Ulimwengu Wa Frimasonri

SHUSHA KITABU

Download (DOC)
Maoni

SURA ZA KITABU

< <
3 / total: 6
Frimasonri - Harun Yahya
Frimasonri
   

 


Matempla na Kaballa

Kitabu kilichoandikwa na Mafyoso Christopher na Robert Lomas kiitwacho The Hiram Key kinafichua mambo fulani ya kweli kuhusu mizizi ya Frimansori. Kwa mujibu wa Waandishi hawa, ni dhahiri kuwa Frimansori ni mwendelezo wa  Matempla. Mbali na hivyo, Waandishi hawa pia, wameviangalia pia vyanzo vya Matempla. Kulingana na dhanna yao, Matempla walipitia hatua kubwa za mabadiliko wakati walipokuwa Jerusalem. Mahala palipokuwa kwa Ukristo wao walianzisha madhehebu nyingine. Katika mzizi wa mabadiliko haya, kuna siri ambayo waliifichua ambayo ni hekalu la Suleiman pale Jerusalem ambalo mabaki yake, walitaka kuyachunguza. Waandishi hawa wanasema kuwa, Matempla walikuwa wakiitumia ule ulioitwa kuwa wajibu wao wa kulinda mahujaji wa Kikristo waliozuru pale Palestina lakini kumbe hiki kilikuwa kisingizio, lengo halisi lilikuwa jingine kabisa. Hakuna ushahidi kuwa wale Waasisi walikuwa wakitoa ulinzi kwa Mahujaji bali tulichokugundua ni kuwa kuna ushahidi mkubwa kuwa walikuwa wakichimbua chini ya mabaki ya hekalu la Herold. Waandishi wa kitabu cha Hiram Key sio wao pekee waliogundua vielelezo vya jambo hili. Gaetani De la Forge, Mwanahitoria wa Ufaransa naye ametoa maelezo kama haya; “jukumu halisi la Wale wanamgambo tisa wa Krusade walikuwa wakifanya utafiti katika eneo hilo ili kupata masalia na kupata kumbu kumbu za maandiko ya awali ambao yanachimbuko ya maelezo ya siri ya dini ya kiyahudi na Misri ya zama za kale. Mwisho mwa karne ya 14 Charles Wilson wa Royal Engeneers alianza kufanya utafiti wa mabaki ya kale kule Jerusalem. Yeye akafka mahala pa kuona kuwa, Matempla walikuwa wamekwenda Jerusale kutaifiti mabaki ya hekalu. Wilson aligundua chimba chimba na fukua fukua china ya misingi ya hekalu na akahitimisha kuwa kazi hii ilifanywa kwa zana ambazo zilikuwa za Matempla. Vifaa hivi vingalipo katika hazina ya mabaki ya kale ya Robert Brydon, ambaye anamiliki hifadhi ya kumbu kumbu zinazohusiana na Matempla. Waandishi wa kitabu cha the Hiram Key wanadai kuwa chimba chimba ya Matempla haikuishia matupu, kwamba ile Komandi iligundua kumbukumbu fulani pale Jerusalem ambayo ndiyo iliyobadili mtazamo wao.

Mbali na hao watafiti wengine nao wana maoni hayo hayo. Yumkini lazima kulikuwa na jambo lililowapelekea Matempla kubadili mfumo wa imani na falsafa yao tofauti na Ukristo licha ya ukweli kuwa hapo awali walikuwa wakristo waliotoa katika  nchi ya Kikristo. Kwa mujibu wa fikra za watafiti wengi jambo hili lilikuwa Kaballa. Maana ya neno Kaballa, ni fasihi simulizi. Misahafu na makamusi yanalifafanua neno hili kama siri kubwa, tawi la siri siri la dini ya Uyahudi. Kwa mujibu wa ainisho hili neno la Kaballa linachukua maana iliyofichikana katika Taurati na maandiko mengine ya dini Uyahudi. Lakini tunapochunguza kwa undani jambo hili tunaona kuwa ukweli wa mambo ni mwingine kabisa. Hakika ya mambo inatuplekea kufikiri hitimisho jingine kuwa Kaballa ni mfumo wenye mizizi ya ushirikina wa kipagani, kwamba ilikuwepo kabla ya Taurati na ilienea ndani ya dini ya Uyahudi hata baada ya kufunuliwa kwa Taurati. Ukweli huu wa kuvutia kuhusu Kaballa unafafanuliwa kuwa ndio chanzo hasa. Murat Orgen Frimansori wa kituruki yeye ansisitiza yafuatayo katika kitabu chake Masonluk Nedir Ve Nasirdir?(Frimasonri ni nini, ikoje?).

“Hatujui vizuri wapi ilikotokea Kabala au namna ilivyojiendeleza ni jina la jumla na kuwa ilikusanywa zamani zaidi kabla ya Taurati. Mwanahistoria wa Ufaransa Gougenot Des Mousseaux yeye anasema kuwa, Kaballa ni ya zamani kabla ya Uyahudi.

Imani ya kale ya Misri juu ya dhana ya evolusheni

Katika kitabu chao kiitwacho,The Hiram Key, waandishi wa frimansori wa kiingereza Christopha Knight na mwenzie Robert Lomas wanadai kuwa Misri ya kale inachukua  sehemu muhimu kuhusiana na vyanzo vya frimansori.    Kwa mujibu wa waandishi hao,fikra muhimu ambayo imezaa frimansori ya sasa kutoka Misri ya kale ni ile ya ulimwengu kujiendesha wenyewe na kutokea kwa bahati nasibu.Wanaifafanua dhana hii kwa maneno haya:

 Wamisri waliamini kuwa maada ilikwishakuwepo siku zote; kwao wao lilikuwa ni jambo lisilo kuwa na mantiki kufikiri kuwa Mungu ndiye anayefanya kila kitu kutokana na hamna.  Dhana yao ilikuwa kwamba ulimwengu ulianza pale ilipotokea mvurugano,na kwamba tokea hapo kumekuwa na ugomvi baina ya nguvu za asili.    Hali hii ya machafuko iliitwa Nun, na kama yalivyo maelezo ya Sumaria kulikuwa na giza tupu sehemu zote, hapakuwa na jua ndipo nguvu kujiumba ilipoamuru maisha yaanze.Nguvu hii isiyoonekana ambayo ilikuwa ndani ya machafuko haikujijua kuwa yenyewe ilikuwepo.   Itakumbukwa kuwa imani zilizoelezwa hapa zinafanana kabisa na madai ya walahidi wa zama hizi, imani zinakuzwa na ajenda ya jamii ya wanasayansi  wakitumia maneno kama vile nadharia ya evolusheni, nadharia ya mchafuko(chaos theory)na mjumuiko wa maada(essential organization of matter). 

