Ulimwengu Wa Frimasonri

SHUSHA KITABU

Download (DOC)
Maoni

SURA ZA KITABU

< <
5 / total: 6
Frimasonri - Harun Yahya
Frimasonri
   

 


Wachawi wa Misri ya kale  

Misri ya kale ya Mafirauni ilikuwa moja ya jamii kongwe Duniyani.  Ilikuwa ni moja ya jamii za kidhalimu mno.  Minara mikubwa ambayo bado ipo tokea enzi hizo za Misri ya Kale-Mapiramid yalijengwa na mamia kwa maelfu ya watumwa waliofanyishwa kazi kwa mijeledi na vitisho vya kunyimwa chakula.  Mafirauni ndio waliokuwa watawala wakuu wa Misri ambao walistahabu kuitwa miungu na kuabudiwa na watu.  Moja  ya vyanzo vya habari juu ya Misri ya kale ni maandiko yao wenyewe.  Maandiko haya yaligunduliwa katika karne ya 19.  Na baada ya jitihada kubwa, herufi za Kimisri zikasomeka na kutoa mwanga mkubwa wa maelezo juu ya nchi hiyo.  Lakini kwa vile maandiko haya yaliandikwa na wanahistoria waliofanya kazi serikalini, yalijaa maelezo ya kuisifu dola.  Kwa upande wetu chanzo cha habari cha hakika juu ya jambo hili ni Qur’an.  Ndani ya Qur’an, katika kisa cha Mussa, tunapata maelezo muhimu juu ya mfumo wa utawala wa Misri ya wakati huo.  Aya zinabainisha kuwa kulikuwa na mihimili miwili ya utawala; Firauni na Baraza lake la ndani. Baraza hili lilikuwa na kazi ya kutoa ushauri muhimu kwa Firauni.  Mara nyingi Firauni alikutana nalo na kufuata maoni ya baraza hilo. Aya zifuatzo zinaonyesha ushawishi wa baraza hilo kwa firauni:

Na alisema Musa:  Ewe Firauni! Mimi ni Mtume nitokaye kwa Mola wa walimwengu.  Yanipasa nisiseme juu ya Mwenyezi Mungu (lolote) ila haki.  Kwa yakini nimekufikieni kwa dalili wazi wazi zitokazo kwa Mola wenu.  Basi wapeleke wana wa Israel pamoja nami (Nchi waitakayo, usiwazuilie hapa Misri ukawa una wadhili).  (Firauni) akasema:  Kama umekuja na hoja basi ilete ukiwa ni miongoni mwa wasemao kweli.  (Hapo Musa) akaitupa fimbo yake (chini).  Na mara ikawa nyoka dhahiri.  Na akatoa mkono wake. Mara ukawa mweupe kwa watazamao.  Wakasema wakuu wa kaumu ya Firauni:  Hakika huyu ni mchawi ajuaye.  Anataka kukutoweni katika ardhi yenu.  Basi mnatoa shauri gani?  Wakasema muache kidogo yeye na ndugu yake (usiwaue) na watume wakusanyao mijini.  Wakuletee kila mchawi ajuaye (7:104-112).

Ikumbukwe kuwa hapa limetajwa Baraza lililokuwa likimshauri Firauni ambapo hapa linamshawishi Firauni kupambana na Musa na linapendekeza mbinu za kukabiliana naye.  Tukiangalia kumbukumbu za Historia ya Misri, tunaona kuwa Baraza hili lilikuwa na matapo mawili; tapo la jeshi na tapo la makasisi.  Hakuna haja ya kufafanua umuhimu wa jeshi.  Kimsingi Jeshi ndilo lililojenga nguvu za tawala za Mafirauni. Tunachopaswa kukiangalia hapa ni jukumu la Makasisi.  Makasisi wa Misri ya kale ni tabaka ambalo katika Qur’an linaitwa kama tabaka la wachawi.  Wao waliwakilisha tabaka la wachawi lililounga mkono utawala.  Ilisadikiwa kuwa watu hawa walikuwa na nguvu fulani na walimiliki elimu ya siri.  Kutokana na mamlaka waliyokuwa nayo, Makasisi walikuwa na ushawishi kwa jamii ya Wamisri na kujihakikishia nafasi yao ndani ya utawala wa Mafirauni. Tabaka hili ambalo katika kumbukumbu za Misri lilijulikana kama Makasisi wa Amon, liljishughulisha na uchawi na kulipa nafasi tabaka la wapagani.  Aidha walijifunza Sayansi mbali mbali kama vile unajimu, mahesabu na jeometri.  Tabaka hili la makuhani lilikuwa ni kundi la siri lililomiliki elimu mahususi.  Makundi kama haya hujulikana kama mashirika ya siri. 

Katika Jarida liitwalo Mason Dergisi (Masonic Journal) ambalo huchapishwa na kusambazwa kwa masoni wa Kituruki, kuna maelezo kuwa mizizi ya Frimansori inatokea katika kundi hili la siri na hasa linatajwa lile la makasisi wa Misri ya kale.  Kadri akili ya mwanadam inavyokuwa, ndivyo Sayansi inavyopiga hatua za maendeleo na kadri sayansi inavyopiga hatua za maendeleo ndivyo idadi ya mambo ya siri inavyoongezeka katika elimu ya Utamaduni wa siri.   utamaduni huu wa siri ambao kwanza ulianzia mashariki; China na Tibeti na kisha kuenea India, Mesopotania na Misri ndio uliojenga msingi wa elimu ya kikuhani ambayo imefuatwa kwa maelfu ya miaka na kuunda msingi wa nguvu ya Makasisi nchini Misri.  Sasa panawezaje kuwepo mahusiano baina ya falsfa ya siri ya makuhani wa Misri ya kale na Mafrimasoni wa leo? Utawala wa  Misri ya kale ambao katika Qur’an unapigiwa mfano kama utawala wa kisiasa uliomkana Mungu ulitoweka maelfu ya miaka iliyopita.  Je waweza  kuwa na athari zozote  hivi leo? Ili kupata jibu la maswali haya, hatuna budi kuiangalia Imani ya Makuhani wa Misri ya kale juu ya chanzo cha ulimwengu na maisha.

Imani ya Misri ya kale juu ya dhana ya Evolusheni ya Kilahidi

Katika kitabu chao The Hiram Key waandishi wa kimasoni Christopher Khight  na Robert Lomas wanadai kuwa Misri ya kale inachukuwa nafasi muhimu kuhusiana na chimbuko la Masonri. Kwa mujibu wa waandishi hawa, dhana kuu ambayo imepandikizwa kwa Masonri wa hivi sasa kutoka Misri ya Kale ni lile la ulimwengu kutokea na kujiendesha wenyewe yaani kutokea kwa bahati nasibu.  Wanaifafanua dhana hii ya kuchekesha kwa maneno haya:

Wamisri waliamini kuwa Maada ndiyo iliyokuwepo wakati wote; kwao wao halikuwa  jambo la kimantiki  kumfikiria Mungu kuwa ndiye aliyeumba kila kitu kutokana na hamna.  Dhana yao ilikuwa hii kwamba Duniya ilianza pale utulivu ulipokuja baada ya mparaganyiko wa vitu na kwamba tangu wakati huo kumekuwa na ugomvi kati ya nguvu za umoja na nguvu za utengano… Ile hali ya mvurugiko iliitwa  Nun, sehemu zote zilikuwa giza totoro, nguvu ya maumbile iliyokuwa ndani yake ikaamuru maisha yaanze.  Nguvu hii isiyoonekana ambayo ilikuwemo ndani ya ile hali ya msambaratiko yenyewe nayo haikujitambua kama ilikuwepo.

Kushabihiana kwa Imani ya Misri ya kale  na dhana ya Evolusheni.

 Katika toleo lililopita tulinukuu maelezo kutoka kwenye kitabu kinachoitwa Hiram  Key kilichoandikwa na waandishi wa Kimasoni Christopher Knight  na Robert Lomas  ambao wanadai kuwa Misri ya kale inachukuwa nafasi muhimu katika vyanzo vya Masoni.  Kwa mujibu wa waandishi hawa, dhana kuu ambayo imeibuka kwa Masonri ya leo kutoka Misri ya kale ni ile ya  ulimwengu kutokea kwa bahati nasibu  na kujiendesha wenyewe.

Izingatiwe kuwa dhana hii inashabihiana na madai ya Walahidi ambayo yanatiwa nguvu na ajenda ya jumuiya ya wanasayansi kwa kutumia maneno haya; “Theory of  Evolution” (nadharia ya evolusheni), “Chaos Theory” (nadharia ya mparaganyiko) na the essential organization of matter(chanzo cha mkusanyiko wa maada). Waandishi hawa wanaongeza kusema kuwa, kuna uwiano kati ya imani za kale za Misri na Sayansi ya leo lakini Sayansi wanayoimaanisha wao ni zile dhana za kilahidi.  Licha ya ukweli kwamba nadharia hizi hazina msingi wowote wa kisayansi bado zimewekwa kinguvu nguvu katika fani ya sayansi kwa takribani karne mbili zilizopita na zinawasilishwa kama nadharia zilizohalalishwa kisayansi.  Sasa tumefika kwenye nukta muhimu, hebu tufanye ufupisho wa maelezo ya kile ambacho tumekisoma hadi kufikia hapa:

1.Lipo kundi la Matempla linalodhaniwa kuwa ndio chimbuko la Masonri. Tumeona kuwa japo kundi hili lilianzishwa likiwa na imani ya Kikristo lakini matempla hawa wakaathiriwa na itikadi fulani za siri walizozikuta Jerusalem.  Wakaachana kabisa na Ukristo na kujiundia jumuiya iliyopingana na dini. 

2. Tmeona kuwa kimsingi itikadi iliyowaathiri matempla ilikuwa kabbalah.

3. Tulipoichunguza Kabbalah, tukapata uthibitisho kuwa ingawaje itikadi hiyo imenasibishwa na Uyahudi lakini ilikuwa ni itikadi ya kipagani na ya zamani kuliko Uyahudi.  Kwamba itikadi hii ilitumbukizwa tu katika dini hii na kwamba mizizi yake halisi inaonekana katika Misri ya kale.

4.Misri ya kale ilitawaliwa kwa mfumo wa kipagani wa Firauni na huko ndiko ilikokutwa dhanna inayounda msingi wa falsafa za sasa zinazomkana Mungu:  Kwamba ulimwengu unajiendesha wenyewe, na umetokea kwa bahati nasibu.

Kwa hakika haya yote yanatupa picha ya wazi kabisa. Sasa swali ni je ni kwa bahati nasibu tu kwamba  falsafa ya makuhani wa Misri ya kale ipo hadi leo,  na kwamba vipo vielelezo vya mfungamano (Kabbalah-Matempla-Masonri) ambao ndio umehusika na uboreshaji wa dhana hii hadi kufikia leo hii?

Je yawezekana kuwa wale Masoni walioweka kumbukumbu yao katika historia ya Duniya tangia karne ya 18, wakifanya mapinduzi wakijenga falsafa na mifumo ya kisiasa ndio warithi wenyewe wa wachawi wa Misri ya kale? Ili kuliweka wazi zaidi jawabu la swali hili, hatuna budi kuchunguza kwa undani ambayo tumeeleza kwa kifupi. 

 Habari ya ndani juu ya kabbalah

“Kutoka” ni jina la kitabu cha pili cha Taurati. Kitabu hiki kinaelezea jinsi wana wa Israel, chini ya uongozi wa Mussa, walivyohama Misri kuepuka udhalimu wa Firauni.  Firauni aliwashurutisha wana wa Israel kuishi kama watumwa na alikataa kuwaachia huru.  Lakini alipokumbana na miujiza aliyoonesha Mwenyezi Mungu kupitia kwa Musa na maangamizi aliyowapelekea watu wake, Firauni alitulia.  Kwa hiyo usiku mmoja  wana waisrael wakajikusanya na kuanza safari ya kuhama Misri.  Baadaye Firauni akawashambulia wana wa Israel lakini Mungu akawanusuru kwa muujiza mwingine alionesha kupitia kwa Mussa. Lakini katika Qur’an ndimo tunamokuta maelezo sahihi zaidi ya kuhama kwao kutoka Misri, hii ni kwa sababu Taurati imehujumiwa baada ya kufunuliwa kwa Mussa.  Ushahidi madhubuti wa hili ni kuwa katika vitabu vitano vya Taurati; Kitabu cha mwanzo, Kutoka, Walawi, Hesabu na kumbu kumbu la Taurati kuna migongano mingi.  Ukweli kuwa kitabu cha kumbukumbu na Taurati kimeishia na maelezo ya kufa na kuzikwa  kwa Mussa ni ushahidi usiopingika kuwa sehemu hii itakuwa imeongezwa baada ya kifo cha Mussa. Katika maelezo ya Qur’an juu ya kuhama kwa wana wa Israel kutoka Misri hakuna mgongano hata kidogo kama yalivyo maelezo mengi mengineyo.  Kisa hiki kimeelezwa kwa usahihi kabisa.  Isitoshe kama zilivyo habari nyingine, Mwenyezi Mungu anatufunulia hekima na siri nyingi katika jambo linalozungumziwa.  Kwa sababu hii pale tunapoziendea habari hizi kwa undani, tunweza kupata mafundisho mengi ndani yake. 

