Ulimwengu Wa Frimasonri

SHUSHA KITABU

Download (DOC)
Maoni

SURA ZA KITABU

< <
6 / total: 6
|
Frimasonri - Harun Yahya
Frimasonri
   

 


Masoni maana yake ni kuachana na dini

 Tunapoyatupiya macho maandiko ya Masoni, tunaona kuwa Masoni wa ngazi za juu wanaelewa mambo ambayo wenzao wa ngazi za chini wanafichwa wasiyajuwe.  Masoni wa ngazi ya juu aitwaye Necdet Egeran anafafanuwa kuwa;

Baadhi ya Masoni huelewa kuwa Mansori ni aina ya nusu-dini na nusu -Taasisi ya hisani ambapo wanaweza kujenga uhusiyano na kuyaendesha kwa utaratibu huwo.  Wengine wanadhani kuwa Lengo la Masonri ni kuwafanya watu  wawe tu wema zaidi.  Aidha wengine wanaona kuwa Mansori ni Taasisi ya kujenga maadili. Kwa kifupi wale wasiojuwa kusoma wala kuandika lugha ya Masoni wanaelewa  alama na hekaya za masoni kwa maana hii au kwa maana iliyosawa na hii.  Lakini kuna masoni wachache sana wanaoweza kujuwa undani wa mambo. 

Mansori iko tafauti kabisa na malengo hayo.  Mansori maana yake ni Elimu ya ufunuwo, kujibuwa na kuanza upya.  Maana yake ni kuachana na utaratibu wa zamani wa maisha na kuingiya katika maisha mapya na matakatifu zaidi.  Katika siri ya chimbuko la Masonri na katika msingi wa dhana ya alama, kuna msururu wa siri zinazotusaidiya kuingiya katika maisha ya ndani zaidi na kujuwa siri ya maisha yetu.  Hivyo, ni katika maisha haya ya ndani zaidi na kwa kuingiya katika maisha hayo  ndipo inapowezekana kupata elimu ya Masonri.  Hapo tu ndipo  inapowezekana kuujuwa undani na nyendo za maendeleo na mageuzi. 

Nukuu hiyo inabainisha kuwa japo Masoni wachache wa ngazi ya chini huwona kuwa masonri ni Taasisi ya hisani na ya kijamii, lakini kwa kweli inahusiyana na siri za maisha ya Mwanadamu yaani haiba ya nje ya mansori kama shirika la hisani na la kijamii, kwa kweli ni mwavuli tu wa kufunika falsafa ya jumuiya hiyo. Kwa uhalisi wake Mansori ni shirika lenye shabaha ya kushajiisha falsafa fulani kwa wadau wake na kwa watu wengine kwa kutumiya mfumo maalumu.  Kama tulivyosema mwanzoni, kipengele cha msingi cha falsafa hii ambacho kimepandikizwa kwa masoni kutoka tamaduni za kipagani hasa hasa upagani wa Misri ya kale ni Ukafiri.

Ukafiri katika vitabu vya Mansori

 (1)  Imani juu ya maada inayojitegemeya

Mansoni wa hivi leo , kama walivyokuwa mafirauni, makuhani na matabaka mengine ya jamii ya Misri ya zamani, huamini umilele wa maada na dhana ya maada kutoumbwa na Mungu Muumba, na kwamba kutokana na maada hii isiyo na uhai, viumbe hai vikazuka kwa bahati nasibu.  Katika maandiko ya Masoni, tunapata maelezo ya kina ya vipengele vya msingi vya falsafa ya ukafiri.  Katika kitabu chake, Mason luktan Esin meleler (Funuwo za Frimasonri, Masta Mason Selami Isindag ameandika kuhusu falsafa hii ya ulahidi:

“Anga lote, angahewa, Nyota, Silika, vitu vyote vilivyo hai na visivyo hai vinajengwa na Atomu.  Wanadamu si chochote bali ni mkusanyiko tu wa Atomu uliojizukiya wenyewe kibahati bahati.  Ule Urari katika mtiririko wa umeme kwenye  Atomu ndio unaouhakikishiya uhai viumbe hai.  Pale urari huu unapovurugika, ndipo tunapokufa, tunarejeya udongoni na kusambazika katika chembechembe za Atomu.

