Kufa Ufufuko Jahannam

SHUSHA KITABU

Download (DOC)
Maoni

SURA ZA KITABU

< <
8 / total: 8
|
KUFA UFUFUKO JAHANNAM - Harun Yahya
KUFA UFUFUKO JAHANNAM
   ADHABU YA KIROHO HUKO JAHANNAM

Hadi hapa, sehemu kubwa ya adhabu zilizoainishwa ni zile za kimwili tu. Hata hivyo pamoja na adhabu hizi za kimwili pia zipo adhabu nyingine za kinafsi. Miongoni mwa hizo ni kujuta, kukosa matumaini, kusikitika, kuhisi kutendewa vibaya (kuonewa), kuadhirika na kukata tamaa. Hisia hizi huibuka kutokana na adhabu mbalimbali anazopata:-

Moto unaopenya hadi kwenye moyo

Kwa namna moja au nyingine, kila mmoja huonja adhabu za kiroho hapa ulimwenguni. Kwa mfano, kumpoteza jamaa yake wa karibu rafiki, mke au mume, mtoto au mtu ambaye ukaribu wake na mtu huyo humtegemea sana, husababisha majonzi katika moyo ambayo hayawezi kuelezeka. Majonzi haya kwa hakika ni aina maalum ya adhabu toka kwa Mwenyezi Mungu aliyoipandikiza katika moyo wa mtu kutokana na kumfanya kwake mtu huyo ni wa kutegemewa kutokana na kupotea kwake au kumuasi kwake Mwenyezi Mungu. Yampasa mwanadamu kudhihirisha mbele ya Mwenyezi Mungu hisia za mapenzi, kuridhika, kunyenyekea, kumuogopa, kumtegemea na urafiki wa hali ya juu. Kushindwa kufanya hivyo na badala yake kuyaelekeza haya kwa asiyekuwa yeye, ambaye pia ameumbwa na Mwenyezi Mungu na hivyo kuhitajia, kwa maneno mengine, humshirikisha na Mwenyezi Mungu na viumbe vyake, husababisha adhabu hii.

Waabudu masanamu pia huonja adhabu hii, hivyo kuweza kupata fundisho kutokana nayo, na hivyo hutarajiwa kuomba msamaha na kurejea kwa Mwenyezi Mungu kabla mauti hayajamkuta. Vipo viumbe vyengine ambavyo mwanadamu amevijengea dhana sawa na masanamu. Miongoni mwa hivyo ni kumiliki vitu, fedha, bahati, jeuri; kwa muhtasari, kitu chochote au dhana yoyote ambayo inaabudiwa kinyume na Mwenyezi Mungu yaweza kufanywa sanamu. Uchungu kwa kupoteza hayo masanamu ambayo huingizwa katika nyoyo za mmoja wao katika dunia hii ni kidogo kulinganisha na adhabu kali itakayowakabili watu katika jahannam. Kwa maana yake halisi, huwa ni onyo. Katika Jahannam, machungu yatakuwa ni halisi na yasiyo na ukomo yakiwasubiri walioabudu masanamu. Wakati mwingine hii adhabu ya kiroho inakuwa kubwa kiasi kwamba, mwingine angeomba adhabu ya kimwili kuliko hii.

Hata kujiua huchukuliwa ni ukombozi. Moto unaopenya hadi kwenye moyo'.

Adhabu kali itamthubutikia kila mwenye kuramba kisogo, msengenyaji. Ambaye amekusanya mali na kuyahesabu. Anadhani ya kuwa mali yake itambakisha milele. Hasha! Bila shaka atavurumizwa katika hutama. Na ni jambo gani litakalokujulisha ni nini hutama? Ni moto waMwenyezi Mungu uliowashwa. Ambao unapanda nyayoni. Hakika watafungiwa humo. Kwa magogo marefu marefu. (Humazali: 1-9).

Pia maumivu makali kupita kiasi katika dunia hii hutoweka, Mabaki yake yanaweza kusalia kwa muda, lakini muda huyafanya yatoweke yale makali yake ya wazi. Katika Jahannam, maumivu makali zaidi hupenya katika nyoyo za makafiri kama vile hasira na kubakia hivyo milele. Mbali na hili, adhabu ya kiroho hutoa hisia ambazo ni kati ya kukata tamaa na kufedhehesha, ghadhabu na bughdha. Adhabu za aina zote mbili, yaani za kiroho na kimwili zitasheheni huko Jahannam zikimsubiri kila aliyechupa mipaka ya Mwenyezi Mungu, kafiri.

