Nani Mwenyezi Mungu?

SHUSHA KITABU

Download (DOC)
Maoni

SURA ZA KITABU

< <
5 / total: 5
|
Nani Mwenyezi Mungu? - Harun Yahya
Nani Mwenyezi Mungu?
   
Muujiza katika Uumbaji wakeSura ya Sita Sayari zinazozunguka kwenye mfumo wetu wa juwa

 

Pluto

Mfumo wetu wa jua ni kama duara. Kwa hiyo, jua ndilo lililo katikati. Katika maduara hayo, Pluto inakuwa katika duara ya mwisho kabisa mithili ya mizunguko ya chembe za Elektroniki inayofanya maduwara katika chembe za Atomu. Pluto ambayo awali ilifahamika kama sayari kabla ya utafiti mpya kuiondoa katika kundi hilo, ni umbile dogo kabisa na lililo mbali zaidi kutoka kwenye Jua. Kuweza kuichunguza Pluto imekuwa vigumu sana kwa Wanaanga kwa kuwa hata ile darubini kubwa kabisa ya Mwanaanga Hubble iliweza kuonesha sehemu tu ya umbile hilo dogo. Pluto imezingirwa na baridi kali sana inayoifanya iwe barafu kabisa. Kipimo cha halijoto yake kinakadiriwa kuwa nyuzi hasi za sentigredi 238 (ambayo ni sawa na nyuzi hasi 396 za Faranihait). Katika kipindi cha baridi ambapo halijoto ya Duniani hushuka hadi nyuzi hasi mbili au tatu Sentigredi( ambayo ni sawa na nyuzi hasi 28 au 26 za Faranihait), Pluto huganda kabisa. Nyuzi hasi 238 za sentigredi ni hali ya baridi kali kuizidi mara 100 ile hali ngumu kabisa ya baridi ya Duniya ambayo watu huweza kuihimili nyakati za baridi. Hali ya hewa iliyopo kwenye umbile la Pluto ikijitokeza hata kwa sekunde chache tu hapa Duniani basi hapatakuwa na uhai. Kutokea nje, Pluto inaonekana kama mpira uliosilibwa au kuzingirwa na barafu. Pluto iko mbali zaidi katika mfumo wa jua. Hapana kiumbe hai kinachoishi katika Pluto. Mwenyezi Mungu ndiye ajuaya zaidi.

Neptuni

Kutoka Pluto kulielekea jua, tunakutana na sayari iitwayo Neptuni. Sayari hii vile vile ina hali ya hewa ya barafu ambapo uso wake una halijoto ya nyuzi hasi za sentigredi 218( nyuzi hasi za Faranihait 360). Angahewa yake imekusanya gesi za sumu kwa uhai wa wanaadamu. Hii ni mbali na yale matufani mabaya sana yenye ukubwa unaofikia kilometa 2000 (Maili 1250) ambayo huanguka juu ya uso wa sayari hiyo kila baada ya saa moja. Kwa hiyo hakuna uwezekano wa kuwepo uhai katika sayari hiyo ila kwa yale ayajuayo Mwenyezi Mungu.

Uranasi

Kutoka sayari ya Neptuni kusonga mbele kidogo kulielekea jua katikati ya duara hili la mfumo wa jua, tunakutana na Sayari ya Uranas. Uranas ni sayari ya tatu kwa ukubwa katika mfumo wetu wa jua. Halijoto ya angahewa yake inakaribia nyuzi hasi za sentigredi 214(sawa na nyuzi hasi 353 za Faranihait), hii ina maana kuwa hali ya hewa ya sayari hii vile vile ni baridi kali kuweza kumfanya Mwanaadamu agande kwa muda wa sekunde moja tu. Angahewa yake imekusanya gesi za sumu ikionesha dhahiri kuwa hakuna kiumbe hai kinachoweza kuishi katika sayari hiyo, kwa kiwango cha ujuvi wa mwanaadamu

Satuni

Tukiendelea mbele zaidi kulielekea jua kutoka Sayari ya Uranasi, tunaikuta Sayari ya Satuni. Kipenyo chake ni kilometa 120,500. Ukubwa wake ni sawa na maumbile 95 yenye ukubwa wa Dunia. Hii ni sayari ya pili kwa ukubwa katika mfumo wetu wa jua. Ni sayari ya aina yake kwa kuwa imezungukwa na liduara kubwa lenye umbile la taili la baiskeli. Duara hilo lililozunguka Sayari ya Satuni limefanyika kwa gesi, majabali na barafu. Halijoto katika sayari hiyo vile vile haiwezeshi kuwepo uhai wa Mwanaadamu na viumbwa vinavyofanana na yeye. Ina nyuzi hasi za sentigredi 178 (sawa na nyuzi hasi 288 za Faranihait).

Jupita

Tukisogea mbele kulikurubia jua kutoka sayari hiyo ya Satuni, tunaikuta Sayari kubwa zaidi katika mfumo wetu wa jua inayoitwa Jupita. Kipenyo cha sayari ya Jupita ni kilometa 143,000. Kipenyo hiki kinaizidi cha Dunia kwa mara 11. Hata hivyo kipenyo cha Jupita kinazidiwa na kile cha Jua kwa mara 10 zaidi. Ukubwa wa Jupita ni sawa na maumbile 318 ya ukubwa wa Dunia. Nayo Jupita inaingia mara 1000 kwa juwa. Hali ya hewa katika sayari hii vile vile haioneshi uwezekano wa kuwepo uhai kwa Mwanaadamu na viumbwa afafananavyo ila kwa alitakalo Mwenyezi Mungu. Ina hali ya hewa ya baridi kali mno.

Maazi

Kutoka Sayari ya Jupita kuelekea kwenye Jua, inafuata Sayari ya Maazi. Maazi ni Sayari yenye ukubwa wa baina ya ukubwa wa sayari za Venasi na Dunia. Ni sayari iliyokufa isiyoweza kufananishwa sana na Dunia. Utafiti wa hivi karibuni ambao umewezesha kufikisha chombo cha anga kwenye sayari hiyo umeweza kuchimbua mchanga wake na kujaribu kuuoanisha na ule wa dunia, hata hivyo walichoweza kusema watafiti wa mradi huo ni kwamba kama udongo huo ungalikuwa na hali ya hewa ya dunia basi ungaliweza kuotesha maboga na jamii ya mamung’unya. Aidha wako katika kufikiria kubadilisha usemi wa “kuwepo uhai” badala yake kuangalia uwezekano iwapo ardhi hiyo inaweza kuruhusu mwanaadamu kuishi kwenye uso wake. Sayari ya Maazi haina uhai huu tuujuao kwa elimu zetu za maumbile. Sababu, Mosi, angahewa yake ina mchanganyiko wa sumu na hewa nyingi ya Kaboni dayoksaidi, pili, sayari hiyo haina sehemu kubwa ya maji yaliyotuwama, kupwa na kujaa au yatiririkayo kama ilivyo katika sayari ya Dunia. Tatu, halijoto katika Sayari ya Maazi inafikia nyuzi hasi za sentigredi 53(ambayo ni sawa nyuzi hasi 63 za Faranihait). Mwisho, ina kipindi kirefu cha upepo mkali wenye dhoruba na tufani za michanga, ambacho huisha baada ya miezi kadhaa. Hali ya hewa ya sayari ya Maazi haitabiriki hubadilika ghafla. Hata hivyo, kwa kuwa Maazi ni sayari inayoikaribia Dunia, zimekuwepo jitihada za Wanasayansi wa mambo ya angani, kujaribu kujuwa kulikoni kwenye Maazi, pengine kuangalia iwapo kuna uwezekano wa mtu kutoka Duniyani kwenda kuishi kwa masiku kadhaa katika sayari hiyo. Watafiti wa taasisi ya NASA tayari wameshatuma chombo ambacho baada ya safari ndefu ya Kilomita miliyoni 106 kilitua katika sayari hiyo na tangu wakati huo kimekuwa kikifanya uchunguzi, uchimbuzi na kurejesha taarifa Duniani kupitiya taasisi hiyo. Baadhi ya taarifa zilionesha kuwepo kwa hali ya unyevunyevu na mvuke ukiashiria pengine kuwepo maji hapa na pale. Hata hivyo kwa mujibu wa uchunguzi uliofanyika awali, ilionekana kuwa maji yaliyoko katika angahewa ya Maazi yangeligandishwa kuwa barafu basi yangelifikia ujazo wa mchemraba wa kilometa moja kwa upande mmoja kulinganisha na yaliyoko katika angahewa ya Duniani yenye kufikia ujazo wa mchemraba wa Kilometa 1000 kwa upande mmoja.

Dunia

Kutoka Maazi kulielekea jua, inafuata sayari ya urujuwani iitwayo Dunia. Kipenyo cha Dunia kinazidiwa kwa mara 11 na kile cha Jupita ambapo kipenyo cha Jupita kinazidiwa na cha jua kwa mara 10. Tutaitazama kwa urefu sayari hii katika sura ya mwisho ya kitabu hiki. Hata hivyo, hebu tujikumbushe nukta moja tu muhimu sana kuhusu sayari ya Dunia. Dunia yetu ndiyo sayari pekee yenye hali ya hewa na mazingira yanayowezesha viumbwa hai kuishi.

Venasi

Kutoka sayari hiyo ya Dunia ambamo Wanaadamu na viumbwa vyengine vinaishi kulielekea jua kidogo, utafiti unatupeleka hadi kwenye sayari inayoitwa Venasi ambayo ni sayari ing’arayo sana katika mfumo wetu wa jua baada ya Jua lenyewe na Mwezi. Kwa mng’aro huo, tangu zama za kale watu wameweza kuigundua sayari hiyo. Japo ipo mbali sana kama ilivyo Sayari ya Satuni ambayo watu wameweza kuifahamu vyema nyakati zote za historia ya Mwanaadamu, sayari ya Venasi imejulikana zaidi kwa ule mng’aro wake nyakati za asubuhi na jioni angani. Kinyume na sayari nyingine, hali ya hewa ya Venasi ni joto sana. Halijoto katika uso wake ni nyuzi za sentigredi 450(sawa na nyuzi 840 za Faranihait), ambayo inatosha kabisa kuyeyusha chuma. Jiografia nyingine ya sayari ya Venasi ni angahewa lake lenye tabaka zito la hewa ya Kaboni dayoksaidi. Mbali ya hilo, angahewa ya Venasi ina matabaka mengine ya asidi kilometa kadhaa katika kina chake. Hakuna kiumbe chochote kinachoweza kusalimika japo kwa sekunde moja katika mazingira haya. Kwa hiyo hali ya Sayari hii haiwezeshi kuwepo uhai kama unavyojulikana na elimu ya maumbile aliyojaaliwa mwanaadamu.

Mekyure

Kutoka katika sayari ya Venasi, kuna sayari ya Mekyure, sayari iliyo jirani na Jua. Mzunguko katika muhimili wake ni wa pole pole sana kutokana na ukaribu wake na Juwa ambapo Sayari hiyo huweza kujizungusha mara tatu tu kikamilifu katika mizunguko yake miwili ya kulizunguka Jua. Hii ndiyo sababu, upande mmoja wa sayari hiyo kuwa na joto kali sana na upande mwingine kuwa na baridi kali sana. Tafauti ya hali ya hewa kati ya usiku na mchana katika Sayari ya Mekyure ni nyuzi za sentigredi 1,000(sawa na nyuzi 1800 za faranihait). Mazingira hayo kwa hakika hayawezi kuruhusu kiumbe kilicho hai kuishi ila kwa elimu ya Mwenyezi Mungu. Utafiti kuhusu sayari hizi zilizopo angani katika mfumo wetu wa jua, unaonesha kuwa kumbe ni sayari ya Dunia tu yenye kuwezesha uhai kwa viumbwa. Sayari zote zilizobaki hazina uhai na ni maumbile yasiyo na shughuli zinazofanana na hizi za Duniani. Ni maumbile yaliyo kimya kabisa. Dunia yetu ina kila kinachohitajiwa kwa uhai wa Mwanaadamu. Ina misitu ya kijani na kirujuwani katika bahari, chanikiwiti katika mimea na nyasi. Kwa hiyo kutokeya mbali inaonekana kuwa eneo maridhawa. Wanaanga wa mwanzo kabisa kwenda mwezini walishangazwa na uzuri wa Dunia kwa jinsi walivyokuwa wakiitazama kutokea huko ikionekana yenye rangirangi za kung’ara.