 Ndama wa dhahabu.

Miyongoni mwa mambo muhimu kuhusiyana na kuhama kwa wana wa Israel kutoka Misri, kama ilivyoelezwa katika Qur’an ni kuwa waliiasi dini iliyofunuliwa kwao na Mwenyezi Mungu licha ya ukweli kwamba Mwenyezi Mungu aliwanusuru na udhalimu wa Firauni kupitia kwa Mussa.  Wana wa Israel hawakuweza kuielewa ile Tawhiid ambayo Mussa aliwafikishia badala yake wao walizidi kuielekea ibada ya sanamu.  Qur’an inauelezea hivi muelekeo huu wa ajabu:  (Na tukawavusha wana wa Israel baharini wakasalimika na balaa la Firauni) na ikawafikia watu waliokuwa wakiabudu masanamu yao.

 “Wakasema ewe Mussa! Tufanyie miungu na sisi yaani masanamu kama wenzetu walivyo na Miungu.” (Mussa) akasema hakika nyinyi ni watu mfanyao ujinga.  Hawa yataangamia haya waliyonayo na ni bure waliyokuwa wakiyafanya. (7:138-139).

Licha ya maonyo ya Mussa, wana wa Israel waliendelea na upotevu wao na pale Mussa alipowaacha na kwenda Mlima wa Sinai, upotevu wao ukadhihirika zaidi.  Akitumia fursa ya kutokuwepo kwa Mussa, mtu mmoja aliyeitwa Samir akawajia na kuwashawishi watengeneze sanamu la ndama na kuliabudu.  Mussa akarudi kwa watu wake kwa ghadhabu na masikitiko.  Akasema:  Enyi watu wangu! Je Mola wenu hakukuahidini ahadi nzuri?  Je umekuwa mrefu kwenu muda (wa) ahadi hiyo (mnaona hazitimizwi) au mmetaka ikushukieni ghadhabu kutoka kwa Mola wenu; na kwa hivyo mmevunja ahadi yangu?  Wakasema:  Sisi hatukuvunja ahadi yako kwa hiyari yetu walakini tulibebeshwa mizigo ya watu (vyombo vya dhahabu tulivyoviazima kwa wanawake wa Kimisri) tukaitupa (motoni ikayayuka ikaundwa mungu).  Na namna hivi hivi alitia Samir (sehemu yake).  Na akawatolea (Akawaundia katika myeyusho huo) Ndama, Kiwiliwili kamili kinacholia.  Na wakasema:  Huyu ndiye mungu wenu na mungu wa Mussa.  Lakini Mussa amesahau (20:86-88).

Kwanini wana wa Israel walikuwa na msimamo wa ukaidi namana hiyo katika kukita masanamu na kuyaabudia?  Ni nini chanzo cha muelekeo huu?

Ni dhahiri kuwa jamii ambayo hapo kabla haikuwahi kuamini masanamu, isingeweza kwa ghafla kufuata mwenendo huo wa  kipumbavu wa kutengeneza sanamu na kuanza kuliabudia.  Ni wale tu ambao ibada ya sanamu ilikuwa ya kawaida kwao ndio ambao wangeweza kuamini upuuzi huo. Lakini, wana wa Israili walikuwa ni watu ambao hapo kabla waliamini Mungu mmoja tangia zama za mzee wao Ibrahim.  Jina hili, “Waisraili”  au “wana wa Israili” mwanzoni kabisa lilitolewa kwa watoto wa Yaqubu, mjukuu wa Ibrahim.  Baadaye jina hili likatumika kwa Wayahudi wote waliotokana naye.  Waisraili walikuwa wameichunga ile imani ya Mungu mmoja ambayo waliirithi kutoka kwa wazee wao; Ibrahim, Is-haqa na Yaqubu (a.s). Wakiwa pamoja na Yusufu (a.s), walikwenda Misri na wakaichunga Imani yao ya Mungu mmoja kwa kipindi kirefu licha ya ukweli kwamba waliishi pamoja na Washirikina wa Misri.  Katika maelezo yaliyotolewa katika Qur’an, inabainika wazi kuwa pale Musa alipowajia, Waisraili bado walikuwa watu walioamini Mungu mmoja.   Isipokuwa tu, ni kuwa pamoja na kuamini kwao Mungu mmoja, Waisraili waliathiriwa na wapagani waliokuwa wakiishi nao na wakaanza kuwaiga, wakibadili dini waliyochaguliwa na Mwenyezi Mungu na badala yake kufuata Ibada ya sanamu ya jamii nyingine.

Tunapolichunguza suala hili kwa undani na kwa kuzingatia kumbu kumbu za historia, tunaona kuwa itikadi ya  kipagani iliyowaathiri Waisraili ilikuwa ni ile ya Misri ya kale.  Ushahidi muhimu wa kushadidia hitimisho hili ni kuwa yule ndama wa dhahabu waliyemuabudia Waisraili wakati Musa alipokwenda mlima Sinai alikuwa mfano halisi wa Masanamu ya Wamisri, Hatha na Aphis.  Katika kitabu chake, Too Long in the Sun, Mwandishi wa Kikristo bw. Richard  Rives ameandika hivi:

Hatha na Aphis Ng’ombe jike  na fahari miungu ya Misri ilikuwa ikiwakilisha ibada ya jua.  Ibada yao ilikuwa ni muendelezo wa historia ya utukuzo wa jua.  Yule ndama wa dhahabu wa mlima Sinai ni ushahidi tosha wa kuthibitisha kuwa karamu iliyotangazwa ilihusiana na ibada ya jua…

Athari za dini ya kipagani ya Misri zilionekana katika sura nyingi tofauti.  Mara baada ya kuwashinda wapagani Imani yao ya kishirikina ikadhihirika wazi kama aya inavyosema:  Ewe Musa! Tufanyie miungu  na sisi (yaani masanamu) kama wao walivyo na miungu.  (7:138).  Na kumbukeni habari hii pia (mliposema ewe Musa hatukuamini mpaka tumuone mungu wazi wazi (2:55). 

Maneno yao haya yanadhihirisha kuwa nao walitaka kuabudu  Mungu wa kimaada ambaye wangemuona kwa macho kama dini ya kipagani ilivyowapatia Wamisri mungu kama huyo.  Mwelekeo huu wa Waisraili kufuata upagani wa Misri ya kale ambao tumeuelezea hapa, ni muhimu ueleweke kwani ndio unaotupa ufahamu wa jinsi kilivyohujumiwa kitabu cha Taurati na unatufahamisha chanzo cha Kabbalah. Tukiyatafakari mafundisho haya kwa mazingatio, tutaona kuwa ni katika vyanzo hivi unapokutikana upagani wa Misri  ya kale na falsafa ya Kilahidi.

Kutoka Misri ya kale hadi Kabbalah

Wakati Musa angali hai, Waisraili walikwishaanza kutengeneza Masanamu kama yale yale waliyoayaona Misri na kuyaabudia.  Baada ya Musa kutawafu (kufariki Duniya), hakukuwa tena na kikwazo cha kuwazuia Waisraili kuzama katika upotofu.  Bila shaka haiwezi kusemwa kuwa ni Wayahudi wote waliokengeuka, lakini baadhi yao walifuata upagani wa Misri. Kwa kweli walishikilia mafundisho ya ukuhani wa Misri (mafundisho ya wachawi wa Firauni)  ambayo yalijengwa kwa msingi wa imani ya jamii hiyo na wakaihujumu imani yao kwa kutumbukiza mafundisho haya ndani yake.  Itikadi ambayo ilitumbukizwa katika Uyahudi kutoka Misri ya kale ilikuwa ni Kabbalah.  Kama ulivyokuwa mfumo wa Makasisi wa Misri,  Kabbalah nao ulikuwa mfumo wa siri na msingi wake ulikuwa utamaduni wa uchawi.   Maelezo juu maumbile ambayo Kabbalah inayatoa ni tofauti kabisa na yale yaliyokutwa katika Taurati.  Ni maelezo ya kilahidi yaliyoegamia dhana ya Misri ya kale juu ya uhai wa milele wa maada.    Murat Ozgen, mwana Frimasonri wa Kituruki ana haya ya kusema juu ya suala hili:

Ni dhahiri kuwa Kabbalah iliundwa miaka mingi kabla ya kuja kwa Taurati.  Sehemu muhimu ya Kabbalah ni ile nadharia juu ya muundo wa ulimwengu.  Nadharia hii iko tofauti kabisa na maelezo juu ya maumbile yaliyopokewa na dini zinazoamini Mungu.  Kwa mujibu wa Kabbalah, mwanzoni kabisa mwa hatua ya kuumbwa kwa ulimwengu, vitu vilivyoitwa Sefiroth vikiwa na maana ya miduara au mihimili yenye sifa za kiroho na kimaada iliibuka.  Idadi ya jumla ya vitu hivi ilikuwa 32.

Ile kumi ya mwanzo ndiyo iliyoshikilia mfumo wa sayari  na mingine iliyosalia imeshikilia makundi ya nyota angani.  Imani hii ya ajabu ya Kabbalah inabainisha kuwa inahusiana kwa karibu na mifumo ya imani ya unajimu.  Kwa hiyo Kabbalah inapinmgana kabisa na dini ya Uyahudi na inanasibiana kwa karibu na imani za zamani za siri za mashariki.  Kwa kufuata mafundisho ya siri na ya kilahidi ya Misri ya zamani ambayo yalijengwa kwa msingi wa uchawi, Wayahudi wakapuuza mambo yaliyoharamishwa katika Taurati.  Wakashikilia ibada za kichawi za Wapagani na hivyo Kabbalah ikawa itikadi ndani ya Uyahudi lakini yenyewe ikienda kinyume na Taurati.  Katika kitabu chake kiitwacho Secret Societies and Subversive Movements, mwandishi wa kingereza Nesta H Webster anasema:

Uchawi kama tuujuavyo ulikuwa ukifanywa na Wakanani kabla ya kuvamiwa kwa  Palestina na Waisraili.  Misri, India na Ugiriki nazo zilikuwa na wachawi  na waaguzi wao.  Licha ya makemeo dhidi ya uchawi yaliyomo katika sheria ya Musa, Wayahudi walijiingiza katika uchawi na ule utamaduni mzuri waliourithi wakauchanganya na mawazo ya kichawi yaliyotoka katika jamii nyingine. 

Tamaduni za kipagani za uchawi wa zama za kale

Katika toleo lililopita tuliona kuwa Wayahudi walipuuza mambo yaliyohamishwa katika Taurati na hivyo kufuatia ibada za kipagani. Kwa ajili hii, Kaballa ikawa itikadi ndani ya dini ya uyahudi ingawaje ingawaje ilipingana na Taurati. Katika kitabu chake kiitwacho Secret Societies, and Subversive Movements, Mwandishi wa kiingereza Nesta Webster ameandika hivi:

Uchawi, kama tuujuavyo ulikuwa ukifanywa na Wakanani kabla Palestina haijavamiwa na Waisrail. Nazo nchi za Misri, India na Ugiriki vile vile zilikuwa ni za Wachawi na Waaguzi wao. Licha ya makatazo yaliyomo katika sheria ya Musa, Wayahudi wakauchanganya utamaduni wao mtukufu na mambo ya uchawi yaliyotoka katika jamii nyingine na mengine waliyoyatunga wenyewe. Hapa ndipo ilipo hoja ya Wapinzani wa Kabballa kuwa hii tunayoijua sisi hivi leo kama Kabbala, kimsingi haikutoka katika Uyahudi. Katika Qur’an, kuna aya inayozungumzia jambo hili. Mwenyezi Mungu anasema kuwa; wana wa Israili walijifunza tamaduni za kichawi za kishetani kutoka nje ya dini yao.

