Muujiza Katika Chembe Ya Atomu

SHUSHA KITABU

Download (DOC)
Maoni

SURA ZA KITABU

< <
4 / total: 4
|
Muujiza katika chembe ya Atomu - Harun Yahya
Muujiza katika chembe ya Atomu
   

 


Sekunde 30 baada ya mlipuko

Wakati tufe lenye moto linapanda, umbile lake la tufe lnabadilika, na hutokea kama uyoga.

Dakika mbili baada ya mlipuko

Umbile la uyoga kwa namna ya wingu hufikia urefu wa kama mita 12,000. Hii ni sehemu ya chini ya ukanda uitwao Stratosphia katika anga. Upepo uvumao katika umbali huu husababisha umbo la uyoga kutawanyika na wingu la chembechembe itoayo mionzi hutanda angani. Chembe hizi huweza kupanda juu zaidi kabla haijashuka tena na kupeperushwa kwenda katika sehemu zingine za duniya.

Mionzi itolewayo na Atomu

Mionzi huweza kuwa kama mifano ya Gama rays, neutrons, electrons, protons, X -rays zikiwa katika mwendo wa kasi sana tuseme kilomita 200,000 kwa sekunde. Ama zingine zipo kama chembe chembe ziendazo kasi na kwa nguvu kubwa. Mionzi ina uwezo wa kupenya katika miili ya binaadam na inapozidi viwango husababisha madhara kwenye Celli kwenye mwili wa binaadam.

Huweza vilevile kusababisha Cell kupoteza hali yake ya kawaida ambayo husababisha magonjwa au kurithisha Cell zenye maradhi kutoka kizazi kimoja hadi kizazi kingine. Hivyo viumbe hai kuwepo kwenye mionzi hii mikali ni balaa tupu. Chembechembe hizi au mionzi hizi inapokuwa kwenye mwendo mkali huweza kupenyeza maada kama mwili wa binaadam. Hugongana vikali atomu au molekuli inapokuwa inapenya. Ama cell huweza kufa au kama zitapona huweza kuzaliana katika namna isiyo ya kawaida kama fi-sheni.

Katika namna hii huweza kuwa kama chembe chembe za Cancer au kwa lugha ya siku hizi Saratani, baada ya wiki, mwezi au hata mwaka baadaye. Mionzi huwa mikali sana katika eneo la meta 1,000 ukizunguka sehemu iliyotokea mlipuko wa nyuklia.

Wale walionusurika hupoteza takribani cell nyeupe zote katika damu zao,wakati huo huo wanakuwa na majeraha katika ngozi zao na wengi wao hufa kwa sababu ya kupoteza damu nyingi kwa wakati mfupi kuanzia siku chache hadi wiki mbili au tatu.

Madhara ya mionzi baada ya mlipuko hutafautiana. Wale wanaoumizwa na mionzi baada ya mlipuko wa lile tufe jekundu kwenye umbali tafauti kutoka kwenye tukio, tuseme kilomita 13, 16 au 22 hupata kuungua ya aina tafauti tuseme ya tatu, ya pili na ya kwanza kwa mfululizo ule wa umbali. Matatizo ya usagaji chakula, na kutokwa kwa damu zinadhibiti, lakini madhara halisi hutokeza baadaye.

Mfano, kupoteza nywele, muunguo wa ngozi, kupoteza nguvu za kiume, kupoteza uzazi, kuzaa watoto taahira au vilema ni jambo la kawaida. Na katika namna hii vile vile kifo huweza kutokea, katika kipindi kutoka siku kumi hadi miezi mitatu. Miaka mingi baadaye, matatizo ya macho, damu, saratani huweza kutokea. Hatari mojawapo ya mlipuko wa bomu la hydrojeni ( namna nyingine ya bomu la nuklea lenye nguvu kubwa ya kuangamiza kwa fu- sheni ya nuklea ya aina mbali mbali ya isotopu ya hydrojeni inapoifanya Helium nuklei) ni kutoa vumbi yenye mionzi inayoingia kwenye mwili wa binaadamu kwa kuvuta hewa, kula chakula au kubaki kwenye ngozi. Vumbi hili husababisha madhara niliyoongelea hapo awali kutegemea na ukubwa au kiwango kilichomfika mtu. Yote haya yanasababishwa na atomu ambazo wala hatuzioni kwa macho yetu haya. Atomu huweza kusababisha maisha na hivyo hivyo inavyoweza kuangamiza. Tabia hii ya atomu huonesha kuwa jinsi ambavyo nguvu za Mweneyezi Mungu aliyemtukufu sana juu ya vitu alivyoviumba.