Katika mada hii tumeona kuwa:

- Sayari zilizo katika mfumo wa jua kuanziya Pluto hadi Mekyure.

- Sayari hizo ziko chini ya himaya ya juwa zikizunguka katika njiya zao huku kila moja ikiwa na hali ya hewa na mazingira tafauti na nyingine.

- Sayari zote zilizoitangulia Dunia, zina halijoto kali sana, hivyo haiwezekani kuwepo uhai katika mazingira yake.

- Sayari zote zinazoifuwatiya Dunia, zina hali ya hewa ya baridi kali sana na nyingine kuzingirwa kabisa na barafu.

Sura ya Saba Maumbile mengine ya anga

Maumbile mengine ya anga yaliyo katika mfumo wetu wa jua ni pamoja na nyota yenye mkia, vijiumbile vidogo vinavyoitwa asteroyid na vimondo. Hayo ni maumbile ya anga yaliyoendelea kuwepo yakitokana na unyenyezi ambao mfumo wetu pia ulitokana nao miaka inayokadiriwa na Wanaastronomia kufikia bilioni sita iliyopita . Hii ni kwa mujibu wa hesabu zetu za Dunia.

Nyota yenye mkia

Nyota zenye mkia zimeumbwa kwa gesi iliyoshikamana barabara na vumbi. Njia zao huzifanya zipite karibu zaidi na juwa. Kadiri Nyota hiyo inavyolikurubia juwa ndivyo uso wake unavyotoa mvuke zaidi kutokana na mwanga mkali wa jua. Mvuke huu huifanya ing’are zaidi. Duara kubwa la gesi na vumbi hujitokeza zaidi katika kiini chake. Duara hili la gesi na vumbi, wanajimu, huliita Koma. Pia kuna mkia ambao nao umeumbwa kwa gesi, ukiwa umetokezeshwa nyuma ya umbile hilo.

Asteroyidi

Asteroyidi ni vijabali vidogo vinavyokwenda kasi na kuanguka huku vikitoa mwanga mkali. Vingi ya vijabali hivi huonekana katika eneo lililo kati ya sayari za Maazi na Jupita. Baadhi ya vijabali hivyo vina ukubwa unaofikia kilometa 1000(maili 620).

Vimondo

Hivi ni vijiumbile vigumu vinavyoanguka katika angahewa yetu kutoka anga za mbali. Vipande vipande vya vijabali ambavyo ni mchanganyiko wa chuma, hujitenganisha kutoka kwenye nyota na vimondo vikubwa. Wakati mwingine Dunia inapopita kwenye wingu la vumbi masalio yatokanayo huungua katika angahewa yetu. Huungua yanapoingia katika angahewa ya Dunia na kupita kasi yakiacha msitari mrefu wa mwanga yanapoelekea kuanguka. Mara nyingi hali hii hushuhudiwa nyakati za usiku. Hivi ndivyo vimondo. Wakati mwingine visipoungua kikamilifu, vimondo hivi huweza kuanguka Duniani. Vimondo vinavyoanguka katika angahewa ya Dunia wanajimu huviita Aeroliti na Meoriti. Kwa kawaida, Vimondo vinavyoingia katika angahewa ya Dunia huweza kuanguka Ardhini. Vikianguka huweza kusababisha uharibifu kulingana na ukubwa wa kimondo chenyewe. Dunia yetu imezungukwa na hatari ya kulipuliwa na Vimondo kila baada ya dakika moja, lakini Mwenyezi Mungu ameyaumba maumbile hayo kwa namna ambayo huungua na kuharibika yakiwa katika angahewa, hivyo hayawezi kusababisha hatari yoyote. Hii inaonesha ni kwa kiasi gani Rehema ya Mwenyezi Mungu ilivyo juu yetu. Ni Mwenyezi Mungu aliyeyaumba maumbile hayo na kuyadhibiti yawe makubwa au madogo, na anayeyaendesha yote na kwa muda wote kwa mpango na utaratibu maridhawa kabisa.

Katika mada hii mafunzo tuliyoyapata ni:

-Maumbile mengine ya anga yakiwemo vimondo, nyota yenye mkia na vijiumbile vingine vidogo.

- Majina yanayotumika kufahamisha sayari yanatokana na lugha ya kigiriki.

- Kwa mkosi mkubwa sana Wagiriki walizinasibisha sayari hizi na majina ya miungu yao.

- Zamani, Wagiriki walikuwa watu wanaoamini miungu mingi kila mungu wakimnasibisha na jukumu fulani.

- Sayari ya Mekyure ilinasibishwa na biashara. Kwa hiyo Mekyure ni mungu wa Kiroma anayehusika na mambo ya biashara kwa Warumi wa jadi hizo.

- Venasi ni mungu wa mapenzi. Maazi mungu wa vita, Neptuni ni mungu anayetawala bahari, Pluto ni mungu wa chini ya Ardhi,

- Jupita ni Mfalme wa miungu yote ya Kigiriki, ama Satuni na Uranusi majina ya miungu ya kale kabisa ya wahenga wa kigiriki.

Sura ya Nane Sayari ya Dunia

Mpaka karne ya 16, miaka 500 iliyopita, watu wengi walikuwa hawafahamu kuwa Dunia ni sayari. Hata hivyo utafiti na uvumbuzi wa mambo ya anga uliokuja kufanyika baadaye, ukawafahamisha wanaadamu wengi kuwa kumbe Dunia nayo ni sayari. Katika karne ya 20, wanaadamu mbali ya kujua Dunia pia ni sayari waliweza kubaini mahali ilipo na mkao wake katika mfumo huu wa jua wenye sayari tisa. Dunia ni Sayari ya tatu kutoka kwenye Jua na ni sayari ya tano kwa ukubwa katika Sayari hizo nane, kipenyo chake kinadiriwa kuwa cha ukubwa wa kilometa 12, 756. Kwa mujibu wa Wanaastronomia, Dunia inazunguka katika njia yake kwa kasi ya maili 70,000 kwa saa moja, maili 1166 kwa dakika moja na maili 19 kwa sekunde moja. Hii ni kasi kubwa mno mtu kuweza kuihisi lakini hata hivyo wanaadamu wanaendesha maisha yao katika Sayari hii inayokwenda kwa kasi hiyo kali bila ya kuhisi kama wanasafirishwa! Vile vile Wanasayansi wanaamini kwamba Dunia ina kiini chenye madini ya chuma ambacho halijoto yake ni nyuzi za sentigredi 7, 500(ambazo ni sawa na nyuzi za faranihait 13,500). Joto hili ni kubwa sana zaidi ya lile la uso wa juu wa jua. Hata hivyo kwa sababu haiwezekani kuhisi japo chembe ya joto hili kubwa sana la kiini cha Dunia, ndiyo maana watu wanaweza kuishi na kuendesha shughuli zao za kila siku bila ya kuhisi ukubwa wa joto hilo. Hii inatokana na gamba la Dunia kuwakinga na kuwahami na joto hilo kubwa ambalo lingeweza kuwayeyusha mara moja. Ni kutokana na Rehema za Mwenyezi Mungu, Dunia imeumbwa na gamba hilo liwezalo kukinga nguvu ya joto ya kiini cha Dunia isiweze kupenya na kuwafikia wanaadamu. Mwenyezi Mungu Ameumba angahewa inayoendana na maumbile ya wanaadamu. Kadhalika Ameifanya mimea iwe na hali inayoweza kutoa na kuhifadhi hewa ya Oksijen kwa ulingano wenye urari na ile ya Kaboni Dayoksaidi. Umbile hili la Dunia na urari wake huo maridhawa unabainisha ya kwamba umeumbwa kwa namna inayowawezesha wanaadamu kuishi. Angahewa na jiografia yake, tangu umbali wa kutoka kwenye Jua mpaka katika aina zote za uwiyano katika mivutano yake, Dunia inathibitisha kuwa imeumbwa makhsusi kuwezesha maisha ya Wanaadamu na viumbwa vyengine alivyoumbiwa avitumiye:

“Yeye Ndiye aliyefanya Ardhi iwe inatumika kwa ajili yenu. Basi nendeni katika pande zake zote na kuleni katika riziki zake, na kwa yeye ndiyo marejeo”(67:15).

Ili kuelewa hilo vyema, tuchukuwe mfano wa tangisamaki ili kutazama uwezekano wa uhai wa wanaadamu katika sayari hii ya Dunia. Ili tangisamaki liweze kuhifadhi samaki, mimea mingine ya bahari pamoja na viumbwa vyengine, lazima liwe na hali inayoendana na maumbile ya samaki au viumbwa kama hivyo. Kwa mfano iwe na themostati yaani kirekebishi cha joto chenye kazi ya kutunza halijoto katika maji yanayoweza kuhifadhi uhai wa viumbwa hivyo. Katika tangisamaki hilo pia kuwe na mota yenye kuingiza na kutoa hewa na mchanga chini yake. Pia kutahitaji kuwekwa tembe maalumu katika maji hayo. Pia pawepo na gamba la kulikinga tangisamaki hilo, mfumo wa uchujaji wa maji yanayoingia na kutoka humo na pia kiwepo chakula muda wote. Yote hayo ndiyo yenye kuwezesha samaki kuishi katika tangisamaki hilo. Hata hivyo, samaki waliyomo humo hawatakuwa na khabari na mazingira hayo ya kuigiza. Muda wote watakuwa wakijihisi wako katika mazingira yale yale ya asili, mazingira yanayoonekana kana kwamba yamezuka tu ghafla. Hawafahamu kuwa jamaa mmoja ametengeneza tangisamaki lenye kirekebishijoto na kuweka sawa viwango vya maji. Vile vile kuwe na mota inayowezesha kuingia kwa hewa na kutoka kwa kiwango kinachoendana na maumbile yao. La kuzingatia hapa ni kuwa samaki hawa wafugwao huku wakielea huko na kule katika matangisamaki hawajui nani aliyewawekea vyakula vinavyoonekana katika kina cha maji yaliyomo. Kwa mfano huu, itakuwa imeeleweka kuwa, chanzo cha vyote hivyo ndani ya tangisamaki hilo, ni yule anayewafuga samaki hao akiwapa kila wanachokihitajia.

Kwa hiyo, ni wazi kuwa maisha katika Dunia hii yanahitaji mifumo makini zaidi kuliko ile ya tangisamaki. Mwanaadamu mwenye busara hawezi kuendesha maisha yake katika Dunia hii kwa ujinga kama ule wa samaki katika tangisamaki. Anajua kuwa ardhi iko pale tayari ikiwa imeumbwa kwa ajili yake, huku akimzingatia yule Aliyeiumba na kuimiliki kama vile yeye anavyoweza kumiliki lile tangisamaki lenye samaki wanaoishi wakiogelea huku na kule, wakivuta hewa na wakila chakula kilichomo, vyote vikiwa vimewekwa na mwenye tangisamaki hilo. Mwenyezi Mungu Ameumba Dunia na maumbile mengine akaweka mizani makini na kuweka utaratibu na mpango madhubuti katika maumbile hayo kuwezesha kuweko uhai katika Dunia hii.

Mtu mwenye akili timamu lazima atataka kumjua Mwenye kumiliki vyote hivi akijaribu kujisaili kuwa nini angepaswa kumfanyia Muumba huyo. Katika Qur’an, Mwenyezi Mungu Anataka watu wamjue Yeye na wayajue yale yanayotarajiwa wayafanye. Muumba ameweka mizania na utaratibu makini unaofanya uhai uwezekane katika sayari hii:

“Na Mbingu Ameziinua juu na Ameweka humo mizani” (Suratil Rahman :7)

“Na Tukaweka katika Ardhi milima ili isiwayumbishe na Tukaweka humo mabonde yawezeshayo njiya za kuwaongoza. Tukaifanya Mbingu kuwa dari iliyohifadhiwa...(Suratil Anbiyaa 31-32).