Wakafuata yale waliyofuata mashetani(wakadai kuwa yalikuwa katika Ufalme wa Suleiman na Suleiman hakukufuru, wakafundisha watu uchawi(waliokuwa wakiujua wenyewe tangu zamani), na(uchawi) ulioteremshwa kwa Malaika wawili, Haruta na Maruta katika(mji wa) Babil. Wala(Malaika hao) hawakumfundisha  yeyote ila mpaka wamambie, hakika sisi ni mtihani(wa kutazamwa kutii kwenu) basi usikufuru. Wakajifunza kwao mambo ambayo kwayo waliweza kumfarakanisha mtu na mkewe(na mengineyo) wala hawakuwa webye kumdhuru mtu yeyote kwa hayo ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na wanajifunza ambayo yatawadhuru wala hayatawafaa. Na kwa yakini wanajua kwamba aliyekhiari haya hatakuwa na sehemu  yoyote katika Akhera. Na bila shaka ni kibaya kabisa walichouzia nafsi zao laiti wanagelijua(2:102).

Ayah ii inabainisha kuwa japo, Wayahudi Fulani walijua kuwa watapata hasara katika maisha ya Akhera lakini bado walijifunza na kufuata tamaduni za kichawi.

Hivyo walikengeuka na toka katika sheria ambayo Mungu aliwashushia. Wakawa wamezitia hasarani nafsi zao kwa kutumbukia katika upagani(Itikadi za wachawi). Mambo yaliyoelezwa katika aya hii yanaweka bayana vinpengele vikuu vya mfarakano katika historia ya Wayahudi. Mapambano yalikuwa baina ya Mitume na wafuasi wai kwa upande mmoja na kwa upande wmingine Wayahudi waliopotoka na kuasi amri za Mungu na kuiga tamaduni za kipagani. Ni muhimu kukumbuka kuwa maovu ya Wayahudi wapotevu yamendikwa katika agano la kale. Ndani ya agano la kale kuna kitabu cha Nehemia ambamo Wayahudi wanaungama na kutubu. Waliokuwa wazawa wa Israili wakajitenga na wageni wote, wakasimama mahali pao, wakasoma katika kitabu cha Torati ya Bwana, Mungu wao, muda war obo ya siku, na siku nyingine, wakaungama, wamuabudu Bwana Mungu wao. Ndipo wakasimama madarajanai ya walawi, Yeshua na Bani, na Kadimieri na Shebania na Kenani, wakamlilia Bwana Mungu wao kwa sauti kuu.

(Wakasema) walakini(Baba zetu) hawakutii, wakaasi, wakaitupa sheria yako nyuma yao, wakawaua manabii wako walioshuhudia juu yao wapate kuwarejeza kwako; wakatenda machukizo makuu. Kwa sababu hiyo ukawatia katika mikono ya adui zao, waliowasumbua na wakati wa shida yao walipokulilia, uliwasikia kutoka mbinguni; na kwa wingi wa rehema zako ukawapa waokozi waliowaokoa katika mikono ya adui zao. Lakini walipokuwa wamekwishastarehe, walitenda mabaya tena mbele zako; kwa hiyo ukawaacha katika mikono ya adui zao, nao wakawatawala; hata hivyo waliporejea na kukulilia, uliwasikia toka mbinguni, ukawaokoa mara nyingi kwa rehema zako, ukawashuhudia ili uwarudishe tena katika sheria yako; lakini walitakabari wasisikilize amri zako,(ambazo mtu akizitenda ataisi katika hizo0 nao wakayaondoa, wakafanya shingo zao kuwa ngumu, wasitake kusikiliza. Ila kwa rehema zako nyingi hukuwakomesha kabisa wala kuwaacha; kwa maana wewe u Mungu Mwenye neema, Mwenye rehema. Basi sasa Ee Mungu, Mkuu Mwenye Uweza, Mungu wa kuogofya mwenye kushika maagano yote yaliyotupa sisi, wafalme wetu wakuu wetu wa makuhani wetu wa manabii wetu, na baba zetu na watu wako wote, tangu zamani za Wafalme wa Ashuru hata leo, na yasihesabiwe kuwa ni madogo. Lakini wewe u mwenye haki, katika hayo yote yaliyotupata; maana wewe umetenda yaliyotenda yaliyokeli lakini sisi tumetenda yaliyo mabaya na Wafalme wetu na wakuu wetu na wakuu wetu na makuhani wetu na Baba zetu hawakushika sheria yako wala hawakusikiliza amri zako na shuhuda zako ulizowashuhudia. Kwa kuwa hawakukutumikia wewe katika Ufalme wao na katika wema wako mkuu uliowapa na katika nchi ile kubwa yenye neema uliyowapa mbele yao wala hawakughairi na kuacha mabaya yao.(Nehemia 9:2-4, 26-29, 31-35).

Kifungua hiki kinalezea tamaa ya kurejea katika imani ya Mungu mmoja ambayo Wayahudi wengi walikuwa nayo, isipokuwa katika kipindi Fulani cha historia kundi moja lilimeguka na kupta ushawishi kidogo kidogo, na baadae likaja kuwa tawala Wayahudi na baadae likaigeuza kabisa dini yenyewe. Kwa sababu hii, katika Taurati na katika vitabu vingine vya Agano la Kale kuna masalia yanayotoka katika mafundisho ya kipagani. Katika kitabu cha mwanzo inaelezwa kuwa Mungu aliumba Ulimwengu kwa siku sita wakati ambapo hapakuwa na chochote. Hii ni im’ani sahihi kabisa na inatokana na ufunuo sahihi. Lakini hapo hapo inasema kuwa Mungu alipumzika siku ya saba huu ni uzushi kabisa. Ni dhanna potofu iliyotoka katika upagani amabo unampa Mungu sifa za kibinaadamu:

Katika aya hii ya Qur’an Mwenyezi Mungu anasema:

Na tumeziumba mbingu na ardhi na vilivyomo katika yao katika nyakati sita wala hayakutugusa machovu(50:38).

Katika sura nyingine za Taurati kuna staili ya uandishi ambayo ni ya utovu wa heshima kwa Mwenyezi Mungu hasa zaidi katika zile sehemu ambazo sifa za kibinaadamu anapewa Mungu. Imani hizi potofu za kulinganisha udhaifu wa kibinaadamu ndizo imani ambazo wapagani walikuwa nazo kwa miungu yao bandia. Maneno mengine ya kufuru ni yale yanayodai kuwa Yakobo, Baba wa Waisrail alipigana mieleka na Mungu akashinda. Ni wazi kabisa hiki ni kisa cha kutungwa ili kuwatukuza Waisrail ni mwigo kutoka katika jamii za Wapagani. Katika agano la kale kuna mtindo wa kumuelezea Mungu kama Mungu wa Utaifa yaani Mungu wa Waisraili peke yao. Lakini Mungu kwa Ulimwengu na viumbe sote. Dhana hii ya dini ya Utaifa katika agano la kale inafanana na dhana za kipagani ambapo kila kabila linaabudia Mungu wake. Katika baadhi ya vitabu vya Agano la kale(mfano, Yeshua) amri zinazotolewa kufanya maovu dhidi ya watu wasiokuwa Wayahudi. Mauaji ya halaiki yanamrishwa bila kujali wanawake, watoto wala wazee. Mwenendo huu wa kinyama unakwenda kinyume kabisa na sheria ya haki ya Mungu, badala yake unarandana na ushenzi wa tamaduni za kipagani za kuabudu Mungu bandia wa vita.

Mafundisho ya kipagani yalivyoongezwa katika Taurati

Katika toleo lilipita tulimalizia kwa maelezo haya; kwamba katika baadhi ya vitabu vya Agano la kale(mfano Yeshua) zinatolewa amri za kufanya maovu dhidi ya watu wasiokuwa Wayahudi. Mauaji ya halaiki yannamrishwa bila kujali Wanawake, watoto wala wazee. Mwenendo huu wa kinyama unapingana kabisa na sheria ya haki ya Mungu, badala yake unarandana na ushenzi wa tamaduni za kipagani za kuabudia Miungu bandia wa vita. Mawazo haya ya kipagani ambayo yametumbukizwa katika Taurati yumkini yana chanzo chake. Lazima tu kulikuwa Matyahudi ambao walifuata mila isiyokuwemo katika Taurati.

Wakaishika na kuitukuza mila hiyo. Kisha, baadaye, Wakatumbukiza katika Taurati mawazo yaliyotokana na mila hii ambayo wao walikubaliana nayo. Chimbuko la Mila hii linaanzia nyuma kabisa kwa makuhani wa Misri(Wachawi katika utawala wa Firauni). Kwa kweli ilikuwa ni Kabbala iliyorithiwa na Wayahudi wengi. Kabbala ilikuwa na sura ambayo iliziwezesha itikadi nyigine za kipagani kujipenyeza katika dini ya Uyahudi na kustawi ndani yake. Wadau wa Kabbalah, bila shaka wanadai kuwa Kabbalah inafafanua tu kwa kina siri zilizofichikana katika Taurati, lakini kwa kweli, kama asemavyo mwanahistoria wa Kiyahudi kuwa Kabbalah si sumu isiyotambulia ambayo imeingia katika dini ya Uyahudi na kuiathiri kabisa. Hapo sasa inawezekana kukuta ndani ya Kabbalah yale masalia ya itikadi ya ulahidi ya Wamisri wa zama za kale.

Kabala-Itikadi inayopingana na itikadi ya kuumbwa kwa ulimwengu.

Katika Qur’an, Mwenyezi Mungu anabainisha kuwa Taurati ni kitabu cha Mungu ambacho kilishushwa kama muongozo kwa Wanadamu.

Hakika tuliteremsha Taurati yenye uongozi na nuru ambayo kwayo Manabii waliojisalimisha waliwahukumu Mayahudi na Watawa na Maulamaa pia, kwa sababu walitakiwa kuhifadhi kitabu hicho cha Mwenyezi mungu, nao walikuwa mashahidi juu yake(5:44).

Kwa hiyo basi, Taurati, kama ilivyo Qur’an, ni kitabu chenye ilimu na maamrisho yanahusiana na Tauhidi inayobainisha kuwepo kwa Mwenyezi Mungu na upweke wake, sifa zake, kuumbwa kwa Wanaadamu na viumbe vingine lengo la kuumbwa kwa binaadamu na kanuni za maadili za Mwenyezi mungu kwa Wanadamu. Hata hivyo, ile Taurati ya asili haipo tena hivi leo. Tuliyonayo hivi leo ni Taurati iliyoandikwa upya na kuhujumiwa na mikono ya binaadamu. Nukta muhimu ni kuwa ile Taurati ya asili na Qur’an zinashabihiana. Mote humo, Mwenyezi Mungu anatambuliwa kama Muumba. Anatambuliwa kama aliyetakasika na aliyeepukana na upungufu wowote ule na amekuwepo bila mwanzo. Chochote kile miinghairi yake ni kiumbe chake. Yeye ndiye aliyeumba ulimwengu wote, maumbile ya angani, maada isiyo na uhai, binaadamu na vyote hai. Mwenyezi mmoja tu.

Wakati ambapo huu ndio ukweli wa mambo, kuna malelezo tofauti kabisa yanyokutikana katika Kabbala, ambayo ni sumu iliyopenya katika mishipa ya uyahudi na kuathiri kabisa mafundisho yake juu ya Mungu; maelezo hayo yanapinga na kabisa na ule ukweli unaokutikana katika ile Taurati ya asili na katika Qur’an. Katika moja ya maandiko yake juu ya Kabbala, mtafiti mmoja wa Amerika, Lance S. Owens anatoa maoni yake juu ya vyanzo hasa vya itikadi hii. Itikadi ya Kabbalah imezaa dhana kadha wa kadha kuhusu Mungu. Nyingi kati ya hizo zimetoka nje kabisa ya mtazamo wa dini. Msingi mkuu wa imani ya WanaIsraili ulikuwa ni Kalima kwamba Mungu wetu ni mmoja. Lakini Kabbala ikdai kuwa wakati Mungu akiishi katika umbile la peke yake ambalo, katika Kabbalah linaitwa Ein Sof- asiye na udhaifu-upweke huu usiojulikana laima utakuwa umeanzia katika maumbile mengi ya kiungu.

