Nani Mwenyezi Mungu?

SHUSHA KITABU

Download (DOC)
Maoni

SURA ZA KITABU

< <
2 / total: 5
Nani Mwenyezi Mungu? - Harun Yahya
Nani Mwenyezi Mungu?
   
Muujiza katika Uumbaji wakeUtangulizi

Wengi miongoni mwa watu, kwa kujidhani kuwa hawana wanayepaswa kuwajibika kwake katika maisha yao ya kila siku, wameshindwa kutafakari juu ya muujiza na maajabu ya ukubwa wa Ulimwengu wanaoishi. Lakini hata kama wangaliweza kufanya hivyo, wasingaliweza kuuzingatia ukubwa huo ingawa kutafakari kwao kungaliwafikisha kuukiri ukweli unaojidhihirisha katika umbile la Ulimwengu kuwa umeumbwa na Muumbaji Hodari, Fundi, Mwenye uwezo usiyomithilishwa, na Hekima iliyopindukia uwezo wa kufikiri alionao Mwanaadamu.

Tuchukue upana wa mji mkubwa mmoja ambao watu wanaishi, tuuangalie kutoka upande mmoja hadi mwingine. Itatudhihirikia kuwa upana huu ni mkubwa mno. Labda tutumie njia nyingine katika kuelewa jambo hili. Tujaalie tumeweza kusafiri kutoka upande mmoja wa nchi yetu hadi mwingine, yaani kutoka mashariki hadi magharibi, hiyo piya haitaweza kutusaidia bali tutashangazwa tu na ukubwa wa eneo la nchi! Huu ni mfano mdogo wa kututia fikirani. Yawezekana wengi kama si wote, wameshasafiri kwa magari ya mabarabarani au ya relini kwenda sehemu za mbali ndani au nje ya nchi. Hebu zivutwe fikira juu ya suala moja muhimu, nalo ni hili. Hivi kuweza kusafiri kuzunguka sehemu zote za Dunia kwaweza kusaidia kuuhisi ukubwa wa Ulimwengu? Jawabu litakuwa hapana. Hiyo ni kwa sababu ukubwa wa Dunia unachukua nafasi iliyo sawa na vumbi kwa kulinganisha na ukubwa wa Ulimwengu huu ambao nao ni sehemu tu katika vile vilivyoumbwa na Mwenyezi Mungu. Ametukuka Mwenyezi Mungu, Mbora wa kuumba!

Sayari hii ya Dunia ni kijitone tu ikilinganishwa na ukubwa wa Ulimwengu wote. Mazingatio yetu yaende pia kwenye umbile la ardhi yetu hii ambayo nayo ni kama kijivumbi tu katika Ulimwengu huu. Wanaadamu wanaendesha mambo yao wakiwa katika kijitone hiki kilichopo Ulimwenguni. Barabara zipitazo zimejengwa kwenye duara hili linalojizungusha lenyewe na kulizunguka jua kwa kasi kubwa sana. Dunia inapojizungusha yenyewe hupatikana usiku na mchana katika saa ishirini na nne. Na inapolizunguka jua kwa muda wa siku 365, unapatikana mwaka mmoja. Iwapo mtu atachukua mawe au ‘matoi’ ya magari kisha akayaweka juu ya mpira aangalie iwapo mawe au ‘matoi’ hayo ya magari yataweza kutuliya hapo juu, kwa hakika atabaini kuwa hayataweza kukaa, yataanguka. La kuzingatia hapa ni jinsi wanaadamu, wanyama na viumbwa vyengine vinavyoweza kukaa siku nzima, juma zima, mwezi mzima, mwaka na miaka juu ya duara hili la sayari ya Dunia lenye kuzunguka kwa kasi kubwa isiyoelezeka, viumbwa hivyo vikiendesha shughuli mbali mbali na kwa furaha bila hata kuanguka! Kwa kweli hayo ndiyo maajabu yenyewe. Je ni namna gani jua linatoa mwanga. Mwanga unaoonekana usingalikuwepo bila ya kuwepo duara hili kubwa ajabu mfano wa yai. Je, bila ya jua ingaliwezekana kufanya shughuli mbali mbali? Kwa kweli isingaliwezekana! Isingaliwezekana kufanyika chochote kwa sababu bila ya jua, kusingekuwa na kitu chochote chenye uhai katika sayari hii ya Dunia. Si mimea, miti, ndege, au mauwa yapendezayo bali hata baba, mama, mtoto, kaka, dada, ndugu, jamaa na marafiki wasingalikuwepo katika Dunia hii.

Mifano hii miwili ya Jua na Dunia yaonesha umuhimu wa maumbile yaeleayo angani katika maisha yetu. Ipo mifano mingi mizuri ya aina hii itakayotolewa katika mada za somo letu hili refu na zuri. Ni somo lenye kuvutia kwa kuwa limelenga kuujua Ulimwengu, limelengwa kumuwezesha msomaji kumjua Muumba Aliyeumba. Ili kuweza kufaidi zaidi, ingefaa maudhui haya yasomwe kwa pamoja baba, mama na marafiki kwa kuwa ni maudhui ambayo mbali ya kusisimua sana, pia yanahitaji mjadala na tafakuri ya pamoja. Kadiri maudhui haya yatakavyosomwa kwa makini zaidi, ndivyo Mwenyezi Mungu, Muumba, Atakavyofahamika Yeye ni nani na ndivyo utakavyofahamika uumbwaji wa Ulimwengu wetu huu na viumbwa vingine. Pia itafahamika lilivyoumbwa jua, mwezi, Dunia na kila kilichomo Ulimwenguni. Somo hili limelengwa kujibu maswali Nani Mwenyezi Mungu, vipi na kwa nini aliumba ili kuchochea mazingatio. Tukiyazingatia kwa makini tutakayojifunza katika maudhui ya kitabu hiki, mienendo yetu itabadilika kwa kuwa itaongozwa na Mwenyezi Mungu katika kila hatua na kwa hivyo itafanya Wanaadamu waishi kwa furaha na amani wakifuata mfumo wa maisha wa Mwenyzi Mungu.

Harun Yahya

Mwandishi


    
2 / total 5
You can read Harun Yahya's book Nani Mwenyezi Mungu? online, share it on social networks such as Facebook and Twitter, download it to your computer, use it in your homework and theses, and publish, copy or reproduce it on your own web sites or blogs without paying any copyright fee, so long as you acknowledge this site as the reference.
About this site | Tengeneza kurasa yako ya nyumbani | Add to favorites | RSS Feed
Mambo yote yanaweza kuynakiliwa, kuchapwa na kusambazwa kwa kurejea katika kurasa hii
(c) All publication rights of the personal photos of Mr. Adnan Oktar that are present in our website and in all other Harun Yahya works belong to Global Publication Ltd. Co. They cannot be used or published without prior consent even if used partially.
© 1994 Harun Yahya.www.harunyahya.com
page_top