ADHABU YA FEDHEHA

Aya nyingi zinazohusu motoni, zinatufahamisha kwamba adhabu za kudhalilisha na kufedhehesha zinawasubiri makafiri huko. Watapa adhabu hizi kutokana na jeuri na kujivuna kwao.

Katika dunia hii, moja katika malengo ya makafiri ni kuwafanya wengine wawatukuze na kufurahia hadhi zao katika jamii na utanashati wao. Fani za kipekee, watoto, ulimbwende, magari na vitu vingine vya kidunia huwa na maana zaidi endapo ndivyo vitakavyotangulizwa mbele yao. Hakika, katika Qur'an, kujitukuza kwa utajiri na vitu, vimeelezwa kama mapambo ya kidunia. Hii hali, hubadilika huko akhera na kuwa adhabu ikiwa ni kudhalilishwa pamoja na machungu ya kimwili. Hii ni kwa sababu, makafiri wanasahau juu ya 'Mwenyezi Mungu, mwenye kusifiwa' (Al-Baqarah: 267), na badala yake wakafanya matamanio ya nafsi zao kuwa miungu yao:

'Je! Umemuona yule aliyefanya matamanio yake, (kile anachokipenda), kuwa Mungu wake? Basi je, utaweza kuwamlinzi wale? (Al-furqan: 43).

Kwa sababu hii muda wake mwingi, umejishughulisha katika kuchuma, kushukuriwa na kusifiwa yeye Mwenyewe, kuliko kumsifu na kumtukuza Mwenyezi Mungu. Amejijengea katika maisha yake kupata furaha toka kwa watu badala ya kutafuta chumo la namna ya kukubaliwa na Mola wake. Hii ndio sababu inayompelekea mwanadamu huyu achukie mno kama atafedheheshwa mbele ya watu wengine.

Kitu kingine kinachomnyongesha kafiri ni kudhalilishwa na kutothaminiwa mbele ya watu. Wapo pia miongoni mwao ambao wengatamani afadhali kufa kwa ajili ya kutukuzwa kuliko kitendo cha kupuuzwa. Hali ya motoni imebeba ujumbe wa aina hii katika kiini chake. Hali hii ngumu ya wakazi wa motoni msingi wake ni kutokana na ujeuri wao. Kama kabla ya hapo hawakuwa wakipuuzwa. Aya nyingi zinathibitisha juu ya ukweli huu.

"Na siku watakapowekwa waliokufuru mbele ya moto. "Mlipoteza vitu vyenu vizuri katika maisha yenu ya dunia. Ninyi mlijifurahisha navyo; leo mtapewa adhabu ya fedheha kwa sababu ya kule kujivuna kwenu bure duniani; na kwa sababu ya kule kuasi kwenu. (Al-Ahqaf: 20).

Wala wasidhani wale waliokufuru kwamba huu muda tunaowapa ni bora kwao. Hakika tunawapa muda na (inatokea ya kuwa) wanazidi madhambi (katika muda huo). Na itakuwa kwao adhabu ya kuwadhalilisha. (Al-Imran: 178).

Makafiri watakuwa katika maelfu ya aina mbalimbali za kushushwa hadhi. Na pengine chini zaidi kuliko hali iliyonayo wanyama hapa duniani. Nyundo za chuma, majambia na minyororo (makongwa pia). Kwa hakika, kudhalilisha ndio msingi mkuu wa adhabu zote za motoni. Kwa mfano, atakapokuwa anatumbukizwa motoni, atakuwa anashushiwa hadhi. Hali hii ya kupuuzwa huanzia tangu pale kafiri atakapokuwa anafufuliwa na kuhukumiwa kuingia motoni. Zaidi ni kwamba adhabu haitapunguzwa. Miongoni mwa mabilioni ya watu, kafiri atachukuliwa na Malaika na kukamatwa kwa kisogo chake na miguu.

Katika maneno ya Qur'an:

'Siku hiyo hataulizwa mtu kwa dhambi zake wala jini. Watajulikana waovu kwa alama zake; basi watakamatwa kwa nywele zautosi na kwa miguu. (Al-Rahman: 39,41).