Uwiano unaofanya maisha yawezekane Duniani

Mambo ambayo tumeyataja mpaka sasa ni machache tu katika uwiano ambao ni muhimu kwa maisha hapa Duniani. Tukiichunguza Dunia, tunaweza kutengeneza orodha ndefu ya “vigezo muhimu ili kujaribu kuonesha uwezekano wa maisha” katika Dunia. Mwanaanga wa Kimarekani Hugh Ross aliandaa orodha yake ndefu ya mambo yenye kuonesha mpangilio na uwiano madhubuti unaowezesha maisha:

1. Uvutano katika uso wa dunia

-Ungekuwa na nguvu zaidi: angahewa lingehifadhi gesi ya nyingi ya ammonia ambayo ni sumu isiyowezesha maisha katika Dunia

-Ungekuwa dhaifu zaidi: angahewa la duniya lingepoteza maji mengi kupita kiasi

2. Umbali kutoka kwenye Jua

-Ungekuwa mkubwa sana: Dunia ingekuwa baridi mno

-Ungekuwa mdogo sana:Dunia ingekuwa na joto mno

3. Unene wa gamba la Dunia;

-Lingekuwa nene sana:Oksijeni nyingi zaidi ingehamishwa kutoka kwenye angahewa kwenda kwenye gamba.

-Lingekuwa jembamba sana:Volkeno na matetemeko yangekithiri.

4. Kipindi cha Mzunguko;

-Kingekuwa kirefu sana: Tafauti za jotoridi wakati wa mchana ingekuwa kubwa zaidi.

-Kingekuwa kifupi sana: Msukumo wa pepo za angahewa ungekuwa mkubwa sana

5. Muingiliano wa nguvu za uvutano na mwezi;

-Ungekuwa mkubwa: Athari za mawimbi kwenye bahari, angahewa na kipindi cha mzunguko kingekuwa kikubwa mno.

-Ungekuwa dhaifu: Mabadiliko ya nafasi ya Obiti yangesababisha kutotengamaa kwa majira na misimu.

6. Eneo la uvutano wa sumaku

-Lingekuwa na nguvu sana: Dhoruba za elekromagnetiki(Umeme -sumaku) zingekuwa kali sana.

-Lingekuwa dhaifu: Kusingekuwa na ulinzi wa kutosha wa kuzuia ‘miale’ mikali kutoka kwenye jua na nyota nyingine.

Uwiano wa mwanga unaoakisiwa na kiasi chote cha mwanga kinachoangaza kwenye uso wa Dunia:

-Ungekuwa kubwa: vipindi virefu vya barafu vingetokea

-Ungekuwa pungufu: “athari za greenhouse ” zingetokea

7. Uwiyano wa Oksijeni na Naitrojen kwenye angahewa;

-Ukiwa mkubwa: Mpangilio wa maisha ungekwenda kwa haraka

-Ukiwa mdogo: Mpangilio wa maisha ungekwenda taratibu.

8. Kiwango cha tabaka la Ozoni katika angahewa:

-Kingekuwa kikubwa: jotoridi katika uso wa Dunia lingekuwa chini mno.

-Kingekuwa pungufu: jotoridi katika uso wa Dunia lingekuwa juu sana.

Mitetemo ya ardhi -ingekuwa mikubwa: Maisha yangeharibika

-Ingekuwa pungufu: viinilishe vya chini ya bahari visingezungushwa mabarani kote kupitia mitetemo.

Haya ni baadhi tu ya mambo yenye kuonesha mpangilio wa lazima ili maisha yawezekane na kuendeleya Duniani. Vigezo hivi vinatosha kuthibitisha kwamba dunia haikutokea kwa bahati nasibu wala kwa mtiririko wa matukio ya kubahatisha. Mwenyezi Mungu ameweka mpangilio, uwiano, mizania na urari unaowezesha kila kiumbwa kuendana na chengine chini ya mtandao mmoja. Kila anayebaini ukweli huu lazima aamini kuwepo kwa Mwenyezi Mungu, uwezo wake usiyo na ukomo na kwa hivyo awe mwenye kushukuru kwa vyote alivyopewa. Kushukuru huko ni kumcha Yeye katika mzunguko wote wa maisha ya mtu ya kila siku.

Katika mada hii tumejifunza:

- Katika karne ya 20, wanaadamu mbali ya kujua kuwa Dunia ni sayari, piya waliweza kubaini mahali ulipo mkao wake katika mfumo huu wa juwa wenye sayari tisa.

- Piya walibaini kuwa Dunia ni Sayari ya tatu kutoka kwenye Jua na ni Sayari ya tano kwa ukubwa katika Sayari hizi tisa.

- Umbile la Dunia na urari wake huwo maridhawa unathibitisha kwamba umeumbwa kwa namna inayowawezesha Wanaadamu kuishi.

- Tangu angahewa na jiografia yake, umbali wa kutoka kwenye Jua hadi kwenye aina zote za uwiano katika mivutano yake, Dunia inathibitisha kuwa imeumbwa makhsusi kuwezesha maisha ya Wanaadamu.

Sura ya Tisa Mahali ilipo Dunia katika Ulimwengu

Swali ambalo kila mwenye kutafakari juu ya maumbile ya angani hangekosa kujiuliza ni hili; je ingekuwaje kama Dunia ingekuwa jirani kidogo na Jua? Jibu la swali hili li wazi. Kila mtu anajua ya kwamba joto la Jua ni kali mno na lenye kuweza kuyeyusha kila kichopo katika ardhi hii. Kwa hakika kama Dunia ingekuwa jirani na Juwa ingefanya angahewa kutokuwepo pamoja na bahari zote. Halijoto ingekuwa ya juu sana kiasi kwamba maji yote ya Dunia yangetokota kwa mchemko. Kwa maana hiyo kusingalikuwa na saliyo la maji katika ardhi. Kwa hiyo, hali ya Dunia yote ingekuwa kavu kama ile ya jangwani. Kwa mfano tumeona kuwa sayari ya Venasi iko jirani na juwa kuliko sayari yetu. Kwa hiyo, halijoto ya sayari ya Venasi ni ya juu zaidi kuliko ya Duniya. Kwa nyakati nyingine, hali hii ya joto ya Sayari ya Venasi hupanda na kufikiya nyuzi za sentigredi 475 (sawa na nyuzi za Faranihait 885). Ili kuweza kuhisi kiasi cha joto kubwa kinachoelezwa na nyuzi hizo za sentigredi, hebu mazingatio yapelekwe kwenye sifuriya lenye maji yaliyobandikwa jikoni yakachemka na kufikiya nyuzi 100 za sentigredi.

Hebu sasa piya tufikirie kinyume chake. Je kama Duniya hii ingekuwa mbali sana kutoka kwenye jua? Kwa jinsi hii, Dunia yetu ingepokeya joto dogo sana. Mtu anaweza kuhisi iwapo ingekuwa hivi, sehemu kubwa ya Dunia ingaliganda na kugeuka barafu. Uso wa Dunia nao ungekuwa hauna kitu ukifanana na ule wa sayari ya Maazi iliyo mbali kidogo kutoka kwenye jua kulinganisha na Dunia. Kwa maelezo hayo tunaweza kuhitimisha kwamba: Dunia yetu iko mahali ambapo ndipo hasa palipokadiriwa na kukusudiwa iwepo. Kama hivyo ndivyo, je yaweza kufikiriwa hili lilitokeyaje? Je mpango huu maridhawa waweza kutokea kwa bahati nasibu? Dunia yetu iwe imejiweka mahali hapo ilipotakiwa iwepo kuwezesha viumbwa kuishi ndani yake? Kwa hakika bahati nasibu haiwezi kupanga utaratibu huwo. Dunia ni umbile au sayari isiyojitambua. Kwa hiyo isingaliwezekana kwa umbile hilo lisilojitambua kuweza kujiweka lenyewe mahali lilipo kwa usahihi mkubwa kiyasi hicho. Ukweli ni kwamba mkao wa Dunia mahali hapo ni alama tosha ya uumbaji wenye ukamilifu wa Muumba:

“Yeye Ndiye aliyefanya Ardhi iwe inatumika kwa ajili yenu. Basi nendeni katika pande zake zote na kuleni katika riziki zake, na kwa yeye ndiyo marejeo”(67:15).

Utafiti wa kinajimu wa hivi karibuni unaonesha umuhimu wa sayari nyingine kwa ajili ya kuwepo kwa Dunia. Kwa mfano, ukubwa wa Sayari ya Jupita na pale ilipo katika mfumo wa juwa ni hali inayoshangaza hasa kwa sababu ya jinsi ilivyo kubwa sana katika mfumo wa juwa. Ukubwa huo wa Jupita huifanya Dunia ibaki katika njia yake licha ya kuwa na mwendo wa kasi katika mzunguko wake wa kulizunguka juwa. Iwapo kusingalikuwa na sayari yenye ukubwa wa Jupita mahali pale ilipo, Dunia ingekuwa angukiyo la vimondo vinavyopukutika kwa maelfu kutoka anga za mbali. Kwa ufupi, Jupita ni kama mlezi na mlinzi anayeilinda Dunia kutokana na hatari ya kuangukiwa na vimondo vyenye madhara. Jupita ingalikuwa katika Obiti tafauti na pale ilipo, Dunia na vilivyomo visingalikuwepo. Mwanaadamu anayejua yote haya, hana budi kukiri kwamba hapana chochote katika Ulimwengu huu kilichoumbwa bila ya kuwa na lengo. Ufahamu wa namna hii ndiyo unaoelezwa na Qur’an kama ifuwatavyo:

“Katika kuumbwa kwa Mbingu na Ardhi na kupishana kwa usiku na mchana, zipo alama(za kuonesha uumbaji wa Mwenyezi Mungu) kwa watu wenye akili (Surat Al Imran aya 190).

Kama aya inavyoeleza, maumbile ya angani na Ardhini yawe mazingatio kwa Wanaadamu wenye kutafakari.

Halijoto ya Dunia

Halijoto ya wastani ya anga za juu ni ngapi? Ni nyuzi hasi za sentigredi 270(sawa na nyuzi hasi 455 za Faranheit). Hiyo ni halijoto isiyowezesha uhai kuwepo. Halijoto ya wastani ya Dunia yetu ni kati ya nyuzi 15 - 20 za sentigredi(ambazo ni sawa na nyuzi 60 - 70 za Faranihaiti). Halijoto hutafautiana kulingana na jinsi mtu anavyozidi kwenda juu katika tabaka za angahewa. Kwa mfano, Bara la Afrika lina hali ya joto. Je yawezekana kutengeneza sanamu la theluji Afrika? Ili mtu aweze kutengeneza sanamu hilo anahitajika kwanza kuwa na theluji . Kwa hiyo kwa kuwa ni vigumu kupata theluji katika mazingira ya joto, hivyo hakuna uwezekano wa kutengeneza sanamu la aina hiyo. Itawezekana tu kufanya hivyo kwa kupanda mlima wa Kilimanjaro ambao ni mrefu zaidi kuliko yote barani Afrika. Kilele cha Mlima Kilimanjaro ambacho kiko juu ya usawa wa bahari, muda wote kimezingirwa na theluji. Hii ni kwa sababu kadiri mtu anavyokwenda juu kutoka Ardhini ndivyo halijoto inavyopungua. Halijoto hushuka zaidi hadi kufikia nyuzi hasi za sentigredi 50(sawa na nyuzi hasi za 58 Faranihaiti) inapofikia katika eneo tabaka la angahewa ambalo Wanaanga wanaliita kwa jina la “Angastrato” . Mbele zaidi ya hapo halijoto hupanda tena. Hata hivyo kwa Ulinzi wa Mwenyezi Mungu, Dunia yetu haina halijoto kubwa zaidi. Utengenezwaji wa kiwango hiki cha halijoto unahusiana na kiasi cha miale ya joto ya jua iangazayo umbali kati ya Dunia na Jua. Katika mada za sura zilizopita, tuligusia mada hii. Hebu sasa tuichambue zaidi. Kwa mujibu wa ukokotozi wa mahesabu ya anga, kupungua kwa asilimia 10 tu kwa nishati itolewayo na jua huweza kusababisha uso wa Dunia kuzingirwa na mita nyingi za matabaka ya barafu. Vivyo hivyo iwapo nishati ya jua itaongezeka kidogo, viumbwa vyote hai vitanyauka na kufa ila kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu. Kasi ya gurudumu la Dunia husaidia pia kuweka urari katika mgawanyo wa halijoto. Juwa hukamilisha mzunguko wake mmoja katika mhimili wake katika muda wa saa 24. Kwa sababu hii, vipindi vya usiku na mchana huwa ni vifupi. Kwa sababu hii ya ufupi, tafauti za halijoto kwa usiku na mchana nazo pia ni ndogo. Umuhimu wa hili unaonekana katika mfano dhahiri tunaoupata kutoka kwenye Sayari ya Mekyure, ambayo mchana wa siku moja tu hudumu kwa zaidi ya mwaka unaohesabika kwa vipimo vya Dunia, wakati huo huo tafauti ya halijoto kati ya mchana na usiku takriban ni nyuzi za sentigredi 1,000(Sawa na nyuzi 1,800 za Faranihait).

