu jinsi atomu, matofali ya vitu vyote hapa ulimwenguni, vilivyo na visivyo na uhai, zinavyofanya maada (matter) kwa namna ambayo siyo ya kawaida. Tulitathimini kabla, chembe chembe hizi ndogo sana na kuona jinsi zilivyo kwenye mpangilio madhubuti sana baina yao. Maajabu ya atomu hayaishii hapo tu bali vile vile ina uwezo wa kutoa nguvu kubwa isiyo na kifani.

Nguvu hii iliyojificha katika atomu ni kubwa sana kiasi ambacho ugunduzi wake umewezesha mwanadamu kujenga mifereji inayounganisha bahari, uchimbaji katika milima, utengenezaji wa mazingira isiyo asili, na kukamilisha miradi mbalimbali ya maendeleo.

Hata hivyo, pamoja na nguvu hii kutumika kuhudumia binadamu kwa upande mmoja, imekuwa ikitumika kwa namna ya hatari sana kwa binadamu wenyewe kwa upande wa pili. Kwa namna ambayo nguvu hii kubwa imekuwa ikitumika vibaya, maelfu ya watu wamepoteza maisha yao kwa muda mfupi sana.

Mifano mizuri ni ile ya Hiroshima na Nagasaki huko Japan wakati wa vita vya pili vya dunia. Katika siku za karibuni, ajali ilitokea huko Chernobyl-Ukraine - Urusi ya zamani wakati mitambo ya Nuclear iliposababisha vifo na majeruhi ya idadi kubwa ya watu.

Kabla hatujatoa taarifa kuhusiana na matukio hayo ya nguvu ya Atomu katika Hiroshima, Nagasaki na Chernobyl, labda tutazame kwa uchache namna nguvu hii kwenye atomu ilivyo na inavyotokea.

Nguvu kubwa iliyojificha kwenye Nucleus

Katika maelezo yetu ya awali kuhusu “maajabu ya maumbile ya atomu”, tulisema kwamba nguvu inayoiweka proton na neutron pamoja katika Nekleas ya atomu ni ile yenye uwezo mkubwa sana (the strong nuclear force). Asili ya nguvu kubwa itokanayo na nukleas husababishwa na sehemu ndogo kabisa ya nguvu hii katika nukleas. Ukubwa wa nguvu hii hutegemea sana na aina ya elementi husika kwa sababu idadi ya protons na neutrons katika nukleas ya kila elementi hutafautiana.

Kwa kiasi nukleas inavyokuwa kubwa, idadi ya neutrons na protons pamoja na nguvu inazoziweka pamoja huongezeka.

Ni vigumu sana kutoa nguvu hii kwani ndizo zinazotumika kuiweka protons na neutrons pamoja katika nukleas. Jinsi chembe chembe hizi zinapokuwa mbali baina yao, inakuwa kama upinde uliokaza kwamba hujaribu kujirudisha kwa nguvu kubwa pale unapovutwa.

Kabla hatujaendelea kwa undani kuhusu nguvu hii labda tu tutafakari tena zaidi. Itakuwaje nguvu kubwa kiasi hiki kuwa katika sehemu ndogo sana kama ya nukleas?

Hii ni nguvu (force) kubwa ambayo imegunduliwa baada ya miaka mingi ya utafiti na maelfu ya watu. Inapokuwa haijatumiwa vibaya inakuwa haina madhara lakini pindi inapotumiwa vibaya inaweza kuuwa mamilioni ya watu.

Aina mbili za matokeo ya teknolojia inayoitwa Fi-sheni (fission) na Fu-sheni (Fussion) huweza kutoa nguvu kubwa sana na ya ajabu kabisa kutoka kwenye nukleas ya atomu, ambayo huweza kuhatarisha mamilioni ya maisha ya binadamu na wanyama (viumbe).

Ijapokuwa milipuko hii kwa mara ya kwanza huonekana hutokea kwenye nukleas ya atomu, lakini kwa uhakika huhusisha sehemu yote ya atomu. Mlipuko unaojulikana kama Fi-sheni husababisha mpasuko ambao Nukleas hujigawa vipande vipande na ile ya Fu-sheni huleta mkusanyiko wa nuklei mbili pamoja kwa nguvu kubwa kabisa. Katika aina zote mbili nguvu kubwa sana isiyo kifani na kwa ajabu kabisa hutolewa.