Yaani kundi la Miungu. Miungu hii ambayo mwanakabbala aliita sefiroth yaani sura au nyuso za miungu. Jinsi ambavyo mungu alitokea katika umoja usioeleweka na kuingia katika wingi ilikuwa ni siri ambayo Wanakabbalah walihangaika kuitafuta.

Ni dhahiri kuwa hii sura ya Miungu inakubaliana na madai ya Washirikina siyo tu Mungu alikuwa katika wingi katika itikadi ya Kabbala bali hata upweke usiojulikana kulichukuwa sura mbili; ya kiume na ya kike, Baba na Mama, Hokhmah na Binah. Hizi ndizo sura za mwanzo za Mungu. Wafuasi wa Kabbala walikuwa wakitumia tamathali za kijinsia kuelezea jinsi maingiliano ya kimaumbile kati ya Hokhma na Binah yalivyozaa maumbile mengine. Jambo jingine la kuchekesha katika theolojia hii ya kishirikina ni kuwa, binaadamu hawakumbwa bali kwa kiasi Fulani na wao Wanaasili ya Kiungu. Bwana Owens, mtafiti wa Kiamerika anaielezea hivi dhana hii.

Picha ya ajabu ya Mungu iliyobuniwa na Kabbalah ina sura ya Upweke na wingi. Kwa mujibu wa dhanna hii ya Kabbalh, Mungu alikuwa Adamu Kadnoni. Mtu alikuwa sawa na Mungu nkatika ile sifa ya asili ya kutoumbwa na katika lile umbile lisilofahamika. Dhana hii ya ajabu inayomuelezea Adamu kana Mungu ilishadidiwa na mafundisho ya Kabbala; thamani ya tarakimu ya majina Adamu na Yehova na Adamu walikuwa sawa, hivyo Adamu alikuwa Mungu. Kwa dai hili binaadamu wote wanapofikia daraja la juu kabisa huwa sawa na Mungu. Theolojia hii inayojumuisha dhanna ya upagani ndiyo iliyojenga msingi uliopotosha chini ya Uyahudi. Wanakabbalah wa kiyahudi wakakiuka mipaka ya kawaida ya binadaamu kiasi kwamba wakafika mahala pa kuthubutu kufanya binaadamu miunga. Mbali na ishara hivyo, kwa mujibu wa theolojia hii, sio tu binaadamu walikuwa miungu bali miungu wenyewe ni wayahudi peke yao; watu wa jamii nyingine walihesbiwa kama binaadamu tu wa kawaida. Matokeo yake ndani ya ndani ya dini ya Uyahudi ambayo, kimsingi, ilianzishwa kwa ajili ya kumtii na kumtumikia Mungu, itikadi hii potofu ilianza kumea lengo likiwa kutimiza ujinga wa Wayahudi.

Licha ya kupinga kwake na Tautrati, Kabbal ikaingizwa katika Uyahudi na hatimaye ikaanza kuihujumu Taurati. Jambo jingine la kuzingatia kuhusiana na mafundisho potofu ya Kabbala ni ule uwiano wa fikra baina yake na upagani wa Misri ya zamani.

Kama tulivyosema awali, wamisri wa zamani waliamini kuwa maada na uhai; kwa maneno mengine walikanusha kuwa maada iliumbwa pasipo chochote. Kabbalah nayo inadai vivyo hiovyo kuhusiana na binaadamu. Inadai kuwa binaadamu hawa kuumbwa na kwamba Wanajiendeashea wenyewe maisha yao.

Kulizungumzia hili kwa maneno ya sasa ni kuwa Wamisri wa kale walikuwa walahidi na kimsingi itikadi ya Kabbala yaweza kuitwa secular Humanism. Ni muhimu kukumbuka dhanna hizi mbili; ulahidi na Secular Humanism ndizo zilizozaa itikadi ambayo imetawala Duniyani kwa zaidi ya karne mbili zilizopita.

Yafaa kuuliza iwapo kuna watu ambao wameziendeleza itikadi za Misri ya kale na Kabbalh tokea katikati ya kipindi cha nyuma cha historia hadi leo hii.

Wale waliokuwa Matempla ndio hao wakawa Mafrimansori

Wakati tulipowazungumzia Matempla huko nyuma, tulisema kuwa kundi hili mahususi la Makruseda liliathiriwa na “siri” waliyoikuta  Jerusalem.

Katika kitabu Foucaut’s Pendulum Mwanafasihi mashuhiri wa Italia umberto Eco, naye anauelezea ukweli huu. Katika riwaya yake yote anasimulia kupitia vinywa vya wahusika wakuu wa riwaya yake kuwa Matempal waliathiriwa na Kabbala na kwamba wale Makabbala walikuwa na siri ambayo chanzo chake chaweza kuwa ni Mafirauni wa Misri ya kale.

Kwa mujibu wa Eco, baadhi ya Wayahudi mashuhuri walijifunza siri Fulani kutoka kwa wamisri wa zamani na baadae wakazi tumbukiza katika vitabu vitano vya kwanza Agano la kale.

Lakini siri hii ambayo ilisambazwa chinichini, ilikuwa ikijulikana kwa Wanakabbala peke yao. Baada ya kuelezea kuwa Wanakabbala waliisoma siri hii ya Misri ya kale katika Hekalu la selemani, Eco pia anaandika kuwa Matempla nao wakaisoma siri hii kutoka kwa walimu wa Kabbala mjini Jerusalem.

Siri hii ilikuwa ikijulikana kwa kikundi kidogo sana cha Waalimu wa Kiyahudi waliobakia Palestina. Matempla wakaisoma kutoka kwa Waalimunhao. Pale Matempla walipofuata itikadi mseto ya Misri ya Kabbal ndipo walipofarakana na dhehebu la Kikristo lililokuwa likiwatawala Ulaya.

Ulikuwa ni mfarakano ambapo wao walishirikiana na nguvu nyingine kubwa ya Wayahudi. Baada ya Matempla kutiwa mbaroni kwa amri ya pamoja ya Mfalme wa Ufaransa na Papa mnamo mwaka 1307, kundi hili likatokomea chini chini lakini athari zake zikabakia. Tena zikawa mbaya zaidi na zilizokuwa na uelekeo madhubuti.

Kama tulivyosema awali, idadi ndogo ya Matempla walinusurika katika kamata kamata na kukimbilia kwa Mfalme wa Scotland, utawala pekee wa Kifalme barani Ulaya ambao hakuyatambua mamlaka ya Papa.

Kule Scotland, Matempla wakajipenyeza katika jumuiya ya Well Builders na wakaitawaa. Jumuiya zikafuata ule utamaduni wa Matempla na hapo ndipo ilipopandwa mbegu ya Masoni.Kama ilivyofafanuliwa kwa kina katika kitabu kiitwacho The New Masonic order, kuanzia karne ya kumi na nane ndipo yanapoonekana masalia ya Matempla na Mayahudi kadhaa walioshirikiana nao katika vipindi mbali mbali vya historia ya Ulaya.

Bila kutoa maelezo mengi, zifuatazo ni nukta muhimu za utafiti. Katika mji wa Province nchini Ufaransa kulikuwa na kambi ya Matempla waliokimbilia nchini humo na kujificha wakati wa ile kamatakamta.

Kielezeo kingine ni kuwa huko ndiko kulikokuwa na kituo mashuhuri cha Ukabbal. Province ndipo mahali ambapo fasihi simulizi ya kabbala iliandikwa katika kitabu. Kwa mujibu wa wanahistoria, uasi wa wakulima nchini Uingereza mwka 1381 ulichochewa na jumuiya Fulani ya siri.

Watafiti wa historia ya Frmasonri wamekubaliana kuwa jumiya hii ya siri ilikuwa ya Matempla. Ule uasi haukuwa tu wa kizalendo bali pia ulilenga kulishambulia kanisa katoliki.

Nusu karne baada ya uasi huu, Kasisi mmoja wa Bohenia John Hus akaanzisha vurugu kulipinga Kanisa Katoliki. Kama kawaida, nyuma ya uasi huu walikuwepo Matempla.

Isitoshe Huss mwenyewe alikuwa akiipenda sana Kabbal. Yeye alikuwa akimpenda sana Avigdor Ben Isaac Kara. Mtu huyu alikuwa Mwalimu mashuhuri wa kiyahudi mjini Prague na pia alikuwa Mwanakabbala.

Vielezeo hivi vinaonesha kuwa ushirikiano baina ya Matempla na Wanakabbala ilileng kubadilisha mfumo wa jamii ya Ulaya. Mabadiliko haya yalijumuisha misingi ya utamaduni wa Kikristo ambao ndio utamaduni mama wa ulaya na badala ya utamaduni huu uwekwe utamaduni uliojengwa kwa misingi ya kipagani kama vile kabbal. Kisha yafuate mabadiliko ya kisiasa. Mfano ni mapinduzi ya Ufaransa na Italia.

Huko mbele tutaona vipindi vya mabadiliko ya Historia ya Ulaya. Katika kila kipindi tutakutana na ukweli kuwa kulikuwa na nguvu iliyotaka kuitenganisha Ulaya mbali kabisa na mafundisho ya Kanisa na badala yake iweke itikadi ya kisekula na hivyo izisambaratishe taasisi zote za dini.

Nguvu hii ilijaribu kuichaguzi Ulaya kuikubali itkadi iliyorithiwa kutoka Misri ya kale kupitia Kabbala. Tulikwishabainisha huko nyuma kuwa misingi ya Usekula ni dhana za Humanism na Matearialism au utu mtu na ulahidi.

Itikadi ya utu- ‘Humanism’

Yasadikiwa na wengi kuwa Humanism ndiyo itikadi madhubuti ambayo inampandikiza mtu hisia za upendo, utulivu, na udugu. Lakini kifalsafa dhana hii ina maana kubwa zaidi. Humanism ni utaratibu wa fikra ambao unaichukulia dhana ya utu kuwa ndio msingi wa lengo lake kuu.

Kwa maneno mengine unawataka watu wajitenge mbali na Mungu Muumba, kisha washughulike tu na maisha yao na utu wao. Kamusi ya kiingereza iitwayo Common Dictionary inaliainisha neon Humanism kama ni mfumo wa itikadi uliojengwa juu ya msingi wa maadili, sifa, na tabia, ambazo zinaaminika kuwa bora zaidi kwa vigezo vya binaadamu wenyewe bila kutegemea mwongozo wowote wa kiungu.

Ainisho la wazi zaidi la humanism limetolewa na wale wanaunga mkono dhana hii. Mmoja kati ya wapiga debe wakuu wa itikadi ya humanism ni bwana Carloss Lamont. Katika kitabu chake, the philosophy of humanism, mwandishi huyu ameandika; “ kwa ujumla Humanism inaamini kuwa maumbile yanatokana na mkusanyiko wa vitu halisi ambavyo msingi wake na nguvu ya maada”.

Kitabu hiki kinazidi kueleza kuwa maada ndio msingi wa Ulimwengu, na kwamba nguvu za kiungu hazipo.

Dhana ya nguvu za Kiungu kwa upeo wa Binaadam haina ushahidi. Kwamba watu hawana roho za kudumu milele yaani zisizokufa, na ulimwengu kwa ujumla hauna Mungu aliyeuumba wala Mungu wa milele.

Kama tunavyojionea wenyewe katika nukuu hizo, Itikadi ya humanism inafanana kabisa na itikadi ya Atheism, na ukweli huu unakubaliwa bila ubishi na Wahumanisti wenyewe.

Zilikuwepo ilani mbili muhimu zilizochapishwa na Wahumanisti katika karne iliyopita. Ilani ya kwanza ilichapishwa mwaka 1933 na ikapitishwa na watu wao muhimu wa wakati huo.

Miaka arobaini baadaye (yaani mwaka 1973), ilani ya pili ya Wahumanisti ikachapishwa. Ilani hii ilithibitisha ile ya awali, lakini ilitiwa nyongeza kufuatia hatua Fulani za maendeleo ambazo zilipigwa wakati huo. Maelfu ya wanafikra, waandishi wa vitabu, na wanahabari, walisaini ilani hii ya pili, ambayo inaungwa mkono na chama cha harakati za wahumanisti wa Amerika. Tukiziangalia ilani hizi tunagundua kuwa, katika kila ilani kuna msingi mmoja mkuu ambao ni dhana ya Atheism.

