Dalili Za Kiyama

SHUSHA KITABU

Download (DOC)
Maoni

SURA ZA KITABU

< <
5 / total: 5
|
Dalili za Kiyama - Harun Yahya
Dalili za Kiyama
   

 


Elimu

Tofauti kubwa inayobainika kati ya krne za 20 na 21 na zama zilizopita ni kuongezeka kwa mwamko wa elimu. Huko nyuma uwezo wa kusoma na kuandika ulihodhiwa na watu wachache. Lakini kuanzia mwishoni mwa karne ya ishirini UNESCO na taasisi za serikali pamoja na mashirika binafsi yamefanya kazi kubwa ya kusambaza elimu.

Kwa mujibu wa ripoti ya UNESCO, kiwango cha elimu ya kujua kusoma na kuandika kilifikia asilimia 77.4 mwaka 1997. Kiwango hiki ni kikubwa mno. Mtume(s.a.w) aliielezea hali hii kama ni dalili mojawapo ya zama za mwisho;

“Mwamko wa elimu(literacy) utaongezeka pale hukumu inapokaribia”(Ahmad Diyaal-Din-Alkhamush Khanawi, Ramuz-al-Ahadith).

Teknolojia ya ujenzi

Dalili nyingine ambayo Mtume(s.a.w) ameitaja kuhusiana na zama za mwisho ni ujenzi wa maghorofa marefu:

“Hakutakuwa na hukumu hadi pale maghorofa marefu sana yatakayojengwa”(imesimuliwa na Abu Huraira)

“Kiama hakitasimama mpaka watu washindane kujenga maghorofa marefu.(Bukhari)

Tukiingalia historia ya usanifu majengo na uhandisi, tunaona kuwa maghorofa mengi marefu yalianza kujengwa na mwishoni mwa karne ya kumi na tisa.

Maendeleo ya Teknolojia kuongezeka kwa matumizi ya chuma cha pua na matumizi ya Kambarau(lifti za kupandia maghorofani) kumeongezeka kasi ya ujenzi wa maghorofa.

Maghorofa marefu yameshamiri kweli kweli hivi leo. Alichokisema Mtume(s.a.w) katika Hadithi kinadhihirika wazi wazi. Watu na mataifa yanashindana kuongeza maroshani ya ghorofa.

Teknolojia ya usafiri

Katika historia yote, kumekuwa na uhusiano kati ya maendeleo na mawasiliano. Jamii ambazo zimeweza kujiwekea miundo mbinu bora ikiwa ni pamoja na mifumo bora ya usafiri zimejipatia maendeleo.

Akizungumzia dalili za zama za mwisho, Mtume(s.a.w) kayataja maendeleo ya usafiri.

“Kiama hakitasimama… hadi muda utakapopita upesi upesi(Bukhari)

Masafa ya mbali mno yatafikiwa kwa muda mfupi.(Ahmad Musnad)

Ujumbe unaobebwa na Hadithi hiyo unadhihirika wazi wazi hivi leo. Katika zama hizi masafa ya mbali yanafikiwa kwa muda mfupi tu. Madege, magari na Treni ni vyombo vinavyoweza kusafiri masafa ya mbali kwa muda mfupi.

Huko nyuma safari za masafa marefu zilichukua miezi. Qur’an pia inavielezea vyombo hivi:

“Na amewaumbia Farasi na nyumbu na punda ili muwapande na (wawe) mapambo. Na ataumba vipano) msivyovijua(6:8).

Hebu tuutafakari huu usemi wa muda utapita upesi upesi katika ile hadithi ya kwanza. Kwa kuzingatia yale tuliyoyaeleza, ni wazi kama Mtume(s.a.w) alivyonena kuwa katika zama za mwisho, kazi zitafanywa kwa muda mfupi kuliko zilivyokuwa zikifanywa huko nyuma.

Kwa kweli maendeleo ya sayansi yamewezesha mambo mengi kutimizwa kwa muda mfupi zaidi. Hadithi hiyo hiyo inathibitisha jambo hili:

Kiama hakitakuja kabla muda kupungua. Mwaka uwe kama mwezi, mwezi uwe kama wiki na wiki iwe kama siku…(Tirmidh).

Mathalani zama zilizopita, mawasiliano ya kimataifa yalichukua majuma mengi lakini sasa yanafanyika kwa sekunde tu kwa tovuti na teknolojia nyinginezo za mawasiliano. Kurahisishwa kwa mawasiliano kumewezesha chombo cha anga cha Marekani kutumwa katika sayari Mars zaidi ya maili milioni 106 ambacho hivi kinaendelea kuleta taarifa mbali mbali za kiuchunguzi duniani pamoja na picha kwa muda mfupi sana.