Fission (Fi-sheni)

Fisheni ni mlipuko katika nuklea ambapo nukleas ya atomu ambayo huwekwa pamoja kwa nguvu kubwa sana “the strong nucleas force” hupasuka na kuwa vipande vipande. Aina ya malighafi inayotumika katika majaribio ya fisheni (fission) ni ile iitwayo Uranium, kwa sababu atomu za Uranium ni kati ya zile zenye uzito mkubwa kabisa. Kwa maneno mengine ni kuwa kuna idadi kubwa sana ya protons na neutrons katika nukleasi yake.

Katika majaribio ya Fi-sheni, wanasayansi wamekuwa wakiigonga nukleasi ya Uranium kwa kutumia neutron yenye mwendo wa kasi sana. Wamekalibiana na hali ya kushangaza sana. Baada ya neutron kuingia katika nukleasi ya uranium, nukleasi hiyo imekuwa si imara au tuseme si madhubuti tena.

Inapokuwa nukleasi siyo madhubuti wenyewe husema “Unstable” ina maana hutokea tafauti kati ya idadi ya protons na neutrons katika nukleasi ambayo hufanya tafauti za uwiano wa umbile hilo.

Baada ya hapo, nukleasi huanza kusambaratika vipande vipande na wakati huo huo kutoa nguvu kubwa sana ili kuleta uwiano. Nukleas, wakati inatoa nguvu hii kubwa, vile vile hutoa vipande hivyo kwa mwendo mkali sana.

Kwa kutazama matokeo ya majabirio hayo, neutrons zimepewa mwendo wa kasi na migongano ya uranium na neutrons katika mazingira maalum yanayoitwa “Reactors”.

Hata hivyo, uranium zimekuwa zikigongwa na neutrons katika viwango maalum na sio tu kwa kubahatisha bahatisha, kwa sababu neutron yoyote inayogonga atomu ya uranium, inapaswa iwe katika wakati na mahala maalum.

Hii ndiyo maana majaribio haya hufanyika baada ya kutazama mahesabu makali ya makisio (probability). Kiasi cha uranium inayotakiwa kutumika, kiasi cha neutrons, muda na mwendo unaotakiwa na neutrons zitakazogonga uranium, lazima ziwe na mahesabu yaliyokamilifu sana.

Baada ya mahesabu yote kukamilika na matayarisho yote kuwepo, nukleasi inagongwa na neutron kwa namna ambayo hupenyeza katika nuklea ya angalau atomu moja na kuzigawanya katika vipande viwili. Katika mgawanyo huu, wastani wa neutron mbili au tatu zitatolewa kutoka kwenye nukleasi kwa mwendo na nguvu kubwa sana.

Neutron zitakazotolewa zitasababisha mitiririko ya mgongano mengine katika nuklei ya urainum zilizobakia. Kila kipande cha nukleasi mpya kitakuwa kama uranium ya awali. Hivyo utakuwa mlolongo unaoendelea wa mlipuko (chain of nuclear reactions).

Kwa mtiririko huu idadi kubwa ya nuklei ya uranium zitagawika vipande na kusababisha nguvu kubwa sana sana kutolewa.

Ni mipasuko hii na nguvu hizi zilizosababisha janga kubwa katika miji ya Hiroshima na Nagasaki, iliyosababisha vifo vya maelfu ya watu.

Mpaka sasa hivi makisio ya vifo vilivyosababishwa na kulipuliwa kwa Atomic Bomb iliyodondoshwa na Marekani katika vita vya dunia vya pili katika miaka ya 1945 huko Hiroshima hukisiwa kuuwa watu wapatao 100,000.

Marekani vile vile ilidondosha Atomic Bomb huko Nagasaki kwa siku tatu baada ya ile ya Hiroshima na kuuwa watu 40,000 pale pale. Wakati huo huo nguvu iliyotolewa iliuwa watu, iliangamiza makazi, na ikasababisha majeruhi ya vizazi kutokana na mionzi iliyoendelea kuwepo kwa miaka mingi iliyofuata hadi leo.