  Knight na Lomas wanaendelea kusema; Cha kushangaza, maelezo haya juu ya maumbile yanaiolezea kikamilifu dhana inayoshikiliwa na sayansi ya leo hasahasa chaos theory.  Knight na Lomas wanadai kuwa kuna uwiano kati ya imani za kale za Misri na sayansi ya leo, lakini wanapozungumza juu ya sayansi ya leo, kama tulivyosema, wanamaanisha dhana za kilahidi,kama vile nadharia ya evolusheni na nadharia ya machafuko.    Licha ya ukweli kwamba  nadharia hizi hazina msingi wa kisayansi,zimewekwa kinguvunguvu katika fani ya sayansi kwa takriban karne mbili zilizopita, na zinawasilishwa kama nadharia zilizohalalishwa kisayansi.(Katika vifungu vifuatavyo tutawatazama wale walioweka nadharia hizi katika ulimwengu wa sayansi.)

    Sasa tumefikia nukta muhimu.  Tuelezee kwa kifupi kile tulichokigundua hadi hapa tulipofika;

 1.Tulianza mjadala wa kujadili oda ya matempla ambayo ndiyo inayodhaniwa kuwa chanzo cha frimansori.Tumeona kuwa, ingawaje matempla kimsingi walionekana kama wakristo lakini waliathiriwa na mafundisho ya siri waliyoyagundua yerusalemu, wakachana kabisa na ukristo na wakawa na Taasisi inayopinga kabisa dini hii wakitekeleza ibada mpya. 

 2.Pale tulipouliza ni itikadi gani hiyo iliyowakumba matempla,tukaona kuwa kimsingi ilikuwa kabbalah.

 3.pale tulipoichunguza kabbalah ,tukapata ushahidi kuwa ilikuwa ni itikadi ya kipagani ambayo ilikuwa ya zamani mno kuliko uyahudi japo inafanana na usufi wa kiyahudi, kwamba ni baadaye kabbalah iliingia katika dini hiyo, na kwamba mizizi yake halisi inaonekana katika Misri ya kale.

4.Misri ya kale ilitawaliwa kwa utaratibu wa kipagani wa Mafirauni na huko tukaikuta dhana inayojenga msingi wa falsafa ya kikafiri ya hivi leo;kwamba ulimwengu unajiendesha wenyewe na kwamba umetokea kwa bahati nasibu.Hii kwa hakika inatoa picha maridadi.Je ni bahati tu kwamba falsafa ya makasisi wa Misri ya kale bado  ipo,na kwamba bado kuna alama za mlolongo wa (kabbalah –matempla –frimansori) .?

 Je hawa mafyoso ambao wameweka kumbukumbu katika historia ya ulimwengu tokea karne ya 18 wakifanya mapinduzi wakiendeleza falsafa na mifumo ya siasa ni warithi wa wachawi wa Misri ya kale?

 Ili kujibu maswali haya vizuri hebu tuyachunguze kwa undani zaidi matukio ya kihistoria ambayo tumeyagusia kwa kifupi tu.

Habari ya ndani juu ya kabbalah

“Kutoka” ni jina la kitabu cha pili cha Taurati.  Kitabu hiki kinaelezeya jinsi wana wa Israel chini ya uongozi wa Mussa, walivyoondoka Misri kuepuka udhalimu wa Firauni.  Firauni aliwashurutisha wana wa Israel kuishi kama watumwa na hakukubali kuwaachia huru. Lakini pale alipokumbana na miujiza aliyoonesha Mwenyezi Mungu kupitia kwa Mussa na maangamizi aliyowapelekea watu wake Firauni alitulia.  Kwa hiyo usiku mmoja wana wa Israel wakakusanyika na kuanza safari yao kuhama Misri.  Baadaye Firauni akawashambulia waisrael lakini Mwenyezi Mungu akawanusuru kwa muujiza mwingine zaidi aliouonesha kupitia kwa Mussa.  Lakini katika Qur’an tunakuta maelezo sahihi zaidi ya kuhama kwao kutoka Misri, kwa sababu Taurati imehujumiwa baada ya kufunuliwa kwa Musa.  Ushahidi muhimu wa hili ni kuwa katika vitabu vitano vya Taurati- Kitabu cha mwanzo, kutoka, walawi, hesabu na kumbukumbu la Taurati- kuna migongano mingi.  Ukweli kuwa kitabu cha kumbukumbu la Taurati kimeishia na maelezo ya kufa na kuzikwa kwa Mussa ni ushahidi usiopingika kwamba sehemu iliyobaki itakuwa imeongezwa baada ya kifo cha Musa. Katika Qur’an, katika maelezo ya kuhama kwa wana wa Israel kutoka Misri kama ilivyo katika habari zote zinazohusiana na jambo hili, hakuna mgongano hata kidogo. Habari hii inaelezwa kwa usahihi kabisa.  Isitoshe kama zilivyo habari nyingine, Mwenyezi Mungu anafunua hikma na siri nyingi katika jambo linalozungumziwa.   Kwa sababu hii pale tunapoziendea habari hizi kwa undani, tunaweza kupata mafundisho mengi ndani yake. 

