Ulimwengu Wa Frimasonri

SHUSHA KITABU

Download (DOC)
Maoni

SURA ZA KITABU

< <
4 / total: 6
Frimasonri - Harun Yahya
Frimasonri
   

 


Dhana ya ‘humanism’

Yasadikiwa na wengi kuwa Humanism ndio itikadi madhubuti.  Inampandikiza mtu hisia za upendo, utulivu na Udugu.  Lakini kifalsafa dhana hii ina maana kubwa zaidi. Humanism ni utaratibu wa fikra ambao unaichukulia dhana ya ubinadamu kama ndio msingi na lengo lake kuu.  Kwa maneno mengine inawataka watu wajitenge mbali na Mungu, Muumba wao na washughulike na maisha yao na utu wao. Kamusi ya Kiingereza iitwayo Common dictionary inaliainisha neno humanism kama ni mfumo wa itikadi uliojengwa juu ya msingi wa maadili, sifa na tabia ambazo zinaaminika kuwa bora  zaidi kwa vigezo vya binadamu wenyewe bila kutegemea muongozo wowote wa Kiungu.

 Ainisho la wazi zaidi la humanism limetolewa na wale wanaounga mkono itikadi hii.  Mmoja kati ya wapiga debe wakuu wa dhana ya humanism ni bwana Corliss Lamont. Katika kitabu chake kiitwacho The philosophy of Humanism, mwandishi huyu ameandika hivi:  Kwa ujumla Humanism inaamini kuwa maumbile yanatokana na mkusanyiko wa vitu halisi ambavyo msingi wake ni nguvu ya maada.  Maada ndio msingi wa Ulimwengu na kwamba nguvu za Kiungu hazipo. Dhana  ya nguvu za Kiungu, kwa upeo wa binadamu, haina uthibisho. Kwamba watu hawana roho za kudumu milele yaani zisizo kufa na  ulimwengu kwa ujumla hauna Mungu aliyeuumba wala Mungu wa milele.

Kama tunavyojionea wenyewe katika nukuu hizo, itikadi ya humanism karibu inafanana kabisa na Itikadi ya atheism, na ukweli huu unakubaliwa bila ubishi na wanahumanisti.  Kulikuwa na ilani mbili muhimu zilizochapishwa na wanahumanisti katika karne iliyopita. Ilani ya kwanza ilichapishwa mwaka 1933, na ikapitishwa na watu muhimu wa wakati huo. Miaka arobaini baadaye, mnamo mwaka 1973, ilani ya pili  ya wanahumanisti ilichapishwa. Ilani hii iliithibitisha ile ya kwanza lakini ikatiwa nyongeza kufuatia hatua fulani za maendeleo ambazo zilipigwa wakati huo.  Maelfu ya wanafikra, Wanasayansi, Waandishi na Wanahabari walisaini ilani ya pili ambayo inaungwa mkono na chama cha harakati za wana humanisti wa Amerika.

Tunapoziangalia ilani hizi, tunakuta kuwa katika kila ilani kuna huu  msingi mmoja mkuu, ambao ni  Dhana ya atheism ambayo inasema ulimwengu na wanadamu hawakuumbwa  bali wanaishi kwa kujiendesha wenyewe, kwamba binadamu hawawajibiki kwa mamlaka yoyote isipokuwa kwao wenyewe, na kwamba Imani juu ya Mungu imedumaza maendeleo ya watu na jamii.  Kwa mfano vipengele sita vya kwanza vya ilani ya kwanza vya wanahumanist ni hivi vifuatavyo:

Mosi:Wanahumanist wanaitakidi kuwa ulimwengu unajiendeshea wenyewe maisha yake na haukuumbwa.

Pili: Dhana ya humanism ina itakidi kuwa Mtu ni sehemu ya maumbile na kwamba ameibuka kutokana na mfumo unaojiendesha wenyewe.

 Tatu: wakishikilia mtazamo wa maisha wakioganiki, Wanahumanisti wanaona kuwa dhana ya pande mbili za nafsi na mwili lazima ipingwe kabisa.

Nne:Itikadi ya humanism inatambua kuwa utamaduni wa kidini wa mtu na ustaarabu wake kama ulivyoelezwa na historia ni zao la hatua za polepole za maendeleo zitokanazo na mahusiano baina yake na mazingira yake  na urathi wa jamii yake. Mtu anayezaliwa katika utamaduni fulani kwa kiasi kikubwa anajengeka kwa utamaduni huo.

Tano: Dhana ya humanism inatangaza kuwa maumbile ya ulimwengu yalioelezwa na sayansi ya leo yanatupilia mbali nguvu yoyote ya mbinguni kuhusiana na maadili ya binadamu.

Sita:  Tunaamini kuwa dhana za theism, deism, modernism na aina kadhaa za itikadi mpya zimepitwa na wakati. 