Katika moto, makafiri watakwenda kwa makundi kwa aina ya adhabu mbaya zaidi kuliko ile ya wanyama wanayopata hapa duniani. Kwa kukamatwa nywele za utosini, na kuburuzwa njiani kisha atatupwa motoni. Hali ya kushindwa kuzuia lolote, ataomba msaada, lakini wapi! Hakuna msaada wowote. Hali ya kukata tamaa itazidisha adhabu.

'Sivyo hivyo! Kama haachi tutamkokota kwa nywele za utosi. Utosi mwongo, wenye madhambi. Basi na awaite wanachama wenzake (wawasaidie). Na sisi tutawaita Malaika wa Motoni. Sivyo! Usimtii, lakini Sujudu na kuwa karibu (na Mwenyezi Mungu). (Alaq: 15 - 18).

Kama aya inavyobainisha; makafiri watakuwa:

'Siku watakayosukumwa katika moto wa Jahannam msukumo (wa nguvu) Na waambiwe huu ndio ule moto ambao mlikuwa mkiukadhibisha. (Attuur: 13 - 14).

Na pia watakuwa: 'Ama wale wanaokusanywa kifudifudi (wanaburuzwa kwa nyuso zao) mpaka katika Jahannam, hao watakuwa mahali pabaya, na wenye kupotea njia ya haki. (Al-Furqaani: 34).

Hivyo hivyo: 'Na watakaoleta ubaya, basi zitasunukishwa nyuso zao motoni. (Waambiwe): "Hivi mnalipwa '(kwa mengine) mbali na yale mliyotenda)". (An-Naml: 90). "Siku watakayokokotwa motoni kifudifudi (na huku wanaambiwa) 'Onjeni Mguso wa Jahannam. (Al-Qamar: 48).

Kudhalilishwa kunazidi mara baada ya kuingia motoni, Mbali na maumivu ya kimwili, maumivu makali yatakuwa ni hisia za kuona kuwa kudhalilika na kuona yu mtu wa chini:-

'Mkamateni mumtupe katikati ya Jahannam. Kisha mwagieni juu ya kichwa chake adhabu ya maji ya moto. "Onja! Wewe ni Mwenye nguvu, Mheshimiwa! Hakika hii ndio ile mliyokuwa mkiitilia shaka (Ad-Dukhan: 47 - 50).

Katika kuwadhalilisha makafiri, kumetayarishwa vifaa maalum; makongwa, minyororo vyote vitatumika.

'Mkamateni na mtieni makongwa. Kisha mtupeni motoni. Tena katika minyororo yenye urefu wa dhiraa sabini mwingizeni (mtatizeni). Hakika yeye alikuwa hamuamini Mwenyezi Mungu - Mtukufu. Wala hahimizi kulisha maskini. (Al-Haqqah: 30 - 34).

Katika ulimwengu huu, kabla wale waliokanusha waziwazi, hata wanyama hawafungwi minyororo. Na kwa wanadamu, ni wale tu ambao hawatendewi haki au watu hatari waliopungukiwa na akili (vichaa) ndio hufungwa minyororo au pingu. Hali ikiwa ndio hivi, wale watakaopelekwa motoni ndio watu wa chini zaidi kuliko wote. Ndio sababu wamefungwa katika 'minyororo isiyopungua dhiraa sabini' kama ilivyobainishwa katika aya hapo juu. Aya nyingine inaelezea tukio hili kwa undani zaidi namna linavyokusudiwa kumuonesha asi kuwa ni wa daraja la chini kabisa:-

'Zitakapokuwa pingu (makongwa) shingoni mwao na minyororo na wanaburuzwa, katika maji ya moto kisha wanaunguzwa motoni. Tena wataambiwa, 'Wako wapi mliokuwa mkiwashirikisha kinyume na Mwenyezi Mungu? . (Al-Muumin: 71 - 74).

. Na kama unastaajabu (juu ya upofu wao), basi cha ajabu kabisa ni usemi wao: 'Je, tutakapokwisha kuwa udongo, kweli tutakuwa katika umbo jipya!' Hao ndio waliomkufuru Mola wao. Watu hao watakuwa na makongwa shingoni mwao. Watu hao ndio wa motoni, humo watakaa milele. (Ar-Raad: 5).

'Siku hiyo utawaona watenda maovu wamefungwa katika minyororo. Nguo zao zitakuwa za lami na moto utazijia nyuso zao. Ili Mwenyezi Mungu ailipe kila nafsi kwa yale aliyoyachuma. Hakika Mwenyezi Mungu ni mwepesi wa kuhesabu. (Ibrahim: 49 -51).' .