Dhana hiyo inasema kwamba Ulimwengu haukuumbwa, na Wanaadamu pia hawakuumbwa.. Kwa msingi huo wanaadam wanaishi kwa kujiendesha wenyewe na kwamba hawawajibiki kwa mamlaka yeyote isipokuwa kwa wao wenyewe.. Na kwamba imani juu ya Mungu inadumaza maendeleo ya watu na jamii. Kwa mfano vipengele sita vya kwanza vya ilani ya Wahumanisti ni hivi vifuatavyo;

Mosi, Wahumanisti wanaitakidi kuwa Ulimwengu unajiendesha wenyewe na haukuumbwa.

Pili, dhana ya humanism inaitakidi kwamba mtu ni sehemu ya maumbile, na kwamba ameibuka kutokana na mfumo unaojiendesha wenyewe.

Tatu, wakishikilia mtazamo wa maisha ya kiagoniki, wahumanisti wanaona kuwadhana ya pande mbili za nafsi na mwili lazima ipingwe kabisa.

Nne, itikadi ya humanism inatambua kuwa utamaduni wa kidini wa mtu na ustaarabu wake kama ulivyoelezwa na historia ni zao la hatua za polepole za maendeleo zitokanazo na mahusiano baina yake na mazingira na mazingira yake. Mtu anayezaliwa katika utamduni Fulani, kwa kiasi kikubwa, anajengeka kwa utamaduni huo. Tano, dhana ya humanism inatangaza kuwa maumbile ya ulimwengu yaliyoelezwa na sayansi ya leo yanatupilia mbali nguvu yeyote ya mbinguni kuhusiana na maadili ya binadamu. Sita, tunaamini kuwa dhana ya theism, deism, modernism na aina kadhaa za itikadi mpya zimepitwa na wakati.

Katika vipengele hivyo, tunaiona waziwazi nafasi ya falsafa ya common ambayo inajidhihirisha yenyewe kwa majina ya Materialism, Darwinism atheism na agnosticism. Katika kipengele cha kwanza dhana ya ulahidi ya uhai wa milele wa ulimwengu umeelezwa wazi. Kipengele cha pili kinasema kuwa binadamu hawakuumbwa. Hivi ndivyo isemavyo nadharia ya evolusheni. Kipengele cha tatu kinakanusha mamlaka ya Mwenyezi Mungu juu ya ulimwengu na walimwengu na kipengele cha sita kinaikataa imani juu ya Mungu. Ikumbukwe kuwa madai haya ndiyo yale yale ya zile duru zenye chuki na dini sahihi. Sababu ni kuwa dhana ya humanism ndio msingi mkuu wa hisia zote zinazopinga dini.

Hii ni kwasababu dhana hii inasema kuwa mtu ataachwa hivyo hivyo bila kuhesabiwa. Katika historia yote huu ndio umekuwa msingi wa madai ya kumkanusha Mungu. Katika aya hii ya Qur’an Mwenyezi Mungu anasema; Je anafikiri binadamu kuwa ataachwa bure? Je hakuwa tone la manii lililotonwa? Kisha akawa kidonge cha damu, kisha akamfanya namna mbili, mwanaume na mwanamke. Je! Hakuwa huyo ni muweza wa kuhuisha wafu?

Hapa Mwenyezi Mungu anasema kuwa watu hawakuachwa tu hivi hivi na anawakumbusha kuwa wao ni viumbe wake. Hii ni kuwa pale mtu anapotanabahi kuwa yeye ni kiumbe wa Mungu, basi aelewe kuwa haishi bila ya kuangaliwa

Miaka sita baada ya kuchapishwa ilani ya humanism, vita vya pili vya Duniya vikaripuka

Katika aya hii ya Qur’an Mwenyezi Mungu anasema, Je! Binadamu anafikiri kuwa ataachwa bure tu (asipewe amri za Mwenyezi Mungu wala makatazo yake)? Je! Hakuwa tone la manii lililotonwa? Kisha akawa kidonge cha damu, kisha akamuumba na akamsawazisha (kuwa mtu kamili)? Kisha akamfanya namna mbili. Mwanaume na mwanamke. Je! Hakuwa hayo ni muweza wa kuhuisha wafu?

Hapa Mwenyezi Mungu anawakumbusha binadamu kuwa wao ni viumbe vyake. Pale mtu anapotanabahi kuwa yeye ni kiumbe wa Mungu basi aelewe kuwa haishi bila ya kuangaliwa bali anawajibika kwa Mwenyezi Mungu.

Dai kuwa binadamu hawakuumbwa ndio msingi wa falsafa ya humanism. Vipengele viwili vya ilani ya kwanza ya Wahumanisti vinatoa ufafanuzi wa itikadi hii.

Zaidi ya hivyo Wahumanisti wanashikilia kuwa sayansi inaunga mkono madai haya. Lakini ni waongo wakubwa.

Tokea ilani yao ya kwanza ilipochapishwa, hoja mbili ambazo wanahumanisti wamezitoa kama hakika za kisayansi, kwamba ulimwengu ni wa milele na wa kievolusheni, zote zimevunjiliwa mbali.

Dhana kwamba ulimwengu ni wa milele ulivunjiliwa mbali na mlolongo wa vumbuzi za angani zilizofanywa wakati ilani ya kwanza ya wanahumanisti ilipokuwa inaandikwa.

Vumbuzi kama vile ulimwengu kutanuka, chanzo cha mionzi ya angani na mahesabu ya uwiano ya Haidrojeni hadi Helium, zimethibitisha kuwa ulimwengu ulikuwa na chanzo chake na kwamba ulitokea kwa mlipuko mkubwa- Big Bang takriban miaka bilioni 15 au 17 iliyopita.

Ingawa wale wanashabikia falsafa ya kihumanisti na ya kilahidi walikataa kuikubali nadharia ya Big Bang lakini hatimaye walishindwa vibaya sana kutokana na ushahidi wa kisayansi ambao umejitokeza.

Jamii ya wanasayansi hatimaye ikaikubali nadharia ya Big Bang kwamba ulimwengu ulikuwa na chanzo chake. Hivyo, Muatheisti Anthony Flew alilazimika kukiri hivi;

….Sasa nitaanza kukiri kuwa Muatheisti lazima atatizike kwa hizi fikra za sasa za maumbile. Kwani inaonekana kuwa wanakosmolojia wanatoa ushahidi kuwa kile alichodai mtakatifu Thomas hakiwezi kuthibitishwa kifalsafa, hii ikiwa na maana kuwa ulimwengu ulikuwa na mwanzo wake.

Nadharia ya evolusheni ambayo ndio hoja kuu iliyomo katika ilani ya kwanza ya humanisti, ikaanza kupoteza nguvu miongo kadhaa baada ya kuandikwa kwake.

Inafahamika hivi leo kuwa ubabaishaji uliofanywa na wanaevolusheni na Waatheisti (na bila shaka Wahumanisti) kama vile A.I. Oparin na J.B.S Haldane katika miaka ya thelasini kuhusiana na chanzo cha uhai hauna msingi wa kisayansi.

Viumbe haviwezi kutokea kwa bahati nasibu kutokana na maada isiyo na uhai kama ilivyodaiwa katika ubabaishaji huo. Kumbu kumbu ya mabaki ya kale inaonesha kuwa viumbe hai hawakuwa hivi walivyo kutokana na hatua za mabadiliko madogo madogo bali walitokea kuwa pamoja wakiwa na sifa zao mbalimbali.

Ukweli huu umekubaliwa na wanaevolusheni wenyewe tangia miaka ya sabini. Sayansi ya viumbe hivi leo imebainisha kuwa viumbe hai hawakutokana na bahati nasibu na kanuni za maumbile bali katika kila kiumbe kuna mfumo madhubuti unaothibitisha kuwa msaniii mwenye hekima ndiye aliyeviumba. Kwa maelezo zaidi rejea kitabu kiitwacho Darwinism refuted. Zaidi ya hivyo, lile dai la uongo kuwa imani ya dini ndiyo sababu inayokwaza watu kuendelea na kuwatumbukiza matatizoni limetupiliwa mbali na ushahidi wa kihistoria. Wahumanisti wamedai kuwa kuondolewa kwa imani ya dini kutawaletea watu faraja na furaha, lakini hali ya mambo imekuwa kinyume chake.

. Vita hii ni kielelezo cha kihistoria cha misiba mikubwa iliyoletwa na itikadi za kifashisti za kisekula. Ikachipuka itikadi ya kikomunisti ya wahumanisti kwanza ilianzia kwa watu wa Urusi, kisha kwa watu wa China, Cambodia, Vietnam, Korea kaskazini, Cuba na katika baadhi ya nchi za Afrika na Latin Amerika. Ulifanyika ushenzi usio na mfano. Jumla ya watu milioni 120 waliuliwa na tawala au Jumuiya za kikomunisti. Ni dhahiri kuwa kundi la Wahumanisti wa magharibi (mabepari) nalo limeshindwa kuleta amani na furaha katika jamii zao na katika maeneo mengine ya Duniya. Kuvunjwa kwa hoja ya Wahumanisti juu ya dini pia kunadhihirika katika fani ya saikolojia. Misingi ya dhana ya Kiatheisti ilibatilishwa na matokeo ya tafiti tokea mwanzoni mwa karne ya ishirini (The Freudian myth). Patric Glynn wa chuo kikuu cha George Washington anaufafanua ukweli huu katika kitabu chake kiitwacho God, The Evidence, The Reconciliation of Faith and reason in a Post Secular World.

Lengo la  Masoni ni kujenga Duniya ya kufuru

falsafa ya kihumanisti ambayo masoni wanaamini kuwa ndiyo falsafa kuu imejengwa kwa msingi wa kumkanusha Mungu. Lakini hii inazusha swali muhimu je masoni wanaitaka falsafa hii kwa ajili yao tu  au wanataka ifuatwe na wengine pia tunapoyaangalia maandiko ya masoni tunaliona bayana jawabu la swali hili. Lengo la jumuiya hii ni kuieneza falsafa hii Duniyani kote ili kuzifutilia mbali dini zinazoamini Mungu muumba. Mathalani katika makala yake iliyochapishwa katika jarida la masoni Mimar Sinan imeelezwa hivi, “masoni hawatafuti chanzo cha fikra za maovu, haki na uadilifu nje ya ulimwengu wa kimaumbile, wao wanaamini kuwa fikra hizi zinaibuka kutoka na mazingira ya jamii ya mtu, mahusiano ya kijamii na vile mtu anavyohangaikia kwa ajili ya maisha yake. masoni wanajitahidi kueneza itikadi hii ulimwenguni kote”. Selami Isindag masoni wa ngazi ya juu wa kituruki ameandika hivi; kwa mujibu wa masoni ili kuwatoa wanadamu katika imani ya nguvu za kiungu inayotokana na maandiko ya dini, ni lazima yajengwe maadili yanayotokana na upendo kwa walimwengu.

 Katika kanuni zao za maadili masoni wamezingatia umbile la mwanadamu, mahitaji yake na maridhio yao, kanuni za maisha ya jamii na taasisi zao , hiyari, uhuru wa kufikiri na kusema mambo yote yanayojumuishwa katika maisha ya kimaumbile. Kwa sababu hii, lengo lake ni kujenga na kuboresha maadili ya utu katika jamii zote. Hapa bwana Isindag ana maana ya kuwatoa wanadamu katika maadili yanayojengwa na vitabu vya dini. Hii ni kuwatenganisha watu wote mbali na dini.  Katika  kitabu hicho hicho Isindag anafafanua lengo hili pamoja na misingi yake ya kujenga utamaduni ulioendelea;

Misingi madhubuti ya masoni ni ya lazima na inajitosheleza kujenga utamaduni ulioendelea.

