Ulimwengu Wa Frimasonri

SHUSHA KITABU

Download (DOC)
Maoni

SURA ZA KITABU

< <
2 / total: 6
Frimasonri - Harun Yahya
Frimasonri
   

 


Historia ya Matempla

Kwa kifupi Matempla hawakutoweka kabisa bali falsafa yao. Imani zao na ibada zao bado zinaendelea chini ya mwavuli wa Frimansori. Dhana hii inatiwa nguvu za ushahidi mwingi wa kihistoria na hivi leo inakubaliwa na idadi kubwa ya Wanahistoria wa magaharibi ima awe Mafyoso au la. Katika kitabu chetu, The new Masonic Order, tumeutathmini kwa kina ushahidi huu. Dhana inayoihusisha mazizi ya Mansori na Matempla, mara nyingi inarejewa katika majarida yanachapishwa na Mansori wenyewe kwa ajili ya Wananchama wao. Wanachama wa Frimansori wanaikubali kabisa dhana hii. Mojawapo ya majarida hayo linaitwa Minnar Sinan(ni jarida la Mafyoso wa Uturuki) ambalo linaelezea uhusiano kati ya komandi ya Matempla na Frimansori kwa maneno yafuatayo”

“Mnamo mwaka 1312, pale Mfalme wa Ufaransa kwa shinikizo la kanisa alipolifunga komandi ya Matempla na mali zao kuwapa askari wa mtakatifu John mjini Jerusalem harakati za matempala hazikukoma. Idadi kubwa ya Matempala wakapata hifadhi katika maskani ya Frimansori iliyokuwepo Ulaya wakati huo. Kiongozi wa Matempla, Mabeignac, akiwa na wanachama wengine, wakapata usalama nchini Scotland chini ya mwavuli wa Wall builder na chini ya jina la Mac Benach. Mfalme Scotland Robert the Bruce akawakaribisha na kuwaruhusu kuwa na ushawishi mkubwa katika maskani za Frimansori nchini Scotland. Matokeo yake maskani za Scotland umuhimu mkuibwa kwa mtazamo wao wa kiufundi na fikra zao. Leo hii Mafyoso wanatumia jina la Mac Benach kwa heshima. Mafyoso wa Ufaransa waliorithi vitu vya Matempla wakareje zao Ufaransa miaka mingi baadaye na kuimarisha ngome yao ya kaaida ikijulikana kama kaaida ya Scotland(Scotish Rights).

Aidha, Mimar Sinan inatoa habari nyingi kuhusu uhusiano wa Matempla na Mafrimasonri. Katika makala yake iliyokuwa iliyokuwa na kichwa Templas and Frimanson inasema sala ya sherehe za uzinduzi wa Komandi ya Matempla ni sawa kabisa na sala Mafyoso wa zama hizi. Kwa mujibu wa makala hiyo hiyo, kama ilivyo katika Mansori wanachama wa Komandi ya Matempla wakiitana Brother(ndugu). Mwishoni mwa makala hayo tunasoma maneno haya; “komandi ya Matempla na shirika la Frimansoni yanashajiishana, kwa kiasi kikubwa hata sala za mashirika haya zinashabihiana kwa maana zimaigwa kutoka kwa Matempla. Kwa ajili hii, Mafyoso kwa kiasi kikubwa wamejifananisha na Matempla na yaweza kusemwa kuwa, kile kinachoonwa kuwa ni usiri mkubwa wa Frimansonri kwa kiasi kikubwa kimeigwa kutoka kwa Matempla. Kwa kufupisha hapa ni kuwa, kama tulivyoona  twaweza kusema kuwa chanzo cha sanaa za Kifalme na usiri wa Frimansori chatokana na Matempla. Mwisho, tunasema kuwa imetokea huko nyuma kwa Matempla na kwamba Mafyoso wamefuata falsafa ya Komandi ya Matempla. Mafyoso wenyewe wanalikubali hili lakini jambo muhimu kwa tafakuri yetu ni nini asili au chanzo cha falsafa hii. Kwa nini Matempla waliachana na Ukristo na kufuata mafundisho mapya. Kitu gani kilichosababisha wafikiye  uamuzi huo? Kwa nini walifanya mageuzi hayo kule Jerusalem na je kupitia tawi hili la Frimansoni kumekuwa na athari gani Duniyani kutokana na Falsafa hii iliyofuatwa na Matempla.

