Nani Mwenyezi Mungu?

SHUSHA KITABU

Download (DOC)
Maoni

SURA ZA KITABU

< <
3 / total: 5
Nani Mwenyezi Mungu? - Harun Yahya
Nani Mwenyezi Mungu?
   
Muujiza katika Uumbaji wakeSura ya Kwanza Uumbaji

Tunajifunza nini tunapotumia neno “uumbaji” wakati tukielezea kitu kinachoitwa kuwepo kutokana na kisichokuwepo. Tunachojifunza kuwa, ni Mwenyezi Mungu peke yake ndiye anayekifanya kitu kiwepo kutokana na kutokuwepo. Ingawa inafahamika kuwa watu nao kadhalika huweza kuunda kitu kisichokuwepo kikawepo kama vile kuchora picha za watu na wanyama, wakaweza kuunda meli na majahazi na wanaunda magari, hata hivyo wanafanya hayo kwa kutumia taswira au malighafi inayopatikana katika Ulimwengu huu na kwa kuigiza vitu ambavyo tayari vipo. Kwa mfano, wanatengeneza nguo wakitumia malighafi ya pamba au sufu za wanyama. Au wanaunda magari, meli na ndege wakitumia malighafi ya vyuma ambavyo madini yake ipo tayari, kadhalika wanaigiza miundo ya vyombo hivyo kutokana na maumbile ya wanyama, ndege na wadudu ambao tayari Mwenyezi Mungu alikwisha waumba. Kwa hakika mwanaadamu haumbi ila anaunda,yaani anaunganisha na kuigiza vilivyopo.

Kuumba ni kukifanya kitu kiwepo kutokana na kutokuwepo, bila ya kuigiza mahali. Bila ya kuigiza mahali, Mwenyezi Mungu Ameumba Ulimwengu ikiwemo hii Dunia na vyote. MwenyeziMungu Amemuumba mtu wa kwanza kabisa Adamu bila ya kuigiza chochote. Alimuumba kwa udongo ambao tayari alikwishauumba. Mwanaadamu ni kiumbe aliyeumbwa baadaye sana, ni baada ya viumbwa vyote kuumbwa,kama tunavyofahamishwa katika Qur’an:

“Hakika ulipita muda mrefu sana Mwanaadamu hakuwa kitu kinachotajwa”. (76:1)

Wanadamu wanaiga tu katika vile ambavyo tayari Mwenyezi Mungu Amekwishaviumba, hata wanapochora picha huigiza picha za vile vilivyokwishaumbwa. Watu wanapochora picha basi picha hizo zitakuwa ama juwa, milima, miti, bahari au watu, hawawezi kuchora kitu kisichokuwepo. Isingaliwezekana kuchora picha ya mti iwapo mchoraji hangekuwa ameuona mti tangu azaliwe. Mtu asiyeona kabisa tangu azaliwe si aghlabu kuchora kwa kuwa hana taswira ya maumbile kichwani kwake. Atakachokijua ni labda jua ambalo hulisikia kuwa ni la duara lenye mwanga wenye joto kubwa. Yeyote yule ambaye hajapata kuona tangu azaliwe itokee ghafla macho yake yafunguke aone, kwa kweli hataweza kuwajua kwa sura hata ndugu zake wa karibu mpaka labda wazungumze asikiye sauti zao. Iwapo watakaa kimya hataweza kuwajua sura licha ya kuwa amekuwa akikaa, kuongea au kucheza nao siku zote. Kwa nini, kwa sababu hakuwa akiwaona. Vivyo hivyo mtu hawezi kuvijua vitu ambavyo hajaviona kabisa, kwa sababu hiyo hataweza kuchora picha zake. Lazima kwanza ziwepo taswira kichwani ndipo mtu aweze kuchora. Kwa mifano hii tunaona kuwa ni Mwenyezi Mungu tu mwenye uwezo wa kuumba kitu bila kuigiza chochote.