Katika vipengele hivyo tunaiona wazi nafasi ya falsafa ya common ambayo inajidhihirisha yenyewe kwa majina ya materialism, Darwinism, atheism na agnosticism.  Katika kipengele cha kwanza dhana ya ulahidi ya uhai wa milele wa ulimwengu imewekwa wazi. 

Kipengele cha pili kinasema kuwa binadamu hawakuumbwa, hivi ndivyo inavyosema nadharia ya evolusheni.  Kipengele cha tatu kinakanusha kuwepo kwa roho kikidai kuwa viumbe wanatokana na maada.  Kipengele cha nne kinapendekeza mageuzi ya kiutamaduni na kinakanusha kuwepo kwa silika aliyopewa bindamu (Silika maalum ya binadamu katika maumbile).

Kipengele cha tano kinakanusha mamlaka ya Mungu juu ya ulimwengu na walimwengu na kipengele cha sita kinakataa Imani juu ya Mungu. Itakumbukwa kuwa madai haya ndiyo  yale yale ya zile duru zenye chuki na dini sahihi.  Sababu ni kuwa dhana ya humanism ndio msingi mkuu wa hisia zote zinazopinga dini.  Hii ni kwa sababu dhana hii inasema kuwa mtu ataachwa hivyo hivyo bila kuhesabiwa. katika historia yote. Huu ndio umekuwa msingi wa madai ya kumkanusha Mungu.  Katika aya moja ya Qur’an Mwenyezi Mungu anasema: 

Je! Anafikiri binadamu kuwa ataachwa bure, (asipewe amri za Mwenyezi Mungu wala makatazo yake)? Je! Hakuwa tone la manii lililotonwa?  Kisha akawa kidonge cha damu, kisha akamuumba na akamsawazisha (kuwa mwanadamu kamili)? Kisha akamfanya namna mbili, Mwanaume na Mwanamke. Je ! Hakuwa huyo ni muweza wa kuhuisha wafu?  

Mwenyezi Mungu anasema watu hawakuachwa tu hivi hivi na anawakumbusha kuwa wao ni viumbe vyake.  Hii ni kwa sababu pale mtu anapotanabahi kuwa yeye ni kiumbe wa Mungu, basi aelewe kuwa haishi bila ya kuangaliwa bali anawajibika kwa Mwenyezi Mungu.

Kwa sababu hii, dai kuwa binadamu hawakuumbwa ndio limekuwa msingi wa falsafa ya humanism  Vipengele viwili vya ilani ya kwanza ya wanahumanisti vinatoa maelezo ya itikadi hii.  Isitoshe wana humanisti  wanashikilia kuwa Sayansi inaunga mkono madai haya. Lakini ni waongo.  Tokeya ilani ya kwanza ya wanahumanisti ilipochapishwa Premesia mbili ambazo wanahumanisti wameziainisha kama hakika za kisayansi, kwamba ile dhana kuwa ulimwengu ni wa milele pamoja na nadharia ya evolusheni zote zimesambaratika.

1. Dhana kuwa Ulimwengu ni wa milele ilivunjiliwa mbali na mlolongo wa vumbuzi za angani zilizofanywa pale ilani ya kwanza ya wanahumanisti ilipokuwa inaandikwa..  Vumbuzi kama vile ulimwengu kutanuka, chanzo cha mionzi ya angani na mahesabu ya uwiano ya Haidrogen hadi helium, zimeonyesha kuwa ulimwengu ulikuwa na chanzo chake na kwamba uliibuka kutokana na hamna  takribani miaka bilioni 15-17 iliyopita kwa mlipuko mkubwa ulioitwa  Big Bang.

Ingawaje wale wanaounga mkono falsafa  ya kihumanisti na kilahidi walikataa kukubali nadharia ya Big Bang lakini hatimaye walishindwa kabisa.  Kutokana na  ushahidi wa kisayansi ambao umejitokeza, jamii ya wanasayansi hatimaye imeikubali nadharia ya Big Bang kwamba ulimwengu ulikuwa na mwanzo wake na hivyo wanahumanisti hawana hoja.  Hivyo mwanaatheist Antony Flew alilazimika kukiri hivi:

.Sasa nitaanza kukiri kuwa mwanaatheisti lazima atatizike kwa hizi fikra za sasa za maumbile.  Kwani inaonekana kuwa Wanakosmolojia wanatoa ushahidi kuwa kile alichodai Mtakatifu Tomas hakiwezi kuthibitishwa kifalsafa hii ikiwa na maana kuwa ulimwengu ulikuwa na mwanzo wake.

2. Nadharia ya evolusheni ambayo ndiyo hoja kuu iliyomo katika ilani ya kwanza ya humanism ikaanza kupoteza nguvu  miongo kadhaa baada ya kuandikwa kwake.  Inafahamika hivi leo ubabaishaji uliofanywa na wana evolusheni na wakiatheisti (na bila shaka wakihumanisti), kama vile A.I. Oparin na J.B.S. Haldane katika miaka ya thelathini kuhusiana na chanzo cha uhai hauna msingi wa kisayansi.