MWISHO

Miili yetu ikiwa imefanywa kwa atomu, tunavuta hewa ambazo ni atomu, tunakula atomu kwenye vyakula na vinywaji.Tunavyoviona sio vingine ila ni migongano ya electrons za atomu ( protons) katika macho yetu. Tunazihisi atomus wakati wa kushika. Ukweli ni kuwa kila mtu anachofahamu leo hii kuwa ni Ulimwengu, ikiwemo Dunia yetu, kinatokana na atomu. Hata hivyo, labda watu wengi sasa hivi hawafahamu ni mtandao wa namna gani atomu iliyonayo. Na hata kama wanafahamu hawakuona umuhimu wa kufanya uchunguzi, kwa sababu wamekuwa wakidhani wakati wote kuwa hii inawahusu wanafizikia na wana sayansi peke yao. Binaadam, hata hivyo, huishi katika namna madhubuti aliyoumbiwa maisha yake yote. Huu ni mfumo ambao moja ya trillioni ya atomu kufanya kiti cha kukalia tunapoandika. Imechukua kurasa na makaratasi mengi kuelezea jinsi gani ilivyo na nguvu kubwa iliyopo katikika atomu. Jinsi teknolojia inavyokwenda na ufahamu wetu kuhusu ulimwengu unavyoongezeka, idadi ya karatasi vile vile zitaongezeka.

Je, sasa mpangilio huu umetokezeaje? Haiwezekani kuwa chembe chembe hizi zimezagaa zagaa kwa kubahatisha tu baada ya mlipuko mkubwa wa Big Bang na kufanya atomu na vile vile mazingira mwanana kwa maisha ya binaadam na viumbe. Ni wazi kuwa haiwezekani kuelezea mfumo huu kwa kubahatisha.Vyote tunavyoona vinatuzunguka na vile ambavyo hatuvioni kama hewa vimetokana na atomu ambayo mifumo ya ajabu ya njia zake imetokana na atomus hizi. Sasa tuseme traffic police gani aliyepo kuongoza mienendo ya atomu kama ilivyo kwenye magari?

Je, inaweza ikawa wewe unadhani kuwa mwili wako unatokana na atomu pekee, sasa ni ipi kati ya atomu hizo inayoongoza nyingine, na ipi inaongoza kipi? Je atomu za ubongo wako ambazo sio tafauti na atomu zingine, zinadhibiti nyingime? Tukisema kuwa atomu za ubongo ndio zinazoongoza basi tunapata majibu ya maswali yetu. Kama atomu zote za ubongo zinaongoza, je zinapataje uwezo wa kutoa maamuzi?

Je ni jinsi gani matrilioni ya atomu ya ubongo yanavyoshirikiana? Inakuwaje atomu moja kati ya zote zingine inapinga uamuzi uliotolewa? Ni jinsi gani atomu zinawasiliana? Kwa kuzingatia maswali ya hapa juu ni wazi kuwa, sio busara kusema kuwa matrillioni ya atomu katika ubongo yanajiongoza. Je ni sawa kudhani kuwa ni moja tu kati ya matrilioni ya atomu inaongoza zingine zinafuata? Tukiamini hivyo basi maswali ya kujiuliza yanatujia:

Ipi kati ya atomu ndio kiongozi na nani anayezichagua?

Ni wapi katika ubongo ilipo atomu hii?

Ni tafauti gani kati ya atomu hii na nyinginezo?

Kwa nini atomu zingine ziitii atomu hiyo bila ya masharti?

