Kufa Ufufuko Jahannam

SHUSHA KITABU

Download (DOC)
Maoni

SURA ZA KITABU

< <
5 / total: 8
KUFA UFUFUKO JAHANNAM - Harun Yahya
KUFA UFUFUKO JAHANNAM
   WASIOJIFUNZA KUTOKANA NA KIFO HALI YAO HAPA DUNIANI NA HUKO AKHERA

Wengi katika watu hawana dhana kamili juu ya kifo. 'Kifo ni pale maisha yanapokwisha' ni miongoni mwa maneno yao. Tukipiga hatua moja mbele, mwingine anadhani kuwa ni pale maisha yanayofuatia yanapoanzia. Ufahamu huu mfinyu humfanya kafiri kufinyanga kila kitu anachotaka katika kipindi hiki kifupi cha maisha haya. Ndio maana wale ambao hawatanabahi juu ya maisha baada ya kufa, wanaotaka kufanya kila liwezekanao katika dunia bila kujali kuwepo kwa upande wa pili. Si wenye kutofautisha zuri na baya. Wanatafuta kutosheleza matamanio yote ya nafsi zao katika uso wa dunia hii. Hali hii imeegemea katika fikra kwamba kifo kinahitimisha furaha na starehe za mwanadamu. Haamini kuwa bado wana miaka mingi usoni, wanayofukuzia mipango ya muda mrefu. Wanadhani kuwa wao wana akili nyingi mno huku wakiwadhania waumini walio na imani isiyotetereka juu ya Mwenyezi Mungu na Akhera na hivyo kujiandaa vyema, kuwa hawana busara. Hii ni moja ya njia pevu itumiwayo na shetani katika kumghilibu Mwanadamu. Mwenyezi Mungu anatutaka tuzingatie hali hii ya kughilibiwa katika aya zifuatazo:-

'Anawaahidi na anawatumainisha; kwani shetani hawaahidi ila udanganyifu. (An-nisaa:120).

Kwa hakika wale wanaorudi kimgongomgongo baada ya kuwabainishia uongofu, shetani amemdanganya; na (Mwenyezi Mungu) anawapa muda (Muhammad:25).

Wakitafuta kujikusanyia mali, jaha na mengineyo, katika dunia hii kama kwamba maisha haya ni ya milele, makafiri huyachulia maisha kama mashindano. Katika uhai wao wote, hujivunia mali na watoto. Majivuno haya huwapa utukufu wa kujtengenezea ambao huwahamisha kabisa kifikra na hivyo kuacha kufikiria Akhera. Hata hivyo aya zifuatazo zinadhihirisha walipoegemea kwa sababu ya upotofu wao:-

'Je wanafikiri ya kuwa yale tunayowapa mali na watoto ndio tunawatangulizia katika kheri? Hapana, lakini hawatambui.' (Muuminuun: 55-56).

Mwanadamu yampasa kuendeleza mali na watoto na kuvijaalia ndio vivutio vyake vikuu ya maisha. Allah anatoa onyo hili kwa kusema:-

'Yasikufurahishe mali yao wala watoto wao. Anataka Mwenyezi Mungu awaadhibu kwa hayo katika maisha ya dunia, na zitoke roho zao, na hali ya kuwa ni Makafiri.' (At-tawbah:55).

Mwenyezi Mungu amempa mwanadamu maonyo na ujumbe mwingi ili kwa huo atanabahi juu ya kifo na Akhera. Katika aya moja, Mwenyezi Mungu anatutaka tuzingatie majaribu au mitihani tunayoipata kama ni sehemu ya kuonywa.

Je hawaoni kwamba wanatiwa mitihani kila mwaka mara moja au mbili? Kisha hawatubu wala hawakumbuki (At-Tawb:126)

Kwa hakika watu wengi hupata mitihani, ili waweze kuomba msamaha mara kwa mara na kujichunga kwa kurejea. Haya yanaweza kutokea mara chache pengine mara moja au mbili katika mwaka kama ilivyobainishwa katika aya. Badala yake, inaweza ikawa ni mikiki mikiki au matatizo ya kila siku. Mwanadamu anashuhudia ajali, vifo au majeruhi. Magazeti na vyombo vingine vya habari hutoa taarifa nyingi kuhusu kifo na rambirambi. Katika muonekano wa matukio kama hayo, mwanadamu anapaswa akumbuke kwamba majanga yanaweza kutokea wakati wowote na muda wowote ule. Pia mtihani wake unaweza ukafikia mwisho. Kuchukua hadhari kama hizo humfanya mja kumuelekea Mola wake kwa moyo mkunjufu, huku akiomba kinga kutoka kwake na akiomba msaada wa kusamehewa kutoka kwake kadhalika.

Mafunzo Muumini anayoyapata kutokana na majanga anayokumbana nayo ni yenye kuendelea. Hata hivyo, matukio hayo hayo huwa na athari tofauti kwa mtu ambaye hana imani (kafiri). Kwa kuhofishwa na fikra juu ya kifo, hujaribu kujisahaulisha na kifo. Kwa kufanya hivyo hutafuta nafuu. Hata hivyo njia hii ya kujilaghai, humsababishia maangamizi na madhara. Hiyo ni kwa sababu, Mwenyezi Mungu huwaokoa na kuwapa muda hadi muda maalum uliowekwa. Na muda huu kinyume na wanavyo fikiri, huwadhuru wao. Mwenyezi Mungu anasema:

'Na lau Mwenyezi Mungu anawatesa watu kwa sababu ya maasi yao; asingalimwacha hata mnyama mmoja juu ya ardhi; lakini anawaakhirisha mpaka muda uliowekwa. Na unapofika muda wao hawawezi kukawilia saa moja wala hawawezi kuutangulia. (An-Nahl"61)

Katika aya nyingine Qur'an inabainisha:

'Wala wasidhani wale waliokufuru kwamba huu muda tunaowapa ni bora kwao. Hakika tunawapa muda na wanazidisha madhambi. Na itakuwa kwao adhabu ya kuwadhalilisha. (Al-Imran: 178)

Mtu aliyeghafilika ambaye hupata mafunzo hata pale kifo kinapomchukua mtu aliyekaribu naye, anakuwa mwaminifu kwa kumuelekea Mwenyezi Mungu pale yeye mwenyewe anapokuwa katika misikosuko ya kifo.