Kama dunia yetu, anga yote na vilivyomo hai na visivyo hai pamoja nasi vimetokana na atomus, sasa nini inayosababisha atomu hizi zisilipuke kama zile za Nagasaki na Hiroshima?

Jibu lake ni kuwa neutrons zinazotakiwa katika mlipuko wa nuklea lazima zitokane na njia ambazo sio asili.

Hii inaonyesha wazi kuwa, Muumba(s.w.), muumbaji wa ulimwengu mzima, ameumba kila kitu kwa makadirio yenye uhakika sana. Kama neutrons zingekuwa katika mwendo mkali zipo nje nje tu basi dunia yetu hii isingekuwa chochote bali dude tu lisilo na maisha yoyote ndani yake.

Mwenyezi Mungu (s.w) ameumba atomu na nguvu kubwa ndani yake ameidhibiti nguvu hii katika njia inayofaa sana kwa maisha ya viumbe.

Fusheni

Nuklia Fu-sheni , ni kinyume cha Fi-sheni yenye maingiliano ambayo nuklei mbili nyepesi huletwa pamoja na kufanya nukleas nzito na nguvu kubwa hutumika na hutolewa. Hata hivyo kukamilisha lengo hili kwa namna inyodhibitiwa ni vigumu sana. Hii ni kwa sababu nuklei huwa na chaji chanya (positive) na husababisha msukumo wa yenyewe kwa wenyewe kwa nguvu kubwa sana zinapojaribu kukaribiana.

Hivyo, nguvu kubwa itakayoweza kuzuia nguvu ya msukumo kati yao lazima itumike kuzileta nukleus hizi mbili pamoja. Nguvu kubwa itokanayo na kasi na nyuzi joto milioni 20 hadi 39 [44].

Hili ni joto kubwa lisilo la kawaida na hakuna malighafi yoyote itakayohimilia joto hili kubwa. Kwa maana hii hakuna namna yoyote hapa duniani Fu-sheni inaweza ikafanyika isipokuwa kwa nguvu ya joto kubwa kama bomu la atomic.

Maingiliano ya fu-sheni hutokea mara nyingi katika jua. Joto na mwanga utokanao na jua ni kwa sababu hydrojeni zinaungana na helium na nguvu inayotokea ni baada ya kupotea kwa maada katika maingiliano haya. Kila sekunde, jua hubadilisha tani milioni 564 ya hydrojeni.

Tani milioni 4 iliyobaki ya maada hubadilishwa na kutolewa kama nguvu (nishati). Tukio hili muhimu la kutengeneza nishati ya jua ni la maana sana kwa sayari zetu na maisha yaliyomo, ambayo imekuwepo kwa mamilioni ya miaka bila ya kupumzika.

Hii inaweza kutufanya tujiulize maswali: Kama kiasi hiki kikubwa cha mamilioni ya maada inapotea kwenye jua kila sekunde, lini sasa jua lote litakuwa limemalizika?

Jua linapoteza tani milioni nne kila dakika. Kama tukifikiria kwamba kuwa jua limekuwa likitoa nishati yake katika miaka bilioni tatu iliyopita, kiasi cha uzito uliopotea katika kipindi hiki ingekuwa tani milioni 400,000 zidisha kwa tani milioni moja. Hii ni sehemu moja ya 5,000 ya uzito wa sasa wa jua.

Hii ni sawa na kupoteza gramu moja ya mchanga kutoka kwenye jabali la kilogramu tano katika muda wa miaka bilioni tatu. Hii inaweka wazikuwa, uzito wa jua ni mkubwa kiasi ambacho itapita muda mrefu sana kabla jua lote halijamalizika.

Binadamu amegundua mchanganyiko uliopo kwenye jua hivi karibuni tu na matukio yanayotokea ndani ya jua katika miaka miachache iliyopita tu.

Hapo awali, hakuna yeyote aliyefahamu matukio kama ya milipuko ya nuklea, fi-sheni au fu-sheni. Hakuna aliyejua jinsi nishati ya jua ilivyokuwa inatokea. Pamoja na kuwa binadamu hakujua yote haya, jua wakati wote imekuwa chanzo cha nishati kwa ajili ya viumbe hapa duniani, kwa mamilioni ya miaka.