Katika zama za nyuma bidhaa zilifika kule zilikopelekwa baada ya safari ndefu za miezi, hivi leo zinafika mapema kabisa. Hivi sasa mamilioni ya vitabu yanaweza kuchapwa kwa muda uliotumika kuchapwa kitabu kimoja karne chache zilizopita.

Katika masuala ya afya na njia za utayarishaji wa vyakula hapahitajiki tena muda mrefu wa kushughulikia kutokana na Teknolojia ya sasa.

Unaweza kutoa mifano mingi mno. Hata hivyo tumalizie hapa kwa kusema kuwa dalili zote alizozieleza Mtume(s.a.w) katika karne ya saba zinaonekana wazi wazi hivi sasa.

Dalili nyingine aliyoitaja Mtume(s.a.w) ni kuongezeka kwa biashara, kama iliyoripotiwa na Ibn Mas’uud(r.a). Biashara inakwenda pamoja na maendeleo ya Teknolojia na usafirishaji wa kisasa umeiwezesha kila nchi duniani kujenga uhusiano na ushirikiano wa karibu wa kibishara na nchi nyingine.

Teknolojia ya mawasiliano

Baadhi ya Hadithi za Mtume(s.a.w) zimeelezea Teknolojia ya leo ya mawasiliano;

“Saa ya mwisho haitafika kabla jumbe hajasemeshwa na fimbo yake.(Tirmidh)

Tukiiangalia hadithi kwa makini, twaweza kuona ukweli uliomo ndani yake. Katika zama zilizopita fimbo ilitumika kuendeshea wanyama wa kupanda hasa hasa ngamia na farasi. Hapa tunaona Mtume(s.a.w). Hapa tunaona Mtume(s.a.w) ametumia tamathali.

Hebu tujiulize ni kitu gani kinachosema ambacho twaweza kukilinganisha na fimbo kwa sifa za maumbile? Jibu la kwamza laweza kuwa simu. Au vyombo vingine vya mawasiliano. Vyombo vya mawasiliano visivyotumia waya kama vile simu za mkononi na simu za upepo kama sattilaiti ni vyombo vya hivi karibuni kabisa. Kwa kuvitazama vyombo tutaona wazi wazi kule kutimia kwa bishara ya Mtume(s.a.w) iliyotolewa miaka 1400 iliyopita. Kwa hivyo huu ni ushahidi kuwa zama zetu ziko jirani na siku ya hukumu. Katika Hadithi nyingine Mtume(s.a.w) anaelezea maendeleo ya Teknolojia ya mawasiliano:

“Hakutakuwa na hukumu mpaka sauti ya mtu imsemeshe yeye mwenyewe(Hadi mtu asemeshwe na sauti yake.(Mukhtasar Tazkira; Allama Qurtubi).

Ujumbe wa Hadithi hii unathibitika hivi leo.Ili mtu aisikiye sauti yake kwanza hurekodiwa na kisha kusikilizishwa. Teknolojia ya kunasa na kutoa sauti ni ya karne ya ishirini.

Huu ndio ulikuwa mwanzo wa maendeleo ya sayansi ambayo ndio imezaa vyombo vya mawasiliano na habari. Unasaji wa sauti sasa umefikia kiwango cha juu kutokana na matumizi ya kompyuta.

Kwa kifupi vyombo vya elektroniki vya hivi leo kuna vipaza sauti ambavyo vimewezesha mtu kujinasa na kujisikia sauti yake mbali ya kanda za rekodi na vionesho vya picha(video). Hii inadhihirisha kuwa Hadithi ya Mtume iliyonukuliwa hapo imetimia. Kwa hiyo hii ni dalili nyingine ya kiama.

Si hadithi hizo tu bali kuna ishara nyingine zilizotajwa na Hadithi zifuatazo:

Mkono utanyooshwa kutoka angani na watu watautazama na kuuona.(Ibn Hajar Haythami, AlQawl al Mukhtasar fil alamat al Mahdi al Muntanzir.

Dalili ya siku hiyo mkono kunyooshwa angani na watu kuacha kuangalia.(Al-Muttaqil al Hindi, AlBurhan fi Ahmad al-Mahdi Akhir al-Zaman)

Ni dhahiri kuwa neno “mkono” katika hadithi hiyo limetumika kwa tamathali. Katika zama zilizopita neno hili huenda halikueleweka zaidi. Lakini ikitazamwa teknolojia ya leo, kauli yaweza kutafsiriwa kwa namna nyingi.