3. Viumbe haviwezi kutokea kwa bahati nasibu kutokana na maada isiyo na uhai kama ilivyodaiwa katika ubabaishaji huu.  Kumbukumbu ya mabaki ya kale inaonyesha kuwa viumbe hai hawakuwa hivi walivyo kutokana na hatua za mabadiliko madogo madogo bali walitokea kwa pamoja wakiwa na sifa zao mbali mbali.

4.  Ukweli huu umekubaliwa na wana evolusheni wenyewe  tangia miaka ya Sabini.  Sayansi ya viumbe hivi leo imebainisha kuwa viumbe hai hawakutokana na bahati nasibu  na kanuni za maumbile bali katika kila kiumbe kuna mfumo madhubuti unaothibitisha kuwa Msanii mwenye hekima ndiye aliyeviumba.  Ukitaka maelezo zaidi rejea kitabu kiitwacho, Darwinism Refuted.

Zaidi ya hivyo dai la uongo kuwa imani ya dini ndio sababu inayowakwaza watu kuendelea na kuwatumbukiza katika mifarakano limetupiliwa mbali na ushahidi wa kihistoria.  Wanahumanisti wamedai kuwa kuondolewa kwa imani ya dini kutawaletea watu furaha na faraja.  Hata hivyo hali imekuwa kinyume cha mambo. 

Miaka sita baada ya kuchapishwa kwa ilani ya humanism, vita vya pili vya Duniya vikalipuka, hii ni kumbukumbu ya misiba mikubwa iliyoletwa na itikadi za kifashisti za kisekula.  Itikadi ya Humanism ya Ukomunisti ikachipuka, kwanza ilianzia kwa watu wa Urusi kisha kwa watu wa China, Cambodia, Vietnam, Korea kaskazini, Cuba na katika baadhi ya nchi za afrika na Latin Amerika, kulikuwa ni ushenzi usio na mfano. 

Jumla ya watu Milioni 120 waliuawa na tawala za Kikomunisti au  jumuiya za kikomonisti.  Ni dhahiri kuwa kundi la wanahumanisti wa Magharibi (mifumo ya kibepari)  nalo limeshindwa kuleta amani na furaha katika jamii zao na katika maeneo mengine ya Duniya. 

Kuvunjwa kwa hoja ya humanism juu ya dini pia kumedhirishwa katika fani ya saikolojia.  The Freudian myth, msingi wa dhana ya kiatheist tokea mwanzoni mwa karneya ishirini imebatilishwa na matokeo ya uchunguzi.  Patric Glynn wa Chuo Kikuu cha George Washington anaufafanua ukweli huu katika kitabu chake kinachoitwa God: The Evidence, The Reconciliation of Faith and Reason in a PostSecular World.

Matempla na Misri ya zamani

 Wanachoelewa wanahistoria wengi kuhusiana na Frimansori ni kuwa chimbuko la Jumuiya hii ni vita vya msalaba. Ukweli ni kuwa ijapokuwa Mansori , kimsingi iliasisiwa na kutambuliwa rasmi nchini Uingereza mwanzoni mwa karne ya kumi na nne, mizizi ya Jumuiya hii imeanzia katika vita vya msalaba mnamo karne ya kumi na mbili.  Katika mkasa huu mashuhuri ndimo linamokutwa kundi la wanamgambo wa vita hivyo vya msalaba waliojulikana kama Knights Templar au Templars. Katika mfululizo wetu tumekuwa tukitumia tafsiri isiyo rasmi ya majina hayo ambayo ni Matempla. Kwa mapana na marefu historia ya Matempla imeelezewa katika kitabu kiitwacho The New Masonic Order.  Hivyo basi katika mfululizo huu tumeielezea kwa mukhtasari tu.  Kwani kuichambua kwetu mizizi ya Mansori na athari zake katika Duniya kwatosha kabisa kufichua maana nzima ya Frimansori. Ijapokuwa baadhi ya watu wanashikilia kuwa vita vya msalaba vilikuwa ni vita vilivyofanywa kwaajili ya Imani ya Kikristo, lakini kimsingi vita hivyo vilifanywa kwa maslahi ya kiuchumi.  Katika kile kipindi ambacho Ulaya ilikuwa katika hali ya umasikini na ufukara, Waislamu  wa mashariki ya kati walikuwa katika hali bora ya kiuchumi.  Mafanikio hayo ya kiuchumi pamoja na utajiri wa Mashariki ya kati  uliwatamanisha sana wazungu wa Ulaya. 