Saikolojia hii inaelezwa ndani ya Qur'an kama ifuatayo:-

'Yeye ndiye anayekuendesheni katika bara na bahari. Hata mnapokuwa katika majahazi na yanakwenda nao kwa upeo mzuri na wakafurahi zao; mara upepo mkali unayajia na mawimbi yanawajia kutoka kila upande, na wanaanza kufikiri ya kwamba wametingwa. (Hapo ndipo) wanapomuomba Mwenyezi Mungu kwa kumtakasia utii. Ukituokoa katika haya, bila shaka tutakuwa miongoni mwa wanaoshukuru. (Yuhus:22).

Akiwa ni mwenye kukata tamaa, mwanadamu hujaribu tena kufanya kama hayo wakati wa kufa. Wakati huo muda uliokadiriwa kwake umekwisha wadia.

Na ungaliwaona waovu wakiinamisha vichwa vyao mbele ya Mola wao, 'Mola wetu" Tumekwisha kuona na tumekwisha kusikia, basi turudishe, tutafanya vitendo vizuri; hakika tumeyakinisha'. Na tungalitaka tungempa kila mtu uongofu wake, lakini imehakikika kauli iliyotoka kwangu. Kwa yakini nitaijaza Jahannam kwa wote hawa; majini na watu. 'Basi ionjeni (adhabu) kwa sababu ya kusahau makutano ya siku yenu hii. Na sisi tutakusahauni.; na onjeni adhabu idumuyo kwa yale mliyokuwa mkiyatenda. (As-Sajidah:12-14).

'Nao humo watapiga kelele, 'Mola wetu! Tutoe humu! Tutafanya vitendo vizuri visivyokuwa vile tulivyokuwa tukifanya.' "Hatukukupeni amri ya (kuweza) kukumbuka mwenye kukumbuka? Na akakujieni Mwonyaji. Basi onjeni (adhabu) madhalimu hawana wa kuwanusuru (Al-Fatir:37)

Juhudi hizi zisizotia matumaini huko akhera na mwisho huo uumizao ni matokeo ya kupuuza kwa mwanadamu na kukosa shukurani kwa kutozingatia lengo halisi la kuwepo kwake hapa duniani na thamani yake. Yeyote asiye na imani hawezi kupata mafundisho kutokana na matukio yanayaomzunguukia; hawezi kusikiliza maonyo yanayotoka kwa Mwenyezi Mungu, akijisingizia ujinga juu ya yale ambayo moyo wake unayajua au kwa makusudi akakanusha na akaona kifo kuwa hakiwezi kumtokea. Anakubaliana na matakwa ya upande dhaifu wa nafsi yake kuliko kupata ridhaa ya Mwenyezi Mungu. Yote hayo hatimae hujitokeza wakati kifo chake kimewadia na hivyo kushikwa na bumbuazi na kuwa mwenye kukata tamaa na kujikuta katika hali iliyoelezwa katika aya hapo juu. Hivyo, kifo kabla hakijamkabili yeyote, lazima mja aamke katika lindi la usingizi wa kughafilika (kukosa mwelekeo), kwani wakati wa kukata roho itakuwa fursa hiyo haipo tena. Hii ni kutokana na kuchelewa kuamka na kuzindukana na hivyo uwezekano kufifilika.

Na toeni katika yale tuliyokupeni, kabla mmoja wenu hayajamjia mauti, kisha akasema, 'Mola wangu! Huniakhirishi muda kidogo nikatoa sadaka na nikawa miongoni mwa watendao mema? Lakini Mwenyezi Mungu haiakhirishi nafsi yoyote inapokuja ajali yake: Na Mwenyezi Mungu anazo habari za yote mnayoyatenda. (Al-Munafiquun: 10-11).

Mtu yeyote mwenye akili muda wote anawaza juu ya kifo kuliko kujiepusha na fikra juu ya kifo. Ndipo tu anaweza kupata ridhaa ya Mwenyezi Mungu na kuepushwa na udhaifu wa nafsi na pia vitimbi vya shetani katika kumhadaa na maisha haya yadanganyayo. Kwa hakika, kuyafanya maisha ya dunia hii ndilo lengo pekee la maisha ni hatari kubwa kwa mwanadamu. Mtume Muhammad (SAW)amea amewakumbusha hili wafuasi wake katika dua yake:

'Usitujaalie maisha ya dunia hii yawe ndio ya kutushughulisha zaidi kuliko yale tunayoyafahamu. (imesimuliwa na Abdallah bin Umar - At-tirmidh, 783).

KUJIANDAA KWA KIFO

Ulimwengu huu ni mahali ambapo mwanadamu anafundishwa. Mwenyezi Mungu amempa majukumu mengi na kumfahamisha mipaka aliyomuwekea. Endapo Mwanadamu atachunga mipaka hii, atafuata maamrisho yake na kuacha makatazo yake, atafikia hali ya ukomavu na hali bora ya utambuzi na busara. Kwa kupata sifa hizo, muumini huonyesha subira ya hali ya juu bila kujali yanayomsibu; humuelekea Mwenyezi Mungu tu na kumuomba yeye peke yake msaada. Hizi ndio njia pekee za kumtukuza Mwenyezi Mungu na kuhisi hasa kujisalimisha kwake kutoka ndani ya nafsi na imani isiyo na ukomo juu yake. Kwa kujua thamani halisi ya neema alizopewa na Mwenyezi Mungu hudhihirisha shukurani za dhati kwa Mwenyezi Mungu na kujisikia yuko karibu naye.

Matokeo yake, anakuwa Muumini muadilifu akitunukiwa sifa nzuri za busara na tabia njema. Si hivyo tu, anakuwa aina ya mtu anayestahili kuingia peponi, mahali palipotimia kwa Uzuri na Ubora.

Lakini endapo mtu hatapata Elimu juu ya hakika ya dunia hii, atashindwa kuonesha mwenendo mzuri na japo hali bora kutokana na mtazamo wa kivitu utawekwa mbele yake, atabakia katika hali zote za mtu mwenye kushindwa. Kwa hakika nabii Adam (amani iwe juu yake) ameletwa duniani kupokea mafunzo na akapewa mtihani maalum ulioandikwa na Mwenyezi Mungu kumuandaa kwa maisha yake ya milele. Mwishoni, akaibuka kuwa mtu mpevu katika tabia njema na mwenendo mzuri wa kupigiwa mfano ndani ya Qur;an. Mwanadamu huyu anaendelea kujaribiwa kwa matukio mengi juu yake. Endapo atafaulu katika kuyaendea atapata malipo mema ya kuendelea huko Akhera, lakini atakapofeli, malipo yake akhera itakuwa kuadhibiwa milele. Hakuna mwanadamu hata mmoja ajuae mwisho wa kujaribiwa kwake itakuwa ni lini. Kwa maneno ya Qur'an:-

'Na nafsi yoyote haitaweza kufa ila kwa amri ya Mwenyezi Mungu kwa ajali iliyowekwa. Na anayetaka malipo ya duniani tutampa, basi, hapa; na anayetaka malipo ya Akhera tutampa huko, na kwa yakini tutawalipa wanaoshukuru. (Al-Imraan: 145).

