SW.HARUNYAHYA.COMhttp://sw.harunyahya.comsw.harunyahya.com - Makala - Iliyowekwa hivi pundeswCopyright (C) 1994 sw.harunyahya.com 1SW.HARUNYAHYA.COMhttp://sw.harunyahya.comhttp://harunyahya.com/assets/images/hy_muhur.png11666Sayansi Inathibitisha Kutoka Mvi kwa Haraka kama Ilivyoelezwa Ndani ya Qur’an

'Dhiki na huzuni,' ugonjwa wa zama hizi, si maradhi yanayoishia kisaikolojia tu. Bali madhara yake hujidhihirisha katika kiwiliwili kwa njia mbalimbali. Matatizo makubwa yanayohusishwa na dhiki na huzuni ni magonjwa ya akili, madawa ya kulevya na utegemezi, kukosa usingizi, maradhi ya ngozi, maradhi ya tumbo na shinikizo la damu, kipandauso, magonjwa ya mifupa, matatizo ya figo, pumu, kudhuru, maradhi ya moyo na matatizo katika ubongo. Na inawezekana kabisa maradhi haya yasitokane na 'Dhiki na huzuni'. Hata hivyo, imethibitika kisayansi kuwa'Dhiki na huzuni,' mara nyingi ndio chanzo cha maradhi haya.

Dhiki ni hisia zote kwa ujumla zinazosababishwa na hofu, kukosa amani, kukata tamaa, msisimko mkubwa, wasiwasi na shinikizo pale uwiano unapokusekana mwilini. Watu wanapopata dhiki, miili yao inapigana na kutoa ishara. Dhiki isiyokwisha inaweza kusababisha uharibifu mkubwa mwilini na kuusababishia kutofanya kazi zake ipasavyo. Mfano wa athari zinazopatikana wakati mwili haufanyi kazi sawasawa ni kutoka mvi haraka. Allah anathibitisha haya ndani ya Qur'an:

Basi nyinyi mkikufuru, mtawezaje kujikinga na Siku ambayo itawafanya watoto wadogo waote mvi? (Surat al-Muzammil, 17).

Katika aya hii, Allah anatuonyesha athari ya dhiki katika nywele zetu kwa kuainisha madhara ya hofu ya siku ya kiama, ambapo itawafanya hata watoto nywele zao ziote mvi. Ukweli huu aliotuelezea  Allah kisayansi tayari umethibitishwa na siku na zama tulizonazo. Hebu tuone namna nywele zetu zinavyobadilika na kufanya mvi.

Vipi nywele zinafanya Mvi?

 

Kuna aina mbili za melanin ambazo huzipa rangi nywele zetu. Moja ni 'eumelanin,' ambayo huzipa rangi nyeusi, na nyingine ni 'pheomelanin,' ambayo huzipa nywele rangi nyeupe. Kadri umri unavyoongezeka, seli katika ngozi ya kichwa zinapungukiwa uwezo wa kutengeneza melanin na hivyo nywele zinapoteza rangi yake na kugeuka kijivu. Wakat baadhi ya nywele zimebakia na rangi yake nyeusi, nyengine zinageuka rangi nyeupe hasa kwa watu wenye nywele nyeusi,  nywele zao zinaonekana zikiwa katika rangi mbalimbali za kijivujivu. Ingawa sayansi haijabainisha kwa ukamilifu mifumo ambao nywele zinapitia hata kuwa nyeupe, imeonekana kuwa matumizi ya Hydrogen peroxide katika saluni huzifanya nywele ziwe nyeupe. Seli zinazozalisha melanin pia huzalisha hydrogen peroxide ambayo kikawaida huvunjwavunjwa na enzyme inayoitwa catalase. Kadri umri unapoongezeka, kiwango cha catalase kinapungua na mkusanyiko wa hydrogen peroxide unazuia utengenezwaji wa melanin. Matokeo yake huwa ni nywele kubadilika na kuwa nyeupe. Basi ni jinsi gani utaratibu wa kisaikolojia unafanyakazi kwa haraka na kuzibadilisha nywele rangi yake?

Dhiki imethibitishwa kisayansi kuzifanya nywele ziwe na Mvi

 

Kichwa wakati mwingine huingia mvi kutokana na hofu au mshtuko au wakati mwingine huwa ni matokeo ya dhiki zisizokwisha. Hii hali ya kubadilika ghafla kwa nywele, anajulikana kama 'canities subita' inahusu zaidi nywele kupoteza rangi hali ile nywele ilopoteza rangi inabakia palepale. Hivi ndivyo  jinsi gani inavyotokea.