Uchu wa utajiri waliokuwanao Wazungu hao wa Ulaya ukavikwa sura ya kidini na kupambwa kwa sifa za Ukristo, japo kwa kweli wazo hasa la kuanzisha vita hivyo lilitokana na tamaa ya maslahi ya kiDuniya.  Ndio sababu kukawa na mabadiliko ya ghafla katika sera za Wakristo wa Ulaya.  Wakaachana na zile sera za amani na utulivu walizokuwa nazo katika nyakati za mwanzo za historia yao na badala yake wakachukuwa mwelekeo wa vita vya kijeshi. Mwanzilishi wa vita vya Msalaba alikuwa Papa Urban wa Pili au Pope Urban  II.  Papa huyu aliitisha mkutano wa baraza lake, Council of  Clermont mnamo mwaka 1095. Katika mkutano huo ile itikadi ya awali ya utulivu waliyokuwanayo Wakristo ikatupiliwa mbali.  Vikatangazwa vita vitakatifu kwa shabaha ya kuzipora nchi takatifu kutoka mikononi mwa Waislamu. Kufuatia tangazo hili la vita, Jeshi kubwa la wanamgambo walioitwa Crusaders likaundwa.  Kwa kiswahili tutatumia neno makruseda hapa na pale katika kutafsiri neno hilo Crusaders.  Jeshi hilo lilijumuisha askari waliokuwa na mafunzo ya kijeshi pamoja na makumi kwa maelfu ya watu wa kawaida.  Wanahistoria wanaamini kuwa hila ya Papa Urban wa pili kuanzisha vita hivyo ilitokana na tamaa yake ya kushinda kinyang’anyiro cha Upapa. 

Isitoshe Wafalme, wana wa wafalme, watawala na watu wengine wa Ulaya waliupokea wito wa Papa kwa furaha kwani walikuwa na malengo ya kujipatia maslahi ya kiDuniya kama alivyosema bw. Donald Queller wa Chuo kikuu cha Illinois, kwamba mashujaa wa Ufaransa walitaka tu kujiongezea nchi.  Nao wafanyabiashara wa Italia walitumai kupanua biashara yao mashariki ya kati…….. Idadi kubwa ya makapuku au walala hoi walijiunga na misafara hii ya kijeshi ili kukimbia maisha magumu waliokuwa wakiishi makwao.  Kote lilikopita,  Jeshi hili la wachumia tumbo lilichinja Waislamu na hata mayahudi kwa tamaa ya kujipatia dhahabu na vito vya thamani.  Makruseda hawa walitumbua matumbo ya watu waliowaua ili eti watowe dhahabu na madini ya thamani ambayo wahanga huenda waliyameza kabla ya kufa.  Tamaa ya mali iliwazidia mno Makruseda kiasi ambacho hawakusita kuvamia na kuteka jiji la Wakristo la Constantinople (Istanbul) katika vita ya nne ya Msalaba. Baada ya safari ngumu na ndefu na baada ya kufanya unyang’anyi na uporaji sambamba na mauaji ya Waislamu, kundi hili la wauaji waloitwa Makruseda likafika Jelusalem mnamo mwaka 1099.  Makruseda hawa waliingia katika jiji hili baada ya kulizingira kwa takriban majuma matano. Walifanya ushenzi wa kupindukia.  Waislamu na Mayahudi wote wa jiji hilo walifyekwa mapanga. Kwa maneno ya mwana historia mmoja, Makruseda waliua Warabu, Waislamu na Waturuki wote waliowakuta humo…Wanaume kwa Wanawake.    Mmoja wa Makruseda hao, bwana Raymond alijitapa hivi kwa hujuma waliyoifanya: 

Baadhi ya watu wetu walifyeka vichwa vya maadui zao, wengine wakawachoma mishale, wengine waliwatesa sana kwa kuwatupa maadui kwenye moto.  Malundo ya vichwa, mikono na miguu yalionekana katika mitaa ya jiji.  Ilibidi mtu akanyage miili ya watu na farasi ili aweze kupita njia.  Lakini yote haya ni madogo kulinganisha na yale yaliyotokea kwenye hekalu la Suleiman mahala ambapo ibada za kidini hufanyika mara kwa mara…Kuanzia ndani ya hekalu hadi kwenye baraza ya hekalu hilo, watu walipita kwenye madimbwi ya damu ambapo damu ilizamisha miguu yao hadi magotini. Kwa muda wa siku mbili tu jeshi la makruseda liliwaua kinyama Waislamu wapatao 40,000.  Baada ya hapo Makruseda wakaifanya Jelusalem kuwa mji wao mkuu na wakaanzisha utawala wa kifalme wa kilatini uliojitandaza kutoka mipaka ya Palestina hadi Antiokia.  Baadaye tena makruseda wakaanzisha mapambano ya kuimarisha mamlaka yao mashariki ya kati.  Ili kuidumisha dola waliyoianzisha, ilibidi waiunganishe.  Katika kutimiza lengo hilo wakaanzisha Komandi za Kijeshi ambazo hazikuwa na mfano wake hapo kabla. Watu waliounda komandi hizi walitokea  Ulaya kwenda Palestina na wakaishi katika majengo mithili ya yale ya Watawa ambamo walipatiwa mafunzo ya kijeshi ili kupambana na Waislamu.  Mojawapo ya Komandi hizi ilikuwa tofauti kabisa na nyinginezo.  Yenyewe ilibadilika muundo na kubadili mwelekeo wa historia.  Komandi hii ilikuwa ya Matempla.