Kipindi hiki kinaweza kuwa kirefu, na vile vile kinaweza kuwa kifupi. Ukweli ni kuwa, hata kama kinakuwa kirefu, ni mara chache kuvuka miaka 70 au 80. Ndio maana, kuliko kujitumbukiza katika kutengeneza mpango wa muda mrefu, mwanadamu, anatakiwa aongozwe na Qur'an na aishi kwa kanuni ya hiyo Qur'an, kwa kujua kwamba, atakwenda kuwasilisha hesabu yake huko Akhera.

Kinyume chake, kushindwa kufanya maandalizi kwa ajili ya Akhera, ni kukosa nafasi moja ya pekee aliyotunukiwa na lengo hili, na hivyo kustahiki kutumbukizwa motoni milele. Haya yatakuwa majuto ya hali ya juu, yenye kuumiza. Isisahaulike kwamba kukosa kuingia peponi milele hakuna sehemu nyingine ya kuingia isipokuwa motoni. Ndio maana kila sekunde inayopotea katika mchezo katika dunia hii ni hasara kubwa na hatua potofu iliyofuatwa kuelekea kwenye maangamizi na mwisho mbaya. Kwa kuwa hivi ndivyo ilivyo, ukweli huu utangulizwe kwa hilo linalotaka kufanywa hapa ulimwenguni. Kama vile mwanadamu afanyavyo maadalizi ya kukabiliana na yale yanayokuja kutokea mbeleni hapa duniani, vivyo hivyo inapasa kutumia juhudi zaidi katika kufanya maandalizi kwa ajili ya maisha yajayo. Hii ni kwa sababu wale watakaokufa si wengine bali ni binadamu hawa hawa. Mwanadamu atashuhudia kila kitu kitakachotokea baada ya kufa kwake. Hivyo somo hili linamhusu kila mwanadamu, kwa maneno mengine kila nafsi. Kwa wale wanaotafuta ukombozi wa milele, Mwenyezi Mungu anaamrisha yafuatayo:-

'Enyi mlioamini! Mcheni Mwenyezi Mungu; na kila mtu aangalie anayoyatanguliza kwa ajili ya kesho; na mcheni Mwenyezi Mungu; hakika Mwenyezi Mungu anazo habari za yote mnayoyatenda. Wala msiwe kama wale waliomsahau Mwenyezi Mungu, na akawasahaulisha nafsi zao. Hao ndio maasi makubwa. (Al-Hashir:18-19).

KUFUFULIWA

Qur'an inafahamisha kuwa:-

'Lakini mtu anataka tu kuyakataa yaliyombele yake. Anauliza,' Itakuwa lini hiyo siku ya kiama? Wakati litakapoparama jicho. Na mwezi utakapopatwa. Na jua na mwezi vikapokutanishwa. Mtu atasema siku hiyo pa wapi mahali pa kukimbilia?' Hakuna mahali pa kukimbilia!" Siku hiyo marejeo ni kwa Mola wako. (Al-Qiyamah:5-12).

IMANI JUU YA MAISHA YAJAYO

Imani juu ya maisha baada ya kufa ni moja katika nguzo muhimu za Imani. Katika sura ya kwanza ya Qur'an, Surat Fat-ha, baada ya sifa yake Mwenyezi 'Mwingi wa Rehema' na 'Mwingi wa Ukarimu', Mwenyezi Mungu anaeleza kuwa 'Yeye ni Mfalme wa Siku ya Malipo'. (Al-fatha 3). Katika aya ya tatu ya sura inayofuata, inaeleza kuwa moja ya Sifa za waumini ni '... Wale wenye kuamini ghaibu (yasiyoonekana)...' (Al-Baqarah:3)

Hii dhana ya 'ghaibu - visivyoonekana' pia inajumuisha kufufuliwa baada ya kufa, siku ya kiama, pepo na moto. Kwa muhtasari kila linalohusiana na maisha baada ya kufa. Kwa hakika katika aya ya nne ya Surat Baqarah maneno '... wana hakika juu ya akhera; msisitizo maalum umewekwa kuhusu imani juu ya maisha baada ya kufa. Imani juu ya visivyoonekana ni alama juu ya Imani ya Akhera ua Kiama na kwa hakika ni muhimu mno. Aina ya imani juu ya akhera kama ilivyoainishwa ndani ya Qur'an inatoa ushahidi wa uaminifu na ukweli wa Muumin. Aliye na imani juu ya Akhera tayari ameweka imani yake isiyo na pingamizi kwa Mwenyezi Mungu, katika kitabu chake na kwa mtume wake. Mja kama huyo anajua kwamba Mwenyezi Mungu ana uwezo juu ya kila kitu na kwamba maneno yake na ahadi zake ni kweli. Matokeo yake, kamwe hawezi kuwa na shaka juu ya Akhera. Kabla ya kuona na kushuhudia hakika hii, aliweka imani yake kwa viwili hivi (uwezo na ahadi ya Mwenyezi Mungu) kama kwamba tayari amekwisha Dua. Haya ni matokeo yanayopatikana kutokana na Imani na matarajio aliyoweka kwa Mwenyezi Mungu na busara aliyotunukiwa.

Zaidi ya hayo, imani isiyotetereka juu ya Akhera, hutakasa aina zote za mashaka, yanayohusishwa na imani juu ya kuwepo Mwenyezi Mungu na pia katika sifa zake, kama iliyofafanuliwa katika Qur'an, na matarajio timilifu kwake na kujisalimisha kwake. Imani hii pia humfanya mtu amjue Mwenyezi Mungu na amkubali katika uhalisia wa kumkubali. Aina hii ya Imani Mwenyezi Mungu huichukulia kuwa ni yenye thamani mno. Katika kurasa za mbele itadhihirika kuwa ushawishi mkubwa katika kuridhika kwa mwanadamu ni kwa kutegemea kuleleka kwenye imani ya kweli juu ya maisha baada ya kufa.