Kabla hatujajibu maswali haya , tutaje jambo moja lingine: Ile atomu inayotakiwa kuongoza nayo inatokana na chembe chembe zingine. Sasa kwa nini na kwa namna gani chembe hizi ziifanye atomu hiyo kiongozi? Nani anayedhibiti chembe hizi? Kama kuna kiongozi mwingine itakuwa sawa vipi kusema kuwa atomu hii ndiyo inayoongoza?

Wakati huu dai kuwa moja ya atomu katika ubongo wetu inakuwa kiongozi sio la kweli. Je idadi kubwa ya atomu katika ulimwengu huu zitakuwaje wakati watu, wanyama, mimea, dunia, hewa, maji, sayari, na vingine vyote vinatokana na atomu?

Ipi kati ya atomu zote hizi zitakazoongoza wakati nazo zimetokana na chembe chembe zingine? Kutoa madai kwamba yote haya yanatokana kwa kubahatisha na kukanusha kuwepo kwa Allah ( s.w) aliyeviumba ulimwengu wote ni sawa na inavyosema Qur-an:

“Na wakazikanusha na hali ya kuwa nafsi zao zina yakini nazo; ( kuwa ni kweli hayo alokuja nayo Nabii Musa.Lakini walizikanusha tu), kwa dhulma na kujivuna. Basi angalia ulikuwaje mwisho wa wafanyao ufisadi.” (Suratil - :14)

Hebu tafakari; mwanaadamu, ambaye ametengenezwa na mpangilio wa atomu kwa namna mbalimbali amezaliwa, amelishwa atomu, na amekulia atomu. Anasoma baadaye vitabu vitokanavyo na atomu katika nyumba zilizojengwa na atomu. Baadaye anapata stashahada au shahada ambayo hutokana na atomu zikisema kuwa wewe ni “nuclear Engineer” au “Mhandisi wa nyuklia” katika cheti chake. Baadaye huweza kutoa mihadhara ya kuhusu atomu. Zinazotokana na kuwepo kwa kubahatisha. Ukisema hivyo hutokuwa tafauti na yule aliyemuelezea nabii Ibraahim (a.s) kama Allah (s.w) anavyoeleza kwenye Qur-an:”

Hukumsikia yule aliyehojiana na Ibrahim juu ya Mola wake kwa sababu Mwenyezi Mungu alimpa ufalme? Ibrahim aliposema : "Mola wangu ni yule ambaye huhuisha na kufisha ,” yeye akasema : "Mimi pia nahuisha na kufisha. ”Ibrahim akasema "Mwenyezi Mungu hulichomozesha jua mashariki, basi wewe lichomozeshe magharibi “ akafedheheka yule aliye kufuru na Mwenyeezi Mungu hawaongozi watu madhwalim “. (Suratil Baqara:285)

“Wakasema Malaika:”Utakatifu ni wako! Hatuna elimu ispokuwa ile uliyotufundisha ; bila shaka wewe ndiye mwenye hikma .” (Suratul Baqara:32).

“Basi sifa zote njema ni za Mwenyeezi Mungu, Muumba mbingu na Muumba wa ardhi ,Muumba wa ulimwengu wote. Na ukubwa ni wake mbinguni na ardhini ,Naye ni Mwenye nguvu, Mwenye hikma.” (Suratil - Jaathiya : 6-37)

                               

 
   
    
4 / total 4
|
You can read Harun Yahya's book Muujiza Katika Chembe Ya Atomu online, share it on social networks such as Facebook and Twitter, download it to your computer, use it in your homework and theses, and publish, copy or reproduce it on your own web sites or blogs without paying any copyright fee, so long as you acknowledge this site as the reference.
About this site | Tengeneza kurasa yako ya nyumbani | Add to favorites | RSS Feed
Mambo yote yanaweza kuynakiliwa, kuchapwa na kusambazwa kwa kurejea katika kurasa hii
(c) All publication rights of the personal photos of Mr. Adnan Oktar that are present in our website and in all other Harun Yahya works belong to Global Publication Ltd. Co. They cannot be used or published without prior consent even if used partially.
© 1994 Harun Yahya.www.harunyahya.com
page_top