Kufa Ufufuko Jahannam

SHUSHA KITABU

Download (DOC)
Maoni

SURA ZA KITABU

< <
4 / total: 8
KUFA UFUFUKO JAHANNAM - Harun Yahya
KUFA UFUFUKO JAHANNAM
   PAZIA LA KUGHAFILIKA AU KUKOSA MUELEKEO AU KUKOSA MALENGO

Kimaumbile binadamu ni mbinafsi; hisia zake huwa kali pale mambo yake ya kimali na mambo mengine ya kimaisha hususan ya kivitu yanapoguswa. Kimaumbile, mwanadamu huhidhihirisha kuwa haafikiani na masuala ya kifo, ambayo kimtazamo kuonesha kuwa jambo hilo linahusu watu wachache. Hali hii ya kutokuwa makini kifikra na hivyo mja kuyumba na kukosa pa kushika, Mwenyezi Mungu ameziita ‘Ghaflatin’. Yaani ‘Mghafala’ Kughafilika.

Maana ya ‘kughafilika’ ni ile hali ya kushindwa kufikia muafaka katika maamuzi na hivyo kushindwa kuyaendea mambo ipasavyo kutokana na upungufu alionao mwanadamu katika utambuzi au hali ya kukosa utambuzi kabisa. Mfano wa kughafilika au kukosa muelekeo imeelezwa katika aya ifuatayo:-

'Imewakaribia watu hisabu yao, nao wamo katika mghafala wanakengeuka tu, (wanapuuza)'. (An-biyaa: 1)

Hisia zilizojengeka miongoni mwa watu ni kwamba yeyote aliyeathirika kutokana na maradhi mabaya basi atakufa. Ukweli ni kwamba, wote wawili, aliyeathiriwa na ugonjwa wa yule aliyejenga hisia kuwa mwenzake atakufa, wote watakufa. Suala ni lini litatokea leo au kesho au baada ya miaka kadhaa, halibadili ukweli huu. Mara nyingi yule aliyeghafilika hupuuza ukweli huu. Kwa mfano, inamkinika kwamba yule aliyeathirika na virusi vya UKIMWI - HIV – atakufa muda si mrefu. Lakini ukweli unabaki kuwa hata yule ambaye ana nguvu aliyejirani na mgonjwa – kama ukweli utasemwa siku moja isiyo na jina naye atakufa. Pengine umauti wake unaweza kumjia kabla ya aliyeathiriwa vibaya na maradhi yatokanayo na virusi vya UKIMWI. Hali hii inaweza kumtokea wakati wowote bila ya kutarajia.

Watu wa familia huhuzunika jirani na kitanda cha mgonjwa. Lakini hawajihuzunikii wenyewe ambao kwa vyovyote siku moja watakufa. Hata hivyo, kutokana na uhakika wa tukio lenyewe la kifo, haitegemewi upokeaji wa tukio uhilitilifiane ama kwa kifo kuwa jirani au kuwa muda mrefu ujao kabisa huko.

Kama kusikitika na kuhuzunika ndio njia sahihi katika kukabiliana na kifo, basi kila mmoja angeanza kujisikitikia au kujihuzunikia yeye mwenyewe kisha kwa ajili ya mwingine. Au ni busara akabiliane kwa kuishinda hali ya kusikitika na kuhuzunika kwake badala yake afanye juhudi katika kuwa na uelewa wa kina juu ya kifo.

Kwa hitimisho hili, kujua sababu zinazosababisha mtu aghafilike itakuwa ni muhimu.

VYANZO VYA WATU KUGHAFILIKA NA KUKOSA MWELEKEO

Kwanza, kutokana na kukosa maamuzi mazuri kutokana na kukosa uelewa na busara.

Watu wengi ndani ya jamii hawajishughulishi katika kufikiria mambo muhimu yanayohusu maisha yao. Mfumo wa maisha wa kundi hili la watu ni kughafilika. Yaani mfumo wao wa maisha ni ule mfumo uliosahau kuwa kuna leo na kesho. Watu hawa huwaza zaidi mambo ambayo si katika vipaumbele huku wakidai kuwa kuwaza ambayo hakuna wavunacho leo ni kupoteza muda kwani wao wametingwa. Ni kwa mnasaba huu kwamba hata wazo kuhusu kifo ni miongoni ya mambo yanayopoteza muda. Wao shughuli kubwa ni kufikiri zaidi matukio yaliyojitokeza badala ya kufikiri mambo ya msingi katika maisha.

La kusikitisha ni kwamba, inapotokea mada juu ya kifo inajadiliwa, kujiridhisha kwa kutoa hoja butu na wanapoelemewa kihoja, badala ya kuunga mkono na kuhisi hoja, wao hujitenga wasiendelee kusikiliza. Muda wote hufikiria mambo madogo madogo ya kimatukio.

Pia, hutokana na mkanganyiko na uhalisia wa maisha. Maisha yaenda kwa kasi mno huku yakiwavutia watu wengi. Kama juhudi ya makusudi haitafanyika, ni dhahiri kuwa kifo kinaweza kusababisha. Kusahau huku hakuondoi ukweli kwani ni lazima kifo kitatokea ama muda mfupi tu ujao au baada ya miaka kadhaa. Kukosekana kwa imani juu ya Mwenyezi Mungu, wengi wao huwa mbali na mitazamo mingi juu ya yale ya Mwenyezi Mungu. Mifano hai ni kama ifuatavyo: Qadar, kumtegemea Mwenyezi Mungu, na kujisalimisha kwake. Huwa anapigania zaidi mahitaji ya kimaada na kupigania maisha mazuri duniani. Kamwe muda wa kujishughulisha na maandalizi ya kifo hana. Dunia imemzonga. Tahamaki kifo kimewadia. Anatamani apewe muda zaidi kwa kujutia aliyoyafanya, lakini hayupo wa kumsaidia tena.

Tatu, kughilibika kutokana na ongezeko la watu

Moja ya sababu inayosababisha watu kughilibika na kukosa muelekeo ni kuongezeka kwa vizazi. Idadi ya watu duniani imeendelea kuongezeka kamwe haipungui. Maisha yanapokolea utamu, mwanadamu hudhani kuwa hiyo ndiyo hatima ya maisha. Humpa hisia za kuweza kutamka kuwa ‘nyota njema huonekana asubuhi’, ‘Vizazi vimeziba pengo la kifo’ Kwa kuona kuwa hakuna tatizo kwani kama aliyekufa ni mmoja na waliozaliwa ni watatu, tatizo liko wapi?’ Fikra kama hizi humpa mwanadamu ujasiri wa kidhalimu na kifisadi wa kutojali kifo. Hata hivyo kuanzia sasa, kama hakutakuwa na vizazi tena, bado tutashuhudia kifo kimoja baada ya kingine na hivyo idadi ya watu kupungua. Kifo kitaanza kuonekana kwamba ni janga kuu. Mtu ataanza kuona watu wanaomzunguuka kwanza kutoweka mmoja baada ya mwingine. Hili litaleta hisia kwamba mwisho usioweza kuzuilika utamkabili tu. Hii ni sawa na wale walio katika mstari wa kusubiri adhabu ya kifo. Kila siku wanashuhudia watu wawili au mmoja wakipungua kwa ajili ya kupelekwa kukamilisha adhabu. Idadi ya watu katika Selo za gereza inazidi kupungua kila uchao. Jinsi siku zinavyozidi kuyoyoma, ndivyo hivyo hivyo wale walio hai gerezani, hulala na hali ya wasiwasi kwamba huenda siku inayofuata ni zamu yao. Kamwe hawawezi kusahau kifo, hapo kwa sekundi hivi.