'Basi wale waliokufuru watakatiwa nguo za moto na yatamiminwa juu ya vichwa vyao maji yachemkayo. Kwa (maji) hayo vitayeyushwa vilivyomo matumboni mwao na ngozi zao (pia). Na kwa ajili yao marungu ya chuma. Kila mara watakapotaka kutoka humo kwa sababu ya uchungu watarudishwa mumo humo na kuambiwa; 'Ionjeni adhabu ya kuungua." (Al-Hajj: 19 - 22).

Kusinyaa kwa nyuso zao na kuwa nyeusi ni moja ya dalili za kuwaonesha watu wa motoni watambulike. Katika dunia hii, unaweza kuwaona watu wasio na furaha au kuwa na huzuni kupitia nyuso zao. Kukosa thamani na kuwa katika daraja la chini. Aidha watu wa motoni wataonekana kama ilivyobainishwa katika aya ifuatayo:-

'Nyuso nyingine siku hiyo ni zenye kudhalilika (Al-Ghaashia: 2).

Mbali na aina mbalimbali za kudhalilisha zilizobainishwahadi sasa, tuzingatie kuwa kutakuwa na aina nyingine za adhabu zenye kudhalilisha huko Jahaanam. Katika Qur'an, neno 'dhalili' limetumika na mifano michache imetolewa ili kuliainisha. Hata hivyo, lazima izingatiwe kuwa hii ina maana kama ambavyo kwa namna yoyote isijifunge kwenye hiyo mifano michache iliyotolewa. Hisia zote, matukio yote yanayochochea udhalilishaji katika nafsi ya mwanadamu katika dunia hii imejumuishwa katika hii nadharia ya 'Udhalilishaji na yote inapatikana huko 'Jahannam'.

MAJUTO YASIYO KWISHA

Itakapofika wakati wa kufufuliwa, aliyekufuru, kwa uchungu kabisa atajua makosa aliyoyafanya. Majuto yanayotokana na makosa yake ambayo hana namna ya kuyaondoa humpa mtetemeko mbaya. Hali yake ya kukata tamaa itadhihirishwa na namna yake ya majuto. Wakati kafiri atakapokuwa anakabiliwa na matendo yake aliyoyafanya hapa duniani, atagundua kuwa hana muda tena wa kurekebisha mambo na hivyo kurejea hadhi yake aliyokuwa nayo. Bado atatamani apewe tena fursa ya kurejea dunia. Kwa mtazamo huu, atatamani kurejea katika maisha ya dunia ili arekebisha makosa aliyoyafanya. Wakati huo huo hatapenda kuwatazama jamaa na marafi zake waliokuwa wakifurahia wote maisha. Urafiki na Ujamaa mizizi yake itakuwa imekatwa wakati huo. Mtindo wa maisha na utamaduni wa watu waliokuwa nao, nyumba zao, magari yao, wake au waume, watoto, makampuni, itikadi walizokuwa nazo wakizitangaza zitakuwa hazina thamani. Jambo jepesi ni kuwa vyote vimebadilishwa na adhabu. Hali ya kutisha itakayokuwepo siku hiyo inabainishwa katika aya zifuatazo:-

'Na ungeona watakavyosimamishwa kwenye moto, wakawa wanasema "Laiti tungerudishwa (ulimwenguni); wala hatutakadhibisha (tena) aya za Mola wetu, na tutakuwa katika wanaoamini." Bali yamewadhihirikia walivyokuwa wakiyaficha zamani. Na kama wangelirudishwa bila shaka wangeyarudia yale waliyokatazwa, na bila shaka hao ni waongo. Na walisema 'Hakuna maisha ila maisha ya dunia; wala sisi hatutafufuliwa.' Na ungeona siku ya kiama watakavyosimama mbele ya Mola wao, akawaambia "Je! Si kweli haya?" Na wao wakasema "Kwa nini? Tunaapa kwa jina la Mola wetu." Aseme (Mwenyezi Mungu) 'Basi onjeni adhabu kwa kule kukanusha kwenu - (Al-an'am: 27 - 30).