Sehemu nyingi ndani ya Qur'an, zipo rejea kuwa makafiri ukanushaji wao juu ya akhera na kutotoa uamuzi juu ya kuthibitika kwake, ndiko kunakowafanya wazidi kuangamia. Kwa hakika wengi katika makafiri wanaamini juu ya kuwepo kwa Mwenyezi Mungu - Lakini kinachowapoteza wengi wao si suala linalohusu kuwepo kwa Mwenyezi Mungu bali ni kuhusu sifa zake. Miongoni mwao huamini kuwa awali Mwenyezi Mungu huumba kila kitu na kuwaacha viumbe wawe wanatenda kutokana na waonavyo wao. Wapo baadhi ambao hushikilia kuwa Mwenyezi Mungu Amemuumba Mwanadamu, lakini ni mwanadamu mwenyewe anayeamua hatima yake. Pia lipo kundi lingine ambalo hushikilia kuwa Mwenyezi Mungu hajui mawazo ya ndani na siri za watu. Wengine huamini juu ya kuwepo kwa Mwenyezi Mungu, lakini hupinga wazo la kuwepo kwa dini au mfumo wa maisha aliouweka Muumba ambao wanaadamu hutakiwa kuufuata. Kundi hili la mwisho linaelezewa na Qur'an kama ifuatayo:-

'Na hawakumhishimu Mwenyezi Mungu kama inavyotakiwa kumhishimu, waliposema: "Mwenyezi Mungu hakuteremsha chochote juu ya binadamu yeyote: (Al-Anam:91).

Matokeo yake, badala ya kukanusha moja kwa moja kuwepo kwa Mwenyezi Mungu, 'Hawampi Mwenyezi Mungu kipimo chake halisi na hivyo basi, huishia katika kukanusha akhera na kuishi bila ya imani. Kwa hakika, kundi linalokanusha moja kwa moja kuwepo kwa Mwenyezi Mungu ni dogo na kundi kubwa hupendelea kutilia shaka katika kushawishika na yale wasiyoamini. Ndio maana Qur'an haizungumzii sana juu ya wale wanaokanusha kuwepo kwa Mwenyezi Mungu. Badala yake zitaonekana rejea nyingi juu ya watu wanaomshirikisha Mwenyezi Mungu na wanaokanusha kufufuliwa, siku ya hukumu, pepo, moto na yale yote yanayohusiana na imani juu ya Akhera. Japo akhera ni hakika ambayo milango mitano ya fahamu haiwezi kuthibitisha, Mwenyezi Mungu ameumba mifano mingi ambayo fikra za mwanadamu zinaweza kuelewa. Ni ukweli usiopingika kwamba hitajio tangulizi ili mtu afaulu mtihani hapa ulimwenguni, lazima afahamu ukweli huu, si kwa kupitia milango ya fahamu, bali busara na maumbile.

Mtu yeyote wa kawaida, baada ya kutafakari, kwa wepesi tu hugundua kwamba vyote vinavyomzunguuka, akiwemo yeye mwenyewe havitajitokeza kwa bahati nasibu bali ni kutokana na Mwenye Nguvu za hali ya juu kabisa, mdhibiti na mwenye utashi yaani Muumba. Kisha, mara huzingatia na kufahamu kuwa kuumbwa kwa akhera ni jambo jepesi mno kwa Mwenyezi Mungu. Zaidi ya hapo atatambua kwamba, kutokana na busara na uadilifu wa Mwenyezi Mungu hufanya hitajio la kuwepo Akhera. Japo hili liko wazi mno, lakini wale wanaokanusha maamrisho ya Mwenyezi Mungu, hawapendi wazo la kuwa watafufuliwa kutoka katika wafu. Kama yule anayetumia maisha yake kuyatosheleza matashi ya nafsi yake. Hayuko radhi kusimama mbele ya Mwenyezi Mungu na kupokea hesabu ya matendo yake aliyofanya katika kipindi cha uhai wake wote. Ndio maana, japo ana yakini kwamba Mwenyezi Mungu yupo, atahiyari kuchagua kwamba akandamize kila fikra inayomjengea utambuzi huo na hivyo kujichanganya mwenyewe. Katika kuweka mawazo yake kwenye ufinyu huo, kafiri huanza bila kutumia busara, kuparaganyisha na kukanusha kufufuliwa na Akhera.

'Na akatupigia mfano, na akasahau kuumbwa kwake - akasema 'Nani atakayeihuisha mifupa na hali imesagika?' (Yasin:78).

Hata hivyo swali hili limebuniwa kwa lengo la kukwepa ukweli na kujikweza katika kujihadaa, linajibu lililo jepesi mno.

'Sema: "Ataihuisha yule aliyeiumba mara ya kwanza, naye ni mjuzi wa kila (namna ya) kuumba. ('Yasin: 9).

Ndani ya Qur'an Mwenyezi Mungu ameweka wazi kwamba milinganyo kama hiyo isiyo na mantiki ni dhana zitokanazo na makafiri:

'(waungu) wa wale wasioamini Akhera wana mifano mibaya (ya kupigiwa). Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye sifa tukufu; naye ni mwenye nguvu Mwenye hekima (Al-Nahl:60).

Wengine, kwa upande wao wamejaribu kuhalalisha misimamo yao kwa kutoa kile kinachoitwa - ufafanuzi.

'Wanasema, "Je! Kweli tutarudishwa katika hali (yetu) ya kwanza? Hata tukiwa mifupa mibovu?' Wanasema (kwa stihizai)" Basi marejeo haya ni yenye khasara: (Naziat: 10 - 12).

Kwa hakika, pamoja na kushawishika juu ya hilo, hawajizuilii kueleza kwamba kuwepo kwa akhera hakuendani na malengo yao ya maisha. Kafiri hujenga busara zake kwa kutegemea matamanio ya nafsi yake. Kwa kuona udhaifu wa madai yake mwenyewe, bado huliendea suala hili kwa kulikwepa kabisa na kwenda mbali zaidi kwa kusaka namna ya kujisaidia kisaikolojia.

'Nao (wakaapa) kwa jina la Mwenyezi Mungu kwa kiapo chao cha nguvu (kwamba) Mwenyezi Mungu hatawafufua wafao. Kwa nini? Ni ahadi iliyolazimika kwake, lakini watu wengi hawajui. (Nahl:38).

Kwa kuyachukulia matamanio na fikra zao kwamba ndio miungu, watu hawa hutamka maneno ili kuondoa hisia zote kwamba kwa halali na haramu na kinyume chake wanatafuta hifadhi kwa vile walivyovijaalia kuwa ndio miungu yao.