Kimsingi, uhalisia wa mambo hautofautiani sana na maelezo ya mfano huu. Anayezaliwa sasa, hana athari zotote kwa yule aliyemkuta duniani kuhusu kifo chake. Hili ni suala lililoeleweka vibaya tu kisaikolojia miongoni mwa baadhi ya watu. Watu waliokuwepo miaka mia moja na hamsini iliyopita katika uso wa dunia hii, leo hawapo – Vizazi vilivyofuata nyuma yao havikuweza kuwakinga na kifo. Vivyo hivyo miaka mia moja ijayo kuanzia sasa, ukiondoa wachache, waliopo katika uso wa dunia hii hawatakuwa hai tena. Hii ni kwa sababu dunia sio Mahali pa kudumu kwa mwanadamu.

NJIA YA MWANADAMU YA KUJIPA MATUMAINI NA KUJIRIDHISHA

Pamoja na sababu zinazopelekea watu kutotilia maanani kifo na hivyo kujitumbukiza katika kughafilika, zipo njia kadhaa anazojihami nazo mwanadamu ili kujiliwaza. Njia hizo ambazo baadhi zitaelezwa hapa chini, humrudisha mwanadamu kuwa sawa na mbuni. Mbuni hufukia kichwa chake katika mchanga ili kujihami katika mazingira ya hatari.

Mosi, kuahirisha kufikiria kifo mpaka miaka ya baadaye katika uhai. Watu kwa kawaida hudhania kuwa wataendelea kuishi hadi watakapofikisha umri zaidi ya miaka sitini au sabini. Hali hii ndio inayotanabahisha sababu zinazopelekea vijana na watu wa makamo kutumia njia hii katika kujihami. Kwa kupiga mahesabu kama hayo kichwani, tafakari juu ya kifo huahirishwa hadi hapo baadaye.

Katika ujana wao au umri wa makamo hawataki kuteseka kwa kufikiria mambo ambayo yatawapa huzuni bure. Na kwa kuwa umri mkubwa hauepukiki, basi kipindi hicho ndicho cha kufikiria kifo. Wakati huo mwanadamu atasugua bongo lake na kutafakari kwa kina juu ya kifo na hivyo kuanza maandalizi ya maisha yajayo.

Hili nalo hutoa nafuu ya kiroho, kwanzi hutoa mwanya wa hisia kuwa ipo haja ya kufanya maandalizi kwa ajili ya akhera (maisha yajayo).

Ukweli unabaki kuwa, kwa kuweka mipango hiyo ya mbali, mwanadamu anahakika ya kukamilisha mipango hiyo. Bado mwanadamu hana hakika juu ya kupumua kwake atafikisha huko au la. Kila uchao mwanadamu anashuhudia watu wa rika lake au wadogo kiumri kuliko yeye wakiaga dunia. Rambirambi za vifo zimetengewa sehemu maalum kwenye magazeti ya kila siku. Kila saa, runinga (television) na redio hutoa taarifa juu ya vifo ama vya mtu mmoja mmoja au vya makundi ya watu. Ama kutokana na ajali, vita au majanga kama kimbunga, matetemeko ya ardhi, mafuriko na kadhalika. Mara nyingi mtu kushuhudia vifo kwa wale waliomzunguuka. Lakini, kamwe hafikirii japo kwa uchache kuwa watu waliomzunguka watashuhudia kifo chake au watasoma katika magazeti babari za kifo chake. Kwa upande mwingine, japo anaweza kuishi kwa muda mrefu, hakuna litakalobadili maisha yake, maadam mtazamo wake umebakia kama ulivyo. Mpaka kifo kitakapomkabili, bado ataendelea kuahirisha kufikiria kifo.

Pili, kudhania kuwa, mtu atatumikia adhabu yake’ motoni kwa muda tu. Mtazamo huu ambao umeenea katika jamii, si chochote ila ni aina ya ushirikina tu. Tangu hapo si imani iliyo na mizizi madhubuti katika Qur’an. Hakuna sehemu kutoka katika Qur’an inayoonesha kuwa mtu ataenda kuadhibiwa motoni kwa kipindi fulani tu kisha atolewe humo kwa kupata msamaha. Kinyume chake, katika aya zote zinazozungumzia suala la adhabu kwa waovu na malipo mazuri kwa watu wema, inaainishwa kuwa siku ya hukumu watu watakuwa katika makundi mawili, yaani waumini na makafiri. Pia kutokana na mafundisho ya Qur’an, imeelezwa kwamba waumini watakuwa peponi milele na makafiri nao watatumbukizwa motoni ambako adhabu yao itakuwa milele.

Na walisema: ‘Hautatugusa moto (wa Jahannam) isipokuwa kwa siku chache tu.” Sema: Je! Mmepata ahadi kwa Mwenyezi Mungu? Kwa hivyo hatutakhalifu ahadi yake. Au Mnamsingizia Mwenyezi Mungu mambo msiyoyajua.”

Naam, wanaochuma ubaya – na makosa yao yakawazunguuka – hao ndio watu wa Motoni; humo watakaa milele. Na wale walioamini na kutenda mema, hao ndio watu wa peponi, humo watakaa milele (Al-Bagara:80–82)

Aya nyingine inayotilia mkazo juu ya hili:-

‘Hayo ni kwa sababu walisema: ‘Hautatugusa moto isipokuwa kwa siku chache.’ na yakawadanganya katika dini yao yale waliyokuwa wakiyazua. Basi itakuwaje tutakapowakusanya katika siku ambayo hapana shaka kuja kwake? Na kila nafsi italipwa kwa ukamilifu kila iliyo chuma, nao hawatadhulumiwa. (Al-Imraan:24 – 25).

Jahannam ni mahali ambapo ukali wa adhabu yake haifikiriki. Hata hivyo, hata kama kubakia katika moto itakuwa ni kwa kipindi tu, yeyote mwenye akili timamu hawezi kuitamani adhabu hiyo kisha eti ndio asamehewe. Motoni ni mahali ambapo, sifa ya Mwenyezi Mungu ya al-Jabbar – (Mwenye kutenza nguvu) na Al-Qahhar (Mwenye Nguvu – Muweza) hudhihirika. Adhabu ya motoni kamwe haiwezi kulinganishwa na adhabu yoyote ya kidunia. Mwanadamu ambaye hawezi kustahamili walau kuungua kwa kidole chake lakini bado akatamka kwamba anaweza kukabiliana na adhabu ya motoni anadhihirisha ule udhaifu wake wa kifikra mara zote, yeyote ambaye haogopeshwi na kupata ghadhabu za Mwenyezi Mungu, hushindwa kumpa Mwenyezi Mungu haki yake ya kutukuzwa. Mtu wa aina hiyo huwa hana chembe japo ndogo ya Imani, na ni mtu maskini ambaye hastahili hata kutajwa.