Katika mada hii tumejifunza:

Kumbe hapakuwa na Ulimwengu kabla ya Mwenyezi Mungu hajauumba.

Mwenyezi Mungu ndiye Aliyeumba kila kitu bila ya kuigiza mahali.

Wanaadamu hawaumbi ila huunda, yaani huigiza katika vile ambavyo tayari Mwenyezi Mungu Ameviumba.

Mwenyezi Mungu ameufanya Ulimwengu uwepo kutoka kwenye ombwe tupu aliloliumba.

Mbingu saba ni nini?

“Basi akazifanya Mbingu saba katika siku mbili, na kila uwingu akaufunulia kazi yake. Na tumeupamba uwingu wa karibu yenu huu kwa mataa na kuulinda. Hiki ndicho kipimo cha Mwenye nguvu, Mwenye kujuwa(41:12).

Wengi hustaajabishwa na uzuri wa anga lenye nyota na miezi inayong’ara. Kwa uzuri huo, wengi wamekuwa wakidadisi juu ya umbile hilo. Neno Mbingu ambalo limetumika katika aya nyingi, moja ya maana zake ni anga. Neno hilo pia lina maana ya maumbile makubwa ambayo Mwanaadamu hajafikia kiwango cha elimu ya kuyajua zaidi, ambayo kwa mujibu wa Qur’an yameumbwa kimatabaka moja likiwa juu ya jiingine. Matabaka yote yamelifunika duara la Ulimwengu:

“Ambaye Ameumba Mbingu saba zilizo tabaka tabaka..(67:3).

“Na tukajenga juu yenu saba madhubuti”(78: !2)

Na bila shaka sisi tumeipamba Mbingu ya karibu kwa pambo la nyota. Na kuilinda na kila shetani asi(37:6-7)

Ulimwengu ni mkubwa ajabu, umekusanya maumbile mengi ambayo ni pamoja na miezi, vimondo, nyota zenye mkia, sayari ikiwemo Dunia na angahewa yake, nyota kubwa zenye kuwaka na zisizowaka, matrilioni ya Magalaksi(Magimba) na mengineyo tusiyoyajuwa:

“Ameumba Mbingu saba kwa siku mbili...” (Surat Fussilat 12).

...Na tumeupamba uwingu wa karibu yenu huu kwa mataa na kuulinda...(41:12)

Anga linaloizunguka ardhi huitwa angahewa nalo lafahamika kama Mbingu ambapo utafiti umeng’amua kuwepo kwa matabaka saba yaliyoizunguka ardhi na vilivyomo ndani yake. Kwa kutumia tafsiri hii, anga la Dunia ambalo huitwa angahewa, nalo lina tabaka saba:

“Mwenyezi Mungu ni yule ambaye ameziumba Mbingu saba na ardhi kuwa mfano wa hizo. Amri zake zinashuka humo ili mjuwe kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye uweza juu ya kila kitu, na kwamba amekizunguka kila kitu kukijuwa”(65:12).

 

Kuumbwa kwa Ulimwengu

Maumbile yaonekanayo angani yote yana uhusiano mkubwa yakiwa yamedhibitiwa katika mtandao mmoja unaoitwa Ulimwengu. Ulimwengu huu ni sehemu tu ya maumbile ya Mwenyezi Mungu kama zilivyo Mbingu saba, Arshi, Pepo, Moto, viumbwa na maumbile mengine mengi anayoyajua Mwenyewe Mwenyezi Mungu yaliyo nje ya duara la Ulimwengu huu:

“Vinamuomba Yeye kila vilivyomo Mbinguni na Ardhini; muda wote Yeye yumo katika mambo(mengine mengine)”(55: 29).