Mwenyezi Mungu anafafanua tabia za watu hawa wanaokanusha kuwepo kwa Akhera:

'Na bila shaka tumewaumbia moto wa Jahannam wengi katika majini na wanadamu: Nyoyo wanazo lakini hawafahamu kwazo, na macho wanayo lakini hawaoni kwayo, na masikio wanayo lakini hawasikii kwayo. Hao ni kama wanyama bali wao ni wapotofu zaidi. Hao ndio walioghafilika. (A'araf:179).

Katika sehemu nyingine ya Qur'an, hali ya watu hawa imefafanuliwa kama ifuatavyo:-

'Je! umemuona yule aliyefanya yale anayoyataka yeye, kuwa ndio Miungu wake; na Mwenyezi Mungu akamuacha apotee pamoja na kuwa ana ujuzi; na akapiga muhuri juu ya masikio yake na moyo wake; na kumtia kitanga machoni pake; basi nani atamuongoza baada ya Mwenyezi Mungu? Basi je hamkumbuki? Na walisema: 'Haukuwa (uhai) ila ni uhai wetu huu wa dunia, tunakufa na tunaishi, wala hakuna kinachotuangamiza isipokuwa (huu huu) ulimwengu; wala wao hawana ilimu ya hayo, wanadhani tu. (Al-Jathiyah: 23 -24).

HALI HALISI YA MAISHA YA KIDUNIA

Makafiri hudai kuwa huwezi kufahamu baadhi ya mambo kwa kutumia busara. Kifo, kufufuliwa na maisha ya Akhera ni miongoni mwa mambo hayo. Mwanadamu anaweza kuyahusisha matukio haya na nadharia yake ya matukio ya usingizi na njozi. Yeyote anayekazania kukanusha kwamba hawezi kufufuliwa baada ya kufa, na pia akasisitiza kuepukana na fikra za kifo, kwa hakika hana habari kwamba anaonja kifo kila usiku na pia kuonja kufufuka kila asubuhi anapotoka usingizi kama ifuatayo:-

'Mwenyezi Mungu hutakabadhi roho wakati wa mauti yao. Na zile zisizokufa (pia) anazitakabadhi) katika usingizi wao. Basi huzizuia zile alizozikidhia mauti, na kuzirudisha zile nyingine mpaka wakati uliowekwa. Bila shaka katika hayo yamo mazingatio kwa watu wanaotafakari. (Az-zumari: 42).

Naye ndiye aliyekufisheni wakati wa usiku, na anayafahamu mnayo tenda wakati wa mchana; kisha yeye hukufufueni humo ili muda uliowekwa umalizike. Kisha, kwake tu (Mwenyezi Mungu) marudio yenu. Akwambieni (yote) mliyokuwa mkiyafanya: (Al-An-am: 60).

Katika aya hizo hapo juu, hali ya usingizi imerejewa kama 'Kifo'. Hakuna kilichobainisha wazi kati ya 'kifo' na usingizi. Kipi tena kinachotokea wakati wa usingizi ambacho kinaoanishwa na kifo? Usingizi ni kusafiri kwa roho ya mwanadamu kutoka katika mwili (kiwiliwili) ambapo hurejea mara mja anapoamka kutoka katika usingizi. Katika kuota, kwa upande mwingine, roho huwa na mwili mwingine kabisa na kuanza kupata muundo mwingine kabisa. Kamwe mwanadamu hawezi kufikiri kwamba haya yanayotokea ni njozi. Anahisi woga, kujuta na maumivu. Ana hamaki au kuhisi furaha tele. Pia, anakuwa na uhakika kabisa kwamba, yale yanayojitokeza kwake ni ya kweli na mara nyingi hutoa hisia zilezile kama yuko hadhiri. Kama ingewezekana kuingilia kati kutoka upande wa nje na kumuambia mwenye kuota ndoto kwamba yale anayoyaona ni hisia na njozi tu, angeweza kudharau na kupuuzia kuwa anachezwa shere tu. Hata hivyo ukweli ni kwamba maono haya hayana uhusiano wa wazi na yale yanayotokea hapa uliwenguni na kwamba yale anayoyaona katika njozi zake ni katika jumla ya picha na mapokezi ambayo Mwenyezi Mungu ameyaelekeza katika nyoyo za wanadamu.

Nukta muhimu anayotakiwa kuzingatia kichwani ni kuwa, kanuni hiyo hiyo ndiyo inayofanya kazi katika muda ambao mwanadamu yuko macho. Mwenyezi Mungu anathibitisha kuwa njozi ziko katika milki yake na udhibiti wake. Hebu mwanadamu aangalie aya ifuatayo:-

'(Kumbuka) Mwenyezi Mungu alipokuonesha katika usingizi wako (kwamba wao makafiri) ni wachache; Na kama angelikuonesha kwamba wao ni wengi mngalivunjika nyoyo na mngalizozna katika jambo hilo. Lakini Mwenyezi Mungu akakulindeni. Bila shaka yeye ni mjuzi wa yaliyomo vifuani. (Anfal: 43).

'Na (kumbukeni) alipokuonesheni machoni mwenu mlipokutana kwamba wao ni wachache (ili mjasirike kupigana nao), au akakufanyeni ninyi kuwa wachache (mno kabisa) machoni mwao (waone upuuzi kupigana kwa hima na watu wachache kama ninyi, Mwenyezi Mungu amefanya hayo) ili alitimize jambo aliloamrisha litendeke. Na mambo yote hurejeshwa kwa Mwenyezi Mungu. (Anfal:44).

Hutoa ushahidi ulio wazi kuwa kanuni hiyo hiyo inayofanya kazi hapa duniani katika maisha ya kila kitu. Uhakika kwamba tunayoyapokea na picha tulizonazo kuhusu maada kwa ujumla wake hutegemea kutaka na kuumba kwa Mwenyezi Mungu na kwamba mbali na hayo, hakuna kuwepo kwa ulimwengu wa nje. Haya yameelezwa katika aya ifuatayo:

'Hakika imepatikana alama kubwa kwenu (ninyi) katika yale makundi mawili yaliyokutana; kundi moja lilipigana katika njia ya Mwenyezi Mungu, na jingine makafiri. (Makafiri) wakawaona (Waislam) zaidi kuliko wao mara mbili kwa kuona kwa macho, na Mwenyezi Mungu humtia nguvu, kwa nusra yake, amtakae. Kwa yakini katika hayo yamo mazingatio (makubwa) kwa wenye busara. (Al-Imran: 13).