Kwa mfano Televisheni ambayo imekuwa sehemu muhimu ya maisha ya leo pamoja na kamera na Kompyuta zaweza kubeba tafsiri ya kauli hiyo.

Neno “mkono” yawezekana limetumika likiwa na maana ya uwezo. Yaweza kuwa na maana pia taswira zinazotoka angani kwa sura ya mawimbi ambayo ni televisheni:

“Sauti itamwita mtu kwa jina lake na hata watu wa magharibi na mashariki watasikia.(Ibn Hajar Haythami, Al Qawl al Mukhtasar fi alamat ala Mahdi al Muntazar).

Sauti hii itavuma itaenea duniani kote na kila kabila litaisikia kwa lugha yao wenyewe(Al-Muttaq al Hindi, al Burhani fi alamat al Mahd Akhir al Zaman).

Sauti kutoka mbinguni ambayo kila mtu ataisikia kwa lugha yake. (Al-Muttaq al Hindi, al Burhani fi alamat al Mahd Akhir al Zaman).

Hadithi hapa zinataja sauti ambayo itasikika dunia nzima na kwa lugha ya kila mtu. Ni dhahiri hii ina maana ya Radio, Televisheni, simu za mikononi na nyenzo nyingine za mawasiliano. Huu ni muujiza kwamba Mtume(s.a.w) alitaja maendeleo ambayo hayakufikirika katika kipindi cha miaka mia moja tu iliyopita.

Mfasiri maarufu Badiuzzaman wakati akifasiri hadithi hizi alieleza kuwa, zimebashiri kimiujiza kuja kwa radio, televisheni na vyombo vingine vya aina hiyo.

Kuzuka kwa manabii wa uongo

Inafahamika kuwa katika kipindi chote cha historia, kumekuwa na manabii wengi wa uongo. Katika hadithi inabainishwa kuwa Manabii wa uongo watazuka kabla ya siku ya hukumu.

Saa ya mwisho haitafika kabla ya kuja kwa Madajali(Wadanganyifu) thelathini kila mmoja akijitambulisha kama nabii wa Allah.(Abu Dawood)

Kwa kutumia fursa ya matazamio ya Waislamu na itikadi ya dini ya kikristo kuwa Nabii Isa au Yesu atarejea, idadi kubwa ya watu wadanganyifu wamejitokeza kudai unabii.

Kumbukumbu zinaonesha kuwa , Manabii wa uongo walianza kujitokeza katika miaka ya 70. Ifuatayo ni baadhi ya mikasa iliyotokana na madai ya unabii yaliyojitolewa na watu mbali mblia katika nchi mbali mbali.

Maafa ya moto; David Koresh na wafuasi wake wapatao 74 katika eneo la Waco, Texas walikufa kwa kujiwasha moto.

Wiki moja kabla ya hapo maeneo mawili ya Uswisi na moja nchni Canada, walikufa jumla ya Wafuasi 53 wa Jouret, wakiwemo na watoto wao. Polisi katika nchi hizo mbili wanafanya uchunguzi kujua kama vifo hivyo ni vya kujiua, kuuawa au yote mawili kutokana na imani za ajabu.

Sun Myung Moon, mwasisi wa Kanisa la Unification anadai yeye ni Masihi aliyekuja kwa mara ya pili. Kanisa la Unification lilianzishwa rasmi na Moon mnamo mwaka 1954. Moon anadai kuwa mwaka 1936 yeye alipokuwa na umri wa miaka 16, Yesu alimtokea upande wa mlimani kaskazini magharibi mwa Korea na kumwambia kuwa Mungu amemchagua kwa kazi ya utume wa kusimamisha Ufalme wa mbinguni na ardhini.

Zaidi ya watu 1000 wahofiwa kufa baada ya kugundulika kwa makaburi mengi zaidi nchini Uganda. Hao walikuwa wafuasi wa mtu aliyedai kuwa nabii Kibwetere. Zaidi ya watu 900, wafuasi wa dhehebu moja, walikutwa wamekufa pamoja katika msitu wa Amerika kusini. Watu wote waliokufa walikuwa wafuasi wa Mchungaji Jim Jones, kiongozi wa hekalu mjini San Francisco.

Qur’an pia inaeleza kuja kwa mnabii wa uongo;

Na ni nani dhalimu mkubwa kuliko yule amtungiyae uongo Mwenyezi Mungu au mwenye kusema: Nimeletewa Wahyi”, na hali hakufunuliwa chochote; na yule asemaye: Nimeteremsha(ufunuo) kama ule aliouteremsha Mwenyezi Mungu. Na kama ungewaona madhalimu watakapokuwa katika mahangaiko ya mauti na malaika wamewanyooshea mikono(kuwaambia) zitoeni roho zenu! Leo mtalipwa adhabu ifedheheshayo kwa sababu ya yale mliyokuwa mkizifanyia kiburi Aya zake(ungeona namna gain wanavyopapatika)(6:93).

