Kufa Ufufuko Jahannam

SHUSHA KITABU

Download (DOC)
Maoni

SURA ZA KITABU

< <
7 / total: 8
KUFA UFUFUKO JAHANNAM - Harun Yahya
KUFA UFUFUKO JAHANNAM
   JAHANNAM

Hakika yeye alifikiri na akapima (la kusema kuitukana Qur'an. Basi ameangamia. Namna gani alivyo diriki (katika kuitukana kwake) Tena ameangamia. Namna gani alivyodiriki (katika kuitukana kwake). Kisha akatazama. Kisha akakunja kipaji (chake) na akafinya uso. Kisha akaipa mgongo (haki) na akatakabari (akajivuna). Na akasema: "Hayakuwa haya (aliyokuja nayo Muhammad) ila ni uchawi ulionukuliwa (kwa wachawi wakubwa kabisa wa zamani). Hayakuwa haya (anayosema) ila ni kauli ya binadamu". Karibuni hivi nitamtia katika moto (unaowaka kweli kweli). Na nini kitakachokujulisha moto huo? Haubakishi wala hausazi. Unababua ngozi mara moja. Na juu yake wako (walinzi) kumi na tisa. (Al-Muddathir: 18 - 30).

UDANGANYIFU NA UHAKIKA

Mahali ambapo makafiri watabakia milele, pameumbwa maalum ili kuwapa machungu katika miili yao na katika nafsi zao. Hiyo ni kwa sababu makafiri watajutia kwa makosa yao makubwa na wakati huo huo uadilifu wa Mwenyezi Mungu hupelekea kundi hili liadhibiwe vikali. Kwa kukosa kwao shukurani na kumuasi kwao Muumba wao, ambaye amempa mwanadamu nafsi, hilo ni kosa kubwa kuliko jingine lolote linaloweza kufanya hapa ulimwenguni. Hivyo basi, Akhera kutakuwa na adhabu iumizayo kwa kosa kubwa la aina hii. Hilo ndilo lengo la kuumbwa kwa Moto. Mwanadamu ameumbwa ili amtumikie Mwenyezi Mungu. Kama atakanusha lengo kuu la kuumbwa kwake, kwa hakika atakachopata ndio stahiki yake. Mwenyezi Mungu amebainisha katika moja ya aya za Qur'an:

'Na Mola wenu anasema: Niombeni nitakujibuni. Kwa hakika wale wajivunao kufanya ibada yangu, bila shaka wataingia Jahannam, wadhalilike. (Al-Muumin: 60).

Kwa kuwa watu wengi wataingia motoni mwishoni, na adhabu humo ni ya kudumu, lengo kuu, na haja ya msingi kwa mwanadamu, iwe ni kuepuka moto. Jambo linalomtisha mno Mwanadamu ni Moto. Na hakuna jambo kubwa zaidi kwa mtu kama kuikinga nafsi yake na huo moto. Pamoja na hili, takriban watu wengi katika ardhi wanaishi katika hali ya kutokuwa na habari na huo moto. Wanajishughulisha na matatizo mengine katika maisha yao ya kila siku. Kwa miezi, miaka, dahari wanashughulika na mambo ambayo ni madogo madogo, huku wakiacha kufikiri juu ya jambo kubwa linalotisha, hatari iliyokuu kwa maisha ya milele. Jahannam iko pambizoni mwao, lakini ni vipofu hawaoni.

'Imekaribia watu hisabu yao, nao wamo katika mghafala; wanakengeuka tu. Hayawajii mawaidha mapya kutoka kwa Mola wao ila huyasikia, na hali wanafanya mchezo. Zimeghafilika nyoyo zao. Na wanasemezana kwa siri wale waliodhulumu (nafsi zao). 'Ni nani huyu (Muhammad) isipokuwa ni binadamu tu kama ninyi? Je, mnafika katika uchawi (mnakiendea kiini macho) na hali ninyi mnaona?" (Al-Anbiyaa: 1- 3).

Watu wa aina hiyo wamejitumbukiza katika mambo ya upuuzi. Wanatumia muda wao wote katika malengo yasiyo na uzio. Muda mwingi malengo yao yamepandishwa chati katika kampuni, ndoa, kufurahia maisha ya familia, kuchuma mabilioni ya fedha au kuwa wahubiri au waenezaji wa itikadi zisizo na maana. Wakati haya yanafanyika, watu hawa hawana habari juu ya majuto yalio mbele yao.

Jamii isiyo na Elimu juu ya Muumba wao ambayo ina watu wa aina hiyo hutamka neno 'Moto' bila ya kuwa na ufahamu kamili juu ya maana yake. Hapa na pale, somo hili huwa sehemu ya mzaha. Hata hivyo, hakuna hata mtu mmoja aliyelipa fikra za kutosha kama inavyostahiki. Kwa watu hawa, Moto ni kitu kilichozushwa na ni cha kufikirika tu. Kwa hakika, Moto ni kitu halisi zaidi kuliko dunia hii. Ulimwengu utakoma kuwepo baada ya muda fulani, lakini moto utabakia milele. Mwenyezi Mungu, Muumba wa ulimwengu na dunia, na vyote vilivyomo ndani yake, vivyo hivyo ameumba akhera, pepo na moto. Adhabu kali iumizayo imeahidiwa kwa wote Makafiri na wanafiki.

Motoni, mahali pabaya pa kufikia ambapo huwezi kufikiria, ni chanzo cha mateso makubwa kabisa. Mateso haya na maumivu hayafanani na aina yoyote ya mateso katika dunia hii. Ni mahali zaidi kuliko maumivu ya aina yoyote au mateso ambayo yeyote amewahi kuyakabili hapa duniani. Kwa hakika hiyo ni kazi ya Mwenyezi Mungu, aliyetukuka katika busara.

Uhakika wa pili kuhusu Jahannam ni kwamba, kwa kila mmoja, mateso haya ni ya kudumu na hayana kupumzika. Wengi katika watu wa jamii hii ya kijahili wana aina moja ya kutokuelewa vizuri nadharia ya Jahannam. Wanadhani wanaweza ' kutumikia hukumu yao huko motoni kwa muda na kisha baada ya hapo wakasamehewa. Hii ni kujipa matumaini tu. Imani hii imesambaa hata miongoni mwa ambao hujiita waumini huku wakipuuza kuekeleza majukumu yao kwa Mwenyezi Mungu. Wanadhani hakuna mipaka kiasi kwamba wanajiingiza katika mambo ya kidunia kuwastarehesha. Kutokana na imani hiyo hiyo, wataingia peponi baada ya kupata adhabu ya muda mfupi huko motoni.Hata hivyo, mwisho unaowasubiri ni wenye kuumiza zaidi kuliko wanavyotarajia. Jahannam ni mahali pa adhabu pasipo na ukomo. Hapafai hata kwa kukaa sekunde moja tu. Katika Qur'an imekuwa ikisisitizwa kwamba adhabu kwa makafiri haipungui wala kuongezwa na ni ya milele. Aya ifuatayo inatilia mkazo ukweli huu kwa uwazi kabisa:

"Na wataishi humo milele" (An-Nabaa:23).

Matamshi yao kwamba,'Nitatumikia adhabu yangu kwa muda na kisha nitasamehewa' ni fikra zilizozalishwa na baadhi ya watu ili kujifurahisha. Kwahakika Mwenyezi Mungu ametutahadharisha na fikra za namna hii kwenye Qur'an kwa kutuonesha kuwa ni fikra ambazo hata Mayahudi walikuwanazo:

Na walisema hautatugusa moto (wa Jahannam) isipokuwa kwa siku chache tu.