Matempla

Watu waliounda Komandi hizo walitoka Ulaya kuja Palestina na wakaishi katika nyumba za kitawa ambamo walipewa mafunzo ya kijeshi ili kupambana na Waislamu.  Kundi moja miongoni mwa vikundi hivi lilitofautiana na makundi mengine.  Lenyewe likabadilika muundo na kubadili mwelekeo wa historia.  Kundi hili lilikuwa la Matempla.  Matempla au kwa jina kamili askari dhaifu wa Yesu Kristo na hekalu la Selemani ni kundi lililoanzishwa mwaka 1118 yaani miaka 20 baada ya Makruseda kuitwaa Jelusalem.  Waanzilishi wa kundi hili walikuwa Askari wa Ufaransa, Hugh dee Payens na mwenziye Godfrey d St.  Omer.  Mwanzoni kabisa kundi hili lilikuwa na watu tisa lakini baadaye likazidi kukuwa. Sababu iliyowapelekea kujiita jina hilo (Matempla) ambalo linatokana na Nomino Temple ni kuwa sehemu waliyochaguwa kuwa ngome yao ni mahali ambapo lipo hekalu la Selemani (Temple of  Solomon) au pia panaitwa Temple Mount (kilima cha hekaluni).  Japo Matempla walijiita “askari dhaifu” lakini kwa kipindi kifupi tu wakawa matajiri wakubwa.  Mahujaji wa Kikristo waliotoka Ulaya kuja Palestina wote walikuwa chin i ya himaya ya kundi hili na kutokana na fedha zao wakatajirika sana.  Mbali na hivyo, kwa mara ya kwanza kabisa matempla wakaanzisha mfumo wa hundi na karadha, sawa na ule wa Benki.  Kwa mujibu wa waandishi wa kingereza, Michael Baigent na Richard Leigh, matempla ndio walioanzisha mfumo wa kibepari wa zama za kati na ndio waliotoa mwelekeo wa kuanzishwa mfumo wa sasa wa Benki unaojengeka kwa misingi ya riba. Walikuwa ni hawa Matempla waliohusika kwa kiasi kikubwa na mashambulizi ya makruseda na mauaji ya Wailsmu.  Kwas sababu hii Kamanda mkuu wa Waislamu Saladin aliyelishinda Jeshi la Makruseda katika vita vya Hattin 1887, na baadaye kuikomboa Jelusalem, aliwahukumu Matemplsa adhabu ya kifo kwa mauaji waliyoyafanya, na akawasamehe Wakristo wengi sana.  Ingawaje waliipoteza Jelusalem na kupata madhara makubwa, bado matempla waliendelea kuwepo. Na licha ya kupungua kwa idadi ya Wakristo nchini Palestina, Matempla waliimarisha mamlaka yao barani Ulaya kuanzia Ufaransa hadi nchi nyingine hivyo pakawa na dola ndani ya dola.  Hapana shaka kuwa nguvu zao za kisiasa ziliwaweka roho juu wafalme wa Ulaya. Aidha kulikuwa na jambo jingine ambalo liliweka Taasisi ya Ukasisi katika hali mbaya.  Kundi hili la matempla lilianza kidogo kidogo kujitoa katika Imani ya Kikristo.  Na wakati walipokuwa bado wapo Jelusalem, walianza kufuata itikadi za ajabu za  kikuhani.  Pia kulikuwa na uvumi kuwa walikuwa wanafuata utaratibu wa ajabu wa sala unaorandana na Itikadi hizo. Hatimaye, mnamo mwaka 1307, Mfalme wa Ufaransa Filip le Bel aliamua kuwakamata wafuasi wa kundi hili.  Baadhi yao wakafau lu kutoroka lakini wengi wao walitiwa mbaroni.  Papa Clement wa tano, naye akaunga mkono hatua hiyo.  Kufuatia kipindi kirefu cha mahojiano na mashtaka, matempla wengi walikiri kufuata imani mpya kwamba waliikana Imani ya Kikristo na kumtukana Yesu katika mikutano yao.