Kama inavyoelezwa katika aya hiyo watu hawa wazushi kwa hakika watapata malipo yao kwa uongo waliozusha. Hapana shaka kuwa utafika wakati ambapo uongo wote wa manabii wa uongo utafutiliwa mbali. Mtume(s.a.w) akasema kuwa baada ya warongo hawa kuondoka ndipo Isa(s.a) atakapokuja tena.

Kama tulivyoeleza kurasa za nyuma kuwa Qur’an inatufahamisha kurejea kwake duniani, na kwamba Waislamu na Wakristo, kwa hamu, wanasubiri ujio wake, kuna Hadithi chache za Mtume(s.a.w).

Mwanazuoni wa kiislamu Shawkani kasema kuwa kuna Hadithi 29 zinazoelezea kurejea kwa Issa na kwamba maelezo yaliyomo katika hadithi hizi hayawezi kupotoshwa.(Ibn Majah)

Kuna jambo moja muhimu linalotujia kutokana na Haithi hizi. Kurejea kwa Isa kutatokea awamu ya pili ya zama za mwisho na ndio itakuwa ishara muhimu(dalili kuu) ya siku ya hukumu. Hadithi zinazohusiana na jambo hili ni hizi;

Saa ya mwisho haitafika mpaka muone mshuko wa Issa(a.s) mwana wa Mariamu(Muslim).

Naapa kwa yule ambaye roho yangu iko mikononi mwake. Mwana wa Maryamu, muda si mrefu atashuka miongoni mwenu(Waislamu) kama mtawala mwadilifu wa haki(Bukheri).

Saa haitasimama hadi pale atakaposhuka mwana wa Maryamu miongoni mwenu kama mtawala mwadilifu(Bukhari)

Mtume(s.a.w) anatueleza kile atakachofanya Isa pale atakaporejea; unapowadia wakati wa kifo chake Isa atakuwa ameonekana tena duniani kwa kipindi cha miaka 40.(Abu Dawuud).

Isa(a.s) mwana wa Maryamu atashuka kutawala kwa miaka arobaini kwa kitabu cha Allah na kwa Sunna yangu hadi anapokufa.

(Al-Muttaqi al Hindi, Al Burhani fi Alamat al Mahdi Akhir al zaman)

Zama bora

Sifa za zama bora zilizoelezewa kwa kina na Mtume(s.a.w) ni dalili muhimu ya siku ya hukumu. Kipindi hicho kinachoitwa “Golden age” kitakuwa bora kwa sababu ya kule kulinganishwa kwake na pepo kwa maelezo ya Mwanachuoni wa kiislamu.

Imeelezwa katika Hadithi kuwa zama hizo bora zitakuwa katika awamu ya pili ya zama za mwisho. Sifa moja kuu ya kipindi hiki cha furaha itakuwa ni ule utajiri wake mkubwa wa mali.

Hadithi zinasema kuwa utajiri huo hautakuwa na mfanowe katika historia:

Umma wangu utapata hali bora katika zama hiyo ambayo mfano wake haujapata kuonekana hapo kabla(ibn Majah).

Umma wangu wa wema na wabaya utaneemeshwa neema ambazo haukupata kuziona kabla(Al-Muttaq al Hind Al Burhan fi Alamat al Mahd Akhira Zaman).

Hadithi nyingine inaelezea utajiri wa zama hizo.

Katika kipindi hicho, ardhi itatupa nje hazina yake.(Ibn Hajar Haythami, AlQawli al Mukhtasar fii alamat al Mahdi al Muntazar)

Hadithi nyingine zinaelezea kuwa miaka ya mashaka na huzuni itakwisha. Hakuna mtu atakayekuwa katika shida. Hakuna mtu atakayetakiwa kutoa zaka.

“Toeni zaka kwani utakuja wakati ambapo mtu atakwenda na zaka yake huku na kule asipate mtu wa kuipokea(Bukhari).

Kwa hakika bidhaa zitakuwa nyingi na zitamwagika kama maji lakini hakuna atakayeziokota(Al Halimi).

Sifa nyingine ya zama bora itakuwa ni kushitadi kwa haki na ukweli. Utakuwa wakati ambapo sheria na haki zitachukua nafasi ya hofu, mfarakano na dhuluma.