Sema: "Je mmeapa ahadi ya Mwenyezi Mungu? Kwa hiyo hata khalifu

Ahadi yake, au mwamsingizia Mwenyei Mungu mambo msiyoyajua"

Naama, wanaochuma ubaya - na makosa yao yatawazunguuka -

Hao ndio watu wa motoni; watakaa humo milele. (Al-Baqarah: 80 - 81).

Kitendo cha mwanadamu cha kuacha kumshukuru Mola wake na badala yake akadumu katika kumuasi Muumba ambaye 'amempa (mwanadamu) kusikia, kuona, akili na huba (Rejea an-Nah: 1:78).

Kunastahiki mwanadamu huyo aadhibiwe, adhabu isiyo na mpaka. Dharura zitokewazo na mmoja wa wanadamu haziwezi kumuepusha na moto. Hakuna nafuu kwa waliokadhibisha dini ya Mwenyezi Mugu na kuendeleza unyama zaidi kwa wanadamu wenzao.

'Na wanaposomewa aya zetu zilizo wazi, utaona chuki juu ya nyuso za wale waliokufuru. Hukaribia kuwashambulia wale wanaowasomea hizo aya zetu. Sema: 'Je! Nikuambieni yaliyo mabaya zaidi kuliko haya? Ni moto wa Mwenyezi Mungu aliowaahidia wale waliokufuru, na ni marejeo mabaya hayo". (Al-Hajj: 72).

Wale waliodumu katika ujeuri dhidi ya Mwenyezi Mungu na wakazidisha uadui dhidi ya waumini, wataishia maneno yafuatayo katika Siku ya hukumu:-

Kwa hivyo ingieni milango ya Jahannam kwa kukaa humo milele. Basi ni mabaya kabisa makazi ya wafanyao kiburi'. (An-Nahl: 29).

Katika moja ya mambo yanayoogopesha zaidi kuhusu moto ni ile tabia yake ya umilele. Mara utakapoingizwa motoni hakuna kurejeshwa tena. Jambo lisilo na shaka kuhusu moto na adhabu nyingine ni ile hali ya mja kubakia katika majuto milele. Mwanadamu hana matarajio mengine. Kila uchao ni adhabu juu ya adhabu kwa kiwango cha makosa yake: Qur'an inaifafanua hali hii katika aya ifuatayo:-

'Na wale waliofanya uovu, makazi yao ni motoni, watakapotaka kutoka humo watarudishwa mumo humo na wataambiwa: Onjeni adhabu ya moto ambayo mlikuwa mkiikadhibisha - (As - Sajidah: 20).

' Watataka (kila namna) watoke katika moto, lakini hawatotoka humo, na watakuwa na adhabu inayodumu (kwao). (Al-Maidah: 37).

ADHABU ZA KUSWAGWA KUELEKEA MOTONI

Jahannam (Motoni)... Hii ni sehemu ambayo sifa za Mwenyezi Mungu, al-Jabbar (MtenzaNguvu), Ali-Qahhar (Mwenye Kushinda), al-Muntaqim (Mwenye kuliizakisasi), zitadhihiri kwa muda wote milele lengo likiwa kukithirisha maumivu kwa mwanadamu. Katika Qur'an Jahannam imetajwa kama vile ni kiumbe hai. Kiumbe hiki kina chuki na kutaka kulipa kisasi kwa makafiri.

Juu ya kiu ya Jahannam iliyonayo dhidi ya makafiri haiwezi kutoshelezwa hata kidogo. Kuwachukia kwake makafiri, Jahannam inaonekana kama iliyopandwa na uwendawazimu. Wakati itakapokutana na makafiri ghadhabu zake zitaongezeka. Kuumbwa kwa moto, ni kutimiza lengo moja tu, kuchochea adhabu isiyovumilika. Kwa hakika itatekeleza majukumu yake ya adhabu isiyovumilika kwa kutoa maumivu makali mno kama itakayokadiriwa na Muumba wake.

Baada ya hukumu ya makafiri kumalizika mbele ya Mwenyezi Mungu, makafiri watachukuwa vitabu vyao kutoka upande wa kushoto. Huu ndio muda watakaoongozwa kuelekea motoni milele. Kwa makafiri, hakuna fursa ya kukwepa. Kutakuwa na mabilioni ya watu, bado kundi hili halitatoa fursa kwa makafiri kutoroka au kupuuzwa asishughulikiwe. Hakuna awezaye kujificha katika kundi hili. Wale watakaopelekwa Motoni watakuwa na shahidi na mwingine atakayeichukuwa nafsi yake.

'Na itapulizwa parapanda (Baragumu); hiyo ndio siku ya makamio, (Siku ya kiama). Na itakuja kwa nafsi moja na mchungaji (wake) na shahidi (wake). (Aambiwe) 'Kwa hakika ulikuwa umo katika ghafla na jambo hili. Basi tumekuondolea (leo) pazia yako; kuona kwako leo kumekuwa kukali'. Na yule (Malaika) aliyekuwa pamoja naye (akiandika amali zake) atasema (kumuambia malaika wa adhabu) "Hayo ndiyo yaliyowekwa tayari kwangu (ya amali zake mbona hizi)." (Wakati huo kutasemwa)." Mtupeni katika Jahannam kila kafiri asi." "Akatazaye kheri, arukaye mipaka, aliyekuwa akijipa shaka (zisizokuwa na sababu). Aliyeweka Mungu mwingine pamoja na Mwenyezi mungu, basi mtupeni katika adhabu kali." (Qaf: 29 - 26).

Makafiri wataswagwa (kuendeshwa) kuelekea kwenye makazi haya ya kutisha. Katika maneno ya Qur'an, wataendeshwa kwa makundi.' Hata hivyo, njiani kuelekea Jahannam, woga utazidishwa katika nyoyo zao. Sauti ya kutisha na kali kutoka motoni itasikika toka mbali.

'Watakapotupwa humo watasikia rindimo (magurumo) lake, na hali ya kuwa inafoka. Unakaribia kupasuka kwa hasira (yake juu ya wabaya) walinzi wake watawauliza: 'Je! hakukufikieni muonyaji? (Al-Mulk: 7-8).

Kutokana na aya hizo, ni wazi kuwa wakati watakapokumbwa tena (yaani watakapofufuliwa), makafiri wote wataelewa kile kilichowaangamiza. Wakati peke yao; hakutawa na marafiki, ndugu, au wenye kuwaunga mkono watakaowasaidia Makafiri hawatakuwa na ujasiri wa kuwa jeuri na watatazama kwa macho ya huruma (yaliyoinamishwa). Moja ya aya imeelekezea tukio hili kwa maneno yafuatayo:

'Na atawaona wanapelekwa (kwenye moto), wamekuwa wanyonge kwa dhila; wanatazama (yanayopita) kwa mtazamo wa kificho. Na walioamini watasema: "Kwa hakika wapatao hasara ni wale waliohasirika nafsi zao na watu wao siku (ya leo hii) ya Kiama." Bila shaka madhalimu watakuwa katika adhabu inayoendelea : (Ash-shuura: 45).