Duara hili tuishilo lenye umbile mithili ya yai ni kichembe tu cha maumbile mengi na makubwa yaliyomo Ulimwenguni. Hii ni sayari iitwayo Dunia au ardhi ambayo ni ndogo sana kuliko hata baadhi ya sayari zilizo karibu yake. Kwa mfano kimpangilio, sayari zilizo katika mfumo wa jua letu hili, kutoka Dunia, inafuata sayari ya Maazi, halafu sayari ya Jupita. Hii sayari ya Jupita ni kubwa kwa zaidi ya mara 318 kuliko Dunia, ikiwa na kipenyo chenye kulizidi umbile la Dunia kwa mara 11. Ukubwa wa sayari hii ya Jupita si wa bure bure tu, bali kwa ujuzi mkubwa alionao Mwenyezi Mungu, sayari hiyo husababisha uvutano kati yake na njia ipitayo Dunia yetu katika kulizunguka jua, mzunguko ambao hutupatia miaka. Uvutano kati ya mduara huo wa njia ya Dunia na duara la Jupita, hufanya Dunia isitoke nje ya mzunguko wake. Kadhalika, kwa utaratibu wa uumbaji wa Mwenyezi Mungu, jua ndilo liwezeshalo kuwepo kwa uhai katika maisha haya ya Dunia. Inafahamika kuwa bila ya jua hakitawezekana chochote katika sayari hii. Kwa hiyo, Mwenyezi Mungu Ameumba maumbile yote kwa uwiano na ulingano uliofungwa chini ya mtandao mmoja wa kila umbile au kiumbwa kimoja kutegemea kingine kwa namna ya ajabu kabisa. Ametukuka Mwenyezi Mungu Muumba wa Ulimwengu na vyote. Yawezekana kila mtu akawa ameshajiuliza maswali kadhaa yenye kustaajabia Ulimwengu huu usio na mwisho ulivyotokea? Namna gani Dunia, jua, mwezi na nyota zing’arazo usiku zilivyotokea kwa mara ya mwanzo kabisa? Hivi anafahamika yule Aliyeumba Ulimwengu huu wenye maumbizi mengi mazuri pamoja na jua hili, Dunia na mwezi wake? Hivi inafahamika nguvu na uwiano uliopo katika Ulimwengu huu unaowezesha kuwepo maisha katika sayari hii ya Dunia?

Hapo kabla hapakuwa na Ulimwengu!

Katika zama za kale sana, Mwanaadamu hakuwa na elimu ya kutosha juu ya mambo ya anga. Vifaa vilivyohitajika kufanyia uchunguzi wa anga vilikuwa duni, havikuwa bora kama ilivyo hivi sasa. Kwa hiyo wakati mwingine watu walipojaribu kuelezea chanzo cha Ulimwengu, walijenga fikira na mawazo ya ajabu kabisa. Kulikuwa na mawazo yaliyodai kuwa Ulimwengu huu ni wa milele. Kabla ya mwanaadamu kupata viona mbali na vifaa vya kuchunguzia anga, baadhi ya watu walikua wakieneza mawazo yaliyodai kuwa Ulimwengu huu hauna mwanzo na utaendelea kuwa hivyo milele!

