SW.HARUNYAHYA.COMhttp://sw.harunyahya.comsw.harunyahya.com - Vitabu - Iliyowekwa hivi pundeswCopyright (C) 1994 sw.harunyahya.com 1SW.HARUNYAHYA.COMhttp://sw.harunyahya.comhttp://harunyahya.com/assets/images/hy_muhur.png11666Usije UkajutaLengo la kitabu hiki ni kuwaonya watu kwa siku ambayo watajuta wakisema” Laiti tungefahamu...,” “Laiti hatungekadhibisha aya za Mola wetu...,” “Laiti tungeliwafuata wale waliotuletea ujumbe...,” “Laiti tungelifanya hili au lile” n.k lengo pia ni kuwaita watu waishi maisha kwa ajili ya Mwenyezi Mungu kama wangali hai ili warekebishe makosa yao.

Ni lazima kufahamu vyema kwamba majuto siku hiyo hayatamkinga mtu yeyote na hasira ya Mwenyezi Mungu. Njia pekee ya kuepukana na majuto hayo ni kujisalimisha kwa Mwenyezi Mungu kama wakati bado upo na kufuata maamrisho ya Mwenyezi Mungu.

Kitabu hiki ni cha kulingania kwa njia ya Allah na kukumbusha adhabu isiyoepukika katika maisha ya akhera siku ambayo hakuna pa kujificha wala kuokolewa. 