KUINGIA MOTONI NA MILANGO YA MOTONI

Mwishowe makafiri watafika katika milango ya motoni. Qur'an inaelezea tikio hili kama ifuatavyo:-

'Na waliokufuru watapelekwa katika Jahannam makundi - makundi, mpaka watakapoifikia itafunguliwa milango yake, na walinzi wake wataambia, "Je hawakuwajieni mitume miongoni mwenu wakikusomeeni aya za Mola wenu na kukuonyeni juu ya makutano ya siku yenu hii?" Watasema: 'Kwa nini? (wametujia)! Lakini limethibiti neno la adhabu juu ya wale walio kanusha (Neno ndio sisi)." Itasema: 'Ingieni milango ya Jahannam mkakae humo". Basi ni ubaya ulioje wa makazi ya wanaotakabari." (Az-Zumar: 71 - 72).

Kwa kila kundi mlango maalum wa motoni umeumbwa kwa ajili yao. Kutegemea ni kiasi gani walimuasi Mola wao, watu watatengwa kwa madaraja. Makafiri watawekwa kila mmoja na sehemu yake kutegemea madhambi waliyoyafanya. Imeelezwa katika Qur'an:

'(Atasema (Mwenyezi Mungu siku ya Kiama awaambie): 'Ingieni motoni pamoja na uma zilizopita kabla yenu; za majini na watu." Kila utakapoingia Umma utawalaani wenzao. Mpaka watakapokusanyika wote humo, wa nyuma wao (wale waliofuata) watasema kwa ajili ya wa kwanza wao (waliowafuata hata wakapotea) 'Mola wetu! Hawa ndio waliotupoteza basi wape adhabu ya moto maradufu (yaani zaidi kuliko sisi).

Atasema: "Itakuwa kwenu ninyi nyote (adhabu) mara dufu, lakini ninyi hamjui tu (bado). (Al-Aaraf: 38).

Aya nyingine zinaeleza kwa undani kuhusu moto. Kwa mfano aya ifuatayo zinasema:

Na bila shaka Jahannam ndipo mahali pao walipoahidiwa wote. Ina milango saba, na kwa kila mlango uko sehemu yao iliyogawanywa (ya kuwa hii ya mlango wa fulani na hii ya mlango wafulani). (Al-Hijr: 43 - 44).

Ambao wamewekewa adhabu iumizayo zaidi ni Wanafiq. Hawa ni watu ambao hutenda kama vile ni Waumini, hapo hawana hata chembe ya imani katika nyoyo zao: 'Bila shaka wanafiki watakuwa katika tabaka ya chini kabisa katika moto. Hutamkuta kwa ajili yao msaidizi (yoyote). (Annisai: 145)

Moto wa Jahannam ni wa kuogopwa, njaa ya makafiri kamwe haitaweza kuondoka (kushiba). Pamoja na kuingizwa watu wengi mno humo, bado inauliza kama kuna nyongeza:

'Siku tutakayoimbia Jahannam: 'Je! Umejaa?" Nayo itasema: 'Je kuna zaidi? (Zaidi na ije tu!)" (Qaf: 30).

Mara unapompokea unamhifadhi humo milele. Mwenyezi Mungu anaifafanua Jahannam katika Qur'an kama ifuatavyo:

'Karibuni hivi tutamtia katika moto (unaowaka kweli kweli). Na nini kitakachokujulisha moto huo? Haubakishi wala hausazi. Unababua Ngozi mara moja. (Muddaththir: 26 - 29).

'Na Jahannam itadhihirishwa kwa wapotevu. Na wataambiwa: 'Wako wapi mliokuwamkiwaabudu (Badala ya Mwenyezi Mugu). Je wanaweza kukusaidieni au kujisaidia wenyewe (Nafsi zao)? Basi watatupwa humo wao na maasi (wengine) Na majeshi ya ibilisi yote (Ash-Shu'ara: 91 - 95)

MAISHA YA KUDUMU NYUMA YA MILANGO ILIYOFUNGWA

Mara baada ya makafiri kuwasili Jahannam, milango itafungwa nyuma yao. Hapa, wataona sehemu inayotisha kupita kiasi. Watagundua mara moja kwamba wamefikishwa motoni, mahali ambapo watabakia humo milele. Kufungwa kwa milango kunaashiria kwamba hakuna ukombozi humo. Mwenyezi Mungu anaelezea hali ya makafiri kama ifuatavyo:- (Al-Balad: 19-20).

Adhabu ya motoni imeelezwa katika Qur'an kwa majina kadhaa:-

'Adhabu kali' (Imran: 176); 'Adhabu Ngumu' (Imran: 4), 'Adhabu iumizayo'(Imran: 21). Ufahamisho uliotolewa hautoshi kutoa picha halisi na pia hautoshi kutoa ufahamu kamili juu ya adhabu ya Jahannam. Kushindwa kuvumilia japo katika adhabu ndogo ya kuchomwa hapa duniani, mtu hawezi kuelewa hasa hali ya kuwekwa katika adhabu ya motoni milele. Zaidi ya hayo, Maumivu yapatikanayo kwa moto hapa duniani kamwe hayawezi kulinganishwa walau chembe na adhabu isiyokifani ya Jahannam. Hakuna mfano wa maumivu wa yale ya Jahannam. (Fajr: 25 - 26).

Kuna maisha ndani ya Jahannam. Lakini ni maisha ambayo kila muda unavyopita ndivyo adhabu inavyozidi kupamba moto. Katika maisha haya kila aina ya adhabu ya kimwili, kiakili na kisaikolojia, pamoja na aina mbalimbali za maumivu na kukoseshwa kuangaliwa kwa rehema yote yatakuwa yakijiri. Haiwezekani kulinganisha na matatizo ya aina yoyote hapa duniani. Watu huko motoni watakuwa wanapata maumivu kwa kupitia njia zote tano za milango ya fahamu. Macho yao yataona picha za kutisha mno na za kuchukiza; Masikio yao watasikia sauti zenye kukera, zikinguruma na vilio, pua zao zitahisi harufu ya kuchukiza na mbaya mno; ndimi zao zitaonja maonjo yasiyo vumilika. Wataihisi Jahannam katika kila chembe hai iliyo mwilini mwao. Hii ni hali anayochochea maumivu makali na kumfanya mtu aonekane kama mwendawazimu kiasi ambacho hali hiyo haiwezi kufikirika katika ardhi hii. Ngozi zao, viungo vyao vya ndani na mwili wao mzima utakuwa unapata machungu. Watu wa motoni watakuwa wanastahamili mno maumivu na hawatakufa. Hivyo, kamwe hawawezi kujiokoa kutokana na adhabu. Ngozi zao zitarudishwa upya kila zitakapounguzwa; adhabu hiyo hiyo ikiendelea milele; ukali wa adhabu kamwe hautapungua. Mwenyezi Mungu anasema ndani ya Qur'an: (At-Tur: 16).