WANAVYOANGALIWA WATU WA MOTONI

Hadhi na vyeo miongoni mwa waja hapa duniani ambavyo huwa vinapewa uzito mkubwa, hupoteza thamani katika Jahannam. Hali ambayo watakuwa nayo viongozi na wafuasi wao itakuwa ni ile ya chini kabisa kiasi cha wao kwa wao kupeana laana.

'Wakati wale waliokuwa wakifuatwa watakapowakana wafuasi wao, na wamekwisha iona adhabu, na maungano kati yao yamekatwa, wale waliowafuata watasema;

"Kama tungepewa fursa nyingine,tungewakana kama wanavyotukanusha." Namna hiyo, Mwenyezi Mungu anawaonesha vitendo vyao kama sababu (au chanzo) cha kuadhibiwa na kupuuza kwao. Kamwe hawataweza kutoka motoni.(Al-Baqarah: 116 - 167).

Watasema katika siku ambayo vichwa vyao vitavingirishwa katika moto kama tungemtii Mwenyezi Mungu na tungemtii Mtume.' Na watasema 'Mola wetu tuliwatii viongozi wetu na watu wakubwa na wametupoteza kutoka katika njia iliyonyooka. Mola wetu! Wape adhabu mara mbili na walaani mara nyingi! (Al-Ahzab: 66-68).

Wakibishana wenyewe kwa wenyewe watasema:

'Naapa kwa Mwenyezi Mungu, tulipotezwa Wakati tuliokulinganisha wewe Mola wa Ulimwengu (na vijiungu wa kubuni). Ni waovu pekee waliotupoteza na sasa hatuna wa kutuombea, hatuna hata rafiki mmoja muaminifu. Na kama tungekuwa na fursa nyingine bila shaka tungekuwa miongoni mwa waumini.' Kwa hakika muna humo dalili, lakini wengi katika watu hawaamini. (Ash-Shu'ara: 96-103).

Miongoni mwa watu wa motoni wanaokabiliwa na adhabu ya milele, kusimangana kutaibuka. Kila mmoja akimlaumu mwingine yeyote. Waliokuwa marafiki katika maovu wataanza kuhojiana wao kwa wao. Chanzo kikubwa cha kuogopana huko ni urafiki walioujenga huku duniani. Walishajihishana kila mmoja kufanya maovu na kupeana ujasiri wa kukanusha. Nadharia au mitazamo yote inayohusiana na urafiki umepotea katika uso wa Jahannam na mishikamano yote iliyoimarishwa duniani imetoweka na kuvunjika. Katikati ya kundi hilo kubwa la watu, bado kila mmoja yuko peke yake akiwalaani wote waliobaki:-

"Atasema (Mwenyezi Mungu), 'Ingieni motoni pamoja na umma zilizopita kabla yenu; za majini na watu.' Kila utakapoingia Ummah, utawalaani wenzao. Mpaka watakapokusanyika wote humo, wa nyuma wao watasema kwa ajili ya wa kwanza wao, 'Mola wetu! Hawa ndio waliotupoteza; basi wape adhabu ya moto mara mbili (maradufu)". Atasema; 'Itakuwa kwenu ninyi wote mara dufu, lakini ninyi hamjui tu. Na wa kwanza wao watasema kuwaambia wa nyuma yao: 'Basi ninyi pia hamkuwa na fadhila kuliko sisi. Kwa hivyo onjeni adhabu kwa sababu ya yale mliyokuwa mkiyachuma. (Aaraf: 38 - 39).

Na wale waliokufuru watasema(katika kutiliana chonza). 'Mola wetu tuoneshe wale waliotupoteza miongoni mwa majini na watu ili tuwaweke chini ya miguu yetu, wapate kuwa miongoni mwa walio chini kabisa (Fusilal/Ha mim Sajdah: 29).

Na (wakumbushe) watakapobishana katika moto huo -wakati madhaifu watakapowaambia wale waliojitukuza, 'Kwa yakini sisi tulikuwa wafuasi wenu, basi Je, mnaweza kutuondolea sehemu kidogo ya moto? Watasema wale waliokuwa wakijitukuza, 'Sisi sote tumo humu; Mwenyezi Mungu amekwisha hukumu baina ya vumbe - (Al-Muumin: 47 - 48).