Mwishowe viongozi wa Matempla ambao waliitwa “Mabwana wakubwa” kuanzia yule kiongozi wao mkubwa kabisa bwana Jacques  de Molay wote walinyongwa kwa amri ya Mfalme na Kanisa mwaka 1314.  Wengi miongoni mwao walifungwa Jela na kundi likasambaratika na kutokomea. Baadhi ya Wanahistoria wanakasumba ya  kuielezea kesi ya Matempla kama ni njama ya Mfalme wa Ufaransa na kuwatoa hatiani Matempla.  Lakini tafsiri hii ya mambo ina upungufu katika vipengere kadha wa kadha.  Mwanahistoria mashuhuri wa Uingereza Nesta H Webster ambaye ana ufahamu mkubwa wa historia ya mambo ya siri anavichambua vipengele hivi katika kitabu chake, Secret Societies and Subversive Movements

Kwa mujibu wa mwanahistoriya huyu ile kasumba ya kuwaondoa hatiani Matempla kwa mambo ambayo wenyewe walikiri kuyafanya katika kile kipindi cha mashtaka haina mashiko.  Mosi wakati wa mahojiano, si matempla wote walioteswa licha ya kukabiliwa na shitka moja. Vyovyote iwavyo kesi ya Matempla ilikwisha sambamba na kukomeshwa kwa kundi lao.  Lakini, ijapokuwa kundi hili lilikoma rasmi hata hivyo halikutoweka kabisa.  Katika ile kamata kamata  ya kushitukiza mwaka 1307, baadhi yao walinusurika.  Kwa mujibu wa tasnifu zilizoegamia nyaraka mbali mbali za kihistoria, idadi ndogo ya matempla ilipata hifadhi katika utawala pekee wa kifalme barani Ulaya ambao haukutambua mamlaka ya Kanisa Katoliki katika karne ya 14, huo ni utawala wa Scotland. Huko walijikusanya upya chini ya hifadhi ya mfalme wa nchi hiyo, Robert The Bruce.  Baada ya muda fulani wakabuni mbinu muafaka ya kujificha ili waendelee kuwepo kwa siri.  Wakajipenyeza katika jumuiya moja kubwa kwenye visiwa vya Uingereza- Wall builders’lodge na baadaye wakapata mamlaka kamili ya kudhibiti Maskani za Jumuiya hiyo. Mwanzoni mwa zama hizi, jumuiya hii ikabadili jina lake, sasa ilijiita “Masonic Lodge.”  Kaida ya Scotland ndio tawi kongwe kabisa la Masonri ambalo limeanza tokea karne ya 14 kwa wale Matempla waliopata hifadhi nchini Scoland.  Kwa kifupi matempla hawakutoweka moja kwa moja  falsafa yao, Imani zao na Ibada zao bado zingalipo chini ya mwamvuli wa Friimansuri.  Dhana hii inathibitishwa na ushahidi mwingi wa kihistoria na inakubaliwa na wanahistoria wengi wa Magharibi wale wa Friimansuri na wasio Friimansori.  Katika kitabu, The New Masonic Order ushahidi huu umeelezwa kwa kina.

Jarida liitwalo Mimar sinan linaelezea uhusiano kati ya lile kundi la Mtempla na Frimansori kwa maneno yafuatayo: 

Mnamo mwaka 1312 pale Mfalme wa Ufaransa alipolikomesha kundi la matempla kwa shinikizo la kanisa, harakati za matempla hazikukomeya hapo.  Matempla wengi sana walijificha katika maskani za Frimansori za Ulaya.  Kiongozi wa Matempla, Mabeignac pamoja na wafuasi wengine wachache walipata hifadhi nchini Scottland wakijificha chini ya jumuiya ya Wall builder kwa kutumia jina la Macbenach.

Mfalme wa Scotland Robert the Bruce akawakaribisha na kuwaruhusu kujijengea nguvu kubwa katika maskani za Masoni nchini humo.  Matokeo yake maskani hizo zikajipatia umuhimu mkubwa kutokana na kazi zao za ufundi  na mawazo yao.  Hivi leo Frimansori wanalitumia kwa heshima jina la Macbenach.  Masoni wa Scotland waliorithi mila ya matempla wakaenda nayo ufaransa miaka mingi baadaye na huko wakajenga msingi wa Kaida (rite) ijulikanayo kama Kaida ya Scotland (Scottish Rite). Aidha Jarida hilo limetoa maelezo mengi kuhusiana na uhusiano baina ya Matempla na Frimansori.  Katika makala yenye kichwa “Templars and Freenasonry” inaelezwa kuwa sala za sherehe za uzinduzi wa ile Komandi ya Matempla ni sawa kabisa na zile za Frimansori hivi leo.  Kwa mujibu wa makala hiyo hiyo, kama ilivyo kwa Mansori, wafuasi wa kundi la Matempla nao pia walikuwa wakiitana kwa jina la Brother (ndugu).