Matempla na Kaballa

Kitabu kilichoandikwa na Mafyoso Christopher na Robert Lomas kiitwacho The Hiram Key kinafichuwa mambo fulani ya kweli kuhusu mizizi ya Frimansori. Kwa mujibu wa Waandishi hawa, ni dhahiri kuwa Frimansori ni mwendelezo wa  Matempla. Mbali na hivyo, Waandishi hawa piya, wameviangaliya piya vyanzo vya Matempla. Kulingana na dhanna yao, Matempla walipitia hatua kubwa za mabadiliko wakati walipokuwa Jerusalem. Mahala palipokuwa kwa Ukristo wao walianzisha madhehebu nyingine. Katika mzizi wa mabadiliko haya, kuna siri ambayo waliifichua ambayo ni hekalu la Suleiman pale Jerusalem ambalo mabaki yake, walitaka kuyachunguza. Waandishi hawa wanasema kuwa, Matempla walikuwa wakiutumia ule ulioitwa kuwa wajibu wao wa kulinda mahujaji wa Kikristo waliozuru pale Palestina lakini kumbe hiki kilikuwa kisingizio, lengo halisi lilikuwa jingine kabisa. Hakuna ushahidi kuwa wale Waasisi walikuwa wakitoa ulinzi kwa Mahujaji bali tulichokugundua ni kuwa kuna ushahidi mkubwa kuwa walikuwa wakichimbua chini ya mabaki ya hekalu la Herold. Waandishi wa kitabu cha Hiram Key sio wao pekee waliogundua vielelezo vya jambo hili. Gaetani De la Forge, Mwanahitoria wa Ufaransa naye ametoa maelezo kama haya; “jukumu halisi la Wale wanamgambo tisa wa Krusade walikuwa wakifanya utafiti katika eneo hilo ili kupata masalia na kupata kumbu kumbu za maandiko ya awali ambao yanachimbuko ya maelezo ya siri ya dini ya kiyahudi na Misri ya zama za kale.

Mwisho mwa karne ya 14 Charles Wilson wa Royal Engeneers alianza kufanya utafiti wa mabaki ya kale kule Jerusalem. Yeye akafka mahala pa kuona kuwa, Matempla walikuwa wamekwenda Jerusale kutaifiti mabaki ya hekalu. Wilson aligundua chimba chimba na fukua fukua china ya misingi ya hekalu na akahitimisha kuwa kazi hii ilifanywa kwa zana ambazo zilikuwa za Matempla.

Vifaa hivi vingalipo katika hazina ya mabaki ya kale ya Robert Brydon, ambaye anamiliki hifadhi ya kumbu kumbu zinazohusiana na Matempla. Waandishi wa kitabu cha the Hiram Key wanadai kuwa chimba chimba ya Matempla haikuishia matupu, kwamba ile Komandi iligundua kumbukumbu fulani pale Jerusalem ambayo ndiyo iliyobadili mtazamo wao. Mbali na hao watafiti wengine nao wana maoni hayo hayo. Yumkini lazima kulikuwa na jambo lililowapelekea Matempla kubadili mfumo wa imani na falsafa yao tafauti na Ukristo licha ya ukweli kuwa hapo awali walikuwa wakristo waliotoa katika  nchi ya Kikristo. Kwa mujibu wa fikra za watafiti wengi jambo hili lilikuwa Kaballa.

 Maana ya neno Kaballa, ni fasihi simulizi. Maandiko na makamusi yanalifafanua neno hili kama siri kubwa, tawi la siri siri la dini ya Uyahudi. Kwa mujibu wa ainisho hili neno la Kaballa linachukua maana iliyofichikana katika Taurati na maandiko mengine ya dini Uyahudi. Lakini tunapochunguza kwa undani jambo hili tunaona kuwa ukweli wa mambo ni mwingine kabisa. Hakika ya mambo inatuplekea kufikiri hitimisho jingine kuwa Kaballa ni mfumo wenye mizizi ya ushirikina wa kipagani, kwamba ilikuwepo kabla ya Taurati na ilienea ndani ya dini ya Uyahudi hata baada ya kufunuliwa kwa Taurati. Ukweli huu wa kuvutia kuhusu Kaballa unafafanuliwa kuwa ndio chanzo hasa. Murat Orgen, Frimansori wa kituruki yeye anasisitiza yafuatayo katika kitabu chake Masonluk Nedir Ve Nasirdir?(Frimasonri ni nini, ikoje?).