Hakuna kupata maumivu ya kutisha huko motoni zaidi ya yale ya kimwili na kiakili. Watu wa motoni watazidi kujuta, wakiangalia kukata tamaa, wakiwa hawana matumaini na wakiendelea hivyo zama na zama wakijuta. Kila upande, kila mahali katika Jahannam pametengenezwa, ili kutoa machungu ya kiakili. Machungu haya ni ya milele. Kama itakoma baada ya miaka milioni au bilioni kadha, hata kipindi kirefu kama hicho kitatoa hisia za matumaini na kuwa ndio hoja kubwa yenye nguvu ya matumaini na furaha, bado, hali ya adhabu ya milele itachochea aina ya kukosa matumaini ambayo haiwezekani kulinganishwa na aina yoyote ya hisia katika dunia hii. Kutokana na Qur'an Jahannam ni mahali ambapo maumivu yasiyo na kifani huonekana. Ni nyembamba, yenye kelele, yenye moshi na ngurumo, ichocheayo hisia na kukosa usalama katika moyo wa mwanadamu. Ni mahali palipo na tabia ya kuwa na harufu ichukizayo, moto uunguzao ndani ya moyo, chakula na kinywaji kibaya, nguo za moto na kinywaji kichungu. Hizi ndizo tabia za msingi za Jahannam. Hata hivyo, kuna maisha yanayoendelea katika mazingira haya ya kutisha. Watu wa motoni wana hisia kali. Wanasikia, wanazungumza na kuhoji, na wanajaribu kutoroka kutoka katika maumivu. Wanaungana katika moto, wanapatwa na kiu na kuwa na njaa, na kuhisi majuto. Kilicho muhimu zaidi, wanataka machungu yaondolewe yasiwepo tena wapate nafuu. Watu wa motoni wataishi maisha ya milele katika daraja la chini zaidi kuliko wanyama katika mazingira haya machafu na ya kuchukiza. Kilicho mbele yao chenye kuyapamba mazingira ni matunda makali ladha yake, yenye miiba na miti ya Zaqqum. Vinywaji vyao kwa upande mwingine ni damu na usaha. Wakati huohuo, moto umewazunguka katika kila upande.

Huku wakibadilishwa ngozi, nyama ikiunguzwa na damu ikitiririka mwili wote, watakuwa wamefungwa minyororo na kuchapwa. Mikono ikiwa imefungwa katika shingo zao, watatumbukizwa katikati ya Jahannam. Malaika wa adhabu kwa wakati huo wakiwaweka wale wakosaji katika vitanda vy moto, na mashuka yao yakiwa ni moto. Makafiri kila wakati watatamani waokolewe kutoka katika hali hiyo. Na badala yake, wanazidi kupata adhabu iumizayo na maangamizi. Wataachwa peke yao. Hali hii yote itakuwa kweli. Ni hakika. Ni hakika zaidi kuliko maisha yetu haya.

Na katika watu wapo wanao muabudu Mwenyezi Mungu kwa ukingoni. Ikimfikia kheri hutulia kwayo, na ukimfikia msukosuko hugeuza uso wake. Amekhasiri dunia na Akhera; hiyo ndiyo khasara iliyo wazi. (Al-Hajj: 11)

Hayo ni kwa sababu walisema: Hautatugusa Moto isipo kuwa kwa siku chache tu. Na yakawadanganya katika dini yao yale ambayo wenyewe waliyo kuwa wakiyazua. (Imran: 24)

Wale wanaofanya kutengeneza pesa, vyeo, utukufu na mambo mengine ya kidunia kama ndio malengo makuu ya maisha na hapohapo wakadharau/wakapuuza mambo mazuri ya Mwenyezi Mungu; wale wanaobadili maamrisho ya Mwenyezi Mungu kutokana na kupenda kwao na kutemani kwao, wale wanaotafsiri Qur'an kwa matakwa yao, wale waliopotea njia kutoka katika njia iliyonyooka - Kwa muhtasari:- Makafiri wote na wanafiqi wote wataingia motoni, isipokuwa wale ambao Mwenyezi Mungu amewarehemu na amewasamehe. Hili ndilo hitimisho la Mwenyezi Mungu katika maneno yake.

Na kwa hakika itakuwa hivyo.(As-Sajida: 13)

Watu hawa tayari wamekadiriwa kuwa ni wa motoni:- (As-A'raf: 179)

ADHABU YA MOTO

Katika maisha ya Jahannam, kubwa kabisa na la msingi kabisa katika adhabu hapana shaka ni kuchomwa moto. Kinyume na aina nyingine za adhabu moto, ni aina ya kipekee ya Jahannam, kwani haisazi chochote katika mwili wa Mwanadamu.

Ni adhabu ipenyayo mwili wa mwanadamu hadi kwenye kiini. Watu wa Jahannam watatupwa katika huo moto uwakao kwelikweli.' (Al-Ma'arij: 15)

Unachoma katika 'Moto Ufokao' ambao ni 'Moto Ubabuao'(Al-layl: 14)

Pia angalia aya za Qur'an, katika Al-Qariah: 8 - 11)

Kutokana na aya hizo; Mwanadamu anaelewa kwamba moto uwakao kweli kweli ni katika Jahannam yote. Katika ufupi huu, hakuna eneo ambalo linaweza kuhifadhika na moto. Moto ukifika kila pembe ya Jahannam. Wakati adhabu za aina mbali mbali za kimwili na kiakili zikiendelea, bado mwanadamu atakuwa hana uwezo wa kukwepa moto. Utakuwa unamuunguza mfululizo. Jahannam Moto wake ni mkubwamno. Katika Qur'an inaelezewa miale ya moto kuwa ni sawa na miale mikubwa sawa na kundi la nzige na kundi la ngamia wa manjano kuonesha ukubwa na uzito wa moto. (Al-Mursalat: 28 - 33)

Wasioamini (Makafiri na Washirikina) watatumia nguvu zao zote kujiepusha na miale (ya moto), lakini haitaruhusiwa. Ni moto ambao:-

'Ambao unawaita wote wanaogeuza migongo yao na wanaokimbia' - (Al-Maarij: 17).

Aya nyingine inafahamisha hatima ya wanaokanusha kwamba (As-Sajida: 20)

Makelele na mitetemo ya wale walioingizwa motoni, itasikika kila upande. Hata hii mitetemo na makelele yenye kuogofya ni miongoni mwa vyanzo vya adhabu kwa makafiri.

Kutakuwa na vilio kwa ajili yao - (An-Nbiyaa: 100).

Ama kwa wale waliokadhibisha, watakuwa motoni, ambamo watatetemeshwa na kufungwa. (Hud:106).

Jahannam ina maumivu yasiyovumilika. Wanadamu hawawezi kustahili maumivu kama ya moto wa ujiti wa kibiriti. Hiyo kwa haya ni zaidi. Hata hivyo maumivu yoyote tunayohisi katika dunia hii ni kidogo mno ukilinganisha na yale yatokanayo na moto wa Jahannam. Hakuna anayebakishwa katika moto wa duniani kwa muda mrefu. Ama atakufa baada ya Sekunde 5 hadi 10 au asikie maumivu kwa kipindi kifupi tu. Hata hivyo moto wa Jahannam unatisha, unaleta maumivu endelevu. Watu wa motoni watakuwa kwenye moto na watabakia humo milele. Kujua kwao kwamba adhabu hii haina ukomo, huwafaya wale walioingizwa humo kuwa katika kipindi cha majonzi na kukosa matumaini. Huhisi kukata tamaa na hivyo kuwa katika hali ya kuhisi maangamizi ya milele.