Kama ilivyo katika njozi, kile kinachoonekana katika taratibu za kila siku na yale yanayodhaniwa yapo katika ulimwengu katika sura yake ya nje ni picha zilizopandikizwa katika nafsi za wanadamu toka kwa Muumba wao, sanjari na hisia alizowafanyia wazipokee kwa wakati mmoja. Picha na vitendo vinavyofanywa na miili ya wanadamu sawa na zile za viumbe wengine, vipo kwa kuwa Mwenyezi Mungu ameumba picha zinazooana na kupokezana hatua kwa hatua. Ukweli huu umebainishwa katika Qur'an:-

Hamkuwaua ninyi lakini Mwenyezi Mungu ndiye aliyewaua, na hutupa wewe (mtume) ulipo tupa walakini Mwenyezi Mungu ndiye aliyeutupa. Aliyafanya haya Mwenyezi Mungu ili awape walioamini hidaya nzuri itokayo kwake. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye asikiaye na ajuaye. (Anfal:17).

Kanuni hiyo hiyo ya Mwenyezi Mungu ndiyo inayotumika katika kuumbwa kwa Akhera na picha na maono yanayohusiana. Wakati kifo kinapowadia, uhusiano wote kuhusu ulimwengu huu na mwili hukatika. Roho hata hivyo ni ya milele kwa sababu Mwenyezi Mungu ameipulizia. Kila kitu kihusianacho na uhai, kifo, kufufuliwa na maisha ya akhera inajumuisha mitazamo kadhaa inayoonwa na roho ya milele. Ndio maana, kutokana na hoja za msingi hakuna tofauti kubwa kati ya kuumbwa kwa ulimwengu huu na ile ya pepo au moto. Vivyo hivyo, mpito kutoka dunia hii kuelekea akhera hauna tofauti na kuamka kutoka usingizini na kuendelea na maisha ya kila siku.

Kwa kufufuliwa, maisha mapya huanza huko akhera akiwa mja na mwili mwingine. Mara hisia zihusuzo pepo au moto zinapodhihirishwa kwenye nafsi, mja huanza kuhisi hayo (ya peponi au motoni). Mwenyezi Mungu, Muumba wa picha zisizo na ukomo vivuli, sauti, harufu, vionjo vihusuvyo maisha haya, pia, kwa utaratibu kama huo, utaumba picha zisizo na ukomo na hisia za peponi hali kadhalika za motoni. Kwa Mwenyezi Mungu, uumbaji, huo ni rahisi mno:-

'Yeye ndiye) Muumba wa mbingu na ardhi pasi na ruwaza; na anapotaka jambo basi huliambia tu, 'kuwa'; nalo huwa (Al-Bawarah: 117).

Hoja nyingine ya kuzingatia ni kwamba, kama ilivyo maisha katika ulimwengu huu yanaonekana kuwa yako wazi na mepesi kuliko ndoto, vivyo hivyo Akhera ikilinganishwa na maisha ya dunia hii. Pia, kama ndoto zilivyofupi kulinganisha na maisha ya dunia hii) ndiyo ilivyo kwa maisha ya dunia hii ukilinganisha na maisha ya Akhera. Kama inavyofahamika, muda au wakati haukutulia kama dhana ya awali ilivyokuwa, sayansi leo hii imethibitisha hili kuwa kuna nadharia ya mvutano (Theory of Relativity). Katika ndoto, tukio linaweza kudhaniwa kuwa kimechukuwa saa kadhaa kumbe limechukuwa sekunde chache tu. Hata ile njozi inayoonekana imetumia muda mrefu, hudumu kwa dakika chache tu. Hata hivyo yule aliyeota hudhani ametumia muda wa masiku au miaka kadhaa akiwa katika njozi hiyo.

Kuhusu muda, na kuonesha kuwa ni suala la kulinganisha na tukio; Qur'an inafafanua:-

'Malaika na Jibril hupanda kwake katika siku ambayo muda wake ni miaka elfu hamsini. (Al-Maarij: 4).

Anapitisha mambo yote yaliyo baina ya mbingu na ardhi, kisha yanapanda kwake kwa siku moja tu ambayo kipimo chake ni myaka elfu mnayotumia ninyi katika kuhesabu kwenu (As-Sajdah: 5).

Mtu anayemaliza miaka mingi katika uliwengu huu, ukweli ni kwamba ameishi muda mfupi sana kulinganisha na nadharia ya muda ya Akhera. Majadiliano yafuatayo katika siku ya hukumu ni mfano mzuri:-

'Atasema: 'Mlikaa muda gani katika ardhi kwa hesabu ya miaka? Watasema. 'Tulikaa siku moja au sehemu ya siku'. Basi waulize wafanyao hesabu'. Atasema, 'Ninyi hamkukaa ila kidogo tu, laiti mngalikuwa mnajua.' Je mlidhani Tumekuumbeni bure na ya kwamba ninyi kwetu hamtarudishwa?" (Al-Muuminun:: 112 - 115).

Kwa vile hali ni hii, ni dhahiri kuwa kupuuzia maisha ya milele kwa ajili ya kuendeleza maisha ya dunia hii ambayo ni ya muda tu ni uchaguzi mbaya. Hii itakuwa wazi zaidi pindi mja anapotafakari ufupi wa maisha ya dunia hii ikilinganishwa na akhera.

Kwa majumuisho, vitu vinavyoitwa maada na kuvijaalia kuwa vipo kwa uhalisia, si chochote bali ni hisia za mwanadamu alizopandikiziwa na Mwenyezi Mungu katika nafsi yake. Mtu anaamini kwamba mwili ni mali yake. Hata hivyo, mwili wenyewe ni kivuliau picha ambayo Mwenyezi Mungu ameipandikiza katika nafsi ya mwanadamu huyo. Mwenyezi Mungu anaweza kuibadili pindi akipenda kufanya hivyo bila kipingamizi chochote. Wakati mwili unapotoweka, ghafla nafsi huanza kuona picha mpya. Kwa lugha nyingine, wakati mtu anapokufa, pazia juu ya macho yake huondolewa na hivyo mtu kugundua kuwa kifo sio kutoweka kama mmoja wao alivyoamini. Haya yamebainishwa katika Qur'an kama ifuatayo:-

Na kutoka roho kutakapomjia kwa hali. (Hapo ataambiwa): 'Haya ndiyo uliyokuwa ukiyakimbia.' Na itapulizwa parapanda (Baragumu); hiyo ndio siku ya makamio. Na itakuja kila nafsi pamoja na mchungaji (wake) na Shahidi (wake). (Aambiwe) "Kwa hakika ulikuwa umo katika ghafla na jambo hili. Basi tumekuondolea (leo) pazia yako; kuona kwako leo kumekuwa kukali (Qaf:19-22).