Nayo ni kukubali kuwa muasisi mkuu wa Ulimwengu ni evulusheni pekee, kunanusha imani ya ufunuo, usufi na imani nyingine, kuikweza dhana ya utu na kazi. Kipengele cha kwanza hapo juu kinataka watu wakanushe kuwepo kwa Mungu. [masoni hawaamini Mungu bali wanaamini evolusheni] kipengelea cha pili kinakanusha ufunuo kutoka kwa Mungu. Na kipengele cha tatu kinatukuza dhana ya utu na dhana ya kazi [kama ilivyokuwa katika ukomunisti].Tukitafakari jinsi mawazo haya yalivyojikita katika ulimwengu wa leo, basi twaweza kujionea ushawishi wa masoni ulimwenguni.  Jambo  jingine la kukumbuka hapa ni je masoni wameziendeshaje harakati zao dhidi ya dini? Tunapoyangalia maandiko ya masoni tunaona kuwa wanakusudia kuingamiza dini hasahasa katika ngazi ya jamii kwa njia ya propaganda. Selami Isindag anatoa mwangaza juu ya jambo hili katika ibara hii ya kitabu chake; Hata tawala za kikatili mno hazikufanikiwa katika jitihada zao za kuingamiza taasisi ya dini. Kwa kweli kutumia kwao mbinu nyingi za kisiasa katika jitihada za kuielimisha jamii ili kuwatoa watu katika imani na masonge ya dini walisababisha upinzani mkali. Nyumba za ibada walizotaka kuzifunga, leo hii zimejaa tele kuliko zilivyokuwa huko nyuma na imani ambayo walitaka kuififiliza imepata wafuasi wengi zaidi. Kwa usemi mwingine tunabainisha kuwa  katika masuala yanayogusa nyoyo na hisia, marufuku na mabavu hayafai kitu. Njia pekee ya kuwatoa watu gizani na kuwaleta kwenye mwanga ni sayansi halisia na kanuni za hoja na hekima. Iwapo watu wataelimishwa kwa njia hii wataheshimu upande wa wahumanisti na kujinusuru wenyewe na imani za kibubusa.

Ili kuelewa kinachosudiwa hatunabudi kuichambua ibara hiyo kwa makini. Isindag anasema kuwa ukatili dhidi ya dini utawafanya watu wa dini wawe na ari zaidi na utaiimarisha dini yenyewe. Hivyo basi ili kuifanya dini isiwe na nguvu Isindag anaona kuwa masoni wanapaswa kuiuwa dini katika ngazi ya elimu anachokikusudia katika sayansi halisia na kanuni za hoja na hekima kwa kweli sio sayansi, sio hoja wala hekima.  Anachokikusudia yeye ni falsafa ya kihumanisti na kilahidi ambayo hutumia misamiati ya ujanja kama mbinu kama vile inavyoonekana katika nadharia ya itikadi ya Darwin. Isindagi anadai kuwa pale dhana hizi zinaposambazwa katika jamii basi wahumanisti watapata heshima yaani kitakachobaki katika dini ni yale mambo tu yanayokubaliwa na falsafa ya kihumanisti. Wao wanataka kukanusha ukweli wa msingi uliomo katika msingi wa dini ya Mungu mmoja. Kwa kifupi masoni wanataka kufutilia mbali chembechembe za imani zinazojenga msingi wa dini. Wanataka kuitweza kazi ya dini iwe kama kipengele tu cha utamaduni ambacho kinazungumzia tu fikra zake juu ya masuala ya kimaadili. Njia ya kutimiza hili, kwa mujibu wa masoni ni kusimika dhana ya kukanusha Mungu katika jamii kwa kisingizio cha sayansi na hoja.

Na hatimaye kufikia lengo lao na kuiondoa dini katika nafasi yake hiyo ya kipengelea cha utamaduni na hivyo kujenga ulimwengu kamili wa kufuru. Katika makala ya Isindag iiyochapishwa na jarida la masoni liitwalo “ Positive Science- The obstacles of mind and Mansonry” anasema matokeo ya haya yote nataka kusema kuwa wajibu muhimu wa masoni sio kuipa mgongo sayansi na hoja kukiri kuwa hii ndio njia bora kwa mujibu wa evolusheni, kueneza imani yetu miongoni mwa watu na kuwaelimisha watu sayansi halisia. Maneno ya Ernest Renan yanabeba uzito zaidi; “iwapo watu wataelimishwa na kuamshwa kwa hoja na sayansi halisia, imani za kibubusa za dini zitaporomoka zenyewe”. Lessing naye anaunga mkono wazo hili; “iwapo wanadamu wataelimishwa na kuamshwa kwa sayansi halisia ipo siku moja hawatakuwa na haja na dini”hili ndilo lengo kuu la Masoni. Wanataka kuifuta kabisa dini na kujenga Ulimwengu unaoegemeya dhana ya utu yaani wanataka kujenga mfumo mpya wa ujahili ambapo watu wamkanushe Mungu aliyewaumba na wajione wao wenyewe ni Miungu. Haya ndio makusudiyo ya kuwepo kwa jumuiya ya Frimasonri

Ulemavu wa hoja za wahumanisti juu ya Dini

Ulemavu wa hoja ya Wahumanisti juu ya Dini pia umedhihirika katika fani ya kisaikolojia. Ile hekaya ya Freud, msingi wa dhana ya ukafiri imefutiliwa mbali kuwa ni uwongo mtupu tokea mwanzoni mwa karne ya ishirini, hekaya hiyo imebatilishwa na data za uchunguzi. Patrick Glynn wa chuo kikuu cha George washington analifafanua jambo hili katika kitabu chake kiitwacho God: The Evidence, The Raconciliation of Faith and Reason in Post secular World.

Ngwe ya mwisho ya karne ya ishirini haikuuendekeza mtazamo wenye mushikeli kiakili. Muhimu zaidi ni kuanikwa hadharani kwa fikra za Freud juu ya Dini (ukiacha mambo mengi mengine) kwamba ni potofu kabisa. Utafiti wa kisayansi katika saikolojia, katika kipindi cha miaka 25 iliyopita umeonesha kuwa, badala ya kuwa bumbuwazi kama Freud na wafuasi wake walivyodai, imani ya dini ni moja ya mambo yanayowiana mno na afya ya akili na maisha ya furaha. Utafiti mmoja baada ya mwingine umeonesha uhusiano madhubuti baina ya imani na mwenendo wa kidini kwa upande mmoja, na maadili kwa upande mwingine, hasa kushughulikia matatizo kama vile vifo vya kujiua, ulevi, madawa ya kulevya, mfadhaiko, mipaka ya starehe ya ngono ndani ya ndoa. Kwa kifupi, ile iliyodhaniwa kuwa hoja ya kisayansi nyuma ya dhana ya Uhumanisti imethibitika kuwa haina ukweli, na ahadi zake zimeishia patupu.

Hata hivyo wadau wa dhana hii hawajaachana na falsafa yao, badala yake wameendelea na jitihada za kuieneza Duniyani kote kwa njia za propaganda. Hasahasa katika nyanja za sayansi, falsafa, muziki, fasihi, sanaa na sinema. Ujumbe wenye mvuto lakini wa uongo ulitungwa na wanaitikadi wa kihumanisti umekuwa ukipandikizwa kwa watu. Wimbo uitwao “Imagine” ulitungwa na Johnn Lennon, mpiga gitaa wa kundi mashuhuri la muziki liitwalo “The Beatles” ni mfano wa propaganda hizo.

Wimbo unasema; “Itakidi hakuna pepo.

 Ni rahisi tu hebu jaribu.

Hakuna Jahannamu.

Juu yetu kuna anga tu.

Itikadi watu wote wanaishi hapa tu.

Hakuna cha kuuliyana wala cha kufiya.

Na wala hakuna Dini.

Huwenda mtasema labda naota ndoto lakini siko peke yangu.

Natumai siku moja mtaungana nasi na Duniya itakuwa moja”. 

Wimbo huu ulichaguliwa kama “wimbo wa Karne”katika kura kadhaa za maonizilizopigwa mwaka 1999. Baada ya kukosa msingi wa kisayansi na wa hoja, uhumanisti unapandikizwa kwa njia za namna hii. Dhana ya humanisti haina uwezo wa kujenga hoja za kupinga Dini na ukweli, inajaribu tu kutumia mbinu za kupumbaza kama hizi. Pale ahadi za ilani ya mwaka 1933 ya wahumanisti ziliposhindikana, ikapita miaka arobaini ambapo baada ya miaka hiyo wahumanisti wakawasilisha rasimu ya pili.

Mwanzoni mwa kitabu, lilifanyika jaribio la kuelezea kwa nini ahadi za kwanza zilishindikana. Licha ya ukweli kwamba ufafanuzi ulikuwa hafifu lakini bado Wahumanisti wakakumbatia falasafa yao. Kipengele kikuu cha manifesto hii kilikuwa kile cha kulinda msingio wa kukana Dini kwa ilani ya 1933. Kama ilivyokuwa mwaka 1933, wahumanisti bado wanaamini kuwa imani ya jadi ya Mungu mmoja, hasahasa imani ya Mungu anayesikia maombi (sala), anayedhaniwa kuwa yu hai na anawaangalia watu, akisikia na kuelewa sala zao na kuweza kuwafanyia jambo fulani, ni imani isiyo na ushahidi na imepitwa na wakati. Sisi tunaamini kuwa Dini za jadi za kibubusa au za nguvunguvu ambazo zinaweka ufunuo, Mungu, ibada au itikadi juu ya mahitaji na maisha ya binaadamu haziwasaidii kitu binaadamu. Sisi kama wapinzani wa imani hiyo, tunaanza na binaadamu sio Mungu.  Kwa kweli haya ni maelezo ya juujuu sana. Ili kuielewa Dini, kwanza mtu anahitaji akili na mafuhumu kuweza kuelewa mambo ya ndani mno. Kitu cha kwanza ni ukweli wa moyo na kuepuka chuki. Jitihada za wahumanisti kuielezea imani juu ya Mungu na ‘Dini za Mungu Mmoja’ kuwa haina msingi na imepitwa na wakati si jitihada mpya, ni mwendelezo wa dai lilelile, ambalo limetolewa kwa maelfu ya miaka na wale wanaomkana Mwenyezi Mungu.

Katika Qur’an, Mwenyezi Mungu analielezea dai hili kongwe lilitolewa na wale wasioamini. Mungu wenu ni Mungu mmoja. Lakini wale wasioamini akhera nyoyo zao zinakataa, nao wanatakabari. Bila shaka Mwenyezi Mungu anayajua wanayoyaficha na wanayoyadhihirisha. Kwa hakika yeye hawapendi wanaotakabari. Na wanapoambiwa (makafiri) “Mola wenu ameteremsha nini? Wanasema’hadithi za uwongo za watu wa zamani” Qur’an (16-22-24). Aya inabainisha kuwa sababu halisi ya wasioamini kuikataa Dini sahihi ni kiburi kilichomo nyoyoni mwao. Falsafa inayoitwa ‘humanism’ ni taathira ya nje ya kiburi hicho cha kumkana Mungu. Kwa maneno mengine ‘humanism’ sio utaratibu mpya wa fikra kama wanavyodai wale wanaounga mkono dhana hii. Ni fikra kongwe ambayo wamekuwa nayo wale wote wanaomkadhibisha Mungu kwa jeuri.

Mizizi ya dhana ya Ukomunisti katika Kaballa

Tumeona kuwa Kaballa ni itikadi ya zamani ya Misri na ikaingia na kuchanganyika na dini iliyofunuliwa na Mungu kwa WanaIsraili. Aidha tumeona kuwa msingi wa Kaballa ni welewa potofu kuwa binadaamu hawakuumbwa. Dhana ya Ukomunisti iliingia Ulaya kwa msingi wa itikadi hii ya Kaballa. Imani ya Kikristo ilijengwa kwa msingi wa imani ya kuwepo kwa Mungu, na imani kuwa Wanadamu ni waja wake walioumbwa naye. Lakini kwa kule kuenea kwa utamaduni wa Matempla sehemu zote za Ulaya, Kaballa ikaanza kuwavutia Wanafalsafa wengi. Kwa hali hiyo, katika karne ya 15 ikaibuka hii dhanna ya sasa ya “humanism” na imeacha taathira  zisizofuta katika uimwengu wa fikra wa Ulaya. Uhusiano huu wa humanism na Kaballa umeelezwa zaidi katika vitabu kadha wa kadha. Mojawapo ya vitabu hivi ni kitabu cha Mwandishi mashururi Malachi Martin, kiitwacho The keys of this Blood. Martin ni Profesa wa Historia katika chuo cha mafunzo ya uaskofu na Biblia cha Vatican- Vatican’s Pontifical Bible Institute: Yeye anasema kuwa athari za Kaballa zadhirihirika wazi kwa Wakomunisti. Katika mazingira ya kuatatanisha na kwa changamoto iliyoweka historia y awali ya Italia, ukaibuka mtandao wa jumuiya za kihumanisti. Jumuiya hizi, mwanzoni zilikuwa za siri. Mbali na usiri jumuiya hizi zilizkuwa na sifa kuu mbili.