“Hatujui vizuri wapi ilikotokea Kabbalah au namna ilivyojiendeleza ni jina la jumla la falsafa moja ya siri iliyojengwa kwa iami i ya kiroho hasa hasa inayohusiana na dini ya Uyahudi Huu ni Usufi wa dini ya kiyahudi lakini baadhi ya mambo iliyonayo yanaonesha kuwa likusanywa zamani zaidi kabla ya Taurati. Mwanahistoria wa Ufaransa Gougenot Des Mousseaux yeye anasema kuwa, Kaballa ni ya zamani kabla ya Uyahudi.

Historia ya Matempla

Kwa muda wa siku mbili tu jeshi la msalaba liliwaua kinyama Waislamu wapatao 40,000. baada ya hapo Wanamgambo hao katili wakaifanya Jerusalem kuwa mji wao mkuu na kuanzisha utawala wa Kifalme wa Kilatini ambao ulijitanua kutoka mipaka ya Palestina hadi Antiokia. Baadaye Wapiganaji hao wa vita vya msalaba wakaanzisha mapambano ya kuimarisha utawala wao katika eneo la mashariki ya kati. Wakaanzisha kambi za mafunzo ya kijeshi kwenye majumba kama yale ya kitawa. Washiriki katika mafunzo hayo walitoka Ulaya kuja Palestina na wakaishi katika majumba hayo. Mojawapo ya Komandi zao za kijeshi ilitafautiyana kabisa na nyingine yenyewe ilibadilika muundo kukidhi haja ya wakati. Komandi hii mahususi ilikuwa ya wale walioitwa mashujaa watakatifu yaani Templars. Templar hii au kwa jina kamili, askari dhaifu wa Yesu Kristo na hekalu la Suleiman, iliundwa mwaka 1118, miaka ishirini baada ya wanamgambo wa msalaba kuitwaa Jerusalem. Waanzilishi wa Komandi hii walikuwa ni Wafaransa wawili, Hugh de Payens na Godfrey dest Omer. Mwanzoni kulikuwa na askari lakini Komandi ikazidi kuimarika. Sababu ya wao kujipa jina templar ni kuwa mahali walipochagua kuwa kituo chao palikuwa na kilima cha temple ambako ndiko hekalu hili gofu liliko. Japo Wanamgambo hawa walijiita Templer yaani askari wanyonge lakini kwa kipindi kifupi tu wakawa matajiri sana. Mahujaji wa Kikristo kutoka Ulaya kuja Palestina walikuwa chini ya udhibiti wa Komandi hii na kwa pesa zake nao wakawa matajiri. Mbali na hivyo, kwa mara ya kwanza wakaanzisha mfumo wa hundi na mikopo sawa na ule wa Benki. Kwa mujibu wa Waandishi wa Kiingereza Michael Baigent na Richard Leigh, walianzisha aina fulani ya ubepari na wao ndio waliopelekea kuanzishwa kwa shughuli za sasa za mabenki zinazotoza riba kutokana na ule mfumo wao wa uchumi uliojengwa kwa msingi wa riba. Walikuwa ni hawa Matemplar ambao walihusika na mashambulizi na mauaji dhidi ya Waislamu. Kwa sababu hii Kamanda mkuu wa kiislamu Salahuddin aliyelishinda jeshi la Makruseda mnamo 1187 katika vita ya Hattin na baadaye kuikomboa Jerusalem, aliwahukumu kifo Matemplar kwa mauaji waliyokuwa wameyafanya na akawasamehe Wakristo wengi. Ijapokuwa waliipoteza Jerusalem na kupata madhara makubwa, Matemplar wakaendelea kuishi na licha ya kupungua kwa Wakristo Palestina, wakaongeza nguvu zao Ulaya wakianzia na Ufaransa na kisha katika nchi nyingine. Ikawa dola iliyokuwa ndani ya dola. Bila shaka nguvu zao za kisiasa ziliwanyima raha watawala wa Ulaya. Pia kulikuwa na jambo ambalo nalo liliwatia homa Makasisi. Kamandi ilianza kujitoa kidogo kidogo katika imani ya Kikristo.