Kuunguzwa uso ni moja ya mambo ambayo hayafakiriwi na yeyote. Hii ni kwa sababu uso au wajihi ni kiungo muhimu ambacho Mwanadamu anajivunia. Unampa mwanadamu kutambulika na ndio unaoonesha waziwazi kile tunachoiita 'Mimi'. Mara nyingi, umbile la kuwa unachukiza au unapendeza huhusishwa zaidi na uso. Kwa kuona picha ya mtu aliyeungua vibaya usoni mwake, huanza kunywea na hatimae mara moja hurejea kwa Mola wake ili alindwe/akingwe dhidi ya majanga kama haya. Hakuna hata mmoja anayetamani apigwe na dhoruba kama hiyo. Hata hivyo makafiri wameghafilika juu ya jambo moja; wanaelekea kwenye hatima inayofanana hivyo; na kwa hakika mwisho huo ni mbaya zaidi. Maumivu yatokanayo na moto wa Jahannam hupenya na kuenea mwili nzima wa mwanadamu. Hata hivyo pindi uso utakapoona moto, yatakuwa ni maumivu yasiyoweza kuvumilika. Macho, masikio, pua, ulimi na ngozi, kwa muhtasari kila kiungo cha fahamu kimo katika sehemu hii ya mwili. Jambo lolote baya katika uso, hata liwe dogo kiasi gani, hutoa hisia kali kwa mwanadamu. Hata hivyo kwa Jahannam, uso ndio utakaogeuzwa geuzwa. Kwa namna hiyo, sehemu muhimu mno ya mwili wa mwanadamu itakuwa imedhurika vibaya sana. Adhabu hii imetajwa katika aya kadhaa, Miongoni mwa hizo i:-

'Siku nyuso zao zitakapogeuzwa geuzwa katika moto, watasema, 'Majuto yetu, kama tungemtii Mola wetu na tukamtii Mtume' (Al-Ahzab: 66).

Nguo zao za lami na nyuso zao zilifunikwa na moto (Ibrahim: 50).

Moto utaunguza nyuso zao, na humo watakuwa ni wenye kutisha, midomo yao ikiondolewa kutoka mahali pake. (Al-Muumin: 104). Ikimaanisha kuwa meno yao yatakuwa nje, baada ya midomo yao kuondolewa.

KUNI ZA JAHANNAM NA MAJI YENYE KUCHEMKA

Katika Qur'an, maelezo kuhusu njia ambayo makafiri watachomwa katika moto ni kuwa; kwanza, makafiri wenyewe watakuwa ndizo kuni za huo moto. Kuchomwa kwao hakufanani na kuchomwa kwa kitu kingine katika moto. Makafiri watakuwa ndio mafuta ya moto.

'Lakini wale wanaokufuru, hawatakuwa chochote ila mafuta (kuni) za moto wa Jahannam.' (Al-Jinn: 15).

Kuni zinazowasha moto huungua kwa muda mrefu zaidi kuliko kitu kingine chochote na kwa mwako mzito zaidi. Vivyo hivyo makafiri watakuwa kuni za moto huu ambao awali waliukanusha. Uhakika huu unabainishwa wazi katika aya zifuatazo:-

'Enyi Mliamini! Jiokoeni nafsi zenu na jamaa zen na moto ambao kuni zaken i watu na mawe... (Tahrim: 6).

'Wale waliokanusha Imani (Makafiri), mali zao na watoto wao hawawezi kuwasaidia chochote mbele ya Mwenyezi Mungu. Wao hawatakuwa kingine zaidi ya kuwa kuni za moto. (Al-Imran:10).

'Kwa hakika ninyi (makafiri), na vile mnavyoviabudu kinyume na Mwenyezi Mungu, mtakuwa kuni za Jahannam! Kwahakika humo mtaingizwa tu! (An-Biyaa: 98).

Pamoja na watu kutumika kama kuni, pia zipo kuni halisi katika kuchochea moto. Hivyo, hali hii nayo ni chanzo kingine cha adhabu. Makafiri ambao awali walikuwa karibu zaidi duniani, kwa mfano mke na mume, watachukuwa kuni kila mmoja kwa ajili ya moto wa mwenzake.

'Imeangamia mikono ya Abu Lahab na ameangamia. Hakikumsaidia chochote katika mali yake na kila alichokichuma. Hivi karibuni ataingizwa katika moto uwakao. Na mke wake (mchukuzi wa) kuni kwa kamba zilizosokotwa za majani ya mtende katika shingo yake.' (Lahab: 1- 5).

Huu ndio mwisho wa uhusiano wa aina zote katika dunia hii. Makafiri ambao walikuwa na tabia ya kusema wanapendana mno na huku wakimuasi Mola wao kwapamoja, watakuwa kuni za mmoja dhidi ya mwingine huko Jahannam. Mke kwa mume au mume kwa mke, ndugu wa karibu na marafiki wote na kati ya watakuwa maadui. Mahandaki hayatajua mipaka. Moto uliokokwa kwa kuni hai na zile zisizo hai, pia zitachemsha maji ambayo yatawaunguza makafiri. Ngozi; ambayo ni moja kati ya viungo vya thamani katika mwili wa mwanadamu iliyotanda juu ya mwili wote wa huyo mwanadamu na unene wake si zaidi ya milimita kidogo tu, huwa ni kiungo muhimu katika mawasiliano baina ya binadamu na dunia ya nje kwa hisia za kugusa. Pamoja na viungo vya sehemu za siri, viungo vingine vya mwili kama vile uso, mikono, vitanga vya mikono, miguu, viungo ambavyo kila mtu huvichukulia kwa uzito wa hali ya juu kabisa, vimefunikwa na ngozi. Pamoja na ukweli kuwa inachukuliwa kama kiungo mja anachojivunia, kutokana na unyeti wake, sasa ngozi itakuwa chanzo kikubwa cha maumivu. Ngozi itakuwa maalum kwa kubabuliwa na moto na maji yanayochemka. Huku moto ukiibabua ngozi, maji nayo hufanya kazi ya kuiivisha na kuinyumbua nyumbua. Maji hayo yachemkayo yatakwangua ngozi yote; ni vigumu kusalia sehemu yoyote ya ngozi ambayo haitaathirika. Awali, ngozi hii nyembamba itavimba na kisha itakuwa inaunguzwa na hivyo hutoa maumivu makali. Hakuna utanashati, utajiri wa mali, nguvu, ujasiri na kwa muhtasari, hakuna kikwazo kutokana na maumivu yaliyofanywa na maji yachemkayo kweli kweli. Kwa maneno ya Qur'an

'... Watakuwa na maji yachemkayo kweli kweli kwa ajili ya kunywa' (Al-An'am: 70).

Katika aya nyingine imesemwa:

'Na kama atakuwa miongoni mwa waliokadhibisha na wakatenda maovu, kwake yeye kuna ukaribishwaji kwa maji ya moto yanayochemka na kuunguzwa kutoka Jahannam. Kwa hakika, hii ndio kweli na hakika. (Al-Waqiah: 92-95).

Aya nyingine imeelezea aina hii ya adhabu kama ifuatavyo:-

(Sauti itasikika): 'Mkamateni na msukumeni mpaka katikati ya Jahannam. Kisha mmiminieni kichwani mwake adhabu ya maji yachemkayo. (Aambiwe) 'Onja hii! Wewe ulikuwa mwenye nguvu, mheshimwa. Kwa hakika hii ni katika yale uliyoyatilia shaka. (Ad-dukhan: 47 - 50).

Mbali na hizi adhabu zilizotajwa juu, pia zipo aina nyingine za adhabu zitokanazo na moto. Miongoni mwao ni kupigwa chapa. Watu wa motoni watapigwa chapa kwa chuma cha moto kilichofikia wekundu. Hata hivyo, vyuma hivi ni machuma ya makafiri kutokana na vile ambavyo Mwenyezi Mungu ameshirikishwa navyo hapa duniani.

'...Kwa wale waliokuwa wakichuma dhahabu na fedha kisha wakazitumia katika njia ambayo si ya Mwenyezi Mungu. Wape habari juu ya adhabu iumizayo. Siku ambayo moto utatolewa katika vile walivyovichuma katika Jahannam, na kwa vitu hivyo watapigwa chapa katika paji la uso, mabegani na migongoni mwao. (Waambiwe) 'Hii ni ile (mali) uliyoizika kwa ajili yenu. Onjeni! kisha, katika vile mlivyochuma (mlichojilimbikizia). (At-Tawbah: 34 - 35).