Katika sehemu ya mwisho ya makala hiyo tunasoma haya yafuatayo: 

Kundi la Matempla na jumuiya ya Masoni ni pande mbili ambazo zimeathiriana kwa kiasi kikubwa.  Hata sala za washirika hawa zinalingana zikiwa zimeigwa kutoka kwa matempla.  Kwa ajili hii Masoni, kwa kiasi kikubwa wanafanana na matempla na hivyo yaweza kusemwa kuwa ile inayoonwa kama itikadi ya siri ya masoni imerithiwa kutoka kwa Matempla. Hivyo inadhihirika wazi kuwa mizizi ya frimansori inaanzia kwa Matempla na kwamba Masoni wamefuata falsafa ya matempla.  Masoni wenyewe wanakubaliana na jambo hili.  Lakini hapa, jambo muhimu kwetu ni chanzo cha falsafa hii.  Kuna maswali haya; kwa nini matempla waliachana na Ukristo na kuwa kundi lenye itikadi mpya?  Nini kilichowapelekea kufanya hivyo? Kwanini walibadilika kule Jelusalem?  Kupitia shirika la Masonri kumekuwa na athari gani ulimwenguni kutokana na falsafa hii iliyofuatwa na Matempla?

 Matempla na Kabbalah

Kitabu kiitwacho The Hiram Key kilichoandikwa na Masoni wawili Christopher Knight na Robert Lomas kinafichuwa mambo muhimu kuhusu mizizi ya frimansori.  Kwa mujibu wa waandishi hawa, ni dhahiri kuwa Mansonri ni muendelezo wa Matempla.  Mbali na hivyo waandishi hawa pia wamevitafiti vyanzo vya Matempla.  Kwa mujibu wa tasnifu yao, Matempla walibadilika kwa kiasi kikubwa wakati walipokuwa Jerusalem.  Badala ya Ukristo, Matempla walifuata itikadi nyingine. Katika mabadiliko haya  kuna siri kubwa ambayo Matempla waliigundua katika hekalu la Selemani kule Jerusalem.

Waandishi hawa wamefafanua kuwa Matempla walitumia kisingizio cha kuwalinda mahujaji wa Kikristo waliokuwa wakitembelea Palestina kwa minajili ya kufikia malengo mengine kabisa:

Hakuna ushahidi wowote kuwa Matempla hawa waliwahi kutoa ulinzi wowote kwa mahujaji hao bali badala yake tunaona kuwa kuna ushahidi kamili kuwa walikuwa wakifanya kazi kubwa ya kuchimba Magofu ya hekalu…

Si waandishi hawa pekee waliogundua jambo hili.  Mwana historia wa Kifaransa Gaetan Delaforge naye anazungumzia jambo hilo hilo:

Kazi kubwa ya wale Matempla tisa ilikuwa ni kufanya utafiti katika eneo lote ili kupata masalio na maandiko yenye maudhui juu ya tamaduni za siri za dini ya Uyahudi na Misri ya zamani.

Mwishoni mwa karne ya 19 Charles Wilson alianza kufanya utafiti wa mambo ya kale mjini Jerusalem, akatoa maoni yake kuwa Matempla walikwenda Jerusalem kwa lengo la kutafiti mabaki ya hekalu.  Wilson aliona alama ya chimba chimba na fukuwa fukuwa chini ya misingi ya hekalu na akasema kuwa haya yalifanywa kwa zana za Matempla.  Zana hizi hadi leo zipo katika hifadhi ya Robert Brydon ambaye anamiliki nyaraka nyingi zenye maelezo kuhusu matempla. 

Waandishi wa kitabu cha Hiram key  wao wanadai kuwa chimba chimba hii ya Matempla haikutoka kapa (haikuishia patupu), kwamba Matempla waligundua mambo fulani ambayo yalibadili mtazamo wao juu ya ulimwengu.  Aidha  watafiti wengi wanakubaliana na jambo hilo.  Lazima kuna jambo fulani tu ambalo liliwapelekea Matempla kufuata utaratibu wa imani na falsafa iliyotofautiana kabisa na ile ya Ukristo licha ya ukweli kuwa kabla ya hapo walikuwa Wakristo na isitoshe walitoka katika ulimwengu wa Kikristo.  Kwa fikra za watafiti wengi jambo walilogundua Matempla ambalo lilibadili mtazamo wao ni Kabbalah. Maana ya neno hili Kabbalah ni Oral Tradition (Fasihi simulizi).  Kamusi mbali mbali zinaliainisha neno hili kama ni tawi la siri na la kikuhani la dini ya uyahudi.  Kwa mujibu wa ainisho hili Kabbalah inafichua maana iliyofichikana ya Taurati na maandiko ya dini ya Uyahudi.  Lakini tunapolichungua jambo hili kwa undani tunaona kuwa kuna mambo mengine kabisa.  Mambo haya ndiyo yanayotupelekea kufikia hitimisho kuwa Kabbalah ni utaratibu ambao mzizi wake unatokea katika ibada ya masanamu ya wapagani.  Hii ni kuwa Kabbalah ilikuwepo kabla ya Taurati na ilitumbukizwa katika dini ya Uyahudi baada ya kufunuliwa Taurati.  Ukweli huu wa kusisimua juu ya Kabbalah unafafanuliwa hivi: Frimasoni wa Kituruki Murat Ozgen katika kitabu chake, Masonluk Nedir ve Nasildir? (Ni nini frimansori na ikoje?), anasema:

“Hatujuwi vyema wapi ilikotokea Kabbalah na jinsi ilivyostawi.  Hili ni jina la jumla la falsafa ya ajabu, ya siri na ya kikuhani hususani ile inayohusiana na dini ya Uyahudi.  Inasadikika kuwa ni Itikadi ya kikuhani ya kiyahudi lakini baadhi ya mambo yaliyomo katika itikadi hiyo yanaonesha kuwa ni Itikadi iliyojengwa zamani  kabla ya Taurati”. 

Mwana historia wa Kifaransa anayeitwa Gougenot des Mousseaux ameeleza kuwa Kabbalah ni kongwe mno kuliko itikadi ya uyahudi.  Naye Mwanahistoria wa Kiyahudi Theodore Reinach anasema kuwa Kabbalah ni sumu isiyofahamika ambayo iliingia kwenye mishipa ya Uyahudi na kuidhuru itikadi nzima.  Salomon Reinach anaiainisha Kabbbalah kama ni mojawapo kati ya pogo mbaya sana za akili ya binadamu.  Sababu ya dai hili la Reinach ni kuwa itikadi ya Kabbalah kwa kiasi kikubwa inahusiana na uchawi. Kwa maelfu ya miaka, Kabbalah imekuwa msingi wa kila itikadi ya kichawi.  Inasadikiwa kuwa “magwiji” wa Kiyahudi wenye elimu ya Kabbalah wana nguvu kubwa za kimazingara.  Halikadhalika watu wengi wasiokuwa Mayahudi wameathiriwa na Kabbalah na wamekuwa wakijaribu kufanya uchawi kwa kutumia mafundisho yake.  Zile tamaduni za siri ambazo zilikuwa na nguvu Ulaya mwishoni mwa zama za kati, kwa kiasi kikubwa mizizi yake ilitokea katika Kabbalah. 

Waandishi kadhaa waliothibitisha kuwa Matempla walibadili muelekeo baada ya kugundua siri fulani kwenye mabaki ya Hekalu la Selemani.  Siri hiyo ni Kabbala.  Kabbala ni utaratibu unaotokea katika ibada ya masanamu ya wapagani. Kwamba, itikadi hii ilikuwepo zamani kabla ya kufunuliwa kwa Taurati.   Jambo la ajabu ni kuwa Uyahudi ni dini iliyoamini Mungu mmoja iliyotokana na ufunuo wa Taurati kwa Mussa (a.s).  Lakini ndani ya dini hii umo utaratibu unaoitwa Kabbalah unaofuata mafundisho ya uchawi yaliyoharamishwa na dini hiyo.  Jambo hili linathibitisha yale tuliyoyaeleza awali kuwa Kabbalah ni kitu ambacho kimeingia katika Uyahudi kutoka sehemu nyingine.  Lakini nini chimbuko la kitu hiki?  Mwanahistoria wa Kiyahudi Fabre d’Olivet anasema kuwa kabbalah ilitoka katika nchi ya  Misri ya zamani.  Kwa mujibu wa mwandishi huyu mizizi ya kabbalah imetambaa kutoka Misri ya kale.  Kabbalah ni utamaduni ambao baadhi ya viongozi wa Waisrael walijifunza katika nchi ya Misri.  Na wao wakaurithisha utamaduni huo kwa kizazi hadi kizazi kwa njia ya fasihi simulizi.  Kwa sababu hii hatuna budi kuiangalia hiyo Misri ya kale ili tuvione vyanzo vya msingi vya mfungamano wa Kabbalah, Matempla na Frimansori.

 
   
    
4 / total 6
You can read Harun Yahya's book Ulimwengu Wa Frimasonri online, share it on social networks such as Facebook and Twitter, download it to your computer, use it in your homework and theses, and publish, copy or reproduce it on your own web sites or blogs without paying any copyright fee, so long as you acknowledge this site as the reference.
About this site | Tengeneza kurasa yako ya nyumbani | Add to favorites | RSS Feed
Mambo yote yanaweza kuynakiliwa, kuchapwa na kusambazwa kwa kurejea katika kurasa hii
(c) All publication rights of the personal photos of Mr. Adnan Oktar that are present in our website and in all other Harun Yahya works belong to Global Publication Ltd. Co. They cannot be used or published without prior consent even if used partially.
© 1994 Harun Yahya.www.harunyahya.com
page_top