Na wakiwa Jerusalem wakaanza kufuata madhehebu ya kikuhani. Kukawa na uvumi pia kwamba walikuwa wakifanya ibada za ajabu ajabu. Mwishowe mnamo mwaka 1307 Mfalme wa Ufaransa Philip akaamua kuwatia mbaroni Matempla hao. Baadhi yao wakafanikiwa kutoroka lakini wengi walikamatwa. Papa Clement wa Tano(Popedement V) pia nae akafanya hivyo. Baada ya kipindi kirefu cha mahojiano na mashitaka, Matempla wengi walikiri kufuata imani ya kikristo na kumtusi Yesu katika mihadhara yao. Hatimaye viongozi wa Matempla ambao waliitwa mabwana wakubwa akiwemo yule kigogo wao, Jecques de Moky wakamnyonga mwaka 1314 kwa amri ya Kanisa na mfalme. Wengi wao wakafungwa jela na Kamandi ikasambaratika na kutoweka kabisa. Baadhi ya wanahistoria wanakawaida ya kuonesha kuwa shitaka lililowakabili Matempla lililotokana na njama za Mfalme wa Ufaransa kwa kuwataja wapiganaji hao wa vita vya msalaba kuwa si watu wenye hatia. Nesta H. Webster, Mwanahistoria mashuhuri wa kiingereza mwenye elimu kubwa ya Histori ya ukuhani anayachambua masuala haya katika kitabu chake, Secret Society and Subversive Movement.

Kwa mujibu wa Webster, kitendo cha kuwatoa Matempla hatiani kwa yale waliyoyafanya katika kipindi cha mashitaka hakiwezi kukubalia kwanza wakati wa mahojiano, si Matempla wote walioteswa. Isitoshe je yale maneno ya kukiri ya Matempla yametokana na mateso waliyopewa? Kwa kweli ni vigumu kusadiki kuwa maelezo yanayotolewa na watu katika nchi mbali mbali yote yakishabiiana kabisa, eti yote yatokane na uzushi. Kama wahanga wangelishurutisha kwa mateso basi wangetoa maelezo yenye mgongano katika kuelezea aina mgongano katika kuelezea aina zote za sala za ajabu ajabu zilizokuwa zikifanyika. Lakini hasha, kila mmoja anaonekana kuelezea vile vile sala zile zile. Vyovyote iwavyo, shauri la Matempla lilikwisha Sawia na Komandi. Japo Komandi ilikoma rasmi kufanya kazi lakini kwa kweli haikutokomea kabisa. Katika kamatakamata ya mwaka 1307, baadhi ya Matempla walifanikiwa kutoroka. Kwa mujibu wa tasnifu zilizoambatanishwa nyaraka mbali mbali za kihistoria, idadi fulani ya watu miongoni mwao walipata hifadhi katika falme moja ya Ulaya ambayo haikutambua mamlaka ya Kanisa Katoliki katika karne ya kumi na nne, nayo ni Scotland.

Huko walijikusanya upya chini ya ulinzi wa Mfalme wa Uskochi Robert the Bruce. Baada ya muda fulani, wakagundua mbinu muafaka ya kujificha ili waendelee kuishi kisirisiri. Walijipenyeza kwenye makazi muhimu katika visiwa vya Uingereza-the wall builders Lodges. Hatimaye wakapata mamlaka kamili ya kumiliki majumba haya. The wall builders Lodges, ikabadili jina lake, mwanzoni mwa zama hizi na sasa ikajiita the Masonic Lodge. Kwa desturi ya Scotland-The Scotish Rite ndiyo tawi kongwe kabisa la Frimansori, hiyo ikiwa ni mwanzoni mwaka Karne ya kumi na nne, pale Matempla- Mashujaa wa msalaba walipopata hifadhi nchini humo.