'Hili ndilo jeshi litakaloingia pamoja nanyi.' Hapakupata mahala pazuri pa kufikia, hakika wao wataingia motoni.' Waseme (hawa wanaosimangwa). 'Lakini ninyi ndio wa kuambiwa namna makaribisho mema! Ninyi ndio mliotusababishia adhabu. Mahala pabaya kabisa hapo.' Waseme (waliokuja nyuma). Mola wetu! Waliotusababishia haya wazidishie adhabu mara mbili huku motoni' Watasema, 'Imekuwaje! Mbona hatuwaoni wale tuliokuwa tukiwahisabu kama waovu? 'Je tuliwafanyia mzaha? Ila macho yetu hawayaoni tu?" Bila shaka haya ya kuhasimiana watu wa motoni ni kweli. (Sad:59 - 64).

KUTAKA KUSAMEHEWA BAADA YA KUKATA TAMAA NA KUKOSA MATUMAINI

Watu wa motoni wamo katika hali ya kukata tamaa kabisa. Adhabu wanazopata ni ngumu mno na hazikatiki. Matumaini yao pekee ni kulia na kuomba waokolewe. Watawaona watu wa peponi na kuwaomba maji na chakula. Watajaribu kutubu na kuomba msamaha kwa Mwenyezi Mungu, juhudi zote hizi zitaambulia patupu.

'Watawaomba walinzi wa motoni: Watataka pia walinzi wa motoni wawe watu wa kati (Mawakala) kati yao na Mwenyezi Mungu na kuwaombeaRehema yake, Mateso humo ni makali, hayavumiliki kiasi kwamba watataka waokolewe japo kwa siku moja tu.

Na wale walio motoni watawaambia walinzi wa Jahannam, 'Muombeni Mola wenu atupunguzie (alau) siku moja ya adhabu.' (Walinzi) wawaambie'Hawakukujieni mitume wenu kwa hoja zilizo wazi? Waseme. 'Kwa nini?" Wawaambie 'Basi ombeni, na madua ya makafiri hayawi ila ni ya kupotea bure'. (Al-Muumin: 49 - 50).

Makafiri watazidi kujaribu kuomba msamaha, lakini bila huruma, hawapatilizwi, wanahangaka:

Watasema, 'Mola wetu! Tulizidiwa na ubaya wetu na tukawa watu wenye kupotea. Mola wetu! Tutoe humu motoni, na kama tutarejea tena katika maovu bila shaka tutakuwa madhalimu. Atasema, 'Hizikeni humo. Wala msiseme nami' Bila shaka kulikuwa na kundi katika waja wangu lilisema: "Mola wetu! Tumeamini, basi tusamehe na uturehemu, nawe ndiwe mbora wawanao rehemu.' Lakini ninyi mliwafanyia stihizai hata wakakusahaulisheni kunikumbuka. Na mlikuwa mkiwacheka. Hakika leo nimewalipa (pepo) kwasababu yakusubiri kwao. Hakika hao ndio waliofuzu. (Al-Muuminuun: 106 - 111).

Kwa hakika haya ndio mawaidha ya mwisho ya Mwenyezi Mungu kwa watu wa motoni. Maneno yake, 'Bakini humu hali ya kuwa ni wenye kupata hiziya na msizungumze nami', ni hitimisho. Kutoka hapo na kuendelea, Mwenyezi Mungu hatawafikiria tena. Watu pia hawapendi kufikiria suala hili.

Wakati waovu wanaungua motoni, wale waliofikia daraja la furaha na Uokovu' wanabakia peponi milele wakifurahia matunda yasiyokwisha waliyopewa na Mola wao. Mateso ya watu wa motoni yatakuwa makali kiasi kikubwa pindi watakapotazama maisha ya watu wa peponi. Kwa hakika, wakati wamo katika adhabu isiyovumilika, wanaweza kutazama furaha ya ya hali ya juu na rehema zilizopo peponi.

Waumini ambao makafiri waliwadharau katika ulimwengu huu, sasa wanaendeleza utimilifu wa furaha, wakiishi sehemu tukufu, nyumba za thamani, wanawake warembo na vyakula na vinywaji vitamu. Hali ya waumini iliyo ya amani na vikorombwezo vyake inazidisha udhalili wa kuwa motoni. Mazingira haya yanaongeza machungu makubwa na majuto kwa adhabu iumizayo.