Njia nyingine inayotumwa katika harakati za kujiridhisha wenyewe na suala la kifo ni kitendo cha kufikiria tayari wanastahili Pepo kwa baadhi ya watu. Watu hawa hujiona kwamba kwa kujihusisha na vitendo vidogo wanavyodhania ni vitendo vizuri na kuepua mambo makubwa ya kufanya. Wameona kuwa hayo wanayofanya yanatosheleza kuwaingiza peponi. Wamezama katika kufanya mambo ya kishirikina na kutamka maneno kadhaa waliyoyasikia wanayoyanasibisha na dini, hawafuati chochote zaidi ya ukweli kwamba wanafuata imani iliyo kinyume kabisa na ile iliyofafanuliwa ndani ya Qur’an. Hujionesha kwamba wao ndio waumini kweli. Wakati huo huo, Qur’an imewaweka katika kundi la wale wanaomfanyia Mwenyezi Mungu washirika:

Na wapigie mfano wa watu wawili: Mmoja wao tulimfanyia (tulimpa) mabustani mawili ya mizabibu tukaizungushia mitende, na pia katikati yake tukatia miti ya nafaka (nyingine). Haya mabustani yote mawili yalijaa matunda yake wala hayakupunguza chochote (katika uzazi wake); akamuambia rafiki yake; ‘Mimi nina mali nyingi kuliko wewe na watu wengi katika milki yangu. Na akaingia katika shamba lake na hali ya kuwa anajidhulumu nafsi yake kwa kusema: “Sidhani abadan’. Wala sidhani kuwa kiama kitatokea. Na kama nitarudishwa kwa Mola wangu bila shaka nitakuta makazi mazuri.” Na mwenzake akamwambia na hali anajibu, ‘Je humuamini yule aliyekuumba kutokana na udongo, kisha kutokana na mbegu ya manii, kisha akakufanya mtu kamili?” Lakini, Yeye Mwenyezi Mungu, ndie Mola wangu na si mshirikishi na chochote. (Al-Kahf: 32 – 38).

Kwa maneno, ‘Lakini kama nitarudishwa kwa Mola wangu’, Mwenye bustani anaonesha hisia zake kwamba hana imani na Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho na hivyo kudhihirisha kwamba ni mshirikina ambaye ana mashaka mengi. Wakati huo huo anadai kuwa ni muumini mkubwa sana. Hivyo, anadhani kwamba hakuna wasiwasi kwamba Mwenyezi Mungu atamlipa Pepo. Tabia hii ya kujifaragua na pia kuwa na vitendo duni vya washirikina ni maarufu mno miongoni mwa watu.

Watu hawa katika nafsi zao wanajua kwamba ni waharibifu. Lakini pindi wanapoulizwa juu ya mwenendo wao huo, wanajaribu kuthibitisha kuwa kwa hakika hawana hatia ya aina yoyote ile. Hudai kuwa kuchunga maamrisho ya dini yao sio muhimu sana. Zaidi, hujaribu kujitakasa, kwa kudai kuwa wanaodhaniwa ni watu wa dini wanaowaona kila upande si waadilifu na wala si waaminifu. Hujaribu kuthibitisha kwamba wao ni ‘watu wazuri’ kwa kusema kuwa hawakusudii ubaya wowote kwa yeyote. Husema kuwa wao hawana kikwazo katika kutoa fedha kwa ajili ya waombaji, ambao wamekuwa wakiutumikia ummah kwa uadilifu mkubwa kwa miaka mingi. Na haya ndio mambo yanayomfanya Mtu awe Muislamu mzuri. Ama hawajui au wanajifanya hawajui kwamba kinachopelekea mtu awe Muislamu si kwa kuonekana mzuri kwa watu tu kwa kuwapa fedha bali ni kwa kuwa mtumwa wa Mwenyezi Mungu na kufuata maamrisho yake. Na mwishowe katika kuiegemeza dini yao waliyoipindisha kwa namna fulani ya kuhalalisha wanayofanya, hubakia katika lindi la uongo. Kwa hakika hii ndio aina hasa ya kukosa kwao uadilifu. Katika kuhalalisha wanayotenda, wanajikinga kwa misemo kama ‘Aina bora ya Ibada ni kufanya kazi’, au kinachoangaliwa ni usafi wa moyo.’ Kwa maneno ya Qur’an huku ni “kumzushia uongo Mwenyezi Mungu” na inastahili kupata adhabu ya milele Jahannam.

Katika Qur’an, watu wa aina hiyo Mwenyezi Mungu amewaelezea kama ifuatavyo:-

'Wanadhani wanamhadaa Mwenyezi Mungu na wale walioamini. Hawamhadai yeyote isipokuwa nafsi zao, lakini hawajui'. (Al-Baqara:8).

Njia nyingine wanayoitumia ni ile ya kuwa ndumila kuwili (wanafiq). Wakati mwingie watu wanapofikiria juu ya kifo, huweka fikra kuwa watatoweka milele. Fikra kama hizo huwafanya waweke kanuni ya kujiliwaza kwamba ni asilimia hamsini tu ya kuwepo uwezekano wa kuwa na na “maisha mengine baada ya kufanya yaliyoahidiwa na Mwenyezi Mungu.” Hitimisho kama hili huamsha matumaini fulani kwao. Wakati wanapotafakari wajibu wa muumini kwa Mola wake, huamua moja kwa moja kukanusha kuwepo kwa maisha ya milele baada ya kifo. Hujiliwaza kwa kusema ‘Tangu hapo, tutarejeshwa kuwa si chochote, na kusagika sagika kabisa katika udongo. Hakuna maisha baada ya kufa.” Dhana kama hizo huondosha kabisa hofu na uwajibikaji, kama vile kuulizwa na kuhesabiwa matendo yao siku ya hukumu au kuadhibiwa motoni. Katika mazingira hayo yote ya namna mbili, husababisha waendeshe maisha yao bila ya malengo (wakiwa wameghafilika) mpaka mwisho wa masiku yao ya kuishi hapa duniani.

HATIMA YA KUGHAFILIKA NI KUKOSA MUELEKEO

Katika sehemu iliyopita, imeainishwa kwamba, maadamu mtu yungali hai, hapana budi kukitilia kifo maanani. Ukumbusho huu umethibitisha kuwepo kwa faida, kwani kumshukuru mwanadamu kujitathmini upya katika yale aliyoyapa kipaumbele katika maisha yake ya kila siku na hivyo kutathmini mitazamo yake kwa ujumla. Hata hivyo upo wakati ambao hali ya kujihami miongoni mwa wanadamu inachukuwa nafasi ya juu na hivyo kuufanya kila uchao wa mtu huyo kuzidi kugubikwa na giza la kughafilika. Kama makafiri wanasubiria kifo katika hali ya kutokuwa na wasiwasi na wana hisia zisizo sahihi kwamba ni aina fulani ya kujiliwaza, hata kama watakuwa wana yakini kabisa ya kukaribia kwa kifo hicho katika miaka inayofuata mbele, wao hawatakuwa na wasiwasi wowote kutokana na blanketi hili. Hii ni kwa sababu kifo kwao wao huwa na maana kuwa ni mapumziko na usingizi mnono, utulivu na unyenyekevu, na nafuu ya milele. Ni maarufu maneno kama Fulani amekufa, amekwenda kupumzika mapumziko ya milele.

