Dalili Za Kiyama

SHUSHA KITABU

Download (DOC)
Maoni

SURA ZA KITABU

< <
3 / total: 5
Dalili za Kiyama - Harun Yahya
Dalili za Kiyama
   

 


Vita na machafuko

Katika Hadithi moja Mtume (s.a.w) alizielezea zama za mwisho hivi: Mtume wa Allaha alisema: Harji (itazidi kuongezeka), Watu wakauliza harji ndio nini? Akajibu, ni mauaji, ni mauaji. (Bukhari).

Maana ya harji iliyotajwa katika hadithi ya hapo juu ya Mtume (s.a.w) ni “machafuko makubwa” na “vurugu” ambavyo havitaishia mahala pamoja bali vitaenea duniani kote.

Pia kuhusiana na swala hili maneno mengine ya Mtume yanasema: Ile saa itafika wakati vurugu, umwagaji damu na machafuko yatakapokuwa mambo ya kawaida. (Al-Muttaqi Al-Hindi, Muntakhab Kanzul Ummaal)

Ulimwengu hautakoma mpaka zije enzi ambapo kutakuwa na mauaji makubwa na umwagaji mkubwa wa damu (Muslim).

Tukizitafakari Hadithi hizo, tunafikishwa katika hitimisho muhimu. Mtume (s.a.w) alielezea mitafaruku, fujo, mauaji na vita vitavyoikumba dunia nzima na kuenea kwa hali ya khofu na akabainisha kuwa matukio haya ni ishara ya Kiama. Tukiangalia katika karne 14 zilizopita, twaona kuwa vita vilikuwa vya Kinchi kabla ya karne 20. Hata hivyo vita ambavyo vimemuathiri kila mtu duniani, vilivyoathiri mifumo ya siasa, na mifumo ya uchumi na jamii, vimerindima zaidi katika nyakati za karibuni hususan katika vita kuu mbili za dunia.

Katika vita kuu ya kwanza ya dunia zaidi ya watu Milioni 20 walikufa, na katika vita kuu ya pili ya dunia, zaidi ya watu Milioni 50 waliuawa. Vita kuu ya pili ya dunia ndiyo inayotambuliwa kuwa ni vita iliyomwaga damu nyingi mno, iliyokuwa kubwa mno na iliyoleta maangamizi makubwa katika historia.

Teknolojia ya sasa ya Kijeshi ikiwa ni pamoja na Silaha za Kibaolojia, Kikemia na Nyuklia ndio iliyozidisha madhara ya vita katika kiwango ambacho hakijapata kutokea katika historia. Kutokana na silaha za maangamizi ambazo zimezidi kuboreshwa, inakubaliwa na wengi kuwa Ulimwengu hautaingia katika vita ya tatu ya dunia.

Migogoro ambayo imetokea baada ya vita kuu ya pili ya dunia, vita baridi, vita vya Korea, vita ya Vietnam, mgogoro wa Warabu na Waisrael vita vya Ghuba na Iraq ni miongoni mwa matukio mabaya sana ya wakati wetu. Hali kadhalika vita vya kieneo, migogoro na vita vya wenyewe kwa wenyewe vimesababisha maangamizi makubwa katika sehemu nyingi za dunia. Katika nchi kama Bosnia, Palestina, Chechnya, Iraq, Afghanistan, Kashmiri na sehemu nyingine nyingi, matatizo haya bado yanaendelea kumkumba mwanadamu.

Mfano mwingine wa machafuko yanayomuathiri mwanadamu mithili ya vita ni Ugaidi unaoratibiwa kimataifa kama wanavyokubali viongozi wengi kuwa vitendo hivi vya Ugaidi vimeongezeka mno katika nusu ya pili ya karne ya 20. Kwa kweli yawezekana kusema kuwa Ugaidi ni jambo makhususi la karne ya 20. Jamii zilizobobea katika ubaguzi, Ukomunist na Itikadi nyingine kama hizo au zenye malengo ya Utaifa zimeshiriki katika vitendo vya kinyama kwa msaada wa teknolojia ya leo. Katika historia ya karibuni tu, vitendo vya Ugaidi mara kwa mara vimeleta maangamizi. Damu nyingi imemwagika na watu wasio na hatia ama wamejeruhiwa au wameuawa lakini bado wanadamu hawajapata fundisho kutokana na matukio haya ya balaa. Katika nchi nyingi za dunia Ugaidi unaendelea kuwa msingi wa tawala na sera.

Kuna aya nyingi katika Qur’an zinazohusiana na jambo hili. Katika Surati Arum inaelezwa kuwa machafuko yameikumba dunia kwasababu ya yale ambayo watu wameyafanya kwa mikono yao:

Uharibifu umedhihiri barani na baharini kwasababu ya yale iliyoyafanya mikono ya watu ili awaonjeshe adhabu ya baadhi ya mambo waliyoyafanya, huenda wakarudi (wakatubia kwa Mwenyezi Mungu) (30:41).

Hatuna budi kusema kuwa aya hii inatukumbusha ukweli muhimu sana. Machungu na Masahibu yanayotokana na makosa ya wanadamu yanatupa fursa ya kutanabahi na kuepuka kuyarudia.