Majuto huja zaidi na zaidi. Kuacha kufuata maamrisho ya Mwenyezi Mungu hapa duniani huwafanya wajione kuwa wao ni wenye majivuno katika sehemu waishiyo akhera. Watawageukia watu wa peponi na kujaribu kuzungumza nao. Wataomba msaada na huruma toka kwao. Lakini, hizi ni juhudi zisizo na matunda. Watu wa peponi nao watawaona watu wa motoni. Majadiliano baina ya watu wa peponi na wale wa motoni yataendelea kama ifuatavyo:-

'Katika mabusatni watawauliza watu wabaya; 'Ni nini kilichokupelekeni motoni?" Watajibu: Hatukuwa miongoni mwa waliokuwa wakiswali. Wala hatukuwa tukilisha maskini. Na tulikuwa tukizama (katika maasi) pamoja na waliokuwa wakizama. Na tulikuwa tukikadhibisha siku ya hukumu. Mpaka mauti yatatujia. Basi hautafaa uombezi wa waombezi (Al-Mudaththir: 40 - 48).

Katika wakati huu, Waumini na wanafiq watabishana kundi moja dhidi ya jingine. Wanafiq ni wale wanaobaki na waumini kwa kipindi fulani tu. Mbali na kukosa imani katika nyoyo zao, na kwa sababu ya maslahi yao binafsi wanatekeleza baadhi ya shughuli za kidini kama vile ni waumini. Hivyo wanavuna chumo la kuwa kwao 'Wanafiq.' Na katika Jahannam, wanaomba waumini wawasaidie. Majadiliano kati ya makundi haya mawili yameinishwa kama ifuatavyo:

'Siku watakaposema wanafiq wanaume na wanafiq wanawake kuwaambia waumini, 'Tungojeeni ili tupate mwangaza katika nuru yenu.' Waambiwe (kwa shihizai) 'Rudini nyuma mkatafute nuru yenu.' Utiwe ukuta baina yao wenye mlango ndani yake mna rehema na nje kwa upande wake wa mbele kuna adhabu. Watawaita 'Je hatukuwa pamoja nanyi?' Watawajibu, 'Ndio, walakini ninyi mlijitia wenyewe katika ukafiri, mkangojea, mkajitia katika shaka na matamanio ya nafsi yakakudanganyeni hata amri ya Mwenyezi Mungu ikaja. Na mdanganyaji amekudenganyeni kuhusu Mwenyezi Mungu. Basi leo hakitapokelewa kwenu kikomboleo wala kwa wale waliokufuru. Makazi yenu ni motoni; ndio kunako kustahikieni; nayo ni marejeo mabaya kabisa. (Al-Hadid: 13 - 15).

ADHABU ITAKAYOENDELEA BILA YA KUOKOLEWA

Mbali na hali zote hizi za adhabu ya Jahannam iliyokwisha elezwa hadi sasa, kuna namna nyingine ya kuzidisha machungu ya adhabu inayotolewa, nayo ni hii ya 'kudumu.' Hapa ulimwenguni, ukweli ni kwamba, hata machungu au maumivu makali kiasi gani hupungua jinsi muda unavyoendelea, Hutoa faraja kwa mwanadamu. Mwisho wa kila machungu ni faraja na hata kusubiri faraja hiyo hutoa matumaini. Lakini, kwa upande wa Jahannam, matumaini kama hayo hayapo. Na hili ndilo linaloumiza watu wa motoni zaidi. Wakati watakapotupwa motoni, wakafungwa minyororo, wakawekewa makongwa, kupigwa na kukusanywa katika sehemu zilizokuwa nyembamba, mikono yao ikiwa imefungwa shingoni mwao, wanajua kuwa hali hiyo itadumu milele. Jaribio lao la kutaka kujiokoa kamwe halitafanikiwa. Hii inaonesha kuwa adhabu yao itaendelea milele. Hali inayowakabili inaelezwa kama ifuatavyo:-

'Kila mara watakapotaka kutoka humo kwasababu ya uchungu, Watarudishwa mumo humo. 'Onjeni adhabu ya kuungua." (Al-Hajj: 22). Jahannam ni sehemu iliyotengwa kabisa. Makafiri wataingizwa humo na kamwe hawatatolewa. Hakuna njia ya kutokea. Hali ya kuona kuwa wamezingira itawadhihirikia makafiri. Wanazunguukwa na kuta zilizo na milango iliyofungwa kwa makufuli. Hali hii chungu wanaohisi ya kuzingirwa inaeelezwa katika Qur'an kama ifuatavyo:-

'Lakini waliokanusha aya zetu, hao ndio watu wa upande wa shari. Moto uliofungiwa utakuwa juu yao. (Balad: 19 - 20).