Ugonjwa unaojulikana kama 'alopecia areata' ni matokeo ya kunyonyoka nywele na kufanya kipara. Harakati za mfumo wa kinga ya mwili kupambana wenyewekwawenyewe husababisha maradhi haya. Dhiki ndio  sababu inayochochea hali hii.

Wanasayansi wanaifanyia uchunguzi hoja kuhusu sababu ya mfumo wa kinga mwilini inayohusishwa na uzalishwaji wa rangi katika nywele. Nywele nyeupe zilizoshwindwa kuzalisha rangi haziathiriki na mfumo wa kinga mwilini, wakati nywele nyeusi ndizo zinazoathirika na ugonjwa huo. Nywele nyeupe hubaki, na kwa kawaida katika hali hii nywele hubadilika ndani ya mwaka mmoja au miezi tu.

Nywele za watu ambao wanapata ghafla matatizo ya hofu na mshtuko wakati mwingine zinageuka kuwa  nyeupe kwa siku moja au siku chache tu. Sababu ya nywele kugeuka nyeupe kwa njia hii imetolewa ufafanuzi mwaka jana na kikundi cha watafiti kikiongozwa na mshindi wa tuzo ya Nobel kwenye kemia Robert Lefkowitz. Utafiti juu ya panya ulionyesha kuwa matatizo yasokwisha yanaharibu mfumo wa DNA, na jambo hili hupelekea nywele kugeuka nyeupe. Kadri dhiki inavyokuwa kubwa zaidi, uharibifu mkubwa unapatikana katika DNA, na nywele zinabadilika kuwa nyeupe kwa kasi.

Allah  anatufahamisha kuwa Dhiki inayosababisha matatizo mbalimbali ya mwili na akili ikiwa ni pamoja na nywele kutoka mvi huwapata watu walioipa mgongo dini kama tunavyofahamishwa ndani ya aya hii, “Na atakaye jiepusha na mawaidha yangu, basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki, na Siku ya Kiyama tutamfufua hali ya kuwa kipofu.”  (Surat Ta Ha, 124). Allah anatufahamisha kuwa wale watakao kufuru atawafanyia vikwazo katika mambo yao na kuwafanyia maisha magumu. Katika aya nyingine Allah anatuambia; “… Na pia wale watatu walio achwa nyuma hata dunia wakaiona dhiki juu ya ukunjufu wake, na nafsi zao zikabanika, na wakayakinika kuwa hapana pa kumkimbia Mwenyezi Mungu isipo kuwa kwake Yeye. Kisha akawaelekea kwa rehema yake ili nao waendelee kutubu. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kupokea toba na Mwenye kurehemu. (Surat at-Tawba, 118)

Haya maisha ya tabu au maisha ya dhiki kama tuyaitavyo leo, ni matokeo kwa wale wasioamini, wanaoishi maisha yalio nje ya maadili ya imani. Leo madaktari wanatuambia kwamba amani na utulivu wa akili ni muhimu kwa ajili ya kuepushwa na madhara yatokanayo na dhiki, raha na utulivu wa akili vitapatikana tu pale mtu atakapoifanya Qur'an kuwa ni sehemu ya maisha yake ya kila siku na kumkabidhi kila kitu Allah. Allah anatuonyesha haya katika aya mbalimbali ndani ya Qur'an kuwa atawapa amani na utulivu Walioamini. (Surat al-Baqarah, 248, Surat at-Tawba 26, 40; Surah Fath, 4, 18) Allah ameahidi kwa waumini kama ifuatavyo: “Mwenye kutenda mema, mwanamume au mwanamke, naye akawa ni Muumini, tutamhuisha maisha mema; na tutawapa ujira wao kwa bora ya waliyo kuwa wakiyatenda..”  (Surat-Nahl, 97)

Adnan Oktar's piece on News Rescue:

http://newsrescue.com/the-rapid-whitening-of-the-hair-described-in-the-quran-has-been-scientifically-proved/

]]>
http://sw.harunyahya.com/sw/Makala/202881/sayansi-inathibitisha-kutoka-mvi-kwahttp://sw.harunyahya.com/sw/Makala/202881/sayansi-inathibitisha-kutoka-mvi-kwaWed, 13 May 2015 18:27:15 +0300
Je, umewahi kutafakari thamani ya wakati?

Je, umewahi kutafakari thamani ya wakati?