Ndama wa Dhahabu

Moja kati ya mambo muhimu kuhusiana na kuhama kwa wana wa Israel kutoka Misri, kama ilivyoelezwa katika Qur’an, ni kuwa waliasi dhidi ya dini iliyofunuliwa kwao na Mungu licha ya ukweli  kwamba Mwenyezi Mungu aliwanusuru na udhalimu wa Firauni kupitia kwa Musa.   Wana wa Israel hawakuweza kufahamu ile Tawhiid ambayo Musa aliwafikishia bali wao walizidi kuielekea Ibada ya Sanamu.  Qur’an inaulezea hivi muelekeo huu wa ajabu-  “Na tukawavusha wana wa Israel baharini (wakasalimika na balaa la Firauni) na wakawafikia watu waliokuwa wakiabudu masanamu yao. Wakasema Ewe Musa! Tufanyie waungu na sisi (yaani masanamu) kama wao walivyo na miungu.  Musa akasema hakika nyinyi ni watu mfanyao ujinga.  Hawa yaataangamia haya waliyonayo na ni bure waliyokuwa wakiyafanya. (7:138-139). 

   Licha ya maonyo ya Musa, wana wa israel waliendelea na upotevu huo, na Musa alipowaacha na kwenda mlima wa Sinai, upotevu wao ukadhihirika zaidi.  Wakitumia fursa ya kutokuwepo kwa Musa, mtu mmoja aliyeitwa Sammir akawajia.  Akawashawishi watengeneze sanamu la ndama na kisha waliabudie.

Musa akarudi kwa watu wake kwa ghadhabu na masikitiko.  Akasema Enyi watu wangu je Mola wenu hakukuahidini ahadi nzuri, je umekuwa mrefu kwenu muda wa ahadi hiyo (mnaona haitimizwi) au mumetaka ikushukieni ghadhabu kutoka kwa Mola wenu; na kwa hivyo mmevunja ahadi yangu?  Wakasema sisi hatukuvunja ahadi yako kwa khiyari yetu walakini tulibebeshwa mizigo ya watu; (vyombo vya dhahabu tulivyoviazima kwa wanawake wa kimisri).  Na namna hivi alitia Samir (sehemu yake).  Na akawatolea (akawaundia katika myayusho huo) ndama, kiwiliwili kamili kinacholia.  Na wakasema; huyu ndio Mungu wenu na Mungu wa Musa lakini Musa amesahau (amekwenda kumtafuata majabalini). (20:86-88).

Ibada ya masanamu ya Waisrael

Kwanini kulikuwa na ung’ang’anizi miongoni mwa wana wa Israel katika kukita na kuabudia masanamu? Nini hasa kilikuwa chanzo cha mwelekeo huu? Ni wazi jamii ambayo hapo kabla haikuwahi kuamini masanamu isingeweza kwa ghafla kufuata mwenendo huo wa kipumbavu kwa kutengeneza sanamu na kuanza kuliabudia.  Ni wale tu ambao ibada ya sanamu ilikuwa ya kawaida kwao ndio ambao wangeweza kuamini upuuzi huo.

Hata hivyo, wana Israel walikuwa watu ambao hapo kabla waliamini Mungu mmoja tokea zama za mzee wao Ibrahimu.  Jina hili “Waisrael” au “wana wa Israel” kwanza kabisa ilitolewa kwa watoto wa Yaqub, mjukuu wa Ibrahimu.  Baadaye jina hili likatumika kwa Mayahudi wote waliotokana naye.

  Waisrael walikuwa wameichunga Imani ya Mungu mmoja ambayo waliirithi kutoka kwa wazee wao; Ibrahimu, Is-haqa na Yaqub (a.s). Wakiwa  pamoja na Yusufu (a.s), walikwenda Misri na wakaichunga Imani yao ya Mungu mmoja kwa kipindi kirefu, licha ya ukweli kwamba waliishi pamoja na washirikina wa Kimisri.

Inabainika wazi katika maelezo yaliyotolewa katika Qur’an kuwa pale Mussa alipowajia, Waisrael walikuwa watu walioamini Mungu mmoja.  Isipokuwa tu ni kwamba pamoja na kuamini kwao Mungu mmoja, Waisrael waliathiriwa na Wapagani waliokuwa wakiishi nao pamoja na wakaanza kuwaiga wakibadili dini waliochaguliwa na Mwenyezi Mungu na kufuata Ibada ya Sanamu ya jamii nyingine.

   Tunapolichunguza swala hili kwa undani kwa kuzingatia kumbu kumbu za historia, tunaona kuwa dhehebu la kipagani lililowaathiri Waisrael lilikuwa lile la Misri ya kale.  Ushahidi muhimu wa kushadidia hitimisho hili ni kuwa yule ngamia wa dhahabu waliyemuabudia Waisrael wakati Mussa alipowenda mlima Sinai, alikuwa mfano wa masanamu ya Misri, Hatha na Aphis.  Katika kitabu chake Too Long in the Sun, muandishi wa Kikristo Richard Rives ameandika hivi;  

Hatha na Aphis Ng’ombe jike na fahari miungu ya Misri ilikuwa ikiwakilisha Ibada ya Jua.  Ibada yao ilikuwa ni muendelezo wa historia  ya utukuzo wa Jua.  Yule ndama wa dhahabu wa mlima Sinai alikuwa ushahidi tosha wa kuthibitisha kuwa karamu iliyotangazwa ilihusiana na ibada ya Jua.  Athari ya dini ya kipagani ya Misri ilionekana katika sura nyingi tofauti.  Mra baada ya kuwashinda wapagani imani yao ya kishirikina ikadhihirika kama aya inavyosema; Ewe Mussa! Tufanyie waungu na sisi (yaani masanamu) kama wao walivyo na miungu. (7:138).

 Na kumbukeni habari hii pia (mliposema, Ewe Mussa hatukuamini mpaka tumuone Mwenyezi Mungu waziwazi. (2:55).  Maneno yao haya yanadhihirisha kuwa wao walitaka kuabudia Mungu wa kimaada ambayo wangemuona kwa macho kama dini yao ya kipagani ilivyo wapatia wamisri  mungu kama huyo.