Mawazo hayo yalikuwa hayo kwa wakati huo! Mtu anaweza kujiuliza hivi nyumba wanayoishi watu au shule wanayosoma wanafunzi ilijengwa lini? Majibu yatakuwa, ilijengwa muda, tarehe au kipindi fulani. Hata misitari hii inayosomwa katika somo hili iliandikwa muda fulani. Vivyo hivyo, kila mmoja wetu alizaliwa siku fulani ndiyo maana baadhi ya watu husherehekea siku zao za kuzaliwa kwao. Miaka inayotumika hivi sasa kwa kufuata mwendo wa jua inanasibishwa na uzawa wa Nabii Isa(a.s), kwa hiyo Isa(a.s) alizaliwa ingawa uzawa wake si ule wa kawaida wa kuhusisha maingiliano ya wazazi wawili, bali yeye alizaliwa na mama tu bila ya baba. Nabii Adamu aliumbwa, hakuwa na baba wala mama, bali aliumbwa na Mwenyezi Mungu kwa udongo kisha akapuliziwa Roho kuwa kiumbe hai(mtu). Mtume Muhammad(s.a.w), alizaliwa kutokana na wazazi wawili, baba na mama, alisherehekea siku ya kuzaliwa kwake kwa kufunga saumu. Mtume(s.a.w) alizaliwa siku ya jumatatu, kwa hiyo kila jumatatu alikuwa akifunga saumu ya Sunna. Waislamu hupaswa kumuiga Mtume Muhammad kwa kufunga funga ya sunna siku ya jumtatu. Kwa kuwa Mtume Muhammad (s.a.w) aliadhimisha siku yake ya kuzaliwa, maana yake Mtume (s.a.w.) aliumbwa kama Wanaadamu wengine na kama viumbwa vyote vya Mwenyezi Mungu. Hiyo ina maana kwamba chochote kionekanacho chenye uhai na kisicho na uhai kilikuja wakati fulani, si kwamba kimekua hivyo bila ya mwanzo. Kwa hiyo, mawazo kwamba Ulimwengu hauna mwanzo kwa sababu umekuwa hivyo, si sahihi. Mifano ifuatayo ni muhimu kwa mazingatio.

Jaalia wakati fulani asubuhi wanafunzi fulani walikwenda shule kwa kupita njia tafauti na ile wanayopita siku zote, ghafla wakaona kinyago. Je, mawazo gani watakayo kuwa nayo juu ya kinyago au sanamu hiyo? Kwa kweli wazo litakalowajia ni kwamba yupo aliyekitengeneza kinyago au sanamu hiyo, na yupo aliyeweka sanamu hiyo hapo. Sasa ikitokea mtu akasema “hapana, kinyago hicho kimekuwepo hapo wakati wote, hakuna aliyekitengeneza, watu watamfikiriaje mtu huyo!” Kwa kweli atakuwa amemshangaza kila mtu na huenda akadhaniwa mpuuzi na mjinga! Kila kazi ya usanii imefanywa na msanii, kwa hiyo kinyago kimetengenezwa na kuwekwa hapo na msanii mchonga vinyago! Wale wanaodai kwamba Ulimwengu umekuwa hivyo ulivyo bila ya kuwepo Muumba, ni watu wenye fikira finyu na upeo mdogo. Wameshindwa kujitafiti na kujitafuta walikotoka. Kinyago ni kipande tu cha mti au jiwe, lakini Ulimwengu unakusanya maumbizi yote ya anga yaliyo chini ya utaratibu maalumu na mifumo mizuri na milinganifu yenye kutatanisha sana kuliko sanamu au kinyago ambacho inaaminika kuwa kimetengenezwa na kuwekwa hapo kilipo na mtu au watu fulani. Watafiti na wachunguzi wa mambo ya anga wa leo wameweza kugundua maajabu makubwa ya anga na kisha kukiri kwamba yule anayesema Ulimwengu huu hauna Muumbaji wake ni mchache wa fikira na mtovu wa shukurani.


    
3 / total 5
You can read Harun Yahya's book Nani Mwenyezi Mungu? online, share it on social networks such as Facebook and Twitter, download it to your computer, use it in your homework and theses, and publish, copy or reproduce it on your own web sites or blogs without paying any copyright fee, so long as you acknowledge this site as the reference.
About this site | Tengeneza kurasa yako ya nyumbani | Add to favorites | RSS Feed
Mambo yote yanaweza kuynakiliwa, kuchapwa na kusambazwa kwa kurejea katika kurasa hii
(c) All publication rights of the personal photos of Mr. Adnan Oktar that are present in our website and in all other Harun Yahya works belong to Global Publication Ltd. Co. They cannot be used or published without prior consent even if used partially.
© 1994 Harun Yahya.www.harunyahya.com
page_top