AINA NYINGINE ZA ADHABU

Kinyume na inavyochukuliwa na wengi, Jahannam sio tu kwamba ni 'jikokubwa' ambamo watu wa motoni wataingizwa. Hii ni kweli. Hata hivyo, adhabu ya Jahannam haikufungika na kuchomwa tu. Watu wa motoni kadhalika watazingirwa na adhabu za aina nyingine za kimwili na kinafsi. Njia nyingi na vifaa vingi hutumika kumuweka mmoja katika adhabu hapa duniani. Mara nyingi adhabu humfanya awe kilema yule anayeadhibiwa. Wakati mwingine hufariki dunia kutokana na maumivu. Wale ambao wamepona wengine huwa mataahira. Bado, ukweli unabaki kuwa mbinu zinazotumika kutoa adhabu katika ulimwengu huu kimlinganisho ni dhaifu au ni ndogo mno kulinganisha na zile za motoni. Watu wa motoni wataadhibiwa kwa njia tofauti kabisa na hizi zitumikazo hapa duniani. Kwa yule ambaye anaadhibiwa kwa kutumia mitambo ya Umeme - umeme wenyewe pamoja na machungu yote ayapatayo mwanadamu kutokana na mitambo na maumivu ya umeme, vyote ni vimeumbwa na Mwenyezi Mungu. Aina nyingine nyingi zisizojulikana za vyanzo vya maumivu na udhaifu wa mwanadamu, vyote vinajenga sehemu ya Elimu iliyokamili, isiyo na upogo. Vivyo hivyo Mwenyezi Mungu ataadhibu kwa namna ambavyo hakuna mfano wake. Hii ni kanuni ya Mwenyezi Mungu Mwenye Nguvu (Al-Wahhad. Katika maneno ya Qur'an, katika Jahannam, kuna adhabu kila mahali. Hakuna ahueni ya kutoadhibiwa, itawaenea watu wa motoni kutoka kila upande. Hawawezi kupewa ahueni wala wao wenyewe kuikwepa adhabu.

'Wanakuuliza juu ya kuharakishwa adhabu. Lakini, kwa hakika Jahannam itawazunguka makafiri wote. Siku hiyo adhabu itawafikia kutoka juu yao na kutoka chini yao. Na (sauti) itasema: 'Onjeni (matunda) ya vitendo vyenu. (An-Kabuut: 54 - 55).

Mbali na hayo, vyanzo vingine huko motoni ni vile vilivyobainishwahapa chini:-

'Jahannam - watachomwa humo - kitanda kibaya (kwa hakika kulala humo)! Wana maskani mabaya Humu! Kisha wataonja, maji yachemkayo, kinywaji cheusi, kilichooza (usaha) na chabaridi kweli kweli na adhabu nyingine mfano wa hizo. (Sad: 56 - 58).

Kutokana na aya hii na nyingine, Mwanadamu atafahamu kuwa kuna aina nyingine za adhabu huko motoni. Zilizo wazi zaidi ni kama vile moto (kuunguzwa), kusimangwa, hizi zimerejewa sana katika Qur'an. Hata hivyo, watu wa motoni hawana kinga kwamba wasiadhibiwe kwa aina nyingine ya adhabu. Kwa mfano, kuna kushambuliwa na wanyama mwitu, kutumbukizwa katika shimo la wadudu, ng'e na nyoka, kuumwa na panya, kuuguza vidonda vitokanavyo na minyoo, na aina nyingine nje ya fikra za mwanadamu ambazo zinaweza kama kuwakabili watenda maovu kwa wakati mmoja.

JOTO KALI, GIZA TOTORO, MOSHI NA WEMBAMBA

Sehemu nyembamba, yenye joto na ambayo ni chafu huudhi mno mtu kuwemo humo katika dunia hii. Mvuke na joto husababisha hali ya kukosa raha; hali ngumu ya upumuaji. Jambo ambalo ni muhimu kwa mwili wa mwanadamu huwa gumu katika mahali ambapo mvuke wake ni mwingi. Kushindwa kupumua, husababisha kulegea viungo, kifua kupandishwa juu na kushushwa. Hata kivuli hakiwezi kutoa nafuu au ahueni katika sehemu yenye joto kali na mvuke mwingi. Hewa nzito ambayo haionekani iliyoenea husababisha kukosa raha. Pia kiwango cha joto na mvuke katika siku za kiangazi ni vigumu kustahmili (au kuvumilika). Hali hii tete, ndiyo itakayoenea Jahannam yote. Mwanadamu ambaye amechukuwa tahadhari aina kwa aina ili kuzuia kuwa katika joto kali hapa duniani, atahisi kukata tamaa huko motoni. Jahannam ni joto kuliko jangwa lolote na chafu zaidi na sehemu ya ukandamizaji kuliko sehemu yoyote inayoweza kufikiriwa. Joto hupenya mwili wa mwanadamu, itaweza kuhisiwa katika kila chembe ya uhai mwilini. Kwa makafiri hakuna uwezekano wa kupata nafuu au joto kupozwa humo. Katika Qur'an, hali ya watu wa motoni imebainishwa kama ifuatavyo:

'Na watu wa kushoto - Ni akina nani hao watu wa kushoto? (Watakuwa) katikati ya moto uwakao wa Jahannam na katika maji yachemkayo. Na katika kivuli cha moshi mweusi. Hakuna (humo) kupumzika wala kustarehe. (Al-Waqiah: 42 - 44).

"Ole wao siku hiyo! Wale wanaokadhibisha! "(Itasemwa)" Ondokeni muendee kile mlichokuwamkikanusha mkidhani ni uongo. Kiendeeni kivuli (cha moshi) kilicho katika mihimili mitatu. (ambacho hutoa) kivuli kisicholeta baridi, na kisichopunguza joto. (Al-Mursalat: 28-31).

Katika mazingira hayo, na kuwemo katika sehemu nyembamba inathibitisha aina nyingine ya adhabu. Aina hii ya adhabu imeainishwakama ifuatavyo:-

'Na wakati watakapotupwa, wakafungiwa pamoja, katika sehemu iliyo njembamba humo, watalilia waangamizwe humo na kisha (isemwe) 'Siku ya leo msiombe kuangamizwa mara moja tu, ombeni kuangamizwa kwenye kujirudia rudia (mara nyingi). (Al-Furqaan: 13 - 14).

Kufungiwa sehemu nyembamba katika dunia hii, humfanya mtu awe kichaa (aharibikiwe kifikra). Kuwekwa katika Selo kwa wafungwa gerezani (tena nyembamba) ni moja ya adhabu mbaya kabisa kwa wafungwa. Kubakia katika mgandamizo wa gari mara baada ya ajali, au kuwa katika vifusi vya majengo yaliyoporomoka mara baada ya tetemeko la ardhi, huchukuliwa kama ni miongoni mwa majanga makubwa. Hata hivyo mifano kama hiyo ni kiwango cha chini mno ukilinganisha na matukio kama hayo huko motoni. Tangu hapo, mtu anayekuwa katika vifusi au mikandamizo mingine, mara nyingi hupoteza fahamu na kufa au kuokolewa hai baada ya muda fulani. Katika hali zote mbili maumivu hutoweka baada ya muda fulani.