  Muelekeo huu wa Waisrael  kufuata upagani wa Misri ya kale ambao tumeuelezea, ni muhimu ueleweke kwani ndio unaotupa ufahamu wa jinsi kilivyohujumiwa kitabu cha Torati na unatufahamisha chanzo cha Kabbalah.  Tukiyatafakari mafundisho haya kwa mazingatio, tutaona kuwa ni katika vyanzo hivi unapokutikana upagani wa Misri ya kale na falsafa ya kilahidi.

Kutoka Misri ya kale hadi Kabbalah

Wakati Mussa angali hai, waisrael walianza kutengeneza masanamu kama yale yale waliyoyaona Misri na kuyaabudia.  Baada ya Mussa kutawafu (kufariki Duniya), hakukuwa na kizuizi cha kuzuia Imani potofu.  Bila shaka haiwezi kusemwa kwamba ni Mayahudi wote waliokengeuka lakini baadhi yao walifuata upagani wa Misri.     Kwa kweli walishikilia mafundisho ya ukasisi wa Misri (wachawi wa Firauni) ambayo yalijengwa kwa msingi wa imani za jamii hiyo, na wakaihujumu Imani yao kwa kutumbukiza mafundisho haya ndani yake.   Itikadi mabayo ilitumbukizwa katika Uyahudi kutoka Misri ya kale ilikuwa ni Kabbalah.  Kama ulivyokuwa mfumo wa makasisi wa Misri, Kabbalah nao ulikuwa mfumo wa siri, na msingi wake ulikuwa utamaduni wa  uchawi.   Kabbalah inatoa maelezo ya maumbile tofauti kabisa na yale yaliyokutwa katika Torati.  Ni maelezo ya kilahidi yaliyoegamia dhana ya Misri ya kale juu ya uhai wa milele wa maada.  Murat Ozgen mwana frimansori wa Kituruki ana haya ya kusema juu ya swala hili;

Ni dhahiri kuwa Kabbalah iliundwa miaka mingi kabala ya Taurati haijaja.  Sehemu zaidi ya Kabbalah ni nadharia juu ya muundo wa ulimwengu.  Nadharia hii iko tofauti kabisa na maelezo juu ya maumbile yaliyopokewa na dini zinazoamini Mungu.  Kwa mujibu wa Kabbalah, mwanzoni kabisa mwa hatua ya kuumbwa kwa ulimwengu, vitu vinavyoitwa Sefiroth maana yake ni duara au mihimili ikiwa na sifa za kiroho na kimaada iliibuka. Idadi ya jumla ya vitu hivi ilikuwa 32.

 Ile kumi ya mwanzo ndiyo iliyoshikilia  Solar System na mingine iliyobaki imeshikilia makundi ya nyota angani.  Imani hii ya kipekee ya Kabbalah inabainisha kuwa inahusiana kwa karibu na mifumo ya Imani ya unajimu.  Kwahiyo Kabbalah inatenganishwa mbali kabisa na dini ya uyahudi na inanasibishwa kwa karibu zaidi na dini za kale za  siri za mashariki.    Kwa kufuata mafundisho ya siri na ya ulahidi ya Misri ya kale ambayo yalijengwa kwa msingi wa uchawi, Mayahudi wakapuuza mambo yaliyoharamishwa katika Taurati.  Wakashikilia Ibada za kichawi za wapagani na hivyo Kabballah ikawa itikadi ndani ya uyahudi lakini ikienda kinyume na Taurati.  Katika kitabu chake kiitwacho Secrety Societies and Subversive Movements, mwaandishi wa Kingereza Nesta H Webster anasema;

Uchawi kama tuujuavyo ulikuwa ukifanywa na Wakanan kabla ya kuvamiwa kwa Parestina na waisrael.  Misri, India na ugiriki nazo zilikuwa na wachawi wao na Miungu yao.  Licha ya makemeo dhidi ya uchawi yaliyomo katika sheria ya Musa, Mayahudi wakipuuzilia mbali makemeo haya  walijiingiza na kuuchanganya utamaduni mtukufu waliorithi na mawazo ya kichawi yaliyotokea katika jamii nyingine.

Wakati huo huo kwa upande wa Kabbalah ya Uyahudi iliyochukuliwa kutoka katika Falsafa ya Persian Magi na ya Neo Platonists, na ya Neo Pythagoreans hapo ndipo penye maelezo kuwa tunachokijua sisi hivi leo kuhusu Kabbalah hakitokani kabisa na uyahudi.  Kuna aya katika qur’an inayozungumzia jambo hili.  Mwenyezi Mungu anasema  kuwa Waisrael walijifunza tamaduni za kichawi za kishetwani kutoka nje ya dini yao;  Wakafuata yale waliofuata Mashetwan, (wakadai kuwa yalikuwa) katika Ufalme wa Suleiman; na Suleiman hakukufuru, bali Mashetwani ndio waliokufuru, wakiwafundisha watu uchawi (waliokuwa wakiujua wenyewe tangu zamani), na (uchawi) ulioteremshwa kwa malaika wawili, Haruta na Maruta katika (mji wa) Babil.  Wala (Malaika hao) hawakumfundisha yeyote  mpaka wamwambie; hakika sisi ni mtihani (wa kutazamwa kutii kwenu); basi usikufuru.

Wakajifunza kwao ambayo kwa mambo hayo waliweza kumfarakanisha mtu na mkewe (na mengineyo).  Wala hawakuwa wenye kumdhuru yeyote kwa hayo ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.  Na wanajifunza ambayo yatawadhuru wala hayata wafaa.  Na kwa yakini wanajua kwamba aliyekhiyari haya hatakuwa na sehemu yoyote katika Akhera.  Na bila shaka ni kibaya kabisa walichouzia nafsi zao laiti wangelijua. (2:102).