Kinyume na kile wanachofikiria, hata hivyo, Mwenyezi Mungu, ambaye ndiye Muumba wa kila kiumbe kutokana na kisichokuwepo na ambaye atavijaalia vife na ambaye atavipa uhai viumbe vyote siku ya hukumu, amewaahidi majuto na adhabu ya milele. Pia, watashuhudia ukweli huu wakati wakifariki dunia, muda ambao walifikiri wanakwenda katika mapumziko ya milele. Watatambua kwamba kifo sio kupotea moja kwa moja, bali ni mwanzo wa ulimwengu mpya uliojaa misukosuko ya adhabu. Hali ya kutisha ya awali ni ya sura za kutisha za malaika wa kifo. Hii ni dalili ya awali ya adhabu kubwa iliyoko mbele.

‘Basi iakuwaje (hali yao), malaika watakapo wafisha wakawa wanawapiga nyuso zao na migongo yao. (Muhammad:27).

Muda huu, ujeuri waliokuwa nao makafiri kabla ya kifo na hali ya majivuno hugeuka kuwa vitisho, kujuta, kukata tamaa na maumivu ya milele. Ndani ya Qur’an hali hii imeelezwa kama ifuatayo:-

Nao husema ‘Je tutakapokuwa tumemezwa katika ardhi, ndio tutarejeshwa katika umbo jipya? Bali wao hawakiri kwamba watakutana na Mola wao! Sema ‘Malaika wa mauti wamepewa jukumu juu yenu, watizinyakuwa roho zenu na kisha mtarejeshwa kwa Mola wenu! Na ungaliwaona waovu wakiinamisha vichwa vyao mbele ya Mola wao” (na Kusema) “Mola wetu! Tumekwisha kuona na tumekwisha kusikia, basi turudishe, tutafanya vitendo vizuri; (hakika (sasa) tumeyakinisha.” (As-Sajidah:10–12).

KIFO HAKIEPUKIKI

Kifo, hasa katika umri mdogo, ni mara chache mno kumpitukia katika akili yake mwanadamu. Kwa kufikiria kuwa huo ndio mwisho mwanadamu hujitahidi kugeuka hata kukifikria. Hata hivyo, japo kukimbia mbali ili ukwepe kifo hakukuponyeshi kukabiliwa nacho, hivyo hivyo kujizuilia kufikiri juu ya kifo hakukuathiri ama kuwepo au kutokuweo kwake. Vyovyote iwavyo kufikiria kuwepo kwa kifo, hakuzuiliki. Kila siku uchao, taarifa za vifo ama vya mtu mmoja mmoja au vya makundi ya watu ndiyo vinavyotawala taarifa za magazeti, maredio, Runinga na vinginevyo. Yanayosemwa juu ya kifo, mwanadamu huwa anayasikia au amepata pia kupita Makaburini. Ndugu na jamaa zake wanakufa. Mtu anapokwenda kwenye mazishi au kutoa rambirambi kwa wafiwa, kwa vyovyote hupita katika ubongo wake habari kuhusu kifo. Kama vile ambavyo mtu anashuhudia kifo cha wengine, hasa wale anaowapenda, ndivyo hivyo hivyo hupata fikra juu ya kifo chake mwenyewe. Fikra hizi humgusa sana ndani ya moyo wake, na hivyo humfanya akose utulivu.

Bila kujali ni kwa nguvu kiasi gani mtu anapiga juu ya kifo, lakini anajua kuwa wakati wowote atakutananacho, ama awe anatafuta hifadhi mahali au anajaribu kukipiga chenga. Kuhesabu muda na sekunde kuelekea kwenye kifo kamwe hakuzailiki japo kwa muda mdogo tu. Popote atakapoelekea, kifo kitamkuta huko. Mduara, unajikurubisha na mwisho utamnyakua.

‘Sema: “Hakika mauti haya mnayoyakimbia, bila shaka yatakutana nanyi; kisha mtarudishwa kwa mjuzi wa siri na dhahiri; hapo atakujulisheni yote mliyokuwa mkiyatenda.” (Al-Jumua:8).

‘Popote mlipo mauti yatakufikieni, na hata mkiwa katika ngome madhubuti (Nisai:78).

Ndio maana mwanadamu analazimika asijidanganye au kupuuza ukweli na badala yake afanye juhudi ili apate furaha kutoka kwa Mola wake ambayo tayari amekwisha mfahamisha kabla. Ni Mwenyezi Mungu pekee anayejua ni lini hasa muda huo utawadia. Mtume Muhammad (s.a.w) amesema njia bora kwa mtu kuepuka adhabu na kuingia katika mwenendo mwema ni kukumbuka kifo mara kwa mara.

Abdallah bin Umar amehadithia, ‘Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w) amesema: ‘Hizi nyoyo hupata kutu kama kipatavyo chuma kinapoathiriwa na maji. alipoulizwa ni nini kinachoweza kusafisha nyoyo, alijibu. Kukumbuka kwa wingi Kifo na Kusoma Qur’an (Al-tirmidh, 673).

KIFO HALISI NA KIFO CHA NAFSI

Je! Umewahi kuwaza namna gani? Na ni kitu gani kinatokea wakati wa kufa?

Hadi leo, hakuna yeyote katika wafu aliyerejea tena katika uhai huu ambaye anaweza kutusaidia mawazo kuhusu uzoefu wake na hisia zake wakati wa kufa. Mwenyezi Mungu ambaye ndiye aliyejaalia uhai kwa mwanadamu na ndiye anayeuchukuwa kwake kwa kufuata utaratibu aliojiwekea, anatufahamisha ndani ya Qur’an kuwa ni nini hasa kinachotokea. Hivyo Qur’an ndio chanzo pekee ambacho mwanadamu anajifunza kuwa kifo kinatokeaje na hasa ni yapi anayohisi na yanayomtokea yule anayekufa. Kifo kama kinavyoelezwa ndani ya Qur’an si sawa na ‘Kifo cha Kimazingaombwe’ mwanadamu anachoshuhudia kutoka nje au kwa sura ya nje. Kimsingi, aya kadhaa zinatufahamisha juu ya tukio lenyewe kama lionekanavyo toka kwa yule anayekufa, ambacho hakuna yeyote anayehisi hivyo ila muhusika tu. Hayo yamebainishwa katika Surat Waqi’ah.

‘Basi Mbora (Roho) ifikapo kooni. Na ninyi wakati ule mnatazama. Nasi tunakaribiana naye zaidi kuliko ninyi, wala ninyi hamuoni (Waqiah:83 – 85).

Kinyume kabisa na kifo cha makafiri, kifo cha watu wema ni rehema tupu.

Wale ambao Malaika huwafisha katika hali njema, wakasema: ‘Amani itakuwa juu yenu; ingieni peponi kwa sababu ya yale (mema) mliyokuwa mkiyatenda. (An-Nahl:32).

Aya hizi zinadhihirisha hoja muhimu na isiyobadilika kuhusu kifo: Wakati wa kukata roho, mtu anayekufa anapita kwenye nini? Na wale walio karibu yake (wanaomtazama) wanapata uzoefu wa aina gani! Ni maono mawili tofauti kwa tukio moja.