Makafiri hapo watafikia kilele cha kufahamu vizuri ukweli:

'(Na huku) wanasema: 'Ole wetu! Nani aliyetufufua malaloni petu?" (waambiwe) 'Haya ndiyo yale aliyokuahidini (Mwenyezi Mungu) Mwingi wa Rehema na waliyoyasema kwa haki mitume: (Tasin: 52).

Kuanzia hapo na kuendelea, makafiri watakuwa ni wenye kujuta kusikokuwa na mfano.

KUFA KWA ULIMWENGU

Ndani ya Qur'an, imeelezwa kuwa mbali na viumbwa vyote, ulimwengu pia utafikiwa na umauti. Si mwanadamu pekee aliye na uhai na umauti. Wanyama na mimea pia hufa. Pia sayari na nyota hufa. Kifo ni jambo linalotokea kwa kila kiumbe. Katika mpango wa Mwenyezi Mungu, watu wote, viumbe vyote vyenye uhai, dunia, jua mwezi na nyota, kwa muhtasari, ulimwengu wote wa maada utatoweka. Katika Qur'an, siku hii inaitwa 'Siku ya kufufuliwa.'

'... Siku watakaposimama watu (wote) mbele ya Mola wa walimwengu wote: (Al-Mutasffin: 6).

Kama vile ambavyo kifo cha mtu kinavyotisha, ndivyo hivyo hivyo kwa kifo cha ulimwengu. Katika siku ya kufufuliwa, wale ambao hawakuwa na imani, watakuwa, kwa mara ya kwanza, na hisia nzito juu ya Ukubwa wa Mwenyezi Mungu na nguvu zake. Ndio sababu siku ya kufufuliwa ni siku ya majuto, ya adhabu, ya kujuta, ya machungu, ya kuhangaika, ya kuchanganyikiwa kukubwa kwa makafiri. Mtu anayeshuhudia siku ya kufufuliwa atakuwa na woga kweli kweli. Woga huu usioelezeka ni mara mia moja uzito wake na zaidi kuliko woga wote mtu anaoweza kuhisi katika dunia hii. Qur'an inaeleza kwa undani hatua kwa hatua ya kile kitakachotokea siku ya kufufuliwa. Namna tukio hili kubwa litakavyokuwa na litakavyotokea kwa watu siku hiyo yamefafanuliwa kwa namna inayogusa moyo.

KUPIGWA PARAPANDA KWA MARA YA KWANZA

Siku ya kufufuliwa huanza baada ya parapanda kupulizwa. Hii ni alama kuwa mfumo wa dunia na ulimwengu wote unabadilika. Unakuwa mfumo mwingine. Mwisho wa maisha ya dunia hii ndio mwisho. Wakati huo huo mwanzo wa maisha mengine umewadia. Hii ni nukta muhimu kuwa hakuna kurejea tena katika mfumo huu ambao tayari umekwisha vurugwa na kuharibiwa kabisa. Hii ni sauti inayotambulisha kwamba maisha ya duniani hapa yamekoma kwa viumbe vyote na kwamba maisha halisi yameanza. Hii ni sauti ya mwanzo inayoamsha woga usio na mazongezonge, kitisho na kuchanganyikiwa katika nyoyo za makafiri. Sauti hii inaashiria mwanzo wa masiku magumu ambayo yataendelea hivyo bila ukomo. Katika Surat Maddaththir, siku hii imerejewa kama ifuatavyo:-

'Hapo tarumbeta litakapopulizwa, siku hiyo itakuwa ngumu, hakuna nafuu kwa makafiri. (Maddaththir: 8 - 10).

Sauti ya tarumbeta kwa hakika itasababisha mtetemeko mkubwa na kukosekana utulivu miongoni mwa makafiri. Hali ya milio isiyoelezeka na kufikirika bila ya chanzo kilicho wazi itakapopenya ulimwengu wote bila kusalia sehemu. Hivyo kila mtu atajua kuwa Mwanzo wa 'Kitu fulani umewadia'. Kukosekana kwa utulivu huo kutasababisha kafiri aanze kuchanganyikiwa na kuhamaki. Mfuatano wa matukio baada ya kupulizwa kwa parapanda kutaikuza hofu kwa kiwango kikubwa kisichomithilika.

KUHARIBIWA KWA ULIMWENGU

Kufuatia sauti ya parapanda na khofu kubwa iliyotawala, matokeo mazito yatatokea. Kwa wakati huu, itawathubutikia watu kwamba, wanakabiliana na janga kubwa. Ni dhahiri kuwa ulimwengu na maisha haya vinakaribia kwisha kabisa. Ndio sababu kila kitu kilicho juu ya ardhi wakati huo kitapoteza thamani kwa muda mfupi tu. Hata sauti ya siku ya kufufuliwa yenyewe inatosha kuvunja uhusiano wa kidunia miongoni mwa watu. Hakuna fikra inayoweza kumzonga mtu katika ubongo wake kwa muda huo zaidi ya kujiepusha na kujiokoa yeye mwenyewe. Woga utakuwa umepanda mno na katika siku hiyo kila mtu atakuwa ni mwenye kufikiria mambo yake tu.

"Basi itakapokuja sauti kali iumizayo masikio, siku ambayo mtu atamkimbia nduguye, Na mamaye na babaye, Na mkewe na wanawae, Kila mtu miongoni mwao siku hiyo atakuwa na hali itakayomtosha mwenyewe. (Abasa: 33-37).

Baada ya mtikisiko mkubwa, ardhi itatoa mizigo yake na itadhihirisha siri zake, hakuna kitakachokuwa na thamani siku hiyo na siku zinazofuatia.

"Wakati ardhi itakapotikiswa mtikisiko wake. Na ardhi ikatoa mizigo yake. Na akauliza Mwanadamu. 'Hii ina maana gani? Siku hiyo ardhi itaeleza habari zake kwa sababu Mola wako ameipa Wahy. (Az-zilzalah: 1 - 5).