Sasa hivi jambo ambalo tuseme ni la kushangaza ni kuwa dunia yetu imewekwa katika umbali sahihi sana kutoka kwenye jua. Jua ambalo ni chanzo cha nishati na ambalo lina ukubwa usio wa kifani, ambayo haipungukiwi wala haiathiriki nishati yake. Inashangaza sana jua hili na nishati yake hii imewekwa katika umbali kutoka kwenye dunia kwa namna ambayo maisha katika dunia inakuwa ya mafaniko makubwa na haiathiriwi na jua. (Mwenyezi Mungu (s.w.) ametukuka).

Ukubwa na uzito wa huu wa jua pamoja na athari za kinuklea zinazotokea katika jua kwa miaka milioni kwa milioni imekuwa katika uwiano madhubuti kabisa na dunia na katika mpangilio usiotoa athari yoyote mbaya. Ili kuelewa maajabu katika maumbile haya ni vizuri kukumbuka kuwa mwanadamu hana uwezo wa kuthibiti hata angalau mitambo yake mwenyewe iliyorahisi kwa ajili ya kutoa nishati ya nuklea.

Hakuna, mwanasayansi wala mwanateknolojia aliyeweza kuzuia ajali iliyotokea kwenye reactor ya Chernobyl huko Ukraine, iliyokuwa sehemu ya Urusi ya zamani hapo 1986.

Inasemekana madhara ya mitambo hii ya nuklea itaendelea kwa miaka 30 hadi 40 ijayo.

Ingawaje wanasayansi wamejitahidi kufunika sehemu hii iliyoathirika kwa kutumia matofali mazito ili kuzuia madhara zaidi yatokanayo na mionzi, iliripotiwa kuwa mionzi bado ilikuwa ikipenyeza matofali hayo. Ukiachilia mbali milipuko ya nuklea hata mionzi tu inayovuja hutoka kwenye mitambo ya nuklea ni hatari sana kwa binadamu. Hata bado wanasayansi hawajapata ufumbuzi wa moja kwa moja kudhibiti hali hii pamoja na matumizi ya risasi (lead) katika kujikinga.

Kwa wakati huu, tunasimama kumuelekea Allah (s.w.) kwa nguvu na uwezo wake na utukufu wake kwa kila kitu ikiwamo chembechembe za atomu katika ulimwengu wetu pamoja na zilizomo ndani yake kama protons, neutrons. Nguvu za Allah (s.w.) na miliki yake juu ya kila kitu alivyoviumba imewekewa wazi katika Qur’an:

Na hushughuliki katika kazi yoyote, wala husomi humo (kitu chochote) katika Qur’an wala hamfanyi kitendo chochote (chengine), isipokuwa sisi tunakuwa mashahidi juu yenu mnaposhughulika nayo. Hakifichikani kwa Mola wako kitu chochote (hata) kilicho sawa na uzito wa mdudu chungu, la katika ardhi wala katika mbingu. Wala (hapana) kidogo kuliko hicho wala kikubwa isipokuwa kimo katika kitabu (cha Mwenyezi Mungu) kielezacho (kila kitu). (Surat Yunus: 61).

Madhara ya Atomic Bomb - Hiroshima na Nagasaki

Bomu la Atomiki lililodondoshwa katika miaka ya mwisho ya vita kuu vya dunia vya pili imethibitishia dunia yote, uwezo na nguvu kubwa ya nishati iliyojificha katika atomu. Bomu zote mbili zilisababisha mamia kwa maelfu ya maisha ya watu kupotea na vile vile kusababisha ulemavu mkubwa kwa waliobakia.

Labda tutazame nguvu kubwa (nishati) iliyopo ndani ya atomu, inayosababisha vifo vya maelfu ya watu kwa sekunde chache, ambayo hutolewa sekunde baada ya sekunde:

Wakati wa mlipuko:

Tuseme bomu la atomiki hulipuka katika urefu wa meta 2,000 kama ilivyokuwa Hiroshima na Nagasaki. Chembe za neutroni zinazoigonga uraniam na ambayo huigawa atomu ya kwanza katika sehemu mbili (vipande vipande) husababisha mitiririko ya milipuko mingine (chain reaction) katika sehemu nyingine iliyobaki. Kwa maneno mengine, neutron inayotolewa wakati kipande cha nuklei moja inapogonga nuklei nyingine na kupasuka kuwa nuklei mpya. Hii ina maana nuklei zinapasuka vipande vipande na kusababisha mitiririko hii (chain reaction) na mlipuko hutokea kwa wakati mfupi sana.