Kwa mfano: Mtu anayetumia maisha yake yote kama kafiri asiye na faida anaweza kuonekana kwa nje, ‘Kifo chake ni cha amani’. Wakati huo huo, Roho, katika mtazamo mwingine, inaonja mauti kwa namna iumizayo kweli kweli.

Kwa upande mwingine,Roho ya Muumini, pamoja na kuonekana kama mwenye kuugulia na kuumia mno, huuacha mwili wake katika hali ya uchaji Mungu. Kwa ufupi kufa kwa mwili na kufa kwa roho kulikoainishwa ndani ya Qur’an ni hali mbili tofauti kabisa.

Kwa kutoujua ukweli huu unaoainishwa ndani ya Qur’an, makafiri ambao hujaalia kifo kuwa ni usingizi wa amani na wa kudumu, pia husaka njia ambayo kwayo wakati wa kufa nao uwe kama maumivu na uwe wa raha.

Ni kutokana na mtazamo huo finyu wa uhalisia, baadhi ya watu ili kuepuka kifo chenye machungu, huamua kujiua ama kwa kuvuta gesi ya sumu, au kunywa sumu yenyewe au kujipiga risasi. Ukweli unabakia palepale, kifo kwa upande wa makafiri namna yake huwa ni sehemu ya adhabu kwa hiyo machungu makali ni lazima yapatikane kwa kiwango kile kile kilichokadiriwa. Kwa upande wa waumini, kifo kinakuwa rehema kwao. Hivyo hawaonji machungu kama yale yapatikanayo kwa waliomkufuru Mwenyezi Mungu. Hata kama kwa nje ataonekana anaugua hasa na kuonesha wazi athari za kuumwa kwake au majeraha yatokanayo na vita vya kuihami dini ya Mwenyezi Mungu.

Qur’an inatubanishia machungu wanayoyapata makafiri wakati wa kutoka roho zao, namna malaika wanavyotoa roho hizo.

Basi itakuwaje wakati Malaika watakapowafisha wakawa wanawapiga nyuso zao na migongo yao. Hayo ni kwa sababu wao walifuata yaliyomchukiza Mwenyezi Mungu na wakachukia yanayomridhisha, basi akaviondoshea thawabu vitendo vyao. (Muhammad: 27 – 28).

Katika Qur’an pia kuna maelezo juu ya mahangaiko ayapatayo mtu muovu ambaye kwa hakika ni matokeo ya taarifa ya Malaika kwake juu ya adhabu ya milele inayomsubiri baada ya kifo:

‘... Na kama ungewaona madhalimu watakapokuwa katika mahangaiko ya mauti, na malaika wamewanyoshea mikono yao (na kuwaambia), ‘Zitoeni roho zenu! Leo mtalipwa adhabu ifedheheshayo kwa sababu ya yale mliyokuwa mkiyasema juu ya Mwenyezi Mungu na kwa vile mlivyozifanyia aya zake’ (Al-An’am: 93).

‘Na laiti ungaliwaona malaika wanapowafisha wale waliokufuru wakiwapiga nyuso zao na migongo yao na (kuwaambia). ‘Ionjeni adhabu ya moto! Hayo ni kwa sababu ya (maasi) yale yaliyofanywa na mikono yenu. Na hakika Mwenyezi Mungu Si mwenye kuwadhulumu waja wake. (Al-Anfal:50–51).

Kama aya zilivyobainisha, kifo kwa wasio na imani ni ‘kipindi tosha cha kupata adhabu iumizayo. Wakati ndugu, jamaa na marafiki wakiwa wamekizinguuka kitanda kuonesha mapenzi kwa ndugu ya huyu, wanaona kila kitu ni shwari tu. Lakini ukweli ni kwamba, kwake yeye anamuona malaika na mauti akimchukuwa roho yake kwa nguvu:

‘Naapa kwa wale (malaika) wavutao kwa nguvu. (Naziat:1)

‘Sivyo (mnavyofanya)! (Roho) itakapofika katika mitulinga, Na kusema; Ni nani wa kumzingua (na kumpoza mgonjwa huyu?” Na mwenyewe akajua kwa hakika kuwa hiyo ni (Saa ya) kufariki (dunia) – (Al–Wiyama: 27 – 28).

Kwa wakati huu, kafiri anadhihirikiwa na ukweli alioukanusha kwa muda wake wote alipokuwa duniani. Kwa kifo, ataanza kuona uchungu, ambao ni matokeo ya majuto yake na kukanusha kwake. Malaika watakapokuwa ‘Wanawapiga migongoni mwao’ na pia ‘Wakiwatoa roho zao kwa nguvu’, ni dalili tu za mwanzo na majuto na mateso yanayowasubiri.’

Kinyume na hali hiyo kwa makafiri, watu wema (waumini) kifo chao huwa ni mwanzo wa furaha ya milele na rehema. Tofauti na kafiri ambaye roho yake huchukuliwa huku akiteseka kwa machungu, roho ya muumini Hutolewa na kuchukuliwa kwa upole.

‘Na kwa wale wanaotoa(roho za watu wema) kwa ulatifu (taratibu).’ (Naziat:2).

Wale ambao malaika huwafisha kwa hali njema, wakasema, “Amani itakuwa juu yenu, ingieni peponi kwasababu ya yale (mema) mliyokuwa mkiyatenda. (An–Nahl:32).

Hii inafananana hali ya mtu anapokuwa usingizini. Ndani ya usingizi, roho kwa utaratibu huhamishwa na kuwekwa katika mazingira tofauti na haya. Hayo yamebainishwa katika aya ifuatayo:-

‘Mwenyezi Mungu hutakabadhi (huchukuwa) roho wakati wa mauti yao. Na zile ambazo bado hazijakufa, wakati wakiwa usingizini. Huzizuilia zile ambazo kifo kimekwisha hukumiwa juu yao, na kuzirudisha nyingine mpaka wakati uliowekwa ... (Az-Zumar: 42).

Huu ndio ukweli kuhusu kifo. Kwa sura ya nje, watu hushuhudia kifo cha mwili; mwili kushindwa kufanya kazi zake za kawaida. Watu hawaoni, kafiri akipigwa usoni au mgongoni wakati wa kukata roho, wala roho inapovutwa hadi kufika katika matulinga ya mabega yake. Ni roho ya muhusika tu ndiyo inayoshuhudia na kuhisi yote haya na kuyakabili. Hata hivyo, kifo halisi ‘kinaonjwa’ katika upana wake wote ambazo hazioani na zile za watazamaji kifo kwa nje. Kwa maneno mengine, yale yanayotokea wakati wa harakati za kifo ni mabadiliko ya hali, kutoka katika mtazamo wa kidunia na kuingia katika mtazamo wa kiakhera. Kwa muhtasari, maelezo ya aya iliyobainishwa hapo juu yaweza kuwa kama ifuatayo:-

‘Ama kwa kuwa kwake Muumini au kafiri, mwanadamu yeyote hawezi kukisogeza kifo chake kwa kukiwahisha zaidi au kukichelewesha baada ya muda uliopangwa japo kwa saa moja. Popote alipo mwanadamu kifo kinaweza kumfikia tu. Katika harakati za kukata roho, ‘Sakarati Mauti’, kila mtu ana namna yake atakayohisi kutegemeana na matendo yake japo katika sura ya nje ni ngumu kuwatofautisha.