Yaani sisi viyumbe tumetokana na Atomu na nishati, na tutarudi tena katika maada na nishati.  Mimeya hutumiya Atomu zetu na viumbe vyote hai tukiwemo sisi hutumiya mimeya.  Kila kitu hutengenezeka kwa vitu hivyo.  Lakini kwa vile ubongo wetu umekuwa zaidi ya wanyama wote, akili ikazuka.  Tukiyangaliya matokeyo ya uchunguzi wa kisaikolojiya,  tunaona kuwa maisha ya utu wetu wenye sehemu tatu za hisiya, akili na hiyari ni matokeo ya utendaji kazi madhubuti wa seli katika tabaka la nje la ubongo na homoni.

 ....Sayansi yakinifu inakubali kuwa hakuna kilichopata uhai kutokana na hamna kile na hakuna kitakachotoweka kabisa kabisa.   Kwa hiyo yaweza kuhitimishwa kuwa hakuna muweza yeyote ambaye watu wanahitaji kumshukuru na kuwajibika kwake.

Ulimwengu huu ni mkusanyiko tu wa nishati isiyo na mwanzo wala mwisho.  Kila kitu kinazalishwa kutokana na mkusanyiko huu wa nishati, huibuka na kufa lakini hakitoweki moja kwa moja.  Vitu hubadilika na kubadilika hali na muundo. Hakuna mambo kama vile kifo au kutoweka; Yapo tu mabadiliko yanayoendeleya daimadumu, mabadiliko ya hali moja kwenda nyingine na mabadiliko ya muundo wa kitu. Lakini ni vigumu kulifafanuwa jambo hili kubwa  na ni vigumu kufafanuwa siri za ulimwengu kwa kutumiya kanuni za kisayansi.   Lakini fafanuzi nyingine zaidi ya zile za kisayansi ni yale maelezo yatokanayo na njozi tu, imani tu ya kibubusa na tena ni Imani ya kipumbavu.  Kwa mujibu wa sayansi yakinifu na hoja ya kiyakili, hakuna roho inayotengana na mwili. 

Hapa msomaji ataona fikra zinazofanana kabisa na zile za vitabu vya wanafikra wanaokanusha Muumba kama vile:  K. Marx , F,. Engels, B. I. Lenin, G.Politzer, C.Sagan na J. Monod.   Wote hawa wanaamini dhana ya msingi ya ulahidi kuwa ulimwengu umekuwepo wakati wote.  Maada ndiyo muhimili pekee wa maisha. Wanadamu wanajengeka kwa maada na hawana roho.  Maada ndiyo iliyomjenga mtu ndani na nje na uhai ukatokeya kwa bahati nasibu.  Ni sahihi kutumiya neno dhana kwani kinyume na dai la Isindag kuwa maelezo haya yanatokana na sayansi yakinifu na hoja ya kiakili, fikra zote hizi zimebatilishwa (zimefutiliwa mbali) na vumbuzi za kisayansi katika nngwe ya pili ya karne ya Ishirini. 

Kwa mfano nadhariya ya mlipuko mkuu inayokubalika katika duru za kisayansi kuwa ni sahihi, inabainisha kisayansi kwamba ulimwengu uliumbwa kutokana na hamna mamiliyoni ya miyaka iliyopita. Kanuni za ‘Thermodynamics’  zaonesha kuwa maada haina uwezo wa kujipangiliya yenyewe na kwamba Urari na mpangiliyo uliyopo ulimwenguni ni matokeyo ya kazi ya uumbaji iliyofanywa kwa nguvu yenye utambuzi. Kwa kule kubainisha kwake usanii wa kuajabisha katika viumbe hai, Baiolojiya inathibitisha kuwepo kwa Muumba aliyeumba vyote1.   Katika makala yake moja, Isindag anazidi kufafanuwa kwamba, kwakweli Masoni ni Wakanusha Mungu na kwa hivyo ni wapinzani wa Dini zinazoamini Mungu na kwamba wanatumiya dhana ya Great Architect  Of the  Universe kwa maana ya Evolusheni ya Maada:

Kwa kifupi sana, nataka kugusiya kanuni na dhanna fulani zinazofuwatwa na Masoni:  Kwa mujibu wa Masonri, uhai huwanza na seli moja, inayojibadilsha na kugeuka kutoka hali moja kwenda nyingine na kuendeleya hivyo hivyo hadi kuwa mtu.  Chanzo, au sababu, au lengo au mazingira ya mwanzo huu hayawezi kufahamika. 