Jiografia ya Dunia vile vile husaidiya kugawanya joto kwa uwiano uliyo sawa. Kuna tafauti ya nyuzi 100 za sentigredi(sawa na nyuzi 212 za Faranihaiti) katikati ya maeneo ya ncha ya Dunia na yale ya ukanda wa Ikweta. Iwapo tafauti ya halijoto hiyo itaendelea kuwepo kwa kiwango kamili, matokeo yake ni kusukumiliwa mbali kwa kila kitu kilichopo eneo husika. Badala yake, Dunia ina vizuwizi vya kijiografia vinavyozuia mwendo kasi mkubwa wa hewa ambao ungesababishwa na tafauti hizo za halijoto. Vizuwizi hivyo ni pamoja na milima kama ile iliyoshikamanisha mashariki na magharibi ikianzia kwenye milima ya Himalaya iliyopo China na kuendeleya hadi Milima ya Taurasi iliyopo Anatolia na Apsi barani Ulaya.

Mpaka hapa tumejifunza jinsi Dunia inavyojiwekea, kujigawia na kujidumishiya halijoto ya kiyasi chake ingawa wakati ikifanya hivyo, anga za juu zina halijoto inayofikia nyuzi hasi za sentigredi 270(sawa na nyuzi hasi 455 za faranihaiti). Kama halijoto ya Dunia ingekuwa baridi au joto sana, kiyasi cha kuhatarisha maisha ya wanaadamu, uhai usingaliwezekana katika Dunia. Kwa hiyo, kiwango sawia cha halijoto ya Duniya kinaonesha Rehema ya Mwenyezi Mungu juu ya watu, mimea, wanyama na viumbwa vyengine.

 

Jinsi umbile la Dunia linavyolindwa na khatari ya maumbile mengine

Tukilinganisha umbile la Dunia na sayari nyingine kwa kigezo cha ukubwa, umbile la Dunia ni mfano wa punje ya njegere. Kwa mfano huu, sayari ya Mekyure kama punje ya ufuta, sayari ya Venasi kama ilivyo Dunia, sayari ya Maazi ni sawa na mbegu ya tikiti, sayari ya Jupita ionekane yenye umbile lenye ukubwa mithili ya chungwa, sayari ya satani kama chenza, sayari za Uranasi na Neptuni kama ndimu na umbile la Pluto liwe mithili ya ufuta kama ilivyo Mekyure. Kando ya sayari hizi, Jua linatazamika kama umbile kubwa la duara sawa na mpira wenye ukubwa unaozidi ule wa mpira wa kikapu ikilinganishwa na umbile la Dunia linalofananishwa na punje ya njegere. Je, ukubwa huu wa umbile la Dunia kulinganisha na sayari nyingine, umetokea kwa bahati nasibu? Au umewekwa hivyo kwa makusudiyo maalumu?

Umbile la Dunia likichunguzwa vyema, kwa urahisi sana litafahamika kuwa limekadiriwa ukubwa ambao ndiyo hasa uliotakiwa kuwa. Iwapo Dunia ingekuwa ndogo kuliko umbile lake la sasa, nguvu ya uvutano ingekuwa dhaifu na nyepesi zaidi kuweza kuhimili angahewa iliyoizunguka. Bila ya angahewa, Dunia ingekuwa ikiangukiwa mara kwa mara na vimondo au kufikiwa na mionzi mibaya itokayo anga za juu. Mbali ya hayo, Oksijeni yote ingetoweka na hivyo kufanya uhai usiwezekane katika sayari hii. Iwapo Dunia ingekuwa kubwa zaidi ya umbile la sasa, nguvu ya uvutano ingeongezeka kwa namna ya ajabu kabisa na kuigeuza angahewa kuwa mchanganyiko mbaya kwa kuwa tangu hapo ina aina nyingi ya hewa za sumu. Mbali ya ujazo wake, vile vile umbile la Dunia ndani yake limewekwa kwa namna maalumu. Matabaka, kutokea kiini cha kati ya Dunia, kila moja linazunguka jingine na mizunguko hii ndiyo inayotengeneza nguvu ya sumaku. Nguvu hii ya sumaku ni muhimu sana katika kuhifadhi uhai katika Dunia. Ikiwa imeanzia mbali kabisa ya uso wa Dunia, nguvu hii huilinda ardhi kutokana na athari ya miyonzi mibaya itokayo anga za juu. Tafiti nyingine za kisayansi zinaonesha kwamba Ulimwengu haukutelekezwa. Kwa hakika Mwenyezi Mungu, Muumba na Mola wa Ulimwengu anauendesha na kuudhibiti. Kwa uwezo wake, Ameumba Magimba(magalaksi), nyota na sayari na kuzifanya zijiendeshe kwa kanuni Alizoziweka. Sayari ya Dunia ambayo wanaadamu wanaishi, ni uumbaji maalumu wa Mwenyezi Mungu. Katika Qur’an, Mwenyezi Mungu Ameelezea uumbaji huu wa ajabu kama Anavyobainisha:

“Ameumba kila kitu na Akakikadiria kipimo chake”(25:2).

Aya nyingine nyingi zinafahamisha kwamba katika sayari hii, Mwenyezi Mungu ameweka kila linalohitajika na Wanaadamu.

Sehemu kubwa ya uso wa Dunia ni maji!

Takribani asilimia 71 ya uso wa ardhi umefunikwa na maji. Zipo dhana kuwa huenda katika sayari ya Jupita mkawemo maji yenye hali ya kumiminika, hata hivyo mpaka sasa utafiti unaonesha ni Dunia pekee yenye maji yaliyo katika hali ya kumiminika. Sayari nyingine zina barafu zilizogandamana muda wote. Katika Sayari ya Dunia, maji yamekusanyika katika maziwa, mito na vijito na kisha katika bahari ambalo ni eneo kubwa lililo wazi lenye kina kirefu, maji ambayo ni muhimu kufanya uhai uwepo katika sayari hii. Kwa mfano, maji yanazuia mabadiliko ya ghafla ya halijoto ya angahewa hivyo kuwezesha viumbwa kuishi katika halijoto ya kiwango kinachoendana na maumbile yao. Vile vile hulainisha hewa kuwa nyevunyevu. Kwa upande mwingine, maji ya bahari husawazisha mkondo wa bahari kupitia mmomonyoko na kupwa kwake. Mfumo huu haupo katika sayari yoyote. Zaidi ya hivyo, bahari hutupa samaki na vyakula vyengine vya bahari. Kula kwetu vyakula vitamu vya bahari, kuogelea na kusafiri kwa maboti, yote hayo ni katika rehema za Mwenyezi Mungu zinazopatikana kupitia neema ya maji. Mwenyezi Mungu Ameumba kila kitu tunachokihitajia kwa ukamilifu wa hali ya juu. Kwa hakika, mbali ya vitu vizuri, pia kuna hatari nyingi kama vile Volkeno zinazofoka ambazo hata hivyo, muda mwingi hua zimetulizana.

Milima

Kwa sababu ya magma(ujiuji mzito) au miamba laini iliyo katika kiini cha ardhi, Volkeno iliyo katika umbile la umajimaji hujichomozesha kupitia nyufa za kiini hicho na hivyo kufoka kwa hasira. Kutokana na mpasuko mkubwa, mara nyingi volkeno hutoa tani za mchanga na takataka katika angahewa. Aina hii ya mpasuko hutengeneza wingu zito la kiza angani. Kisha magma huanza kutiririka katika uso wa ardhi kumwagikia kwenye misitu na miji iliyo jirani. Magma inayotiririka kutoka kwenye volkeno huitwa Lava (Chemchem moto). Baada ya muda, chemchem hii hupowa na kutulizana katika uso wa Dunia kisha hugandamana na kutengeneza miamba. Katika historiya yote, miji mingi imekuwa ikiharibiwa na majanga ya volkeno zilizo hai ambazo hufoka. Kwa mfano, mnamo karne ya mwanzo, mlipuko wa volkeno uliharibu mji wa Pompeii na kisha, Roma wakati huo ukiwa mji mzuri. Chemchem moto iliufikia mji wa Pompeii ambao ulijulikana kwa jinsi wakazi wake walivyokuwa waovu zama hizo wakikiuka wazi wazi makatazo ya Mwenyezi Mungu na kutenda maovu kwa sherehe na kujipongeza. Ulikuwa mlipuko wa ghafla ambao uliwafudikiza, kuwaunguza na kuwauwa watu kabla hawajajiyokowa. Watu hao walikufa mara moja. Tukiyo hilo ambalo halikuweza kuepukika, liliangamiza uhai wa watu wa mji huwo. Chemchem hiyo, inafanana na ile iliyoelezwa katika Qur’an kama ifuatavyo:

“...basi tuliwapelekeya kimbunga cha changarawe, na miongoni mwao wako waliotolewa roho kwa ukelele na miyongoni mwao wako tuliowadidimiza Ardhini, na miyongoni mwao wako tuliowagharikisha..”(29:40).

Aya hizi zinabainisha kuwa Mwenyezi Mungu ni mwenye uwezo juu ya kila kitu, huweza kukiharibu chochote kile pale anapotaka. Hakuna anayeweza kujiokoa na adhabu yake. Hata hivyo Mwenyezi Mungu ni Msamehevu na Mrehemevu kwa waja wake. Katika vitabu vya Mwenyezi Mungu kuna mifano ya dhahiri inayoonesha urehemevu wa Mwenyezi Mungu usiyo na ukomo. Kutokea mara chache kwa milipuko ya Volkeno ni Rehema nyingine ya Mwenyezi Mungu tunayopaswa kuizingatia.

Angahewa ni muhimu kwa maisha ya Dunia

Maana ya neno Mbingu ambalo limetumika katika aya nyingi, ni anga. Tafsiri nyengine ya aya ya Qur’an juu ya Mbingu saba ni matabaka saba ya angahewa:

““Mwenyezi Mungu ni yule ambaye ameziumba Mbingu saba na ardhi kuwa mfano wa hizo..”(65:12)

Vile vile, neno hilo hufasiriwa kuwa ni lile anga wazi lililo juu ya sayari ya Duniya. Neno Mbingu pia kama tulivyoona kurasa za nyuma lina maana ya maumbile makubwa ambayo Mwanaadamu hajawa na elimu wala teknolojia ya kuyajua kwa wakati huu ambayo kwa mujibu wa aya yamekaa kimatabaka moja likiwa juu ya jingine yakiwa yamelifunika duwara la Ulimwengu:

“Ambaye Ameumba Mbingu saba zilizo tabaka tabaka..(67:3)

Kwa kutumia tafsiri ya kwanza, Duniya na anga lake liitwalo angahewa, limezungwa na matabaka saba mithili ya mkao wa Mbingu zilivyoufunika Ulimwengu kwa matabaka saba moja juu ya jingine:

“Mwenyezi Mungu ni yule ambaye ameziumba Mbingu saba na ardhi kuwa mfano wa hizo. Amri zake zinashuka humo ili mjuwe kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye uweza juu ya kila kitu, na kwamba amekizunguka kila kitu kukijuwa”(65:12)

Tabaka saba za angahewa la Dunia

Sifiyatropo: Hili ni tabaka la mviringo la angahewa lililo jirani na uso wa Dunia. Wembamba wa tabaka hili hushabihiana na hali ya hewa iliyopo katika anga letu. Halijoto yake huyeyuka na kutengeneza umajimaji kadiri mwinuko unavyoongezeka kutoka usawa wa bahari. Halijoto katika mwinuko uliyo juu zaidi huwa kati ya nyuzi hasi za sentigredi 51(sawa na nyuzi hasi 60 za Faranihaiti) hadi nyuzi hasi za sentigredi 79( sawa na nyuzi hasi 110 za Faranihaiti).