KIFO CHAMUUMINI

Jua kuwa kifo hakiepukiki. Kwa Umri wake wote uliompitukia, Muumini hujiandaa kwa kifo.

Malaika wa mauti humpa bishara njema kuwa ataingia peponi.

Malaika hutoa roho yake Muumini kwa upole.

Muumini huhisi haja ya kuwapa habari njema waumini wengine waliobaki hapa duniani kwamba ahadi ya Mwenyezi Mungu ni kweli na kwamba hakuna kuogopa wala kusikitika kwa waumini. Hata hivyo, hili halitaruhusiwa.

KIFO CHA KAFIRI

Atakutana na kifo alichokuwa muda wote wa uhai wake akikikwepa.

Katika kipindi cha Sakarati Mauti (Kukata roho) atakuwa mwenye kukumbwa na mtetemeko wa hali ya juu na hivyo kumuumiza.

Malaika watamkunjulia mikono na kumpa habari kuwa atakuwa mwenye kuathirika kwa adhabu ya motoni inayomsubiri.

Malaika wataitoa roho yake hali ya kuwa wanampiga usoni na mgongoni mwake.

Roho yake inachukulikuwa kwa nguvu na hivyo kusababisha maumivu makali mno yaendayo ndani.

Roho ichukuliwapo na ikafika katika mitulinga ya mabega yake hakuna yeyote katika wanadamu awezaye kumponya na kifo kilichokwisha wadia.

Roho inachukuliwa kwa shida kubwa wakati anajiingiza katika kukanusha.

Wakati wa kukata roho, hakutakuwa na fursa tena ya kuonesha kuwa sasa anaamini au anatubia itakayo kubaliwa.

Kifo cha mwili namna kinavoonekana katika sura ya nje, yaani kwa (wale wanaotazama mwili wa marehemu) hutoa mafunzo kadhaa ya kuyazingatia:-

Namna kifo cha mwili kinavyomrejesha mwanadamu na kuonekana si lolote wala chochote humfanya mwanadamu kujua hakika ya mambo muhimu sana. Hivyo basi, ‘kifo cha mwili’ na kaburi, kinachomsubiri kila mmoja katika wanadamu, pia kinahitajika kuainishwa na kuzingatiwa.

KIFO CHA MWILI KAMAKIONEKANAVYO KATIKA SURA YA NJE

Punde mtu anapofariki dunia, wakati roho inatengana na mwili wa mwanadamu, huacha nyuma mwili usio na uhai. Kama ilivyo kwa viumbe kama nyoka, ambao hujibua ngozi yao au kuchuna ngozi ya juu ya mwili wake kuacha jibuo lisilo na uhai naye akiendelea na maisha mengine, vivyo hivyo kwa mwanadamu. Roho ambayo imetoka katika mwili, hendelea na maisha mengine yenye hakika huku mwili (ganda) likiachwa bila ya uhai wowote.

Tangu wakati huo na kuendelea, hatakuwa tena uhusiano na mwili wake kwa namna yoyote ile. Mwili ule uliodhaniwa ndio ‘mwanadamu mwenyewe’ kwa kipindi chote cha uhai wake, utabadilika na kuwa mlundikano wa nyama tu. Kwa kifo chake, mwili wake utabebwa na watu wengine. Watakuwepo watu wakiwa wanalia na kuomboleza. Kisha mwili huo utapelekwa chumba cha kuhifadhia maiti kwa usiku nzima. Siku inayofuata hatua za mazishi zinaanza. Mwili uliokufa, sasa umekuwa mkakamavu, utaoshwa kwa maji baridi. Wakati huo huo alama za kifo zitaanza kuonekana huku baadhi ya sehemu za mwili wake zikianza kubadilika rangi na kuwa zambarau. Kisha mwili huo utavishwa sanda na kuwekwa katika jeneza la mbao. Wakati wanaelekea makaburini, maisha ya mitaani yataendelea kama kawaida. Baadhi ya watu watakapokuwa wanashuhudia anayepitishwa, wataonesha kujali huku kundi kubwa likiendelea na mapambano yao ya maisha ya kila siku. Huko makaburini, jeneza lake litabebwa na wale vipenzi vyake au wale wanaodhaniwa wana mapenzi naye. Si ajabu, pia watakuwepo watu wakiendelea kulia na kuomboleza. Kisha watu watawasili katika makazi yasiyoepukika, kaburi. Katika kikuta cha sementi, jina lake litaandikwa. Mwili wake katika jeneza na kuwekwa katika mwanadani. Maiti ikiwa tayari kabla ya kutolewa kwenye jeneza, sasa dua mbalimbali zikiendelea kuombwa watu watakuwa wamejiandaa kwa kazi moja muhimu, kuuweka mwili kwenye mwanandani na kufukia shimo lenye mwili wake (kaburi). Mwisho, watu watabeba mabeleshi, makoleo, machepeo, sululu na majembe na kuanza kufukia kaburi kwa udongo. Hatimae, udongo utaifikia sanda yako na hivyo hakutakuwepo tena nafasi ya kupata mwanga. Hapo watu watarejea majumbani na kuacha kimya kizito makaburini. Watu watarejea katika shughuli zao kama kawaida. Kwa Mwili aliozikwa, maisha yatakuwa hayana maana tena. Nyumba nzuri, warembo, sehemu ya kupunga upepo, vyote vitakuwa havina maana tena. Mwili ule hautakutana na marafiki zake tena. Kuanzia hapo na kuendelea, kitakachokuwa na uhakika ni kwamba udongo na wadudu na bakteria ndio waishio humo.

Mwanaadamu amewahi kufikiria juu ya hali ya mwili wake baada ya kufa utakuwaje?

Kwa kuzikwa, mwili utaoza kwa haraka mno kutokana na sababu za aina mbili, zile za umbile la mwili wenyewe, au zile za nje ya mwili. Mara baada ya kuwekwa kaburini na kufukiwa, bakteria na wadudu wengine wataanza kuzaliana mwilini kutokana na kukosekana hewa ya oksijeni. Gesi itakayotengenezwa kutokana na viumbe hawa itapelekea mwili kugandamizwa, kuanzia kwenye kiwiliwili (tumbo) umbile likibadilishwa na muonekano wake kadhalika. Damu itaanza kutoka mdomoni, na puani kutokana na shinikizo (pressure) la hewa katika kifua. Hali itazidi kuwa mbaya kwani nywele, kucha, nyayo na mikono vitameguka meguka.

Hali hii ya nje itaendelea sanjari na viungo vya ndani navyo kuathirika vibaya. Viungo kama mapafu, moyo na ini navyo vitaoza. Wakati huu tumboni nako hali si shwari. Ngozi haiwezi tena kustahamili shinikizo la gesi. Hivyo tumbo litapasuka, na kutoa harufu mbaya sana. Kuanzia katika fuvu hadi mishipa vitaachana kutoka mahali vilipokuwa. Nyama na ngozi vyote vitasagika sagika kabisa. Ubongo utaoza na kuonekana kama udogo tu. Hali hii itatendeka hadi mwili utakapobakia huwa mifupa tu.