Kuangamia kwa Miji mikuu: Vita na majanga

Miongoni mwa mambo aliyoyasema Mtume kuhusana na zama za mwisho ni hili:

Miji mikuu itaangamia na itakuwa kana kwamba haikupata kuwepo hapo kabla (Al-Muttaq Al-Hindi Al Burhan fi Alamat Al Mahadi Akhir al Zaman)

Kuangamia kwa miji mikuu iliyozungumzwa katika hadithi hii kunatukumbusha maangamizi ambayo yanatokea hivi leo kutokana na vita na majanga mbali mbali ya asili. Silaha za kisasa za Nyuklia, Madege ya Kivita, Mabomu, Makombora na Zana nyingine za kisasa zimesababisha maangamizi yasiyosemeka.

Zana hizi za hatari zimeleta kiwango kikubwa cha maangamizi ambacho dunia haijapa kukiona hapo kabla. Kwahakika miji mikuu ndio imekuwa malengo makuu ya mashambulizi na imekuwa ikiathirika zaidi kutokana na maangamizi haya. Maangamizi yasiyo na mfano ya vita ya pili ya dunia ni kielezeo cha haya. Kwa kutumika bomu la Atomic katika vita kuu ya dunia, miji ya Hiroshima na Nagasaka iliangamizwa kabisa.

Kutokana na Mabomu mazito, miji mikuu ya Ulaya na miji mingine mikubwa imepata kiwango kikubwa cha hasara. Buku la marejeleo (Encylopedia Britannica) linaelezea hasara iliyosababishwa na vita kuu ya pili ya dunia katika miji ya Ulaya:

Maangamizi yaliyotokea yameigeuza sehemu kubwa ya Ulaya kuwa kama taka taka na ilimalizwa na mabomu ya moto, bara bara zilijaa mashimo matupu, sura ya nchi ilikuwa giza tupu njia za reli zikaharibiwa na kutofanya kazi, madaraja yalibomolewa na bandari zilijaa Meli. Berin, anasema Jenerali Lusias D. Clay, Naibu Gavana wa Jeshi katika ukanda wa Post war German, lilikuwa kama jiji la wafu.

Kwa kifupi maangamizi ambayo yalisababishwa na vita ya pili ya dunia yanashabihiana kabisa na hadithi ya Mtume (s.a.w) .

Sababu nyingine ya maangamizi ya miji mikuu ni majanga ya asili. Ni ukweli wa kitakwimu kuwa zama tunazoishi hivi leo zimeshuhudia kuongezeka kwa idadi na madhara ya majanga ya asili. Katika miaka kumi iliyopita, majanga ya asili yaliyosababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa yalikuwa ni mambo ambayo hayakuwahi kutokea.

Maangamizi, Umasikini, mauaji, machafu kuongezeka

Sababu nyingine ya maangamizi katika miji ni majanga ya asili. Kulingana na takwimu, zama zetu zimeshuhudia ongezeko la idadi na ukubwa wa majanga ya asili. Katika kipindi cha miaka kumi iliyopita kulikuwa na majanga yaliyosababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa. Haya yalikuwa ni majanga ya aina yake.

Hatari kubwa ya uchafuzi wa hali ya hewa unaosababishwa na viwanda ni tishio kwa dunia nzima. Viwanda vinavuruga urari wa angahewa ya dunia na kuongeza mabadiliko ya hali ya hewa. Mwaka 1998 ulikuwa ni mwaka wa joto kali sana duniani tangu rekodi za hali ya hewa zianze kuwekwa. Kwa mujibu wa maelezo ya kituo cha taarifa za hali ya hewa cha Marekani, idadi kubwa ya majanga yaliyotokana na hali ya hewa ilikuwa mwaka huo wa 1998.

Kwa mfano, Kimbunga kimeelezewa na wachunguzi wengi kuwa ndio janga baya mno la kimaumbile lililoikumba Amerika ya kati. Katika miaka michahe iliyopita vimbunga, dhoruba, tufani na majanga mengine yameleta maangamizi katika bara la Amerika na katika sehemu nyingine kadha wa kadha za dunia. Mbali na hayo mafuriko nayo yameleta maangamizi katika maeneo kadhaa ya watu.

Aidha mitetemeko ya ardhi, Volkeno nayo pia yamesababisha maangamizi makubwa. Hivyo basi maangamizi yote haya yaliyotokea katika miji ni ishara muhimu.

 
   
    
3 / total 5
You can read Harun Yahya's book Dalili Za Kiyama online, share it on social networks such as Facebook and Twitter, download it to your computer, use it in your homework and theses, and publish, copy or reproduce it on your own web sites or blogs without paying any copyright fee, so long as you acknowledge this site as the reference.
About this site | Tengeneza kurasa yako ya nyumbani | Add to favorites | RSS Feed
Mambo yote yanaweza kuynakiliwa, kuchapwa na kusambazwa kwa kurejea katika kurasa hii
(c) All publication rights of the personal photos of Mr. Adnan Oktar that are present in our website and in all other Harun Yahya works belong to Global Publication Ltd. Co. They cannot be used or published without prior consent even if used partially.
© 1994 Harun Yahya.www.harunyahya.com
page_top