    Aya hii inabainisha kuwa japo Wayahudi fulani walijuwa kuwa watapata khasara katika maisha ya Akhera lakini bado walijifunza na kufuata tamamduni za uchawi.  Hivyo walikengeuka na kutoka katika sheria ambayo Mungu aliwashushia, wakiwa wameuza nafsi zao wenyewe na kutumbukia katika upagani (itikadi za kichawi).  Ni kibaya walichojiuzia nafsi zao kwa maneno mengine maana yake waliacha imani yao.   Mambo yaliyozungumziwa katika aya hii yanaonesha vipengele vikuu vya mfarakano katika historia ya Uyahudi.  Mapambano yalikuwa kati ya mitume ambao Mwenyezi Mungu aliwashusha kwa mayahudi pamoja na mayahudi walioamini na kuwatii kwa upande mmoja dhidi ya wale mayahudi waliopotoka na kuasi amri za Mungu na kuiga tamaduni za kipagani wa watu walioishi nao ambao walifuata ada za utamaduni wao badala ya sheria ya Mungu.

Waliokuwa Matempla  ndio hao  wakaja kuwa Mafrimansori

Katika nadhariya ya mafundisho ya kabala, sio tu kulikuwa na utitiri wa miungu bali hata ule upweke wa mwanzo wa mungu usiojulikana na wenye maelezo tata juu ya asili yake pia una pande mbili; upande wa kiume na wa kike yaani ubaba na umama. Hokhmah na Binah ndizo zilizokuwa sehemu mbili za mungu. Wanakabala walitumia wazi wazi tamathali za kijinsia kuelezea maingiliano ya kimaumbile kati ya Hokmah na Binah yaliyozalisha maumbile mengine zaidi.  Jambo jingine la kuchekesha katika theolojia hii ya kishirikina ni kuwa, kwa mujibu wa theolojia hii binadamu hawakuumbwa bali kwa kiasi fulani na wao wana asili ya kiungu.  Bwana owens, mtafiti wa kiamerika anaielezea hivi dhana hii;

Picha ya ajabu ya Mungu iliyobuniwa na kabala ina sura ya upweke na wingi.  Kwa  dhana hii ya kabala Mungu alikuwa Adamu kadmon: yaani binadamu mkubwa wa kwanza.  Mtu alikuwa sawa na Mungu katika ile sifa ya asili ya kutoumbwa na katika lile umbile la kutatanisha. Dhana hii ya ajabu inayomuelezea Adamu kama mungu ilishadidiwa na mafundisho ya kabala: thamani ya tarakimu ya majina Adamu na Yehova katika kiebrahania ni 45 kila moja.  Kwa hiyo katika mafunzo ya kabbala Yehova na Adam walikuwa sawa, hivyo Adam alikuwa mungu.  Kwa dai hili binadamu wote wanapofikia daraja la juu kabisa huwa sawa na Mungu

 Theolojia hii inayojumuisha dhana ya Upagani ndiyo iliyojenga msingi uliopotosha dini ya Uyahudi.  Wanakabbala wa kiyahudi wakakiuka mipaka  ya akili ya kawaida ya binadamu kiasi kwamba wakafika mahala pa kuthubutu kuwafanya binadamu miungu.  Mbali na hivyo, kwa mujibu wa theolojia hii, sio tu binadamu walikuwa miungu bali miungu wenyewe walikuwa Wayahudi peke yao; Watu wa jamii nyingine walihesabiwa kama binadamu tu wa kawaida.

Matokeo yake ndani ya dini ya uyahudi ambayo kimsingi ilianzishwa kwa ajili ya kumtumikia na kumtii mungu, itikadi hii potofu ilianza kumea,  lengo lake likiwa kutimiza ujinga wa wayahudi.  Licha ya kupingana kwake na Taurati ,  kabbala ikaingizwa katika uyahudi na hatimaye ikaanza kuihujumu Taurati.  Jambo jingine la kuzingatia kuhusiana na mafundisho potofu ya kabbala ni ule uwiano  wa fikira baina yake na Upagani wa misri ya zamani.  Kama tulivyosema awali, wamisri wa zamani waliamini kuwa maada ilikuwa na uhai;  kwa maneno mengine walikanusha kuwa maada iliumbwa pasipo kitu chochote. Kabbala nayo inadai hivyo hivyo kuhusiana na binadamu.  Inadai kuwa binadamu hawakuumbwa na kwamba wanajiendeshea wenyewe maisha yao. Kulizungumza hili kwa maneno ya sasa ni kuwa wamisri wa kale walikuwa walahidi na kimsingi itikadi ya kabbala yaweza kuitwa secular humanism.  Ni muhimu kukumbuka kuwa dhana hizi mbili ulahidi  na secular humanism ndizo zilizotoa itikadi ambayo imetawala Duniyani kwa zaidi ya karne mbili zilizopita. Yafaa kuuliza iwapo kuna watu ambao wameziendeleza  itikadi za misri za kale na kabbala tangia katikati ya kipindi cha nyuma cha historia hadi leo hii.