Je, umewahi kufikiri sekunde, dakika, saa, siku, mwezi na mwaka  vipitavyo?

Wakati mwengine tunapokuwa tumetulia tunahisi kama muda nao umetulia. Tahamaki baada ya saa au siku kupita mtu anatambua kuwa wakati umekwenda haraka sana.

Kila mtu hivi sasa analamika namna muda unavyokwenda mbio, kiasi hata marafiki wanafikia kusema, "Wiki ilopita tu tulikuwa pamoja, ajabu imekuwa kama jana!" "Nilikosha gari yangu wiki iliyopita, ajabu namna ilivyochafuka kwa muda mfupi tu! "Basi vipi tunatumia kitu hichi cha thamani tulichotunukiwa kinachopita kwa kasi?

Wakati unakwenda mbio

Kama tutatafakari kidogo, tutaona kuwa muda tulioubakisha katika ulimwengu huu unamalizika harakaharaka. Binaadamu anapitia mambo mengi baina ya utoto na makuzi yake ikiwa ni pamoja na, kusomeshwa, maisha ya kujitegemea na taaluma mbalimbali za kazi, ndio kusema maisha ya kila siku ya kila mtu yanazunguka hapohapo. Mambo kama mitihani ya darasani, tafrani za kazini na majukumu ya ndani vinapokutana pamoja mtu hujikuta tayari amezongeka. Hali hiyo humsahaulisha madhumuni halisi ya maisha au kwa maneno mengine husahau hata sababu ya kuwepo kwake hapa duniani.

Katika hali isiyoepukika, kila siku utakutana na taarifa za vifo unaposoma magazeti ua kusikiliza vyombo vya habari. Watu wengi hupata mshtuko wa ghafla unaowazindua na baadae huguswa na aliyekufa. Kama marehemu alikuwa kijana, watu huona amekufa  mapema na ameyakosa mambo ya msingi kama kazi na ndoa. Ukweli wa jambo hili ni kwamba, kifo kinamfika mtu yeyote wakati wowote. Hakijali mtoto, kijana au mzee, kinaweza kuja katika sura ya maradhi ya moyo au ajali ya barabarani. ingawa watu wanatafakari juu ya mambo haya, baada ya muda mfupi mawazo yao yanafutika na wanarudi kuendelea na shughuli zao na kupanga mipango mengine kama vile halikupita jambo lolote.

Lakini umewahi kujiuliza kuhusu mipango uliyojiwekea imekuwa kama ulivyopanga?

Basi tutambue kuwa, sisi si wapangaji. Kila mara mambo huja kinyume.

Kwa-kawaida tunapanga kwa ajili ya baadaye, lakini ni lazima muda wote tufahamu kuwa mambo yetu yapo chini ya udhibiti wake Allah. Mambo yote Alikwisha yapangwa, na tunaonyeshwa kila siku. Mwenyezi Mungu ametufanyia siri kubwa sana. Siri inayohusisha utulivu wa maisha yetu na mwisho mwema. Sababu ya kusema haya ni pale Allah anapotuonyesha  ukweli huu ndani ya Qur'an kama inavyofuata:

Mmeandikiwa kupigana vita, navyo vinachusha kwenu. Lakini huenda mkachukia kitu nacho ni kheri kwenu. Na huenda mkapenda kitu nacho ni shari kwenu. Na Mwenyezi Mungu anajua na nyinyi hamjui. (Surat al-Baqara, 216)

Mawazo kuwa kujiliwaza ni jambo la kufurahisha ni wazo ovu lililopangwa na shetani. Kupoteza muda, au 'kutupa wakati, kama inavyochukuliwa na wengi ni jambo la kawaida katika jamii zisizoishi katika misingi ya dini. Kwa hali yeyote, muda wote waumini wanatakiwa kutumia muda wao waliopewa na Allah kujikurubisha kwake na kutafakari namna ya kuutumikia Uislamu na Waislamu.

Hakika wakati ni kitu muhimu chenye thamani kubwa kuliko dhahabu.  Lazima mtu awe na matumizi bora ya wakati. Badala ya kuangalia tamthilia kwa masaa manne au matano, Muislamu atumie muda huo kujifunza utamaduni wa uislamu wake, ajiongezee elimu ya dini yake, asaidie watu, aweke mazingira yake safi na ajipange vizuri katika asili yake na maendeleo.