Sifiyastrato: Hili ni tabaka la angahewa mviringo lililo juu ya Sifiyatropo. Halijoto yake hupanda kadiri mtu anavyoelekea juu.

Sifiyameso: Hili ni tabaka mviringo lililo juu ya Sifiyastrato. Halijoto yake hushuka hadi kufikia nyuzi hasi 73 za sentigredi(sawa na nyuzi 100 za Faranihait).

Sifiyathemo: Hili ni tabaka lililo juu ya Sifiyameso. Halijoto yake hupanda kwa kasi ndogo. Tafauti ya halijoto ya hapa kati ya usiku na mchana ni zaidi ya nyuzi za sentigredi 100(sawa 212 za Faranihait).

Sifiyaeksosi: Ni tabaka anga linaloanzia kwenye mwinuko wa zaidi ya kilometa 500(maili 310) juu kutoka uso wa Dunia.

Sifiyaiyonosi: Jina la tabaka hilo iyoni hutokana na aina ya gesi yake ambayo hubadilika kuwa iyoni.

Sifiyamagneto: Kuwepo kwake kwenye eneo lenye sumaku, tabaka anga hili huitwa Sifiyamagneto. Tabaka hili, ambalo hufanya kazi ya ulinzi, lipo kati ya Kilometa 3,000 na 30, 000(Maili 1,850 na 18, 500) juu ya uso wa Dunia. Tabaka hili huilinda Dunia kutokana na mionzi hatari inayotoka angani, ambayo huitwa ukanda wa Vanaleni.

Ili kuweza kufahamu vyema umuhimu wa angahewa, tutafiti sayari nyingine, hasa Sayari ya Mekyure ambayo haina angahewa. Tumekwisha ona umuhimu wa angahewa katika maisha yetu na tumekwishaeleza umuhimu wa gesi katika angahewa kama vile Oksijeni au hali ya usumaku iliyopo katika tabaka la angahewa ya Sifiyamagneto inavyolitulinda na hatari za miale na mionzi mibaya. Vile vile katika angahewa ndipo unapopatikana uzito wa kila kitu ambao ni muhimu kwa uhai. Angahewa imetengenezwa kwa hewa nyepesi. Hata hivyo hii haina maana kuwa angahewa haina uzito. Kwa hakika tabaka hizi za hewa zilizo juu kilometa nyingi, zina uzito mkubwa sana.

Kwa mujibu wa utafiti uliyofanyika, angahewa lina uzito wa tani nyingi zikimsukuma kila mmoja wetu. Huu unaitwa msukumo wa hewa. Iwapo tunasukumwa na angahewa vipi hatugongani? Hatugongani kwa sababu miili yetu imeumbwa na nguvu ya kujishikiza na uzito wa angahewa. Hatuwezi kufanya lolote au hata kuishi iwapo mazingira yetu yatakuwa na msukumo mdogo wa angahewa. Hiyo ni kwa sababu, bila ya msukumo, mzunguko wa haraka wa damu katika miili yetu ungekuwa mkubwa mno katika mishipa yetu. Ni kutokana na uwiano huo kati ya miili na angahewa ndiyo maana tunaweza kuishi, vinginevyo mishipa yetu ingalipasukia mbali kutokana na msukumo mkubwa wa damu. Kwa hiyo haiwezekani kwa mwanaadamu kuweza kuishi katika mazingira kama yale ya sayari ya Mekyure yasiyo na angahewa. Katika sayari ya Venasi, ipo angahewa lakini msukumo wake ni mara 90 zaidi ya ule wa angahewa ya Dunia, kwa hivyo sayari hiyo haina mazingira yanayoweza kuruhusu uhai kwa wanaadamu na viumbwa wengine wa Dunia hii.

Kutokana na maelezo hayo, sasa inafahamika kuwa hakuna uhai unaoweza kuwepo katika sayari ya Venasi kwa kuwa katika mazingira ya msukumo mkubwa zaidi ya mara 90 ya ule wa Dunia, viumbwa vyote vitakuwa vikijigonga ovyo na kutapanyika.Tukirejea nyuma kidogo katika ile nukta ya awali, tunaona kuwa Angahewa ni moja ya viwezeshi muhimu vya maisha ya wanaadamu hapa Ardhini. Angahewa ina kazi nyingi, mojawapo ni kuwezesha kuwepo gesi ambazo nazo huwezesha uhai wa mwanaadamu katika sayari hii. Iwapo angahewa isingalikuwepo, gesi isingekuwepo, hivyo viumbwa visingeweza kupumua na kwa hivyo kusingalikuwa na uhai katika Dunia ila kwa idhini yake Mwenyezi Mungu. Kazi nyingine ya angahewa ni kuilinda Dunia na hatari zinazotoka anga za juu kama vile vimondo. Angahewa huzuwia vimondo vinavyoungua kwa maelfu visiangukie Duniani na kusababisha majanga. Angahewa vile vile huzuwiya mionzi hatari kupenya katika eneo la uso wa Dunia. Kutokana na kuzuiliwa na angahewa, ni asilimia saba tu ya miyonzi hiyo mibaya ambayo hupenya na kuufikia uso wa Dunia. Hata hivyo kuhusiana na asilimia hii saba ya mionzi hatari inayopenya na kuufikia uso wa Dunia pana fundisho jingine kubwa hapa. Mionzi hiyo ambayo huwezesha uhai katika ardhi ni ile tu ambayo Dunia inaihitaji. Na kwa kadari ya Mwenyezi Mungu umbali kati ya Dunia na jua ni ule uliohitajika; si mbali sana na si karibu sana. Kwa hiyo ile asilimiya saba ya miyonzi khatari inakuwa sehemu ya miyonzi inayohitajika katika uhai wa Dunia. Je angahewa hii ambayo ni muhimu sana kwa maisha yetu imetokeya tu yenyewe kwa bahati nasibu?

Ulinganishi mzuri unaoonesha kutokuwezekana kwa uhai kutokea kwa bahati nasibu ni huu ufuatao: Hebu tuyapeleke mawazo yetu kwenye keki tulazo majumbani. Nini kinachozipa keki hizi ladha tamu? Hapana shaka, utamu huo ni kwa sababu keki hizo zimepikwa na kuwekwa viungo na vionjo vilivyomo katika ule unga wa ngano ambao ulichanganywa na kuokwa kwa joto munasaba. Je, mpishi aliyepika keki hizo hahitajiki? Kwamba keki hizo zaweza kujipika zenyewe? Kwa hakika mawazo hayo yatakuwa ni ya ajabu sana.

Je, angahewa iliyozunguka ardhi yenye matabaka saba kama yalivyoonekana, yaweza kuwa imetokea yenyewe kwa bahati nasibu? Kwa kweli haiwezekani kutokea kwa bahati nasibu. Iwapo Mwenyezi Mungu asingeumba angahewa, uhai katika Dunia usingaliwezekana ila kwa siri zake Mwenyewe. Dunia ingalikuwaje kama Mola wetu asingaliilinda ambapo vimondo vikubwa vingeishambulia na kuiharibu kabisa. Kwa kweli Mwenyezi Mungu ni mwenye uwezo wa ajabu kabisa. Kwa hiyo mazingatio kwa angahewa ni moja ya njia ya kuujua uwezo Mtukufu wa Mwenyezi Mungu.

“Je hamuoni jinsi Mwenyezi Mungu Alivyoziumba Mbingu saba kwa utaratibu- tabaka tabaka(71:15).

Kufaa kwa angahewa kwa uhai wa Dunia

Anga ya Dunia imesheheni aina zote za nyuso za kijiografia. Hebu tutazame umbile maalumu la angahewa yetu. Angahewa ya Dunia ina asilimia 77 ya gesi ya Naitrojeni, asilimia 21 ya gesi ya Oksijeni na asilimia moja ya Kaboni dayoksaidi na gesi nyingine.

Hewa ya Oksijeni

Hewa ya Oksijeni ni muhimu kwa maisha ya wanaadamu na wanyama. Kwa kuwa, nishati inayohitajika kwa uhai wa viumbwa inapatikana kupitia hatua za kikemikali ambazo nyingi ya hizo hutokana na Oksijeni, hiyo ndiyo sababu mara kwa mara Oksijeni yahitajika, kwa kuwa inatuwezesha kupumua. Kiwango cha Oksijeni kilichopo katika angahewa ndicho kinachohitajika kwa uhai. Iwapo kiwango hicho kingeongezeka, badala ya asilimia 21 ikawa 22, hiyo ingetosha kusababisha mmuliko mmoja wa radi kuunguza misitu yote. Iwapo kiwango hicho kingekuwa kama asilimia 25, moto mkubwa ungeliunguza Dunia yote kwa kuwa Oksijeni ni gesi inayoshika moto kwa haraka. Ni muhimu kujisaili swali lifuwatalo: Ingetokeya nini iwapo Oksijeni iliyopo katika angahewa ingekuwa imetumika yote?

Licha ya uchafuzi wa hewa uliofanyika karne iliyopita, hiyo haijawa tishio kwa kuwa zaidi ya asilimia 80 ya Oksijeni inayozalishwa katika Dunia yetu inatokana na viumbwa vidogo vya bahari visivyoonekana ila kwa darubini kubwa. Hivyo kwamba, iwapo misitu yote ingetoweka bado Oksijeni ingaliendelea kuwepo. Ni mfumo madhubuti unaodumisha na kudhibiti kiyasi cha Oksijeni katika angahewa. Mfumo huu unaitwa mfumo mzunguko. Wanyama na wanaadamu wanavuta Oksijeni na kutoa nje hewa ya Kaboni dayoksaidi. Mimea kwa upande mwingine, inavuta Kaboni dayoksaidi na kutowa nje Oksijeni . Mimea imekuwa ikidumisha na kuendeleza uhai kwa kubadili Kaboni dayoksaidi kuwa Oksijeni. Kila siku mabilioni ya tani za Oksijeni yanazalishwa kutoka kwenye mimea na kutawanywa kwenye angahewa.

Jambo moja yafaa lizingatiwe. Kwa nini iwe ni mimeya tu ndiyo inayozalisha hewa ya Oksijeni. Je isingaliwezekana kwa viumbwa vyote kuweza kuzalisha Oksijeni? Hapa jibu lisilo shaka wala utata ni hapana, kwa kuwa uhai usingelikuwa mwepesi zaidi iwapo kila kiumbe kingalikuwa kikitoa hewa ya Oksijeni. Kinyume chake, iwapo wanyama na wanaadamu vile vile wangalikuwa wakizalisha hewa ya Oksijeni, kiasi cha Oksijeni katika angahewa kingalikuwa kikubwa zaidi kiasi kwamba angahewa ingaligeuka kuwa yenye kutatarika kwa muda mfupi. Kwa hivyo, cheche ndogo tu ingaliweza kusababisha moto mkubwa wa ajabu.