Wakati tulipowazungumzia Matempla huko nyuma,  tulisema kuwa kundi hili maksusi la makuruseda liliathiriwa na “siri” waliyoikuta Jerusalem,  kutokana na siri hiyo wakaachana  na  Ukirsto na wakaanza kufuata mafundisho ya  kichawi.  Tukasema kuwa watafiti wengi waliishia kutoa maoni yao kuwa siri hii ilihusiana na kabbala.  Kwa mfano katika kitabu chake,  Histoire de la Magie (Historia ya uchawi ) mwandishi wa kifaransa, Eliphas Le’vi, anatoa ushahidi wa kina kuwa Matempla walijingiza katika itikadi ya siri ya kabbala,  kwamba walifundishwa itikadi hiyo kwa siri.  Ndio kusema itikadi hii pamoja na mizizi yake ya misri ya kale ilipandikizwa kwa Matempla kupitia kabbala. Katika kitabu chake Foucault’s Pendulum,  mwanafasihi mashuhuri wa Italia, Umberto Eco, naye anausimulia ukweli huu.  Katika riwaya yake nzima anasimulia kupitia  vinywa vya  wahusika wakuu wa riwaya yake kuwa Matempla waliathiriwa na kabbala na kwamba wale makabbala walikuwa na siri ambayo chanzo chake chaweza kuwa  Mafirauni wa misri ya kale. Kwa mujibu wa Eco, baadhi ya mayahudi mashuhuri walijifunza siri fulani zilizo toka kwa wamisri wa zamani na baadaye wakazipenyeza katika vitabu vitano vya kwanza vya Agano la kale.  Lakini siri hii ambayo ilisambazwa kwa siri ilikuwa ikifahamika kwa wana kabbala peke yao.  (zohari, iliyoandikwa Hispania na kuunda kitabu cha msingi cha kabbala inazungumzia siri za vitabu hivi vitano. Baada ya kueleza kuwa Wanakabbala waliisoma siri hii ya Misri ya kale katika vipi hekalu la Suleiman ,  Eco pia anaandika kuwa Matempla nao wakaisoma siri hii kutoka kwa walimu wa kabbala mjini Jerusalem. Siri hii ilikuwa ikijulikana na kikundi kidogo sana cha walimu wa kiyahudi waliobakia Palestina matempla wakaisoma kutoka kwa walimu hao.  Pale matempla walipofuata itikadi mchanganyiko ya wamisri  na wakabbala ndipo walipofarakana na dhehebu la kikiristo lililokuwa likitawala Ulaya. Ulikuwa ni mfarakano ambapo wao walishirikiana na nguvu nyingine kubwa ya mayahudi. Baada ya matempla kutiwa mbaroni kwa amri ya pamoja ya Mfalme wa Ufaransa na Papa mnamo mwaka 1307 ,  kundi hili likatokomea chini chini lakini athari zake  zikabakia, Tena zikawa hatari zaidi na zenye uelekeo madhubuti.

Kama tulivyosema awali idadi ndogo ya Mtempla ilinusurika katika kamata kamata na kukimbilia kwa Mfalme wa Scotland, utawala pekee wa kifalme wa Ulaya ambao haukuyakubali Mamlaka ya Papa.  Kule Scotland wakajipenyeza katika jumuiya ya Wall-builders na wakaitwaa.  Jumuiya zikafuata utamaduni wa Matempla na hivyo mbegu ya frimansori ikapandwa Scotland. Hadi leo hii kanuni kuu ya Frimansori ni ule utaratibu wa kale wa maombi wa Scotland. Kama ilvyofafanuliwa kwa kina katika kitabu kiitwacho The New Masonic Order, kuanzia karne ya kumi na nne ndipo yanapoonekana masalia ya Matempla na Mayahudi kadhaa walioshirikiana nao katika vipindi mbalimbali vya Historia ya Ulaya.  Bila kutoa maelezo ya kina zifuatazo ni nukta muhimu za utafiti:

-Katika Mji wa Province nchini Ufaransa kulikuwa na kambi ya Matempla waliokimbilia nchini humo. Wakati wa ile kamatakamata Matempla wengi sana walijificha huko.  Kielezeo kingine cha eneo hilo ni kuwa hilo ndilo lililokuwa kituo mashuhuri cha Ukabbala barani Ulaya.  Province ndipo mahala ambapo fasihi simulizi ya Kabbala ilandikwa katika kitabu.

- Kwa mujibu wa wanahistoria,uasi wa Wakulima nchini Uingereza mwaka 1381 ulichochewa na Jumuiya fulani ya siri.  Watafiti wanaoitafiti Historia ya Frimansori wanakubaliana kuwa Jumuiya hii ya siri ilikuwa ya Matempla.  Ule uasi haukuwa tu wa kiraia bali pia ulikusudiwa kulishambulia Kanisa Katoliki.-Nusu karne baada ya uasi huu, kasisi mmoja wa Bohemia, John Huss akaanzisha vurugu kulipinga Kanisa Katoliki.  Kama kawaida nyuma ya vurugu hizi walikuwepo Matempla.  Isitoshe Huss mwenyewe alikuwa akiipenda sana Kabbala.  Yeye alikuwa akimpenda sana Avigdor Ben Isaac Kara. Mtu huyu alikuwa Mwalimu mashuhuri wa Kiyahudi katika jamii ya kiyahudi katika mji wa Prague na pia alikuwa Mwanakabbala.

Vielelezo kama hivi vinaonesha kuwa ushirikiano kati ya Matempla na Wanakabbala ulilenga kubadilisha mfumo wa jamii ya Ulaya.  Mabadiliko haya yalijumuisha misingi ya utamaduni wa Kikristo ambao ndiyo utamaduni-mama wa Ulaya na badala ya utamaduni huu uwekwe utamaduni uliojengwa kwa msingi wa mafundisho ya kipagani, kama vile Kabbala na baada ya mabadiliko haya, yafuate mabadiliko ya kisiasa.  Mifano ni mapinduzi ya Ufaransa na Italia.

Huko mbele tutaona vipindi vya mabadiliko ya Historia ya Ulaya.  Katika kila kipindi tutakutana na ukweli kuwa kulikuwa na nguvu iliyotaka kuitenganisha Ulaya na mafundisho ya Kanisa na badala yake iweke itikadi ya Kisekula na hivyo izisambaratishe taasisi zote za dini.  Nguvu hii ilijaribu kuichagiza Ulaya kuikubali itkadi iliyorithiwa kutoka Misri ya kale kupitia Kabbala.  Tulikwishaeleza huko nyuma kuwa msingi wa itikadi hii ni dhana hizi mbili; Humanism na Materialism (Utumtu na Ulahidi).