Hali si hivyo kwa Jahannam. Hakuna mwisho wa maumivu katika moto na hivyo hakuna matumaini. Katika uchafu, unaonuka, uliooza, sehemu yenye fukuto na moshi uliojaa. Makafiri hali ya kuwa mikono yao imefungwa katika shingo zao na kuwekwa katika chumba kidigo, watakuwa kwenye kuadhibika kikweli kweli. Watajitahidi, kupambana ili wapate ukombozi, lakini wapi! Hawezi japo kusogea. Mwishowe, ataomba aruhusiwe kupotea, kama ilivyoelezwa katika aya, na kutamani japo awe amekufa. Ombi hili litarejeshwa kwake. Katika shimo hilo dogo alimowekwa atabakia kwa miezi, miaka na pengine mamia ya miaka. Kukosa amani kutajaza moyo wake, wakati akiomba zaidi ya mara elfu ili atoweke. Mara ataondolewa si kwa kupata wokovu bali atakuwa anahamishiwa katika kituo chengine cha adhabu mumo humo motoni.

CHAKULA VINYWAJI NA MAVAZI

Ulimwengu umesheheni aina mbalimbali za vyakula. Viko ambavyo ni vitamu na vyenye vimea vinavyohitajika mwilini. Vingine ni vichachu, vichungu na vikali, vyote vikihitajika kwa mpangilio maalum mwilini. Kila kimoja ni katika Rehema ya Mwenyezi Mungu. Aina mbalimbali za nyama, matunda na mbogamboga vyenye rangi mbalimbali, ladha na harufu, maziwa na vilivyosindikwa kutokana na maziwa, asali na aina nyingi katika vimea vya vyakula vinavyozalishwa na wanyama na viungo vya aina zote, vyote hivi vimeumbwa maalum na Mwenyezi Mungu na kwa uungwana akapewa Mwanadamu kutokana na dhima aliyopewa tangu kuumbwa kwa ulimwengu huu. Zaidi ya hayo, hisia za mwanadamu zimeumbwa kwa namna ambayo zinaweza kupokea vyakula hivi vyenye ladha ya aina yake. Kwa kupelekwa wahy (ufunuo) na Mwenyezi Mungu, Mwanadamu anapata hamu katika vyakula visivyo na uvundo na wakati huohuo akikereka kwa vyakula vilivyooza na kunuka, usaha na kadhalika. Huu nao ni aina ya wahy toka kwa Mwenyezi Mungu.

Upendeleo, mkubwa zaidi ya huu hapa duniani, umewekwa maalum katika Pepo, na kutokana na huo waumini watavuna manufaa hayo milele. Hii ni zawadi ya Mwenyezi Mungu ambaye hutoa Rehema na Utukufu. Wakazi wa motoni kwa upande wao, kutokana na vitendo vyao vibaya walivyofanya katika dunia hii, watawekwa mbali na rehema ya Mwenyezi Mungu, ambaye ni Al-Razzaq, hivyo yote watayokabiliana nayo ni adhabu.

Ni katika siku ambayo watapelekwa mbele ya moto 'Mmepata vitu vyenu vizuri katika maisha ya ulimwenguni. Na mpepata faraja kutokana nayo; lakini leo mtalipwa adhabu idhalilishayo kwa vile mlikuwa Jeuri katika ardhi bila ya kutenda uadilifu, na kwamba mlizidi katika kuchupa mipaka. (Al-Ahqaf: 20).

Hakutakuwa tena na upendeleo kwao. Hata kule kukutana na mahitaji muhimu inakuwa adhabu. Chakula maalum kimeaumbwa na Mwenyezi Mungu kama sehemu ya adhabu. Kuleta maumivu. Chakula pekee kilichoandaliwa kwa ajili yao ni pamoja na matunda makali yenye miiba na mti wa Zakkum, ambao kamwe haunenepeshi wala hauondo njaa. Bali hutoa machungu, kuchana midomo, shingo, matumbo na kutoa ladha na harufu yenye kuchukiza. Katika Qur'an tunaona ufafanuzi wa sehemu zote mbili, wa peponi palipo na uzuri uliotukuka na vyakula vizuri, na ule wa motoni wa vyakula visivyovumilika kwa ajili ya watu wa motoni.

'Je! Karibisho la namna hii silo bora au kupata mti wa Zakkum? Kwa hakika tumeufanya kuwa jaribio kwa watenda maovu. Hakika ni mti ulioota toka chini kabisa ya Jahannam. Matunda yeke ni kama kichwa cha shetani. Bila shaka wao watakula katika huo wajaze matumbo yao: (As-Saaffat: 62 - 66).

Hakuna chakula kitakachokuwepo kwa ajili yao ila miiba michungu. Hakinenepeshi wala hakiondoi njaa. (Al-ghaashiyah: 6 - 7).

Watu wa motoni kwa kuwa kwao waasi na wasiomshukuru Mwenyezi Mungu wanastahili adhabu hiyo. Kama adhabu, wanakabiliana na karibisho la aina hiyo. Katika Surat Waqi'ah, karibisho hili limeelezwa kama ifuatavyo:-

'Hakika wao kabla ya haya walikuwa wakiishi maisha ya anasa. Na walikuwa wakishikilia madhambi makubwa makubwa. Na walikuwa wakisema 'Nini! tutakapokufa na kuwa udongo na mifupa kweli tutafufuliwa? Na wazee wetu wa zamani?" Sema, Bila shaka, wa mwanzo na wa mwisho. Wote kwa hakika watakusanywa katika mkutano wa siku maalum. Kisha, ninyi mliopotea na kukadhibisha, kwa hakika mtaonja mti wa Zaqqum, kisha mtajaza matumbo yenu. Na mtakunywa maji yachemkayo juu yake: Kwa hakika mtakunywa kama ngamia mgonjwa aliye na kiu sana. Hiyo ndio karamu yao ya siku ya malipo. (Al-Waqi'ah: 45 - 56).

Hapa ulimwenguni, mara kadhaa, mtu anaweza akaugua kutokana na kuvimba na kuumwa mno koo au maumivu ya tumbo. Hata hivyo katika Jahannam, kamwe hakuna muda utakaopita bila maumivu kutokana na aina hizi za maumivu. Vyakula wanavyotakiwa kula vyenyewe vinakera. Kama watadiriki kumeza, wataona kama walivyokula matumboni mwao vyuma vilivyo yeyushwa.

'Bila shaka mti wa Zaqqum. Ni chakula cha (kuliwa na) maasi. (Kwa umoto wake ni) kama shaba iliyoyeyushwa; huchemka matumboni kama mchemko wa maji ya moto kabisa. (Kuambiwe): Mkamateni (huyu asi) na mumtupe katikati ya Jahannam. Kisha mwagieni juu ya kichwa chake adhabu ya maji ya moto. (Aambiwe) 'Onja! Ulikuwa wewe ni mwenye nguvu, Mheshimiwa. Hakika hii ndio ile mliyokuwa mkibishana, (mkitilia shaka). (Ad-Dukhan: 43 - 50).

Kamwe hakishibishi. Katika hali kama hii, watu wa motoni wataumia milele, kwa njaa ya ajabu. Adhabu hii si kwamba inatokea mara moja tu. La! Hii ni adhabu ya kujirudia rudia milele. Watu wa motoni watahisi njaa kwa kiwango cha hali ya juu. Watu hawa watajaribu mara kwa mara wapatiwe msaada, haupatikana msaada kwao ila kupewa matunda ya miiba yaliyo machungu yanayofanya wachanganyikiwe kwa uchungu. Kisha wanakimbilia maji yachemkayo. Na maji haya kamwe hayawezi kuyeyushwa.