Kwa upande mwingine, iwapo viumbwa vyote hai, ikiwemo mimeya, vingalikuwa vikizalisha hewa ya Kaboni dayoksaidi, hewa ya Oksijeni iliyopo kwenye angahewa ingalifyonzwa na kutoweka kwa haraka na kwa hivyo viumbwa hai kwa idadi kubwa sana vingalianza kufa kutokana na kugugumiya kwa kukosa hewa kutokana na mkandamizo wa hewa inayotakikana katika kupumuwa. Mbali ya kuwalinda Wanaadamu, angahewa huhifadhi Oksijeni inayohitajika katika upumuaji. Nchini Kwa Rehema yake, Mwenyezi Mungu Ameumba mifumo mingi inayoingiliana ili kuwezesha Oksijeni ibaki katika kiwango kinachotakiwa. Wanadamu wanatakiwa kuzingatia kwa kila pumzi wanayopumua. Hiyo ni Rehema ya Mwenyezi Mungu kwa wanaadamu. Iwapo Mwenyezi Mungu asingehiyari hivyo, kusingekuwa na angahewa wala Oksijeni na kwa hivyo viumbwa wasingekuwepo katika Dunia hii. Ndiyo maana Muumini anapotaka kufanya jambo hana budi kuanza kwa kulitaja jina la Muumba, Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mrehemevu.

Mada yetu imezungumziya juu ya:

- Angahewa ya Dunia yenye asilimia 77 ya gesi ya Naitrojeni, asilimia 21 ya gesi ya Oksijeni na asilimia moja ya Kaboni, Agoni na gesi nyingine.

- Umuhimu wa hewa ya Oksijeni kwa maisha ya wanaadamu na wanyama unatokana na nishati yake inayohitajika kwa uhai wa viumbwa.

- Tunahitaji Oksijeni kwa ajili ya kupumuwa. Bila ya kuwepo Oksijeni wanaadamu hawataweza kupumuwa na kwa hivyo uhai hautakuwepo katika sayari hii.

Sura ya Kumi Mawingu yapeperukayo

Tuangaliapo angani, wakati fulani tunaona mirundi sawa na milima inayofanana na moshi wenye rangi nyeupe au njano, wakati mwingine meusi tii. Wakati fulani mirundi hiyo hufanana na maumbile fulani. Hayo ni mawingu. Kila mmoja kwa wakati wake yawezekana ameshawahi kutafakari juu ya namna gani mawingu yalivyotokea. Kila siku joto la juwa husababisha maji yaliyoko kwenye uso wa Dunia kupata hali ya joto joto yaani uvuguvugu. Aina hii ya maji au uvuguvugu unaposambaa katika hewa hubadilika kuwa mvuke. Hewa inayokuja jirani na ardhi huwongeza mvuke huo. Hewa hii ya joto hupanda kusafirisha mvuke huo mpaka angani. Huko angani, mvuke uliyo ndani ya hewa yenye joto hukabiliana na hewa baridi, hivyo hubadilika kuwa manyunyu na kisha vijiwe vya barafu.

Maji ya bahari ambayo kiasili yana chumvi na yale ya maziwani ambayo huwa na madini mbali mbali, nayo husafirisha vijichembe vya chumvi mpaka angani. Vijichembe hivi vya chumvi ni vidogo mno visivyoweza kuonekana na macho ya kawaida. Kwa siku, upepo husafirisha angani vinyunyu vilivyokusanya mamilioni ya tani za chumvi. Chumvi hizi hutengeneza viini katika matone ya mvua inayotarajiwa. Kutokea Ardhini, mawingu angani huonekana kama vifurushi vya pamba vinavyopeperuka, kiasi cha kuashiria mrundikano mkubwa mno, bila ya uzito. Lakini, kwa hakika ni mafuwele ya maji yanayoonekana kama vifurushi vya pamba vinavyobadilika na kuwa mvua, hapo ndipo tunaposhuhudia tani za maji yanayonyesha Ardhini. Kwa wastani mawingu hukusanya tani 300,000 za maji (tani moja ni sawa na kilogramu 1,000 (ambayo ni sawa na paundi 2,200). Tani 300,000 ni sawa na kilogramu milioni 300(sawa na paundi milioni 660). Ikizingatiwa kuwa uzito wa mtu mzima mmoja ni kati ya kilogramu 60-70(Paundi 130-150), basi kwa wastani uzito wa mawingu ni mkubwa sana, ni zaidi ya tani 300,000 zinazopeperushwa angani. Mwenyezi Mungu huteremsha mvua kutoka katika mawingu makubwa ili kuhuisha ardhi iliyo kame. Kwa namna hii, kila kona ya ardhi hupata mvuwa ya kutosha kulingana na wakati wake. Katika Qur’an, Mwenyezi Mungu:

Je, huoni ni ya kwamba Mwenyezi Mungu Anayaendesha mawingu, kisha huyaambatanisha pamoja, kisha huyafanya mirundi? Basi utaona mvuwa ikitoka katikati yake; Naye huteremsha kutoka juu katika milima ya mawingu-mvuwa ya mawe, akamsibisha nayo amtakaye na kumuepusha nayo Amtakaye; hukurubia muwanga wa umeme wake kupofowa macho(24:43).

Mbali ya hilo, Mwenyezi Mungu anayavuta mazingatio yetu katika usafi na utwahara wa maji anayoyateremsha kutoka mawinguni.

...Na tunayateremsha maji safi kutoka Mbinguni(Surat al Furqan 48).

Kama aya inavyoeleza, maji yanayoteremshwa Ardhini ni safi na twahara yakiwa yamechujwa vyema na kubakisha kiyasi kidogo sana cha chumvi na madini. Hii ni rehema kubwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu; udongo nao hupokeya kiyasi cha chumvi inachokihitaji kutoka katika mvuwa. Iwapo mvuke uliyotoka baharini na wenye kiyasi kikubwa cha chumvi ungeshuka kwa njia ya mvua katika hali yake ya asili, ni wazi ungekuwa na madhara kwa uhai katika sayari hii. Iwapo maji ya mvua yangalikuwa na chumvi chumvi, yangaliharibia mbali udongo na mimea, hali ambayo ingesababisha vifo kwa viumbwa hai katika ardhi. Kwa kifupi, uhai katika ardhi ungalikoma. Hata hivyo hili halitokei kwa sababu Mwenyezi Mungu ni mwingi wa Rehema kwa watu. Mwenyezi Mungu analibainisha hilo katika aya ifuatayo:

“Je mnayatafakari maji mnayoyanywa”. Je? Mumeyateremsha nyinyi mawinguni au Sisi ndiyo tunaoyateremsha? “Tungalitaka Tungaliyafanya ya chumvi, basi mbona hamshukuru?(56:70).

Maelezo yanayopatikana kutoka katika aya hizi yanaweka wazi kwamba Mwenyezi Mungu Ameumba kila kitu kwa ajili maalumu ya kuwezesha uhai kwa wanaadamu. Kama tulivyoona, Mwanaadamu hana uwezo wa kupata kila analolihitajia kwa ajili ya maisha yake. Ni kwa ridhaa ya Mwenyezi Mungu ndiyo maana anaweza kuishi katika ardhi hii. Kwa sababu hiyo, kila dakika anatakiwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu aliyemuumba, kwamba yeye ni Muumba wa kila kitu na kwa hivyo mara kwa mara Amshukuru.

Katika mada hii tumejifunza:

-

Jinsi maji yanavyotengenezwa mvuke, namna mawingu yanavyotengenezwa na baadaye kugeuzwa mvua.

-

Mvua yenye kipimo maalumu

Mvua hunyesha kwa kipimo maalumu kilichokadiriwa na Mwenyezi Mungu. Tafiti za hivi karibuni zimekuja kugundua kipimo hiki. Mahesabu ya tafiti hizo yamegundua kwamba ni tani zisizopungua milioni 16 za mvua, hudondoka kwa njia ya matone kwa kila sekunde ya muda ule mvua inaponyesha. Kwa mwaka, tani hizi hufika trilioni 505. Kwa hivyo mvua inyeshayo kila mwaka katika uso wa Dunia ni kipimo cha tani trilioni 505. Na kwa mujibu wa tafiti hizo, tani hizo hulingana katika mwaka mmoja hadi mwingine. Ukweli huu uliokuja kubainika wazi na sayansi za kileo, umeelezwa kwa ufasaha katika Qur’an ya Mwenyezi Mungu tangu kuumbwa kwa Ulimwengu.

“...Na ambaye Ameteremsha maji mawinguni kwa kipimo maalumu”(Surat az Zukhruf 11).

Ni jambo la kufurahisha sana kwamba Mwenyezi Mungu ametaja kipimo maalumu cha mvua anayoiteremsha kutoka mawinguni. Ugunduzi wa hivi karibuni unaonesha kuwa kiasi cha mvua kinachonyesha kila mwaka ni kile kile. Kiasi cha maji kilichoelezwa hapo juu ambacho ni mzunguko wa maji, hudumisha na kuendeleza uhai hapa Ardhini. Kama kipimo hicho kingalikuwa cha kubahatisha isingaliwezekana kudumisha hali hiyo hata kama ingalitumika teknolojia ya kileo. Mabadiliko madogo tu katika mzunguko wa maji yaweza kusababisha mvurugiko mkubwa kwenye maumbile katika kipindi kifupi sana. Na huo utakuwa ndiyo mwisho wa uhai ardhini. Hata hivyo, hilo kamwe halitatokea, uso wa ardhi kwa muda wote hupokea maji kwa kiwango kile kile cha mvuwa.

“Mwenyezi Mungu huteremsha maji Ardhini kwa kiwango maalumu.”

Alhamdulillah, imefahamika kuwa Mwenyezi Mungu ndiye anayedhibiti kiwango cha ushukaji wa maji Ardhini. Vinginevyo, isingaliwezekana kuwepo kiasi cha mvua kinachofanana kwa kila mwaka Ardhini. Mwenyezi Mungu ndiye Mola wa Ulimwengu, na kila kitu kinakwenda kulingana na utashi wake.

Upinde wa mvua

Bila shaka kila mmoja ameshapata kuuona upinde wa mvua. Na kama yupo ambaye hajapata kuuona basi walau ameona picha ama kwenye kitabu au kwenye runinga. Upinde wa mvua ni duara kubwa la rangi saba angani. Kuonekana kwa upinde wa mvua kwa kweli kunastaajabisha, kwa vile umbile hilo na rangi zake, linapendeza mno. Hivi mazingatio yetu yameshawafikisha wanaadamu walio wengi katika kuhoji rangi hizo zilivyotokeya?

Upinde wa mvua mara nyingi hujitokeza kipindi ambacho Jua huchomoza mara baada ya mvua kunyesha. Ni mtiririko wa elektroni hewani inayoyeyusha na kuunga metali) lenye rangi saba zilizojiweka kitabaka moja juu ya nyingine. Upinde wa mvua huonekana kama taji la mauwa, lenye kuvutia sana. Upinde wa mvua kwa hakika ni zao la miale itokanayo na rangi saba zitokanazo na mwanga wa jua. Kwa hakika, mionzi myeupe ya jua kiasili ina rangi mchanganyiko. Rangi hizi zinazotokana na jua zina mpangilio maalumu wa taswira zitokanazo na miali ya mnunurisho. Rangi za msingi za spektra ni nyekundu, rangi ya chungwa, njano, kijani, samawati, na urujuwani. Weupe wa mwanga wa jua hujitengeneza pale rangi hizo zinapojichanganya. Mara tu mwanga wa jua unapopenya katikati ya tone la mvua, rangi inayotengenezwa hujitokeza. Hiyo ni kwa sababu maji hupindisha au hutenganisha rangi kutoka kwenye mwanga. Rangi hizi zilizotenganishwa hupita kwenye matone ya maji na kujiainisha katika pande tafauti. Ili kuweza kupata mfano wa rangi hizi, mtu achukuwe glasi ya maji na aimulike mwanga mkali ndani yake. Hapa glasi ya maji itakuwa mfano wa uwazi wa tone la maji. Kisha itaonekana pale glasi hiyo itakapowakiwa na mwanga huo mkali, kiupinde kidogo cha maji kitajitokeza pembezoni mwake. Upinde wa mvua kwa kawaida huonekana kama ni nusu duara, hivyo sivyo. Upinde wa mvua, kwa hakika ni duara kamili lakini haiwezekani kuliona duara lote kwa upande mmoja wa ardhi. Ndiyo maana, mara kwa mara huonekana kama nusu duwara. Ni pale mtu anapokuwa kwenye ndege angani ndipo huweza kuliona duwara lote la upinde wa mvuwa. Katikati ya duara la upinde wa mvua aghalabu huwa ndipo katikati pa duara la jua. Pale jua linapojitokeza zaidi, upinde huo vile vile hujitokeza zaidi ili kuendelea kubaki katika kiwango kile kile cha jua.