Mwanahistoria wa Kiyahudi, Theodore Reinach anasema kuwa kabbalah ni sumu ya ajabu kabisa inayoingia ndani ya vena za Uyahudi na kuziathiri kabisa.  Salomoni Reinach anaiainisha kabbalah kama ni moja ya pogo za akili ya mwanadamu. Sababu ya maelezo haya ya Reinach kuwa kabbalah ni moja ya pogo za akili ya binadamu ni kuwa mafundisho yake yananasibiana kwa kiasi kikubwa na uchawi.  Kwa maelfu ya miaka, kabbalah imekuwa moja  ya misingi ya kila Ibada ya uchawi.  Inasadikika kuwa wasomi wa kiyahudi (Rabbis) wanaosomea kabbalah wana nguvu kubwa za kichawi. Aidha watu wengi wasiokuwa wayahudi wameathiriwa na kabbalah na wamejaribu kutumia uchawi kwa kutumia mafundisho yake.  Mambo ya siri ambayo yalikita mizizi Ulaya mwishoni mwa zama za kati hasa yale yaliofanywa na wanakemia, kwa kiasi kikubwa mizizi yake ipo katika kabbalah. Jambo la ajabu ni kuwa Uyahudi ni dini ya Mungu mmoja inayokwenda kwa ufunuo wa Taurati ya Musa (a.s) lakini ndani ya dini hii kuna utaratibu unaoitwa kabbalah ambao unafuata yale mafundisho ya msingi ya uchawi yaliyoharamishwa na dini hii.  Hii inathibitisha ukweli tuliouelezea hapo juu na inabainisha kuwa kabbalah kwa uhalisi wake ni jambo ambalo limeingia katika Uyahudi kutoka nje ya dini hii. Lakini nini chanzo cha jambo hili?

Mwanahistoria wa Kiyahudi Fabre d’Olivet  anasema kuwa kabbalah ilitokea katika Misri ya kale.  Kwa mujibu wa mwandishi huyu, mizizi ya kabbalah imetambaa kutoka Misri ya kale.  Kabbalah ni hadithi iliyosikiwa na baadhi ya viongozi wa Waisrael katika Misri ya kale na ikawasilishwa kwa njia ya fasihi simulizi kutoka kizazi hadi kizazi. Kwa sababu hiyo, lazima tuiangalie Misri ya kale ili tuone vyanzo hasa vya kabbalah- matempla na Frimansori.

Wachawi wa Misri ya zamani

Misri ya kale ya Mafirauni(Mafarao) ilikuwa moja ya nchi zilizokuwa na tamaduni kuu za enzi hizo ulimwenguni.  Ilikuwa moja ya nchi za kidhalimu kabisa.  Minara mikubwa ambayo bado ipo tangia enzi hizo za Misri ya kale kama mapiramidi yalijengwa na mamia kwa maelfu ya watumwa waliofanya kazi,kwa vitisho vya bakora na kunyimwa chakula hata kufikia mahala pa kufa. Mafirauni, watawala wakuu wa Misri walijitapa kuwa wao ni miungu na kwamba waabudiwe na watu. Moja ya vyanzo vya habari kuhusu Misri ya Kale ni maelezo yao wenyewe.Maelezo haya yaligunduliwa katika karne ya 19 na baada ya kazi ngumu, herufi za Kimisri zikasomeka na hivyo taarifa nyingi kuhusu nchi hiyo zikapatikana.  Lakini kwa vile maelezo haya yaliandikwa na Wanahistoria waliokuwa serikalini, yamejaa maelezo ya upendeleo ambayo yalikusudiwa kuitukuza dola.