Mwili, uliodhaniwa kuwa ndio mtu, utakuwa umepotea kabisa kwa njia ambayo kwa hakika ni yenye kutisha mno. Wakati kundi la wale waliobaki hai likiendelea kuomboleza na kufanya visomo mbalimbali, minyoo, wadudu a bakteria katika udongo, nao watakuwa wanashambulia na kuumaliza kabisa mwili kwa kuula.

Kama umauti wake umetokana na ajali na utakuwa haukupata fursa ya kuzikwa, matokeo yake yatakuwa ni yenye kutisha zaidi. Mwili wake utakuwa na wadudu mithili ya mzoga anavyoshambuliwa na wadudu katika joto la kawaida kwa kipindi kirefu. Mara ulaji huo utakapokamilika kinachosazwa ni mifupa tu.

Kwa nini? Kwa hakika hii ni kutokana na mpango wa Mwenyezi Mungu kuwa mwisho wa mwili wa mwanadamu uwe huo. Kwa utaratibu huo, somo lenye kuhitajia mazingatio litakuwa limepatikana. Mwisho huu unaomsubiri Mwanadamu, kumtanabahisha kuwa yeye sio ‘huu mwili pekee’ bali ni ‘Roho’ iliyomo ndani ya mwili huu. Kwa maneno mengine mtu lazima atanabahi kuwa yeye ni zaidi ya mwili huu. Mwisho huo wa kushitua, pamoja na mazingatio yake, umefanywa hivyo, ili mwanadamu ajue kwamba yeye sie ‘nyama na mifupa.’ Kwamba yeye si ule mwili uliokufa katika ujumla wake. Yeye ni roho iliyotoka na kuhifadhiwa anakokujua Muumba ukisubiri kuvikwa umbile jingine utakapofufuliwa na baada ya hukumu. Na kwa ajili hiyo yeye si huo mwili unaoshambuliwa na wadudu pale kaburini na kuchakachika kabisa.

MAISHA YA ULIMWENGU HUU NI YA MUDA TU

Mwanadamu amekwishapata kufikiri ni kipi kinachomfanya atumie muda mwingi na juhudi kubwa katika kuuweka mwili wake uwe safi? Ni kwanini mwili mchafu, mdomo unaonuka, mwili uliotapakaa girisi wa fundi makanika au nywele zisizotunzwa vizuri hauvutii? Kwa nini mwanadamu hutoka jasho?

Na kwanini jasho lake huambatana na harufi mbaya yenye kuudhi? Tofauti na hali hiyo, kwa upande wa mimea, hiyo hutoa harufi nzuri. Mawaridi au muasumini kamwe si wenye kukera pamoja na ukweli kwamba haukuwa katika udongo na kubakia katika mazingira ambayo ni ya vumbi na machafu. Mwanadamu hawezi kamwe kufikia hali ya mawaridi au muasumini na harufi ya mimea ya aina nyingine yenye kutoa harufi nzuri. Hali hii ni ukweli bila kujali kwamba anaangalia mwili wake vizuri au la!

Hivi mwanadamu amewahi kutafakari kwa nini ameumbwa hali ya kuwa ni mwenye udhaifu kwa kiwango hiki? Kwa nini Mwenyezi Mungu ameumba mimea ikawa ni yenye kutoa harufi nzuri kwa kiwango hiki na mwanadamu naye licha ya kuoga na kujisafisha mara kwa mara awe ni mwenye kutoa harufu mbaya katika mazingira yaliyoelezwa juu?

Udhaifu wa mwanadamu si katika kutoa harufi mbaya tu, bali pia unapatikana kwa kuchoka, kuumwa njaa, kupata majeraha, kupata magonjwa sugu na kadhalika. Yote haya yameonekana ni ya kawaida mno kwa binadamu. Lakini tafakuri inabainisha kuwa yamo mafunzo makubwa mno ndani yake. Ingewezekana kabisa kuwa mwanadamu asitoe harufi mbaya katika mwili wake. Vivyo hivyo ingewezekana mtu asiugue kabisa japo kichwa au maradhi mengine. Udhaifu wote huu kwa mwanadamu hautokei kwa bahati nasibu au hautokei kwa bahati nasibu. Yote yameumbwa na Mwenyezi Mungu kwa kudhamiria kwa malengo mahususi. Mwenyezi Mungu amempa mwanadamu jukumu maalum na akamjaalia udhaifu.

Mbinu hiyo inafanya kazi ya aina mbili kimalengo. Mosi, humfanya mwanadamu atanabahi kuwa yeye ni kiumbe dhaifu, ‘Mtumwa’ wa Mwenyezi Mungu. Kuwa mkamilifu ni Sifa ya Mwenyezi Mungu. Watumwa wake kwa upande mwingine ni dhaifu mno na hivyo humhitajia mno Mwenyezi Mungu ambaye ndiye Muumba wao. Haya yanafafanuliwa katika Qur’an kama ifuatavyo:-

Enyi Watu! Ninyi ndio wenye haja kwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mkwasi, asifiwaye. Kama akitaka atakuondoeni na ataleta viumbe wapya. Na jambo hili si gumu kwa Mwenyezi Mungu – (Fatir: 15 – 17).

Udhaifu wa mwili wa Mwanadamu muda wote humkumbusha juu ya udhaifu wake. Mwanadamu anaweza kudhania kuwa yeye ni bora na kiumbe mkamilifu. Lakini, ukweli ni kwamba anahitajia kwenda haja kila siku. Na anayoyaona huko humfanya atanabahi juu ya ukweli kuhusu yeye kwa nafsi yake.

Pili, udhaifu wa mwanadamu husaidia kumkumbusha ukweli kuwa maisha haya siyo ya kudumu. Hii inatokana na sababu kuwa udhaifu unaompata mwanadamu ni wa aina yake kwa mwili wa Mwanadamu. Katika maisha yajayo; watu wa peponi watakuwa na miili mingine. Mwili dhaifu na usiotimilifu na mnyonge katika Ulimwengu huu, sio mwili halisi wa Muumin, atakaokuwa nao bali huu ni umbile la muda analobaki nalo kwa muda mahsusi tu hadi atakapoondoka katika ulimwengu huu.

Ndio maana, katika ulimwengu huu, uzuri usio na upungufu haujawahi na hautaweza kufikiwa. Yule mwanadamu anayevutia kimaumbile, mtimilifu na mrembo, pia huenda haja, akitokwa na jasho, hutoa harufi mbaya mdomoni nyakati za asubuhi, hapa na pale akiugua madonda au mapele kwenye ngozi yake. Mtu huhitaji kujiwekea ratiba ya kila siku kujisafisha na kujiweka msafi. Baadhi ya watu wana nyuso za kuvutia lakini hawana maumbo yenye kuvutia. Wapo baadhi ambao hali zao ni kinyume na hayo. Wapo wenye macho ya kuvutia lakini pua kubwa. Ipo mifano mingi ya aina hiyo. Mtu anaweza kuonekana mrembo kwa nje, lakini kwa ndani ana maradhi makubwa mno. Anaweza kuwa mremba wa kutazamika lakini ana tabia mbaya na za kukera zisizovumilika.