Wakati ndio jambo lililokuwa muhimu sana kwa Mtume wetu Muhammad (Rehma na Amani ziwe Juu yake). Kwa hakika alitumia kwa makini kila sekunde na dakika kwa manufaa ya Umma wa kiislamu na jamii kwa ujumla. Hii ndio sababu Mtume Muhammad (Rehma na Amani ziwe Juu yake) akikerwa sana na watu wanaochezea wakati.

Ni muhimu sana kuwa na matumizi bora ya wakati. Moja ya matatizo yanayo wakabili  watu wengi leo ni kupiga soga na kutumia muda mwingi bila kuthamini umuhimu wake maishani. Watu wanakosea sana kwa hili,

Kila kitu duniani kitafikia mwisho

Watu, wanyama, maua, matunda na vyakula hata kama vimehifadhiwa  kwenye baridi vyote vitaangamia. Maisha ya milele yapo peponi pekee. Huko hakuna mwisho. Ujana unaendelea. Watu daima watabaki vijana. Ukiisha chuma tunda peponi, jipya linatokea muda uleule. Kinyume na hapa duniani inapotubidi tusubiri kila tunda na msimu wake. Peponi hakuna tatizo la msimu wa matunda. Unatumia muda kwa uwapendao. Utafanya unachopenda wakati unaopenda. Utajipamba upendavyo. Hakuna maradhi, uchovu wala kuhangaika. Kuna raha za zisizokatika. Kinyume kabisa na maisha haya ya duniani. Daima tunahangaikia. Kamwe hatutosheki. Tunapopata tukitakacho, mfano  simu mpya, inatushughulisha muda mfupi, likitolewa toleo jipya sote tunataka tulipate badala ya lile la mwanzo.

Kila mtu atatumia muda uleule alopangiwa na Allah. Hivyo upotezaji muda unapunguza manufaa ya muda wako wa kuishi hapa duniani na wala hutoupata tena ukisha kupita.

Allah ni Muumba wa kila kitu

Allah ameahidi kutulipa pepo yenye uzuri usiokwisha. Matarajio ya kuipata pepo yatazidi tutakapoilinganisha na maisha haya ya ulimwenguni. Kwa mfano hapo ulipo unapofumba macho na kuleta taswira ya mambo mazurimazuri na ukatamani yatokee, Allah atakufanyia mambo mazuri milele huku ukiyaona waziwazi hata akili haijapa kufikiri.

Tumekwisha ahidiwa kupata hatima njema pindi tutakapofuata maelekezo yake Allah hali tumeondoa shaka, wala hatujiweki roho juu kwa jambo lisilo na maana. Tunapaswa kutafakari neema nyingi tulizopewa bila ya kusahau dhumuni la kuwepo kwetu hapa duniani na kubadilisha mfumo wa maisha yetu uende sambamba na maelekezo ya dini.

Kila sekunde, dakika na saa inayotupitia ni hatua moja kuelekea kaburini. Muda mfupi tuliopewa hapa ulimwenguni daima ndio utakaoamua makazi yetu ya  milele huko Akhera. Hivyo, kuwa na matumizi sahihi ya wakati ndio jambo bora la kuazimia. Ndani ya Qur'an, Allah anatufahamisha kuwa maisha haya ya dunia ni maisha ya muda mfupi,

“Atasema: Mlikaa muda gani katika ardhi kwa hisabu ya miaka?’

Watasema: Tulikaa siku moja au sehemu ya siku. Basi waulize wanao weka hisabu.’

Atasema: Nyinyi hamkukaa huko duniani ila kidogo, laiti ingeli kuwa mnajua.” (Surat al-Mu’minun, 112-114)

Muumini wa kweli lazima ajichunge kukaa bure ili shetani asije akampambia  dunia. Kwa njia hiyo pekee ndipo mtu anaweza kusalimika. Qur'an inatufahamisha kuwa waumini hawakai bure:

“Na ambao hujiepusha na mambo ya upuuzi,” (Surat al-Mu’minun, 3)

News Rescue:

http://newsrescue.com/being-a-time-engineer/%23axzz3VY1JePN1

]]>
http://sw.harunyahya.com/sw/Makala/202235/je-umewahi-kutafakari-thamani-yahttp://sw.harunyahya.com/sw/Makala/202235/je-umewahi-kutafakari-thamani-yaMon, 27 Apr 2015 14:32:36 +0300
KUYAANGALIA MAMBO KWA MUSTAKBALI WAKEUtambuzi wa mu’min kuwa yumo kwenye mtihani humuongoza azingatie mambo yake kwa sura ya kuyaangalia mbeleni. Lakini “kuyaangalia mambo mbeleni” kunamaanisha nini hasa?