Mwenyezi Mungu Ameumba rangi hizi mchanganyiko zenye kupendeza machoni ili wanaadamu waweze kukiri uwezo na sifa zake. Mwenyezi Mungu ana uwezo wa kuumba idadi ya vitu vizuri isiyo na ukomo. Kwa hiyo, maumbile haya yawashawishi Wanaadamu katika kuukiri uwezo wa Mwenyezi Mungu ili wawe wenye kushukuru kwa kumuabudu katika kila hatua ya maisha yao.

Mbaamwezi ing’arayo usiku

Mwezi hufanana na jiwe kubwa lenye umbile la mpira linalozunguka Dunia. Nyakati za usiku anga likiwa jeupe, mwezi hung’ara vizuri. Mwanga wa mwezi hautokani na mwezi wenyewe. Ni kama kioo, kinachoakisi mwanga wa jua. Hali ya Mwezi imeelezwa vizuri katika Qur’an kama ifuwatavyo:

“Ametukuka kweli kweli yule Aliyejaaliya mkusanyiko wa nyota angani na Akaweka humo taa itowayo mwanga na mwezi ung’arao(Surat al Furqaan).

Kwa kawaida wanaadamu wanaona upande mmoja tu wa mwezi kwa kuwa unajizungusha wenyewe na wakati huo huo ukizunguka Dunia kila baada ya siku 29. Tuangaliapo angani, nyakati za usiku, wakati fulani huonekana duara kamili na wakati mwingine nusu duwara. Kwa kadiri Mwezi unavyozunguka Dunia, sura yake huchukua maumbile tafauti. Dunia na Mwezi kila moja humvuta mwenziwe, lakini nguvu ya uvutano ya Dunia huzidi ile ya mwezi kwa mara sita zaidi. Licha ya kuzidiwa hivyo kiuvutano na Dunia, Mwezi nao huivuta Duniya na kusababisha kupwa na kujaa kwa bahari kwa kiwango kile kile kinachobaki katika usawa wa eneo la bahari. La kuzingatia kuhusu uweza wa Mwenyezi Mungu katika uumbaji ni kwamba kama isingalikuwa nguvu ya uvutano wa mwezi na Dunia na katikati yake kuwepo angahewa ya Dunia inayodhibiti na kukibakisha mahali pake kila kilichopo katika ardhi; basi Dunia katika kujizungusha kwake kwa kasi katika muhimili wake na katika kulizunguka jua, ingesababisha maji ya bahari kutotuwama yakikupwa na kujaa na kubaki yalivyo bila ya kumwagika. Ukichukua chombo kilichojaa maji kisha ukakiinamisha chini juu ni wazi kuwa maji yatamwagika. Lakini tunaona licha ya Dunia kuzunguka kwa kasi, maji ya bahari hayamwagiki kwa sababu Mwenyezi Mungu Ameumba angahewa kwa kuiambatanisha na Dunia ambayo hukivuta na kukibakisha chini kila kilicho juu ya uso wa Dunia. Kama nguvu ya uvutano ya Mwezi ingalikuwa kubwa zaidi ya hii ya sasa, kupwa na kujaa kwa maji kungesababisha kiwango cha maji kuongezeka na hatimaye kufurika na kutawanyikia nchi kavu. Katika mazingira hayo, maeneo yaliyo jirani na bahari yangalikuwa na mafuriko nyakati zote. Hata hivyo, wakati wa kupwa na kujaa, maji ya bahari hubaki katika kiwango cha kawaida kwa sababu Mwenyezi Mungu amekadiria vilivyo nguvu ya uvutano ya mwezi na Dunia kuweza kuyalinda maji ya bahari yabaki kama yalivyo ili kuwahifadhi wanaadamu na janga la mafuriko makubwa.

Nyakati za usiku na majira

Wakati ikijizungusha yenyewe katika muhimili wake, Dunia yetu hubetuka kidogo kutoka katika njiya yake. Hali hiyo ndiyo hufanya kuwepo kwa majira; masika, kiangazi na kipupwe. Mwenyezi Mungu angalitaka angaliweza kuifanya Dunia ibaki katika njia yake bila ya kujibetuwa, hivyo kusingalikuwa na majira. Halijoto ingalikuwa moja Duniani kote. Kwa hivyo tangu chakula tulacho na hewa tuvutayo, aina ya maisha tuishiyo na mazingira kwa jumla yangalikuwa tafauti na haya ya sasa. Usiku na mchana unapatikana vipi katika anga linaloonekana kiza tupu. Ardhi yetu ambayo inaogelea katika anga hilo, inajizungusha yenyewe katika mhimili wake hivyo kuna kutafautiana baina ya usiku na mchana. Nyakati za asubuhi, wanaadamu huamka juwa likiwapa mwanga na usiku unapoingia huwa kiza. Dunia inapokuwa katika mwendo wake wa kasi katika njiya yake vile vile hujizungusha yenyewe katika muhimili wake. Kwa hiyo kadiri inavyojizungusha, upande unaolielekea juwa huwa ndiyo wenye mwanga. Tafauti na Sayari ya Dunia, Sayari ya Uranasi hujizungusha katika pande zake kama vile inaanguka. Hii husababisha Sayari hiyo kubiringika mithilli ya pipa wakati ikizunguka jua ikiwa katika njia yake. Msitari wa kati wa Uranasi hulielekea juwa kwa nyuzi 98 kutoka kwenye Obiti, kwa hivyo kila ncha ya sayari hiyo hulikabili jua vilivyo kwa karibu kila sehemu ya mzunguko huo. Kwa hivyo huchukua miaka 84 ya Dunia kwa Uranasi kulizunguka jua. Kwa muda wote huo, kila ncha ya Uranasi hupokea mwanga wa Jua au huwa na kiza kwa mfululizo.

Nini kingalitokea iwapo Dunia nayo ingalikuwa na mwendo kama wa sayari ya Uranasi ambapo mchana ungalikuwa upande mmoja kwa muda wote na usiku ungalikuwa kama hivyo hivyo pia. Bila ya shaka, kwa muda wote wa miaka 84, watu wangalizaliwa na kuishi hadi kufa bila ya kuona mchana au usiku. Kwa hiyo kama hali ingalikuwa ni hiyo watu wasingalikuwa na muda maalumu wa kulala. Kila mmoja angalijiamulia mwenyewe kwenda kulala au kuwa macho kwa nyakati tafauti. Hivi ingalikuwa mchana tu wanaadamu wangaliweza kulala na kukoroma? Hata hivyo, wasingaliweza kuuona mwezi na nyota ambazo huonekana usiku wakati wa kiza. Vivyo hivyo kama ingalikuwa usiku tu wanaadamu wangalikuwa wakiishi kwenye kiza tu. Kwanza wasingaliweza kuliona jua, anga zuri la samaa au maumbile mengine mazuri yanayoonekana nyakati za mchana. Hakuna anayejua ni vipi muda wa kulala ungalikuwa au ungeanzaje. Wangalikuwa wakifanya shughuli zao nyakati za kiza na kupumzika wakiwa kizani. Kilicho muhimu zaidi ni jinsi mimea inavyohitaji nyakati zote mbili kuweza kusitawi. Kwa hali hiyo mimea isingalikuwepo. Na kwa hivyo Ulimwengu huu ungalikosa uhai. Mwenyezi Mungu Ameumba usiku na mchana ili kurahisisha maisha. Kwa kuumba usiku na mchana, Ameyaweka maisha katika utaratibu maalumu. Sababu za kuumbwa usiku na mchana zimeelezwa katika Qur’an kama ifuwatavyo:

“Na Yeye ndiye Aliyekufanyieni usiku kuwa nguwo na usingizi kama kufa, na Akaufanya mchana uwe kama ndiyo kufufuka”(Surat Furqan).

Wakizingatia kwamba kila siku uvumbuzi na ugunduzi wa kisayansi hufanyika, lakini hakuna hata moja kati ya hizo umepata kitu kipya mbali ya vile ambavyo tayari vipo katika maumbile. Hakuna uvumbuzi wowote ambao ulifanya Dunia ijizungushe yenyewe katika mhimili wake ili upatikane usiku na mchana. Ni Mwenyezi Mungu peke yake Aliyefanya hivyo kwa kuwa Ndiye Muumba wa Mbingu, Ardhi na vyote vilivyomo. Wanaadamu wanapaswa kuleta mazingatio kwamba iko siku ambayo Mwenyezi Mungu Aliyeumba usiku na mchana, ataviondoa siku moja. Ikifikia hapo, maisha ya wanaadamu yatakuwa katika hamkani kubwa na zaidi ya hivyo viumbwa hawataendelea kuwepo tena.

Katika Qur’an, Mwenyezi Mungu Anabainisha kwamba Angalipenda angaliweza kuufanya usiku au mchana uwe wa kuendelea:

“Iwapo Mwenyezi Mungu Akiufanya usiku uwe wenye kuendelea mpaka siku ya kiyama, ni Mungu gani asiyekuwa Mwenyezi Mungu atakayekuleteeni mwanga?(28:71).

“Iwapo Mwenyezi Mungu Akiufanya mchana uwe wenye kuendelea mpaka siku ya kiyama, ni Mungu gani asiyekuwa Mwenyezi Mungu atakayekuleteeni usiku?(28: 72).

Aya hizi zinabainisha wazi kuwa si usiku wala mchana ambao ungaliweza kuwepo bila ya Mwenyezi Mungu kutaka. Ulimwengu huu tunaouona na maumbile mengine yaliyo nje ya Ulimwengu huu tusiyoweza kuyadiriki kwa milango yetu ya fahamu na kila kitu vyote vimeumbwa na Mwenyezi Mungu. Ni Mwenyezi Mungu aliyewaumba wanaadamu kwa umbo kamilifu kabisa na ndiye Aliyeumba kila kitu.

Hitimisho

Katika kitabu hiki, yameshuhudiwa maajabu ya uumbwaji wa Ulimwengu. Wasomaji wameona ya kwamba uko utaratibu wa hakika wenye uwiano na ulinganifu wa ajabu kabisa. Wameona kwamba, Dunia ni sayari iliyoumbwa kwa makusudi kabisa kuwezesha viumbwa kuishi. Watu wametokeya baada ya miaka mingi kupita baada ya kuumbwa Dunia na maumbile mengine. Kama ingalikuwa wanaadamu hawakuumbwa na Muumba mmoja mweledi, wasingalikuwa na maumbile yanayowiana na hali au mazingira ya Dunia waliyoyakuta baada ya muda mrefu wa wao kutokuwepo.

“Hakika zilipita dahari(karne) nyingi Mwanadamu hakuwa kiumbe kinachotajwa”(76:1).

Katika kuhitimisha, hebu tuchukuwe mfano mmoja tu kutoka katika mwili wa Mwanaadamu kuonesha muungano na uwiano wa ajabu unaothibitisha kuwapo kwa Muumba mweledi, mfano huu ni ule Mfumo wa mawasiliano mwilini.

Wengi wetu twaijua minara mirefu ya mawasiliano na wengi wetu pia tumeiona mitambo ya kurushia taarifa na habari katika Televisheni. Taswira inayotujia kichwani ni ile ya mtambo uliojaa antena na vifaa tata vya umeme. Taswira hii ni sahihi kwa sababu, ili kuvijua vifaa vya teknolojia iliyotumika katika ufungaji wa mitambo hiyo, mtu lazima awe na utaalamu wa uhandisi katika mambo ya elektroniki na mawasiliano. Aidha karibu sote tunakubali kuwa nyenzo hizi ni muhimu mno katika kutuwezesha kupata mawasiliano na watu mbalimbali katika sehemu mbalimbali za Ulimwengu.