Kama ilivyobainishwa katika aya hapo juu, watayabugia kama wanywavyo ngamia waliochanganyikiwa kwa kiu. Ili adhabu hii ifanywe kali zaidi, makafiri wataswagwa kuingizwa motoni hali yakuwa ni wenye kiu kweli kweli. Hayo, tunafahamishwa katika aya ifuatayo:-

'Na tutawachunga waovu (kuwapeleka) katika Jahannam, hali ya kuwa wana kiu kubwa. (Mariam: 86).

Mbali na maji yachemkayo, kinywaji kingine chenye kuchukiza kwa ajili ya watu wa motoni ni usaha. Maji haya (usaha) yanatokana na mwasho, moja katika vinavyotoka katika mwili wa Mwanadamu hali yakuwa na harufu mbaya kabisa, ni chaguo la pili la makafiri. Usaha watapewa makafiri pamoja na damu. Katika aya nyingine, inaainishwa kuwa usaha utapewa makafiri pamoja na maji yachemkayo, ili makafiri waonje ladha mbaya ya usaha na wapate ukali wa maji ya moto katika ufahamu wao wote. Pamoja na kule kuumiza kwake na kutovumilika, bado makafiri watakunywa ili kutosheleza mahitaji yao kuonesha hamu yao ya kunywa ili kukata kiu. Mara watakapoonja adhabu hii watakimbilia nyingine. Hali hii pia itaendelea milele. Kutokana na kutokatika kwa kiu, watu wa motoni watakuwa wanahaha katika kusaka vya kuondosha kiu yao.

'Hawataonja humo baridi wala kinywaji; Ila maji yachemkayo sana na usaha. (An-Nabaa: 24 - 26).

'Basi leo hapa hana rafiki mpenzi: Wala hana chakula ila maji ya usaha: Hawakili hicho isipokuwa wakosa - (Al-Haqqah: 35 - 37).

Makafiri watafanya juhudi kutaka kuumeza huu mchanganyiko, lakini haitaleta nafuu. Damu na usaha utawakereketa lakini hawafi:

'Ambaye mbele yake kuna Jahannam na atanyweshwa maji ambayo ni usaha. Awe anayagugumiza lakini hawezi kuyameza. Na (sababu za) mauti zitamjia kutoka kila mahali, lakini hatakufa. Na mbele yake kuna adhabu kali vile vile. (Ibrahim: 16 - 17).

Katika hali hii ya kukata tamaa, kwa njia ya majadiliano maalum, wakazi wa motoni watawaona watu wa peponi. Watashuhudia neema mbalimbali za kustaajabisha walizoruzukiwa. Hili nalo litazidisha machungu yao. Wakati huohuo, watu wa motoni wataomba sehemu katika vile walivyopewa watu wa peponi. Lakini hili nalo litatupiliwa mbali:-

'Na watu wa motoni watawaita watu wa peponi, (kuwaambia): 'Tumiminieni (Tumwagieni) maji au (kitu) katika vile alivyokupeni Mwenyezi Mungu." Waseme (watu wa peponi), "Hakika Mwenyezi Mungu ameharamisha vyote viwili hivyo kwa makafiri."(Al-Aaraf: 50).

Mbali na fursa hizo, nguo za watu wa motoni pia zimetengenezwa kwa ajili yao tu. Ngozi ya mwanadamu ni yenye hisia kali; hata kugusa jiko la mafuta lililopata joto au pasi kwa sekunde moja hutoa maumivu yasiyo na kifani. Katika hali kama hiyo aliyeungua hupata maumivu kwa muda wa masiku kadhaa, hali kidonda kikioza na kuvimba au kupona. Jahannam, kwa upande wake, kuna mavazi ya moto kuliko chuma kilichoyeyushwa, ambacho hugeuka kuwa miale ambayo hufunika ngozi na kuuguza kabisa kabisa.

"... Basi wale waliokufuru watakatiwa nguo za moto na watamiminiwa juu ya vichwa vyao maji yachemkayo. Kwa maji hayo vitayeyushwa vilivyomo matumboni mwao na ngozi zao (Pia). (Al-Hajj: 19 - 20).

'Na utawaona wakosa siku hiyo wamefungwa katika minyororo. Nguo zao zitakuwa za lami, na moto utazijia nyuso zao (uzibabue). (Ibrahim: 49 - 50).

'Watakuwa na magodoro ya moto wa Jahannam; na nguo zao za kujifunikia (pia). Na hivi ndivyo tunavyowalipa madhalimu. (Al-Araf: 42).

MALAIKA WA ADHABU

Pamoja na adhabu yote hiyo itakayowakabili makafiri; hakuna hata nafsi moja itakayoweza kutoa msaada kwa watu wa motoni. Hakuna nafsi itakayoweza kuuokoa kutoka katika adhabu. Kwa kutekelezwa huku, kutawapa uchungu mkubwa wa upweke. Kwa madhalimu, Mwenyezi Mungu anasema katika Qur'an: 'Hivyo, hii leo, hana rafiki.' '(Al-Haqqah: 35).

Miongoni mwao kuna 'Malaika wa adhabu ambao ataadhibu kikweli kweli. Hawa ni wakali, wasio na huruma, walinzi wanaotisha, wasio na jukumu lingine zaidi ya kuwaadhibu waovu. Madhumuni ya kuwepo kwao ni kulipiza kisasi kwa wale walio muasi Mwenyezi Mungu, na wanatekeleza jukumu lao hilo kwa ustadi mkubwa na tahadhari.

'Enyi Mlioamini! Jiokoeni nafsi zenu na watu wenu na moto ambao kuni zake ni watu na mawe. Wanausimamia Malaika wakali; wenye nguvu, hawamuasi Mwenyezi Mungu kwa amri zake na wametenda waliyoamrishwa'. (At-Tahyrm: 6).

'Sivyo hivyo! Kama haachi, tutamkokota kwa nywele za utosi. Utosi muongo, wenye Madhambi. Basi na awaite wanachama wenzake. Na sisi tutawaita malaika wa motoni. Sivyo!, Usimtii, bali Sujudu na uwe karibu - (Al-A'laq: 15 - 19).

Malaika hawa wa adhabu huwafanya makafiri wahisi laana ya ghadhabu za Mwenyezi Mungu kupita kiasi, na yenye kutesa mno. Nukta moja hapa inahitaji mazingatio; Malaika wa motoni (wa adhabu) kamwe hawawezi kufanya ukatili au kutokuwa waadilifu. Kazi yao wao ni kutekeleza adhabu kwa kiwango ambacho makafiri wanastahili. Malaika hawa wenye kudhihirisha uadilifu mkubwa wa Mwenyezi Mungu, ni viumbe watakatifu ambao hutekeleza majukumu yao kwa ridhaa na unyenyekevu mkubwa kwa Mwenyezi Mungu.


    
7 / total 8
You can read Harun Yahya's book Kufa Ufufuko Jahannam online, share it on social networks such as Facebook and Twitter, download it to your computer, use it in your homework and theses, and publish, copy or reproduce it on your own web sites or blogs without paying any copyright fee, so long as you acknowledge this site as the reference.
About this site | Tengeneza kurasa yako ya nyumbani | Add to favorites | RSS Feed
Mambo yote yanaweza kuynakiliwa, kuchapwa na kusambazwa kwa kurejea katika kurasa hii
(c) All publication rights of the personal photos of Mr. Adnan Oktar that are present in our website and in all other Harun Yahya works belong to Global Publication Ltd. Co. They cannot be used or published without prior consent even if used partially.
© 1994 Harun Yahya.www.harunyahya.com
page_top