Ijapo taabu na shida humkumba binadamu, hali hio hakika si ya kudumu milele bali ni ya muda wa kupita tu. Mtu, kwa mfano, anaweza kutuhumiwa kiuwongo kuwa amefanya hatia fulani na kudhulumiwa. Bila shaka utakuja wakati ukweli wa mambo utadhihirika. Hata kama taabu inayompata mtu huyo haitakwisha hapa duniani, kwa ajili ya dhuluma hiyo, wale waliosababisha hiyo dhuluma watapata jazaa yao kamili siku ya Kiyama. Na vilevile, yule aliyedhulumiwa anatarajia kupokea zawadi nzuri sana kwa subira yake katika siku hiyo. Wakati unakwenda haraka sana, na kama mambo mengine yale, hali hii itawadia mwishowe kama vile kasi ya mwendo wa kufumba na kufumbua jicho. Pia Qur’ani inadhihirisha kuwa dhiki hufuatiwa  na faraja kwa Mwislamu:

Basi kwa hakika baada ya dhiki faraja. Hakika baada ya dhiki faraja. (Surat Al-Inshirah, 5-6)

Mu’min anaamini kwa uadilifu kamili na kwa haki iliyo ya daima ya Mola wetu, anategemea faraja baada ya dhiki, na hakati tamaa kwa hali yoyote ile. Anakumbuka vyema kuwa taabu anayoipitia itabadilika mbeleni kwa kuja kuwa furaha kubwa kwake hapa duniani na Akhera.

Mwislamu anajua kuwa anaitizama qadari. Lengo moja zuri sana katika siri hii ni kuangalia kila kitu kile kwa nia ya kumuamini Allah kabisa, kwa radhi ilio timamu na utiifu kamili. 

Tusisahau kuwa msimamo wa hali hii ni pekee tu kwa wale waumini wa kweli wa Mwenyezi Mungu, kwa wale ambao wameridhia kabisa hali ya qadari ndio wanaoweza kuutambua kikamilifu. Watu wasiokuwa na dini, kwa upande mwengine, wanaangukia chambo cha kufa moyo na kukata tamaa, huwa na wasiwasi na kuonekana kubanwa na shida nyingi sana kwa sababu ya kukosa kuwa radhi na mambo ya qadari, wanadhania kuwa hakuna njia ingine yoyote ile mbele yao. Kwa vile hawana matumaini wala mategemeo ya Akhera, daima huwa ni watu wenye kuhangaika kwa wasiwasi na taabu nyingi.  Hali ya watu kama hao inaelezwa hivi katika aya ingine:

Basi Yule ambaye Allah anataka kumwongoza, hufungulia kifua chake Uislamu. Na Yule ambaye Allah anataka kumhukumu kupotea, hufanya kifua   chake kuwa na dhiki na taabu kama anaepanda angani.  Namna hii Allah       anajaalia uchafu juu ya wale wasioamini. (Surat al-An'am, 125)

Hali hii ya taabu ilioelezewa kwenye aya ni kidonda cha kujitonyesha, hali ambayo inachimbukia kwenye shina la ukosefu wa watu kuiamini qadari ilioumbwa na Mwenyezi Mungu. Uhakika wa kuwa Mwenyezi Mungu, Mfalme, Mwenye uhai wa maisha na milele, anayeendesha qadari ya mtu, ni baraka kubwa sana kwa yule mtu aliyeamini. Lakini kwa wale wenye imani dhaifu na wale wasioamini basi hawana uwezo wa kutambua thamani ya baraka hiyo. Hawawezi kuwa radhi na qadari, kwa hiyo wanataabika katika kila wakati wa maisha yao. Hali hii hasa ni natija ya athari ya ukosefu wao wa kumuamini Allah vilivyo ndio maana inakuja kuwakumba maishani mwao hapa duniani. Watu hao wanajidhulumu nafsi zao wenyewe.

Hakika Allah hawadhulumu watu chochote; lakini watu      wanajidhulumu wenyewe nafsi zao. (Surat Yunus, 44)

]]>
http://sw.harunyahya.com/sw/Makala/21564/kuyaangalia-mambo-kwa-mustakbali-wakehttp://sw.harunyahya.com/sw/Makala/21564/kuyaangalia-mambo-kwa-mustakbali-wakeWed, 10 Mar 2010 18:58:32 +0200