Ulimwengu Wa Frimasonri

SHUSHA KITABU

Download (DOC)
Maoni

SURA ZA KITABU

< <
1 / total: 6
Frimasonri - Harun Yahya
Frimasonri
   

 


Chimbuko la Frimasonri

Ufahamu walionao wanahistoria wengi ni kuwa chimbuko la shirika la “Frimansori” ni vita vya msalaba-Crusades, ukweli ni kuwa ingawa shirika hili lilianzishwa na kutambulika rasmi nchini Uingereza mwanzoni mwa karne ya kumi na nane, mizizi yake inaanzia nyuma katika karne ya kumi na mbili. Hata kama baadhi ya watu watang’ang’ania kiyasi gani  kuwa vita vya msalaba vilikuwa ni misafara tu ya kijeshi iliyofanywa kwa jina la Ukristo, kimsingi, ilikuwa ni misafara iliyofanywa kwa minajili ya kupata maslahi ya kimali. Katika kipindi ambacho Ulaya ilikuwa ikikabiliwa na umaskini mkubwa na ufukara, mafanikiyo na utajiri wa mashariki ya kati uliwavutia sana wazungu wa Ulaya. Hii ndiyo ilikuwa sababu ya mabadiliko ya ghafla ya Wakristo wa Ulaya kutoka zile sera zao za utulivu na kuingia katika vita vya kijeshi. Mwanzilishi wa vita hivi vya msalaba alikuwa Papa Urban wa pili(Pope Urban II). Papa huyu aliitisha baraza lake, “Council of Clermont” mnamo mwaka 1095 ambapo ile itikadi ya awali ya utulivu waliyokuwa nayo Wakristo ikawekwa kando. Vikatangazwa vita vitakatifu kwa hila ya kuzipora nchi takatifu kutoka mikononi mwa Waislamu. Kufuwatia azimio la baraza hilo, Jeshi kubwa la wapiganaji wa vita hivyo likaundwa, likishirikisha askari wenye mafunzo ya kitaalamu na maelfu ya wapiganaji wa kujitolea. Wanahistoria wanaamini kuwa hila ya Papa Urban II ilitokana na tamaa yake ya kupata nafasi ya ugombea katika kinyang’anyiro cha Upapa. Tukumbuke kuwa mfumo wa uongozi wa kikatoliki chini ya Papa unatokana na tabaka la Umwinyi uliowakandamiza watu kwa kisingizio cha Dini.

 Wafalme wa Ulaya na Warithi wao waliuafiki wito wa Papa kwa shangwe kumbe malengo yao yalikuwa ya kiduniya kama alivyosema Donald Queller wa Chuo Kikuu cha Illinos, wakuu wa Ufaransa walitaka tu kujiongezeya nchi. Nao wafanyabiashara wa kitaliano walitumai kupanua biyashara katika bandari za mashariki ya kati. Idadi kubwa ya watu masikini wakajiunga na misafara hiyo ili nao wakajikomboe kiuchumi kutokana na hali zao ngumu za maisha. Umati huu wa watu wenye uchu wa mali uliuwa Waislamu wengi na hata Wayahudi kila mahali ulipopita. Kwa sababu tu ya uchu wao wa kujipatia dhahabu na vito vya thamani, wanamgambo hawa wa Crusade walitumbua matumbo ya wale waliowauwa ili wapate dhahabu na madini ya thamani ambayo walidhani wahanga wameyameza kabla ya kufa. Uchu wao wa mali ulikuwa mkubwa mno kiasi kwamba hawakusita kufanya chochote. Baada ya safari ndefu na ngumu ya uporaji mwingi na mauaji makubwa dhidi ya Waislamu, genge hili lililoitwa la Wanamsalaba likafika Jerusalem mnamo mwaka 1099. Baada ya Jiji kuzingirwa kwa karibu majuma matano, Makruseda wakaingia ndani. Walifanya ushenzi makubwa sana. Waislamu na Wayahudi wa Jiji hilo walikatwakatwa mapanga. Mwanahistoria anasema, Waliwaua Waarabu, Waturuki wote waliowakuta humo, Wanaume kwa Wanawake mmoja wa Makruseda hao Raymond akajitapa kwa mauaji haya kwa kusema:

“Baadhi ya watu wetu walikatakata vichwa vya maadui zao, wengine wakawachoma mishale, wengine wakawatesa kwa kuwatupa kwenye moto. Malundo ya vichwa, mikono na miguu, yalionekana katika mitaa ya Jiji. Mtu alilazimika kukanyaga miili ya watu na farasi ili kupita njia. Lakini yote hayo ni madogo kulinganisha na ale yaliyotokea kwenye hekalu la Suleiman, mahali ambapo shughuli za kidini hufanyika. Katika hekalu hilo, watu walipita kwenye madimbwi ya damu, miguu ilizama hadi magotini.”

 
   
    
1 / total 6
You can read Harun Yahya's book Ulimwengu Wa Frimasonri online, share it on social networks such as Facebook and Twitter, download it to your computer, use it in your homework and theses, and publish, copy or reproduce it on your own web sites or blogs without paying any copyright fee, so long as you acknowledge this site as the reference.
About this site | Tengeneza kurasa yako ya nyumbani | Add to favorites | RSS Feed
Mambo yote yanaweza kuynakiliwa, kuchapwa na kusambazwa kwa kurejea katika kurasa hii
(c) All publication rights of the personal photos of Mr. Adnan Oktar that are present in our website and in all other Harun Yahya works belong to Global Publication Ltd. Co. They cannot be used or published without prior consent even if used partially.
© 1994 Harun Yahya.www.harunyahya.com
page_top