Kufa Ufufuko Jahannam

SHUSHA KITABU

Download (DOC)
Maoni

SURA ZA KITABU

< <
2 / total: 8
KUFA UFUFUKO JAHANNAM - Harun Yahya
KUFA UFUFUKO JAHANNAM
   Utangulizi

Kifo kinaweza kumkabili mtu wakati wowote. Nani ajuae, pengine huu ndio wakati wenyewe. Au, kinaweza kuwa karibu zaidi kuliko mategemeo yake.

Pengine kuidurusu mistari hii ndio fursa yake ya mwisho, ukumbusho wake wa mwisho au onyo la mwisho kwake kabla kifo hakijamkabili. Kwa kweli mja anayeendelea kuisoma mistari hii, hajui kama atakuwa hai baada ya saa moja kumalizika. Hata kama uwezekano huo po, lakini uwezekano wa lipi linalofuata uhakika huo hana. Yawezekana muda wake wa kuishi ukawa mfupi zaidi ya hapo kabla kifo hakijamkuta.

Uhakika wa kumaliza kusoma kitabu hiki pia hana. Kifo kwa hakika kinaweza kuwadia wakati wowote, muda mfupi kabla mwanadamu hajawa na fikra juu yake.

Kwa hakika mwanaadamu atakufa. Kama itakavyo kuwa kwa wale awapendao waliopita na wajao naye vivyo hivyo kifo kwake hakina budi. Miaka mia moja ijayo mwanadamu huyu hatakuwa na hata mmoja katika watu wa wakati huo anayemfahamu ambaye atasalia katika uso wa dunia.

Mwanadamu amekuwa anashughulishwa mno na malengo yahusuyo maisha yasiyo na ukomo katika bongo lake. Miongoni mwa malengo hayo ni kumaliza kidato cha sita, kuingia chuo kikuu, kumaliza chuo kikuu, kuwa na kazi yenye hadhi, kuoa au kuolewa, kulea watoto, kuongoza maisha yenye amani. Haya ni baadhi ya malengo yaliyo ya kawaida kabisa na ya jumla aliyonayo mwanadamu katika mipango yake. Mbali na haya, yapo mengine elfu na zaidi yanayoonesha hali halisi inayomzunguka mwanadamu.

Kifo ni moja ya mambo machache katika maisha ambayo kutokea kwake kuna uhakika wa asilimia mia moja. Baada ya miaka mingi ya kufanya kazi kwa juhudi na maarifa, mwanafunzi anafanikiwa kuingia chuo kikuu, lakini mwanafunzi huyu anaaga maisha njiani akielekea darasani.

Mtu mwingine ambaye hivi karibuni tu ndio kaajiriwa afanye kazi, anapoteza maisha yake asubuhi ya siku ya kwanza wakati anaelekea kazini. Ajali ya barabarani nayo inamaliza uhai wa maharusi wawili ambao ndio tu wamo katika siku yao ya kwanza ya kufunga ndoa. Mfanyabiashara naye ambaye mambo yake yanamuendea vizuri, huonelea kusafiri kwa ndege ni njia bora ya kuharakisha mambo yake. Lakini, lililojificha ambalo halijui ni kwamba ni usafiri huo huo wa ndege ndio utakaofikisha tamati ya maisha yake katika ajali mbaya kupita kiasi na hivyo roho yake kunyakuliwa na kuwa mwisho wa uhai wake hapa duniani.

Katika hatua kama hiyo, mipango itakuwa haijatekelezwa. Kuiacha mipango nyuma, maana yake ni kuwa haitatekelezwa tena milele kwani mwanadamu amefikia kilele, mahali ambapo hawezi kurejea tena kuja kuitekeleza. Hata hivyo, muhimu ni kuwa mwisho huu mwanadamu hakuupangilia. Kwa masikitiko makubwa, kwa miaka kadhaa, mwanadamu ametumia muda huo katika kuichambua na kuiweka sawa mipango ambayo tangu hapo haitakuja kutekelezwa tena. Zaidi mwanadamu huyu hakuchukuwa muda wake katika kuwaza lile ambalo kutokea kwake kwa hakika ni kwa asilimia mia moja.

Ni kwa njia gani basi mwanadamu ambaye mwenye busara na utambuzi wa hali ya juu atapangilia vipaumbele vyake? Hivi ataweka mipango yake kwa kuzingatia kile ambacho ana uhakika wa kutokea kwake au kwa kile ambacho hana hakika ya kutokea kwake? Wengi, imedhihirika, wamekuwa wakiweka vipaumbele katika yale malengo ambayo kuyatimiza kwake hakuna uhakika wa mia kwa mia. Bila kujali hatua ya maisha waliyonayo kwa wakati huo, utawaona bado wanaendelea katika kupanga mipango ya kuwa na kesho nzuri yenye kutimiza zaidi maisha yake ya mbeleni hapa duniani. Tabia hii itaonekana ya hekima zaidi, kama mwanadamu, sio kiumbe. Bado ukweli unasalia kwamba mipango yote hatima yake ni ule usio na kigeugeu, usio na shaka, nao ni ule unaoitwa kifo.

Hivyo sio busara kuacha kujali kifo, ambacho kutokea kwake kuna hakika badala yake kuendeleza juhudi kubwa na mazingatio kwenye mambo ambayo ama yanaweza kutokea au yanaweza yasitokee na kukamilika.

Hivyo, kutokana na kuwa na maneno yasiyoingia akilini ambayo bado yanatafuna fikra zetu, wanadamu tumeshindwa kuona jambo hili ambalo liko wazi mno.

Kwa hali hii, mwanadamu, hawezi kukamilisha taratibu za kuwa katika hali yao ya maisha halisi ambayo huanza mara baada ya kufa. Watakuwa si wenye kufanya maandalizi yoyote yale kwa ajili ya maisha hayo. Mara watakapofufuliwa, hawataongoza kuelekea popote zaidi ya Jahanam, mahali palipoandaliwa rasmi kwa ajili yao.

Madhumuni makuu ya kuandika kitabu hiki ni kumfanya mwanadamu atafakari juu ya jambo ambalo anajizuia kulifikiria na kumuonya juu ya jambo lililo na uhakika wa kutokea. Kuacha kulifikiria, kwa hali yoyote ile hakufanyi kuwa ndio kupatikana kwa suluhisho.

Harun Yahya


    
2 / total 8
You can read Harun Yahya's book Kufa Ufufuko Jahannam online, share it on social networks such as Facebook and Twitter, download it to your computer, use it in your homework and theses, and publish, copy or reproduce it on your own web sites or blogs without paying any copyright fee, so long as you acknowledge this site as the reference.
About this site | Tengeneza kurasa yako ya nyumbani | Add to favorites | RSS Feed
Mambo yote yanaweza kuynakiliwa, kuchapwa na kusambazwa kwa kurejea katika kurasa hii
(c) All publication rights of the personal photos of Mr. Adnan Oktar that are present in our website and in all other Harun Yahya works belong to Global Publication Ltd. Co. They cannot be used or published without prior consent even if used partially.
© 1994 Harun Yahya.www.harunyahya.com
page_top