Mafundisho ya kipagani yalivyoongezwa katika Taurat

Ni muhimu kukumbuka kuwa maovu ya Wayahudi wapotevu, yameandikwa katika kitabu kitakatifu cha Mayahudi-Agano la Kale.  katika kitabu cha Nehemia ambacho ni kitabu cha historia kilichomo katika Agano la Kale, Wayahudi wanakili dhambi zao na kutubu. Waliokuwa wazawa wa Israel wakajitenga na wageni wote, wakasimama, wakaziungama dhambi zao, na maovu ya Baba zao.  Basi wakasimama mahali pao, wakasoma katika kitabu cha Torati ya Bwana, Mungu wao, muda wa robo ya siku; na robo nyingine wakaungama, wakamuabudu Bwana, Mungu wao.  Ndipo wakasimama madarajani pa Walawi, Yeshua, na Bani, na Kadimieri, na Shebania, na Bani, na Sherebia, na Bani, na Kenani, wakamlilia Bwana, Mungu wao kwa sauti kuu.

(Wakasema;) Walakini (Baba zetu) hawakutii, wakakuasi, wakaitupa sheria yako nyuma yao, wakawaua Manabii wako walioshuhudia juu yao wapate kuwarejeza kwako; wakatenda machukizo makuu.  Kwasababu hiyo ukawatia katika mikono ya adui zao, waliowasumbua; na wakati wa shida yao, walipokulilia, uliwasikia kutoka mbinguni; na kwa wingi wa rehma zako ukawapa waokozi walio waokoa katika mikono ya adui zao.  Lakini walipokuwa wamekwisha kustarehe, walitenda mabaya tena mbele zako; kwahiyo ukawaacha katika mikono ya adui zao, nao wakawatawala; hata hivyo waliporejea na kukulia, uliwasikia toka mbinguni, ukawaokoa mara nyingi kwa rehma zako; ukawashuhudia ili uwarudishe tena katika sheria yako; lakini walitakabari, wasisikilize amri zako, bali waka zikhalifu hukumu zako, (ambazo mtu akizitenda ataishi katika hizo) nao wakayaondowa mabega yao, wakafanya shingo zao kuwa ngumu, wasitake kusikiliza.  Ila kwa rehema zako nyingi hukuwakomesha kabisa wala kuwaacha; kwa maana wewe u Mungu mwenye neema, Mwenye rehema.  Basi sasa, Ee Mungu, Mkuu, mwenye uweza, Mungu wa kuogofya mwenye kushika maagano na rehema, mashaka yote yaliyotupata sisi, wafalme wetu, na wakuu wetu, na makuhani wetu, na manabii wetu, na Baba zetu, na watu wako wote, tangu zamani za wafalme wa Ashuru hata leo, na yasihesabiwe kuwa ni madogo.  Lakini wewe u mwenye haki, katika hayo yote yaliyotupata; maana wewe umetenda yaliyo kweli lakini sisi tumetenda yaliyo mabaya; na wafalme wetu, na wakuu wetu, na makuhani wetu, na Baba zetu, hawakushika sheria yako wala hawakusikiliza amri zako na shuhuda zako ulizo washuhudia.  Kwa kuwa hawakukutumikia wewe katika ufalme wao, na katika wema wako mkuu uliowapa, na katika nchi ile kubwa yenye neema uliowapa mbele yao, wala hawakughaili na kuacha mabaya yao.  (Nehemia 9, 2-4, 26-29-31-35).

Kifungu hiki kinaelezea tamaa ya kurejea katika Imani ya Mungu mmoja ambayo Wayahudi wengi walikuwa nayo, isipokuwa katika kipindi cha historia ya Wayahudi kundi moja lilimeguka na kupata nguvu kidogo kidogo, na likaja kuwatawala wayahudi na baadaye likaegeuza kabisa dini yenyewe.  Kwasababu hii katika Torati na katika vitabu vingine vya agano la kale kuna masalia yanayotoka katika mafundisho ya Kipagani, na pia kama yaliyotajwa hapo juu yanawasukuma kurejea katika dini sahihi.  Mathalani;

- Katika kitabu cha mwanzo cha Taurati, inasemwa kuwa Mungu aliumba ulimwengu mzima kwa siku sita kutokana na hamna.  Hii ni sahihi na inatokana na ufunuo sahihi.  Lakini, hapo hapo inasema kuwa Mungu alipumzika siku ya saba, huu ni uzushi kabisa.  Ni dhana potofu iliyotoka katika upagani ambao unampachika Mungu sifa za kibinadamu.  Katika aya hii ya Qur’an, Mwenyezi Mungu anasema;

Na Tumeziumba Mbingu na Ardhi na vilivyomo kati yao katika nyakati sita, wala hayakutugusa machovu (50:38).

Katika sura nyingine za Taurati kuna staili ya uandishi ambayo ni ya utovu wa heshima kwa Mungu, hasa hasa katika zile sehemu ambazo sifa za kibinadamu anapewa Mungu.  Imani hizi potofu za kulinganisha udhaifu wa kibinadamu ndizo imani ambazo wapagani walikuwa nazo kwa miungu yao bandia. Maneno mengine ya kufuru ni yale yanayodai kuwa Yakobo, Baba wa Waisrael alipigana myeleka na Mungu, na akashinda.  Ni wazi kabisa hiki ni kisa cha kutungwa ili kuwatukuza Waisrael, ni mwigo kutoka katika jamii za wapagani.  Katika Agano la kale kuna mtindo wa kumuelezea Mungu kama Mungu wa utaifa – yaani Mungu wa Waisrael peke yao.  Lakini Mungu ni Mola wa Ulimwengu na viumbe vyote.  Dhana hii ya dini ya utaifa, katika Agano la kale inafanana na dhana za kipagani ambapo kila kabila linaabudia Mungu wake.

-Katika baadhi ya vitabu vya agano la kale (mfano, Yeshua)  amri zinatolewa kufanya maovu dhidi ya watu wasiokuwa wayahudi.  Mauaji ya halaiki yanaamrishwa bila kujali wanawake, watoto wala wazee.  Mwenendo huu wa kinyama uko kinyume kabisa na sheria ya haki ya Mungu, bali badala yake unarandana na ushenzi wa tamaduni za kipagani za kuabudia Mungu bandia wa vita.