Bila shaka, kwetu sisi, chanzo cha habari juu ya jambo hili ni Qur’an.  Katika Qur’an, katika kisa cha Musa, tunapewa habari muhimu kuhusu utawala wa Misri. Aya za Qur’an zinabainisha kuwa kulikuwa na mamlaka kuu mbili za utawala nchini Misri; Firauni na baraza lake la ndani. Kazi ya baraza hili ilikuwa ni kumtukuza Firauni; mara zote firauni alikuwa akikutana nalo na katika nyakati fulani fulani alikuwa akifuata maoni ya baraza lake . Aya zinazonukuliwa hapa chini zinaonyesha kazi ya baraza hilo;  “Na alisema Musa; Ewe Firauni! Mimi ni Mtume nitokae kwa Mola wa walimwengu.  Yanipasa nisiseme juu ya Mwenyezi Mungu lolote ila haki tu.  Kwa yakini nimekufikieni kwa dalili waziwazi zitokazo kwa Mola wenu.  Basi wapeleke wana wa Israel pamoja nami katika (nchi waitakayo, usiwazuilie hapa Misri ukawa unawatesa).  Firauni akasema kama umekuja na hoja basi ilete ukiwa ni miongoni wa wasemao kweli.  Hapo Musa akaitupa fimbo yake  (chini).  Na mara ikawa nyoka dhahiri.  Na akatoa mkono wake.  Mara ukawa mweupe kwa watazamao.  Wakasema wakuu wa kaumu ya Firauni (pamoja na yeye Firauni); hakika huyo ni mchawi ajuae (uchawi vema). Anataka kukutoeni katika ardhi yenu.  Basi mnatoa shauri gani?  Wakasema (kumwambia firauni).  Muache kidogo yeye na ndugu yake (huyu Haruni anayejipa Utume pamoja naye, usiwaue).  Na watume (wakusanyao mijini wakukusanyie wachawi wakubwa wakubwa wote).  Wakuletee kila mchawi ajuae Qur’an sura (7:104-112). Izingatiwe kuwa hapa limetajwa baraza la Firauni ambalo linamshauri, na ambalo linamuhamasisha kupambana na Musa na linapendekeza mbinu fulani.  Tukiziangalia kumbukumbu za Historia ya Misri, tunaona kuwa kada kuu mbili za baraza hili zilikuwa ni jeshi na Taasisi ya Ukasisi.  Hakuna haja ya kufafanua umuhimu wa jeshi; Jeshi hili ndilo lililojenga nguvu za tawala za Mafirauni.  Ila tulitazame kwa mazingatio zaidi jukumu la Makasisi hawa.  Makasisi wa Misri ya kale walikuwa ni tababaka la watu ambao katika Qur’an wametajwa kama wachawi.  Hawa waliwakilisha dhehebu ambalo liliunga mkono utawala.  Iliaminika kuwa nao walikuwa na madaraka maalum na walikuwa na elimu ya sihiri.  Kwa madaraka haya, waliwavuta watu wa Misri na kuimarisha nafasi yao katika utawala wa Mafirauni.  Tabaka hili kwa mujibu wa kumbukumbu za Misri, lilijulikana kama Makasisi wa Amoni. Hawa walikuwa na kazi ya kufanya uchawi na kuendesha dhehebu lao la kipagani; mbali na hivyo pia walisomea sayansi mbalimbali kama vile unajimu, hesabati na  Jiometri.  Tabaka hili la makasisi ilikuwa ni Taasisi iliyokuwa na elimu maalum.    Katika jarida lililoitwa Mason Dergisi,  Jarida lililosambazwa kwa mafyoso wa Uturuki, Mizizi ya Frimansori inatajwa kuanzia katika Taasisi hii ya siri, na wanatajwa rasmi makasisi wa Misri ya kale. Tafakuri inavyozidi kukuwa kwa wanadamu, Sayansi nayo inazidi kupiga hatua na kadri Sayansi inavyopiga hatua siri nyingi zinazidi kuongezeka katika mfumo wa siri.  Katika hatua hii ya maendeleo shughuli ya siri ambayo kwanza ilianzia Mashariki, China na Tibet na kisha kuenea India, Mesopotamia na Misri ikajenga msingi wa elimu ya ukasisi ambayo imefanyiwa kazi kwa maelfu ya miaka na kujenga msingi wa madaraka ya makasisi nchini Misri. Kuna uhusiano gani kati ya falsafa ya siri ya Makasisi wa Misri ya zamani na Mafrimansori wa hivi leo?  Misri ya zamani ni mfano hai wa mfumo wa siasa usio na Mungu uliotajwa katika Qur’an,ambao ulitokomea maelfu ya miaka iliyopita.  Je waweza kuwa na athari hadi leo?  Kupata jibu la maswali haya lazima tuziangalie Imani za Makasisi wa Misri ya kale kuhusiana na chanzo cha Ulimwengu na maisha. Kwa kifupi Matempla hawakutoweka kabisa bali falsafa yao. Imani zao na ibada zao bado zinaendelea chini ya mwavuli wa Frimansori. Dhana hii inatiwa nguvu za ushahidi mwingi wa kihistri na hiv leo inakubwaliwa na idadi kubwa ya Wanahistoria wa magaharibi ima awe Mafyoso au la. Katika kitabu chetu, The new Masonic Order, tumeutathmini kwa kina ushahidi huu. Dhana inayoihusisha mazizi ya Mansori na Matempla, mara nyingi inarejewa katika majarida yanachapishwa na Mansori wenyewe kwa ajili ya Wananchama wao. Wanachama wa Frimansori wanaikubali kabisa dhana hii.