Neutrons zinakwenda kwa mwendo wa kasi sana kiasi kwamba bomu hutoa nguvu (nishati) kubwa sana ya kama bilioni 1000 kilo-calories (viwango vya rika hizi ni kilo-electron volls) katika kipindi cha moja ya milioni ya sekunde. Joto la hewa wakati bomu linalipuka hupada kwa mamilioni ya nyuzi joto na presha (pressure) hupanda kuwa atmosphere milioni moja.

1/1000 ya sekunde baada ya mlipuko

Kipenyo cha kile kilicholipuka huongezeka na mionzi mbalimbali hutolewa. Mionzi hii husababisha mlipuko - cheche za mwanzo. Cheche hizi huweza kusababisha upofu kwa wale wote wanaokuwepo katika umbali wa kilomita kumi kutoka kwenye sehemu ya tukio.

Mwanga unaotoka hapa ni mara mia zaidi ya ule utokao kwenye jua. Muda ambao mwanga huu hutolewa ni mdogo sana kiasi ambacho mtu huweza kukosa hata muda wa kufumba macho.

Presha (pressure) wakati wa mlipuko huleta madhara makubwa ndani ya majumba. Husababisha kubomoka kwa majumba, maghorofa, madaraja na kadhalika. Katika sehemu za karibu na milipuko vumbi kubwa hutolewa.

Sekunde ya pili baada ya mlipuko

Ukubwa wote wa kile kilcholipuka pamoja na hewa inayoizunguka hutengeneza kitu kama tufe lenye moto. Joto linalotokana na tufe lenye moto ambayo sehemu yake ya nje lina joto kubwa kama jua, ina uwezo wa washamoto kila kilichokaribu naye kwenye eneo la kilometa nne hadi tano la mzunguko. Mionzi itokanayo na tufe lenye moto huweza kuwa nguvu ya kila kionacho. Wakati huu wimbi la hofu linatoka kwenye tufe hili kwa kasi kubwa sana.

Sekunde ya sita baada ya mlipuko

Wakati huu, wimbi hilo huanguka duniani na kusababisha madhara. Kiasi cha kilometa moja na nusu cha umbali kutoka sehemu hii, hutokea presha mara mbili zaidi ya ile ya kawaida. Uwezekano wa watu kuishi katika hali hii ni asilimia moja.

Sekunde 13 baada ya mlipuko

Wimbi huishia kwenye ardhi na hufuatiwa na milipuko inayosababishwa na misogezo ya hewa na lile tufe lenye moto. Mlipuko huu humezwa ardhini katika mwendo wa 300 - 400 kilometa kwa saa. Kwa wakati huu, tufe la moto linapowa na ujazo wake unapungua. Kwa sababu ni nyepesi kuliko hewa, hupaa juu. Mpao huu husababisha upepo kwenye dunia kubadilika na huwa upepo mkali kuelekea katikati, ijapokuwa mwanzoni ulikuwa unaelekea nje kutoka kwenye sehemu ya mlipuko.

 
   
    
3 / total 4
You can read Harun Yahya's book Muujiza Katika Chembe Ya Atomu online, share it on social networks such as Facebook and Twitter, download it to your computer, use it in your homework and theses, and publish, copy or reproduce it on your own web sites or blogs without paying any copyright fee, so long as you acknowledge this site as the reference.
About this site | Tengeneza kurasa yako ya nyumbani | Add to favorites | RSS Feed
Mambo yote yanaweza kuynakiliwa, kuchapwa na kusambazwa kwa kurejea katika kurasa hii
(c) All publication rights of the personal photos of Mr. Adnan Oktar that are present in our website and in all other Harun Yahya works belong to Global Publication Ltd. Co. They cannot be used or published without prior consent even if used partially.
© 1994 Harun Yahya.www.harunyahya.com
page_top