Sauti ya kutisha itakayofuatiwa na majuto mazito, pia kutakuwa na mlipuko wa ndani kwa ndani ambao utaharibu kila ambacho Mwanadamu alikuwa akikiona ni chenye thamani kubwa. Kwa mfano, watu huthamini nyumba zao, ofisi zao, magari yao, na maeneo yao ya mashamba na mabustani. Baadhi ya watu huchukulia kuwa nyumba ndio lengo lao kuu la maisha. Hata hivyo, thamani ya nyumba yake huyeyuka mara moja katika siku ya kufufuliwa. Utajiri wa vitu, ambao watu huashiria ndio malengo yao ya maisha, utatoweka ndani ya sekunde chache. Malengo ya yule aliyefanya juhudi ili apandishwe cheo katika kampuni kama hitajio lake kuu la maisha itakuwa wakati huo imekosa thamani. Ama mwingine aliyetumia muda wote katika maisha akipigania madaraka katika nchi yake atakakumbana na hali hiyo hiyo ya kushitua. Kwa uchungu atashuhudia nchi yake ikipotea...

Kila kitu kitapoteza thamani yake ... isipokuwa yale yaliyofanywa ili kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu. Haya yamebainishwa katika Qur'an,

'Basi itakapofika hiyo balaa kubwa (ya kiama), Siku ambayo mtu atakumbuka kila alilolifanya. Na moto mkali utaoneshwa kwa kila aonaye. (An-Naziat: 34 - 36).

KUSAGIKA SAGIKA KWA MILIMA

Maangamizi yatakayotokea siku ya kufufuliwa yamepituka katika fikra za yoyote. Milima, inayoaminika kuwa madhubuti na isiyoyumba katika ardhi, itaendeshwa. Itanyanyuliwa kutoka kwenye mizizi yao na kisha kusaga sagwa. Hata mtetemesho kidogo wa ardhi hueneza hofu katika nyoyo za watu na kuathiri nyoyo zao kuona kuwa hakuna usalama. Huwafanya wayaache majumba yao na kutumia usiku wote katika mitaa wakiwa wanaranda randa kwa khofu. Kwa hivyo ndivyo, aina ya maangamizi yatakayopelekea milima kupeperushwa inathibitisha kuwa tukio hili si la kuvumilika hata kidogo. Ndani ya Qur'an, milima siku hiyo imeelezwa hali yake kama ifuatayo:-

'Na litakapopulizwa baragumu pulizo mmoja tu. Na ardhi na milima ikaondolewa na ikavunjwa mvunjo mmoja. Siku hiyo hilo tukio litakuwa limekwisha tokea. (Al-Haqqah: 13 - 15).

Kwa hakika siku ya hukumu imewekewa wakati maalum. Siku itakapopigwa parapanda nanyi mtafika makundi makundi. Na mbingu zitafunguliwa ziwe milango milango. Na milima itaondolewa itakuwa kama mangati (mlenga) kama maji akiona kwa mbali. (Nabai: 17 - 20).

'Na milima itakapoendeshwa (angani kama vumbi). Na ngamia wenye mimba pevu watakapoachwa, Na wanyama mwitu watakapokusanywa. (At-kakwyr: 3 - 5).

'Siku ambayo watu watakuwa kama madumadu (watoto wa nzige) waliotawanywa. Na milima itakuwa kama sufi zilizochambuliwa (ziikawa zinapeperuka). (Al-Qaariah: 4 - 5).

Siku hiyo kutakuwa na matukio ambayo nguvu kuu isiyozuilika, kubwa kiasi cha kufanya milima, majabali, ardhi vipeperushwe kama sufi. Watu watajua hakika kuwa tukio hili ni la kipekee lisilo na mfano. Watashuhudia kuwa asili kuu ambayo hapo zamani walikuwa wakiiabudu kama masanamu na vile ambayo walidhania kuwa vinao uwezo, kuua siku hiyo haviwezi kujikinga visiwe ni vyenye kukaribiwa kabisa. Wakati huo ni wakati ambao hisia za kujazwa na uhalisia wa yule mmiliki wa ulimwengu utakuwa umewadia. Pamoja na uthibitisho huo, hakuna lolote litakalowafanya makafiri waone kuwa ni lenye kuwanufaisha. Na ukweli ni kuwa kujua kwao siku hiyo hakutawasaidia chochote. Wakati huo watakuwa wamezingirwa na nguvu hii kubwa ambayo awali walipokuwa katika maisha ya dunia walikuwa wakiikwepa kuifikiria. Watajua hakika ya mambo ambayo walishindwa katika uhai wao wote kuipokea kama njia ya busara na hekima. Tishio lililoumbwa na Nguvu isiyo na mipaka kamwe haliwezi kuelezeka ila kwa yule atakayelishuhudia mwenyewe. Hali hiyo inaenea kila kiumbe, chenye uhai na kisicho na uhai. Hufanya basi kila kitu kuwa katika mwelekeo wa kudhibitiwa. Wanadamu, wanyama na maumbile asili vyote vitasagwasagwa katika huo mtetemesho. Milima haitakuwa tena vigingi, bahari haiwi tena isiyo na mipaka na mbingu haziwi tena mbali kama ilivyokuwa awali. Jua, nyota na ulimwengu wote vimezunguukwa na khofu ya siku ya kufufuliwa vyote vinarejea kwa Muumba wao. Kama ilivyo kwa milima kuwa itakunjwakunjwa kama changarawe jangwani, mwanadamu naye bila kujitambua atakunjwa kufuatia milima, nyota na bahati vyote vikipitia hatua ya kuharibiwa kabisa kabisa.

KULIPULIWA KWA BAHARI

Kwa vipawa alivyonayo Mwanadamu leo hii, ni vigumu kwa fikra zake kuweza kupokea na kuelewa vitisho vya siku hiyo ya kufufuliwa.

'Na bahari zitakapowashwa moto. Na roho zitakapounganishwa (na viwiliwili vyake). (Tawyr: 6 - 7).

(Na bahari zitakapopasuliwa. (Inftar: 3). Kuharibiwa huko kutakuwa katika Qadar ya Mwenyezi Mungu na Uwezo wake. Hali hii hutoa picha ya ukubwa wa jambo lenyewe.


    
5 / total 8
You can read Harun Yahya's book Kufa Ufufuko Jahannam online, share it on social networks such as Facebook and Twitter, download it to your computer, use it in your homework and theses, and publish, copy or reproduce it on your own web sites or blogs without paying any copyright fee, so long as you acknowledge this site as the reference.
About this site | Tengeneza kurasa yako ya nyumbani | Add to favorites | RSS Feed
Mambo yote yanaweza kuynakiliwa, kuchapwa na kusambazwa kwa kurejea katika kurasa hii
(c) All publication rights of the personal photos of Mr. Adnan Oktar that are present in our website and in all other Harun Yahya works belong to Global Publication Ltd. Co. They cannot be used or published without prior consent even if used partially.
© 1994 Harun Yahya.www.harunyahya.com
page_top