Sifa ya kwanza ni kwamba zilipinga tafsiri iliyozoeleka ya Biblia kama ilivyodumishwa na mamlaka za kikasisi na za kijamii na pili zilizpinga misingi ya kifalsafa na kitheolojia iliyotolewa na Kanisa kwa ajili ya maisha ya kijamii na kisiasa. Kwa kifupi jumuiya za kihumanisti zilizoundwa katika kipindi hicho zilizotaka kuingiza utamaduni mpya wenye mizizi ya Kaballa ndani ya utamaduni wa kikatoliki barani Ulaya. Zilikusudiya kuleta mabadiliko ya kijamii na kisiasa. Mbali na Kaballa katika msingi wa utamaduni huu mpya pia kulikuwa na itikadi za misri ya kale. Prof. Martin ameandika. Waasisi wa zile jumuiya za Kihumanisti walikuwa Waumini wa nguvu kuu- Mwasisi mkuu wa Ulimwengu-ambaye walimwakilisha kwa sura ya Tetragramatton-neno la herufi nne YHWH..(Wahumanisti) wakaazima alama nyingine –Piramid na jicho moja linaloona mambo yote..kutoka kwenye vitabu vya Misri. Wahumanisti Wanatumia dhana ya mkuu wa ulimwengu-Great Architect of the universe; Msamiyati unaotumiwa na Masoni hadi leo. Hii inaonesha kuwa lazima yawepo mahusiano kati ya Wahumanisti na Masoni.

Alama za Misri ya kale katika maskani za Masoni

Moja kati ya mambo muhimu yanayothibitisha uhusiyano kati ya Misri ya kale na Masoni ni zile alama zao. kwa Masoni alama ni kitu muhimu sana. Masoni wenyewe hubainisha maana ya falsafa yao kwa wanachama wao kwa njia ya alama. Masoni anayepanda ngazi kati ya ngazi 33 za mamlaka ya kimasoni hujifunza maana mbalimbali za kila alama katika kila hatua. sote twajua kuwa Masonri huelezea dhana zake na maadili yake kwa njia ya alama na hadithi yaani tamthilia. Tamthilia hizi hurejea historia ya zama za nyuma. Twaweza hata kusema kuwa zinagusia hekaya za nyuma kabisa ya historia. Kwa utaratibu masonri imeonesha mambo ya kale ya mafundisho yake. Dhana za Wamisri wa zamani ndizo zinazowakilishwa na alama  hizi . Kila mahala katika maskani za masoni na mara kwa mara katika machapisho ya masoni michoro ya mapiramidi na masanamu huonekana. Iwapo tutaichagua Misri ya kale kuwa ni jamii kongwe zaidi, sidhani kama tutakuwa tumekosea. Isitoshe ule ukweli kuwa ibada, na falsafa inayokutikana katika Misri ya kale ndiyo hiyo hiyo iliyomo katika masonri, unavuta hisia zetu. Katika zama za kale za Misri ibada za awali katika hekalu la Memphis zilizodumu kwa muda mrefu, zilifanywa kwa mazingatio makubwa na shauku kubwa na zimeonesha mlingano na ibada za kimasoni. Hebu tuiangalie mifano michache ya uhusiano kati ya Misri ya kale na masoni.

Piramidi chini ya jicho; Alama mashuhuri kabisa ya masoni inaonekana katika nembo (ngao) ya Taifa la Marekani.  Katika nembo hii kuna nusu Piramidi ambapo juu yake kuna jicho ndani pembe tatu. Jicho hili ndani ya pembe tatu ndiyo alama ya kudumu inayokutwa katika maskani za masoni na katika machapisho yao yote.  Idadi kubwa ya maandiko yanayozungumzia masoni husisitiza ukweli huu. Lile Piramid chini ya jicho ndani ya pembe tatu lenyewe lina mvuto mdogo sana.  Hata hivyo piramidi hili lina maana kubwa mno ya kufahamia falsafa ya masoni. Mwandishi ya kimarekani Robert Hieronimus amendika tasnifu ya kiitikadi juu ya nembo ya Marekani ambapo ametowa maelezo muhimu sana. Anuwani ya tasnifu ya Hieronimus ni “An Historic Analysis of the Reverse of the America great seal and its relationship to the Ideology of Humanist Psychology” (utafiti wa kihistoria wa siri ya nembo kuu ya Marekani na uhusiano wake na itikadi ya saikolojia ya kihumanisti). Tasnifu yake inaonesha kuwa waasisi wa America ambao kimsingi walitumia nembo hiyo walikuwa ni Masoni na hivyo waliiunga mkono falsafa ya kihumanisti. Uhusiano kati ya falsafa hii na Misri ya kale unabainishwa na alama ya Piramidi iliyowekwa katikati ya nembo hiyo. Piramid hili linawakilisha Piramidi la Cheops moja ya minara mikubwa kabisa ya Firauni.

Maana ya nyota ya pembe sita ya Masoni;Alama nyingine mashuhuri ya masoni ni nyota yenye pembe sita iliyoundwa kutokana na pembe tatu kuwa juu ya pembe tatu nyingine.  Hii pia ni alama ya utamaduni wa Wayahudi na leo hii inaonekana kwenye bendera ya Israel. Inafahamika kuwa kwa mara ya kwanza Nabii Suleiman aliitumia kama nembo. Hivyo basi nyota ya pembe sita ni nembo ya Nabii na alama ya kiungu lakini Masoni wana dhana tafauti. Wao hawaikubali nyota ya pembe sita kama alama ya Nabii Suleiman, bali wanasema ni alama ya itikadi ya kipagani ya Misri ya kale. Makala yenye kichwa ‘Allegory and symbols in our Rituals’ [Isitiari na alama katika ibada zetu] iliyochapishwa katika jarida la Mimar Sinan, inaelezea mambo mengi kuhusu jambo hilo kama ifuatavyo; mchoro wa alama mbili za pembe tatu moja juu ya nyingine unaonesha kuwa zina thamani sawa. Alama hii inayotumiwa na Masoni inajulikana kama nyota ya Daud, ni mchoro unaotokana na alama moja ya pembe tatu kuwa juu ya alama nyingine ya pembe tatu, leo hii inajulikana kama alama ya Uyahudi na inaonekana katika bendera ya Israel lakini ukweli ni kuwa asili ya alama hii ni Misri ya kale. Nembo hii kwanza kabisa ilitengenezwa na Matempla, ambao waliitumia kama urembo katika nakshi za kuta za Makanisa yao.  Hii ni kwa sababu wao ndio walikuwa watu wa kwanza kugundua mambo muhimu kuhusu Ukristo mjini Jerusalem. Baada ya Matempla kusambaratishwa alama hii ikaanza kutumika katika Masinagogi. Lakini kwa Masonri bila shaka tunaitumia alama hii kwa maana ya jumla ya Ulimwengu mzima kwamba ilitokea katika Misri ya kale.  Kwa maana hii tumeunganisha nguvu mbili pamoja. Kwa kweli hatuna budi kuzitafsiri alama zote za masoni kwa mnasaba wa hekalu la Selemani. Kama ilivyobainishwa na Qur’an Selemani alikuwa Nabii ambaye baadhi ya watu walitaka kumpaka matope na kuonesha kwamba hakuwa Muumini wa Mungu mmoja. Katika aya hii ya Qur’an Mwenyezi Mungu anasema; “Wakafuata yale waliyoyafuata mashetani, wakadai yalikuwa katika Ufalme wa Nabii Suleiman, na Suleiman hakukufuru” [2:202].  Masoni wamejenga dhana hii kimakosa kwa kumsingizia Nabii Seleman kuwa ni muwakilishi wa itikadi za kipagani za Misri ya kale kwa sababu hiyo wanampa nafasi muhimu katika itikadi zao.  Katika kitabu chake “The occult Conspiracy” mwanahistoria wa kimarekani Michael Hoarld anasema kuwa tangia zama za kati, Suleiman (astaghfirullah!) amekuwa akisadikiwa kama “mchawi” na kwamba yeye ndiye aliyetumbukiza mawazo ya kipagani ndani ya dini ya Uyahudi!

Hoarld anaendelea kueleza kuwa masoni wanaliitakidi hekalu la Seleman kuwa ni hekalu la kipagani, na kwa sababu hiyo ni muhimu kwao. Picha hii potofu anayopachikwa Nabii Seleman, ambaye alikuwa mja mnyenyekevu na mtiifu kwa Allah (s.w) inabainisha misingi ya Masonry.

Alama ya nguzo mbili; Alama nyingine muhimu katika maskani ya Masoni ni ile ya nguzo mbili katika lango la kuingilia. Maneno “Jachin” na “Boaz” yamechongwa juu ya nguzo kwa kuiga nguzo mbili kwenye lango la hekalu la Selemani. Lakini kwa kweli Masoni hawana maana kuwa nguzo hizi ni alama ya kumbukumbu ya Seleman bali ni ishara ya mambo ya kumuhujumu Seleman. Chanzo cha nguzo hizi ni Misri ya kale. Makala yenye kichwa ‘Allegory and symbols in our Rituals’ inaeleza hivi; kwa mfano nchini Misri Horus na Set walikuwa waanzilishi pacha na washikiliaji wa mbingu.  Nguzo mbili katika maskani zetu asili yake ni Misri ya kale. Moja kati ya nguzo hizi ilikuwa kusini mwa Misri katika jiji la Thebes, na nguzo nyingine ilikuwa kaskazini katika mji wa Heliopolis. Katika lango la kuingilia hekalu la Amenta lililotengwa kwa ajili ya Ptah Mungu mkuu wa Misri kulikuwa na nguzo mbili kama zile zilizopo kwenye hekalu la Selemani.Katika riwaya za kale zinazohusu Jua nguzo hizo zinatajwa zikipewa majina ya akili na kipawa.

Istilahi za Kimisri zitumiwazo na Masoni

Katika kitabu chao, The Hiram Key, Masoni wa Kiingereza Christopher Knight na Robert Lomas, wanaonesha mizizi ya Masoni katka jamii ya wamisri wa zama zilizopita. Jambo muhimu wanalofichufua ni kuwa maneno yatumikayo katika hafla ya kumpandisha masoni ngazi iitwayo Master Mason ni; ma’at-neb-men-aa,ma’at-baa’ na. Knight na Lomas wanaeleza kuwa maneno haya, mara nyingi hutumiwa bila kuzingatia maana yake, lakini ni maneno ya Wamisri wa zama za nyuma, ambayo yana maana hii; “Great is the established master of freemasonry, great is the spirit of Freemasonry” “Aliyepandishwa ngazi ya masta Masoni juu, juu zaidi, mori wa masoni juu, juu zaidi”

Waandishi hawa wanasema kuwa neno Ma’at maana yake ni ufundi wa majengo[maboma] na tafsiri ya karibu zaidi ya neno hilo ni masonry yaani uwashi. Hii ina maana kuwa Masoni wa hivi leo bado wanaienzi lugha iliyotumika maelfu ya miaka iliyopita katika Misri ya zama hizo.

Filimbi ya wachawi ya Mozart

Mojawapo ya vitu vilivotengenezwa na Masoni ni filimbi ya wachawi magic flute, huu ni wimbo wa mtunzi mashuhuri wa nyimbo aliyeitwa Mozart. Mozart alikuwa Masoni. Ni jambo linalofahamika kuwa sehemu kubwa ya wimbo huo ina ujumbe wa Masoni. Na ujumbe huu unanasibiana kwa karibu na upagani wa Misri.  Jarida la Mimar Sinan linafafanua jambo hili kama ifuatavyo;

Yafahamika kuwa, kuna uhusiano wa wazi kati ya ibada za Misri ya zama za nyuma na ibada za Kimasoni. Hata wakijaribu vipi wale wanaojaribu kuitafsiri filimbi ya wachawi kwamba eti ni hadithi tu kuhusu mashariki ya mbali, lakini msingi wake ni ibada za Wamisri. Ni miungu wa kiume na wa kike wa mahekalu ya Misri ambao wameshajiisha utunzi wa maneno ya filimbi ya wachawi.