Sasa hebu fikiria; hali itakuwaje iwapo minara yote ya mawasiliano pamoja na vituo vya mawasiliano vitafungwa kwa muda mfupi tu? Hapana shaka kuwa hali hiyo itasababisha vurugu na wasiwasi. Hata hivyo, hata kama hali hiyo itasababisha hasara kubwa ya mali lakini bado hasara hiyo inaweza kufidiwa. Lakini endapo mawasiliano baina ya seli zetu Trilioni 100, au mawasiliano ndani ya seli moja tu yatakatika kwa muda mchache sana na hivyo taarifa zisifike katika vituo vyao, matokeo yake ni kifo. Mifumo ya sasa ya mawasiliano inatengenezwa kwa kutumia nyenzo za elektroniki na zana zenye Teknolojia za hali ya juu lakini teknolojia ya mifumo ya ndani ya mawasiliano ya seli, ambayo pia ni tete mno wanaadamu kuielewa yenyewe inajengwa kwa nyenzo zitokanazo na protini. Ndani ya protini hakuna njia za umeme au hata vyombo vya kupokea umeme kama vile vilivyomo katika nyenzo za kawaida. Humo mna Atomu tu za Kaboni, Haidrojeni, Oksijeni na Naitrojeni. Inakisiwa zipo takribani Protini 30,000 za aina mbalimbali katika kiwiliwili cha mtu na kati ya hizo, ni asilimia mbili (2%) tu ya protini hizo ndiyo ambayo kazi yake inafahamika kikamilifu. Kazi ya Protini nyingi zinazofanya kazi katika mwili kwa kiasi kikubwa bado haijafahamika.

Mfumo wa mawasiliano miongoni mwa seli kwa namna fulani unafanana na mifumo inayotumiwa na binadamu. Kwa mfano juu ya kiwambo au utando wa seli kuna “Antena” ambazo zinaziwezesha seli hizo hupokea taarifa zinazozifikia. Chini kidogo tu ya Antena hizi kuna vituo ambavyo vinatafsiri taarifa zilizotumwa kwenye Seli. Antena hizi zipo juu ya utando wa seli wenye upana wa Milimita Miamoja elfu unaozingira Seli. Kipokezi hiki cha mawasiliano ambacho hujulikana kama “tyrosine kinase” kina sehemu kuu tatu: Antena, Bodi na mkia. Umbile la sehemu ya Antena inayotoka kwenye utando wa seli linafanana na Antena ya Dishi inayotumika kukusanya taarifa za Satellite. Kila Antena moja ya dishi hukusudiwa kupokea mawasiliano fulani ya Setellite, vivyo hivyo kuna vipokezi tafauti ambavyo huelewa lugha ya taarifa zinazobebwa na molekuli mbalimbali za homoni. Taarifa zitokeazo katika seli/ homoni mbalimbali huingia katika Antena juu ya utando wa seli, lakini kila antena hukusudiwa kupokea taarifa moja tu. Huu ni mfumo wa aina yake ambapo hata mara moja taarifa haiwezi kupelekwa kimakosa katika Seli nyingine.

Uwiano mkubwa uliopo baina ya homoni na Antena unaoonekana katika kila kazi ya kibailojia waweza kulinganishwa na uhusiano kati ya funguo na kitasa. Kwamba, ni ule ufunguo sahihi tu ndio unaoweza kufungua kitasa husika. Hii ni kusema kuwa, ni ile seli husika tu ndiyo itakayohusika na ujumbe uliotumwa, ambapo kwa seli nyinginezo ujumbe huo hauna maana kabisa. Pale homoni inapoifikia seli, huufanya mfumo huu mzima wa ajabu uwe katika harakati. Kupitia mfumo maalumu wa mawasiliano, ujumbe unaokwenda kwenye seli hupelekwa kwenye DNA ya Seli hiyo. Kisha seli hiyo huingizwa katika utendaji kazi kwa mujibu wa ujumbe huo. Ili kuelewa jinsi utendaji huu wa kazi ulivyo wa ajabu, hebu jaribu kulifikiria tukio ambalo mtu yeyote anaweza kukutana nalo katika maisha ya kila siku . Taarifa hutumwa kupitia mtandao wa Intaneti na kumfikia yule ambaye kompyuta yake imeunganishwa katika mtandao wa Intanent katika kompyuta nyingine.Taarifa inayotumwa kwenye kompyuta husambazwa katika sehemu nyingine, kwa mfano katika kichapishio (Printa) ambapo printa nayo huuweka ujumbe katika karatasi. Watu wamekuwa wakitumia kompyuta tangu miaka ya themanini:

Kompyuta imekuwa ikitumika majumbani na makazini, na tangu miaka ya tisini, mtandao wa intanet umekuwa sehemu ya maisha ya watu. Iwapo siku moja itatokea kusoma habari katika gazeti kuwa kametengenezwa ka ngamiza (kakompiyuta) kadogo mno ambako hakaonekani kwa macho na kwamba kompyuta hako kana mawasiliano na kompyuta nyingine, jawabu lako litakuwa tafauti kabisa. Pengine hutaamini kuwa tekinolojiya hii ya mawasiliano yaweza kufanyika kwa kompyuta ya saizi hiyo. Hata hivyo, katika maisha halisi; kuna mfumo wa mawasiliano wenye teknojiya ya hali ya juu zaidi unaofanya kazi katika eneo dogo mno lisiloonekana kwa macho. Ule ukweli kwamba ujumbe unaotoka katika antena za seli husambazwa kwa kasi kubwa kwenye mzingo wa seli na kwamba teknolojiya hiyo ya hali ya juu hutumika katika mchakato wa mawasiliano, ni wa ajabu kabisa kuliko kijikompyuta kidogo kisichoonekana kwa macho matupu. Hii ni kwa sababu seli ni pande la nyama na kiwiliwili chako kizima, kuanziya macho yako unayosomeya gazeti hili hadi mikono yako unayoshikiya gazeti hili hujengeka kwa seli zinazofanya kazi pamoja.

Katika mwili wa kila mmoja wetu kuna chembe ndogo ndogo zipatazo Trilioni mia moja ambazo zina mfumo wa hali ya juu wa mawasiliano. Katika awamu ya mwisho ya karne ya ishirini kulikuwa na hatua nyingi za maendeleo ya kisayansi katika nyanja ya mawasiliano ya seli. Hatua kubwa zilipigwa katika ugunduzi wa mitandao ya mawasiliano ndani kabisa ya miili yetu. Kwa mfano tukiangalia tuzo za nishani ya nobeli zilizotolewa katika miaka kumi na miwili iliyopita, tuzo zipatazo sita zilizotolewa katika fani ya tiba, zilitolewa kwa ajili ya ule utafiti uliofanywa katika eneo la mawasiliano. Ni umbali gani tulifikia katika mwaka 2003? Je ni hatua gani mbele ulimwengu wa sayansi unatakiwa kupiga? Jibu la swali hili ni muhimu kweli kweli kwa sababu majibu tutakayoyatoa yatatusaidia kuelewa kuwa mfumo wa mawasiliano ya seli ni ajabu kubwa ya maumbile.

Katika nchi mbali mbali duniani kuna Taasisi nyingi ambazo zinatumia bajeti ya mamilioni ya Dola kufanya utafiti wa jambo hili. Hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2000, Shirika la mawasiliano ya seli (Alliance for Cellular Signaling- AFCS) lilianzishwa. Vyuo vikuu vipatavyo ishirini pamoja na mamia ya wanasayansi wa shirika hili, na Muwasisi wake, Alfred Gilman walizawadiwa nishani ya Nobel mwaka 1994 kwa ile kazi juu ya mawasiliano ya seli, Prof. Gilman alikuwa na haya ya kusema kuhusiana na suala hili:

“Iwapo ubongo unahitaji sukari, Ini lazima liizalishe. Kama misuli inahitaji damu zaidi, Moyo lazima udunde kwa kasi zaidi. Mamia ya Sigino tafauti za kikemikali hutiririka mwilini mzima kutoka kwenye seli moja, kushajiisha kazi za seli nyingine. Daima Seli humiminikiwa na idadi kubwa ya Sigino za kikemikali ambazo huziambia nini cha kufanya na vipi zitende kazi zao.Tatizo kubwa na ambalo ni gumu zaidi kulitafiti ni namna zote hizi zinavyofanyakazi pamoja”.

Wapo Wanasayansi wanaolizungumzia suala hili kwa uwazi na ukweli. Mmoja wao ni yule mshindi wa mwaka 1999 wa tuzo ya Nobeli, Gunter Blobel ambaye alifanya utafiti wa mfumo wa maalumu “zip code” katika seli. Profesa huyu mashuhuri duniani alisema yafuatayo katika mahojiano juu ya jambo hili:

“Inatahayarisha kuona jinsi tunavyoelewa kidogo sana juu ya namna seli inavyofanya kazi na hiyo itachukuwa muda mrefu na mrefu mno kuitafiti. Karne ya ishirini na moja, kufuatia maendeleo ya sayansi, imetuwezesha kujua zaidi maajabu yasiyo kifani ya mawasiliano ndani ya seli zetu”.

Kwa mtu mwenye kuelewa yaani mtu mwenye akili, kila mfumo unaogunduliwa huwa ishara kwake ya hekima na uweza mkubwa wa Mwenyezi Mungu na ni ishara ya kutuwaidhi kuwa yeye ndiye Mola pekee anayestahiki kutukuzwa na kushukuriwa.

Yeye ndiye Mwenyezi Mungu, Muumbaji, Mtengenezaji, Mfanyaji wa sura; Mwenye majina mazuri. Kinamtukuza kila kilichomo mbinguni na ardhini. Naye ni Mwenye nguvu, Mwenye Hikima. (59:24)

Tulichokiona katika maudhui ya kitabu hiki hakika kinathibitisha kwamba si Ulimwengu, Dunia wala maumbile ambayo yangaliweza kuwepo kutokana na mfuatano wa utukiaji wa pole pole wa maumbile katika hali ya kubahatisha kama wanavyoeleza watu wasiyojua. Yote haya yanabainisha ukweli kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye uwezo usiyo na ukomo, Mwenye kudra, Ameumba Ulimwengu, nyota, sayari, milima na bahari kwa ukamilifu, na amevipa uhai vitu vyote vinavyoishi. Uumbaji huu wenye ukamilifu unaelezwa katika Qur’an:

“Je, nyinyi ni wenye umbo la nguvu zaidi au Mbingu? Yeye amezijenga? Akainua kimo chake na akazitengeneza vizuri. Akautia kiza usiku wake na Akautokezesha mchana wake. Na ardhi baada ya hayo Akaitandaza. Akatowa ndani yake maji yake na malisho yake. Na milima akaisimamisha kwa ajili ya kukustarehesheni nyinyi na mifugo yenu(Surat Naziat 27:33).

Muda wote, wanaadamu wanatakiwa wazingatie kwamba Mwenyezi Mungu Ameumba ulimwengu na maumbile, Amewaumba wao na kila kitu walichonacho. Kila wanachokimiliki ni Rehema kutoka kwa Mwenyezi Mungu, kwa ajili hiyo wanapaswa kuzingatiya ukweli wa kimaumbile kwa kuvuta fikira juu ya Rehma na Neema walizopewa, kisha wawe wenye kumshukuru Muumba kwa kutekeleza maamrisho na kuacha makatazo yake katika kila hatua ya maisha yao ya kila siku na kisha waseme kama walivyosema Malaika:

“Utakatifu ni wako! Hatuna ilimu isipokuwa ile uliyotufundisha; bila shaka Wewe ni Mjuzi na Ndiwe Mwenye hikima”(2:32).


    


5 / total 5
|
You can read Harun Yahya's book Nani Mwenyezi Mungu? online, share it on social networks such as Facebook and Twitter, download it to your computer, use it in your homework and theses, and publish, copy or reproduce it on your own web sites or blogs without paying any copyright fee, so long as you acknowledge this site as the reference.
About this site | Tengeneza kurasa yako ya nyumbani | Add to favorites | RSS Feed
Mambo yote yanaweza kuynakiliwa, kuchapwa na kusambazwa kwa kurejea katika kurasa hii
(c) All publication rights of the personal photos of Mr. Adnan Oktar that are present in our website and in all other Harun Yahya works belong to Global Publication Ltd. Co. They cannot be used or published without prior consent even if used partially.
© 1994 Harun Yahya.www.harunyahya.com
page_top