Kama tunavyosema katika Hadithi, dunia itajaa haki badala ya ukandamizaji na mateso(Ahmad Diya’al Din al Kamushkanawi, Ramuz al Ahadithi)

Miongoni mwa sifa bora za kipindi hicho ni kunyamaa kwa silaha(kutulia kwa milio ya silaha), kutoweka kwa uadui, migogoro na kukoma kwa misambaratiko ya kijamii. Badala yake kutashamiri urafiki na mapenzi miongoni mwa watu.

Kiasi kikubwa cha pesa kilichotumika kugharimia vita na viwanda vya silaha sasa kitawekezwa kwenye chakula, afya, maendeleo, utamaduni na mambo yatakayoleta furaha kwa watu wote.

Sifa nyingine ya kipindi hiki cha neema itakuwa ni kurejea katika misingi ya dini ya Mwenyezi Mungu kama ilivyofundishwa na Mtume(s.a.w). Zile sheria na mila zilizobuniwa baada ya Uislamu zitaondoshwa. Tafauti za Waislamu katika kuitekeleza dini yao zitakoma.

Kwa kifupi, zama bora ni kipindi cha neema nyingi, maisha bora, amani furaha, utajiri na faraja. Utakuwa ni wakati ambao maendeleo katika sanaa, tiba, mawasiliano, uzalishaji, usafirishaji na katika maeneo mengine ya maisha yatakuwa katika sura ambayo haikuwahi kuonekana katika historia ya dunia. Na watu wataishi kwa kuzingatia mafundisho ya Qur’an.

Baada ya zama bora

Tunaposoma habari za Mitume katika Qur’an tunaona kuwa kanuni ya Mwenyezi Mungu imefanyakazi katika zama zote. Jamii zinazomkadhibisha Mtume wa Mwenyezi Mungu na kumpiga vita basi huishia kuangamizwa.

Lakini wale wanaomtii Mtume hupata neema nyingi za kidunia na Ustawi wa Kiroho ambao dini sahihi huwaletea. Lakini baada ya kupita mitume hawa, baadhi ya Watu huanza kukengeuka na kuikanusha dini sahihi kuanza kuishirikisha na Mwenyezi Mungu.

Mifarakano na migongano hutokea. Kwa kweli watu wa jamii hizi wamejikuta wakiangamia kwa mikono yao wenyewe. Kanuni, hapana shaka, itafanya kazi katika zama za mwisho. Mtume(s.a.w) amebainisha kuwa kiama kitakuja baada ya kifo cha Isa(a.s) na mwishoni mwa zama bora kama tulivyosoma.

“Baada ya yake(Nabii Isa) siku ya hukumu itakuwa jambo la muda mfupi mbele(Ahmad Diy’aal Din al Kamushkanawi, Ramuz Al Ahadith).

Siku ya hukumu itakuja baada yake(Nabii Isa)( Ahmad Diy’aal Din al Kamushkanawi, Ramuz Al Ahadith.

Hapana shaka zama mwisho na zama bora vitakuwa vipindi ambapo onyo la mwisho litatolewa kwa Wanaadamu. Hadithi nyingi zinaelezea kuwa hapatakuwa na mema baada ya kipindi hiki.

Hivyo tunaona kuwa muda mfupi baada ya kifo cha Isa(a.s) watu duniani watakuwa waovu na wataitupa dini sahihi. Ule wingi wa mali katika zama bora utawazuzua na hivyo kuharibikiwa. Hapa twaweza kusema kuwa katika mazingira haya ndipo kiama kitakapotokea lakini Allah ndiye ajuaye.

Kwa jinsi tulivyoziona dalili za kiama, yaweza kusemwa kuwa Karne hii ya ishirini na moja inaashiria mwanzo wa enzi mpya kabisa za historia ya dunia.

Tunamuomba Allah atufishe na kutufufua hali ya kuwa ni Waislamu.

 
   
    
5 / total 5
|
You can read Harun Yahya's book Dalili Za Kiyama online, share it on social networks such as Facebook and Twitter, download it to your computer, use it in your homework and theses, and publish, copy or reproduce it on your own web sites or blogs without paying any copyright fee, so long as you acknowledge this site as the reference.
About this site | Tengeneza kurasa yako ya nyumbani | Add to favorites | RSS Feed
Mambo yote yanaweza kuynakiliwa, kuchapwa na kusambazwa kwa kurejea katika kurasa hii
(c) All publication rights of the personal photos of Mr. Adnan Oktar that are present in our website and in all other Harun Yahya works belong to Global Publication Ltd. Co. They cannot be used or published without prior consent even if used partially.
© 1994 Harun Yahya.www.harunyahya.com
page_top