]]>
http://sw.harunyahya.com/sw/Vitabu/46603/usije-ukajutahttp://sw.harunyahya.com/sw/Vitabu/46603/usije-ukajutaMon, 29 Aug 2011 00:15:41 +0300
Kufa Ufufuko JahannamMiongoni mwa sababu kubwa zinazowafanya watu wakengeuke na kufanya washughulike tu na matashi yao ni kule kutotaka kwao kufa. Ulimwengu na wanadamu wote waishio humo, hawataishi milele. Kinachowasubiri wale wakanao ulimwengu ujao ni hatari kubwa. Hasira za moto wa milele wa Jahanamu zitakuwa dhidi yao. Kitabu hiki kikiegemea aya za Qur’an kinatoa picha ya maelezo ya muda wa kufa, siku ya hukumu na adhabu za motoni, na kinatoa hadhari juu ya hatari kubwa inayotukabili.
]]>
http://sw.harunyahya.com/sw/Vitabu/9357/kufa-ufufuko-jahannamhttp://sw.harunyahya.com/sw/Vitabu/9357/kufa-ufufuko-jahannamThu, 18 Sep 2008 23:08:26 +0300
Nani Mwenyezi Mungu?Tangu zama za zama, watu wamekuwa wakiutafakari Ulimwengu na chanzo cha uhai na wametowa mawazo yao mbali mbali juu ya suala hili.  Tunaweza kuyagawa mawazo hayo katika makundi  mawili. Mosi, yale yanayofafanuwa Ulimwengu kwa mtazamo wa kukanusha uumbaji na pili yale yanayoona kuwa Mwenyezi Mungu ndiye Aliyeumba maada na Ulimwengu kutokana  na Ombwe Tupu na kuupangiya utaratibu. Viumbe vyote hai na visivyo hai, vinavyoonekana na visivyoonekana, vilitokana na kazi ya Mwenyezi  Mungu.  Wanadamu, Majini, Wanyama, Mimeya, Magimba (Magalaksi), Nyota, Sayari, miyezi na vimondo vyote vimeumbwa na Mwenyezi Mungu. Usanii bora, mahesabu, urari na mpangiliyo unaoonekana katika Ulimwengu na kwa viumbe hai ni vielezeo vya Imani hii.]]>http://sw.harunyahya.com/sw/Vitabu/8204/nani-mwenyezi-munguhttp://sw.harunyahya.com/sw/Vitabu/8204/nani-mwenyezi-munguWed, 09 Jul 2008 21:50:33 +0300Ulimwengu Wa FrimasonriKwa karne kadhaa sasa kumekuwa na hofu, gumzo na minong’ono  juu ya mitandao inayoendesha siasa za Ulimwengu kwa siri. Mitandao hiyo ni Freemansory na Mafyay  ambayo yote iko chini ya nguvu za uzayuni wa kimataifa. Kitabu hiki kimejaribu kuielezea mitandao hiyo zaidi kikiwa kimejikita katika ule mashuhuri wenye jina la “Freemasonry” au kwa utohozi usiyo rasmi “Frimansori”.  Mtandao huu umejengwa na watu walioamua kujitoa muhanga wenye kuzingatia miiko na tahadhari zote ili kufanikisha lile walilolikusudia. “Frimansonri” ni tafsiri  inayogeuza kidogo matamshi, inatanguliza n kabla ya s na kisha n. Freemansonry-Frimansori. Katika kitabu hiki tutatumia tafsiri hii pamoja na neno Mafya.]]>http://sw.harunyahya.com/sw/Vitabu/8203/ulimwengu-wa-frimasonrihttp://sw.harunyahya.com/sw/Vitabu/8203/ulimwengu-wa-frimasonriWed, 09 Jul 2008 21:46:53 +0300Dalili Za KiyamaKatika kipindi chote cha historia ya ulimwengu, Wanaadamu wameuelewa ukubwa wa milima na upana wake, na ukubwa wa mbingu kutokana na njia zao mbali mbali za uchunguzi ijapokuwa wamekuwa na fikra potofu kuwa maumbile haya yatadumu milele.  Imani hii ndio iliyozaa falsafa za kishirikina na za kilahidi za Ugiriki na dini za Sumeria za Misri ya kale.]]>http://sw.harunyahya.com/sw/Vitabu/8202/dalili-za-kiyamahttp://sw.harunyahya.com/sw/Vitabu/8202/dalili-za-kiyamaWed, 09 Jul 2008 21:44:30 +0300Muujiza Katika Chembe Ya AtomuPamoja na wanasayansi kufanya jitihada kubwa za kitafiti  kubaini ukubwa wake, mapana  na umbali wake, ukubwa wa umbile la mbingu umepindukia uelewa wa Mwanaadamu licha ya kipawa kikubwa alichonacho cha akili yenye uwezo wa kutambuwa kila kitu. Mbingu hii na vilivyomo ndani yake vimetoka wapi? Vinaelekea wapi? Mwisho wake wapi? Na jinsi gani inavyofuata mtandao maalumu na wa pekee wa kutii sheria za kisayansi ambazo hazijulikani zilivyoanza?]]>http://sw.harunyahya.com/sw/Vitabu/8201/muujiza-katika-chembe-ya-atomuhttp://sw.harunyahya.com/sw/Vitabu/8201/muujiza-katika-chembe-ya-atomuWed, 09 Jul 2008 21:40:31 +0300Pepo: Maskani Ya WauminiKwa kuwa ufahamu juu ya maisha ya Peponi umezungukwa na hakika za kiimani, basi ulinganishi uliofanyika kitabuni humu unawianishwa na maisha halisi ya ulimwengu huu. Katika baadhi ya sura au sehemu, yametolewa maelezo linganishi ili kumuwezesha msomaji kupima na kutafakari ili kupata uoni huru unaotokana na hakika za kimsingi zenye hoja madhubuti. Kitabu hiki kimelenga kusaidia kumpa msomaji uhalisia wa kile ambacho pengine amekuwa akikisikia, kujifunza na kukiamini muda wote bila ya kuwa na walau taswira yake.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu aikubali jitihada hii, atusamehe upungufu wetu na atie Tawfiiq waja wake watakaokisoma waweze kuyafahamu vyema maudhui ya kitabu hiki. Maudhui haya yawe chachu ya kuwaweze kuishi kulingana na atakavyo YEYE, wapate kufaulu na kuzawadiwa Pepo tukufu.

]]>
http://sw.harunyahya.com/sw/Vitabu/4594/pepo-maskani-ya-wauminihttp://sw.harunyahya.com/sw/Vitabu/4594/pepo-maskani-ya-wauminiThu, 09 Aug 2007 15:17:04 +0300