Maisha hutokana na mchanganyiko wa maada na nishati na kisha hurejeya tena katika vitu hivyo.  Anasema endapo tutakubali kuwa Great Architect of the Universe ndiyo msingi mkuu na ndiyo upewo usiyo ukomo wa wema na uzuri, na kuwa ndiyo kilele cha evolusheni, na kuwa ndiyo hatuwa yake kuu kabisa na ndiyo lengo ambalo wanadamu wahangaike kuliendeya, na kama hatulipi sifa ya umbile, basi twaweza kuepukana kabisa na itikadi za kibubusa.  Kama tuonavyo, moja ya misingi mikuu ya falsafa ya Masoni ni kwamba vitu hutokana na maada na hurejeya tena katika maada. Muhimu katika mtazamo huu ni kuwa, Masoni hawaioni falsafa hii kama ipo kwa ajili yao tu; bali wanataka kusambaza mawaza haya katika jamii zote.  Isindag anaendeleya;

Masoni aliyepata mafunzo kwa misingi ya itikadi hizi huikubali dhima ya kuelimisha watu... Na kuwaadilisha kwa kuwafundisha misingi ya hoja na sayansi yakinifu.  Kwa utaratibu huwo, Masonri huenezwa kwa watu, hufanyakazi kwa niyaba ya watu licha ya watu wenyewe kuwepo. Maneno haya yanabainisha vipengele viwili vya jukumu la Masoni katika jamii: 

Mosi, chini ya mwavuli wa Sayansi yakinifu na hoja, Masoni hujaribu kupandikiza katika jamii falsafa ya kilahidi ambayo ni dhana ya Misri ya kale.  Pili, wanakusudiya kufanya hivi bila kujali  watu.  Yaani hata kama jamii inaamini Mungu na haina utashi wa kuikubali falsafa ya kilahidi, Masoni watakazana tu kufanya jitihada za kuubadili mtazamo wa watu juu ya ulimwengu bila ridhaa yao. Kuna jambo muhimu ambalo hatuna budi kulitiliya maanani hapa.  Lugha ambayo Masoni huitumiya ni ya ghiliba.  Katika maandiko yao hasa hasa yale yanayolengwa kwa watu wa jamii nyingine, huwa wanatumiya lugha inayokusudiya kuonesha kuwa falsafa yao haina ubaya, ni ya busara na stahamala. 

fano wa hili waweza kuonekana katika nukuu ya hapo juu.  Katika dhana ya kuwabadilisha watu kwa kuwafundisha misingi ya hoja na sayansi yakinifu.  Kwa kweli falsafa ya Masoni haihusiyani kabisa na sayansi wala hoja.  Yenyewe inahusiyana na dhana ya kale ambayo inavuma kwa sura ya sayansi.  Si lengo la Masoni kuwaadilisha watu bali kusudiyo lao ni kupandikiza watu falsafa yao.  Kwa kukamiya  kwao kuwa watafanya hivyo hata bila ya ridhaa ya watu, tunaona kuwa wao si watu wenye stahamilivu.  Ikiwa ni sehemu ya itikadi zao za kilahidi, Masoni wanakanusha kuwepo kwa roho na maisha baada ya kifo.  Masoni hawaamini kuwepo kwa roho ya binadamu na wanapinga kabisa imani ya kuwepo kwa maisha mengine baada ya kifo. 

 
   
    
6 / total 6
|
You can read Harun Yahya's book Ulimwengu Wa Frimasonri online, share it on social networks such as Facebook and Twitter, download it to your computer, use it in your homework and theses, and publish, copy or reproduce it on your own web sites or blogs without paying any copyright fee, so long as you acknowledge this site as the reference.
About this site | Tengeneza kurasa yako ya nyumbani | Add to favorites | RSS Feed
Mambo yote yanaweza kuynakiliwa, kuchapwa na kusambazwa kwa kurejea katika kurasa hii
(c) All publication rights of the personal photos of Mr. Adnan Oktar that are present in our website and in all other Harun Yahya works belong to Global Publication Ltd. Co. They cannot be used or published without prior consent even if used partially.
© 1994 Harun Yahya.www.harunyahya.com
page_top