Minara ya pembe nne iliyochongoka juu

Alama nyingine muhimu ya Masoni ni obelisk. Huu ni mnara mrefu wa pembe nne , umechongoka kwa juu, ambao ni sehemu ya ubunifu majengo wa Misri ya kale. Piramidi ndio ncha ya mnara huu. Minara hii ilichongwa na wasanii wa uchongaji wa Misri ya kale. Kwa karne nyingi ilikuwa imezikwa chini hadi pale ilipokuja kuoenekana mnamo karne ya kumi na tisa. Ikahamishiwa kwenye miji mikuu ya nchi za Magharibi kama vile New York, London na Paris.

Mnara mkubwa kabisa kuliko yote ulipelekwa Marekani. Mpango wa kuupeleka huko ulifanywa na Masoni. Hii ni kwa sababu minara hiyo pamoja na michoro yake inadaiwa na Masoni kuwa ni alama zao halisi. Jarida la Masoni linataja mnara wenye urefu wa mita 21 uliopo New York. Mfano hai wa minara hii ni mnara uitwao Cleopatra’s needle, uliotolewa na Gavana wa Misri bw. Ismail kama zawadi kwa Marekani mwaka 1878. Mnara huu hivi sasa upo katika eneo la center park la NewYork. Sehemu yake ya chini imesilibwa kwa nembo za Kimasoni. Huu ni mnara ambao kwanza kabisa uliirikwa mnamo karne ya kumi nasita kabla ya Yesu, kwenye lango la kuingilia ndani ya hekalu la Sun god katika eneo la Heliopolis.

Hadithi ya mjane

Dhana muhimu ya utambulisho wa Masoni ni ile ya mjane. Masoni hujiita watoto wa mjane, na picha za wajane mara nyingi huonekana katika machapisho yao. Ni nini chanzo cha dhana hii? Huyu mjane ni nani? Tunapoyapekua maandiko ya Masoni, tunaona kuwa alama ya mjane kimsingi inatokana na hadithi ya paukwa pakawa ya Wamisri wa zamani za kale. Hii ni hadithi ya Osiris na Isis. Osiris alikuwa mungu wa kimila na Isis ndio mkewe. Kwa mujibu wa hekaya hii, Osiris alikuwa muhanga wa kifo cha mahaba “a victim of a crime of passion”ambapo Isis akawa mjane. Kwa hiyo mjane huyo wa Masoni ni Isis.

Makala moja katika jarida la Mimar Sinan inalifafanua jambo hili kama ifuatavyo; Hadithi ya Osiris na Isis inazungumziwa sana katika makala nyingi na katika mihadhara mingi. Ni moja ya hadithi za Misri ya kale zinazohusishwa mno na Masoni. Sifa ya kuwa kasisi wa hekalu la Isis ni ile ya mtu kuwa na uanachama wa masoni. Humo mwangaza wa jua huwa tunu muhimu ili mtu azikwe kwenye giza la mashariki, kila siku jua la asubuhi linapoanza kutua mchana, hufanya kazi ya Osiris  , kama vile Horus  kwa nuru yake kubwa, alivyochukua nafasi ya baba yake aliyeuawa. Hivyo mjane ambaye watoto wake ni sisi si mwingine zaidi ya Isis mjane wa Osiris. Tunaona kuwa masonri ambayo inajieleza kuwa imejengeka kutokana na akili na sayansi, kwa kweli ni hadithi ya paukwa pakawa iliyojaa imani za ajabu ajabu za uchawi.

Bikari  na pimamraba

Bikari (compass) na pimamraba (square) ni miongoni mwa alama mashuhuri za masoni. Bikari huwekwa juu ya pimamraba. Masoni wanapoulizwa juu ya alama hii, husema kuwa alama hiyo huwakilisha dhana za sayansi, jiometri na kipawa cha akili. Lakini kwa kweli alama hizo zina maana nyingine kabisa.

Tunaweza kuiona maana hii katika kitabu kilichoandikwa na mmoja wa Masoni mashuhuri, Albert Pike. Katika kitabu chake kiitwacho Marals and Dogmas, ameandika hivi; Pimamraba … ni alama ya kimaumbile inayowiyana na duniya hii. Ni alama ya mke na mume. Ni alama ya asili mbili ambayo hapo kale ilihusishwa na mungu,,… Braham na Maya kwa Waariyan, Osiris na Isis kwa Wamisri. Kwa vile jua ni dume basi mwezi ni jike.

Hii ina maana kuwa pima mraba na bikari , nembo mashuhuri ya masoni, ni alama ya wapagani wakiariyani  ambayo historia yake inaanzia Misri ya kale kabla ya Ukristo. Mwezi na Jua katika nukuu hiyo ya Pike ni alama muhimu katika jumuiya ya Masoni na haina maana nyingine zaidi ya kuwa kielelezo cha imani potofu za jamii za kale ambazo ziliabudu mwezi na jua.

Falsafa ya kipagani ya masoni

Hadi hapa tulipofika, tumejifunza kuwa misingi ya masoni imeegemeya itikadi ya kipagani  inatokeya Misri ya kale na kwamba huko ndiko inakofichama maana halisi ya dhana na alama za masoni. Kwa sababu hiyo, masoni wanapingana na dini zinazoamini mungu mmoja. Masonri ndio itikadi ya wahumanisti, walahidi, na wanaevolusheni.  Mwana historia wa Kiamerika, Michael Hoard anaielezea siri hii ambayo hufichuliwa kwa masoni wa ngazi za juu tu. Kwa nini Wakristo wanaikosoa Frimasonri?….. Jibu la swali hili lipo katika siri za Frimasonri. Laiti “siri hizi” zingetolewa hadharani, inatia shaka kama maana ya “siri hizo” ingeliweza kueleweka kwa wale ambao hawakuyajua mafundisho ya jamii za kichawi na dini ya kale. Kwa kweli yatia shaka kama wadau wa kawaida wa masoni wanaelewa “siri hizi” zinawakilisha nini.  Katika duru za ndani za masoni, Inner cicle of Masonry, miongoni mwa wale waliopata daraja za juu, wamo wanaoelewa kuwa, wao ni warithi wa utamaduni wa kale uliokuwepoa kabla ya Ukristo ambao ni wa zama za upagani. Tukitazama andiko la masoni wa Kituruki, tunaona kuwa wale masoni wa ngazi za juu ndio tu wenye kujua mambo ambayo wenzao wengine wanafichwa. Masta masoni Necdet Egeran anaelezea jinsi masoni wa ngazi za juu wanavyolitazama jambo hili.

Kwa upande mwingine, Frimasonri ni Shirika jingine la Wayahudi. Uanachama wa Shirika hili umegawanyika katika ngazi mbalimbali zinazoitwa “Degrees.” Ili kuingia katika kila ngazi , kuna sheria na kanuni mahususi zinazoambatana na masharti maalum. Mtu anayehusika na ngazi fulani anaweza tu kusuhubiana  na mwanachama wa ngazi hiyo hiyo na uhusiano huu hutazamwa kwa makini sana kiasi kwamba mdau anayehusiana na ngazi fulani hawezi kusikia mipango, shabaha  wala malengo ya siri ya wadau wa ngazi nyingine.

Malengo ya ngazi za juu za Frimasonri yanafichwa na kuhifadhiwa kwa siri kubwa kwenye faili nyeti mno kiasi ambacho mtu anaweza kupitisha hata maisha yake yote ndani ya shirika hili bila kuambulia kitu. Mbinu za jumuiya hii na njia za ufanyaji kazi wake ni za siri kubwa kiasi kwamba Encyclopedia Britannica ambayo ina habari nyingi juu ya masuala mengi, imelazimika kukiri kuwa ushahidi ni haba sana kuwezesha undani wa lodges kung’amuliwa. Kumbukumbu za lodge na mambo yanayoihusu “zinafichwa” kwelikweli ambapo  wale wasio wanachama hawawezi kusikia hata neno moja kuhusiana zao. Wanachama Frimasonri huwasiliana kwa mfumo maalum wa maandishi (code) na huwatambua wanachama wenzao kwa mfumo wa siri wa alama na maneno. Pia wana utaratibu wa kivyao wa kubishiana (kupigiana) hodi milangoni mwao ambapo wenyewe huweza kutambuana haraka hasa wanapokuwa katika nchi za kigeni.

Mdau Frimasonri anapofanya ziara katika nchi ya kigeni, hahitaji utambulisho rasmi kwa wadau wenzie mahala popote pale. Yeye anachohitaji ni kuwa na anuani tu kisha ule utaratibu maalum wa kupiga hodi humfanya yule aliyemo chumbani kutambua na kwenda mlangoni kumkaribisha. Katika mikusanyiko na mikutano na katika hafla ndani ya nchi mbalimbali wao hutambuana na kusabahiana bila shida yoyote na bila kusemeshana hata neno moja. Hujuana na kusalimiana kwa njia ya alama,  maneno ya siri, ishara na uchezeshajichezeshaji wa mikono na viwiliwili vyao. Kwa mfano alama yao kuu ni pembe tatu ambayo wenyewe huuita EYE.

Iwapo Masoni yupo katika mazingira ya ugenini na anataka kujua kama kuna wenzie wangapi katika hafla ya kijamii na kadhalika au kama yeye ndiye anayetaka kujitambulisha kwa masoni waliopo kwenye umati wa watu, kitu pekee anachotakiwa kufanya ni kuweka vidole vyake vya mkono katikati ya vifungo[vishikizo] vya koti lake au kizibao chake na kufanya alama ya pembe tatu kwa vidole vyake kwa upande mmoja na pindo la koti kwa upande mwingine. Wanachama wenzie wote waliopo hapo mara moja watamuitikia kwa ishara na pia kila mmoja atawajua wengine bila kusemeshana neno. Masoni hupendelea kuwaingiza katika jumuiya yao Viongozi wakuu wa nchi, Viongozi wa kiraia au viongozi wa kijeshi au Vigogo wa makampuni ya biashara ya wenyeji na wageni. Hakuna kipingamizi cha tabaka,rangi , dini wala utaifa katika kujiunga na jumuiya hiyo.

Bali viongozi wa nchi hushawishiwa zaidi na wakitiwa mkononi, huendeshwa kwa mujibu mpango uliowekwa. Wanatumiwa kwa namna ambayo wenyewe hawawezi kuyatambuwa malengo yaliyofichikana ambayo yanatimizwa kupitia kwao. Pengine kuna watu wawili watatu tu au pengine hakuna hata mmoja mwenye asili ya utaifa wa kiyahudi ambaye ni mwanachama wa umoja huu wa siri katika nchi.  Lakini jumuiya daima hutimiza malengo ya Uzayuni [mtandao wa kimataifa wa wayahudi]. Jumuiya hii kwanza ilianzishwa Uingereza mnamo mwaka 1717. muungano wa lodges zipatazo nne ukaunda Lodge kuu grand lodge mjini London pamoja mfumo mpya wa alama za siri. Kuhusiana na kazi na majukumu ya Masoni, pitio la itifaki litafichua ukweli. Haya ni maelezo yanayobainisha kila kitu, na serikali inayotaka kuinusuru nchi yake na hatari ya malengo ya chombo hiki chenye nguvu na ushawishi, basi haina njia nyingine ila kuking’olea mbali. Hapana shaka hiyo haitakuwa kazi rahisi kwani mizizi ya shirika hilo imeota ndani kabisa ya mfumo wa serikali ya nchi. Kwa kweli  mikono ya masoni ni mirefu mno.

 
   
   
5 / total 6
You can read Harun Yahya's book Ulimwengu Wa Frimasonri online, share it on social networks such as Facebook and Twitter, download it to your computer, use it in your homework and theses, and publish, copy or reproduce it on your own web sites or blogs without paying any copyright fee, so long as you acknowledge this site as the reference.
About this site | Tengeneza kurasa yako ya nyumbani | Add to favorites | RSS Feed
Mambo yote yanaweza kuynakiliwa, kuchapwa na kusambazwa kwa kurejea katika kurasa hii
(c) All publication rights of the personal photos of Mr. Adnan Oktar that are present in our website and in all other Harun Yahya works belong to Global Publication Ltd. Co. They cannot be used or published without prior consent even if used partially.
© 1994 Harun Yahya.www.harunyahya.com
page_top