Juu ya yote haya, yule aonekanaye mtimilifu kwa kumtazama huzeeka na kufa. Ama yawezekana, katika ajali ya barabarani isiyotegemewa, mwili wake unaweza kupata majeraha yasiyopona. Izingatiwe kuwa, sio mwili wa mwanadamu pekee ambao si mtimilifu, la hasha, pia maua ya aina zote nayo hunyauka, vyakula vyote vitamu navyo huharibika kwa kuoza. Yote haya mwanadamu anayashuhudia hapa ulimwenguni. Umri mfupi katika ulimwengu huu, aliopewa na Muumba na miili ya wanadamu waliyopewa kama zawadi na Mwenyezi Mungu haitakikani wamsahau Mola wao. Maisha ya kudumu na umbo timilifu yatapatikana katika maisha ya Akhera tu. Qur’an inafafanua hili katika aya isemayo:

‘Basi vyote mliyopewa ni starehe ya maisha ya dunia tu, lakini kilichoko kwa Mwenyezi Mungu ni bora na chenye kudumu. Watakistahiki wale walioamini na wakawa wanamtegemea mola wao tu. (Ash-Shuura: 36).

Katika aya nyingine, lengo halisi la ulimwengu huu limefafanuliwa kama ifuatayo:

Jueni ya kwamba maisha ya dunia hii ni mchezo na upuuzi na pambo la kufahamishana baina yenu, kufahamishana kwa mali na watoto. Ni kama mimea inastawi vizuri wakati wa mvua, hili huwafurahisha wenye mashamba, kisha hunyauka ukaiona imepiga umanjano, kisha inakuwa mabua. Na akhera kuna adhabu kali, na msamaha wa Mwenyezi Mungu na radhi. Na hayakuwa maisha ya dunia ila ni starehe idanganyayo: (Al-Hadyd:20).

Kwa muhtasari katika ulimwengu huu, Mwenyezi Mungu, kama dalili ya kuonesha nguvu yake zisizo kikomo na elimu yake iliyopea, ameumba vitu vingi vizuri na vya kustaajabisha, na hali kadhalika vitu dhaifu mno. Vitu vya kudumu na bora kupita kiasi ni kinyume cha kanuni za ulimwengu huu. Hakuna akili ya mwanadamu inayoweza kufikiri pamoja na maendeleo ya teknolojia na ufundi uliofikiwa, kuweza kubadili kanuni hii ya Mwenyezi Mungu. Ndivyo hivyo ili watu wapiganie kufikia maisha baada ya kufa ni kuonesha shukurani na kumtukuza Mwenyezi Mungu. Aidha imekuwa hivyo ili watu waweze kutanabahi kuwa zawadi hizi tulizojaaliwa nazo si za ulimwengu huu wa muda bali ni zawadi kwa ajili ya ulimwengu wenye kudumu ulioandaliwa kwa ajili ya waumini. Katika Qur’an hayo yamebainishwa kama ifuatayo:-

‘Lakini ninyi mnapenda zaidi maisha ya dunia. Hali ya kuwa ya Akhera ni bora na yenye kudumu.’ (A’laa:16 - 17).

Aya nyingine inasema: ‘Hayakuwa maisha hayo ya dunia ila ni upuuzi na mchezo; na nyumba ya Akhera ndio maisha hasa: Laiti wangalijua (Ankabuuti:64)

Kuna mpaka mwembamba sana baina ya ulimwengu huu (ambao ni wa muda) na maisha halisi ya Mwanadamu (Akhera). Kifo ndicho kinachonyanyua pazia hili. Kutokana na kifo, mtu anakata uhusiano na mwili wake na dunia hii, na kisha anaanza maisha ya milele na umbile lake halisi za asili ni hizo zinazohusu maisha baada ya kufa.

Kukonda, kutokamilika na kutodumu ni miongoni mwa kanuni za ulimwengu huu, hivyo si halisi na zisizobadilika. Kanuni halisi zimefumwa katika mfano ambao msingi wake mkuu ni kutokuwa na mwisho, yaani ni za milele. Kakuna kufa na ni zenye ubora wa hali ya juu kabisa.

Kwa maneno mengine, iliyokawaida ni maua yasiyonyauka, mtu asiyezeeka, matunda yasiyooza. Kanuni halisi huweka taratibu za utambuzi wa haraka juu ya yale anayopenda mwanadamu ikiwemo kuondolewa maumivu, ugonjwa, kutokwa jasho na hata kuhisi baridi. Hata hivyo, kanuni zisizo za kudumu (za muda) ndizo zinazotawala ulimwengu huu wa muda, wakati ambapo sheria halisi zinahusiana na ulimwengu wa maisha yajayo. Yote tunayokumbana nayo yasiyo na utimilifu na yenye mapungufu katika dunia hii yapo kutokana na mpango wa makusudi wa kupindisha hizo kanuni halisi.

Kuendelea kwa kanuni halisi baada ya zile za muda, zijulikanazo kama kiama au maisha baada ya kufa sio mbali sana kama inavyofikiriwa. Mwenyezi Mungu anaweza akakatisha maisha ya mwanadamu wakati wowote ule akipenda. Hapo hapo mja atakuwa amekwisha fika katika ulimwengu huo uliotawaliwa na kanuni za kudumu. Mpito huo unaweza kuwa ndani ya muda mfupi mno, kiasi cha kupepesa jicho. Hii ni sawa na kuamka kutoka kwenye njozi. Aya ya Qur’an inafafanua kuhusu umri katika dunia hii kwa kusema:

Atasema ‘Mlikaa muda gani katika ardhi kwa hisabu ya miaka? Watasema, ‘Tulikaa siku moja, au sehemu ya siku.’ Basi waulize wale wajuao hesabu.’ Atasema, ‘Ninye hamkukaa humo ila kidogo tu, laiti mngalikuwa mumejua. Je, mlidhani ya kwamba tumekuumbeni bure na ya kwamba ninyi kwetu hamtarudishwa? (Al-Muuminun: 112 - 115).

Wakati kifo kinapowadia, njozi nazo hufikia ukomo na mwanadamu huanza maisha halisi. Mwanadamu ambaye ameishi duniani kwa kitambo kifupi mno, kiasi cha kupepesa jicho, anakuja mbele ya Mwenyezi Mungu kuhesabiwa matendo yake.

Kama katika maisha yake alizingatia kifo na akaishi kwa kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu. Katika Qur’an wale watakaopewa kitabu ‘kwa mkono wa kulia’ wamenukuliwa kama ifuatayo:-

‘Basi ama yule atakayepewa daftari lake kwa mkono wake wa kuume atasema ‘Haya someni daftari langu.’ Hakika mlijua ya kuwa nitapokea hisabu yangu. (Al-Haqqah: 19 - 20).


    
4 / total 8
You can read Harun Yahya's book Kufa Ufufuko Jahannam online, share it on social networks such as Facebook and Twitter, download it to your computer, use it in your homework and theses, and publish, copy or reproduce it on your own web sites or blogs without paying any copyright fee, so long as you acknowledge this site as the reference.
About this site | Tengeneza kurasa yako ya nyumbani | Add to favorites | RSS Feed
Mambo yote yanaweza kuynakiliwa, kuchapwa na kusambazwa kwa kurejea katika kurasa hii
(c) All publication rights of the personal photos of Mr. Adnan Oktar that are present in our website and in all other Harun Yahya works belong to Global Publication Ltd. Co. They cannot be used or published without prior consent even if used partially.
© 1994 Harun Yahya.www.harunyahya.com
page_top