Mawazo haya ya kipagani ambayo yametumbukizwa katika Taurati yumkini yana chanzo chake.  Lazima kuna mayahudi ambao walifuata mila isiyokuwemo katika Taurati.   Wakaishika na kuitukaza mila hiyo.  Baadaye wakatumbukiza katika Taurati mawazo yaliyotoka katika mila hii ambayo wao waliyaunga mkono.  Chimbuko la mila hii linaanzia nyuma kabisa kwa makuhani wa Misri (Wachawi katika utawala wa Firauni ).

Kwa kweli ni Kabbala iliyorithiwa na wayahudi wengi.  Kabbala ilikuwa na sura ambayo iliziwezesha itikadi za Wamisri na Wapagani kujipenyeza katika dini ya uyahudi na kustawi ndani yake.  Wahusika wa Kabbala  hapana shaka wanadai kuwa Kabbala inafafanua tu kwa kina siri zilizofichikana kabisa katika Taurati, lakini , kwa kweli kama asemavyo mwanahistoria wa kiyahudi aliyezungumzia Kabbala kuwa Kabbala ni sumu isiyotambulika ambayo imeingiya katika dini ya uyahudi na kuiathiri kabisa. Hapo sasa inawezekana kukuta ndani ya Kabbala masalia ya itakdi ya Ulahidi ya Wamisri wa zama za kale.  

Kabbala – Itikadi inayopingana na dhana ya kuumbwa kwa ulimwengu.

Katika Qur’an , Mwenyezi Mungu anabainisha kuwa Taurati ni kitabu cha Mungu ambacho kilishushwa kama muongozo kwa Wanadamu,

Hakika tuliteremsha Taurati yenye uongozi na nuru;  ambayo kwayo Manabii waliojisalimisha  (kwa Mwenyezi Mungu waliwahukumu Mayahudi, na Watawa na Maulamaa pia (walihukumu kwa hiyo Taurati), kwasababu walitakiwa kuhifadhi kitabu (hicho) cha Mwenyezi Mungu; nao walikuwa mashahidi juu yake.  (5:44).

 Kwahiyo, Taurati, kama ilivyo Qur’an, ni kitabu chenye elimu na amri zinazohusiana na Tawhiid yanayoelezya kuwepo kwa Mwenyezi Mungu na upweke wake, sifa zake, kuumbwa kwa wanadamu na viumbe wengine, lengo la kuumbwa kwa binadamu, na sheria za maadili za Mwenyezi Mungu kwa wanadamu.  Hata hivyo ile Taurati ya asili haipo tena hivi leo.  Tuliyonayo hivi leo ni Taurati iliyoandikwa upya na kuhujumiwa na mikono ya binadamu.  Kuna nukta muhimu kuwa ile Taurati ya asili na Qur’an zinashabihiana, Mwenyezi Mungu anatambuliwa kama muumba.  Anatambuliwa kama aliyetakasika na aliyeepukana na mapungufu yote na amekuwepo bila mwanzo.  Chochote minghairi yake ni kiumbe chake.  Yeye ndiye aliyeumba ulimwengu wote, maumbile ya angani, maada isiyo na uhai, binadamu na viumbe vyote hai.  Mungu ni mmoja tu. Wakati huu ukiwa ndio ukweli halisi, kuna maelezo tofauti kabisa yanayokutikana katika Kabbala, ambayo ni sumu iliyopenya katika mishipa ya uiyahudi na kuuathiri kabisa.  Mafundisho yake juu ya Mungu yanapingana kabisa na ule ukweli halisi juu ya maumbile unaokutikana katika ile Taurati ya asili na katika Qur’an. 

Katika moja ya maandiko yake juu ya Kabbala, mtafiti mmoja wa Amerika, Lance S. Owens anatoa fikra yake juu ya vyanzo vya itikadi hii ambapo imani ya Kabbala imesababisha dhana kadhaa kuhusu Mungu, nyingi miongoni mwa hizo zimetoka kabisa katika mtazamo wa dini.  Msingi mkuu wa imani ya Waisrael ulikuwa ni kalima kuwa Mungu wetu ni mmoja.  Lakini Kabbala ikadai kuwa wakati Mungu akiishi katika umbile la peke yake ambalo katika Kabbala linaitwa Ein Sof asiye na udhaifu – upweke huu usiojulikana lazima utakuwa umeanzia katika maumbile mengi ya kiungu.  Yaani kundi la Miungu. Miungu hii ambayo mwana Kabbala aliita Sefiroth yaani sura au nyuso za Miungu.  Njia ambayo Mungu alitokea katika umoja usioeleweka na kuingia katika wingi ilikuwa ni siri ambayo wana Kabbala walihangaika kuitafuta.  Ni dhahiri hii sura ya Miungu mingi  inakubaliana na madai ya washirikina.  Siyo tu Mungu alikuwa katika wingi katika itikadi ya Kikabbala bali hata kule kutokea kwake mwanzoni katika upweke usiojulikana kulichukuwa sura mbili ya kiume na ya kike, Baba na Mama, Hokhmah na Binah hizi ndizo sura za mwanzo za Mungu.  Wafuasi wa Kabbala walikuwa wakitumia tamathali za kijinsia kuelezea jinsi maingiliano ya kijinsia ya Hokhmah na Binah yalivyozaa  maumbile mengine.

 
   
    
3 / total 6
You can read Harun Yahya's book Ulimwengu Wa Frimasonri online, share it on social networks such as Facebook and Twitter, download it to your computer, use it in your homework and theses, and publish, copy or reproduce it on your own web sites or blogs without paying any copyright fee, so long as you acknowledge this site as the reference.
About this site | Tengeneza kurasa yako ya nyumbani | Add to favorites | RSS Feed
Mambo yote yanaweza kuynakiliwa, kuchapwa na kusambazwa kwa kurejea katika kurasa hii
(c) All publication rights of the personal photos of Mr. Adnan Oktar that are present in our website and in all other Harun Yahya works belong to Global Publication Ltd. Co. They cannot be used or published without prior consent even if used partially.
© 1994 Harun Yahya.www.harunyahya.com
page_top