'Na sema huu ni ukweli uliotoka kwa Mola wenu, basi anayetaka na aamini na anayetaka na akufuru. Hakika tumewaandalia madhalimu moto, ambao kuta zake zitawazunguuka. Na wakiomba msaada, watasaidiwa kwa kupewa maji kama ya shaba iliyoyeyushwa itakayoziunguza nyuso zao. Kinywaji kibaya kilioje hicho. Na mahala pabaya palioje. (Al-Kahf: 29). 'Hao mahali pao ni Jahannam, wala hawatapata makimbilio ya kutoka humo. (An-Nisaa: 121).

Wakati makafiri watakapouona moto, watafahamu dhahiri shahir mahali watakapokuwa. Watatambua wazi kuwa hakuna njia yoyote ya kutokea humo. Katika hatua hii, dhana ya muda itakuwa haina maana, na adhabu ya milele inaanza. Uhalisia wa maumivu na mateso ndio hali halisi huko. Hapo itapita miaka mia, elfu au mamilioni, bado mja hajakaribia ukomo. Miaka milioni moja haina maana mbele ya milele. Wakazi wa motoni watasubiri mwisho, lakini ni tamaa isiyo na pakushika. Ndio maana umilele wa Jahannam unasisitizwa mno:-

'Mwenyezi Mungu amewaahidi wanafiqi wanaume na wanafiq wanawake na makafiri moto wa Jahannam kukaa humo daima. Huo unawatosha, na Mwenyezi Mungu amewalaani; nao wana adhabu itakayodumu. (At-Tauba: 68).

Lau kama hawa wangekuwa Mungu wasingeifikia (hiyo Jahannam). Na wote humo watakaa milele - (Al-Aniyaa: 99).

Na wale waliokufuru, watakuwa katika moto wa Jahannam, hawatahukumiwa kufa wala hawatapuguziwa adhabu yake. Hivi ndivyo tunavyomlipa kila asiye na shukurani. (Fatir: 36).

Machungu yote hapa duniani yana tamati. Muda wote kunakuwepo kuokolewa. Yeyote anayeathirika kutokana na machungu ama anakufa, au machungu yake yanapunguzwa. Lakini, Jahannam maumivu yanaendelea bila kupunguzwa, bila kutoa tahafifu japo kwa sekunde chake.

KUMBUSHO MUHIMU ILI KUEPUKA ADHABU

Katika kitabu chote hiki, imesisitizwa kwamba wale wanaozikataa amri za Mwenyezi Mungu, Mola wao, katika ulimwengu huu na wakakanusha juu ya kuwepo kwa Muumba hawatakuwa na ukombozi kesho Akhera. Na kwamba watakabiliana na adhabu yenye kutisha huko Jahannam.

Hivyo basi, bila ya kupoteza muda, kila mmoja anaweza kutambua hali yake mbele ya Mwenyezi Mungu na kujisalimisha kwake. Kinyume chake atajuta na kukutana na mwisho wenye kuogofya.

Mara nyingi wale waliokufuru watatamani lau wangelikuwa Waislamu. Waache wale na wafurahi na liwadanganye tumaini lao la Uongo. Karibuni hivi watajua. (Al-Hijr: 2 - 3).

Njia ya kuepuka adhabu ya milele, njia rehema ya milele na kufikia kukubaliwa naMwenyezi Mungu kuko wazi.

Kabla hujachelewa, kuwa na imani ya kweli. Tumia muda wako kwa kufanya mema ili upate radhi yake.


    
8 / total 8
|
You can read Harun Yahya's book Kufa Ufufuko Jahannam online, share it on social networks such as Facebook and Twitter, download it to your computer, use it in your homework and theses, and publish, copy or reproduce it on your own web sites or blogs without paying any copyright fee, so long as you acknowledge this site as the reference.
About this site | Tengeneza kurasa yako ya nyumbani | Add to favorites | RSS Feed
Mambo yote yanaweza kuynakiliwa, kuchapwa na kusambazwa kwa kurejea katika kurasa hii
(c) All publication rights of the personal photos of Mr. Adnan Oktar that are present in our website and in all other Harun Yahya works belong to Global Publication Ltd. Co. They cannot be used or published without prior consent even if used partially.
© 1994 Harun Yahya.www.harunyahya.com
page_top