Mojawapo ya majarida hayo linaitwa Minnar Sinan(ni jarida la Mafyoso wa Uturuki) ambalo linaezea uhusiano kati ya komandi ya Matempla na Frimansori kwa maneno yafuatayo”. “Mnamo mwaka 1312, pale Mfalme wa Ufaransa kwa shinikizo la kanisa alipolifunga komandi ya Matempla na mali zao kuwapa askari wa mtakatifu John mjini Jerusalem harakati za matempala hazikukoma. Idadi kubwa ya Matempala wakapata hifadhi katika maskani ya Frimansori iliyokuwepo ulaya wakati huo. Kiongozi wa Matempla, Mabeignac, akiwa na wanachama wengine, wakapata usalama nchini Scotland chini ya mwavuli wa Wall builder na chini ya jina la Mac Benach. Mfalme Scotland Robert the Bruce akawakaribisha na kuwaruhusu kuwa na ushawishi mkubwa katika maskani za Frimansori nchini Scotland. Matokeo yake maskani za Scotland umuhimu mkuibwa kwa mtazamo wao wa kiufundi na fikra zao. Leo hii Mafyoso wanatumia jina la Mac Benach kwa heshima. Mafyoso wa Ufaransa waliorithi vitu vya Matempla wakareje zao Ufaransa miaka mingi baadaye na kuimarisha ngome yao ya kaaida ikijulikana kama kaaida ya Scotland(Scotish Rights). Aidha, Mimar Sinan inatoa habari nyingi kuhusu uhusiano wa Matempla na Mafrimasonri. Katiika makala yenye kichwa Templas and Frimanson inasema sala ya sherehe za uzinduzi wa Komandi ya Matempla ni sawa kabisa na sala Mafyso wa zama hizi. Kwa mujibu wa makala hiyo hiyo, kama ilivyo katika Mansori wanachama wa Komandi ya Matempla wakiitana Brother(ndugu). Mwishoni mwa makala hayo tunasoma maneno haya; “komandi ya Matempla na shirika la Frimansoni yanashajiishana, kwa kiasi kikubwa hata sala za mashirika haya zinashabihiana kwa maana zimaigwa kutoka kwa Matempla. Kwa ajili hiyo, Mafyoso kwa kiasi kikubwa wamejifananisha na Matempla na yaweza kusemwa kuwa, kile kinachoonwa kuwa ni usiri mkubwa wa Frimansonri kwa akisai kikubwa kimeigwa kutoka kwa Matempla. Kwa kufupisha hapa ni kuwa, kama tulivyosema katika anuani ya makala haya, twaweza kusema kuwa chanzo cha sanaa Kifalme na usiri wa Frimansori chatokana na Matempla. Mwisho, tunasema kuwa imetokeya huko nyuma kwa Matempla na kwamba Mafyoso wamefuata falsafa ya Komandi ya Matempla. Mafyoso wenyewe wanalikubali hili lakini jambo muhimu kwa tafakuri yetu ni nini asili au chanzo cha falsafa hii. Kwa nini Matempla waliachana na Ukristo na kufuata mafundisho mapya. Kitu gani kilichowapelekea kufikia uamuzi huo? Kwa nini walifanya mageuzi hayo kule Jerusalem na je kupitia tawi hili la Frimansoni kumekuwa na athari gani Duniyani kutokana na Falsafa hii iliyofuatwa na Matempla.

 
   
    
2 / total 6
You can read Harun Yahya's book Ulimwengu Wa Frimasonri online, share it on social networks such as Facebook and Twitter, download it to your computer, use it in your homework and theses, and publish, copy or reproduce it on your own web sites or blogs without paying any copyright fee, so long as you acknowledge this site as the reference.
About this site | Tengeneza kurasa yako ya nyumbani | Add to favorites | RSS Feed
Mambo yote yanaweza kuynakiliwa, kuchapwa na kusambazwa kwa kurejea katika kurasa hii
(c) All publication rights of the personal photos of Mr. Adnan Oktar that are present in our website and in all other Harun Yahya works belong to Global Publication Ltd. Co. They cannot be used or published without prior consent even if used partially.
© 1994 Harun Yahya.www.harunyahya.com
page_top